ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE33%

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE Mwandishi:
Kundi: Imam mahdi (a.s)

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
  • Anza
  • Iliyopita
  • 20 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 22948 / Pakua: 4534
Kiwango Kiwango Kiwango
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

10

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 13

MAISHA MAREFU YA HADHRAT MAHDI IMAM WETU WA ZAMA HIZI

Hadhrat Mahdi(a.s) alizaliwa mwaka 255(a.s) na yu hai hadi leo. watu hutilia shaka juu ya maisha yake marefu ya zaidi ya miaka elfu moja. ubishi upo kwamba mtu akitimiza miaka mia huwa mdhoofu, hajiwezi na pungwani, kwa hivyo vipi mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 1100 huweza kuwa na afya nzuri? suala hili hujibiwa kwa aya nyingi za qur'an, hadithi na kwa dalili za kiakili. kwanza, ni jambo dhahiri lililothibitishwa kihistoria kwamba watu wengi wakiwemo waumini na makafiri miongoni mwao, wanajulikana kuwa wameishi zaidi ya miaka elfu moja, kwa hakika tutathibitisha katika sura hii kwamba baadhi ya hao wapo hai hadi leo.

Qur'an tukufu inapozungumzia juu ya nabii yunus imeeleza:

فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾ لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾

Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa." (37:143 - 144).

Nabii Yunus alikuwa binadamu. Ikiwa allah kwa uwezo wake anaweza kumweka hai binadamu tumboni mwa samaki bila huyo binadamu kupata mwangaza, upepo, chakula hata maji mpaka siku ya kiyama, kwa nini haiwezekani kwake kumweka mtume wake (au mrithi wa mtume wake) hai kwa muda wa miaka 1,000 au 2,000? hakuna mtu anayeweza kutia shaka juu ya uwezo wa mungu. kwa hivyo, swali linaloweza kuulizwa ni je, ni kweli hadhrat mehdi(a.s) yu hai, na kama yupo hai kwa nini haonekani? masuala hayo yamezungumziwa katika sura nyingine ya kitabu biki. hata masunni wamekubali na kuandika juu ya maisha marefu ya hadhrat mehdi(a.s) hayo pia katika sura nyingine katika kitabu hiki. wafuatao ni binadamu, mitume watukufu na vile vile washirikina na makafiri ambao walijaliwa maisha marefu mno: mitume na waumini:

Nabii Nuh miaka 2,000 hadhrat lukman miaka 3,800 nabii suleiman miaka 700 miaka nabii hood miaka 464 nabii adam ambaye aliishi miaka 930 na kuacha ayali ya watu .40,000 nabii shish miaka 900 bibi hawa (mke wa nabii adam) miaka 930 manabii wanne ambao wangali hai hadi leo mbinguni kwa maelfu ya miaka: nabii idris alichukuliwa mbinguni wakati umri wake ulikuwa umekwishatimia miaka 890 na yupo huko kwa miaka elfu kwa maelfu. nabii issa yupo mbinguni kiasi cha miaka 2,000. makafiri na washirikina: iblis tangu milele, anak binti wa nabii adam, miaka 3,000. ouj bin anak, miaka 3,600 mfalme jamshed miaka 1,000 zahaq tazi (mpwa wa jamshed) miaka 1,000 aaad bin our bin irem saam bin nooh miaka 1,200 shaddaad, miaka 900. cyrus, mfalme wa iran miaka 1,000 dajjal, miaka 1,375 na yu hai hadi leo.

Duniani nabii khidhr yu hai leo miaka 4,000 na hutembea dunia nzima. nabii elias yu hai kiasi cha miaka 4,000-5,000 na hutembea dunia nzima. hatimaye, hoja moja ya kirazini. ikiwa atatokea mtu mmoja akada kwamba anaweza kutembea juu ya maji, bila shaka watu wote watamzunguka na kuona kwamba kweli huyo anatembea juu ya maji na kushangazwa na kumwamini yeye kama mtu mtakatifu. lakini ikiwa baada ya rnuda mfupi atatokea mtu mwingine na kudai hilo, mshangao wa watu utapungua na hawatakuwa wengi kumwangalia mdai wa pili kama walivyomwangalia wa kwanza. dai kama hilo halitakuwa tena jambo la kushangaza. kama akitokea mdai wa tatu watu hawatashangazwa hata kidogo na hakitakuwa kitu kipya tena.

Vile vile, ikiwa watu wengi wamekwishaishi maisha ya maelfu ya miaka ya maelfu na kwa hakika manabii khidhr na elias wamekwishaishi maisha zaidi ya miaka 4,000-5,000, na wakiwa na afya nzuri huku wakitembea dunia nzima, basi haliwezi kuwa jarnbo la kustaajabisha kuwepo hai na mwenye afya nzuri kwa imam wetu wa kumi na mbili(a.s) kwa miaka 1,110-1,200. si ajabu wala kustaajabisha tena wakati wakristo na waislamu hukubali iblis na dajjal wapo hai hadi leo na agog magog wapo hai kwa tangu maelfu ya miaka ya zama ya alexander mkuu.

Kwa hakika manabii khidhr na elias wapo hai ijapokuwa kipindi chao cha unabii na uongozi umemalizika. hiki ni kipindi cha unabii wa mtume muhammad(s.a.w.w) na kanuni za kiislamu zilizopangwa kutokana na aya za qur'an zitadumu hadi siku ya kiyama. kwa hivyo, muda mrefu wa uhai wa manabii na mfano bora sana kuhusu maisha marefu ya imam wa zama hizi, hadhrat mehdi(a.s) aliyejaliwa na mungu.

Idadi kubwa ya wanazuoni wa kisunni wamenakili katika vitabu vyao habari juu ya kuzaliwa kwa hadhrat mehdi(a.s) katika mwaka 255 a.h. na kuwepo hai kwake hadi leo na vile vile kunakili habari za watu walionana naye. hata hivyo, wengi wao huamini kwamba hadhrat mehdi(a.s) hajazaliwa bado na atazaliwa katika siku za mwisho na yeye ndiye atatawala kwa insafu na usawa. sababu kuu kuhusu itikadi hii ni kwamba wakimkubali kuwa hadhrat mehdi(a.s) amekwishazaliwa watalazimika kumkubali kama yu hai na ameghibu na bidhaa yake itakuwa kuacha imani juu ya makhalifa kumi na wawili wanaowakubali, na kufuata itikadi ya ithnaasheri ambayo inaamini kwamba ukhalifa unakomea kwa hadhrat mehdi(a.s) , imam wa kumi na mbili.

Kwa wanaomkataa hadhrat mehdi(a.s) amekwishazaliwa na yungali hai, kuwa ana pahala pake anapoishi, watoto na wahudumu wake na kukutana na watu kwa sababu tu kwamba pahala anapoishi hapakuonyeshwa katika ramani na si rahisi kufika ni kujidanganya nafsi zao. papo hapo, hao wanaomkataa imam mehdi(a.s) wenyewe wanawaamini wale waliojificha na hawaonekani na kwamba maskani yao hayajaweza kutambulika. kwa mfano, katika kitabu cha "rehla eibne battuta" (ibne battutta aliyefariki 779 a.h.), ambacho kinaeleza juu ya safari yake ndefu kwenda arabuni, iraq, asia na china, katika juzuu la pili ukurasa 64 imenakiliwa kuwa: "katika safari yangu nilifika had! china ambako nilisimuliwa juu ya sheikh wa ajabu mwenye umri wa miaka 200, lakini hakuna mtu yeyote aliyemwona akila, kunywa wala kuzungumza na mtu mwingine. alikuwa na afya nzuri lakini hakufunga ndoa, akiishi ndani ya pango lakini akitoka nje wakati akitaka kufanya ibada. hivyo niliamua kwenda pamoja na sahibu zangu kumwona huyo sheikh pangoni mwake.tuiipofika tulimwona amesimama nje ya pango lake. Nilimsalimu na akanijibu. Baadaye akaushika mkono wangu na maneno yake yalifasiriwa kwangu na mkalimani kwamba mimi ninaishi upande wa magharibi wa dunia na yeye anaishi upande wa mashariki wa dunia.

Tena akaniambia kwamba katika safari yangu nimeona vitu vya kumstaajabisha na ninakumbuka kuzuru kisiwa ambamo kulikuwa hekalu moja na humo ndani nilimwona mtu ambaye alinipa sarafu kumi za dhahabu. nikamjibu kwamba tukio hilo nakumbuka vizuri sana. akanijibu kwamba mtu yule alikuwa yeye mwenyewe (sheikh). papo hapo nilimbusu mkono wake, naye akanyamaza kimya kwa muda mrefu. ghafla yeye akaingia ndani ya pango. tulimsubin nje kwa muda mrefu sana lakini hakutokea, kwa hivyo tuliamua kumfuata ndani lakini tuliambiwa kwamba hatutaweza kumwona tena. mtumishi wake alikuwa na vipande vya karatasi ambavyo alinikabidhi na humo ndani kuliandikwa kwamba sheikh amemkabidhi zawadi kwa ajili ya wageni na kwa hivyo mimi niondoke. niliposisitiza kutaka kumwona huyo sheikh mhudumu akaniambia kwamba hata nikisubiri miaka kumi sitaweza kumwona tena kwa sababu yeye haonani na mtu yeyote mara ya pili.

Mimi nilihisi kuwa huyo mtu alikuwa pale pale na mimi, ila alikuwa haonekani tu. sisi tuliduwazwa na tukatoka kwenye hilo pango. mwandishi aliendelea kusema "mimi niliwasimulia tukio hakimu shaikhul islam na awahududin bukhari nao walithibitisha kwamba mtu yeyote aliyemwona huyo sheikh (huko china) mara ya kwanza hawezi kumwona tena na yule mhudumu aliyewakabidhi hiyo bahasha ni huyo mtu mwenyewe lakini alibadilisha sura yake. sahaba wake mmojawapo alithibitisha kwamba aliwahi kujificha kwa miaka 50 na kujitokeza ghafla. hakuna cho chote katika pango hilo lakini mhitaji yeyote aombapo msaada hupatiwa pesa. huyo sheikh (wa china) alisimulia hadithi ya mtume(s.a.w.w) na kuzungumza mambo yaliyopita. yeye hudai kwamba angalikuwa wakati wa mtume mtukufu(s.a.w.w) angalimsaidia bila wasiwasi wowote. naye huwalaani vikali mno muawiya na yazid.

Zaidi ya hayo katika kitabu hicho hicho juu ya safari zake mwandishi aandika kwamba awahuddin bukhari alimwambia kwamba yeye (bukhari) aliwahi kuingia ndani ya hilo pango na huyo sheik alipeana naye mkono. anakumbuka kwamba alikuwa katika kasri kubwa iliyopambwa sana na sheikh huyo alikaa juu ya kiti cha enzi na kuvaa taji kichwani mwake huku akizungukwa na magashi. aliona mito hupita na vile vile miti yenye matunda matamu. aliokota tunda moja ili ale lakini ghafla alijikuta yuko peke yake nje ya hilo pango. mandhari yale yalipotea na akajikuta peke yake. papo hapo akaondoka. mambo ya kustaajabisha kama hayo yanayomhusu sheikh yamenakiliwa katika vitabu vya sunni na huonekana kwamba waislamu wapo tayari kumwamini huyo sheikh, kuhusu kujificha kwake na miujiza ya kustaajabisha wakati hata jina lake halifahamiki. lakini, bado wanatia shaka juu ya hadhrat mehdi(a.s) , wakati qur'ani tukufu, hadithi na historia na vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa kiislamu hutoa maelezo ya kutosheleza juu yake, kughibu kwake na miujiza yake.

SURA 14

KUGHIBU KWA MITUME

Sheikh Abu Jaafer Muhammad bin Babawayhi anayejulikana kwa jina la S heikh Saduq amenakili kwamba: aliambiwa na sheikh Najmuddin Abu Said Muhammad bin Hassan kuandika kitabu juu ya hadhrat Mahdi(a.s) na aliahidi kuandika atakapo rudi nyumbani tehran. aliporudi tehran hakuweza kuitimiza ahadi hiyo kwa sababu alishughulikia familia yake na matatizo mengine. siku moja aliota ndoto kwamba yuko makkah anatufu kaaba. 'alipomaliza kutufu mara yasaba na kubusu hajaril aswad (jiwe jeusi) alimwona mtu mtukufu mwenye uso uliokuwa unatoa nuru karibu na mlango wa kaaba. yeye alitia shaka kwamba huyo ni imam wake na akamwamkia ipasavyo. huyo mtu akamjibu na kumwuliza kwa sababu gani hakuandika kitabu juu ya kughibu (ghaibat). Sheikh akajibu kwamba amekwishaandika mengi kuhusu ghaibat lakini huyo mtu akasema: "la, sasa katika kitabu hicho eleza ghaiba ya manabii waliotangulia". huyo sheikh akaamka usingizini mwake na akalia. usiku kucha akakesha katika ibada na siku ya pili akaanza kuandika kitabu kuhusu [kughibu kwa imam(a.s) .

Katika sura hii, tutaelezea kwa ufupi kuhusu kujificha kwa manabii wawili. kujificha kwa Nabii Musa(a.s) sheikh sadooq ananakili kutoka kwa imam wa nne(a.s) kuwa kabla ya kufariki dunia nabii yusuf aliwakusanya ayali wake na wafuasi wake na kubashiri yatakayo tokea. akawaambia kwamba watapata rnateso makubwa katika utawala wa firaun. firaun atawafanya wanaume wao watumwa na kuwachinja na ataamrisha matunbo ya wake zao yakatwe ili watoto wauawe kabla ya kuzaliwa. allah atamwamrisha hadhrat mussa mwana wa lavi bin yakub kutokeza. atakuwa rnrefu wa kimo na mwenye uso wa rangi ya hudhurungi.

kwa muda wa miaka 400 chini ya utawala dhalimu wa firaun, waisraeli waliteseka. mtume alikaa mafichoni. Waisraeli waliomba mungu kwa bidii sana kuja kwa nabii mussa. baada ya muda mrefu walipata ishara ya kuz.aliwa kwa nabii mussa ambayo iliwapatia matumaini makuu. miongoni mwa hao waisraeli alikuwa mwanazuoni mcha mingu ambaye akiwatuliza hao waisraeli kuwabashiria juu ya kuzaliwa kwa nabii musa na ushindi wake juu ya firaun. Mateso ya firaun yaliendelea na ilimlazimu huyo mwanazuoni kujificha pangoni mwituni. Baada ya waisraeli kuchoka kuendelea kuvumilia mateso ya kubebeshwa magogo na mapande mazito mazito ya mawe walituma ujumbe kwa huyo mwanazuoni kuhusu mateso waliyopata. Wakamweleza kwamba maneno yake kuhusu ushindi ulikuwa 'faraja kwao na wakamwomba arudi kuishi nao na kuwafariji tena katika mateso.

Mwanazuoni huyo akawaalika Waisraeli hao kwake msituni. Wachache wakaenda kumtembelea. Usiku mmoja wenye mwangaza akatabiri kwamba wakati wa kuja. kwa mkombozi ulikaribia. walipokuwa wame.shughulika katika mazungumzo yao. wakamwona kijana mmoja mrefumwenye uso mwangavu mbele yao. Huyo mwanazuoni ambaye akizijua sifa za nabii musa papo hapo akasujudu kumshukuru mungu na waisraeli wote walienda sijda kumshukuru mola. walibusu miguu ya nabii musa na kueleza mateso waliyopata kutoka kwa firaun. Nabii Musa akawatuliza na kuwahakikishia kwamba ushindi umekaribia na akapoteamachoni mwao. Nabii Musa akaelekea madyan nyumbani kwa nabii shuaib na akafunga ndoa na binti wa nabii shuaib kwa sharti ya kumtumikia nabii shuaib kwa muda wa miaka kumi.

Kipindi cha kwanza cha kujificha kwa nabii musa ni sawa na kughibu kwa hadhrat mehdi(a.s) kwa muda mfupi. usumbufu kwa waisraeli ulizidi kuongezeka na subira ilikuwa inapungua. kwa hivyo, baada ya miaka kumi walienda kamwona huyo mwanazuoni ambaye aliwaarifu kuwa alikuwa amepata ilhamu kutoka kwa mwenyezi mungu ya kuwa ushindi wao ungepatikana katika miaka arobaini. kusikia hivyo, wao wakatamka "alhamdulillah" (sifa zote ziwe kwa mungu). Kushukuru huku kulimfurahisha mungu. naye akawapunguzia muda wa kuteseka uwe wa miaka ishirini. habari hii njema alipashwa mwanazuoni huyo na mungu. mwanazuoni akawaeleza waisraeli kuwa shukraini zao zimeleta faida hiyo. kusikia tu hivyo, waisraeli wakasema "rehema na huruma zote hutoka kwa mwenyezi mungu peke yake". Hapo tena mwanazuoni huyo akapata ilhamu ya kuwa mwenyezi mungu amewapunguzia huo muda uwe wa miaka kumi. waliposikia hayo wakasema kuwa hapakuwa na mwingine ila mwenyezi mungu mwenye uwezo wa kuwakomboa.

Punde si punde, wakamwona nabii musa ametokeza. wakasujudu kwa mwenyezi mungu na kumbusu miguu nabii musa ambaye aliwafikishia habari njema ya kuwa aliamrishwa na allah kujitokeza ra kumkabili firaun na akawaamrisha waondoke. baada ya hapo nabii mussa akaelekea kwenye kasri ya firaun ambaye akaamrisha wachawi wake wahudhurie. nabii musa akatoka misri na waisraeli 600,000, wake kwa waume, wazee na vijana, na akavuka mto. lakini firaun na wafuasi wake wengi walipojaribu kuuvuka mto wakazama. Hivyo inathibitika kujificha kwa hadhrat musa na majaribio na mitihani kwa wafuasi wake. vivyo hivyo wafuasi wa mtume muhammad(s.a.w.w) hujaribiwa na kutahiniwa. kujificha kwa nabii suleiman nabii dawood alirithiwa ufalme na nabii suleiman. baadaye nabii suleiman kwa amri ya mungu akajificha kutoka wafuasi wake na tatika kipindi hicho akapata taji ya ufalme. hadithi yake ni kama ifuatayo: nabii dawood aliimarishwa na mungu kumteua mwanawe wa mwisho suleiman kuwa mrithi wake. nabii dawood aliwajulisha wanawe na wafuasi wote juu ya uamuzi huo. waisraeli hawakupendezwa na uamuzi huo eti ulikuwa sio wa insafu kwa sababu nabii suleiman alikuwa mdogo kuliko wote na kaka zake walikuwa wenye uwezo na ujuzi.

Nabii Daudi akawaambia kwamba: hakuna yeyote anayeweza kutengua amri ya Mungu. Lakini kuwatosheleza akawaomba wanawe kuweka vitawi vilivyoandikwa majina yao katika chumba maalum, na vile vile akamwomba nabii suleiman kuweka vitawi vilivyo andikwa jina lake katika chumba hicho maalum. Siku ya pili wote walitakiwa wafike kuangalia kwamba vitawi gani vime mea na kuota majani na matunda. mwenye vitawi vilivyo mea na kuota majani na matunda ndiye atakuwa mrithi wake. wote waliridhika na wazo hilo na wakaleta vitawi. Siku ya pili walipofungua hicho chumba ilionekana kuwa vitawi vya nabii suleiman tu vilikuwa vimeota majani na kuzaa matunda. kwa hivyo wote walikubali uteuzi wa nabii suleiman.

Kuthibitisha zaidi ustahilifu wa Nabii Suleiman, nabii Daudi akamtahini elimu yake na uwezo wake kadamnasi ya waisraeli. akamwuliza "kitu gani humpa mtu furaha na utulivu wa moyo?" nabii suleiman akajibu "kusamehewa na mungu na kusameheana watu wenyewe". nabii dawood tena akamwuliza: "kitu gani chenye ladha mno?" "huba na urafiki wa ukweli kwani upendo na urafiki wa ukweli ni zawadi na rehema kutoka kwa mungu juu ya viumbe wake." (katika zamana hii zawadi ya mungu ya mapendano na urafiki imepotea na badala yake uadui, husuda na dhuluma imezagaa ambayo ni adhabu kutoka kwa mwenyezi mungu). nabii dawood alifurahishwa sana na ubora na usahihi wa jibu kutoka kwa mwanae. akawauliza waisraeli kama wameridhika kwamba nabii suleiman alistahili urithi kwa kila njia.

Baada ya kifo cha nabii dawood, nabii suleiman kutokana na amri ya mungu alienda kujificha. Katika kipindi hicho wafuasi wake waliteseka na kupata shida. nabii suleiman alikwenda kujificha katika nchi ya jirani ambako aliolea na kuishi na wakwe zake. Siku moja mkewe akamwambia kwamba anampenda sana kwa tabia zake, sifa na ukarimu wake. lakini huona dhila kutegemea wazazi wake na alimpa wazo la kujitafutia maisha yake na kujitetegemea kimapato. Nabii Suleiman akajibu kwamba: hakuwa na ujuzi wa kazi yoyote ya kujikimu kistahiki kwa sababu hakuhitajika kufanya kazi (kwa muda alikuwa mwana wa mfalme). Hata hivyo, aliahidi kwamba siku ifuatayo atakwenda sokoni kujitafutia mapato. alijiandaa kwenda kufanya kazi, lakini hakufanikiwa chochote. mkewe mwema akamtuliza moyo na akampa hima kwamba ajaribu sikuya pili.

Siku ya apili vile vile nabii suleiman akarudi mikono mitupu. tena mkewe akamsihi asivunjike moyo na kumhakikishia kwamba kutokana na rehema ya mungu atafanikiwa. siku ya tatu nabii suleiman akenda pwani na kumwomba amtumikie mvuvi kwa ujira wowote, mvuvi akakubali ombi na jioni yake akampa nabii suleiman samaki wawili kama ujira wake. nabii suleiman alifurahi na akamshukuru mungu nabii suleiman akamkata samaki huyo vipande na kumsafisha. tumboni mwa samaki mmoja nabii suleiman akapata pete moja. kwa vile alikuwa nabii, akatambua kuwa hiyo pete ni dalili yq ufalme. akasafisha hiyo pete akaiweka kwenye leso na kuweka mfukoni mwake. baadaye, akawachukua hao samaki wawili na kwenda nyumbani, ambako akamwona mkewe amefurahi sana.

Huyo mkewe akamwita baba yake akamwonyesha samaki wawili, nabii suleiman hapo akamwuliza baba mkwe " unajua mimi nani" huyo baba mkwe akajibu kwamba nabii suleiman alikuwa mtu mwema na yeye (bab mkwe) akimhesabu kama mwanawe lakini alikuwa hamjui kama yeye ni nani. Hapo nabii Suleiman akamsimulia kwamba yeye ni mwana wa Nabii dawood, mwana wa mfalme na mriuthi wa kiti cha ufalme. akatoa hiyo pete kutoka mfukoni mwake na kuivaa. papo hapo, majini na ndege kutoka pande zote walikusanyika bele yake. Nabii Suleiman akaelekea kwenda mji mkuu pamoja na mkewe na wakwe zake. Wafuasi wake walifurahi sana kumwona nabii Suleiman na wakamshukuru Mungu. Hii ni mifano miwili kuhusu kujificha kwa mitume. Wafuasi wa kila mtume walijaribiwa. kujificha kwa manabii Yusuf Ibrahim na Idris kumeelezwa katika vitabu vingine. Kwa kufupisha kitabu hiki hatuandiki habari hiyo humu.

11

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 15

HADHARAT MAHDI (A.S) NA WSIO WAISLAM

Allamah Gulam Husein Kanturi ameandika katika kitabu chake Intisarul islam (1917) kwamba: jamaa yake wa karibu Hakim Seyyid Zafer Mahdi alirudi lahore baada ya kwenda kuhiji pamoja naye. Mnajimu mmoja wa kihindi alimjia na akamwomba Seyyid amwulize swali. Seyyid alimwomba apokee zawadi bila ya kumuuliza swali, lakini huyo mnajimu alikataa kupokea zawadi bila kuulizwa swali. Huyo Seyyid alikerwa sana kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa mnajimu. lakini, hata hivyo, alimwuliza ili aweze kujua kwamba huyo mnajimu alikuwa anaweza kubashiri juu ya mambo yajayo, mambo ya kale na kumweleza nini alikuwa anafikiria.

Huyo mnajimu aliendelea kueleza juu ya jambo gumu; Seyyid huyo akamwomba amweleze juu ya mtu anayemfikiria kwa wakati huo. huyo mnajimu akafikiria na kufanya hesabu kwa uwezo wake wote lakini bila mafanikio. mwishowe akaweza kupata undani wa habari ya huyo anayefikiriwa; sura yake na sifa zake ambazo zilimshangaza yeye mwenyewe. huyo mnajimu akamwambia seyyid kwamba huyo mtu anayefikiriwa ni mfalrne wa dunia na akhera. ameng'amua kwamba hata akijitahidi maisha yake yote hataweza kujua habari kamili ya buyo mtu. akaeleza kwamba huyo ni mfalme wa duniani na akhera, na vile vile mfalme wa wafalme duniani.

Kusikia hivyo, huyo seyyid alifurahishwa sna na akasema kwakmba kwa wakati huo alikuwa akimfikiria imam mahdi(a.s) ambaye mnajimu aliweza kumtambua. hapo sayyid akamwamrisha mhudumu wake kuleta kashida nzuri sana na kumvika begani. mnajimu huyo alikataa kupokea zawadi yoyote na machozi yalimlenga lenga. "sitaki ,sitaki, sihitaji zawadi ya kashida. leo kutokana na suala lako nimepata ufumbuzi mkubwa na wenye thamani kuliko ufalme wowote duniani. Nimeongozwa kwenye njia ya ukweli na nimemfahamu bwana wangu wa kweli. Sina tama ya kitu chochote duniani" hapo mnajimu akalia sana na seyyid na wenzake wote pia wakalia.

Mwandishi (hayati) wa kitabu hiki alitembelewa katika mwaka 1930 a.d. na mnajimu mmoja kutoka bombay ambaye alikuwa na umri mkubwa, ndevu nyeupe na akijitambulisha kuwa ni husein brahmin. baniani wa aina ya brahmin alietokana na kizazi cha wafuasi wa iamam husein (a.s) alimwomba mwandishi amwulize suali lakini kwa vile hayati alikuwa na shughuli nyingi hakumjali. hata hivyo, mnajimu huyo aliendelea kukaa hapo na baada ya muda mfupi akaanza kumweleza habari ya maisha yake yaliyopita nay a baadaye, biashara yake, burudani, tabia zake njema na mbaya na vilevile afya yake, mwandishi alishangazwa; kwa hiyo, alianza kumsikiliza kwa makini. asilimia tisini na tisa ya aliyoeleza yalikuwa ya kweli. kwa hivyo, mwandishi akasema: "nimejishughulisha kwa muda mrefu sasa kujua habari za rafiki yangu. Nataka kujua yuko wapi, ana hali gani, yu hai au amefariki dunia, ana raha au ana shida na kama kuna uwezekano wowote wa kuonana naye. ukinipa jibu la kunitosheleza nitakupa rupia 25 za kihindi."

Kusikia hayo, mnajimu huyo akaanza kupiga mahesabu yake juu ya karatasi. kabla ya hayo alimsimulia mwandishi mambo mengi bila ya kufanya mahesabu yoyote. Mwandishi alipomwuliza kwa nini anafanya hivyo, mnajimu akamjibu kwamba aliweza kutoa habari zote kwa kutazama paji la uso wake, lakini sasa anahitaji msaada wa kalamu ili aweze kutafuta habari za rafiki yake. baada ya michoro mingi juu ya karatasi na mahesabu ya vidole na kuinamisha kichwa mara kwa mara kwa muda wa robo saa akasema: "Bila shaka rafiki yako unayemfikiria ni mtu mkubwa sana. yeye hutawala juu ya ulimwengu na mbinguni, hana wasiwasi wala shida yoyote ila fikra juu ya dini ya jadi yake. bila shaka yu hai na ana raha ya kila aina. karibu atajitokeza kutawala india, asia na dunianzima, na akaendelea kueleza sifa nyingi njema ya huyo rafiki (imam Mahdi a.s) ambazo zilimfurahisha mwandishi kiasi cha kumpa mnajimu rupia 25. mwandishi tena akamwuliza siku gani huyo mfalme atajitokeza ? akafanya mahesabu na akasema karibu sana katika muda wa miaka 25 au 30 atajitokeza na kushinda dunia nzima. (tanbihi: hakuna mtu yeyote anayeweza kutoa taarifa kwa uhakika siku gani mungu ataamua kumwamrisha imam mehdi(a.s) kujitokeza.

Hata hivyo mahesabu ya wanajimu yamethibitisha kuweko na kughibu kwa hadhrat mehdi(a.s) . muhaki-el-tusi, mwanazuoni maarufu wa shia ithnaasheria, alisumbuliwa sana na suala la "upekee wa mungu", ambalo aliulizwa na mlahidi (asiye amini mungu). alifanya mahesabu ya kinajimu kutafuta wapi hadhrat mehdi(a.s) atakuwa kwa wakati huo na akaona kwamba atakuwepo masjid-ul-kufa. kwa hivyo papo hapo aliondoka najaf, akakutana na imam(a.s) na akapata jibu la kumtosheleza na kutatua tatizo lake.

Imam(a.s) akamwuliza vipi alijua kwamba yeye yupo pale (masjid-ul-kufa). akamjibu kuwa kutokana na mahesabu yake, imam(a.s) akamsihi kwamba asirudie tena jambo hilo na muhakiki Attusi aliomba msamaha na kueleza kwamba alifanya hivyo kwa sababu ya tatizo alilo nalo na kuahidi kuwa asingerudia padri mmoja wa kiingereza alichapisha kitabu kiitwacho "maajabu arubaini ya siku zijazo" kutokana na kitabu cha nabii. daniel, kubusu vita, njaa na alama zingine zitakazo jitokeza katika siku za mwisho wa dunia. Kitabu hicho kilipendwa sana na kilichapishwa 1925 a.d., ambacho "hayati mwandishi alikisoma mwenyewe. padri huyo kaandika kuwa kutakuwa vita kuu katika siku zijazo na nchi tisa tu za ulaya zitasalimika.

Nchi ya kumi itakuwa syria ambayo mfalme wake yumkini atakuwa muhammad mehdi. huyo mehdi atakuwa mpinzani mkali wa ukristo. atavamia ulaya, atashinda na hatimaye kushinda dunia nzima. lakini atatawala kwa miaka saba tu na baadaye nabii issa atatokeza na ukristo utaenea duniani kote. hapo nabii issa atatawala miaka elfu moja. mwandishi (hayati) mwenyewe binafsi amekiona kitabu hicho toleo la l6 na kusoma yaliyomo, lakini katika matoleo yaliyo fuata jina la. mehdi limefutwa. padri huyo labda alitanabahi kwamba jina hilo huthibitisha ukweli wa uislam na wa imam mehdi(a.s) . Hata hivyo, ufutaji wa jina la Mahdi(a.s) hauwezi kukanusha ukweli. yeyote ambaye anaweza kupata nakala ya toeo la 16 la kitabu hicho ataweza kuhakikisha kwa dhati jina la imam mehdi(a.s) lilivyotajwa bayana.

Kwamba hadhrat mehdi(a.s) atatawala dunia nzima ni ushahidi madhubuti kuhusu kujitokeza kwake. kwamba baada ya utawala wake wa miaka saba utafuata uenezi wa ukristo duniani na nabii issa atatawala kwa miaka elfu moja si jambo la kuwababaisha wafuasi wa hadhrat mehdi(a.s) . ni imani yetu kwamba nabii issa atakuja baada ya muda mfupi wa kujitokeza kwa hadhrat mehdi(a.s) na dini pekee ya ukweli, uislam, itaenea dunia nzima. nabii isa kamwe hakudai kuwa mwana wa mungu na hakufundisha kwamba kuna mungu zaidi ya mmoja na huyu mungu ana mshirika yeyote. yeyote anaye amini katika upekee wa mungu, mtume muhammad(s.a.w.w) pamoja na manabii wote ni mwislamu. waumini wa nabii adam na manabii waliofuata ambao wamezingatia mafundisho yao, na kujizuia na maasi wote ni waislamu. katika qur'an tukufu kuhusu nabii Ibrahim Mungu anasema: "Amewaiteni jina la waislam ." (22:78).

Katika zaburi aliyoteremshiwa nabii dawood, aya ya nne, sura 19, murmuz, imeandikwa kwamba katika siku za rnwisho za dunia atakuja mtu mmoja ambaye atakuwa na kivuli cha wingu juu yake na ambaye ataeneza usawa na insafu.

katika kitabu cha mtume safyay, aya ya 3, imeandikwa: "Tahadharini kwamba katika siku za mwisho duniani atatokeza mtu mmoja ambaye atasababisha watu wote kumwabudu mungu mtindo mmoja (wote wataamini katika upekee wa mungu). Katika kitabu cha mabaniani (hindoo) fat ankal imeandikwa kuwa, "maisha duniani yatagawanyika katika vipande vinne, na kila kipindi kitagawanyika katika mida maalum na kila muda utakuwa wa kipindi cha miaka elfu nne. dunia itaendelea kwa muda wa miaka 256,000 na mwisho atatokeza mtu rnmoja muadham. huyo atatokana na kizazi cha viongozi wakuu wawili, mtume wa mwisho(s.a.w.w) na mrithi wake ajulikanaye kwa jina la bishan. Jina la huyo mtu atakaye tokeza itakuwa mwongozi (Mahdi) na atakuwa walii wa ram (Mungu).yeye atatawala dunia kama walivyotawala mitume walio pita na ataonyesha miujiza mingi; yeyote atakayemkubali huyo (Mahdi) ataokoka. Atakuwa na maisha marefa na ataishinda dunia nzima, atabomoa jumba la masanamu somnath na kutokana na amri yake sanamu kuu jaganath litapata uwezo wa kusema na baadaye litaporomoka. mwishowe kwa agizo lake masanamu yote yatavunjwa duniani kote.

Katika kitabu cha dini ya hindoo kiitwacho nasak, imeandikwa kuwa: "wakati dunia itakapo karibia kwisha kutakuwa ufalme ambamo ukweli na insafu itatawala. hazina zilizojificha chini ya bahari kuu, majabali au ardhi zitajitokeza na kuanza kuelezea siri zitajitokeza na kuanza kuelezea siri zote za duniani na mbinguni. katika kitabu cha dini ya waabudu moto "zand vapa zand" ambacho huaminiwa kama kataremshiwa nabii zardosh, kuhusu hadhrat mehdi(a.s) . vile vile katika vitabu vingine "kosab na azwasan' imeandikwa juu ya habari za imam mehdi(a.s) . Hakim jamasap katika kitabu kuhusu Mtume(s.a.w.w) na warithi wake amearidhia: "mtume mmoja atazaliwa katika milima ya uarabuni, atapanda ngamia na atakaa na kula na watumwa (hatakuwa mtu mwenye kiburi).

Yeye atafuta dini zingine zote, atashinda iran na kubatilisha dini ya waabudu moto. mrithi wa mwisho wa huyo mtume(s.a.w.w) atakayetokana na kizazi cha binti wa mtume(s.a.w.w) atatawala dunia nzima kwa uwezo aliopewa na mungu. utawala wake utaanzia makkah na utaendelea mpaka siku ya kiama. Atamkamata na kumfunga adui wa mungu, aharman (iblisi) na malaika kutoka mbinguni watafika kwake. atawafufua (waliokufa na kupata uhai kwa amri ya mungu) wema na waovu. atawapa jazaa wema na kuwaadhibu waovu. atamfufua baba yake nabii khidhr, nabii elias, mahras, lafvas baba wa ahasata lalis, nuh, shamasun na solan shamueel. Vile vile atawafufua namrood, firaun, hamman na kuwachoma moto."

Mengi yameandikwa kuhusu huyo mfalme (hadhrat Mahdi a.s.) wa siku za mwisho za dunia. katika vitabu vingi vya manabii wa zamani na vile vile katika vitabu vitukufu: torat, injiil na zabur na vile vile katika vitabu vingine vya dini zingine (zisizokuwa za kiislamu). zaidi ya hayo, wakristo, mayahudi, waabudu moto na mabaniani wanamsubiri mwongozi. wakristo humsubiri nabii issa na mayahudi nabii mussa. kwa hivyo, dunia nzima humsubiri huyo 'hadi' ambaye atasafisha dunia hii kutokana na maovu, fitina, ugomvi, vita, maafa, mateso au ulahidi na kueneza usawa wa uadilifu. kwa jumla, imani ya watu wote duniani huthibitisha imani yao juu ya "anayesubiriwa" na huimarisha hoja ya kwamba hao wote waliodai kuwa mehdi ni wadanganyifu tu. hawakuweza kutimiza chochote kama anavyotarajiwa kutimiza mehdi wa kweli.

Bayasajee aliandika kitabu 'bothiran sandhram' na gosai tulsidasji alitafsiri hicho kitabu katika lugha ya kihindi. Katika sura ya 12; ya tafsiri hiyo, ukurasa 212, ameandika: "Mimi sitaandika chochote kutokana na maoni yangu lakini ukweli mtupu ulioandikwa katika ved na purana. Katika muda wa miaka kumi nguvu zote zitamalizika na hakuna yeyote atakuwa na nguvu kama hiyo tena. badala ya hayo nyota itang'aa pahala patakatifu duniani. Miujiza yasiyoaminika yatafanyika na walii aliyekamilika atateuliwa duniani. yeyote atakayetamani kupata ridhaa ya mungu atawajibika kumtii muhammad. baadaye atatoka mtu atayejulikana kwa jina la mehdi. uwezo wote utakuwa wake (imenakiliwa kutoka gazeti la kisunni molvi-delhi- rasool, safar/rabiul awwal. 135z ah).

12

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

SURA 16

HADITHI KUHUSU MUDA WA KUSUBIRI (INTIDHAR) NA MAJARIBIO YA MUDA HUO

1. Hadhrat imam Ali Ridhaa(a.s) amessema kwamba: katika qur'ani Mwenyezi Mungu amezungumzia juu ya kugojea:

"Basi ngojeni; ngojea hapo. mimi vilevile nitakuwemo katika wale wanaongojea" (7:71).

2. Hadhrat Ali(a.s) amesema:"ngojea (msubiri) kutokeza imam mehdi; hivyo, yeyote atakayesubiri amri zetu atazawadiwa cheo cha shahidi anayegalagala katika damu yake" .

3. Hadhrat imam Jaafar Sadiq(a.s) ameeleza: "kutakuwa kipindi ambamo imam(a.s) atakuwa haonekani kwa wafuasi wake ambao itawabidi wavumilie mateso kutoka maadui wao kwa muda mrefa mmo siku ya kiyama watapewa habari njema kutokana na imani yao juu ya imam aliyeghibu, madhambi yao yatasamehewa na mema yao yatazawadiwa, na kwa sababu ya hao waumini duniani kutanyesha mvua na kuota vyakula. wasingekuwepo allah aangeliwateremshia adhabu hao wahalifu.

4. Imam Jaafar Sadiq(a.s) amesema kwamba:"Mwumini yeyote atakaye msubiri imam wake aliyeghibu kwa makini akifariki dunia atapewa jazaa ya kuishi na imam mehdi (a.s)." .

5. Imenakiliwa kutoka abdulhamid wasti kwamba yeye alilalamika kwa imam hadhrat muhammad baqir(a.s) kwamba kusubiri daima usiku na mchana kwa ajili ya mwokozi wa mwisho huathiri shughuli za kila siku maishani. imam akajibu "yeyote mwenye imani kuwa mungu atamwokoa kwa mkono wa wokovu, mungu mwenyewe humtimizia mambo yake. mwenyezi mungu amteremshie rehema huyo mwumini ambaye huvumilia shida kwa ajili yetu na hueneza hdithi zetu (mambo ya dini) kwa waumini wengine." adbulhamid akauliza tena, kama huyo mtu akifariki dunia kabla kujitokeza imans(a.s) je? imam akamjibu kwamba yeyote anaetamani kwamba atakapojitokeza hadhrat mehed(a.s) yeye awe mmoja wa wasaidizi wake kwenda vitani naye, atapata daraja kama ya mtu yule ambaye aliyeishi pamoja na hadhrat mehdi(a.s) na kupigana vita vya dini kutokana na amri yake (imam mehdi).

6. Mtume mtukufu(s.a.w.w) aliwaambia masahaba wake: " katika siku za mwisho za dunia wema wa mwumini mmoja utazidi wema wa watu 25 wenu". Masahaba wakalalamika kwamba wao walikuwa pamoja na mtume(s.a.w.w) na wamekwenda vitani naye. lakini mtume(s.a.w.w) akajibu, "siku za mwisho duniani waumini watakuwa wamezingirwa na maadui, kuzungukwa na maafa yaliyo sababishwa na maadui wao, lakini hata hivyo watakuwa imara katika imani yao kiasi hata nyinyi hamtaweza kulingana nao.

7. Imam wa tano, hadhrat muhammad baqir(a.s) . akiwahutubia marafiki na mashia juu ya dhuria ya mtume(s.a.w.w) akasema:"kumbukeni kwamba bila shaka rntatahiniwa katika uthabiti wa imani yenu na hiyo imani itatoweka bila nyinyi kufahamu. hilo jambo litakuwa kama mfano wa wanja, unapokuwa machoni hudhihirisha athari yake lakini hutoweka (yeyuka) bila mtu mwenyewe kufahamu. vilevile kati yenu watakuwa watu ambao asubuhi wataamka waumini lakini magharibi watakuwa wamepotelewa na imani yao bila wao wenyewe kufahamu" .

8. Hadhrat imam Jaafar Sadiq(a.s) amesema:"Wakati waovu namakafiri watakapoeleza (julikana) imani yao kadamnasi na waumini kudhihirisha imaniyao na tofauti baina ya waumini na makafiri kudhihirika, na watu kukata tamaa na kufa moyo ndipo imam (a.s) atajitokeza." maana ya hadithi hii ni kuwa yatakuwa majaribio magumu mno. wale watu ambao hawajali dini yao na kwa hivyo ni wazembe wa kuswali, au kufunga na kutekeleza maagizo mengine ya kidini, waliojishughulisha katika mambo ya dunia, na ni wadhalimu watafedheheka, na kwa upande mwingine wale wacha mungu waswalihina, wanaofunga mwezi wa ramadhani na kutekeleza maagizo mengine, wema, waoambao toba, wenye huruma na wathabiti katika imani yao watafaulu majaribio hayo.

9. Zaidi ya hayo imam Jaafar Sadiq(a.s) alimwambia Abu Basir kwamba: theluthi mbili ya wafuasi wa hadhrat hujjat(a.s) wataacha dini (kwa sababu ya dhambi zao na uzembe wao watakata tamaa na kwanza kuuliza ikiwa imam(a.s) yupo ughaibuni kwanini hajitokezi? Kwa hivyo, watapoteza imani yao juu ya imam(a.s) .

10. hadhrat imam muhammad baqir(a.s) amesisitiza kwamba bidii ifanywe ya kuwasimulia waumini hadithi ya kughibu na kuonekana tena kwa hadhrat imam mehdi(a.s) na wale wasioamini waache walivyo.

11. Hadhrat Ali(a.s) ameserna: "Nyinyi waumini ni kama nyuki. Watu duniani watafikiri nyinyi wanyonge, wanyenyekevu, na msiothaminika. hawatatambua sifa zenu. kumbukeni kwamba imam wenu hatatokeza mpaka nyinyi mtapo gombana na kila mtu kumwita mwenzie mwongo kutokana na mafarakano baina yenu. katika siku hizo za majaribio na mitihani wachache mno watabakia juu ya imani yao kwa uthabiti".

SURA 17

ALAMA ZITAKAZO DHIHIRIKA KATIKA SIKU ZA MWISHO ZA DUNIA

Wakati huu, yaani siku za mwisho (Akhiru Zamani) dunia imezingirwa na ulahidi, ukafiri, udhalimu, uovu na ukandamizi. binadamu amezongwa na ugomvi, vita, jefule na amepoteza imani juu ya mungu. Hata hivyo, kipindi hiki kinajulikana kama ni kipindi cha ustaarabu, elimu, utafiti, ufumbuzi na hekima. jumuia zingine zimefuata nyayo ya maendeleo ya kipindi hiki nasi twashawishika tufuate mtindo huo. Hata hiyyo, maendeleo yote ya zamana hii humezwa na ugomvi, vita na dhuluma.

Hadhrat Ali(a.s) amesema kwamba:katika siku za mwisho za dunia binadamu atapoteza busara yake na kupotoshwa katika mawazo yake, kila kilichokuwa chema atakiona kibaya na kiovu, lakini uzushi (bidaat) katika mambo ya dini, uasherati, uhayawani utatukuzwa . kuna hadithi nyingi zinazoeleza alama za siku za mwisho za dunia. nyingi zimekwisha dhihirika na zingine zinadhihirika. alama muhimu zitadhibirika katika muda mfupi kabla ya kujitokeza kwa imam(a.s) .

Hadithi chache kuhusu alama hizo ni kama zifuatazo:

1. Mtume mtukufu(s.a.w.w) ameridhia kuwa utafika wakati:

a) Mtu atamthamini mwanazuo (Aalim) kufuatana na mavazi mazuri yake.. (wataangalia mapambo ya mwanazuoni, mwanazuoni wa kweli atadharauliwa na atabaki fukara).

b) watu watatamani kusikia qur'ani kutokana na uzuri wa sauti ya wasomaji (qur'ani husikilizwa katika redio, na kaseti kutokana na uzuri wa sauti ya wasomaji).

c) watu watamwabudu mungu katika mwezi wa ramadhani tu. (katika miezi mingine usomaji wa qur'ani, ibada na saumu vitasahaulika). ukija wakati kama huo watu watateseka kutokana na watawala dhalimu.

2. hadhrat ali (a.s) amesema kwamba: "katika siku za mwisho za dunia mfalme wa iran atapinduliwa. ataomba msaada kutoka wasio waislamu. mashavu ya miguu yake yatakuwa membamba (yeye kwa maumbile atakuwa mnene mno). jina la mfalme huyo litakuwa ahmed (huyo alikuwa mfalme wa mwisho katika ukoo wa kajar). alipopinduliwa alikimbilia paris (ufaransa) na kufia huko huko. hata jina lake lilibashiriwa miaka 1300 kabla ya hadhrat ali(a.s) .

3. Hadhrat ali(a.s) vile vile alisema katika siku hizo waislamu watavaa vitambaa vya rangi shingoni mwao.

4. Vilevile amesema: "tehran itakuwa kama gereza na jahannam kwa waumini, lakini pepo kwa wale wasio na imani. hapatakuwa kitu chochote cha dini (uislam), wanaume watakuwa na tabia za kike na wanawake watadharau buibui, watatembea uso wazi masokoni na kujazana barabarani.

5. katika vyuo watakuwa wanafunzi wa aina mbili:

a) Wale ambao wanajifunza falsafia.

b) Wale ambao wanajifunza mambo yasiyo husiana na uislamu.

6. Hadhrat imam Jaafar Sadiq(a.s) amesisitiza kuwa: "Wakati nchi zinazingirwa na balaa, fitina na uovu inafaa mtu ahame kwenda kuishi katika jiji la qum, iran, ambalo litakuwa pahala pa amani na kuepukana na maafa, vyuo vya elimu vitahamia qum kutoka najaf, karibu na wakati wa kujitokeza kwa imam mehdi(a.s) . qum kutakuwa makao makuu ya kujipatia masomo ya dini ya kiislam.

7. Namna wanawake wanaotembea bila haya na kutojifunika huku kujipamba ni mojawapo ya alama za mwisho wa dunia. kuna hadithi nyingi kuhusu alama kama hii na tunazinakili chache tu.

a) Hadhrat Ali(a.s) amesema"Wanawake watakuwa hawana haya. watajihusisha na wanaume wasiokuwa waume zao. mitindo ya usukaji wa nywelie utafanana na nundu iliyojitokeza ya ngamia. wanawake hao katu hawataingia peponi" (kitu kilichobashiriwa na mtume(s.a.w.w) na maimamu kabla ya miaka 1300 kinaonekana dhahiri kabisa na kuthibitisha ukweli wa hadithi hizo, na wa uislaam).

Mwanazuoni huyo akawaalika waisraeli hao kwake msituni. wachache wakaenda kumtembelea. usiku mmoja wenye mwangaza akatabiri kwamba wakati wa kuja. kwa mkombozi ulikaribia. walipokuwa wame.shughulika katika mazungumzo yao. wakamwona kijana mmoja mrefumwenye uso mwangavu mbele yao. huyo mwanazuoni ambaye akizijua sifa za nabii musa papo hapo akasujudu kumshukuru mungu na waisraeli wote walienda sijda kumshukuru mola. walibusu miguu ya nabii musa na kueleza mateso waliyopata kutoka kwa firaun. nabii musa akawatuliza na kuwahakikishia kwamba ushindi umekaribia na akapoteamachoni mwao. nabii musa akaelekea madyan nyumbani kwa nabii shuaib na akafunga ndoa na binti wa nabii shuaib kwa sharti ya kumtumikia nabii shuaib kwa muda wa miaka kumi.

Kipindi cha kwanza cha kujificha kwa nabii musa ni sawa na kughibu kwa hadhrat mehdi(a.s) kwa muda mfupi. usumbufu kwa waisraeli ulizidi kuongezeka na subira ilikuwa inapungua. kwa hivyo, baada ya miaka kumi walienda kamwona huyo mwanazuoni ambaye aliwaarifu kuwa alikuwa amepata ilhamu kutoka kwa mwenyezi mungu ya kuwa ushindi wao ungepatikana katika miaka arobaini. kusikia hivyo, wao wakatamka "alhamdulillah" (sifa zote ziwe kwa mungu). kushukuru huku kulimfurahisha mungu. naye akawapunguzia muda wa kuteseka uwe wa miaka ishirini. habari hii njema alipashwa mwanazuoni huyo na mungu. mwanazuoni akawaeleza waisraeli kuwa shukraini zao zimeleta faida hiyo. kusikia tu hivyo, waisraeli wakasema "rehema na huruma zote hutoka kwa mwenyezi mungu peke yake". hapo tena mwanazuoni huyo akapata ilhamu ya kuwa mwenyezi mungu amewapunguzia huo muda uwe wa miaka kumi. waliposikia hayo wakasema kuwa hapakuwa na mwingine ila mwenyezi mungu mwenye uwezo wa kuwakomboa.

Punde si punde, wakamwona nabii musa ametokeza. wakasujudu kwa mwenyezi mungu na kumbusu miguu nabii musa ambaye aliwafikishia habari njema ya kuwa aliamrishwa na allah kujitokeza ra kumkabili firaun na akawaamrisha waondoke. baada ya hapo nabii mussa akaelekea kwenye kasri ya firaun ambaye akaamrisha wachawi wake wahudhurie. nabii musa akatoka misri na waisraeli 600,000, wake kwa waume, wazee na vijana, na akavuka mto. lakini firaun na wafuasi wake wengi walipojaribu kuuvuka mto wakazama. hivyo inathibitika kujificha kwa hadhrat musa na majaribio na mitihani kwa wafuasi wake. vivyo hivyo wafuasi wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) hujaribiwa na kutahiniwa.

Kujificha kwa nabii suleiman nabii dawood alirithiwa ufalme na nabii suleiman. baadaye nabii suleiman kwa amri ya mungu akajificha kutoka wafuasi wake na tatika kipindi hicho akapata taji ya ufalme. hadithi yake ni kama ifuatayo: nabii dawood aliimarishwa na mungu kumteua mwanawe wa mwisho suleiman kuwa mrithi wake. nabii dawood aliwajulisha wanawe na wafuasi wote juu ya uamuzi huo. waisraeli hawakupendezwa na uamuzi huo eti ulikuwa sio wa insafu kwa sababu nabii suleiman alikuwa mdogo kuliko wote na kaka zake walikuwa wenye uwezo na ujuzi.

Nabii dawood akawaambia kwamba hakuna yeyote anayeweza kutengua amri ya mungu. Lakini kuwatosheleza akawaomba wanawe kuweka vitawi vilivyoandikwa majina yao katika chumba maalum, na vile vile akamwomba nabii suleiman kuweka vitawi vilivyo andikwa jina lake katika chumba hicho maalum. siku ya pili wote walitakiwa wafike kuangalia kwamba vitawi gani vime mea na kuota majani na matunda.

Mwenye vitawi vilivyo mea na kuota majani na matunda ndiye atakuwa mrithi wake. wote waliridhika na wazo hilo na wakaleta vitawi. siku ya pili walipofungua hicho chumba ilionekana kuwa vitawi vya nabii suleiman tu vilikuwa vimeota majani na kuzaa matunda. kwa hivyo wote walikubali uteuzi wa nabii suleiman.

Kuthibitisha zaidi ustahilifu wa nabii suleiman, nabii dawood akamtahini elimu yake na uwezo wake kadamnasi ya waisraeli. akamwuliza "kitu gani humpa mtu furaha na utulivu wa moyo?" nabii suleiman akajibu "kusamehewa na mungu na kusameheana watu wenyewe". nabii dawood tena akamwuliza: "kitu gani chenye ladha mno?" "huba na urafiki wa ukweli kwani upendo na urafiki wa ukweli ni zawadi na rehema kutoka kwa mungu juu ya viumbe wake." (katika zamana hii zawadi ya mungu ya mapendano na urafiki imepotea na badala yake uadui, husuda na dhuluma imezagaa ambayo ni adhabu kutoka kwa mwenyezi mungu).

Nabii daudi alifurahishwa sana na ubora na usahihi wa jibu kutoka kwa mwanae. akawauliza waisraeli kama wameridhika kwamba nabii suleiman alistahili urithi kwa kila njia. baada ya kifo cha nabii dawood, nabii suleiman kutokana na amri ya mungu alienda kujificha. katika kipindi hicho wafuasi wake waliteseka na kupata shida. nabii suleiman alikwenda kujificha katika nchi ya jirani ambako aliolea na kuishi na wakwe zake. siku moja mkewe akamwambia kwamba anampenda sana kwa tabia zake, sifa na ukarimu wake. lakini huona dhila kutegemea wazazi wake na alimpa wazo la kujitafutia maisha yake na kujitetegemea kimapato. nabii suleiman akajibu kwamba hakuwa na ujuzi wa kazi yoyote ya kujikimu kistahiki kwa sababu hakuhitajika kufanya kazi (kwa muda alikuwa mwana wa mfalme).

Hata hivyo, aliahidi kwamba siku ifuatayo atakwenda sokoni kujitafutia mapato. alijiandaa kwenda kufanya kazi, lakini hakufanikiwa chochote. mkewe mwema akamtuliza moyo na akampa hima kwamba ajaribu sikuya pili. siku ya apili vile vile nabii suleiman akarudi mikono mitupu. tena mkewe akamsihi asivunjike moyo na kumhakikishia kwamba kutokana na rehema ya mungu atafanikiwa. siku ya tatu nabii suleiman akenda pwani na kumwomba amtumikie mvuvi kwa ujira wowote, mvuvi akakubali ombi na jioni yake akampa nabii suleiman samaki wawili kama ujira wake. nabii suleiman alifurahi na akamshukuru mungu nabii suleiman akamkata samaki huyo vipande na kumsafisha. tumboni mwa samaki mmoja nabii suleiman akapata pete moja.

Kwa vile alikuwa nabii, akatambua kuwa hiyo pete ni dalili yq ufalme. akasafisha hiyo pete akaiweka kwenye leso na kuweka mfukoni mwake. baadaye, akawachukua hao samaki wawili na kwenda nyumbani, ambako akamwona mkewe amefurahi sana. huyo mkewe akamwita baba yake akamwonyesha samaki wawili, nabii suleiman hapo akamwuliza baba mkwe " unajua mimi nani" huyo baba mkwe akajibu kwamba nabii suleiman alikuwa mtu mwema na yeye (bab mkwe) akimhesabu kama mwanawe lakini alikuwa hamjui kama yeye ni nani. hapo nabii suleiman akamsimulia kwamba yeye ni mwana wa nabii daudi, mwana wa mfalme na mriuthi wa kiti cha ufalme. akatoa hiyo pete kutoka mfukoni mwake na kuivaa. papo hapo, majini na ndege kutoka pande zote walikusanyika bele yake.

Nabii Suleiman akaelekea kwenda mji mkuu pamoja na mkewe na wakwe zake. wafuasi wake walifurahi sana kumwona nabii suleiman na walimshukuru mungu. hii ni mifano miwili kuhusu kujificha kwa mitume. wafuasi wa kila mtume walijaribiwa. kujificha kwa manabii yusuf ibrahim na idris kumeelezwa katika vitabu vingine. kwa kufupisha kitabu hiki hatuandiki habari hiyo humu.

5

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

MWANAMKE KATIKA QUR'ANI

Sasa tunataka kujibu swali iwapo Uislamu unamtazama mwanamke kuwa ni sawa na mwanaume kama binadamu au unamuona ni wa hadhi ya chini kuliko mwanaume. Falsafa maalum ya Uislamu juu ya haki za kifamilia. Kuhusiana na haki za mwanaume na mwanamke, Uislamu, una falsafa yake maalum ambayo ni tofauti, yale yaliyotokea miaka 1400 iliyopita na yanayotokea hivi sasa. Uislamu hauamini kuwa katika mambo yote mwanaume na mwanamke wana haki na majukumu yanayofanana.

Katika mambo fulani haki na majukumu yao ni tofauti na matokeo yake ni kuwa katika baadhi ya mambo nafasi yao inafanana na ya wanaume na katika baadhi ya mambo haifanani na ya wanaume. Hii sio kwa sababu Uislamu, kama falsafa nyingine, unamtazama mwanamke kwa dharau au jinsia yake sio bora kama ya mwanaume.

Uislamu unazitofautisha jinsia hizi mbili kwa sababu nyinginezo za msingi. Unaweza kuwasikia wafuasi wa mifumo ya Kimagharibi wakitaja kanuni za Kiislamu kama vile mahari, matunzo, talaka, ndoa za mitala na mengineyo, kuwa haya yote ni kama matusi kwa mwanamke na yanashusha hadhi yake. Wanawapotosha watu kuwa sheria na kanuni hizi hazina maana na ulazima na zinamfanya mwanaume aonekane ni bwana mkubwa. Wanasema kwamba katika kipindi chote cha historia, kabla ya karne ya 20, sheria na kanuni zote duniani ziliwekwa kwa kuzingatia kuwa mwanaume ni mwenye jinsia bora zaidi na kwamba mwanamke aliumbwa kwa maslahi na starehe ya mwanaume. Sheria zilizopitishwa na Uislamu pia ziko hivyo hivyo, zinampendelea mwanaume.

Wanadai kuwa Uislamu ni dini ya jinsia ya kiume. Hawamtambui mwanamke kuwa ni binadamu kamili. Hii ndio sababu haujampa haki sawa na mwanaume. Ungekuwa unamtambua kuwa ni binadamu kamili usingeruhusu ndoa za mitala (mke zaidi ya mmoja), usingehesabu ushahidi wa wanawake wawili kuwa ni sawa na wa mwanaume mmoja, usingeamuru gawio la mwanamke liwe nusu ya gawio la mwanaume, usingeamrisha papangwe bei ya mwanamke chini ya kivuli cha mahari na usingemfanya mwanamke awe tegemezi kwa mwanaume kwa upande wa matunzo, badala ya kufanya ajitegemee kiuchumi na kijamii.

Kwa kuzingatia yote haya ni dhahiri kuwa mafundisho ya Uislamu yanamtazama mwanamke kwa jicho la dharau. Uislamu unadai kuwa dini ya usawa lakini, katika mahusiano ya kifamilia hakuna usawa wowote uliozingatiwa. Wanashikilia kuwa katika suala la haki, Uislamu wazi wazi unampendelea mwanaume na ndio maana umempa miliki zote hizi. Tukipenda tunaweza kuweka hoja yao katika muundo wa kimantiki kuwa: Kama Uislamu unamhesabu mwanamke kuwa ni binadamu kamili ungekuwa umempa haki sawa na zinazofanana na zile za mwanaume, maadamu haujafanya hivyo basi haumhesabu kuwa ni binadamu kamili.

Usawa au kufanana? Hoja hii imejengwa juu ya msingi kwamba kwa vile heshima ya binaadamu ni sawa kwa mwanaume na mwanamke, hivyo lazima wote wapate haki zinazofanana bila kujali majukumu yao katika maisha. Hapana shaka, utu na heshima yao ni sawa kwao wao wote; wote wanapaswa kuwa na haki sawa. Lakini vipi kuhusu kufanana kwa haki zao?

Ikiwa badala ya kufuata kibubusa mawazo ya Kimagharibi tutaamua kufikiri sisi wenyewe, swali la kwanza linalokuja akilini ni iwapo kweli haki sawa zinamaanisha haki zinazofanana. Kwa kweli hayo ni mambo mawili tofauti. Usawa ni haki ya kuwa na daraja sawa kithamani na hadhi ambapo kufanana maana yake ni kulandana. Inawezekana baba akagawa mali zake kwa watoto wake watatu kwa usawa lakini sio kwa kulingana. Jaalia mali yake inajumuisha vitu mbali mbali kama vile maduka, mashamba na badhi ya mali zilizokodishwa. Baba kwa kuzingatia vipaji vyao na mambo ambayo kila mmoja anapenda, anaamua kumpa mmoja duka, mwingine shamba na wa tatu mali zilizokodishwa.

Anazingatia kuwa thamani ya mali aliyopewa kila mmoja wao ni sawa na wengine na kila mmoja amepewa kutokana na kipaji chake. Hivyo aligawa mali yake kwa usawa lakini sio kwa kulingana. Uwingi ni tofauti na ubora, na usawa ni tofauti na kufanana. Uislamu hauamini juu ya kulingana (uniformity) kwa mwanaume na mwanamke. Lakini wakati huo huo hauwapendelei wanaume katika maswala ya haki. Umezingatia kanuni ya usawa kati ya mwanamke na mwanaume lakini haukubaliani na kufanana kwa haki zao. Usawa ni neno linalifurahisha, kwa sababu linaashiria hali ya kutobagua. Lina utukufu maalum. Linaamsha na kuleta heshima, hasa linapohusiana na haki. Ni neno zuri lilioje 'Usawa na Haki.' Mtu yeyote mwema atafurahishwa na uzuri wake. Lakini hatuwezi tukaelewa ni kwa jinsi gani mambo yalifika hatua hii kiasi cha kuwa wengine ambao walikuwa vinara wa sayansi na falsafa nao wanataka kuingiza mawazo yao juu ya kufanana kwa haki kati ya wanawake na wanaume huku kwetu.

Hii ni sawa na mtu kuuza viazi vitamu kwa jina la mapeasi. Hapana shaka kuwa Uislamu haujatoa haki zinazofanana kati ya mwanaume na mwanamke katika mambo yote. Lakini pia haujaamuru majukumu na adhabu zinazofanana kwa jinsia hizi mbili. Yote kwa yote ni kuwa thamani ya jumla ya haki za mwanamke sio ndogo kuliko ile ya mwanaume. Tunataka kuthibitisha nukta hii. Hapa linazuka swali, kwa nini haki za mwanaume na mwanamke hazijafanana katika mambo yote. Je isingekuwa vizuri zaidi kama haki zao zingekuwa zinafanana katika mambo yote? Ili kulijadili hili swali kikamilifu, tutajadili chini ya vichwa vya habari vitatu. Mtazamo wa Uislamu juu ya nafasi ya mwanamke kutokana na maumbile yake. Athari za tofauti za kimwili kati ya mwanaume na mwanamke. Je, hili linasababisha tofauti ya haki zao pia? Ni nini falsafa ya sheria za Kiislamu, ambazo wakati fulani zinatofautisha kati ya mwanaume na mwanamke? Je falsafa hii bado ni thabiti?

Nafasi ya mwanamke katika utaratibu wa Kiislamu.

Qur'ani sio mkusanyiko tu wa sheria. Sio chombo cha sheria na kanuni kavu bila maelezo ya madhumuni yake. Ina sheria na pia ina historia, mawaidha ya kidini, maelezo ya malengo ya maisha, na maelfu ya mambo mengine katika sehemu mbalimbali, Qur'ani huelezea mambo yenye sura ya kisheria na katika sehemu nyingine hueleza lengo la maisha. Hufunua siri za dunia, mbingu, mimea, wanyama na wanaadamu. Huelezea siri za maisha na kifo, heshima na aibu, kupanda na kushuka, mali na umaskini.

Qur'ani sio kitabu cha falsafa, lakini kimeelezea kwa ufasaha sana maoni yake (Qur'ani) juu ya falsafa ya masomo matatu ya msingi; Ulimwengu, mwanadamu na jamii. Haiwafundishi wafuasi wake sheria peke yake, na haijishughulishi na mawaidha na nasaha (maonyo) peke yake, bali kwa kupitia tafsiri yake ya maisha (maumbile), huwapa wafuasi wake mtazamo maalum na namna pekee ya kufikiri. Msingi wa kanuni za Kiislamu juu ya masuala ya kijamii kama vile umiliki, serikali, haki za kifamilia n.k ni tafsiri ya maisha na mambo mengine tofauti tofauti.

Moja ya mambo yaliyoelezwa katika Qur'ani ni kuumbwa kwa mwanaume na mwanamke. Qur'ani haijakaa kimya juu ya jambo hili. Haijaacha mwanya kwa wadukuzi wa kifalsafa kuibua falsafa yao juu ya kanuni za mwanaume na mwanamke. Uislamu umetoa maoni yake juu ya mwanamke. Ili kujua maoni ya Uislamu juu ya mwanamke, tutazame Qur'ani inachosema juu ya tabia yake ya ndani. Dini nyingine pia zimelizungumzia suala hili, lakini ni Qur'ani peke yake ambayo katika Aya kadhaa inaelezea wazi wazi kuwa mwanamke ameumbwa kutokana na spishi za mwanaume, na wote mwanamke na mwanaume wana tabia za ndani zinazofanana.

Akimzungumzia Adam, Mwenyezi Mungu anasema;"Yeye (Allah) aliwaumba nyinyi wote kutokana na nafsi moja, na kutokana nayo (hiyo nafsi moja) akamuumbia mwenza wake (Suratun-Nisaa 4:1). Na juu ya mwanadamu kwa ujumla, Qur'ani inasema; "Amewaumbieni wake zenu kutokana na nyinyi. ' (Suratul Nisaa, Suratul Aali Imran na Suratul Ruum). Tofauti na vitabu vingine vya kidini hakuna sehemu yoyote katika Qur'ani ambapo imetajwa kuwa mwanamke ameumbwa kwa kutumia vitu duni au kuwa ana asili ya ukupe au ni wa asili ya upande wa kushoto. Uislamu hauungi mkono dhana ya kibiblia kuwa mwanamke ameumbwa kutokana na ubavu wa kushoto wa Adam. Uislamu hauna mtazamo wa dharau juu ya asili ya mwanamke na tabia zake za ndani.

Kuna nadharia nyingine ya dharau kwa wanawake iliyokuwa imeenea sana siku za nyuma, na imeacha alama mbaya katika siku za nyuma, na imeacha alama mbaya katika fasihi ya dunia. Kwa mujibu wa nadharia hiyo mwanamke ndio chanzo cha madhambi yote. Kuwepo kwake tu kunahamasisha uovu. Mwanamke ni shetani mdogo. Inasemekana kuwa katika kila dhambi na uhalifu uliotendwa na mwanaume kuna mkono wa mwanamke. Wanaume wenyewe hawatendi madhambi, ni wanawake wanaowasukumia kwenye madhambi. Pia inasemekana kuwa shetani hawezi kumwendea mwanaume moja kwa moja. Ni kupitia mwanamke ndio huwapotosha wanaume.

Shetani humchochea mwanamke na mwanamke humchochea mwanaume. Adam aliondolewa peponi kwa sababu ya mwanamke. Shetani alimshawishi Hawa, na ni Hawa aliyemshawishi Adam. Qur'ani imesimulia kisa hiki cha peponi lakini hakuna iliposema kuwa shetani au nyoka alipompotosha Hawa na Hawa akampotosha Adam. Haimlaumu Hawa wala haimuondoi katika hatia. Qur'ani inasema;"Tulimwambia Adam, 'Kaa Peponi; wewe na mke wako, na kuleni humo matunda popote mpendapo lakini msiusogelee mti ule msije kuwa miongoni mwa madhalimu ." (Suratul Baqara, 2:35). Inaweka kiwakilishi cha watu wawili. Pia Qur'ani inasema; "Kisha Shetani aliwatia wasiwasi." "Naye akawaapia (kuwaambia) kwa hakika mimi ni mmoja wa watoao shauri njema kwenu . (Suratul Aaraf 7:20-21).

Hivyo Qur'ani inapinga vikali dhana ya uongo iliyokuwa imeenea sana wakati wa kuteremshwa Qur'ani na miwangwi ambayo bado inasikika katika sehemu mbali mbali za dunia hii leo. Ilimuondoa mwanamke katika mashitaka kwamba yeye ni mchochezi wa dhambi na kwamba yeye ni shetani mdogo. Nadharia nyingine ya dharau kwa mwanamke ambayo imekuwepo ni juu ya nafasi ya kiroho ya mwanamke.

Ilidaiwa kuwa mwanamke hawezi kuingia peponi. Hana uwezo wa kiroho na msaada wa Mungu kumuwezesha kufanya hivyo. Hana uwezo wa kufikia ukaribu wa Mwenyezi Mungu kama mwanaume anavyoweza kufanya. Lakini Qur'ani katika Aya mbali mbali imesema wazi wazi kuwa malipo ya pepo na ukaribu na Mwenyezi Mungu havitegemei jinsia ya mtu.

Inategemea na imani na amali (vitendo), na hakuna tofauti kati ya mwanamke na mwanaume juu ya hili katika Qur'ani, wametajwa watakatifu wa kiume na watakatifu wa kike. Qur'ani imewatukuza wake wa Adam na Ibrahim na mama yake Nabii Isa na Musa. Imewataja wake wa Nuhu na Lut kuwa hawakuwa stahili ya waume zao na haijamshahau mke wa Firauni ambaye ametajwa kuwa ni mwanamke mtukufu aliyekuwa mikononi mwa mwanaume muovu. Katika visa vyake Qur'ani imeweka mizania. Mashujaa wake ni wa kiume na wa kike. Wakati, ikimzungumzia mama yake Nabii Musa, Qur'ani inasema, "Tulimjulisha mama yake Musa kwa kumwambia;'Muweke katika sanduku na mtupe katika mto. Mawimbi yatamfikisha ufukweni . (Suratul Taha; 20:39). Juu ya mama yake Issa, Qur'ani inasema kuwa alifikia daraja tukufu ya kiroho kiasi kwamba malaika walikuwa wakiongea naye wakati anasali. Alikuwa akipokea chakula kutoka peponoi. Daraja la kiroho lilimshangaza hata Zakaria, Mtume wa wakati huo.

Kumekuwa na mifano mingi ya wanawake mashuhuri na watakatifu katika historia ya Uislamu. Ni wanaume wachache tu wanaweza kufikia daraja la Khadija, mke kipenzi wa Mtume(s.a.w.w) na hakuna mwanaume anayefikia daraja la bibi Fatima Zahra, binti kipenzi wa Mtume isipokuwa Mtume mwenyewe na Imam Ali(a.s) . Ana daraja kubwa kuliko hata la watoto wake ambao ni Maimamu, na hata la Mitume wote isipokuwa Mtume wa mwisho.

Uislamu hauwabagui wanawake dhidi ya wanaume katika 'safari ya kumuendea Allah' isipokuwa humuona mwanaume kuwa mwenye kufaa zaidi kuchukua jukumu la utume, ambalo yaweza kuelezewa kama safari ya kurudi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa watu. Nadharia nyingine ya dharau kwa wanawake inahusiana na kujihini na kutooa/kutoolewa. Baadhi ya dini zinaona kuwa tendo la ndoa ni kitu kichafu, kwa mujibu wa imani ya wafuasi wake, wanaoweza kufikia kilele cha juu cha daraja la kiroho ni wale tu ambao watamaliza maisha yao yote bila kuoa/kuolewa. Kiongozi mmoja wa dunia wa kidini anasema, "Kateni mti wa ndoa kwa shoka ya ubikira.' Viongozi hawa wa kidini wanavumilia ndoa tu kama uovu wenye nafuu.

Kwa maneno mengine wanashikilia kuwa kwa kuwa watu wengi hawawezi maisha ya bila kuoa/kuolewa na inaeleweka kwamba hawataweza kujidhibiti na hivyo kujiingiza katika zinaa za wanawake/wanaume wengi, basi ni bora waoe ili wasije kukutana na mwanamke zaidi ya mmoja. Watu hawa wanatetea kukaa bila kuoa au kuolewa na kujihini kwa sababu wanaona tendo la ndoa si kitu kizuri. Wanaona upendo kwa mwanamke kuwa ni uovu mkubwa wa kimaadili.

Uislamu unapinga vikali upuuzi huu. Unaiona ndoa kuwa ni taasisi tukufu na kukaa bila kuoa/kuolewa kuwa ni uchafu. Kumpenda mwanamke ni sehemu ya tabia ya Mtume. Mtukutu Mtume amesema; "Napenda vitu vitatu, manukato, mwanamke na swala." Bertrand Russel anasema, "Dini zote, isipokuwa Uislamu, zinalitazama tendo la ndoa kwa jicho baya. Uislamu unalitazama kwa maslahi ya kijamii, umeliwekea utaratibu maalum na kulidhibiti, lakini haulitazami kama uchafu." Nadharia nyingine ya dharau kwa mwanamke ni kuwa mwanamke ameumbwa kwa maslahi ya mwanaume. Uislamu hausemi hivyo. Umeeleza malengo ya maisha kwa uwazi kabisa. Imeeleza kuwa dunia, mbingu, hewa, mawingu, mimea na wanyama vyote vimeumbwa kwa ajili ya mwanadamu. Haijasema mwanamke ameumbwa kwa ajili ya mwanaume. Kwa mujibu wa Qur'ani mwanaume ameumbwa kwa ajili ya mwanamke na mwanamke ameumbwa kwa ajili ya mwanaume.

'Wao (wanawake) ni nguo zenu na nyinyi (wanaume) ni nguo zao (2:187). Ingekuwa Qur'ani imeeleza kuwa mwanamke ni nyongeza (kiambatanisho) ya mwanaume na aliumbwa kwa ajili ya starehe yake (mwanaume) mtazamo huu ungekuwa umetazamwa katika sheria za Kiislamu, lakini Qur'ani haijasema hivyo. Hauyaelezei malengo ya maisha hivi. Haumuoni mwanamke kuwa ni kiambatanisho tu cha mwanaume. Ndio maana mtazamo huu haujazingatiwa katika sheria za Kiislamu. Nadharia nyingine ya dharau kwa mwanamke ni kuwa mwanamke ni uovu usioepukika. Katika siku za nyuma, watu walimtazama mwanamke kwa dharau sana na walimuona kuwa ni chanzo cha mikosi na aina zote za matatizo.

Kinyume chake Qur'ani imesisitiza kuwa mwanamke ni baraka kwa mwanaume na ni chanzo cha raha na faraja kwake. Kwa mujibu wa nadharia nyingine ya dharau kwa mwanamke ni kuwa hawakuthamini mchango wa mwanamke katika uzazi. Waarabu wa kabla ya Uislamu na baadhi ya jamii nyingine waliomuona mwanamke kama mfuko tu wa kukuzia mbegu ya mwanaume.

Sehemu mbali mbali ya Qur'ani imesema:'Tumewaumba kutokanana na mwanaume na mwanamke. ' Wazo hili limeelezwa katika Aya nyingine za Qur'ani. Hivyo Uislamu ulikomesha fikra hiyo kuwa mwanamke ni mfuko tu wa kukuzia mbegu ya mwanaume. Ni dhahiri sasa kuwa Uislamu hauna kabisa mitazamo yoyote ya kumdharau mwanamke. Sasa muda umefika wa kueleza kwa nini haki za mwanaume na mwanamke hazifanani. Ni kufanana, hapana, Ni kulingana, sawa.

Tayari tumeshasema kuwa katika suala la mahusiano ya kifamilia na haki za mwanamke na mwanaume, Uislamu una falsafa yake ambayo ni tofauti kabisa na ile iliyokuwa ada (kawaida), miaka 1400 iliyopita na ilivyo sasa. Pia tumesema kuwa hakuna ubishi wowote kuwa mwanaume na mwanamke ni sawa kama binadamu na haki zao za kifamilia zinapaswa kuwa sawa kithamani. Kwa mtazamo wa Uislamu wao wote ni binadamu na hivyo wana haki sawa. Nukta inayopaswa kuangaliwa hapa ni kuwa mwanaume na mwanamke, kwa sababu ya tofauti zao za kijinsia, wanatofautiana katika mambo mengi. Asili yao haitaki wafanane.

Nafasi hii inataka wasifanane katika haki nyingi, majukumu, wajibu na adhabu. Katika nchi za Magharibi jitihada inafanyika sasa kuzifanya haki na majukumu yao kufanana, na kupuuza tofauti zao za asili na za ndani. Hapa ndio kuna tofauti kati ya mtazamo wa Kiislamu na mfumo wa Kimagharibi katika nchi yetu, nukta inayobishaniwa ni suala la kufanana kwa haki sio usawa wa haki kati ya mwanamke na mwanaume. Usawa wa haki ni nembo tu ambayo imewekwa kwa makosa katika zawadi hii ya Kimagharibi.

Mwandishi wa kitabu hiki katika vitabu na hotuba zake mara zote amejiepusha kutumia nembo hii ya uongo na kamwe hajakubali kulipa jina la usawa jambo ambalo kiuhalisia ni kufanana kwa haki. Ulaya ya kabla ya karne ya 20 ni mfano dhahiri wa dhulma kwa mwanamke. Mpaka mwanzoni mwa karne ya 20 mwanamke wa Ulaya alinyimwa haki za kibinadamu katika maisha ya kila siku na kisheria. Hakuwa na haki sawa wala zinazofanana na mwanaume.

Ni katika muongo uliopita ambapo kutokana na harakati za pupa, wameanza kumpa haki zake za msingi, lakini bado hajaweza kupata haki zinazochukuana na maumbile yake na mahitaji yake kimwili na kiroho. Kama mwanamke anataka haki na usawa na furaha katika familia lazima alitupilie mbali wazo la kufanana kwa haki. Hiyo ndio njia pekee ya kuimarisha uchangamfu kati ya mwanaume na mwanamke.

Katika hali hiyo, sio tu kwamba mwanaume atazikubali haki za mwanamke, lakini pia atakuwa tayari kumpatia, na katika baadhi ya mambo atatoa haki nyingi zaidi tena bila kumdanganya. Halikadhalika hatudai kuwa katika jamii ya Kiislamu mwanamke anapata haki sawa na mwanaume. Mara nyingi tumesema kuwa ni muhimu kwamba nafasi ya mwanamke iangaliwe upya na apewe haki lukuki ambazo Uislamu umempatia, na ambazo amekuwa akinyimwa katika kipindi chote cha historia. Hata hivyo, haifai kuiga staili na mifumo ya Kimagharibi kibubusa, mifumo ambayo imesababisha madhara makubwa huko Magharibi kwenyewe.

Tunachodai ni kuwa kutofanana kwa haki kati ya mwanaume na mwanamke, kwa mujibu wa mipaka ya maumbile na tofauti zao ndio kutenda haki zaidi. Hukidhi mahitaji ya haki za asili vizuri zaidi, hutoa hakikisho kwa furaha ya familia na huisukuma jamii mbele katika njia ya maendeleo bora zaidi. Inaweza kukumbukwa kuwa tunadai kuwa haki ya asili inataka kwamba, katika baadhi ya mambo, kuwe na kutokufanana kwa haki ya mwanaume na mwanamke.

Kwa vile linahusiana na falfsafa ya haki, suala hili lina sura ya kifalsafa asilimia mia moja. Linahusiana pia na kanuni ya haki na usawa, kanuni kuu za sheria ya Kiislamu na falsafa ya uanazuoni wa Kiislamu. Ni kanuni ya usawa iliyoleta mafundisho ya kukubaliana kati ya akili na sheria ya Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa elimu ya sheria ya Kiislamu au tuseme ya Kishia, kama ikithibitika kuwa usawa unataka kuwa katika hali fulani, basi sura hiyo ndiyo itachukua sura ya kisheria bila kujali hoja zozote nyingine dhidi yake, kwani kwa mujibu wa mafundisho ya msingi ya Uislamu, sheria lazima katika hali yoyote isivunje au kuhalifu uadilifu wa asili na haki na za msingi.

Wanazuoni wa Kiislamu kwa kufafanua kanuni za usawa waliweka msingi wa falsafa ya haki, ingawa kufuatia matukio fulani ya kihistoria yasiyofurahisha, hawakuweza kuiendeleza kazi nzuri waliyoianza. Walikuwa ni Waislamu ambao, kwa mara ya kwanza walilitupia macho suala la haki za kibinadamu na kanuni za usawa, na walizitoa katika haki yake ya asili na kama kanuni zinazojitegemea bila kuathiriwa na sheria za kimikataba. Waislamu walikuwa vinara katika fani ya haki za asili za binadamu. Lakini hawakujaaliwa kuiendeleza kazi yao na hatimaye, baada ya karne nane, iliendelezwa na wasomi na wanafalsafa wa kizungu na wakajichukulia sifa hiyo.

Wazungu walileta falsafa za kijamii, kisiasa na kiuchumi na walijulisha watu, jamii na mataifa juu ya thamani ya maisha na haki za binadamu. Kwa maoni yetu mbali na sababu za kihistoria kulikuwa na sababu za kisaikolojia na kimkoa pia, ambazo ziliwazuia Waislamu wa Mashariki (Asia) kuendeleza suala la haki za msingi za binadamu.

Ni moja ya tofauti kati ya hulka ya nchi za Mashariki (Asia) na zile za Magharibi. Nchi za Mashariki zinazingatia maadili na za Magharibi zinazingatia haki. Mtu wa Mashariki ana upendo zaidi na anaamini kuwa lazima asamehe awe na moyo wa ubinadamu. Lakini mtu wa Magharibi anaamini kuwa kama binadamu lazima azijue na kuzilinda haki zake na lazima asiruhusu wengine wazipore. Utu unahitaji maadili na haki pia. Utu unahusiana na haki na maadili. Moja tu katika hizi haitoshi kuwa kigezo cha sifa bora za binadamu. Uislamu ulikuwa na hadi sasa unazingatia yote mawili haki na maadili.

Katika Uislamu, dhati, kusamehe, na matendo mema ni sifa takatifu na za kibinadamu. Lakini wakati huo huo mtu kujua haki zake na kuwa tayari kuzitetea, ni jambo takatifu na la kibinadamu. Hata hivyo, nchi za Mashariki kwa kiasi kikubwa zimekaliwa na Waislamu, na kwa hiyo, japokuwa awali yote yalikuwa yakizingatiwa maadili na haki lakini pole pole walijikuta wanabaki kushikilia maadili peke yake. Hivi sasa tunashughulikia suala la haki ambalo pia linaweza kuwa suala la kifalsafa na linafaa kujadiliwa kwa kirefu.

Inahusiana sana na maana halisi ya haki na ukweli halisi wa haki uadilifu na sheria uliokuwepo hata kabla ya kuwepo kwa sheria duniani, na ambao maana zake haziwezi kubadilishwa na sheria yoyote.

Montesquieu anasema, "Kabla ya sheria kutungwa na watu, kulikuwepo mahusiano yenye uadilifu baina ya watu kwa msingi wa sheria ambazo zilitawala mahusiano baina ya vitu vyote vilivyokuwepo. Ni kuwepo kwa mahusiano haya kulikosababisha kuundwa kwa sheria hizi. Kusema kwamba kabla ya watu kutunga sheria hapakuwa na uadilifu au dhuluma katika kuyaongoza na kuyadhibiti mahusiano ya watu ni sawa na kusema kuwa kabla ya mduara kuchorwa, nusu vipenyo vyake havilingani." Herbert Spencer anasema; "uadilifu unachaganganyika na kitu fulani mbali na hisia; yaani haki za msingi za binadamu. Lazima tuheshimu haki za binadamu ili uadilifu uwepo kiuhalisia." Wengi wa wasomi wa Ulaya wana mtazamo kuwa maazimio yote ya haki za binadamu yamechukuliwa kutoka katika haki za msingi za binadamu. Kwa maneno mengine, haki za msingi za binadamu zimechukuwa sura ya maazimio ya haki.

Kama tunavyojua, Montesquieu, Spencer n.k. wamesema kitu kimoja, juu ya uadilifu kama walichosema wanafalsafa wasomi wa Kiislamu juu ya msingi wa razini wa wema na uovu na kanuni ya usawa. Miongoni mwa Waislamu wamekuwepo wasomi ambao wamekana kuwepo kwa haki za asili na wanashikilia kuwa uadilifu ni jambo la kimkataba.

Halikadhalika, imani hii imekuwepo miongoni mwa wazungu. Mwanafalsafa wa Kiingereza, Thomas Hobbes alikana kabisa na akadai kuwa uadilifu sio kitu halisi. Azimio la haki za binadamu ni falsafa sio sheria. Ni kejeli kusema kuwa Azimio la Dunia la haki za binadamu ambalo linatoa hakikisho la usawa wa haki kati ya mwanaume na mwanamke, imeidhinishwa na Bunge la nchi fulani, wanaume na wanawake wa nchi hiyo wanapaswa kuwa na haki sawa.

Hata hivyo, si jambo lililo katika mamlaka ya kisheria kwa Bunge la nchi yoyote kuidhinisha au kukataa Azimio kwa vile yaliyomo humo kwenye Azimio, hayana sura ya kimkataba, hivyo hayaangukii kwenye mamlaka yake ya kisheria. Azimio la Dunia hushughulikia haki za asili, zisizoondosheka na zisizobatilishika za binadamu na kama inavyodaiwa na Azimio lenyewe, haki hizi ni sehemu muhimu na ya lazima ya heshima ya mwanadamu na zimebuniwa na mamlaka yenye nguvu ya maumbile yenyewe.

Kwa maneno mengine, haki hizi zimetolewa na kupewa wanaadamu na chanzo kile kile kilichowapa akili, utashi na heshima. Kama ni hivyo, hali ya mambo yaliyomo katika Azimio hili inalazimisha kuwa hakuna mamlaka yoyote ya binadamu inayoweza kuyabuni au kuyafuta. Sasa hapa linakujaje suala la kuidhinisha Azimio hilo katika chombo cha kutunga sheria? Kwa kusema kweli, Azimio la Haki za Binadamu ni falsafa sio sheria. Na kama ni hivyo inafaa kuidhinishwa na wanafalsafa na sio na watunga sheria (wabunge).

Hakuna Bunge ambalo linaweza kutunga falsafa kwa kulumbana na kupiga kura. Vinginevyo kwa nini, muswada unaoelezea nadharia ya Einstein juu ya 'relativity' (kwamba vipimo vya mwendo nafasi na wakati vinawiana) au nadharia nyingine inayosema kuwa kuna maisha katika karne nyingine haijapelekwa Bungeni ili ikaidhinishwe na chombo kitukufu? Kiuhalisia, sheria ya asili haiwezi kupitishwa au kukataliwa kama sheria ya kimkataba.

Kupitisha sheria ya asili (maumbile) ni sawa na kupitisha sheria kuwa kupandikiza chipukizi la mpeasi kwenye muepo (tufaa) kutafanikiwa lakini kupandikiza mpeasi kwenye mforosadi (mulberry) hakutafanikiwa. Kila azimio lolote linapotolewa na kikundi cha wanafalsafa, kila taifa hupeleka kwa wanafalsafa wake, na kama watalipitisha basi ndio wananchi wote wa nchi hiyo wanapaswa kuzingatia maelekezo yake kama ukweli wa ziada wa kisheria. Mamlaka ya kisheria itapaswa kutopitisha sheria inayopingana na maelekezo hayo.

Lakini mataifa mengine hayatalazimika kuyazingatia maazimio haya maadamu hayajathibitishwa, kwa mujibu wa maoni yao, kuwa haki hizo zipo duniani. Na zaidi ya haya, kwa vile suala hili haliwezi kupimwa au kujaribiwa, halihitaji vifaa au maabara n.k Ni suala la kifalsafa ambalo vifaa vyake ni ubongo, akili na nguvu ya hoja. Hata kama mataifa mengine yatalazimika kuwafuata walio wengi katika suala la mantiki na falsafa na wanahisi kuwa hawana uwezo wa kutosha wa kufikiri kifalsafa wao wenyewe, sisi Waislamu hatuwezi kufuata mfano wao.

Tumeonyesha huko nyuma kuwa tuna uwezo mkubwa wa kushughulikia masuala ya mantiki na kifalsafa. Kwanini tuwafuate wengine leo? Inashangaza kwamba wakati wasomi wa Kiislamu walitilia uzito sana kanuni ya uadilifu na haki za msingi za binadamu na wanazikubali kama sheria ya dini, bila kusita wala ubishi wowote, yote haya yakakubaliwa na akili (kuwa ni haki), leo mambo yameharibika kiasi cha kuwa tunataka wabunge waidhinishe kutambuliwa kwa haki za binadamu. Falsafa haiwezi kuthibitishwa kwa kujaza kuponi.

Ni kejeli na dhihaka kubwa kuliko hata hiyo iliyotangulia, kujaribu kuamua suala la haki za binadamu kwa kuandaa kura za maoni kwa wavulana wadogo na wasichana wadogo. Je ni akili kweli kuchapisha kuponi na kuwaambia wavulana na wasichana wadogo waijaze ili kujua asili ya haki za binadamu na kama ni za aina moja au mbili. Hata hivyo, hapa tunataka kulijadili suala la haki za mwanamke kwa utaratibu mzuri na kifalsafa, na kwa kuzingatia haki za msingi za binadamu.

Tungependa kujua kama kanuni zinazotaka wanadamu wote wapate na kufaidi haki zao za msingi walizopewa na Mwenyezi Mungu, zinalazimisha au hazilazimishi kuwa mwanaume na mwanamke wawe na nafasi moja sawa katika haki zao. Tunawaomba wasomi, wanafalsafa na wanasheria wa nchi yetu, ambao wanaweza kuwa ni watu pekee wenye mamlaka ya kutoa maoni juu ya suala hilo na kuziangalia hoja zetu kwa jicho la umakinifu.

Tutawashukuru sana kama watatoa maoni yao ya kimamlaka kukubaliana na hoja zetu au kuzipinga. Katika kulijadili suala hili, ni muhimu kwanza kujadili msingi wa haki za binadamu. Haki za mwanaume na mwanamke zitajadiliwa baadaye. Katika muktadha huu, haitakuwa makosa kuzungumzia kidogo harakati za kutaka mabadiliko katika karne chache zilizopita, ambazo zimeleta wazo la usawa wa haki kati ya mwanaume na mwanamke.

Tazamo fupi la historia ya haki za wanawake Ulaya. Mazungumzo ya haki za binadamu yalianza karne ya 17. Waandishi na wanafalsafa wa karne ya 17 na 18, kwa uvumilivu mkubwa, waliyatangaza na kuyaeneza mawazo yao juu ya suala la haki za msingi na zisizobatilishika za binadamu. Jeans-Jacques Rouseau,Voltaire na Montesquieu ni miongoni mwa waandishi na wanafalsafa hawa. Matokeo ya kwanza ya kivitendo ya kuenea kwa mawazo yao yalikuwa ni mapambano ya muda mrefu kati ya watawala na raia wa Uingereza. Mwaka 1688 Waingereza walifanikiwa kumshawishi mfalme akubali kuwapa baadhi ya haki za kisiasa na jamii walizokuwa wameziandika katika hati iliyojulikana kama 'The Bill of Rights.' Matokeo mengine muhimu ya kuenea kwa mawazo haya yalikuwa ni Vita vya Uhuru vya Wamarekani dhidi ya Uingereza.

Makoloni kumi na tatu ya Uingereza huko Amerika ya kaskazini yaliasi, kufuatia kuwekewa kodi kubwa sana, na hatimaye walipata uhuru wao. Mwaka 1776 mkutano ulifanyika Philadelphia, mkutano ambao ulitoa Azimio la Uhuru. Dibaji yake inasema; "Tunauchukulia ukweli huu kuwa dhahiri kwamba watu wote wameumbwa wakiwa sawa na kwamba wamepewa na muumba wao haki fulani zisizoondosheka, na kwamba miongoni mwa hizo ni haki ya kuishi, uhuru na kupata furaha au kufurahia.

Ili kuhakikisha kupatikana kwa haki hizi, serikali zinawekwa na watu, zinapata madaraka yao kutokana na idhini ya watawaliwa; na kwamba wakati wowote serikali ya muundo wowote inapokiuka malengo haya, ni haki ya watu kuibadilisha au kuiondoa, na kuweka serikali mpya, ikijengwa chini ya msingi wa kanuni hizi na kupata madaraka yake kwa utaratibu huu, itawahakikishia wananchi usalama na furaha yao.

Na lile linaloitwa Azimio la Haki za Binadamu lilitolewa baada ya Mapinduzi ya Ufaransa, lina kanuni fulani za jumla zinazoonekana kuwa sehemu muhimu na ya lazima ya katiba ya Ufaransa. Azimio lina dibaji na ibara 17. Ibara ya kwanza inasema kuwa watu wote huzaliwa wakiwa huru na hubaki huru katika maisha yao yote. Haki zao zinafanana. Katika karne ya 19 mawazo mapya yalitokeza katika uwanja wa haki za binadamu kiuchumi, kijamii na kisiasa. Haya yalisababisha kuibuka kwa ujamaa, ushiriki wa wafanyakazi katika faida na kuiondoa serikali kutoka mikononi mwa mabepari kwenda mikoni mwa wavuja jasho (wafanyakazi).

Hadi mwanzoni mwa karne ya 20, majadiliano yote yalikuwa yamejikita juu ya haki ya watu dhidi ya serikali au haki za tabaka la wavuja jasho dhidi ya waajiri na makabaila. Katika karne ya 20, suala la haki za mwanamke dhidi ya haki za manaume liliibuka. Ni juzi tu katika karne ya 20 ambapo Uingereza iliyokuwa ikijulikana kama demokrasia kongwe, ilipotambua usawa wa haki kati ya mwanaume na mwanamke. Ingawa Marekani kiujumla ilikuwa imezitambua haki za binadamu katika karne ya 18 katika Hati ya Azimio la uhuru, lakini bado haki ya kupiga kura kwa wote ilitolewa mwaka 1920.

Ufaransa pia ilitoa haki ya wanawake kupiga kura katika karne ya 20. Kwa kiasi fulani, katika karne ya 20 sehemu kubwa ya watu duniani walijitokeza kuunga mkono mabadiliko makubwa katika mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke, katika nyanja za haki na majukumu. Kwa mujibu wao lengo la uadilifu wa kijamii halingeweza kufikiwa kwa kufanya mabadiliko baina ya mataifa na kati ya wafanyakazi na waajiri na mabepari bila pia kuleta mabadiliko katika mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke.

Hii ndio maana dibaji ya Azimio la Haki za Binadamu kwa wote, lililotolewa mwaka 1948 linasema kwamba "Ambapo heshima ya utu wa mtu mmoja mmoja na usawa wa haki kati ya mwanaume na mwanamke" Machafuko yaliyosababishwa na maendeleo ya kuboreka kwa mashine (mitambo) katika karne ya 19 na 20, na hali mbaya ya wafanyakazi iliyofuatia, hasa kwa wafanyakazi wa kike, yalisababisha macho yaelekezwe kwenye masaibu ya mwanamke na ndio maana suala la haki zao lilizingatiwa sana.

Mwanahistoria anasema, "Kwa vile serikali ilikuwa haijali, masaibu ya wafanyakazi na tabia ya waajiri wao, mabepari walifanya walivyopenda". Wamiliki wa viwanda walikuwa wakiwaajiri wanawake na watoto kwa ujira mdogo sana, na kwa vile masaa ya kufanya kazi yalikuwa mengi mno, wengi wao waliugua magonjwa mbali mbali na wengine walikufa katika umri mdogo." Hii ilikuwa ni historia fupi ya harakati za Haki za Binadamu Ulaya.

Kama tunavyojua, ibara zote za Azimio la Haki za Binadamu ambazo ni mpya kwa wazungu, zilishawekwa na Uislamu katika karne 14 zilizopita, na baadhi ya wasomi wa Kiarabu na Kiirani katika vitabu vyao wamefanya ulinganisho kati ya mafundisho ya Uislamu na maelekezo (masharti) ya ibara hizi. Bado kuna tofauti katika baadhi ya vipengele vya maazimio haya na mafundisho ya Uislamu. Hili ni somo la kuvutia. Kwa mfano Uislamu unakubali usawa kati ya haki ya mwanaume na mwanamke, lakini haukiubali kufanana kwa haki hizi. Heshima ya mwanadamu na haki za binadamu. Ambapo kuitambua heshima na utu wa mwanadamu na haki zisizoondosheka za wanaadamu wote ni msingi wa uhuru, haki na amani duniani."

"Ambapo kutozingatia na kudharau haki za kibinadamu kumesababisha vitendo vya kishenzi na kuikasirisha dhamira njema ya mwanadamu na kuja kwa ulimwengu ambao ndani yake watu watafurahia uhuru wa kujieleza na imani, na uhuru wa kuondokana na hofu na shida imetamkwa kuwa ni hamu kubwa ya watu wa kawaida." "Ambapo italazimu, ikiwa mwanadamu hana kimbilio, kama njia ya mwisho, ana haki ya kuasi utawala wa kidhalimu, na kwamba haki za binadamu zitapaswa kulindwa na utawala wa kisheria." "Itakapobidi, kukuza maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa." "Ambapo watu wa Umoja wa Mataifa, katika heshima ya utu wa mwanadamu na katika usawa wa haki za mwanaume na wanawake, na wamedhamiria kukuza maendeleo ya kijamii na kiwango cha ubora wa maisha, katika hali ya uhuru zaidi." "Ambapo Baraza kuu la umoja wa Mataifa linatamka Azimio hili la Haki za Binadamu kwa wote kama kigezo cha wote cha kupimia mafanikio ya watu wote na mataifa yote ili hadi kufika mwisho kila mtu na chombo cha jamii, kwa kulizingatia Azimio akilini mwao walijitahidi kwa kufundisha na kutoa elimu, kukuza tabia ya kuheshimu haki hizi na uhuru na kwa hatua za kimaendeleo za kitaifa na kimataifa, ili kulinda utambulisho na zingatio miongoni mwa nchi wanachama wenyewe na miongoni mwa watu wa nchi zilizo chini ya mamlaka yao ya kisheria" Kama tulivyoona mwanzo, kila neno na kila sentensi katika azimio hili limepigiwa hesabu kali, limechukuliwa kwa uangalifu mkubwa. Hili ni dhihirisho la maw azo ya wanafalsafa na wanasheria wataka mabadiliko wa karne nyingi. Nukta muhimu za dibaji ya Azimio la haki za binadamu.

Azimio hili lina ibara 30, japo baadhi ya ibara zimezidi kiasi na baadhi ya nukta zimerudiwa katika ibara nyingi. Nuktra muhimu za ibara ni kama ifuatavyo: Binadamu wote wana haki za msingi zisizobatilishika na haki ya kutambuliwa utu wao. Utu wa binadamu na haki za binadmau ni kwa ajili ya wote na hivi havigawiki. Vinawahusu watu wote bila kujali rangi, utaifa au jinsia. Binadamu wote ni wanafamilia, hivyo hakuna aliyebora kuliko mwingine. Kuzitambua kikamilifu haki za binadamu na utu wa binadamu ni msingi wa uhuru, haki na amani. Yaliyomo katika Azimio yanaashiria kuwa chanzo cha matatizo yote, vita, vitendo vya kishenzi vinavyofanywa na mtu mmoja mmoja na watu dhidi ya wengine ni kutozitambua haki za binadamu na utu wa binadamu.

Kutozitambua huku huwalazimisha baadhi kuasi dhidi ya wengine na hivyo kuhatarisha amani na usalama. Hitajio na kinachotamaniwa kikubwa zaidi katika kufanikisha azma hii ni kuzaliwa kwa dunia ambayo ndani yake kutakuwa hakikisho la uhuru wa imani, usalama na hali nzuri kimaisha pamoja na hakikisho la kuondokana na ukandamizaji, hofu na umasikini. Azimio lenye ibara 30 limeundwa ili kufikia lengo hili. Imani juu ya heshima kwa utu wa mwanadamu na haki za msingi za kibinadamu lazima ikaziwe na kuingizwa pole pole akilini mwa watu wote, kupitia ufundishaji na elimu.

Heshima kwa utu wa mwanadamu. Kwa vile Azimio la Haki za Binadamu limeundwa kwa msingi wa heshima kwa utu, uhuru na usawa kwa nia ya kufufua haki za binadamu, lazima liheshimiwe na kila mtu makini. Sisi watu wa Mashariki (Asia) tumekuwa tukiamini juu ya kuuheshimu utu wa binadamu kwa muda mrefu. Uislamu umetilia sana mkazo katika kuuheshimu utu pamoja na haki za binadamu, uhuru na usawa. Hao waliyoyahamasisha haya, wanastahiki shukrani zetu.

Hata hivyo, haya ni maandishi ya kifalsafa yaliyoandikwa na mikono ya kibinadamu, sio malaika. Hivyo kila mwanafalsafa anayo haki ya kuyachambua na kuonyesha nukta zake dhaifu. Hapana shaka kwamba Azimio la haki za Binadamu lina udhaifu wake, lakini hivi sasa hatuna nia ya kuonyesha udhaifu huo. Badala yake; tunaonyesha nukta zake nzuri.

Msingi wa Azimio hili ni heshima ya utu wa mwanadamu kwa sababu, kwa kuwa nazo hizo, mwanadamu anapata haki fulani ambazo viumbe wengine hawapati, kwa vile hawana utu huo. Hii ndio nukta nzuri ya Azimio hili. Falsafa ya Kimagharibi inamshusha hadhi mwanadamu. Hapa tena tulikutana na swali kongwe la kifalsafa; Ni nini asili ya utu wa mwanadamu ambao humtofautisha yeye na farasi, ng'ombe na njiwa? Hapa ndipo inapodhirika migongano kati ya msingi wa Azimio la Haki za Binadamu na tathhmini ya Kimagharibi juu ya mwanadamu. Falsafa ya Kimagharibi toka zamani imekuwa ikimshushia hadhi mwanadamu.

Chanzo cha yote ambayo yalikuwa yakisemwa zamani kuhusu mwanadamu na cheo chake kitukufu ilikuwa ni katika Mashariki (Asia). Sasa mifumo mingi ya falsafa ya Ulaya inayakejeli yote hayo. Mwanadamu kwa mtazamo wa Kimagharibi, amekuja (duniani) akiwa na cheo cha mashine. Kuwepo kwa roho na asili ya ukarimu kumekataliwa.

Wazo kwamba ulimwengu una lengo la msingi linaonekana kuwa ni wazo la kupinga maendeleo. Sasa hakuna mtu katika nchi za Magharibi anayeweza kusema kuwa mwanadamu ni mfalme wa viumbe. Kwa mujibu wa nadharia ya sasa ya kizungu, imani hiyo ilikuwa ni chipukizi (tawi) la unajimu wa Ptolem, ambayo ilikuwa inaaminika kuwa dunia ndio kitovu cha ulimwengu na nyota ziliaminika kuwa zinaizunguka dunia. Sasa kwa kuwa nadharia hii imeshakufa na kwa kutoweka kwake, hakuna nafasi tena ya mwanadamu kudai kuwa ni mfalme wa ulimwengu.

Kwa mujibu wa Wazungu, hata zamani ilikuwa ni kwa sababu ya ubinafsi wake ndio maana akajifanya kuwa bora kuliko viumbe wengine. Maisha yake ni ya kiumbo tu. Mtu akishakufa, mwili wake huoza na hapo ndio mwisho wa habari! Mzungu haamini kuwa roho inaweza kuishi peke yake. Kwa mtazamo huu, hajioni kuwa na tofauti yoyote kati yake na mimea na wanyama. Kwa hiyo anaona kuwa hakuna tofauti yoyote ile ya msingi kati ya asili ya vipawa vya kiakili na kiroho vya mwanadamu na sifa nyingine za maada kama vile joto, linalotoka kwenye makaa ya mawe.

Maisha kwa viumbe vyote, ikiwa ni pamoja na mwanadamu, yanamaanisha mapambano yasiyokwisha ya kuweza kuishi. Hii ndio kanuni ya msingi ya maisha. Mwanadamu mara zote amekuwa akipambana ili awe mshindi katika mapambano haya, na ili kuilinda nafasi (hadhi) yake amebuni kanuni za kimaadili kama vile uadilifu, wema, ushirikiano, uaminifu n.k. Kwa mujibu wa baadhi ya matapo yenye nguvu ya kifalsafa ya Kimagharibi mwanadamu ni mashine tu inayosukumwa na maslahi ya kiuchumi. Dini, maadili, falsafa, sayansi, fasihi na sanaa nyingine, vyote ni vikorombwezo tu. Miundo mbinu yake ni mfumo wa uzalishaji mali na ugawaji wa mali, na mambo haya ndiyo yanayotawala nyanja zote za maisha ya mwanadamu.

Sio hivyo tu, baadhi ya wanafalsafa wa Kimagharibi wana mtazamo kwamba vipengele vya kijinsia ndivyo vyenye ushawashi halisi wenye nguvu katika shughuli zote za mwanadamu. Maadili, falsafa, sayansi, dini na sanaa vyote hivyo ni miundo ilyobadilishwa na kurekebishwa ya jinsia. Hatuelewi ni jinsi gani tunaweza kuzungumzia utu wa mwanadamu na haki za msingi na ni jinsi gani tunaweza kuzifanya kuwa msingi wa matendo yetu yote, ikiwa tunakana kwamba maisha hayana lengo lolote la msingi, ikiwa tunafikiri kuwa mapambano ya kuweza kuishi na mapambano yatakayombakisha mwenye nguvu zaidi ndio sheria pekee zinazotawala maisha, ikiwa tunaamini kuwa mwanadamu ni mashine tu kama mashine nyingine (lakini) iliyopewa mikono ya binadamu, ikiwa tunashikilia kuwa hakuna roho na kwamba yote yanayozungumzwa juu ya roho ni kuzidisha chumvi kwa kiroho, ikiwa tunashikilia kuwa maslahi ya kiuchumi na ngono ndiyo yanayosukuma shughuli zote za mwanadamu, ikiwa tunajali kuwa wema na uovu ni dhana linganifu tu, ikiwa tuna maoni kuwa muongozo wa kimungu wa asili na wa kimaono ni upuuzi na ikiwa tutasema kuwa mwanadamu ni mtumwa wa matamanio yake na anaweza kunyenyekea kwa nguvu tu.

Maoni ya Kimagharibi juu ya mwanadamu yanapingana na utu wake na yameiporomosha hadhi yake katika kila pembe katika pembe ya sababu ya kuumbwa kwake, umbile lake, nia yake na dhamira yake. Baada ya kufanya yote haya, nchi za Magharibi zimetangaza Azimio la hali ya juu lenye busara kuhusu utu wa mwanadamu na cheo na haki za msingi zisizoondosheka na takatifu, na wametoa wito kwa kila mtu kulitekeleza hilo. Kabla ya kutoa Azimio hili la hali ya juu zuri na lenye busara, nchi za Magharibi kuhusu utakatifu na haki za asili za mwanadamu, wangeipitia upya tafsiri yao juu ya mwanadamu.

Tunakiri kuwa sio wanafalsafa wote wa Kimagharibi wana mtazamo huu. Wengi wao wanamtazama mwanadamu kama tunavyofanya sisi watu wa Mashariki (Asia). Tuna mtazamo ambao watu wengi wa Magharibi wanaung'ang'ania na ambao unawashawishi watu duniani kote. Azimio la Haki za Binadamu lilipaswa litolewe na wale ambao wanamuona mwanadamu kuwa ni zaidi ya roboti ambao wanafikiri kuwa malengo yake hayaishii kwenye silika za kibinadamu na kinyama na ambao wanaamini juu ya dhamira ya kibinadamu. Azimio la Haki za Binadamu lilipaswa litolewe na watu wa Mashariki ambao wanaamini kuwa mwanadamu ni khalifa wa Mwenyezi Mungu katika dunia. Qur'ani Tukufu inasema:

"Kwa hakika nitamuweka khalifa katika ardhi." (2:30) Ni wale tu wanaoamini kuwa mwanadamu ana lengo na makusudio ndio wanaoweza kuzungumzia juu ya haki za binadamu.

"Enyi watu, bila shaka lazima mjitahidi sana kwa ajili ya Mola wenu, kujitahidi kukubwa kabisa hadi mtakapokutana Naye." (84:6). Azimio la haki za binadamu linaifaa mifumo ile ambayo inaamini kuwa mwanadamu ana muelekeo wa asili wa kutenda mema;"Naapa kwa roho na kwa yule aliyeifanya kuwa timilifu na aliyeipa ujuzi (elimu) juu ya uovu na uchamungu." (91:7-8). Azimio la haki za Binadamu haliafikiani na njia za fikra za Kimagharibi.

Kufikiri kwao kunazifaa tu tabia za watu wa kimagharibi ambao huua hisia za kibinadamu, hucheza na tabia za wanaadamu, hujali fedha zaidi kuliko mtu, huabudu mashine (mitambo), huona mali kama Mungu na huwanyonya wanaadamu wengine. Ubepari umepata nguvu na mamlaka yasiyo na kikomo kiasi cha kuwa ikitokea kuwa milionea mmoja atamrithisha mbwa wake kipenzi mali zake, mbwa huyo ataheshimika kuliko watu, watu wengi tu watamtumikia mbwa huyo kama makatibu muhtasi na makarani na wataonyesha heshima ya hali ya juu kwa mbwa huyo.

Leo hii swali kubwa la kijamii kwa mujibu wa Qur'ani, ni je, mwanadamu amejisahau mwenyewe? Sio tu kwamba amejisahau yeye tu bali amemsahau hata Mungu wake pia. Akili zake zote amezielekeza kwenye maisha ya kidunia na mali na amepuuza kabisa kujifikiria na kujipima. Anafikiri kuwa amepoteza roho yake. Mawazo kama haya ni ya hatari sana na yanaweza kuondoa kabisa thamani ya utu na ubinadamu.

Ustaarabu wa sasa unaweza kuzalisha kila kitu chenye ubora wa juu kabisa, lakini hauwezi kumtengeneza mtu halisi. Gandhi anasema kuwa mzungu anastahili kuitwa bwana wa dunia. Anamiliki raslimali zote za kidunia na anafanya vitu ambavyo mataifa mengine wanaamini kuwa ni Mungu tu anayeweza kuyafanya.

Lakini ni kitu kimoja tu ambacho mzungu hawezi kukifanya nacho ni kujifikiria na kujipima. Hilo peke yake linatosha kuthibitisha kutokuwa na maana kwa kumeremeta kwa ustaarabu wa kisasa. Kama ustaarabu wa Kimagharibi umemtaabisha mzungu kwa ulevi na ngono basi ni kwa sababu ya kujisahau na kujipoteza badala ya kujitafuta. Uwezo wake wa kivitendo wa kuvumbua, kugundua na kuzalisha zana za kivita unatokana na kujikwepa nafsi yake na sio kwa sababu ya uwezo wake wa kipekee wa kujidhibiti. Kuogopa kwake upweke, ukimya wake na tamaa yake ya fedha kumemfanya asiweze kusikia sauti yake ya ndani.

Kushindwa kwake kujitawala ndio kichocheo chake cha kuuteka ulimwengu. Hii ndio sababu kila anakokwenda mzungu hueneza mitafaruku na ghasia. Kama mtu akipoteza nafsi yake mwenyewe, hakuna faida yoyote kuushinda ulimwengu. Wale ambao wamefundishwa na Injili kuwa wamisionari wa ukweli, upendo na amani, wanazunguka kutafuta dhahabu na watumwa. Badala ya kutafuta msamaha wa Mwenyezi Mungu na uadilifu katika ufalme wa Mungu, kama Injili inavyofundisha wanatumia dini yao kama kifutio cha madhambi zao (kwa kumfanya Yesu, Mtume mtukufu wa Mungu kuwa kafara ya dhambi kwa kila amuaminiye). Badala ya kufundisha na kuhubiri ujumbe wa Mungu, wanawadondoshea mabomu watu wasio na hatia. Hii ndio sababu, Azimio la Haki za Binadamu linakiukwa na nchi za Magharibi. Falsafa inayofuatwa na watu wa Magharibi katika maisha yao kivitendo inafanya kushindwa kwa Azimio hili kusiepukike.

4

5

6

7

8

9