17
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
SURA 25
JE INAWEZEKANA KUONANA NA IMAM MAHDI
KATIKA KIPINDI CHA KUGHIBU KWAKE KWA MUDA MREFU (GHAIBATULKUBRA)?
Wapinzani wetu wanatucheka itikadi yetu kwamba hadhrat mahdi
ameishi maisha ya kutoonekana kwa muda wa miaka elfu na mia moja. kwa mfano, munshi khadim hussein anaandika katika gazeti la kikadiyani la lugha ya urdu na ambalo hutolewa kila mwezi kwa jina la tahshizulazham katika sura iitwayo tahkike akheruzzaman kwamba huona ajabu kabisa kwamba ijapokuwa hadhrat mahdi
yu hai kwa miaka 1100 hakuna mtu anadai kwamba kaonana naye (hadhrat mahdi a.s.). hoja hii ya gazeti hilo haina msingi wala itibari maana watu wengi wanaonana na hadhrat mahdi
na taarife kamili imeelezwa katika vitabu vya shia ithnaasheri. katika sura ya mwisho ya kitabu hiki tumesimulia habari za watu wachache waliokwisha bahatika kukutana naye. hata hivyo vitabu vikuu vingi vya kisunni vimeeleza habari za waislamu walio onana na hadhrat mahdi
.
Mwanazuoni mashuhuri wa kisunni, allama sha'arani, amenakili katika kitabu chake lawakihul .anwar kwamba sheikh hassan iraqi amesimulia kuwa: "siku moja nilipoingia ndani ya msikiti wa ijumaa wa ummayad niliwaona watu wengi wameketi kumzungukia mtu mmoja aliyekuwa akihutubia juu ya hadhrat mahdi
. mimi niliathirika sana na hiyo hutuba na nikaanza kupata shauku ya kutaka kuonana na hadhrat mahdi
na tokea siku hiyo nilikuwa namwomba mungu anijalie bahati hiyo. muda wa mwaka mmoja ulipita. siku moja nilikwenda katika msikiti huo kwa ajili ya swala ya magharibi na baada ya swala hiyo nilimkuta mtu aliyevaa kilemba cha kiirani akinijongelea. akanigusa begani na kuniuliza sababu gani nilikuwa nikimwomba mungu kwa bidii kuonana naye. mimi nikamwuliza yeye nani na akanijibu kwamba ni hadhrat mahdi
. papo hapo nikambusu mkono wake na nikamkaribisha nyumbani kwangu akakubali mwaliko wangu na kuwa mgeni wangu kwa muda wa siku saba. katika muda huo alinielimisha juu ya mambo ya dini na kunishauri nifunge kila siku moja na kuacha rnoja na koswali rakaa mia tano kila siku. siku ya saba wakati wa kuniaga akanishauri kutoonana na mtu yeyote, bali kujishughulisha katika ibada ya mungu na nisisumbuke kuhusu riziki yangu kwa sababu hiyo nitapatiwa.
Nilimsindikiza hadi mlangoni na akaniambia nirudi nyumbani mwangu. tokea siku hiyo nilikaa nyumbani kwangu kwa usalama. mwandishi anasema kwamba alipomwuliza umri wake wakati huo imam
akajibu kwamba umri wake ulikuwa miaka 620. mwandishi huyo huyo amenakili tukio hilo katika kitabu chake kingine yawakit wal jawahir ukurasa 288 kilichochapishwa misri.
Isitoshe visa hivyo vya watu kuonana na hadhrat mahdi
na majina yao yamehifadhiwa katika vitabu vya kisunni k.m. kifayatuttalib, matalibul usul na yanabiul mawadah na kadhalika. katika kitabu cha mwisho kilichoandikwa na sheikhul islam wa istanbul, sheikh Suleiman Kanduzi, sura ya 83 imetengwa kwa ajili ya maelezo ya watu walio onana na Imam Mahdi
.
1.
Maelezo hayo yanatolewa kwa muhtasari tu hapa Ali abdulla bin saleh anaeleza kuwa: "Nilipomwona Imam Mahdi
huko makkah karibu na hajarul as-wad (jiwe jeusi) watu walikuwa wakisukumana ili wapate kusonga mbele. HapoImam Mahdi
akawaambia kwamba kitendo hicho ni kinyume cha amri ya Mungu.
2.
Muhammad bin Shazan Kabuli anasimulia kwamba: alipoonana na Imam Mahdi
imam huyo alimwita kwa jina lake maalum linalojulikana na watu wa nyumbani mwake tu na kupatiwa majibu ya kutosheleza maswali aliyomwuliza ima
3.
Muhammad bin Othman alimwona Imam Mahdi
huko kaaba amenyanyua mikono yake kuomba dua na kusema "eh mungu timiza ahadi ulionipa mimi".
4.
Zarif Abunasr anahadithia kwamba: alipobahatika kuonana na Imam Mahdi
yeye (imam as.) alisema: "mimi ni mrithi wa mwisho wa mtume mtukufu(s.a.w.w)
na kwa ajili yangu watu wataepuka na maafa duniani."
5.
Muhammad bin Abdulla Kufi ametoa taarifa ya majina ya watu kumi na wawili ambao walikuwa watumishi wa serikali na wengine 53 ambao wote walionana na hadhrat mehdi
6.
Hassan ibne wajna nasibi ameeleza kuwa: "mimi nilihiji mara 53 na kila mara huko kaaba nilikuwa nikimwomba mungu amjalie kuonana na imam
. mara moja katika safari ya 54 nilipokaa huko makkah alitokea mwanamke mmoja ambaye akahiita kwa jina langu hassan na kuniomba nifuatane naye. tulipofika kwenye nyumba ya bibi khadija (mke wa kwanza wa mtume(s.a.w.w)
tukasimama. imam mahdi
mwenyewe akaja mlangoni. mimi nikamwamkia na akaniambia "hassan, mimi niko na wewe kila mwaka unapokwenda kuhiji. sasa wewe acha nyumba yako na uende kuishi katika nyumba ya imam jaffar sadiq
na usisumbuke kuhusu maisha yako. utapatiwa chakula na mavazi unayohitaji." vile vile akanifundisha dua moja.
Niliishi katika hiyo nyumba kwa muda mrefu na nilipatiwa mahitaji yangu juu ya wakati.
7.
Ali bin Ahmed Kufi anasimulia kwamba: mara moja alipokuwa akitufu kaaba akashituka ghafla kumwona kijana mwenye uso unaong'aa. katika msituko huo akamwuliza huyo kijana yeye nani, na akajibiwa: "Mimi ni imam na wakati huu na ni mahdi ambaye atajaza dunia kwa uadilifu na usawa. Kwa hakika hujja (khalifa wa mungu) daima huwapo duniani." baadaye akatupa fimbo aliyoshika mkononi mwake. Mimi nikanyanyua hiyo fimbo na nilipoiangalia nimeona imegeuka ya dhahabu, nikamrudishia hiyo fimbo.
Rashid hamdani anasimulia: "mara moja nilipokuwa narudi kutoka hijja nilipotea njia. nilijikuta peke yangu msituni. nilikwenda hatua chache tu nikaona bustani ambayo ikinukia viziiri. ghafla nikaona hema moja zuri na nje yake walikuwa wahudumu wawili. waliponiona mimi mmojawapo akaingia ndani na baada ya muda mfupi akarudi na kunikaribisha ndani ya hema. Ndani humo alikuwa ameketi mtu mwenye haiba na uso unaong'aa. Juu ya kichwa chake kulikuwa upanga mrefu ulioning'inia hewani. nikamsalimia, naye akanijibu na kusema: "mimi ni qaim (aliyesimama) ambaye nitajitokeza siku za mwisho wa dunia na kwa upanga huu nitatawala dunia kwa insafu na usawa." mimi nikapiga magoti na yeye akasema:
Hakuna wa kumsujudia yeyote ila mungu; nyanyua kichwa chako jina lako ni rashidna wewe ni mkazi wa hamdan. Unahitaji nini? je, unahitaji kufika nyumbani kwako? mimi nikajibu, "ndio seyyid yangu, mimi nina hamu sana kufika nyumbani kwangu" akanizawadia mkoba mmoja na kumwagiza mhudumu mmoja anifikishe nyumbani kwangu. tukaondoka pale na baada ya hatua chache tu mhudumu akaniambia: "angalia, hapa ni makazi yako; endelea. Nilipogeuka na kumwangalia huyo mhudumu sikumwona. nilipofika nyumbani niliona kuwa katika mkoba huo hadrat mahdi alinizawadia sarafu hamsini za dhahabu. sarafu hizo zilitufanya tuishi kwa raha sana."
Hayo yote yameandikwa katika kitabu kimoja kiitwacho yanabiul-mawaddah. Licha ya hayo, kuna visa vingi vilivyonakiliwa katika vitabu vingi vya kisunni na hata kutaja majina ya watu walio onana na imam
na sababu za kuonana naye. bila shaka katika vitabu vya shia kuna visa vingi vilivyohadithiwa. udogo wa kitabu hiki hauruhusu kuingiza maelezo marefu.
SURA 26
VISA SITA VYA WATU KUKUTANA NA IMAM MAHDI
Kisa cha kwanza:
uwekaji wa jiwe jeusi (hajar-ul-aswad) pahal a pake na imam wetu wa wakati huu hadhrat mahd
. mwanazuoni wa kishia, abil kassim jaffar ibne muhammad kavliyah, amenakili katika kitabu chake kuwa: "katika 307 a.h. jeshi la karamala lilivamia kaaba. tukufu na kuondosha jiwe jeusi (Hajarul Aswad). Baadaye waliamua kurudisha hilo jiwe wakati ambapo mimi nilikuwa nikijiandaa kwenda kuhiji na nilifika baghdad. mimi nilijua kwamba atakayeweza tu kuweka hilo jiwe jeusi (Hajarul Aswad) ni imam wa wakati huu na ilikuwa kwa nia hiyo ya kuonana na imam
ndiyo niliamua kwenda kuhiji mwaka huo. kwa bahati mbaya huko baghdad nikawa mgonjwa sana. Kwa hiyo nikamwomba ibne hashim aende kuhiji kwa niaba yangu na nikampa fedha za kugharimia safari hiyo pamoja na barua. nikamsisitizia kwamba kwa hali yoyote lazima aonane na mtu yule atakayeweka hilo jiwe jeusi (Hajarul Aswad) na kumkabidhi barua hiyo".
Ibn Hashim anahadithia: "Mimi nilikwenda makkah na nikawalipa fedha nyingi wahudumu huko kaaba ili wanipatie nafasi karibu na Hajarul Aswad. umati rnkubwa wa watu ulikusanyika huko msikitini. nilishuhudia kwamba watu wakuu na wanazuoni walijaribu kulirudisha hiio jiwe jeusi (Hajarul Aswad) pahala pake lakini bila mafanikio; jiwe hilo liliendelea kucheza. ghafla kijana mmoja mwenye haiba na uso wa kung'aa akajitokeza na kwa mikono yake iliyobarikiwa akaliweka jiwe hilo nafasi yake. hilo jiwe likaganda barabara.
Umati walipata msisimko na kwa furaha wakasema kwa sautikubwa "allahu akbar". Baada ya kuweka hilo jiwe kijana huyo akaondoka. Mimi nilimfuata nikiwasukuma watu kama kichaa. Huyo kijana alikuwa anakwenda polepole lakini sikuweza kumfikia ijapokuwa mimi nilikuwa nakwenda mbio mno. mwisho tukafika msituni nje ya jiji. huyo kijana akasimama, akageuka na kuniomba hiyo barua. bila kusoma hiyo barua akaniambia "mwarifu mwandishi wa barua hii kwamba, atapona ugonjwa wake na ataishi muda wa miaka 30 mingine".
Kusikia hayo mimi nililia kwa kuhemkwa. katika kipindi hicho huyo mtukufu alitoweka machoni mwangu." Ibn Hashim alirudi kwa ibne kavliyah na kumsimulia maneno aliyoyasema imam
na kama alivyobashiri imam mwanazuoni huyo aliishi miaka 30 zaidi. kisa cha pili kuonekana kwa hadhrat mehdi
huko" kandhar afghanistan katika jawabu lake kwa mwanazuoni mwingine, mulla abul kassim kandhaar amesimulia kuwa: katika mwaka 1266 a.h, mimi nilikuwa kandahaar, huko afghanistan nikihudhuria darasa la unajimu na falsafa kutoka kwa mwana wa mulla abdulrahim mulla habibullah. siku moja ya ijumaa nilimtembelea nyumbani kwake.
Alikuwa amekaa sebuleni akiwa pamoja na wanazuoni wengi, mahakimu na viongozi wa jiji walioegemea kuta. Kati yao alikuwa mulla gulam muhammad, kadhim mkuu, sadra muhammad ali khan na mwanazuoni kutoka misri ambao wote hao walikuwa masunni. mfanyabiashara mmoja wa kishia, wana wa mwenyeji, mwana wa kadhi na mimi tulikuwa tumekaa kuelekea qibla. majadiliano ya mantiki na ya kidini yakaanza. kadhi mkuu alizungumzia kwa kirefu dhidi ya shia, kuwakashifu mashia na kudai namna shia walivyokuwa wajinga na wapuuzi kwa kuamini kwamba hadhrat mahdi
amekwisha zaliwa kutokana na hadhrat imam hassan askari
mwaka 255 a.h. na kughibu katika mwaka 260 a.h. na kuwa yungali hai hadi leo. Wote waliafikiana naye, ila mtu mmoja tu: mwanazuoni aliyetoka misri ambaye alikuwa sunni na alishiriki katika majadiliano ya awali ya kukashifu mashia.
Lakini katika suala hilo yeye hakuwaunga mkono masunni wenzake. alipomaliza mazungumzo yake kadhi mkuu, mwanazuoni kutoka misri akasema: " sasa nisikilizeni mimi kwa makini. "Mimi nilikuwa ninapata mafunzo ya hadithi kutoka kwa mufti katika shule moja huko tawleen. Mufti alizingumzia sura, urefu na jamali ya hadhrat mahdi
. kulikuwa mazungumzo marefu juu ya somo hilo. Ghafla wote tukakaa kimya kwa sababu kijana mmoja mwenye sifa hizo na urefu huo alionekana amekaa na sisi. kila mtu akainama na kunyamaza. hakuna mtu aliyethubutu kunyanyua jicho lake au kunene neno".
Mwanazuoni wa kimisri alipomaliza kusema hayo waliohudhuria wote wakainamisha vichwa vyao na wakakaa kimya. Baada ya muda mfupi tu wote waliloana kwa jasho. mimi mara moja tu nilinyanyua macho yangu ili nimwone imam
. alikuwa amekaa katikati yetu na kila mtu alikuwa kimya akimwangalia mwenzake. kwa hakika mimi nilishtuka. hata hivyo, sikuthubutu kusema neno. mmoja baada ya mmoja wakaanza kuondoka bila kuagana. usiku huo mzima mimi sikupata usingizi na nilikuwa katika hali ya furaha mno kwa kupata fursa ya kuweza kuonana na imam
. zaidi ya hayo, wapinzani walipata jibu muafaka la hoja yao juu ya wakati, yaani kuwepo kwa imam
, kughibu na uwezo wake juu ya dunia nzima kulithibitika bayana'. Hata hivyo, mimi nilihuzunika sana kwa sababu niliweza kumwona imam wangu mara moja tu, lakini ukweli ni kwamba sikuthubutu kunyanyua kichwa changu mara ya pili."
Mulla abdul kassim anaendelea kusema: "siku ya pili nilihudhuria darasa la mulla abdulrahim ambako imam
alitutembelea. mwalimu wangu akaniita faraghani katika maktaba na kuniuliza", je uliona kulitokea nini jana? hadhrat mahdi
mwenyewe alitutembelea na sisi sote tuliloana kwa jasho, tulipigwa na butaa na hivyo tuliondoka bila hata kuagana. Kwa hofu nikasema kuwa sijaona kitu chochote. yeye (mwalimu) akasema: "hilo ni jambo dhahiri, kwa nini unakanusha? wengi waliohudhuria jana wameniandikia kuhusu waliyoyaona jana na kushangazwa na kisa kilichotokea jana." Siku ya pili mtaani nikaonana na huyo mfanyabiashara. Yeye akasema "Mwenyezi Mungu ametusaidia kwa kutupatia nafasi ya kuonana na hujjat (khalifa) wake duniani. zaidi ya hayo sardar alikhan akasadiki ukweli kuhusu imam mahdi
na kugeuka shia".
Baada ya siku chache nilionana na mwana wa pili wa kadhi mkuu ambaye aliniambia kwamba baba yake angependa nimtembelee. mimi nilikataa moja kwa moja lakini alishikilia nimtembelee baba yake na mwishowe nililazimika kwenda kuonana na kadhi mkuu. nilikwenda kuonana na huyo kadhi mkuu na nikamwamkia. akanijibu na kunikaribisha kuketi karibu naye. wakati huo mwanazuoni wa kimisri na watu wengi walikuwa wamekaa hapo. huyo kadhi mkuu akaniuliza juu ya tukio la usiku huo. mimi nikajibu kwamba nilichoona tu ni watu kuondoka (kutawanyika) bila kuagana. wote waliohudhuria wakaniita 'mwongo'. wakasema kwamba walimwona mtu mwenye haiba alikuwa amekaa nao amepinda magoti yake. kadhi alisema kuwa mimi ni mwanafunzi wa fiqhi (elimu kuhusu maamrisho ya kidini). "hawezi kusema uwongo. huwezekana kwamba wale watu waliokuwa na shaka kuhusu imam mahdi
wamemshuhudia. lakini huyu akiwa shia mwenye itikadi thabiti. Juu ya imam
hakushuhudia hayo."
Waliohudhuria wote walitoshelezwa na maelezo ya kadhi. kisa cha tatu ziara ya hadhrat mahdi
nyumbani kwa mwanazuoni maarufu -agha seyyid mahdi - huko hilla iraq huko hilla kulikuwa na mfanyabiashara mmoja kwa jina la shekh ali ambaye alikuwa mmojawapo wa waumini. anaeleza kuwa "siku moja asubuhi niliamua kwenda nyumbani kwa agha seyyid mahdi bahrul-uluum kumsalimia. njiani nikapita karibu na kaburi la seyyid muhammad zidmeah. nikamwona mtu mwenye haiba kuu amesimama karibu na hilo kaburi akisoma suratul fatiha. huyo alikuwa mwarabu mwenye uso unaong'aa. nilipomwona mtu huyo na mimi nikasimama kusoma fatiha. baadaye nikamsalimu. akanijibu na kuniambia "o Ali, unakwenda kumwona seyyid muhammad ?" mimi nikajibu "ndiyo". njiani akaniambai, "o Ali usikate tamaa. Umepata hasara kubwa katika biashara. Hiyo ndiyo hali ya utajiri kwa sababu fedha haikai daima kwa mtu mmoja. mungu atakusaidia wewe ijapokuwa ulikuwa umewajibika kwenda kuhiji lakini hukutekeleza. hata hivyo, usijali, utakuwa tajiri tena. Mimi nilishangazwa sana vipi mtu nisiyefahamiana naye alipata habari kuhusu hasara niliyoipata? hata hivyo, nikajibu kuwa mungu ndiye anayestahili sifa zote na apendaye yeye ndio huwa. Hapo tulikuwa tumekwishafika nyumbani kwa mujtahidi (mwanazuoni). Mimi nikangoja na nikamwomba atangulie. yeye akajibu 'ana sahibuddar' kumaanisha: "mimi ndiye mwenye nyumba" (moja wapo ya sifa na majina ya heshima ya imam mahdi
ni sahibuddar".
Hapo akanikamata mkono na kunitanguliza na akanifuata. katika nyumba hiyo kulikuwa chumba kikubwa ambamo huyo mujtahid akiendesha darasa. Wanafunzi wake walikuwa wanamsubiri. nafasi hiyo ya mujtahidi ilikaliwa na huyo mtu (imam mahdi
na mimi nikakaa kando karibu na nafasi ya mujtahidi. Huyo mtu akanyanyua kitabu kimoja kilichoandikwa na mujtahidi mwenyewe na akaanza kusoma na kuwaelekeza wanafunzi kuwa: "kitabu hiki ni cha maana sana. Kuna dalili thabiti kuhusu kanuni za dini". katika muda huo mujtahid alitoka chumbani mwake na kumwona huyo mtu mwenye haiba amekaa juu ya nafasi yake. Kumwona mujtahid, huyo mtu akasimama na kumpisha nafasi yake, lakini huyo mujtahid akasisitiza akae hapo hapo na mujtahid akakaa kwa heshima mbele yake. Mujtahid huyo alishawishika sana kumwuliza jina lake huyo mtu na anatokea wapi lakini alishindwa. Mujtahid akaanzisha mafunzo kama kawaida na mtu huyo akatoa maoni yake. Kabla ya hapo sijapata kusikia dalili na maelezo kamilifu kwa ufasaha na uwazi kama alivyoeleza mtu huyo. Mwanafunzi mmoja mjinga na mjeuri akamkatiza kauli na kumwuliza kwamba yeye anafahamu nini juu ya swala hilo, lakini huyo mtu alitabasamu na kukaa kimya.
Baadaye huyo mtu akaomba maji na msaidizi akaanza kujaza maji katika bilauri kutoka kwenye mtungi mkubwa. Huyo mtu akasema 'hayo maji katika mtungi huu siyo safi kwa sababu kuna mjusi amefia humo" na akaomba maji kutoka mtungi mwingine. Maji yaliletwa na huyo mtu akayanywa. Mujtahid hapo akamwuliza anatokea wapi, akajibu kuwa ametoka mji wa suleimanlyya. Mujtahidi akamwuliza alianzalini safari yake kutoka suleimaniyya, naye akajibu "niliondoka jana. Najibpasha amekwishaingia mjini na jeshi la serikali na kuliteka. amemweka kizimbani gavana mwasi ahmed na badala yake amemteua abdulla pasha kuwa gavana" umbali kutoka suleimaniyya hadi hilla ulikuwa safari ya siku kumi na mimi nilishangazwa huyo mtu amefika hapa namna gani katika muda mfupi ilihali gavana wa hilla au mtu yeyote mwingine hana taarifa juu ya ziara yake. Hata hivyo, nikanyamaza kimya!
Hapo teaa huyo muadham akasimama ili aondoke. Mujtahid akamsindikiza mpaka mlangoni. Kurudi tu mujtahid akawauliza wanafunzi kwa sababu gani hawakumwuliza huyo muadham ameweza vipi kusafiri umbali kutoka suleimaniyya mpaka hilla katika usiku mmoja wakati safari kutoka suleimaniyya mpaka hilla huchukua siku kumi? Wanafunzi wakamwuliza mujtahid sababu gani yeye mwenyewe hakumwuuliza muadham swali hilo.
Mujtahid akajibu kuwa wakati huo alipotelewa na fahamu. Yeye (mujtahid) akatuomba sisi sote tutoke nje kumtafuta huyo muadham ijapokuwa yeye alikuwa na uhakika kwamba hatutamwona kwa sababu aliamini kwamba huyo muadham alikuwa imam mahdi
mwenyewe. chombo kilichokuwa na maji hakikuwepo usoni lakini alijua kwamba mjusi alifia ndani humo. Ili kuhakikisha ukweli ukweli huo, hicho chombo kililetwa na kweli alionekana mjusi mmoja mrefu humo. tena katika maswali ya dini alikuwa anaelewa mambo yote na kueleza kikamilifu.
Hapo tena mimi nikaeleza vipi nilikutana naye njiani na alinizungumzia juu ya biashara yangu na hasara niliyoipata, na mimi kutokwenda kuhiji. wote waliamini kwamba huyo muadham hakuwa mtu yeyote mwingine ila hadhrat hujjat
mwenyewe. Baada ya siku kumi gavana wa hilla akapata taarifa ya kutekwa kwa suleimanniyya ambayo iliimarisha zaidi imani ya wote kwamba walibahatika kuonana na hadhrat mahdi
na wakamshukuru mungu kisa cha nne mwanafunzi wa najaf aonana na hadhrat mehdi
katika msikiti wa kufa mwanazuoni wa najaf, sheikh abdul hadi anahadithia kuwa: "Muumini mmoja katika mji wa Najaf, haji ali, akienda msikiti wa sahlah kila usiku wa kuamkia jumatano. siku moja nilimwuliza kama aliwahi kubahatika kuonana na imam mahdi
.
Akanijibu kwamba miaka mingi kabla yeye pamoja na wanafunzi wenzake na waumini(wengine walikuwa wakienda kukesha huko msikitini kufa kila usiku wa jumatano. (msikiti wa sahlah uko kufa, iraq). Walikuwa kumi na mmoja na kila wiki mmojawao huleta chakula, chai na tumbaku, siku moja ilikuwa zamu ya mwenye duka, yeye aliandaa kila kitu lakini alisahau kuvichukua alipokwenda msikitini. Tulikwenda msikiti wa sahlah na baada ya kuswali swala ya isha tukaenda msikiti wa kufa na baadaye tukakusanyika katika chumba kimoja kula chakula. Wote walikaa kimya. hata huyo mwenye duka aliyewajibika kuleta chakula vilevile alikaa kimya na kuinamisha kichwa chake kwa fedheha. Alikiri kwamba ijapokuwa aliandaa vifaa vyote lakini alisahau kuleta pamoja naye. Aliahidi kwamba atakapofungua duka siku ya pili atatuonyesha alivyokiandaa. Kwa hivyo, sisi tulijiandaa kupitisha usiku huo wa baridi kwa njaa. Ghafla tukasikia mlango ukibishwa na mmoja wetu ambaye alishikwa njaa sna usiku huo wa baridi alikwenda kufungua mlango na kuuliza nani alikuwa anagonga mlango usiku wote huo.
Huko mlangoni akakutana na mtu mwenye uso wa kung'aa na wenye haiba na akasalimiana naye pale pale. alijibiwa kwa sauti ya kufurahisha. rafiki yetu akamwuliza huyo (mgeni) akauliza: 'mtapendelea kupata mgeni usiku huu? rafiki yetu akamkaribisha kwa dhati. huyo mgeni akaingia ndani na kukaa pamoja na sisi. Tulihisi furaha na faraja mioyoni mwetu kwa sababu ya huyo mgeni kuwa nasi. Alianza kuzungumza taratibu na kwa sauti ya kupendeza. Alitusimulia hadithi za mtume mtukufu(s.a.w.w)
na kumtaja mtume(s.a.w.w)
kuwa ni babu yetu'.
Baada ya muda mfupi, akatuambia kuwa hatukuwa tumekunywa chai na kuwa yeye alileta viungo vyote vya chai katika mfuko wake. sisi sote tulifurahika mno kwa sababu usiku huo wa baridi kama tusingeweza kupata chakula basi hata chai ingetutosheleza. mmoja wetu akatoa viamkajengo vyote pamoja na sufuria na makaa. mwenzetu alipokuwa anapika chai mgeni alikuwa akitufarajisha na hadithi muhimu sana. baada ya kunywa chai tukarudisha vyombo vyote na akanendelea kuzungumza na sisi. baada ya muda mfupi tu akatamka: "nyinyi nyote mna njaa kwa sababu hamkuwa na chakula chochote. toeni chakula mfukoni mwangu mle. sisi tulifurahi sana na ukarimu huo na tukamshukuru mungu. mmoja wetu akatoa chombo kilichojaa chakula kutoka katika mkoba huo.
Tulipofunua hicho chombo tuliona wali uliopikwa vizuri pamoja na nyama. chakula kilikuwa moto nacho kilipikwa muda mfupi tu uliopita. tukala mpaka kushiba. alipoona chakula kimebaki akatuambia tumpelekee mhudumu wa msikiti.
Usiku wa manane mgeni huyo akatushauri tulale. hivyo sote tukapata usingizi na kulala. Tulipoamka asubuhi tukaswali swala ya asubuhi na baadaye tulipokuwa tunajiandaa kurudi najaf tukamkumbuka mgeni wetu. Tukaanza kumtafuta kila mahali msikitini lakini hatukumwona. tulimwuliza mhudumu wa msikiti kama alimwona mtu yeyote lakini alijibu hakumwona mtu yeyote kuingia msikitini usiku maana milango ya msikiti ilifungwa. kwa hivyo, hakuna aliyeweza kuingia au kutoka.
kwa hivyo, sisi sote tulistaajabishwa. Baadaye tukang'amua kwamba vipi katika ule mkoba mdogo tuliweza kuona vyombo vya kupikia chai bila kuwemo vyakula humo ndani na baada ya muda mfupi tuliweza kupata vyombo vilivyojaa vyakula bila kuona alama yoyote ya vyombo vya kupikia chai. Zaidi ya hayo saa nyingi zilipita tangu huyo mgeni (imam Mahdi a.s.) alipofika na wakati chakula kilipoanza kugawanywa kilikuwa kimoto na chenye ladha na kututosheleza sote kumi na mmoja mpaka tushibe. hivyo, tukaamini kwamba hayo yote yaliyotokea yalikuwa miujiza. tena tukakumbuka kwamba huyo muadham (imam mahdi a.s.) alipokuwa akisimuli hadithi za mtume(s.a.w.w)
akimtaja mtume(s.a.w.w)
kuwa ni babu yake na mwishowe kutoweka machoni mwetu. Sote tulikuwa na hakika kwamba mgeni wetu aliyetufikia usiku uliopita hakuwa mtu yeyote mwingme ila imam wetu hadhrat hujjat
. tulisikitishwa sana kwamba hatukuweza kumtambua imam wetu usiku huo.
Kisachatano maskani ya imam wetu (imam mahdi a.s) katika hilla (iraq) agha hujjatul islam seyyid ali akbar khui mwanazuoni maarufu huko mashhad (iran) amesimulia: "nilipokwenda iraq kuzuru makaburi ya maimam wetu
nilikwenda hilla ambako niliona jengo lenye kuba. kwenye mlango mkuu niliona maandishi yakisema: "makamu sahebuzzaman" na watu wengi huzuru mahala hapo. Niliuliza watu kuhusu jengo hilo na nikaambiwa kwamba hilo jengo lilikuwa mali ya mwanazuoni agha sheikh ali hallawi ambaye alikuwa mcha mungu na kila saa akimkumbuka imam wetu
.
Yeye alikuwa akiuliza sababu gani imam
ilikuwa hajitokezi wakati hadithi husema kwamba masahaba 313 wa imam wanahitajika na wakati huu kuna waumini wengi duniani na hilla peke yake ina wanazuoni wacha mungu zaidi ya elfu moja. Hilo lilikuwa hoja kuhusu kujitokeza kwa imam
lililosumbua mara kwa mara alipokuwa anatembelea bustani nje ya mji. alikuwa amepotea katika mawazo hayo. Ghafla akamwona mwarabu mmoja anamkaribia na baada ya kusalimiana naye mwarabu huyo akamwuliza sababu iliyofanya azungumze peke yake kwa hasira. Akajibu kwamba dhuluma na dhambi zimetawala duniani kote lakini imam
hajitokezi.
Yeye (imam a.s.) anahitaji masahaba waaminifu 313 tu, ilihali katika hilla peke yake kuna wanazuoni wacha mungu zaidi ya elfu moja. Huyo sheikh akajibiwa: "eh sheikh, mimi ni imam wako na sivyo kama wewe unavyofikiri. katika hilla nzima wewe na yule mchinja nyama tu mnastahili kuwa masahaba wangu halisi. Nitakuthibitishia hayo. Nenda ukachague wanazuoni 40 wacha mungu katika hilla na uwaambie kwamba usiku wa alhamisi imam
atafika nyumbani kwako (kwa aga sheikh ali hallawi). Waalike kuja nyumbani kwako baada ya swala ya isha. wewe uwalete mbuzi wawili na uwafunge nyumbani kwako ghorofani na umwambie huyo mchinja nyama alete buchari yake.
Waweke hao wageni wakae sebuleni na mimi mwenyewe nitafika huko. sheikh alifurahi mno kusikia hayo lakini mara alijikuta yuko peke yake papo hapo, akaenda kuonana na mchinja nyama na kumhadithia mambo yote. baadaye kama alivyoagizwa akawaalika wanazuoni wacha mungu arubaini. ambao walifurahi sana kujua kuwa watamwona imam
kama ilivyoahidiwa. 'sheikh ali akanunua mbuzi wawili. usiku wa alhamisi watu walioalikwa walikusanyika nyumbani kwa sheikh ali na kujishughulisha katika dhikri ya mungu na kumswalia mtume(s.a.w.w)
pamoja na dhuria yake. katika muda mfupi harufu nzuri ikatapakaa kote na mwanga wenye nguvu ukamulika nyumba. Mwanga huo pole pole ukawapitia wote waliohudhuria sebuleni na ukaendelea huko juu ghorofani. Wote walishangaa na mshangao kusema kuwa imam
amefika na wakasoma takbir na salawat (takbir ni allahu akbar salawat ni kumswalia mtume(s.a.w.w)
pamoja na dhuria yake). Waliuona mwanga tu. hawakuona umbile la mtu yeyote.
Baada ya muda mfupi wakasikia sauti kutoka juu ikimtaka sheikh ali kumpeleka huyo mchinja nyama. Mchinja nyama huyo alipanda juu. Imam
akamwamrisha amchinje mbuzi mmoja. Kwa miujiza ya imam
huyo mbuzi hakupiga kelele hata kidogo. Damu ya huyo mbuzi aliyochinjwa ikatiririka kutoka darini mpaka chini uani. wageni walipoona hiyo damu wakaingiwa na hofu. wote hao wakaamini kwamba imam
amemchinja mwuza nyama. hapo tena wakasikia sauti nyingine kumtaka sheikh ali aende juu. sheikh ali alipoflka juu imam
akaamrisha huyo mbuzi wa pili achinjwe. Damu ya huyo mbuzi wa pili ilitiririka mpaka waliko wageni. Wageni hao wakatetemeka na kuamini kwamba hata sheikh ali amechinjwa. waliogopa na kufikiria kwamba sasa itakuwa zamu yao ya kuchinjwa. Basi wote wakakimbia na hata mmoja hakubakia.
Hapo tena imam
akamwambia sheikh ali aende huko chini na kuwaleta hao wageni, lakini alimwarifu kwamba hatamkuta hata mtu mmoja. sheikh ali alipofika sebuleni akaona watu wote wameondoka. kurudi juu kwa imam
alipigwa na butwa. Imam
hapo akamwuliza: "je, umesadiki hao watu wana imani namna gani juu ya imam wao?" kuokoa maisha yao wote wamekimbia, hawakuwa na subira hata ya kuonana na mimi. Kwa hivyo sasa wacha kukereka rohoni mwako kuhusu kujitokeza kwangu. katika wale watu arubaini uliowateua katika hilla, bila nyinyi wawili wote wamekimbia. Hali hiyo iko katika nchi". Baada ya kusema hayo imam
akatoweka. "kutukuza ziara ya imam
nyumbani kwa shekh ali, yeye (shekh ali) akatengeneza nyumba hiyo kwa upya na akatoa wakf na kuipa jina la "makamu sahiuz-zaman" hadi leo nyumba hiyo ipo hilla na watu wengi huizuru. Wengi wameomba haja zao na wamefanikiwa. Licha ya hilla tu kuna pahala pengine panapohusika na kufika kwa imam mahdi
.
1. Katika maziara ya wadisusalaam huko najaf kuna pahala panapojulikana kama makamu Sahibu zaman ambapo watu hufika kwa ajili ya ziara na hufanikiwa wanachoomba.
2. Baina ya kufa na najaf kuna msikiti unaojulikana kama sahla ba humo kuna nafasi inayonasibishwa na imam
.
3. Katika mji wa naa'maaniyyah, ulioko kati ya baghdaad na wasta kuna nafasi iliyopatiwa jina la imam
na watu wengi huenda huko kwa ajili ya ziara.
Kuna pahala pengine ambapo imam
hutembelea. nafasi hizo zilizotembelewa na imam
watu huenda kuzuru na kuomba dua zao. kama tulivyoeleza juu, katika pahala paitwapo na'maniyyah mwanazuoni mmoja sheikh ibne abil jawad alibahatika kuonana na imam
. Yeye anahadithia: "mimi nilibahatika kuonana na imam
na nikamwambia kuna pahala pawili patakatifu pamepatiwa jina lake, moja huko na'maniyyah na kwingine huko hilla. yeye (imam a.s.) akajibu" usiku kuamkia jumanne na siku ya jumanne mimi huja na'maniyyah. usiku wa kuamkia ijumaa na siku ya ijumaa mimi huenda hilla. Lakini wakazi wa hilla hawana tabia nzuri. hawaniheshimu mimi wala hawapaheshimu pahala pangu. Wanapoingia hawanisalimii na wala hawawaswalii babu zangu kumi na wawili. Mwumini yeyote akizuru pahala pangu hilla, akiniamkia asome salawat mara kumi na mbili, aswali rakaa mbili asikitike kwa mungu kumwomba mungu haja zake zisikilizwe.
Mimi (abiljawad) nikamwomba: "Eh bwana wangu, nifundishe hiyo dua inayotakiwa kusomwa hilla". Imam
akanisomea hiyo dua mara tatu ili niweze kuihifadhi kwa moyo. Dua biyo ni kama ifuatayo: "Allahumma kad akhzattaadibu minnl hatta massanniyadhur waanta arhamur raahimiiin, wain kana maktarafu minaaddhunub astahikku bihi azaf azaf ma addabtani bihi anta halimunzu antin ta'fuan kasir hatta yasbiku afwaka adhabak". Dua hiyo isomwe mara tatu na baada yake isomwe salawat.
Kisa cha sita mwujizawa kuponyesha jeraha pajani mwa ismail harkali mwanazuoni wa kishia ali ibne issa arbali amesimulia katika kitabu chake kashful ghumma tukio la ismail bin hassan harkali lililotokea katika kipindi cha utawala wa khalifa mustansir ukoo wa bani abbas. Yeye anahadithia kwamba ismail bin hassan harkali alifariki dunia akiwa rika yake lakini hakuwahi kuonana naye. Hata hivyo, alisimuliwa na mwanae harkali, shamsudin, hadithi alivyopokea kutoka baba yake. (ismail bin hassan harkali). Wakati nilipokuwa kijana nilipata jeraha kwenye paja la mguu wa kulia. Hilo jeraha lilizidi kachimba ndani kwa ndani na wakati wa kipupwe jeraha hutumbuka na kutoa damu na usaha kwa nguvu. Mimi nilisafiri kutoka mji wangu harkal kwenda hilla kupata ushauri wa mwanazuoni maarufu wa kishia mujtahid agha raziyyudin ali ibni tawiis.
Akanichukua kwa waganga wa hilla na kuwaonyesha jeraha lakini wote wakatoa ushauri mmoja kwamba hilo jeraha limechimba mpaka mishipa ya damu na kwa hivyo upasuaji wa jeraha hilo huweza kuhatarisha ukataji mishipa na kusababisha kifo popo hapo. kwa hivyo amenishauri nifuatane naye baghdad ambako tutaweza kuonana na waganga wa kikristo. Waganga wa kikristo baada ya kuangalia jeraha waliniambaia kwamba hakuna matibabu yake. Katika hali hiyo nikawaza kwamba huko kabla ya kurudi nyumbani nitazuru makaburi ya maimarn huko samarra. Mujtahid aliafikiana na wazo hilo na hata kunifanyia mpango wa fedha na mambo rnengine kuhusu safari hiyo. Nilipofika huko samarra (pahala walipozikwa maimam wawili):
1. Imam wa kumi, muhammad taqi aqs.
2. Imam wa kumi na moja, hassan askari
nikazuru makaburi mawili hayo na nikenda huko sardab sehemu iliyo chini ya ardhi. Huko nikasoma ziara, nikaomba mungu nikalia na kuomba msaada wa imam mahdi
.
Alhamisi asubuhi nikaenda nje ya jiji nikaoga mtoni, nikafua nguo zangu na nikarudi mjini. Nilipokaribia kuta za jiji nikawaona watu wanne juu ya farasi; wawili wao walikuwa vijana, na mmoja wa makamu na katika hao alikuwa mmoja mwenye haiba na uso mwangavu na upanga kiunoni. Mimi nilidhani hao ni wachungaji. Waliponiona wakasimama na kunisalimu na mimi nikajibu. Yule mtu mwenye haiba aliyekuwa katikati akasema: 'Ismail unataka kurudi nyumbani kwako kesho? Mimi nikajibu "ndio, ninahamu sana ya kurudi nyumbani." Mtu huyo akaniambia nimkaribie nami nikamkaribia na kufika karibu na farasi wake. Akauweka mkono wake mmoja begani kwangu na kuinama chini akalibinya jeraha langu kwa nguvu sana kwa mkono wa pili. Iliniletea maumivu mno. Baadaye akarudi kwenye farasi wake. mtu wa makamu aliyekuwa upande wa kulia akaniambia, "eh ismail umeponyeshwa" mimi nikajibu, "kwa rehema ya mungu sote tutapata uokovu. mimi nilishangazwa kuona kwamba ingawa jina langu lilikuwa likitajwa kila mara, lakini mimi nilikuwa simjui hata mmojawapo na nilikuwa mgeni kabisa katika hilo jiji. Baadaye huyo mtu wa makamu akanisimulia kwamba yule mtu aliye katikati ni mwenyewe imam Mahdi
.
Papo hapo nikamwangukia na kumbusu mguu wake. yeye akatangulia na mimi nikamfuata nyuma. Hapo hadhrat imam mahdi
akaniambia nirudi mjini lakini nikasema baada ya kuonana na imam
kamwe sitaachana naye. Hata hivyo, imam
akaniamrisha nirudi na kuongezea kwamba jambo hilo (la kurudi jijini) lilikuwa bora kwangu. Lakini mimi niliendelea kumfuata nyuma. mtu wa makamu akasema: "eh ismail huoni hata haya wakati imam anakwambia mara mbili mbili uende zako na wewe unaendelea kutotii amri yake?" mimi nikahuzunika sana na nikapigwa na bumbuwazi. Imam
akageuka na kuniambia: "utakapofika baghdad, khalifa abu jaffar mansur atakutumia mtu na atakapojua kuwa wewe umepona atakuzawadia dinari elfu moja. Usikubali zawadi hiyo, mwombe mwanangu seyyid ibni tawoos kwa kunitaja mimi amwandikie barua mfanyabiashara ali ibni awz akupe pesa kadri unavyohitaji na mimi vilevile nitamshauri huyo mfanyabiashara akupe pesa wewe."
Na hapo hao wapanda farasi wanne wakatoweka mimi nikabakia katika huzuni kuu na nikalia kwa nguvu sana. mwisho nikarudi samarra hali yangu ghairi na masikitiko. wahudumu wa makaburi ya maimam
waliponiona hali yangu walistaajabika na wakaniuliza kuhusu afya yangu. mimi nikawauliza hao wapand farasi wanne waliotoka nje ya jiji walikuwa nani? wao wakafikiri walikuwa wachunga wanaoishi karibu na jiji. nikawaeleza kwamba mmojawapo katika wale alikuwa hadhrat mahdi
. wao wakapigwa na butaa na wakasema wanashangazwa kwa nini mimi sikumwomba (imam mahdi a.s) aniponyeshe ugonjwa wangu. Hapo nikawaeleza tukio zima na nikaondoa nguo iliyofunika jeraha. (kabla ya hapo kwa majonzi ya kuachana na imam
mimi hata sikufikiria kuangalia jeraha). Wao wakasema kwa msisimko vilevile kwamba hakuna alama ya aina yoyote kuonyesha kulikuwa jeraha kwenye mapaja yote mawili. Papo hapo mimi nikazingirwa na watu wote ambao wakaanza kusoma salawat kwa ajili ya mtume mtukufu(s.a.w.w)
. kwa furaha kuu wakaanza kuchana nguo yangu ili kila mtu atabaruku na kipande cha hicho kitambaa.
Niliogopa kwamba watanikanyaga na nitakufa. wahudumu wakaingiwa na hofu na wakanibeba na kunitoa katika kikundi cha watu na kuniweka mahala pa usalama. Baada ya muda mfupi hakimu kutoka jiji akaja kwangu na kuniuliza siku gani niliondoka baghdad na mimi nikamjibu niliondoka wiki moja iliyopita. Siku ya pili saa nane nikaondoka kuelekea baghdad. nikapitisha usiku huo kwenye makazi nje ya baghdad na asubuhi yake nikaingia mjini. Habari kuhusu tukio langu zilikwishafika baghdad na umati mkubwa wa watu ulikuwa baghdad ukinisubiri kunikaribisha. Nilipofika darajani watu hao wakaniuliza jina langu. Waliposikia jina langu wakanizingira. wakaanza kuchana chana vipande vipande nguo zangu. polisi wakaingilia kati na kuniokoa. Wakanichukua mjini nako vilevile nikazungukwa na watu. Mujtahidi Seyyid Ali ibni Tawoos alikuja kuniona na mimi nikamhadithia tukio zima.
Huyo mujtahid aliwahi kuona jeraha hiyo na akainua nguo yangu kuangalia jeraha mwenyewe. Alipoona kuwa jeraha limepona kikamilifu na hakuna alama yoyote kuonyesha kidonda alizimia hapo hapo. alipopata fahamu akalia kwa nguvu sana na akanichukua kwa waziri wa khalifa mustansir. Waziri huyo alikuwa mkaazi wa qum na shia. Akaangalia mapaja yangu yote mawili na alipothibitisha kwamba hakuna alama yoyote us jeraha akawaita waganga wale bingwa wa kikristo nilioonana nao ili wajitosheleze nafsi zao. Hao waganga walithibitisha kwamba waliokwisha ona jeraha hilo na kwamba tiba ya pekee ilikuwa kupasua jeraha hilo ambalo lingeweza kuhatarisha maisha yangu. Waziri tena akawauliza hao waganga ingelichukua siku ngapi hilo jeraha kukauka limngekuwa limepasuliw? wakajibu muda usioweza kupungua miezi miwili, lakini kovu na hilo shimo lingebakia pale pale.
Waziri tena akawauliza kwamba muda gani umepita tokea wao kuona jeraha hilo na wakajibu ni siku kumi tu. Hapo waziri akanyanyua nguo yangu kwenmye paja na waganga wakashangazwa kuwa hapakuwa hata alama au kovu pahala pa jeraha, ila ngozi nyororo. Mganga mmoja wa kikristo akasema kwamba hiyo ni kazi ya bwana yesu. Waziri akajibu kwamba wao walishindwa kutibu hilo jeraha ambalo limetibiwa bila kuacha kovu au alama na waziri alielewa vizuri huo mwujiza ulikuwa wa nani.
Waziri akamjulisha khalifa mustansir ambaye akaniitisha kwake na kuangalia paja langu ili kujitosheleza nafsi yake kwamba huo mwujiza ulikuwa wa hadhrat mahdi
. Akanipa sarafu elfu moja za dhahabu lakini nilikataa kuzipokea. akaniuliza sababu gani nimekataa kuzipokea. nikamjibu kwamba imam
aliyeniponyesha ugonjwa wangu alinikataza kupokea hizo sarafu. Kusikia hayo khalifa alihuzunika na kulia. Mimi nikaondoka sebuleni kwake. kufuatana na maagizo ya imam
mujtahid seyyid ali ibni tawoos akaniandikia barua kwa ali ibni awz ambaye akanipa fedha nilizohitaji.
SHARTI YA KUCHAPA
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini
ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
MWISHO WA KITABU