ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE0%

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE Mwandishi:
Kundi: Imam mahdi (a.s)

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi: Marehemu Mulla Muhammad Jaafar Sherif Dewj
Kundi:

Matembeleo: 21861
Pakua: 3996

Maelezo zaidi:

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 21861 / Pakua: 3996
Kiwango Kiwango Kiwango
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

8

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 9

IDDUL-BARAAH (KISMATU RIZKI)

Iddul-Baraah ambayo ni tarehe 15 shaaban ni usiku wa baraka na furaha kwa waislamu wote. usiku huo umependekezwa sana kwa ajili ya ibada na hasa Duau Kumail (dua ambayo imam Ali(a.s) alimfunza sahaba wake qumail ibne ziyad) na ziara (mamkizi) ya imam hussein(a.s) . mamilioni ya wanazuoni hukusanyika huko karbala katika usiku huo. waislamu duniani kote husherehekea usiku huo kwa kuwasha taa kwa wingi majumbani mwao ili kuzidisha utukufu katika kukumbuka na kusherehekea kuzaliwa kwa imam wa kumi na mbili. kuna hadithi nyingi katika vitabu vya sunni na shia kuhusu iddul-baraah na hapa tunanakili chache zinazohusika: kwanza, neno "baraat" katika lugha ya kiarabu lina maana ya "kumwachia huru," "kufungua," "kuruhusu" au "msamaha". kufanya ibada usiku huo humpatia mja rehema na msamaha wa mwenyezi mungu. mtume mtukufu(s.a.w.w) amesema kwamba:Usiku huo Mwenyezi Mungu hupanga riziki, umri wa kila mtu na orodha ya watu watao kwenda kuhiji mwaka huo.

Mtume(s.a.w.w) vile vile amesema kwamba:katika usiku huo Mwenyezi Mungu anawasamehe waumini wengi mno kuzidi hata manyoya ya kondoo wa kabila la kalb. akaongezea kunena kuwa:"Mwenyezi mungu hukubali ibada zote usiku huo, na kuwasamehe waumini wote ila tu wale wanao abudu miungu, wale ambao huanzisha mambo mapya"

Katika dini kinyume cha amri ya mwenyezi mungu, wale wanaodharau ndugu na jamaa zao, na waasi wanaoendelea kutenda maasi bila ya kutubia. Mtume(s.a.w.w) amewasihi wanafunzi wake kukesha usiku wa l5 Shaaban katika ibada na kumwomba mwenyezi mungu na kufunga siku ya pili kwa sababu mungu anawasubiri sana usiku huo kuwasamehe viumbe wake wanao kumbuka madhambi yao na kuomba toba na huwazidishia riziki yao wale wanao omba hivyo.

Imam Jaffar Sadiq(a.s) amependekeza kwamba mtu awe tohara kwa kukoga usiku huo ili uzito wa dhambi upunguzwe na vile vile kusoma ziara (maamkizi) ya imam hussein(a.s) ili asamehewe madhambi yake.

Imam Zainul Abidin(a.s) amesema: ikiwa mtu anatamani kuwaamkia manabii 124,000 basi siku hiyo azuru kaburi la imam hussein(a.s) na kusoma ziara yake (imam hussein) usiku wa 15 shaaban kwa sababu mitume wote pamoja na malaika wote wanazuru kaburi la imam hussein(a.s) . kwa hakika waliobahatika ni wale wanaokuwa karbala usiku huo na kuweza kusoma ziara ya imam hussein(a.s) .

Imam Muhammad Baqir(a.s) amesema kwamba: Baada ya 'lailatul Qadri' katika mwezi wa ramadhani, usiku wa 15 shaaban umebarikiwa zaidi kuliko nyusiku zote. Mwenyezi mungu ameahidi kukubali dua ya waumini na hatakataa ombi lolote ila tu ombi hilo likiwa kinyume cha amri zake. kwa kweli usiku huo mtu asomaye subhanallah, alhamdu lillah lailaha illallah, allahu akbar, madhambi yake yatafutwa na ibada yake kukubaliwa.

SWALA NA DUA ZILIZO PENDEKEZWA SANA

A. DUA-UL-KUMAIL.

B. SWALA YA RAKAA NNE (Kila baada ya rakaa mbili unatoa Salam)

katika kila rakaa baada ya suratul-Faatiha Utasoma Suratul-Ikhlas mara 100.

kuna swala na ibada nyingi zingine ambazo zimeelezwa katika vitabu vya ibada.

Kama ulivyo usiku huo, siku ya 15 shaaban vile vile imebarikiwa namo imependekezwa ibada na dua pamoja na kusoma ziara ya imam hussein(a.s) . sura 10.

Utoto (ujana) wa hadhrat Mahdi(a.s) mwenyezi mungu alimjalia hadhrat mehdi(a.s) hekima na ubora tangu kuzaliwa kwake. kama vile mitume issa na yahya walivyokuwa na maarifa na hekima, imam mehdi(a.s) pia alijaaliwa na uwezo wa kuonyesha miujiza, uwezo wa kusema na kusoma qur'an akiwa susuni bado. siku ya pili baada ya kuzaliwa hadhrat mehdi(a.s) , mhudumu mmojawapo, nasseem khatoon, alipokaribia susu yake alienda chafya. imam(a.s) kama vile ilivyo mila ya kiarabu akamwambia "mungu akuteremshie rehma" na akamweleza "mtu yeyote anaye enda chafya anahakikishiwa kwamba hatafariki kabla ya siku tatu kupita". mhudumu mwingine masr alipokaribia susu, hadhrat mehdi(a.s) alimwomba amletee sandali nyekundu. alipoleta sandali imam(a.s) akamwuliza "unanijua mimi?" mhudumu akajibu, "wewe sayyid yangu na mwana wa tajiri yangu." Imam akasema: "Mimi sikuuliza hayo. mimi ni imam wa kurni na mbili, imam wa mwisho. mwenyezi mungu atajaalia ushindi dhuria ya mtume mtukufu(s.a.w.w) kwa mkono wangu namimi nawafuasi wangu tutakomesha dhuluma na maafa duniani".

Siku arobaini baada ya kuzaliwa imam(a.s) , bibi halima khatoon alipokwenda kwa imam hassan askari(a.s) alishangazwa kumwona hadhrat mehdi(a.s) amekua kama mwana wa miaka miwili. imam hassan askari(a.s) akamweleza kwamba wana wa imam hukua kwa haraka kuliko watoto wengine. miujiza mingi ilionyeshwa na hadhrat mehdi(a.s) wakati yungali mtoto bado. mmojawapo ni kamaufuatao: ahmed bin ishak bin sadulashary anahadithia kwamba safari moja alikwenda kwa imam hassan askari(a.s) kutaka kumwuliza nani atakuwa imam baada yake. kabla hajamaliza kuuliza suala hilo, imam Askari(a.s) akasema "Eh Ahmad, Mungu haachi pengo la hujjah wake duniani na hujja wake atakuwepo mpaka siku ya hukumu na kwa sababu ya kuwepo kwake ndiyo Mwenyezi Mungu huteremsha rehema na kuepusha maafa ." baada ya hapo akauliza swali. hapo imam Hassan Askari(a.s) akamleta mtoto mmoja wa miaka mitatu mwenye uso uliojaa nuru na akamwambia Ahmad, "Eh Ahmad, wewe ni katika masahaba waaminifu na kwa hivyo ninakuonyesha mwana wangu; yeye ni hujjat wa mungu, imam baada yangu na mrithi wangu. Yeye ataeneza insafu na usawa duniani. " Ahmad aliposhangazwa na hayo akamsikia huyo mtoto akisema: "Eh Ahmad, mimi ni mrithi wa mwisho na maimam wa haki. dunia itaendelea kwa sababu yangu. mimi nitachukua kisasi na kuwaadhibu maadui wa dini. wakati dunia itapoghilibiwa na ulaghai, dhuluma, ukandamizaji na uovu, mimi nitajitokeza kwa amri ya mungu na nitatawala kwa insafu na usawa ."

Siku ya Shahada ya imam Hassan Askari(a.s) jiji zima la Samarra liligubikwa na huzuni. Hata mayahudi na wakristo walihuzunika. maduka yote yalifungwa. Imam Hassan Askari(a.s) alifariki dunia tarehe 8 rabiul awwal (mfungo sita) .mwaka 260 a.h. umri wake ulikuwa miaka 28-29. wakili wake, othman bin said, aliandaa mazishi ya imam hassan askari(a.s) . jeneza lilipokwisha kuwa tayari mashia (wafuasi wa maimam kumi na wawili) na waislamu wote, pamoja na wakuu wa jeshi walikutanika nyumbani mwa imam hassan askari(a.s) kuomboleza msiba huo. ndugu yake imam hassan askari(a.s) , baba mdogo wa imam mehdi(a.s) jaffar tawwab akajitokeza na kutaka kuongoza swala ya maiti.

Alisimama karibu na jeneza na watu wote walikwisha jipanga katika safu ili waswali. jaffer alipotaka kuanza swala, mtoto mdogo mmoja, uso wake uking'ara kama mbalamwezi akaja na kumwambia Jaafar "Eh baba mdogo, jongea mbali, mimi ninastahili zaidi kuliko wewe kuongoza swala ya maiti ya baba yangu mzazi". jaffar alikuwa hajawahi kumwona hadhrat mehdi(a.s) kabla ya hapo na kwa hivyo alibabaika na kurudi nyuma. hadhrat mehdi(a.s) akaongoza swala na kuondoka. hakuna mtu aliyeweza kujusuru kumwuliza chochote hadhrat mehdi(a.s) wala kuweza kuzungumza naye.

Baada ya kuongoza swala, hadhrat mehdi(a.s) alikwenda kuonana na mtumishi wa baba yake kwa jina la adyan na kumwuliza juu ya barua aliyopewa. adyan alimkabidhi barua hiyo imam mehdi(a.s) . kabla ya kufariki imam hassan askari(a.s) alimtuma adyan kwenda baghdad kupeleka barua na alimweleza kuwa atakaporudi na jibu yeye (imam hassan askari(a.s) atakuwa amekwishafariki dunia na kwa hiyo amkabidhi jibu mtu atakaye ongoza swala ya maiti na atakayedai barua hiyo kutoka kwake (adyan). alimwambia kuwa mtu huyo ndiye atakuwa mrithi wake na imam wa wakati huo.

Jaafar tawwab alijitahidi sana ili apate mali ya kaka yake pamoja na uimam. alikwenda mpaka kwa khalifa wa wakati huo kutaka msaada wake. lakini khalifa alimjibu kwamba kumpatia uimam haikuwa kazi yake ila shia wa nduguze wakimkubali na kumtambua ndipo jaffar ataupata uimamu. matukio mengi yalitokea katika utoto wa imam(a.s) , lakini hatusimulii katika kitabu hiki. imam zaman(a.s) katika kasri ya khalifa mu'tamid abbasi.

Mmoja wa wahudumu wa imam hassan askari(a.s) . ali bin zamahyar anasimulia kwamba kazi yake moja wapo ilikuwa kumleta imam mehdi(a.s) kwa imam hassan askari(a.s) kutoka ghorofa ya chini (sardab) ambako imam mehdi(a.s) akiishi na mama yake narjis khatun na baada yake kumrudisha tena huko chini (Sirdab). wakati baba (imam hassan askari(a.s) alipokuwa na mwanaye (imam mehdi a.s) na kuzungumza naye ali zamahyar alikuwa hawezi kufahamu mazungumzo hayo. siku moja tarishi kutoka kwa khalifa mu'tamid abbas alitumwa kwenda kwa imam hassan askari(a.s) kuleta salamu ya khalifa kwamba amepata habari kwamba imam hassan askari(a.s) amebarikiwa na mwana lakini hakumjulisha khalifa ili yeye (khalifa) aweze kushirikiana na imam kufurahia kwa kuzaliwa huyo mwana. kwa hiyo khalifa alikuwa anasubiri kwa hamu sana kumwona huyo mtoto. hapo imam hassan askari(a.s) akamwamrisha ali bin zamahyar kumleta huyo mtoto (imam mehdi(a.s) na kumchukua kwa khalifa. kusikia hayo ali zamahyar alijawa na hofu kwa sababu alikuwa na uhakika khalifa atamwua huyo mwana (imam mehdi a.s.). imam hassan askari(a.s) alipomwona ali zamhayar amehofishwa sana akamwambia asiogope kumpeleka huyo mtoto kwa khalifa kwa sababu allah mwenyewe atamhifadhi hujjat (dalili ya kuwepo kwa mungu.

ali Zamhayar anasema: "Mimi nilikwenda ghorofa ya chini na nikaona nuru iliyoje iking'aa usoni mwa imam mehdi(a.s) , nuru ambayo sikuwahi kuiona maishani mwangu. kiwaa kwenye shavu la kulia kiking'ara kama nyota. nilimbeba mabegani na nilipotoka nje ya nyumba niliona uso wake umetoa nuru ambayo ilimulika jiji la samarra mpaka mbinguni. wakazi wa mjini waliacha shughuli zao na kumwaangalia macho huyo mtoto (imam mehdi a.s.). wanawake na watoto walikuwa wakimchungulia huyo mtoto mwenye nuru, kutoka madirishani na ghorofani. punde si punde barabara zilijazana kwa watu na ilikuwa shida kwangu kupita nifike kwa mfalme. tarishi wa mfalme ilimbidi aniongoze njia nzima.

Nilipofika kitaluni niliona khalifa na washauri wake na walinzi waliaibika na ung'avu wa uso wa lmam mehdi(a.s) . mimi nikaenda moja kwa moja mpaka kwa mfalme na nikasimama upande wa kulia nikimbeba imam mehdi mabegani na kumkabili khalifa. baada ya muda mrefu waziri aliyesimama karibu na khalifa akamnong'oneza khalifa. mimi nilikuwa na hakika kwamba walizungumza juu ya kumwua imam mehdi(a.s) na hapo mwili wangu mzima ukatetemeka. khalifa papo hapo aliamrisha walinzi wake wamwue mtoto (imam mehdi a.s.). walijaribu kuvuta panga zao kutoka kwenye ala zao lakini panga hazikutoka.

Khalifa akasema hizo panga zimekwama kwa mazingaombwe ya mwana wa hashim (maimam wote wanatokana na ukoo wa bani hashim). kwa hivyo aliamrisha uletwe upanga kutoka beit al mal (hazina ya serikali) ambao hautaathirika na uchawi. upanga uliletwa kutoka beit-al-mal lakini huko pia ulikwama katika ala. khalifa pamoja na washauri wake walipigwa na butaa. hapo tena khalifa aliamrisha waletwe simba watatu wakali kutoka matundu yao. papo hapo wakaletwa hao simba.

"Mimi (Ali zamahyar) niliamrishwa nimweke mtoto (imam Mahdi a.s.) mbele ya simba hao. nilitetemeka nilipopewa amri hiyo katili. ghafla mtoto (imam mehdi(a.s) akaninong'oneza na kusema: "usiogope, niweke mbele ya simba hao." nikatimiza amri yake. nilishangazwa sana kuona kwamba hao simba watatu walinyanyua mikono yao na kunisaidia kumweka mtoto juu ya sakafu. baadaye wakasimama kwa taadhima mbele ya imam(a.s) huku wameinamisha vichwa vyao. simba mkongwe ghafla akaanza kusema katika kiarabu fasihi kuthibitisha upekee wa mungu, unabii wa mtume muhammad(s.a.w.w) na kutaja majina ya maimam kumi na moja na kumwamkia huyo mtoto (imam mehdi a.s.) na kuendelea, "wewe ni hujjat wa mungu duniani. mimi ninataka kushtaki kwako. hawa simba wawili vijana wanavamia chakula chote tunacholetewa na kuninyima hata hisa yangu, na ninaendelea kubaki na njaa."

mtoto (imam a.s.) akatamka adhabu ya dhuluma (kosa) hiyo na kusema kuwa hao simba vijana wageuke wakongwe na huyo mkongwe arudishiwe ujana wake na afya yake. Kabla imam(a.s) hajamaliza hayo matamshi simba wawili vijana wakazeeka na kudhoofu na yule mkongwe akageuka kijana na mwenye nguvu. kuishuhudia miujiza hiyo khalifa na washauri wake wote wakanadi allahu akbar kwa mshangao na msisimko. hapo khalifa akaamrisha kwamba huyo mtoto (imam a.s.) arudishwe kwa wazazi wake. mimi (ali zamhayar) nilimshukuru mola na nikambeba imam a.s. kurudi naye nyumbani. njiani barabara zote zilijaa watu na kila mtu alishangazwa na nuru ya imam(a.s) . nilipofika nyumbani nikamhadithia yote imam hassan askari(a.s) ambaye alifurahi na kumshukuru mungu."

9

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 11

KUGHIBU KWA MUDA MFUPI (GHAIBATU-S-SUGHRA) NA MAWAKILI WA IMAM

Baada ya kifo cha baba yake na kufuatana na maagizo yake imam hassan askari(a.s) , imam wetu wa wakati, hadhrat mehdi(a.s) amejificha kutoka macho ya watu, tarehe 10 shawwal 260 a.h. umri wake ulikuwa miaka mitano. kujificha kwake kwa kipindi hicho huitwa kughibu kwa muda mfupi (ghaibatu-Sughra). hata hivyo aliteua baadhi ya masahaba wake kuwa mawakili ambao wakiandikiana na wafuasi wake na kujibu maswali kwa maandishi. kipindi hicho kiliendelea kwa muda wa miaka sabini na baada ya hapo kukatokea kughibu kwake kwa muda mrefu ambao unaendelea hadi leo. katika kipindi hicho cha kughibu kwa muda mrefu hakuteuliwa mwakilishi yeyote na mawasiliano kwa maandishi yamesimama. kwa hiyo, imam(a.s) sasa anasubiri amri ya mungu ili ajitokeze. mada hii tutaizungumza kwa marefu na mapana katika sura ifuatayo. Mawakili katika muda wa kughibu kwa (imam mehdi a.s.) muda mfupi

Wakili wa kwanza alikuwa Othman bin Said ambaye alikuwa wakili wa Imam wa kumi pia na imam wa kumi na moja. Yeye alikuwa mwenye umri mkubwa na mwanazuoni mwenye hekima kubwa. Akawa wakili wa imam mehdi(a.s) kwa muda mfupi tu wa kipindi cha mwaka mmoja na nusu. imam mehdi(a.s) alimwarifu kwamba atafariki dunia baada ya muda mfupi na amteue mwanae muhammad kuwa wakili na kuwa uteuzi huo utangazwe hadharani.othman bin saidi alifariki baghdad na kuzikwa huko, waumini wengi mara kwa mara huzuru kaburi lake.

Wakili wa pili alikuwa muhammad bin othman imam(a.s) alimwandikia "Eh Muhammad bin Othman, baba yako alibahatika sana kupata mwana mwema kama wewe mwenye sifa nyingi njema. kila siku mwombe mungu akujalie rehema yake. mwenyezi mungu akusaidie." muhammad bin othman alikuwa mwanazuoni mcha mungu. alikuwa mtu mwenye msaada mkubwa kwa mashia na akiendesha uwakala wa imam(a.s) kufuatana na maagizo ya imam(a.s) . alipokaribia kufariki dunia imam(a.s) alimtumia ujumbe wa kumteua hussein bin rauh kuwa wakili kumrithi yeye (Muhammad bin Othman). muhammad bin othman akafariki dunia 305 a.h. baada ya kuwa wakili wa imam(a.s) kwa muda wa miaka hamsini. amezikwa baghdad na waumini wengi huzuru kaburi lake. wakili wa tatu alikuwa sheikh abui kassim hussein bin rauh. alikuwa mwanazuoni mashuhuri, mcha mungu, mwenye tabia nzuri na akiheshimiwa na kupendwa na masunni wengi. alimtumikia imam(a.s) na mashia wake kwa dhati na kwa bidii. mengi aliyokamilisha yameelezwa katika vitabu vingine. Abul kassim hussein bin rauh alifariki dunia 326 a.h.

Wakili wa nne alikuwa aly bin muhammad samary. Yeye alikuwa wakili wa mwisho. Na uwakala wake ulidumu kwa muda wa miaka mitatu. Muda mfupi kabla ya kufariki dunia alipata ujumbe ufuatao kutoka kwa imam(a.s) "kwa jina la mungu: ali samary, mungu awajaalie subira na jazaa waumini wenzake kutokana na kifo chake. Baada ya siku sita wewe utafariki dunia hii. Kwa hivyo, kamilisha mambo yako yote, kwa sababu baada yako hatateuliwa mrithi wako kuwa wakili wangu kwa sababu nimeamrishwa na mungu nighibu kwa muda mrefu. katika muda wa kughibu kwangu watu watakuwa na roho ngumu, maafa na dhuluma zitaenea na wazandiki wengi watajitokeza. Kutakuwa na alama mbili za kuashiria kujitokeza kwangu. sufiani (ukoo moja na jeshi lake) atatokea kutoka syria na sauti kubwa mno itasikika kutoka mbinguni ambayo mataifa yote yatasikia na watu wote bila kujali lugha wanayotumia watasikia na kufahamu. Kama alivyosema imam(a.s) ali samary alifariki baghdad tarehe 15 shaaban na kuzikwa huko huko. Watu huenda kuzuru kaburi lake kama wanavyokwenda kwenye makaburi ya mawakili wenzake waliotangulia.

SURA 12

KUGHIBU KWA MUDA MREFU (GHAIBAT-AL-KUBRA) SIRI YAKE NA MAJIBU YA UWAMBI DHIDI YAKE

Katika kipindi cha kughibu kwa muda mfupi imam(a.s) akijibu maswali ya mawakili na wafuasi wake moja kwa moja. baadaye mungu alimwamrisha aghibu kwa muda mrefu na tokea siku hiyo imam(a.s) haonekani. katika kipindi hicho imam(a.s) hataonekana dhahiri, na hakuna mtu yeyote atakayeweza kudai kuwa ni wakili aliyeteuliwa na imam(a.s) wala kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na imam. Kwa hivyo badala ya mtu maalum kuteuliwa naibu wake, wanazuoni wacha mungu huhesabiwa ni kama mawakili wa imam(a.s) . ili kuwatambulisha wale wanaostahili kukubaliwa kama manaibu wake, imam(a.s) ametangazakuwa:"wale wanazuoni wa kidini ni watetezi wa dini, wanaojizuia nafsi zao dhidi ya maasi na kumfuata imam (a.s). kila muumini anawajibika kuwafuata wanazuoni hao. wanazuoni hao ni manaibu wetu kama vile sisi tulivyoteuliwa na mungu. wataowapinga hao watakuwa wapinzani wetu na hao watakaotupinga sisi ni wahalifu wa mungu."

Uwambi mwingi umeelekezwa dhidi ya kughibu kwa imam(a.s) kwa muda mfupi na muda mrefu. inasemekana kwamba imam(a.s) amejificha kwenye ghorofa ya chini kwa kuogopa na kwa hivyo hatupati faida yoyote ilihali yule imam wa wawambi anaonekana dhahiri. kwanza ni lazima kuthibitisha ukweli wa daawa hilo la uimam; la sivyo, kuonekana kwa imam haina faida yoyote. Katika sura mojawapo iliyotangulia katika kitabu hiki imekwisha thibitika kwa aya za qur'an na hadithi kwamba imam mendi(a.s) ni imam wa kweli wa wakati huu na imam wa kumi na mbili. sura hii itazungumzia kuwa kughibu kwake hakukufanyika kwa woga au kitisho ila iliamuliwa na mungu kuwa hivyo. Kama vile dunia inanufaika wakati jua linapojificha nyuma ya mawingu, vivyo hivyo viumbe wa mungu wanafaidika ijapokuwa imam haonekani.

Nabii Musa alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu mwenye kila uwezo wa kumhifadhi. Lakini nabii Musa alikimbia na kwenda kujificha kutokana na dhuluma za firaun. Kama ilivyoelezwa katika qur'an (28:21): "kwa hivyo yeye ameondoka akiwa na hofu, na kusubiri".

Wakati huo allah angeliweza kumjalia nabii Musa muujiza wa "fimbo" na kumwamrisha amkabili firaun. Lakini Mungu hakufanya hivyo ila kumwamrisha Musa akimbie kutoka Misri na kujificha kutoka kwa Mayahudi kwa muda wa miaka kumi au kumi na tano. Katika kipindi hicho Waisraeli (Mayahudi) waliteseka chini ya utawala wa firaun. je, kwa muda huo wote Mungu hakuwa na uwezo? hiyo ilikuwa kwa ridhaa na uamuzi wake mungu kuwatahini firaun na wafuasi wake waasi na washirikina na kutahini subira na imani ya wafuasi wa musa. mwenyezi mungu hafanyi haraka kumwadhibu mtu. Kutokana na hayo imedhihirika kwamba kujificha kwa nabii musa kulikuwa ni jaribio kwa binadamu duniani. Kwa hivyo alijificha kwa amri ya mungu kwa muda maalum uliowekwa na mungu.

Baada tu ya kifo cha hadhrat Imam Hassan Askari(a.s) imam wa kumi na moja, papo hapo imam mehdi(a.s) angeweza kuanza kuwaadhibu wadhalimu makafiri na waovu kwa uwezo wanaopewa maimam na uwezo aliojaliwa na mungu kudhibiti viumbe wake. Kwa hivyo, imam angelazimika kuwaua waislamu wengi sana wakati ambapo waumini walikuwa wachache tu. wengi wa hao waislamu (wafuasi wa banu umayya na bani abbasi wenye tamaa na vile vile washirikina na makafiri) wangepaswa wauliwe na katika muda mfupi tu umati mkubwa wa watu duniani ungemalizika. kwa hivyo, kusingetokea fursa ya watu kuzaliwa kwa wingi na kusubiri mpakaimammehdi(a.s) kujitokezailiwaweze kujaribiwa subira na imani zao juu ya mungu. watu wote hao waliozaliwa na kuishi kwa imani juu ya mungu wamejipatia pepo, kadhalika na wale watakao zaliwa kabla kujitokeza kwa Imam(a.s) . kwa hivyo, kughibu na kujitokeza kwake (imam a.s.) ni hiari ya mwenyezi mungu ambaye hana mshiriki, mshauri au msaidizi. mwenyezi mungu ameiumba dunia hii kutokana na mapenzi yake na kuwajaribu binadamu. katika sura 29 ya qur'an, Al-anakabut (buibui), aya 2, Mwenyezi Mungu anasema:"je watu wataachiwa tu kwa kusema tu sisi tunaamini bila kujaribiwa?"

Wafuasi wa Nabii Nuh walijaribiwa vikali kama inavyoelezwa bayana katika qur'an, hadithi na historia. vivyo hivyo na wafuasi wa kila nabii. kwa muda wa miaka mitatu mtume muhammad(s.a.w.w) ilimbidi akabili njaa na dhiki katika pango kutokana na vitisho vya makuraishi wa makkah. baada ya washirikina kuzingira nyumba yake kutaka kumwua ilimbidi aondoke nyumbani mwake peke yake katika usiku wa manane na kuihama makkah. kwa amri ya mwenyezi mungu alimteua hadhrat ali(a.s) alale kitandani mwake. je, mungu hakumjalia huyo nabii nguvu za kutosha kuwaangamiza maadui wa mungu na kueneza dini ya mungu? ahadi ya mungu ilikuwa bado kufika ili amri yake ipate ushindi dhahiri. kwa hivyo, kufuata amri ya mungu, mtume(s.a.w.w) ilimbidi ahame kutoka makkah. Yeye (Mtume) alikuwa bado hajaamrishwa kuchukua silaha kwa msaada wa pekee wa mtoto wa ami yake ali(a.s) na masahaba wake wachache.

Juu ya hayo, kufuatana na hali ilivyo katika nyakati mbali mbali manabii ibrahim na suleiman na manabii wengine waliamrishwa na mungu kujificha. mambo hayo yameelezwa katika qur'an na vile vile katika historia, ila hatuyaelezi hapa kwa sababu kitabu hiki kitakuwa kirefu. Ingawa imam(a.s) wa wakati huu ameghibu, lakini kuwepo kwake ni fadhila na huruma ya Mwenyezi Mungu. Kwa hakika, asaa hiyo nuru ya Mungu yaani walii wake na mrithi wa mtume(s.a.w.w) asingekuweko duniani, dhambi na dhuluma zingeghariki dunia kiasi ambacho dunia isingenusurika hata kwa muda mfupi kutokana na ghadhabu ya mungu. kutokana na qur'an na hadithi ardhi ingelinyimwa mvua na hakuna tunda iolote lingeliota kuwapatia viumbe chakula. hao ambao hawamwamini mungu, mtume wake(s.aw.w) na qur'an wasingekubaliana na maadili hayo. hivyo, kutoamini na kuwa na msimamo wa kiburi haiwahusu waumini.

Zaidi ya hayo, imani na waumini hupata mwongozo na msaada kutoka kwa imam wa wakati huu. tunaeleza mifano michache hapa ili kufariji imani za waumini. kiasi cha maili mia moja kutoka najaf (alipozikwa imam ali(a.s) ambayo ni kituo maarufu cha taalimu cha mashia, akiishi mwanazuoni mashuhuri sana. (mujtahid sheikh allam hilli). Siku moja watu wengi walimwuliza juu ya amrisho kuhusu mazishi ya mwanamke mjamzito aliyefariki dunia, lakini mwenye mtoto hai tumboni mwake. walimwuliza kwamba huyo mama azikwe hivyo hivyo au kwanza wamtoe mtoto tumboni mwake? aliwashauri kwamba huyo mama azikwe kama alivyo. baada ya watu kumaliza ada zote kuhusu maiti, walibeba jeneza na kuelekea makaburini. hapo wakamkuta mtu mmoja aliyepanda farasi anawazuia njiani, na kuwaambia kwamba huyo allama amebadilisha uamuzi wake wa kwanza na kuagiza kwamba huyo mama asizikwe kama alivyo, bali atolewe mtoto kwanza kabla ya kuzikwa. Mtoto alitolewa kwa usalama na mama kuzikwa.

Baada ya muda wa miaka miwili au mitatu huyo allama alitembelewa na mtu mmoja akifuatana na mtoto mdogo (aliyetolewa kutoka tumboni mwa mama aliyefariki). Huyo mtu alimwuliza allama: "je, unamjua huyu mtoto? huyu ni yule ambaye kufuatana na amri yako alitolewa tumboni mwa mama yake aliyefariki. Wewe kwanza ulishauri kwamba mama yake azikwe pamoja na mtoto aliyekuwa tumboni mwake, lakini baadaye ulimtuma mtu aliyepanda farasi kuja na amri kwamba mtoto atolewe tumboni mwa mama yake". Allama alishangazwa sana kusikia hayo na uso wake uligeuka rangi kwa sababu alivyokumbuka yeye hakumtuma yeyote kubadilisha uamuzi wake. Alingamua kuwa iwapo imam mehdi(a.s) asingekwenda kumsaidia, angekabiliwa na dhambi ya kusababisha kumzika mtu aliye hai. tokea siku hiyo akajifungia mlango na akaamua kutotoa uamuzi wowote juu ya mambo yanayohusu dini ili asijerudia kosa lile tena. baada ya muda mfupi alipokea barua kutoka kwa imam(a.s) ikimwambia kwamba asijali mambo hayo yaliyopita na aendelee kutoa fatuwa. Ikiwa kwa bahati mbaya atakosea basi imam(a.s) anaelewa mambo yote na anafika kuwasaidia mashia - wafuasi wake. licha ya wafuasi kunufaika kwa uongozi wa imam(a.s) ijapokuwa angali ameghibu, iakini msaada wake pia unafika wakati unapohitajika.

Imenakiliwa katika biharul anwar kwamba katika enzi za utawala wa kiingereza watu wote wa bahrain walikuwa waisiam na mfuasi wa madhehebu ya kisunni aliteuliwa gavana wa nchi hiyo. Nchini humo walikuwa mashia wengi iakini gavana huyo na waziri wake walikuwa na uadui na mashia. Siku moja waziri alimzawadia gavana makudhumani ambao juu yake alidai kwamba majina ya makhalifa wanne wa kiislamu yalijitokeza kwa kudra ili kuhakikisha ukweli wa madhehebu ya sunni na makhalifa wanao aminiwa. Hapo akamshawishi gavana kuwaita wanazuoni wa kishia awaonyeshe hilo tunda ili waache madhehebu na itikadi ya kishia na kukubali ukweli wa itikadi ya kisunni. Akasisitiza kwamba wakikataa kukubali ukweli wa itikadi ya kisunni basi wasihesabiwe tena kama waislamu na wauawe au walazimishwe kulipa kodi (jiziya) maalum ambayo hulipwa na wakazi wasio waislamu.

Gavana alipoangalia hilo tunda na kuona mwandiko "lailaha illa allah, muhammadun rasulullah - Abu Bakar, Omar, Othman Ali khulafau Rasulullah" aliathirika sana na kutokana na ushauri wa waziri akawaita wanazuoni wa kishia, akawaonyesha tunda hilo na kuwapa hiari tatu kama alivyoshauriwa na waziri wake. Wanazuoni wa kishia walistaajabishwa. wakaomba muda wa siku tatu kutoka kwa gavana, ambaye aliwapa huo muda kwa ridha yake, ili wampatie jibu. waligharikika na mshangao na hatimaye wakaamua kuomba msaada kutoka kwa imam wao hadhrat mehdi(a.s) . wanazuoni wacha mungu watatu wakateuliwa na ikaamuliwa kwamba kila mmoja wao kila usiku atoke nje ya jiji na kwenda kumwomba auni Imam(a.s) . siku mbili za kwanza wanazuoni wawili wakakesha kuswali na kumwomba mungu awapatie msaada wa imam(a.s) lakini bila mafanikio. usiku wa tatu mwanazuoni' wa tatu akaenda nje ya jiji kuomba kwa bidii mno ili apate msaada kutoka kwa imam(a.s) . alfajiri alimwona mtu mwenye haiba ambaye alijitambulisha kwamba ni imam wake. huyu mtu akamwuliza mwanazuoni shida yake. mwanazuoni akamjibu kwamba kama kweli yeye ni imam(a.s) basi anaelewa tatizo linalomkabili. imam(a.s) akamjibu kwamba yeye ana habari kamili ya balaa iliyowapata lakini wasikate tamaa ila wafuate maagizo yake. kisha imam akasema, "kesho asubuhi wewe na wenzako mwende kwenye kasri ya gavana na kumwambia kuwa mtampatia jibu nyumbani kwa waziri.

Waziri atakataa jibu hilo lakini lazima msisitizie hilo na mhakikishe kwamba waziri hafiki nyumbani kabla nyinyi kufika. mwende nyumbani kwa waziri mkifuatana pamoja naye hadi paani. waziri atababaika sana na atajitahidi kutangulia lakini nyinyi mumziwie kutangulia na kufika kabla nyinyi hamkufika. huko ghorofani mtaona mfuko katika kishubaka ukutani. mfungue huo mfuko na mumwonyeshe gavana vitu vilivyomo mle. humo ndani kutakuwemo kalibu ambayo juu yake mtaona maandishi yaliyotokeza juu ya komamanga. hizo ni kalibu zilizovishwa na waziri juu ya makomamanga yalipoanza kuota na zilipoanza kukomaa maandishi hayo yalizidi kuimarika. gavana ataathirika na hayo na atakubali kwamba jambo hilo lilikuwa ulaghai wa waziri. 58

Baadaye mwambieni gavana kwamba kuna ushahidi mwingine kuhusu ulaghai huo. mumwombe gavana amwamrishe huyo waziri avunje hilo tunda mbele yenu na gavana ataathirika na uwezo wa mungu na ulaghai uliofanywa. asubuhi ifuatayo huyo mwanazuoni (muhamad bin ali) akaenda nyumbani kwa gavana pamoja na wenzake. walimwomba gavana wafuatane nyumbani kwa waziri pamoja naye (waziri) kama alivyoagizwa na imam(a.s) . mwishowe gavana akamwamrisha waziri avunje hilo tunda. alipolivunja tunda hilo vumbi nyeusi likatoka na kumwingia machoni na kwenye ndevu huyo waziri. hapo kila mtu akacheka. gavana ilimbidi kusadiki ulaghai uliotendwa na waziri na kuamuru waziri huyo kuuliwa. wanazuoni wa kishia waliondoka hapo kwa heshima. tukio hilo linajulikana sana. kaburi la huyo mwanazuoni aliyeonana na imam(a.s) limehifadhiwa na waislamu wengi huzuru kaburi hilo. hakika hizo huthibitisha kwamba imam(a.s) yu hai, yupo na sisi na inapolazimika huja kuwasaidia mashia wanapokabiliwa na msiba. matukio mengi kama hayo yameorodheshwa katika kitabu hiki kwingineko. imam hadhrat mehdi(a.s) alizaliwa samarra na alighibu kupitia ghorofa ya chini iliyoungana na jengo la maziara ya maimam wa kumi na wa kumi na moja. uwingi wa umati wa samarra ni masunni (90-95%) ambao wanaamini juu ya uhai wa hadhrat mehdi(a.s) kwa sababu miujiza mingi hutokea huko. zaidi ya hayo, imam(a.s) anapokuja kuzuru makaburi ya baba na babu yake (maimam wa kumi na kumi na moja) jiji zima hujaa nuru. waarabu wa huko hufurahia kwa msisimko na wanawake hupanda juu maghorofani kufurahia kuja kwa imam(a.s) .

Hata katika usiku wa giza, Imam(a.s) anapozuru, hilo jiji hung'aa kwa nuru. ikiwa mtu yeyote akinyosha kidole au akitoa ufunguo na kuuning'iniza basi hutoa mwanga kama mshumaa. hata baada ya miujiza mingi kutokea samarra, hao waarabu hawaachi kuwasumbua mashia wanao kuja kwa ajili ya ziara. allah maisha hukamilisha mathibitisho yake. miujiza mingi na dalili nyingi hutokeza kuthibitistia ukweli wa imam(a.s) na uhai wa hadhrat mehdi.(a.s) ili imani ya waumini iimarike na uwe uthibitisho kwa wabishi. hata hivyo, bado kuna maswali machache yanayoulizwa na majibu yake ni kama yafuatayo: suali: ikiwa imam mehdi(a.s) atajitokeza sasa, bila shaka uovu na ukandamizi na kufuru vitakoma duniani, amani, usalama na utii kwa mungu utadhihirika, na waumini hawatakua na shaka yoyote.

Jibu: dunia hii ni pahala pa majaribio kwa binadamu. mwenyezi mungu amekamilisha mathibitisho yake juu ya kila mtu. kujitokeza kwa imam(a.s) hutegemea amri ya mungu. mtu yeyote hana haki ya kuharakisha au kudadisi dadisi. iicha ya hayo, hata baada ya kuja kwa imam(a.s) waliopotoshwa watapotoka. wengi waliomwona mtume(s.a.w.w) na maimam wetu, kushuhudia miujiza na kusikia maagizo yao, lakini walipotoshwa kwa tamaa ya dunia na wakabakia bila imani hata kuwasaidia wadhalimu (bani umayya na bani abbas) na kusahabisha upinzani na uadui dhidi ya maimam wetu na hatimaye kuwaua. kwa hivyo, ni jambo dhahiri kwamba mwenyezi mungu hutenda kila jambo kwa kupenda yeye mwenyewe.

Swali : waislamu wengi huishi katika hali ya vitisho kutoka maadui wao, hudharauliwa na kuteswa. huomba msaada kutoka kwa imam(a.s) lakini matatizo yao hubakia pale pale. kwa hivyo shaka nawasiwasi huingia moyoni mwao ambalo siyo jambo jerna.

jibu : siku moja mwana mmoja wa mama mmoja akawa mgonjwa mahututi sana na hapakuwa na tamaa yoyote ya huyo mwana kupona, huyo mama alisema kwamba ikiwa mungu yupo naye ndiye mwenye kila uwezo na mwenye rehema bila shaka huyu mwana atapona tu, au la sivyo imani yake juu ya mungu haina maana. huyu mtoto akafariki. je, uwezo wa mungu na rehema ya mungu hubatilika kwa hayo?

Ikiwa huyo mtu anayeomba msaada kutoka kwa imam(a.s) ni mkandamizi na asiye na imani na haswali basi hastahili msaada wowote. kwa hivyo, huyo mtu akipata au asipate msaada haitaathiri ukweli wa imam(a.s) . haina umuhimu wowote kwa imam(a.s) ikiwa mtu anaamini uimam au dalili, alama, aya za qur'an na hadithi za kuthibitisha uimam wa hadhrat mahdi(a.s) kuukubali uimam wake humletea manufaa mwumini mwenyewe na kwa ajili ya wokovu wake binafsi. katika jambo la dini hakuna mtu anaye lazimishwa. baada ya mtume(s.a.w.w) , mwenyezi mungu ameteua warithi kumi na moja, mmoja baada ya mmoja, huku duniani kwa ajili ya mwongozo wa binadamu na wote wameuliwa kwa upanga au sumu na wadhalimu kama yazid, bani umayyah au bani abbas.

Zaidi ya hayo, hao maimam wlikuwa wanaonekana na kuishi pamoja na watu na vilevile kuonyesha miujiza mingi. wao (maimam) wameongoza waislaam, wachache tu waliwaamini na wengi wao (waislaamu) wakawaacha hao maimam(a.s) . hata kama huyo imam wa kumi na mbili (hadhrat mahdi a.s) angekuwa anaonekana angalikabiliwa na mambo hayo hayo. kwa hivyo mwenyezi mungu amemhifadhi kwa muda maalum.