15
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
SURA 20
HADITHI KUHUSU KUJITOKEZA KWA IMAM MAHDI
NA ALAMA MAALUM ZITAKAZO TANGULIA
Vitabu vyote vya sunni vimehadithia hadithi juu ya kujitokeza kwa imam
. hii ni dalili kwamba imam
wa wakati huu yu hai, kwa sababu mtu atakayeweza kujitokeza lazima awe hai na aliyeghibu na si yule ambaye bado hajazaliwa.
1)
Imenakiliwa katika juzuu la pili la tarikhe khamis kuwa: "wakati atakapojitokeza mehdi, muhammad bin hassan askari
malaika watatangaza kujitokeza kwake. Yeye ni khalifa aliyeteuliwa na mungu na katika kipindi cha utawala wake mbuzi watakuwa malishoni pamoja na mbwa mwitu na watoto wa binadamu watakamata nyoka na visusuli na kucheza nao."
2)
Katika kitabu cha asafurraghbin, ukurasa 140, sheikh muhyiddin amenakili kutoka kitabu cha kiarabu futuhat kuwa: "hakuna shaka yoyote kwamba hadhrat imam mehdi
atatokeza, lakini wakati ule dunia nzima itakuwa imejaa udhalimu, ukandamizi, na dhambi na huyo imam as. atasafisha hayo yote na ataijaza dunia kwa insafu na usawa. "yeye atatokana na dhuria ya mtume mtukufu(s.a.w.w)
kutokana na binti yake fatima
kwa utaratibu ufuatao: mwana wa fatima atakuwa imam hussein
atakayemzaa alia zainul abedin
ambaye atamzaa muhammad ai-baqhir
atakayemzaa jaffar sadiq
atakayemzaa musa
atakaye mzaa ali ridha
ambaye atamzaa hassn askari
ambaye mwanaye atakuwa muhammad mehdi
atakaye pokea kiapo cha utii katika kaaba takatifu".
3)
Ibne abbas amearidhi katika faraidussimtayn kutoka mtume mtukufu(s.aw.w)
kuwa: "watakuwa makhalifa 12 walioteuliwa na mungu, wa kwanza wao ni hadhrat ali
na mwisho atakuwa mwanangu mehdi
. nabii issa atakapoteremka kutoka mbinguni ataswali nyuma ya mehdi
. dunia nzima itang'aa kwa nuru ya mungu. utawala wa hadhrat mehdi
utaenea kutoka mashariki mpaka magharibi duniani kote (hadithi tatu hizi zote zilizotajwa zimehifadhiwa katika vitabu vya sunni).
vitabu hivyo vya kisunni vile vile vimethibitisha kwamba hadhrat mehdi
atakapojitokeza atastawisha uislam kuwa ni dini ya pekee duniani kote na kueneza insafu na huyo atakuwa mwana wa imam hassan askari
hao wote waliodai kuwa mehdi (kadiani mirza na wengineo) na wale ambao hudai kuwa imam wa wakati huu na mehdi hawakuweza kushinda dhuluma na ukandamizi kwa namna yoyote. alama zitakazoashiria kujitokeza kwa imam mehdi
alama zitakazotangulia kabla ya kujitokeza kwa imam hadhrat mehdi
na hali ya dunia itakavyokuwa imekwisha elezwa. Sasa tutazingatia alama maalum ambazo zitatangulia kabla imam hajajitokeza:
i)
Dajjal atatokeza.
ii)
Sauti kubwa itasikika kutoka mbinguni.
iii)
Sufiani atatokea na ataanzisha vita vikali.
iv)
Jeshi la sufiani ghafla litamezwa na mpasuko wa ardhi baina ya makkah na madina.
v)
Seyyid mahshumu na mcha mungu atauawa makkah.
vi)
Seyyid anayetokana na dhuria ya imam hassan
atatokeza na jeshi lake.
vii)
Sura ya binadamu itaonekana mbinguni kabili ya juwa.
viii)
Kutatokea kupatwa mwezi na juwa mara mbili katika mwezi mtukufu wa ramadhan kinyume cha hali ya kawaida na hesabu: kutakuwa kupatwa juwa
tarehe 15 na tarehe ya mwisho wa mwezi.
ix)
Nyakati tatu itasikilizana sauti kubwa kutoka mbinguni katika mwezi mtukufu wa ramadhan. alama hizi zimekwishaelezwa bayana kwingineko.
Imam Jaafar Sadiq
amesema kwamba: kutakuwa kupatwa kwa jua na mwezi kinyume cha hali ya kawaida na kabla ya tukio hilo thuluthi mbili ya waislamu watakuwa wamegeuka makafiri.
Hadhrat Ali
amesema kwamba kabla ya kujitokeza kwa hadhrat mehdi
kutamwagika damu kwa uwingi, vifo kwa tauni vitakithiri na mchwa watatokeza kwa wingi mara mbili.
SURA 21
KAFIRI DAJJAL CHONGO
siku moja hadhrat Ali
mwishoni mwa hotuba yake katika msikiti wa kufa aliwaomba watu wamwulize maswali wanayotaka kabla yeye kufariki dunia. Sasa bin sawhan akasimama na kuuliza: "eh kiongozi wa waumini! Wakati gani hadhrat hujjat atatokeza"? Imam Ali
akajibu: "kwanza zitatokeza alama nyingi moja baada ya moja. Sikiliza kwa makini kuhusu hizi alama na uzikumbuke. Watu watapotosha dhana ya ibada, watakhini amana, watahalalisha uongo, watakula riba, watakuwa waovu, na waasharati na hawatawapenda jamaa zao, wataona fahari kufanya dhuluma, watapamba Qur'an tukufa, misikiti yenye minara mirefu itajengwa, wataheshimiwa waovu na wadhalimu, misikiti itajaa watu wa kuswali lakini watu hao hawatakuwa na umoja, watawashirikisha wake zao katika biashara ili kupata utajiri, wataamini maneno ya waasi na kuwatii, waovu na wapotovu watakuwa viongozi wa majamii, wataweka vifaa vya ghina (muziki) (gita na piano), wanawake watapanda farasi (baiskeli) na kuwaiga wanaume (kwa mavazi ya kiume), watu watajishughulisha na kutekeleza mambo ya dunia kabla ya kuswali faradhi na kuonekana waungwana lakini mioyo yao itakuwa imejaa ufasiki".
Alipofika hapo asbag bin nabata akauliza, dajjal ni nani? imam ali
akajibu: "jina la Dajjal ni sayad bin sed. Waovu tu ndio watamfuata na waungwana watamkimbia. Dajjal atatokea yahudiyya mjini isfahan Iran. atakuwa na jicho moja na hilo jicho litakuwa kwenye paji la uso na litang'aa sana. Mboni ya jicho lake litakuwa wekundu na karibu na jicho lake litakuwa limechorwa neno kafiri ili lisomeke na wote. Mbele yake kutaonekana mlima wa moshi na kisogoni kwake kutaonekana kilima cheupe. Yeye atatokeza wakati wa njaa kali, watu watababaika na vilima hivyo kufikiria hiyyo ni vyakula na kumkimbilia huyo dajjal. Atapanda punda rangi ya majivu ambaye hatua yake moja itakuwa sawa na masafa ya maili moja.
Akipita karibu na mto wowote maji yake yatakauka. kwa sauti kubwa itayosikika na watu na majini wote yeye atanadi, "eh nyinyi rafiki zangu, njooni kwangu mbio. Mimi ni muumba wa vyote ulimwenguni. Nimeumba vitu katika maumbile mbalimbali na mimi ndiye mtoa riziki mimi ninawaita kwenye maongozi yangu kwa sababu mimi ni mungu na nina uwezo juu ya vitu vyote."
Imam Ali
tena aliendelea kuwatahadharisha watu kwamba yule adui wa mungu ni mdanganyifu wa nafsi yake kwa sababu yeye anakula na kunywa. zaidi ya hayo mungu wenu siye chongo, wala hali wala kunywa, hana mwili na haondoki kutoka pahala pamoja na kwenda pengine. mjitahadhari! wafuasi wa huyo mwovu watakuwa watoto wa haramu na mayahudi. hadhrat mehdi
atamwua dajjal huko sham kwenye mlima mkubwa unaoitwa tallu affik siku ya ijumaa saa tatu baada ya jua kuchwa. baadaye kutatokeza tukio kuu. akasoma aya kutoka qur'an tukufu isemayo:
"Na sisi tuliwasimulia kwamba kuna mtu hutembea kwa wepesi na kuzungumza nao
". (27.28).
Mtu huyo (Imam a.s) atatokeza kutoka mlima wa saffa uliopo makkah. atakuwa amevaa pete ya nabii suleiman na kushika asa ya nabii mussa.
Atagusa paji la uso la waumini kwa pete hiyo na papo hapo kutachoreka maneno "hadha mu'min" (huyu ni mtu aliyeamini). Atagusa paji la uso la makafiri na papo hapo patachoreka maneno "hadha kafir (huyu kafiri). Juwa litachomoza kutoka magharibi na yeye atanyanyua kichwa mbele ya juwa na watu wote duniani wataweza kumwona. wakati huo mlango wa toba utafungwa na vitendo havipatiwi jazaa ila vya wale walio amini kabla ya tukio hilo kwa sababu imani bila amali haikamiliki."
Katika kitabu kimoja cha kisunni, kamaluddin, abdulla bin umar amesimulia kwamba siku moja baada ya swala ya asubuhi mtume mtukufu(s.a.w.w)
pamoja na masahaba zake walikwenda kutembea mjini. mtume(s.a.w.w)
akasimama karibu na nyumba moja na kugonga mlango wa nyumba hiyo. alitoka mwanamke mmoja aliyemtambua mtume(s.a.w.w)
na kumwuliza kwamba angeweza vipi kumsaidia mtume(s.a.w.w)
. mtume akamjibu kwamba alitaka kuonana na mwanae, abdulla. mama huyo alijibu kwamba mwanae alikuwa mgonjwa wa akili na kwa hivyo huchafua nguo zake na kuzungumza maneno ya kiburi mara kwa mara. mtume(s.a.w.w)
akaomba ruhusa ya kuingia ndani kumwona huyo mgonjwa. mama huyo akamruhusu mtume(s.a.w.w)
lakini aliomba asamehewe ikiwa mwanawe huyo atazungumza vibaya na mtume.(s.a.w.w)
.
Mtume(s.a.w.w)
akaingia ndani pamoja na masahaba. yule maluuni alikuwa amevaa nguo nene na kuzungumza peke yake. mama yake akamwambia anyamaze kwa sababu mtume mtukufu(s.a.w.w)
alikuja kuonana naye. kusikia hivyo akanyamaza. mtukufu mtume(s.a.w.w)
akasema: "ingelikuwa huyo mama asingemwambia kunyamaza, mngelisikia anayosema na mngeelewa hali nilivyoeleza". tena mtume(s.aw.w)
akamwuliza kwamba anaona nini. alijibu, "mimi ninashuhudia haki na ubatili na nina ona arsh ya mungu inaelea juu ya maji". bwana mtume(s.a.w.w)
akamsihi atoe shahada juu ya upweke wa mungu na unabii wake. naye akajibu, "ninatoa shahada juu ya upekee wa allah na mimi mwenyewe ni mtume wa mungu kwa sababu wewe hustahili utume zaidi yangu." mtume(s.a.w.w)
akaondoka.
Siku ya pili mtume mtukufu(s.a.w.w)
, pamoja na masahaba wake walikwenda kumwona tena nyumbani kwake. kwa idhini ya mama akaingia ndani na wakamwona amekaa juu ya mtende anapayukapayuka tena mama yake akamgombeza na kumwambia akae kimya na kuteremka chini. siku hiyo tena mtume akachukiwa na akasema "ingekuwa mama yake asingemwambia kunyamaza, nyinyi mngeamini kwamba huyo ni dajjal mfasiki, ambaye nimekwisha watahadharisheni naye" mtume(s.a.w.w)
akaondoka. mtume(s.a.w.w)
tena pamoja na masahaba wake akaenda kumwona siku ya tatu na alipoingia ndani akamwona huyo abdulla akicheza na mbuzi waliokuwa karibu naye.
Mtume(s.a.w.w)
akamsihi akubali upekee wa mungu na unabii wake na akamwambia aseme mtume(s.a.w.w)
alikuwa na wazo gani. huyo akasema "addhukh adhukh" (dukh maana yake mvuke na siku hiyo hiyo suratul dukhan iliteremshwa na mtume(s.a.w.w)
alisoma sura hiyo aliposwalisha swala ya alfajiri. mtume(s.a.w.w)
akamjulisha 'atakayo mungu ' ndivyo huwa na wewe hutafikia mradi wako." mtume mtukufu(s.a.w.w)
baadaye akawaeleza masahaba "wake kwamba huyo abdulla ndiye dajjal mfasiki ambaye habari zake alikwishawaeleza. atatokeza duniani siku za mwisho na kabla ya hapo mungu atakuwa amemweka mahabusu katika kisiwa kimoja. atawaletea watu utatanishi mkubwa siku za mwishoni. manabii wote kabla ya mtume mtukufu(s.a.w.w)
waliwatahadharisha wafuasi wao kuhusu dajjal. kadhalika, mtume wetu(s.a.w.w)
ametutanabahisha sisi kuhusu huyo dajjal na akaongeza "msidanganyike na huyo: mungu wetu siyo chongo, wala hana mwili na huyo mwovu (dajjal) atajitokeza siku za mwisho amepanda punda".
Dajjal atajitokeza siku za mwisho na ataishi kwa muda wa siku arubaini na atatembelea kila sehemu ya dunia juu ya punda wake. mwisho atauliwa huko syria kwa mikono ya imam mehdi
.
SURA 22
HAKIKA KUHUSU KUJITOKEZA KWA IMAM WA KIPINDI HIKI
Imam Mahdi
wakati uliopangwa wa kujitokeza kwa hadhrat mehdi
utapowadia upanga wake "dhulfiqar" utajitokeza nje ya ala yake na kwa kudra ya mungu utapata kauli na kusema: "Eh hujjat wa Mungu, wakati wa kujitokeza kwako umewadia. tafadhali jidhihirishe mbele ya watu duniani" Imam jaafar Sadiq
amesema: "Atakapojitokeza imam mehdi (a.s) ataingia katika jiji la makkah. atakuwa amevaa mavazi ya mtume (s.a.w.w). kilemba cha njano, na atashika fimbo na kuvaa viatu vya mtume (s.a.w.w). mbele yake watakuwa mbuzi wachache waliodhoofika
".
Hakuna mtu katika makkah atakayeweza kumtambua imam mehdi
. ataingia kaaba akionekana kijana kabisa. ataignia katika kaabah tukufu usiku wa manane. Jibriil, Mikaiil na malaika wengine katika vikundi vikubwa watateremka kutoka mbinguni kuja ka’aba na kumwamkia imam Mahdi
. Jibril atampasha imam habari kuhusu maagizo ya Mungu Subhana wa taala kwamba chochote atakachopenda na kuamrisha kitakuwa. Imam
hapo atachukua mkono wake wa kulia na kuweka juu ya uso wake na kusema:
وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي صَدَقَنَا وَعْدَهُ وَأَوْرَثَنَا الْأَرْضَ نَتَبَوَّأُ مِنَ الْجَنَّةِ حَيْثُ نَشَاءُ فَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿٧٤﴾
"Nao watasema: Alhamdulillah, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye tutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!." (39: 74).
Baadaye hadhrat hujjat
atasimama kwenye pembe moja ya kaaba tukufu na kutangaza "Eh nyinyi mlioteuliwa mahsusi na allah kunisaidia mimi tafadhali mje kwangu" sauti hiyo itasikika katika kila nchi lakini khassa na waumini 313 katika asia, afrika na china. baadhi ya hao waumini watakuwa juu ya miswala, wengine watakuwa wamelala, lakini wote watafunga safari kwenda makkah na katika muda mfupi mno watajikuta wamekwisha fika kwa imam
.
Wakati huo Jibreel atabusu mkono wa Imam
na kula kiapo cha utii kwa imam
. na kufuatwa na malaika wengine. baadaye viongozi wa majini na hao waumini 313 watakula kiapo cha utii. watu wa makkah kutahamaki hayo watashangazwa na watauliza hao watu ni nani na wanatokea wapi? vile vile watajiuliza kwa sababu gani usiku huu umekuwa marini na kwa miujiza mingi inaonekana. wengi wao watajibu kwamba hawajui; ila watu wanne kutoka madina ambao watawajulisha kwamba kiongozi wao mwenye uso marini ni imam
.
Baada ya kupambazuka kutasikika sauti (mwito) katika lugha ya kiarabu duniani kote ikitangaza: "eh nyinyi viumbe mliokuwa mbinguni na ardhini, shaksi aliyejitokeza ni mehdi anayetokana na dhuria ya mtume(s.a.w.w)
. baadaye hiyo sauti (tangazo) itaeleza majina kamili ya hadhrat mehdi na nasaba yake mpaka imam hussein
na itawataka watu kula kiapo cha utii kwa imam
na kuwaonya kwamba kuhalifu ni kugeuka kafiri. malaika, majini na wale 313 pamoja na waumini wengine watadhihirisha imani yao na utii kwa imam
.
Huo mwito utasikika vizuri mno katika nchi zote, misitu na milima yote na wanaume kwa wake na watoto wote watashangazwa nao. Wakati wa machweo kutasikika mwito mwingine ukitangaza: "Eh watu, sikilizeni. mungu wenu amejitokeza kutoka misitu ya yabis (palestine) na jina lake ni othman bin amsasah anayetokana na ukoo wa umayyah na dhuria ya yazidi bin muawiyah. Mwelekee kwake na kula kiapo cha utii mwongozwe njia ya haki". Malaika majini na waumini halisi watabatilisha tangazo hilo kuwa ni uzushi na uwongo mtupu. Makafiri wanafiki na wasioamini dini watababaishwa na tangazo hilo na kupotoshwa.
Baadaye imam Mahdi
akishikilia kaaba tukufu atanadi "Eh viumbe vyote wa mungu nisikilizeni! mimi nimejaliwa na wema, uwezo na miujiza yote ya mitume wote, pamoja na sifa zote za mtume mtukufu (s.a.w.w) na maimam na elimu ya vitabu vitakatifu vyote.
" waumini wote watakubali tamko hilo. hapo tena mtu mmoja ajulikanaye kama dabbatul ardh atatokeza baina ya rukn na maqam akishika fimbo na pete mkononi. huyo. (dabbatui ardh) atapoiweka pete hiyo kwenye paji la uso wa waumini papo hapo maneno "huyu mwumini" yatajitokeza na atapoiweka hiyo pete juu ya paji la uso wa makafiri maneno "huyu kafiri" yatajitokeza.
Baada ya hapo mtu mwenye uso wake uliogeuka nyuma atafika kwa imam
na kusema, "eh bwana wangu! Mimi na ndugu yangu tulikuwa katika jeshi la sudani na tulivamia ardhi yote baina ya damascus na baghdad kusababisha hasara na maangamizi. Baadaye tulielekea madina na makkah na jeshi la watu 300,000 tukikusudia kuingia makkah kubomoa kaaba tukufu na kuua umati mzima wa jiji.
Tulifika usiku jangwa la bayadana lililopo baina ya madina na makkah. Baada ya usiku wa manane tulisikia sauti: "Eh bayadana, waangamize makafiri wadhalimu. Papo hapo kwa amri ya allah ardhi ikapasuka na maaskari wetu 300,000, mali zetu pamoja na wanyama wetu wakamezwa na ardhi, haikubakia alama yoyote. Mimi na ndugu yangu tu tulisalimika. akatokea malaika mmoja na kutupiga makofi kwa nguvu mno na kusababisha nyuso zetu kuelekea nyuma (migongoni). Hapo huyo malaika akinielekea mimi akaniambia, "eh bashir elekea makkah na mpe imam
taarifa njema kuhusu maangamizi ya jeshi la sufiani. Tena baadaye alimwelekea ndugu yangu na kusema: "eh nazir elekea damascus na mwarifu sufiani kuhusu kuangamia jeshi lake na vilevile mpe taarifa ya kujitokeza kwa hadhrat mehdi
huko makkah. Msihi aje ajisalimishe kwa imam
na kuomba msamaha kwa maovu yake na akifanya hivyo toba yake itakubaliwa. (lakini hata hivyo huyo mtu mwovu hataomba msamaha na atajitumbukiza jahanam). Baada ya kusikia hayo yote imam
kwa mikono yake iliyo barikiwa ataurudisha uso wake uwe sawa. hadhrat mehdi
ataelekea kufa kutoka makkah na jeshi kubwa la malaika na majini. msikiti wa kufa utakuwa mahakama na msikiti wa sahlah makazi yake.
Mtume mtukufu(s.a.w.w)
amebashiri kwamba imam Mahdi
. atapata ushindi katika usiku mmoja na kukamilisha malengo yake. Hadithi hii ya mtume mtukufu(s.a.w.w)
ni ushahidi kamili wa kubatilisha daawa ya wale wote waliojidai kuwa wao ni mehdi
na vilevile ya wale ambao watafanya daawa ya kuwa mehdi
. Mji mkuu wa utawala wa imam
utakuwa kufa ambao utakuwa umepanuka hata kumeza jiji la najaf. kila inchi ya ardhi hiyo itathaminika sana na waumini kutoka kote kote dumanai watakutana huko (kufa). Jiji la kufa litakuwa na urefu wa maili 54 na kuungana na mji wa kerbala, katika zamana hiyo mwenyezi mungu subhana wa taala atatimiza kila matilaba ya waumini.
Imam
hapo atatuma jeshi kubwa kwenda damascus ambalo litashinda jeshi la sufiani na kumwua sufiani. Sawia ya hapo imam husein
pamoja na masahaba wake 72 ambao waliuawa karbalaa pamoja na waumini halisi watarudi duniani kwa amri ya mola. Hao watu watafika mbele ya imam mehdi hadhrat ali
na maimam wengine watarudi duniani. Mtume mtukufu(s.a.w.w)
pamoja na masahaba wake waliouawa vitani (jihadi) vilevile watarudi duniani. wale ambao hawakumwamini mtume(s.a.w.w)
, kumsumbua, kumzulia kuwa ni mchawi na kumtuhumu maovu mengine watarudishwa duniani na kuadhibiwa kwa dhuluma na uonevu waliotenda. vilevile atarudi nabii issa na mitume wengine pamoja na waumini. Hakutakuwa dini ila moja tu, uislaam, ulimwenguni kote. Dunia hii itajaa baraka za mungu. hali itakayokuwa wakati huo imekwisha elezwa katika vitabu vingine.