13
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
SURA 18
BIBI, AZALI, BAHI KAMA VILE HUKO PUNJAB
Mirza alifanya daawa ya utume na umehdi, huko iran, kabla ya miaka 100, yalizuka madhehebu mapya ya babi, azali na bahai. wafuasi wa madhehebu hayo hadi leo wako iran na india. katika kitabu kidogo kama hiki haiyumkiniki kueleza maisha ya babi azali na bahai na ubatilisho wa madai yao. hata hivyo, tutaeleza kwa muhtasari historia ya madhehebu haya.
Mwanzilishi wa ubabi alikuwa mirza ali mohammad mirza raza shirazi. vichepuko vya madhehebu ya babi vikawa madhehebu ya azali na bahai yakimhesabu baab kuwa mtume na ishara ya habari njema kwa sababu alibashiria juu ya ndugu hao wawili. katika mabahai, baab hujulikana kuwa ni mtu mmoja tu aliyebaki hai kutokana na dhuria ya mtume(s.a.w.w)
na mirza husseinali ni nabii issa wa pili anaye subiriwa. baada ya kifo cha mirza muhammad baab, wafuasi wake hawakumtambua au kumkubali mirza yahya subhe azal au mirza husseinali kama walivyomkubali baah. mirza alidai kwamba baab alitangaza kuja kwake (mirza yahya). Mirza husseinali baha mwanzoni alimkubali ndugu yake na kueneza madhehebu yake kwa niaba ya nduguye lakini baadaye akageuka na kutangaza kuwa madhehebu ya nduguye ni udanganyifu na kubatilisha madai yake kuwa ni ya uongo kuanza kueneza madhehebu yake mwenyewe ya ubahai.
Kutokana na mafarakano baina ya ndugu wawili hao, damu nyingi ilimwagika. Wafuasi wa mirza yahya wakajitambulisha kuwa maazali na wa mirza husseinali kuwa mabahai siku hizi wamisionari wa kibahai wameenea kote katika mabara ya asia, ulaya na afrika. Vipi mtu anaweza kuwa na daawa ya kuteremshiwa wahyi wakati yeye mwenyewe amebadilisha dini yake mara tatu! Kwanza alikuwa shia ithnaasheri, baadaye akaungana na madhehebu ya ubabi na baadaye kuwa misionari wa madhehebu ya nduguye mirza yahya azali. Hatimaye akawa mwanzilishi wa madhehebu yake na kujitangazia kuwa yeye ni mehdi anayesubiriwa. Madhehebu yake ni mchapuo wa madhehebu ya ubabi.
Albayan husemekana ni kitabu alichoteremshiwa mwanzilishi wa madhehebu ya baab. maadili kadhaa kutoka kitabu hicho yanaorodheshwa hapa. Itadhihiri kwamba maadili yote ni kinyume cha maagizo ya qur'an na hadithi.
1.
Swala ya jamaa hukatazwa.
2.
Badala ya raka 17 za kila siku mtu aswali rakaa tisa tu na kuna mabadiliko mengi katika hizo swala.
3.
Kufunga katika mwezi wa ramadhan kumekatazwa na badala yake mtu afunge siku 19 tu kuanzia tarehe 1 machi (asrarul akaeed, uk. 830.
4.
Kuoga tohara baada ya mtu kujamiiana na mwanamke au kutoka manii usingizini sio lazima.
5.
Mwanamke yeyote, ila mama mzazi, huweza kufungwa naye ndoa.
mwanzoni, mwanzilishi wa madhehebu ya babi mirza muhammadali baab alikuwa shia ithnaasheri. alikuwa mwanazuoni wa kidini huko najaf-iraq. Baadaye alikwenda iran na akaanza uombezi. alikuwa akisimama kichwa wazi juani kwa muda mrefu. mwishowe, akapotelewa na akili na kujitangazia kila daawa. Katika 1844 a.d., mirza ali muhammad akaanza kutangaza dini yake. Akatangaza yeye ni mlango wa mungu (huwezi kumfikia mungu bila kupita kwake), mti wa toor, mehdi anayesubiriwa na mwishowe nabii.
Katika majadiliano bayana na mwanazuoni wa shia itbnaasheri akatangasza "kauli zangu ni bora na zenye ufasaha zaidi kuliko qur'ani. Madhehebu yangu hubatilisha uislaam. Tahadharini mimi nitawaua wapinzani wangu wote". Aliwaamuru wafuasi wake kuongeza katika adhana kauli ya ushahidi kwamba ali muhammad ni dalili ya mungu na vile vile natoa shahada kwamba ali muhammad ni mlango wa mungu".
Katika washabiki wakuu wa kueneza na kukubali madhehebu ya babi alikuwa mwanamke mmoja, kurratui ayn, ambaye alikuwa binti wa mwanazuoni naye aliolewa na mwanazuoni. Alikuwa mwanamke mjanja, aliyeelimika na msemaji hodari. Jina lake la mwanzo lilikuwa zarrin taj na alikuwa mwanamke mwenye sura nzuri sana. Kutokana na mafarakano na mumewe akaungana na madhehebu ya babi ili alipize kisasi dhidi ya mumewe. Kila alipopata fursa alionyesha umbo na uzuri wake kwa kuvua buibui lake hadharani. Siku moja alipanda juu ya mimbari mbele ya watu wengi, akavua buibui na kutangaza: "marafiki na maadui! Kutokeza kwa madhehebu ya babi kumebatilisha uislam.
Amri zote kuhusu swala, saumu, kutoa sadaka na kadhalika zimetanguliwa. Tahadharini hadhrat baab ataiteka dunia nzima na karibuni hakutakuwa na dini yoyote duniani ila ubabi na kwa hivyo kila mtu anawajibika kuungana nasi kwa wingi kadri iwezekanavyo." achilieni mbali buibui ambalo lawatenganisheni na wanawake. Mkumbuke kuwa mwanamke ni ua linalonukia la bustani la dunia hii. hivyo, lichume na kulistaladhi. ua huzawadiwa kwa marafiki. tamaa mbele giza. msikose kuwapa marafiki zenu, wake zenu na maana vikwazo kama hivyo vimekwisha ondolewa katika madhehebu ya ubabi. Staladhi raha zote za dunia maana hakuna lolote baada ya kifo." mwenye akili hahitaji maelezo zaidi kuhusu imani ya madhehebu hayo.
Ubahai ubahai ulianzishwa 1853 b.k. na mwanzilishi wake ni hussein ali ambaye hujulikana kama bahaullah, huko mazinderan iran baada ya kuacha madhehebu ya ubabi. Watu wengi waliuawa. Mwishowe kwa amri ya shah wa iran, nasiruddin, bahaullah akafungwa jela na kufia huko gerezani 1886. Alirithiwa na mwanawe abbas effendi ambaye alistakimu katika jiji la akka huko falestina.
Profesa browne aandika kwamba ubahai ni muundo mpya wa ubabi. kama vile mababi humtukuza ali mubammad (baab) kuwa mtukufu mno vivyo hiyyo mabahai vile vile humfikiria mirza husseinali bahauddin kuwa mtu mtukufu mno. mabahai huamini kwamba ali muhammad baab alibashiri tu juu ya kutokeza kikamilifu kwa amri ya mungu na hilo likafuatwa na kuzaliwa kwa bahauddin kwa sababu mirza hussein ali alikuwa kiwiliwili cha mungu. Hata bahaullah mwenyewe alipokuwa gerezani alitangaza kwamba "hakuna mungu ila mimi mwenyewe aliyefungwa na kukandamizwa." Mtu atamfikiria nini huyo mungu anayefungwa gerezani na anayekandamizwa? madhehebu hayo vipi huweza kuhesabiwa kuwa na uhusiano wowote na uislam?
Kitabu cha kwanza cha mabahai kilikuwa aykaan. baada ya kujitangazia kama yeye mwenyewe ndiye mungu akachapisha kitabu cha pili kiitwacho aqdas ambacho kinadaiwa kuwa ni bora kuliko vitabu vyote vya dini. Katika humo imearidhiwa: "mama zenu tu hamwezi kulala nao na ustaarabu tu unakataza kutoa kanuni kuhusu kumfeli mtoto mwanamume mwenye sura ya kupendeza". hivyo, inamaanisha kwamba mtu anaruhusiwa kuingiliana na kila mwanamke ila mama yake mzazi na vile vile kufeliana na mwanaume mwenzie. Uchochezi wa babi-bahai ulisababisha umwagaji mkubwa wa damu huko iran. wanazuoni, mawaziri na mwishowe shah wa iran nasirrudin shah waliuawa. Idadi kubwa ya mababi na mabahai waliokuwa iran ni mayahudi wa hamadan kashan na yazd waliokubali madhehebu hayo, na vile vile maparisi wa iran na india. waislamu wachache mno walikubali madhehebu hayo.
Mmisionari mkuu wa madhehebu ya bahai, mirza hassan niku, alikuwa mwakilishi wa abbas effendi, mwana wa bahaullah. Abbas ambaye alitunukiwa jina kuu la "jibrael" na mabahai. Jina lake la kiislaam lilikuwa abdulhussein ayni naye alikuwa mfuasi mkuu wa madhehebu hayo. Hao wote pamoja na wamisionari wakuu wa madhehbu hayo wakatubu na kuandika vitabu dhidi ya ubahai na kufichua mabaya ya madhehebu hayo. Avarah katika kitabu cha kashful hiyal amechapish kibayana picha zinazofichua siri za madhehebu hayo. Kwa sababu tu kuimarisha upinzani dhidi ya uislaam huko iran ndiyo mayahudi na maparisi walijiunga na madhehehbu hayo.
Mdai umehdi katika karne ya 13 na 14, mirza kadiani mwanzoni mwanazuoni mubalighi wa kisunni. pole pole, akaanza kudai umehdi, unabii na mwishowe uungu. Vile vile, mirza mohammad ali baab wa ubaabi na husseinali bahaullah wa ubahai mwanzoni walikuwa mashia kila mmoja akaanzisha madhehebu mapya na wakadai kuwa ni wawakilishi wa baab, mehdi, nabii na mwishowe mungu.
Babu zake his highness agakhan walikuja india kutoka iran wakiwa shia ithnaasheri na kuamini maimam kumi na wawili, watukufu kumi na wanne na wakifuata sheria za kuswali, kufunga ramadhaai na kanuni zote za madhehebu ya shia. Siku za mwanzoni, viongozi wa dini ya agakhan walijulikana kwa jina la 'peer' jamatini watu wa kiswali na kufunga ramadhani. Qur'an ikisomwa na watu wakiamini maimam kumi na wawili. Pole pole katika karne hii maaghakani ikaanza daawa ya umehdi, unabii na hatimaye kiwiliwili cha mungu.
Mwanzoni wafuasi wa agakhan wakijulikana kwa jina la bhagat na mashia ithnaasheri subhanya. baadaye waaghakani wakajigeuza kuwa maismaili na kitambo kidogo wamekuwa wakijitambulisha kama shia imami ismailia. kwa upande mwingine, kwa mujibu wa itikadi ya shia ithnaasheri, tangu kuja kwa uislam, imani katika qur'an, maimam kumi na wawili, kuzaliwa kwa hadhrat mehdi
, kughibu kwake na kutokeza mara ya pili kumethibitishwa kutokana na qur'an, hadithi na historia. Dalili madhubuti za uhakika huo na ufanunuzi wake umeelezwa kikamilifu katika kitabu hiki.
Waliodai umehdi walijitokeza mmoja baada ya mwingine, na kueleza nadharia zilizokuwa kinyume na tofauti na maadili ya kiislam kama ilivyoelezwa katika qur'an na hadithi. Hapana shaka wadai wote hao hawawezi kuwa wakweli kwa sababu ubashiri uliopo ni wa mehdi mmoja tu. Hadithi maarufu ya mtume mtukufu(s.a.w.w)
kwamba watakuwa maimam kumi na wawili baada yake na wa mwisho ni hadhrat mehdi
imenakiliwa na wanazuoni maarufu wa kisunni katika vitabu vifuatavyo:
1.
Kanzul umal, juzuu la 6, uk. 198
2.
Sunan Abi Daud uk. 588
3.
Jaamiu Tirmidhi uk. 269
4.
Sahih Muslim, juzuu la pili, uk. 119
5.
Sahih Bukhari, kitabul fitan, babul istikhlaf, juzuu la 29, uk.629
bila shaka mtume mtukufu(s.a.w.w)
alitangaza hadithi hiyo kuhusu maimam kumi na wawili kutokana na amri ya mwenyezi mungu mwenyewe. Kwa hivyo, lazima wawe warithi 12 wa mtume(s.a.w.w)
. Basi imani yoyote kuamini warithi zaidi ya kumi na wawili wa mtume(s.a.w.w)
haiwezi kuwa na ridhaa ya mungu na mtume(s.a.w.w)
.
Ifuatayo ni orodha ya madai ya warithi wa mtume(s.a.w.w)
:
1.
Msururu wa kwanza ni wa khulafaul rashidin ambao walikuwa wanne tu na sio kumi na wawili.
2.
Msururu wa pili wa daawa ya urithi ni kutoka nasaba ya bani umayya ambao walikuwa kumi na wanne.
3.
Msururu wa tatu ulikuwa wa bani abbasi ambao walikuwa 37 (thelalhini na saba).
4.
Msururu wa nne ulikuwa mchanganyiko wa watu wa misri na bani abbas ambao walikuwa kumi na wanane. halaku khan alikomesha ukhalifa wa bani abbas huko baghdad, na mfalme wa misri alimtawaza mwana wa mfalme wa bani abbas kuwa khalifa na kufanya idadi yao iwe kumi na wanane.
5.
Msururu wa tano unatokana na makhalifa wa kituruki. khalifa wa kwanza wa kituruki salim sultan aliiteka misri na kuanzisha ukhalifa wa kituruki. idadi ya makhalifa hao ilikuwa thelathini, lakini alipokuja mustafa kamal pasha akakomesha ukhalifa huo; kwa hivyo, duniani sasa hayupo khalifa wa kisunni.
Madai ya madhehebu mengine:
1.
Madhehebu ya babi azali na bahai, ambayo yamejitenga mbali na itikadi ya uislam, hayawezi kufikiriwa kwamba ni madhehbu ya kiislaam.
2.
Vile vile ukadiani hupinga moja kwa moja imani ya uislam na kwa hivyo madhehebu hayo pia siyo ya kiislaam.
3.
Hata hivyo waumini wa madhehebu ya dawoodi bohora ni waislamu lakini huamini maimamu ishirini na mmoja na vile vile huamini hadi leo kuwa imam wao wa mwisho, imam tayab, amejificha, hivyo daawa yao huzidi idadi ya imam kumi na wawili.
4.
Waismailia wafuasi wa agakhan, huamini imam wao wa kipindi hiki ni wa 49; kwa hiyyo, idadi yao buzidi idadi iliyotajwa na mtume(s.a.w.w)
zaidi ya mara nne.
5.
Ni shia ithnasharia peke yao tu ndio wanawaamini maimam kumi na wawili, kama ilivyosimuliwa na hadithi ya mtume(s.a.w.w)
. imam wa kwanza ni hadhrat ali
na wa kumi na mbili ni hadhrat mehdi
kama ilivyoridhiwa katika vitabu vitano mashuhuri vya madhehebu ya kisunni na kutajwa katika vitabu vingi vingine. jina maalum la kila imam
lilitajwa na mwenyewe mtume(s.a.w.w)
. ukweli huu vile vile umethibitishwa katika vitabu maarufu vya kisunni, k.m.
1.
"Mawaddatul Qurba" uk. 34, kilicho andikwa na allama seyyid alihamdani, kilichochapishwa bombay press.
2.
"Arjahul Matalib", uk. 402, lahore press.
3.
Yanabiul Mawaddah", uk. 445, kilichoandikwa na allama
sheikh Suleiman Kanduzi, sheikh wa istanbul. istanbul turkish press.
4.
Tarikhul Rawzatul Ahbab", Yanabiuel Mawadda juzuu 3, uk. 27. licha ya hivyo, kuna vitabu vingi vimetaja majina halisi ya imam mehdi
.
5.
Babu zake agakhan wa siku hizo wakiamini maimam kumi na wawili kama ilivyoelezwa katika vitabu vyao ambavyo tumekwishavitaja.