ABU HURAIRAH
0%
Mwandishi: ASIYEJULIKANA
Kundi: VITABU VYA HADITHI
Mwandishi: ASIYEJULIKANA
Kundi:
Pakua: 6820
Maelezo zaidi:
Mwandishi: ASIYEJULIKANA
Kundi: VITABU VYA HADITHI
Mwandishi: ASIYEJULIKANA
Kundi:
ABU HURAIRAH
ABU HURAIRAH NA HADITH
Kila kitu, baadaye kilikuja kupitia yeye. Baadhi ya sheria na itikadi za Dini, yote hayo yalikuja kupitia sentenso zake ambazo hazikuwa katika dini asili hapo mwanzoni. Je ni sentenso ngapi unazozidhania wewe kuwa ziliwatenganisha Wakristo kuacha uasili wao?
Yupo mtu mmoja aitwaye Abu Hurairah ambaye historia yake mimi nitaweleteeni hapo mbele baada ya punde. Mtu huyu anasema mwenyewe : Amehadithia Abu Hurairah: Hakuna Sahaba hata mmoja wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kama mimi ambaye amehadithia Hadith zaidi yangu isipokuwa 'Abdallah bin Amr (bin al-'As) ambaye alikuwa akiziandika ambapo mimi sikufanya hivyo.
Juzuu zote tisa za Sahih Bukhari zina Ahadith 7,068. Kati ya hizo kiasi cha Ahadith 1100 zimenakiliwa na mtu huyu, yaani tuseme katika maneno mengine kuwa yeye amenakili Ahadith kiasi cha 15.56% za Ahadith zote za Sahih Bukhari (kiasi cha 1/6). (Hapa mbeleni nitawapatieni idadi sahihi za Ahadith alizozinakili Abu Hurairah katika Sahih Muslim).
Kama vile nilivyoonyesha juu ya "Abu Hurairah", yeye alijipinga mwenyewe na vile vile kisayansi. Hadith ifuatayo ni wazi ambapo yeye anainakili kwani inapingana na vile 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na 'Umm Salamah walivyoipokea. Iwapo sisi tutakubali kuwa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na 'Umm Salamah walikuwa katika nyumba ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) wakati mwingi zaidi kuliko wake zake wengine, basi kwa urahisi tutambua pale penye tatizo.
Haya yapo katika ukurasa wa 81, katika sura: Iwapo mtu aliye katika hali ya saumu akiamka asubuhi akiwa katika Janaba (je saumu yake itakuwa sahihi?) Hadith hii imetarjumiwa na mtarjumu tu hadi mwishoni mwa aya ya kwanza. Kufikia hapo, aliacha kutarjumu. Hata hivyo, bado ipo katika lugha ya Kiarabu. Kiasi kinachobakia ni tarjuma yangu. Iwapo wewe hautataka kuniamini, ninakushauri urejee katika maandishi ya Kiarabu. Zaid ya hayo, mimi nitakuletea vianzio zaidi kwa ajili ya kuelezea na tarjuma nilioyoifanya.
Amehadithia 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na Umm Salamah: "Baadhi za nyakati Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa akiamka asubuhi huku akiwa katika hali ya janaba baada ya kujamiiana na wake zake. Yeye alikuwa akioga na kufunga saumu.
Imehadithiwa na Abu Bakr bin 'Abdur-Rahman: Mimi na baba yangu tulimwendea'Aisha naye akasema: "Mimi ninatoa shuhuda kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) nyakati zingine alikuwa akiamka asubuhi akiwa katika hali ya Janaba kwa sababu ya kujamiiana, na wala si kutokwa manii usingizini na alikuwa akifunga saumu siku hiyo." Kutoka hapo alimwendea Ummu Salamah ambaye nae pia alihadithia hivyo hivyo.
Marwan alimwambia Abdu Rahmani ibn Harith: Kula kiapo kwa kuyasikia haya, Abu Hurairah atapiga makelele. Wakati huu, Marwani alikuwa mjini Madinah. Abu Bakr akasema: Abdu Rahmani hakupendezewa na haya. Baadaye ikatokezea kuwa tukakutana Dhil-Hulaifah ambapo Abu Hurairah alikuwa na kipande cha ardhi. Abdu Rahman akamwambia Abu Hurairah: Mimi nakwambia haya, na iwapo Marwan asingelikuwa ameniuliza mimi (kwa kula kiapo) haya, basi mimi nisingelizungumzia hayo kwako wewe. Ndipo hapo alipoitaja Hadith hiyo aliyoelezwa na 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na Ummu Salamah. Yeye (Abu Hurairah) alisema: Al-fadhli Ibn Abbas ameninakili mimi hivyo yeye ni mtu aliye elimika zaidi. Hammam na Ibn Abdullah Ibn Umar wamenakili kutokea Abu Hurairah kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliamrisha kufunguliwa kwa saumu (na msifunge), (ni dahiri) kuwa mapokezi ya mnyororo huo (ni kutokea 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na Umm Salamah) unaaminiwa zaidi.
Swali :
Abu-Hurairah (RA) alikuwa karibu mno na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa miaka michache, hata hakwenda sokoni? Je unaelewa ni kwa kipindi gani Abu-Hurairah alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ?
Jibu la swali linapatikana kutokea marejeo ya Ki-sunni:
1. Al-Milali wa Al-Nihal, ya ibn al-Jawzi, Pub. Egypt.
2. Sirat Ibn Hisham, Pub. Egypt.
Abu-Hurairah alisilimu miaka miwili tu kabla ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Hivyo, itawezekanaje kwake yeye kuripoti Ahadith 2000 katika Sahih Al-Bukhari peke yake, wakati ambapo zipo Ahadith chache kabisa zilizoripotiwa na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Al-Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Al-Imam Hussain ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) au Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) Je utaelezaje masuala kama haya? Mimi kwa hakika ninapendelea katika malengo na majibu yako ya kisayansi huku ukisaidiwa na baadhi ya marejeo.
Jibu :
1) Abu Hurairah alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa muda wa masaa24!!! Na hivyo ndivyo alivyoweza kuzielezea Ahadith zaidi
2) Yeye alizielezea Ahadith nyingi mno kwa sababu ya kuwa pamoja na Masahaba wengineo
Kwa hakika Masahaba walikuwa ni Waislamu wema na waliokuwa wakiaminiana, na hivyo ndivyo alivyoweza kuzichukua baadhi ya ahadith kutokea Masahaba
Jibu :
Ama kwa kuhusiana na upinganashi unaotolewa, kile niwezacho kukisema mimi ni kwamba inambidi msomaji arejee vitabu vya Fiq-h!!!! Na haya nimeyasema kwa mara nyingi zilizopita kwani kwa kuutolea uamuzi Hadith, inakubidi urejee vitabu vya Fiq-h. Kwani si jambo la moja kwa moja. Mfano wa kitabu cha Fiqhi al-Sunnah.
Kwa upande wa pili, iwapo wewe utakuwa na kitabu cha Fiq-h al-Sunnah naomba uzingatie kuwa wakati Said Sabiq (mmoja wa Wanazuoni wa Kisunni anayeheshimiwa na vile vile mwandishi wa vitabu vinavyotambulikana kama kitabu tulichokitaja hapo juu) anapozungumzia baadhi ya masuala, mara nyingine yeye huzungumzia kimtazamo wa Kishi'a kwa suala hilo. Kwa mfano: Zawaji al-Mut'ah, Qanun Al-Hawal Al-Shakhsiyyah (Kanuni za Ndoa).
Vile vile chunguza mwelekeo wake pale anapowazungumzia Waislamu Mashi'a au Wanazuoni wa Ki-Shi'a! Tafadhali sana naomba unijulishe kile unachokifikiria baada ya kupitia Sura mbili za kitabu hicho.
1
ABU HURAIRAH
WAPOKEZI WA HADITHI
Wapokezi wa Hadithi Miongoni mwa Masahaba wote na wale waliokuwa wamemtembelea Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , ni wachache tu ambao walioziripoti Ahadith katika Sahih Idadi yao ni ndogo kabisa hata kuliko idadi ya vidole. Wakati ambapo riwaya nyingine inasemwa kuwa kiasi cha watu 1400 walikwenda pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) huko Hudaibiyyah. Mji mtukufu wa Madina ulikuwa na wakazi zaidi ya 3000. Katika Vita vya Makkah (Fath-al-Mubin), zaidi ya watu 10,000 walishiriki. Katika Hajj ya mwisho ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , kiasi cha watu idadi hiyo walikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Kutokea watu wote hawa, ni watu wachache mno waliotajwa katika Sahih. Miongoni mwa hao waliotajwa wapo watu kama Abu Hurairah ambaye alisilimu kiasi cha miaka mitatu tu kabla ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Mtu mwingine ni 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa ambaye nae pia amenakiliwa Ahadith nyingi. Tuangalie alikuwa na umri gani:
Amehadithia babake Hisham: Bi.Khadija alifariki miaka mitatu kabla ya Hijrah ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwenda Madina. Na huko Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliishi kwa muda wa miaka miwili au zaidi na ndipo hapo alipomwoa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa aliyekuwa na umri wa miaka sita, na ndoa hiyo ilitimika pale alipokuwa na umri wa miaka tisa.
Mahisabu ya kirahisi yanasema:
1) Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimposa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa kabla ya Hijra ya kwenda Madina (mwaka mmoja kabla ya Hijra). Wakati huo 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa alikuwa na umri wa miaka sita.
(Riwaya nyingineyo inasema kuwa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa mwenyewe anasema kuwa yeye alikuwa bado akicheza na michezo ya kitoto katika siku hizo).
2) Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) almwoa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa katika mwaka wa pili wa Hijra, pale 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa alipokuwa na umri wa miaka tisa.
3) Tukuchukulia kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliishi kwa miaka 10 baada ya Hijrah, 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa aliishi kwa muda wa miaka 8 tu ya utu uzima wake pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Jambo moja napenda kuongezea hapa, nitatoa marejeo halisi, kuwa wanawake huwa ni watu wepesi kusahau maneno halisi au hata maneno yenyewe. Kwa hakika haya ni maumbile ya wanawake. Na hivyo kwa kuwa 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa alikuwa ni mwanamke hivyo ni jambo la kawaida kutegemea kuwa yeye pia atakuwa amesahau baadhi ya Ahadith katika hali ya uhalisi wake. Sasa naomba tuchunguze idadi ambazo mimi ninawaleteeni mbele yenu kuhusiana na watu mbalimbali waliozipokea ahadith. Mimi sidai kuwa idadi hiyo ni sahihi kabisa, kwani mimi mwenyewe sikuzihisabu kwa vidole. Ama kwa uhakika mimi binafsi nimezihisabu Ahadith zilizopokelewa na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na wana wake. Baadhi ya ahadith ambazo zimeandikwa na Imam Bukhari kwa kurejewa vile vile zimeingizwa katika idadi hiyo. Kimatokeo, itakubidi baadhi ya nyakati upunguze kwa 100 kutokea humo.
Jumla ya Ahadith zilizopo katika Juzuu 9 za Bukhari: 7,068
Na. JINA IDADI %
1 'Aisha bint Abu Bakr 1250 17.68
2 Abu Hurairah 1100 15.56
3 Ibn-Umar, mwana wa Umar 1100 15.56
4 Anas-Ibn-Malik 900 12.73
5 Abdullah-Ibn-'Abbas 700 9.9
6 Jobair-Ibn-'Abdullah 275 3.89
7 Abu-Musa-'Ashari 165 2.33
8 Abu-Said-Al-Khudhri 130 1.84
9 'Ali ibn Abi Talib 79 1.11
10 'Umar-Ibn-Khattab 50 0.71
11 Umm Salamah 48 0.68
12 Abdullah-Ibn-Masud 45 0.64
13 Muawiyah Ibn-Abu Sufian 10 0.14
14 Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib 8 0.11
15 Hussain ibn 'Ali ibn Abi Talib 2 0.03
16 Ali-Ibn-Husain 6 0.08
JUMLA 83
Kama vile uonavyo wewe mwenyewe katika jedwali la hapo juu, zimechukuliwa Ahadith chache kabisa zilizopokelewa na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na Watoto (Wajukuu wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) wake. Mimi sijawapatieni bado majina ya wengine waliozielezea Ahadith. Mwandishi wa kitabu hiki cha Bukhari alikuwa akiishi katika zama za Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) , mwana wa Al-Imam Zainul 'Abidiin(a.s) na vile vile zama za Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) Kwa hakika yeye hakutaja hata Hadith moja kutokea hao. Kwa hakika hiki ndicho kilikuwa ni kipindi ambacho Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) na Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) walikuwa wakizielezea Ahadith zilizowafikia wao kutokea Wazazi(a.s) wao hadi Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na, mwisho ambapo ndipo kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) mwenyewe. Katika maneno mengine, Imam Bukhari hakuwathamini hawa Watoto wa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) iwapo walistahili kuzielezea Ahadith, na aliwadhania wao kuwa ni waongo. Kwa hakika ukipitia vianzio vya Kishi'a, utaona kuwa watu hawa hawakuwa kimya bali walikuwa ni waelezaji wakubwa wa Ahadith za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kutokea Wazazi(a.s) wao hadi kufikia Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) mwenyewe. Je jambo hili si la kuvutia?
Kukiri? Hadithi ifuatayo si ngeni vile yaliyopo ndani mwa Hadith yanavyo kwenda. Mwanzani Abu Hurairah ananakili Hadith kutokea Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Na pale watu walipomwuliza iwapo yeye Abu Hurairah aliisikia mwenyewe hadith hiyo kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) au sivyo, yeye alijibu kuwa yeye hakumsikia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na akaielezea yeye mwenyewe.
1) Kile nikuombacho wewe unisaidie kuigawa hadith hiyo ya kwanza katika sehemu mbili :
a) Sehemu ya kwanza iwe ile ambayo imesemwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
b) Sehemu ile ambayo imesemwa na Abu Hurairah tu.
2) Nitakuomba unieleze kwa uwazi kabisa ni kwa nini watu walimwuliza iwapo maneno hayo yalikuwa yametamkwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Hadi pale kiwango cha elimu yangu inapohusika, watu waliuliza hivyo pale walipoisikia Hadith ikiwa ngeni kwao, kama vile Hadith zinazozungumzia mambo ya maishani na baadhi ya matukio ambayo yalikuwa hayaaminiki kwao, na ambayo kwa hakika yanatokezea nyakati hizi. Je ni jambo gani la kustaajabisha katika Hadith hii, na ni kwa nini watu walimwuliza Abu Hurairah iwapo alikuwa akizungumza kile alichokisikia kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) au sivyo.
3) Nitapendelea iwapo wewe kwa uwazi utaniambia kile ambacho kisingelitokea iwapo watu wasingelimwuliza Abu Hurairah iwapo sehemu yoyote ile ya hadith ilikuwa kwa hakika imezungumzwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) au sivyo.
4) Iwapo watu wasingelimwuliza Abu Hurairah iwapo Hadith hiyo ilikuwa imezungumwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) au sivyo, kidhahiri, watu wangeliichukulia Hadith nzima kama ni maneno aliyoyasema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Ukweli ni kwamba, vyovyote vile, Abu Hurairah amesema baadhi ya maneno yake mwenyewe na kuongezea baadhi ya maneno katika Hadith ambapo (inawezekana) imetamkwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Mimi nitapenda uniambie ni kwa nini unamwamini mtu kama huyo ambaye anaongezea baadhi ya maneno yake mwenyewe katika maneno ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
5) Je unaweza kuniorodheshea Hadith zote ambazo zimeelezwa na Abu Hurairah na kwamba zimekubaliwa na Imam Bukhari na Muslim, na kuchora mstari ulio wazi kabisa baina ya maneno yaliyozungumzwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) au Abu Hurairah mwenyewe. Kwa hakika mimi sielewei vile mtu anavyojiruhusu mwenyewe kuzungumza kile ambacho hajakisikia kutokea Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na hata akathubutu kuziingiza katika maneno ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) hata bila ya kutoa tahadhari. Au ni kwa nini anazungumzia vya kwake mwenyewe kabla ya kuelezea wazi wazi hapo mwanzoni mwa maneno yake kuwa hayo yalikuwa ni maneno yake binafsi na kamwe si ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ? Mfano wa pili unaonyesha wazi wazi kuwa Abu Hurairah ameongezea (inawezekana) katika yale aliyoyazungumza Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Je itakuwaje pale ambapo hakuna mtu yeyote aliyetutanabahisha kuhusu kuongezewa maneno ya ziada ya Abu Hurairah?
Amehadithia Abu Hurairah kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:
"Sadaqa iliyo bora kabisa ni ile ambayo itolewayo wakati mtu awapo tajiri, na mkono utoao ni bora kuliko mkono ule unaopokea, na wewe inakubidi uanze kuwasaidia kwanza wale wanaokutegemea.' Mke husema, 'Wewe ama unipatie chakula au talaqa.' Mtumwa husema, 'Nipe chakula na ufaidi huduma zangu.' Mtoto husema, 'Nipe chakula, je unaniachia kwa nani?' Watu wakasema: 'Ewe Abu Hurairah! Je hayo umeyasikia kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ?' Naye akajibu, 'La, bali hayo ni kutokana mimi mwenyewe."
Nitapenda kujua ni kwa nini Abu Hurairah alizoea kuongezea mahala penginepo pia? Anas bin Malik amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:
"Msifanye vinywaji katika Ad-Dubba' wala katika al-Muzaffat. Abu Hurairah alizoea kuongezea zaidi maneno al-Hantam na An-Naqir. Imehadithiwa na Abu Hurairah kuwa mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kusema:
"Mimi nilijamiiana na mke wangu katika siku ya Mwezi wa Ramadhani (akiwa katika saumu)." Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza:"Je unaweza kumfanya mtumwa mmoja awe huru?" Mtu huyo akajibu kuwa hawezi. Ndipo hapo tena Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipomwuliza:"Je unaweza kufunga saumu kwa muda wa miezi miwili mfululizo ?"
Tena mtu huyo akajibu kuwa asingeweza. Basi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akamwuliza: "Je unaweza kuwalisha masikini 60 ?" Hapa tena mtu huyo akajibu kuwa asingeliweza kuwalisha masikini sitini. (Abu Hurairah Akaongezea): Ndipo hapo kikapu kilichokuwa kimejaa tende kilipoletwa mbele ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na akamwambia mtu huyo, "Walishe (masikini) kwa haya kama kaffarah."
Mtu huyo akasema, (Je niwalishe haya) masikini kuliko sisi wenyewe? Hakuna nyumba ya wa masikini kuliko sisi baina ya milima ya Mji wa Madina." Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema, "Basi walishe watu wa nyumba yako kwa hayo." Asili Ya Abu Hurairah Masunni kwa kawaida huzitaja baadhi ya Ayah za Qur'an Tukufu kuonyesha kuwa Masahaba ambao walishiriki katika Viapo vya Hudaibiyyah wanalo daraja la juu (mema) na wanaheshimiwa mno. Vyema, hapa, mimi sitaki kujiingiza katika usahihi wa kuitafsiri na kuielewa kwake. Je wewe unajua kuwa wakati huo Abu Hurairah hakuwa Mwislamu, na wala hakuwa miongoni mwa wale walioshuhudia Viapo vya Hudaibiyyah ? Naam! Abu Hurairah kamwe hakushuhudia Viapo vya Hudaibiyyah! Abu Hurairah alikuwa Myahudi, na alisimu Siku ya Khaibar ambayo ilikuwapo mwaka mmoja baada ya Viapo vya Hudaibiyyah, na aliishi miaka mitatu tu pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
1. Abu Hurairah alisilimu siku ya Khaibar. Haya yanathibitishwa na Jabir ibn 'Abdullah (Hadith ya pili).
Abu Hurairah alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika siku ya Khaibar Mimi sihitajiki kusisitiza suala hili kuwa Vita vya Khaibar vilikuwa baina ya Waislamu na Mayahudi. Abu Hurairah alikuwa Myahudi kabla ya kusilimu.
2. Abu Hurairah alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa kipindi cha miaka mitatu tu (yeye mwenyewe anathibitisha hayo katika Hadith ya kwanza) "Nilikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa kipindi cha miaka mitatu"3)- Labda, wewe unaelewa vyema vile wengineo walivyomsalimia pale aliposilimu siku hiyo. Amehadithia Abu Hurairah: Mimi nilikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa muda wa miaka mitatu, na katika miaka iliyokuwa imebakia katika umri wangu nilikuwa na shauku kubwa ya kuzielewa ahadith za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kama vile nilivyokuwa katika miaka mitatu ile. Mimi nimemsikia akisema, akionyesha kwa mikono yake hivi: 'Kabla ya Saa, utapigana na watu ambao watakuwa na viatu vya manyoa na wakiishi al-Bariz.' (Sufiani, mnakili wa mnakili, alisema mara moja, "Na hao ndio watu wa al-Bazir."
Amehadithia Ja'bir bin 'Abdullah:
"Kuwa yeye alipigana katika Ghazwa kuelekea Najd pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na wakati Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliporejea , naye pia, alirejea nae. Wakati wa usingizi wa mchana uliwachukua wakati walipokuwa katika bonde lililokuwa limejaa miti ya miiba. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliteremka chini ya farasi wake na hivyo ndivyo walivyokuwa watu wote wakatawanyika katikati ya miti hiyo ya miiba, wakijistiri katika vivuli vya miti hiyo. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alijipatia kivuli chini ya mti wa Samura na kuuning'iniza upanga wake juu ya mti huo. Sisi tulilala kidogo ambapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alituita kwa ghafla, na tulipomwendea tukakuta kuwa Mbedui mmoja alikuwa ameketi pamoja nae. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema kuwa Mbedui huyo aliuchukua upanga wake kutokea ala yake wakati yeye akiwa amelala. Wakati nilipoamka, nikaukuta upanga huo upo mkononi mwake na akiniambia "Je ni nani anayeweza kukuokoa kwangu?" Mimi nikamjibu, "Allah swt" Na sasa huyu hapa ameketi." Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) hakumwadhibu (kwa hayo).
Kwa kupitia kundi lingine la waelezaji wengine wa riwaya, Ja'bir alisema: "Sisi tulikua pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) (katika Vita vya) Dhat-ul-Riqa', na tulitokezea chini ya mti wenye kivuli na tukamwachia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) (apumzike chini ya kivuli chake). Alitokezea Mapagani mmoja huku upanga wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ulipokuwa ukining'inia mtini. Mpagani huyo aliutoa upanga huo kutokea ala yake kwa kisiri na alimwambia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) 'Je waniogopa mimi?' Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimjibu, 'hapana.' Ndipo hapo Mpagani huyo aliposema,'Je ni nani anayeweza kukuokoa wewe kutoka kwangu?' Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimjibu, 'Allah swt.' Masahaba wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) walimtishia huyo, na mara Iqamah ya Sala ilisemwa, na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisali raka'a mbili za Sala ya Khofu pamoja na kundi mojawapo ya makundi mawili, na kundi hilo lilikwenda pembeni, na hapo tena Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisali Raka'a mbili zinginezo pamoja na kundi lingine. Hivyo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisali jumla ya Raka'a nne ambapo watu walisali raka'a mbili tu."
(Mwelezaji wa mwelezaji) Abu Bishr aliongezea, Mtu huyo alikuwa Ghaurath bin al-Harith na Vita vilipiganwa dhidi ya Muharib Khasafa." Jabir akaongezea, "Sisi tulikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) hapo Nakhl ambapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisali Sala ya Khofu." Abu Hurairah akasema, "Mimi nilisali sala ya Khofu pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) wakati wa Ghazwa (yaani Vita) vya Najd." Abu Hurairah alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) siku ya Khaibar !! Amehadithia 'Anbasa bin Said:
Abu Hurairah alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kumwuliza (kutaka hisa katika mali iliyopatikana katika Vita vya Khaibar au ngawira). Kwa hayo, mmoja wa wana wa Said bin al-'As alimwambia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) 'Ewe Mtume wa Allah swt ! Usimpe huyo (Abu Hurairah).' Kwa hayo Abu Hurairah alimwambia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) 'Huyu ndiye mwuaji wa Ibn Qauqal.' Mwana wa Sa'id akasema, 'Maajabu gani! Jitu dogo (au mwovu) litokalo Qadum Ad-Dan!" Amehadithia Abu Hurairah: Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimtuma Aban kutokea Madina kwenda Najd akiwa Kamanda wa Sariya. Aban na wenzake walimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) huko Khaibar baada ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akiwa ameishaikomboa Khaibar, na mafigo ya farasi zao zilitengenezwa kwa moto wa mitende. Mimi nilisema, 'Ewe Mtume wa Allah swt! Usiwape hisa ya Ngawira.' Kwa hayo Aban akasema ( kuniambia mimi), "Maajabu! Wewe unashauri jambo ingawaje wewe ni wewe, ewe mtu mdogo (au mwovu) utokeae Ad-Dal (myungiyungi)!" Kwa kuyasikia hayo, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema, "Ewe Aban, kaa chini!" Na hakuwapa hisa yoyote.
Amehadithia Said: Aban bin Said alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kumsalimia. Abu Hurairah akasema, Ewe Mtume wa Allah swt! Huyu (Aban) ni mwuaji wa Ibn Qauqal." (Kwa kuyasikia hayo), Aban alimwambia Abu Hurairah, "Usemayo wewe yanavyostaajabisha! Ewe, mtu mdogo (au mwovu) ukitokea Qadum Dan, ukinituhumu mimi kwa (mauaji) ya mtu ambaye Allah swt amemjaalia (shahada) kwa mikono yangu, na kwamba Allah swt ameharamisha udhalilisho wangu mikononi mwake.'
2
ABU HURAIRAH
HALI YAKE KIAKILI NA KIMWILI
1. Baada ya Abu Hurairah kusilimu, alikuwa hana kitu chochote. Yeye alikuwa akiwaambia watu wasome Ayah ya Qur'an Tukufu, si kwamba alikuwa akitaka kufaidika nayo.
Yeye alikuwa akitaka mtu huyo awe na hisia ya kidini na hivyo aweze kumwalika Abu Hurairah kwa ajili ya chakula cha mchana au usiku.
Suala hili linajulika vyema kabisa kama "Kuchanganya Tumbo na Dini." Au kuchanganya Dini na pesa, tumbo, uwezo, au kwa vitu vya kawaida , au visivyo na maana).
2. Hata watu hawaamini kuwa Abu Hurairah anaweza kuhadithia hadith kiasi hicho. (Hakuna marejeo sasa: Imesemwa kuwa Abu Hurairah amehadithia Hadithi 40,000 katika uhai wake. Tukigawa Hadith hizo kwa kipindi cha miaka mitatu ya Usahaba wake, tunapata Hadith 36 kwa siku (!!! ).
Marejeo niliyokwishayatoa hapo nyuma zinathibitisha kuwa, yeye mwenyewe Abu Hurairah, amekiri kuwa hakuna mtu yeyote miongoni mwa Masahaba ambaye amehadithia Hadith nyingi kama za kwake. Tukitambua ukweli huu kuwa yeye ndiye mtu wa pili katika kiwango cha kuhadithia wingi wa Ahadith katika Bukhari na Muslim, basi tunafikia uamuzi kuwa yeye Abu Hurairah atakuwa amehadithia Hadith nyingi mno zaidi ya hizo ambazo zimerekodiwa katika vitabu hivi viwili.
Katika mojawapo ya Hadith, yeye Abu Hurairah mwenyewe, amekiri kuwa watu walikuwa wakimtuhumu yeye kwa ukichaa au mwenda wazimu.
3. Jambo la kuvutia hapa ni kwamba hakuna hata Hadith moja iliyohadithiwa na mtu yeyote mwingine (mbali na yeye Abu Hurairah mwenyewe) kuzungumzia mema ya Abu Hurairah. Iwapo wewe utachunguza Bukhari na Muslim nzima kuhusu sifa ya Abu Hurairah, basi Hadith yoyote ile utakayoipata kuhusiana na Usahaba wake pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na elimu yake basi itakuwa imehadithiwa na yeye mwenyewe (Abu Hurairah mwenyewe na wala si mtu mwingine)! Ambapo upande mwingine, wewe utakaposoma wema na sifa za Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) (na wengineo kama Salman, Umar, Zubair ), basi utaona kuwa wapo wengine wanaomsifu Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) (na wengineo) kwa Hadith mbalimbali. Lakini haya vyovyote vile hayapatikani pamoja na Abu Hurairah. Hadith zote kama: Mimi nilikuwa mtoto mzuri, au nilifanya hivi na vile zimehadithiwa na Abu Hurairah mwenyewe tu (na wala si mtu mwingine).
Mimi nakutaka unijibu iwapo utakubaliwa ushahidi wa mtu ajisemaye kuwa yeye ni mtoto mwema. Amehadithia Abu Hurairah: "Watu walikuwa na desturi ya kusema kuwa Abu Hurairah anahadithia Hadith nyingi mno." Kwa hakika mimi daima nilijiweka karibu mno na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na nilikuwa nikiridhika kwa kile kilichoshibisha tumbo langu. Mimi sikula mkate uliochachuka na wala sikuvaa mavazi yalirembeshwa kwa mistari, na kamwe hakuna mwanamme au mwanamke aliyekuwa amenihudumia mimi, na mara nyingi nilikuwa nikilibana tumbo langu kwa mawe kwa sababu za njaa, na mimi nilikuwa nikiwaambia watu wanisomee Ayah ya Qur'an Tukufu ingawaje nilikuwa nikiijua, ili kwamba anichukue nyumbani kwake na kunilisha chakula. Kwa hakika miongoni mwa watu waliokuwa wakarimu kwa masikini kuliko wote alikuwa ni Ja'far bin Abi Talib. Kwa hakika yeye alikuwa akituchukua nyumbani kwake na kutulisha chochote kile kilichokuwapo. Yeye vile vile alikuwa akitupatia mifuko (ya ngozi) tupu ya siagi ambayo alikuwa akiichana na tukilamba chochote kile kilichokuwamo ndani yake."
Amehadithia Abu Hurairah:
"Mimi niliambatana na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa ajili ya kulijaza tumbo langu; na ndiyo kwa maana hiyo mimi sikula mkate uliochomwa wala kuvaa nguo za hariri. Na wala hakuna mtumwa kijakazi wala wa kiume aliyenihudumia mimi, nami nilikuwa nikijifunga mawe tumboni mwangu na nilikuwa nikimwomba mtu yeyote anisomee Ayah ya Qur'an Tukufu ingawaje nilikuwa nikiijua, ili kwamba inawezekana akanichukua nyumbani kwake na kunilisha chakula. Ja'far bin Abi Talib alikuwa mkarimu kwa masikini, yeye alikuwa akituchukua nyumbani kwake na kutulisha chochote kile alichokuwanacho nyumbani mwake, (na kama kulikuwa hakuna chochote kile), yeye alikuwa akitupatia mifuko mitupu ya ngozi (ya asali au siagi) ambapo sisi tulikuwa tukichana na kulamba chochote kilichokuwamo kimebakia."
Amehadithia Muhammad:
Sisi tulikuwa pamoja na Abu Hurairah pale alipokuwa akivaa nguo mbili za katani zilizokuwa zimetiwa rangi ya udongo mwekundu. Yeye alisafisha pua yake kwa nguo hiyo huku akisema, 'Hongera! Vyema sana! Abu Hurairah anasafisha pua yake kwa katani! Ulifika wakati ambapo mimi nilikuwa nikianguka bila fahamu baina ya Mimbar ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na nyumba ya 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa ambapo mtu aliyekuwa akipita hapo alinikanyaga shingoni kwa miguu yake, wakinichukulia mimi kuwa mwenda wazimu (kichaa), lakina kwa hakika, mimi sikuwa na ukichaa wowote, mimi sikuugua chochote kile isipokuwa njaa tu."
Amehadithia Abu Hurairah:
Wakati mmoja ambapo nilipokuwa katika hali ya ulegevu (kwa kutokana na njaa kali), nilionana na 'Umar bin al-Khattab, hivyo nilimwomba anisomee Ayah ya Qur'an Tukufu. Yeye aliingia nyumbani mwake na kunitafsiria. (Na mimi niliondoka zangu) baada ya kutembea umbali kidogo, nilidondoka chini juu ya uso wangu kwa sababu ya ulegevu wangu ambao ulitokana na njaa kali mno. Mara ghafla nikamkuta Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akiwa amesimama kichwani mwangu. Akaniambia, "Ewe Abu Hurairah!" Nami nikamjibu, "Labbaik ewe Mtume wa Allah swt na Siddiq!" kwa hayo akanishika mkono, na kuniinua. Ndipo alipokuja kujua kile kilichokuwa kikinisumbua. Hivyo akanichukua nyumbani kwake na akaniagizia bakuli kubwa la maziwa kwa ajili yangu. Mimi niliyanywa maziwa hayo, na ndipo hapo aliponiambia, "Kunya mengine, Ewe Abu Hurairah!!" Hivyo, mimi niliyanywa tena, kwa kumaliza, ambapo tena alisema, "Kunya zaidi." Hivyo mimi niliyanywa tena hadi pale tumbo langu lilipojaa na kuonekana kama bakuli.
Baadaye mimi nilikutana na 'Umar na kumwelezea yote hayo yaliyotokea, na kumwambia, "Mtu fulani, ambaye anayestahiki zaidi yako wewe, alilichukua suala hili. Kwa kiapo cha Allah swt, mimi nilikwambia wewe unisomee Ayah ya Qur'an Tukufu wakati ambapo mimi ninazielewa vyema zaidi yako wewe." Kwa hayo 'Umar aliniambia, "Kwa kiapo cha Allah swt! Iwapo ningalikubali na kukushughulikia wewe, basi ingalinipendezea kwangu mimi kuliko kuwa na ngamia wazuri wekundu." Kujaaliwa kwa ghafla uwezo maalum zaidi Je hautaingiwa na shaka iwapo mtu akijaaliwa kwa ghafla uwezo maalum zaidi ya watu wengine, lakini sisi hatujawahi kusikia kuwa Abu Hurairah alikuwa na uwezo maalumu zaidi ya watu wengine. Ghafla anatokezea mbele ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kuishi nae kwa muda wa miaka mitatu na tunaona kuwa anakumbuka kila kitu kwa nguvu fulani za kiajabu ?
Jambo hili si la kumfanya mtu awe Msunni au Mshi'a kwa kuulizia je Abu Hurairah alikuwa akiropoka ? Mtu huyu alikuwa akiutumia muda wake mdogo huo pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa kujipatia faida zake binafsi na kuendelea kujipatia uhusiano kila pale palipojitokeza jambo ambalo lilihitaji ushauri na maoni, basi kwa nini yeye alijitokeza pamoja na Hadith ambayo yeye kwa haraka kabisa aliikumbuka kwa ukamilifu!! Hususan Abu Hurairah alikuwa akimchukia 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na ni jambo la kuzingatiwa kuwa yeye alitunga hadith ambayo 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa aliipinga wazi wazi kabisa.
Jambo la kustaajabisha ni kwamba ubongo wa Abu Hurairah uligeuka kuwa wa ajabu kabisa baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Jambo lolote au suala lolote lililojitokeza wakati wowote ule, basi yeye alizungumzia mambo ambayo hakuna mtu mwingine aliyejua au kuyasikia hapo kabla. Wow! Kwa hakika tunaona wazi kuwa mtu huyu alikuwa akijitakia manufaa kwa ajili yake katika kujipatia nafasi na harakati zake za kisiasa na kijamii. Kuhadithia Hadith Nyingi Mno ? 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa amehadithia Hadith (1250) nyingi mno kuliko Abu Hurairah katika Sahih Bukhari. Ibn Umar amehadithia (1100) kiasi kama cha Abu Hurairah (1100) katika Bukhari. Idadi nimezitaja hapo awali katika jedwali. Mimi sikuulizia ni kwa nini 'Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa ameripoti hadith nyingi kiasi hicho kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na wala sikuulizia kuhusu Ibn 'umar, au Ibn 'Abbas au wengineo.
Lakini nilichokiuliza ni: Itawezekanaje kwa mtu aliyekuwa kasoro ya miaka mitatu aweze kuhadithia Hadith nyingi kiasi hicho? Tunayaachilia mengineyo. Abu Hurairah amehadithia hadith 5,374 tu. Iwapo tutachukua kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa miaka mitatu kamili pamoja na Abu Hurairah: 5,374/3 = 1791.33 Ahadith kwa mwaka, 1791.33/(365-11) = 5.06 Ahadith kwa siku.
Wewe utaniuliza kwa vipi tena? Je itawezekanaje kwa mtu kufanya hivyo kila siku? Je kwa nini alikuwa amejitolea kiasi hicho ambapo kulikuwapo watu waliokuwa bora zaidi kuliko yeye, kama vile 'Umar, mtoto wake, Ibn 'Abbas na Abu Bakr hawakuweza kufanya hivyo? ( Kwa uzani wa Abu Hurairah, hata Hadith 5 kwa siku?) Bila ya kutaja kuwa Abu Hurairah amehadithia Hadith zaidi mno kuliko Sahaba yeyote, kutegemea kauli yake mwenyewe. Baadhi wanasema kuwa Abu Hurairah amehadithia kiasi cha Hadith 40,000. Hata watu walikuwapo karibu nae walishangazwa na mtu huyu kwa kuhadithia kwake huku ( kwa kutegemea kauli ya Abu Hurairah mwenyewe). Sehemu ya pili ni kwa nini mtu kama huyu amehadithia sawa na riwaya za Agano la Kale? ( sehemu ambazo zimekanushwa na itikadi na imani za Kiislamu?)
Sasa ndipo wewe unaanza kuhisi nakisi ya elimu yako. Je unajua kuwa Sahaba na Ndugu wa Kijamaa wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Abdullah Ibn Abbas alipewa baraka za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na siku moja alimpiga kwa mkono kifua chake na alimwomba Allah swt akisema: "Allahumma faqqihhu fiddini wa 'allimhu min ta'uwili l kitabi" ( Ewe Allah swt! Mjaalie elimu ya Dini na mfanye mfasiri wa Kitabu (yaani Qur'an Tukufu)? Na kwa muujiza, Ibn 'Abbas akawa Hibr l umma (Imam wa 'Ummah), hiyo ilikuwa ni muujiza mojawapo wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Vivyo hivyo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alivyomwombea Abu Hurairah wakati alipolalamikia udhaifu wa kukumbuka kwake: Kama vile ulivyojionea kuwa Ibn 'Abbas (R) anatambuliwa hata na Masahaba wengineo kuwa yeye alikuwa akiijua taawil (tafsiri) ya Qur'an Tukufu. Kwa hakika huku ni tofauti na kukariri ! Leo hii tunawaona watu wengi wakikariri Qur'an Tukufu nzima, lakini haimaanishi kuwa wao wanajua maana halisi iliyomo.
Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ni mtu mwingine ambaye alisema kuwa hakuna Ayah yoyote katika Qur'an Tukufu ambayo yeye alikuwa haijui ilipoteremshwa na sababu ya kuteremshwa kwake na nini kilichokuwa kikimaanishwa. Kwa hakika Masahaba wengi walitambua haya kuhusu Shakhsiyyah hizi na zipo Ahadith zinazosadikiwa katika kuthibitisha elimu yao hiyo. Sasa, tukirejea kwa Abu Hurairah, sisi hatuoni mahala popote kuwa Abu Hurairah aliipata kipaji hiki cha maajabu yoyote baada ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kumwombea dua!!!
Vile vile nitapenda kuongezea usahihisho kuwa Abu Hurairah baada ya kuishi kwake kwa kipindi kasoro ya miaka mitatu pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , hakuhadithia au alijiepusha na kuzisema Ahadith katika zama za makhalifa watatu Abu Hurairah alianza kuhadithia Hadith hususan katika kipindi cha Mu'awiyah ibn Abu Sufian yaani takriban miaka 30 baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Hivyo yeye alijiwekea kifuani mwake Hadith hizo 3000 na zaidi kwa kipindi chote hicho bila ya kumwambia mtu yeyote.
Ushahidi nilionao ni kwamba Abu Bakr, Umar na 'Uthman hawakuruhusu usemaji na uandishi wa Hadith. Imeripotiwa kuwa Abu Hurairah aliulizwa iwapo alihadithia Hadith katika zama za 'Utman bin 'Affan? Abu Hurairah alijibu kuwa yeye asingelithubutu kufanya hivyo, kwani wao wangalimpiga iwapo angelithubutu kuhadithia Hadith!!
Kwa hakika si kosa kuchunguza maisha na mienendo ya Sahaba yeyote, hususan Abu Hurairah. Kwani wote hao ni wanaadamu tu ambao wanaweza kukosea kwa madaraja mbalimbali, na wala hatusemi kuwa Allah swt hawezi kuwasamehe makosa yao, iwapo Allah swt mwenyewe ataamua kufanya hivyo. Hivyo ni wajibu wetu kutambua wazi kuhusu wale tunaowafuata iwapo kweli ni waaminifu ili tusije tukapotoka kwani Allah swt ametujaalia neema kubwa mno ambayo ni fahamu na akili. Hivyo iwapo tutawaona kuwa hawafai au wapo mashakani, basi tujiepushe nao ili tusije tukaiharibu Akhera yetu.
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
YALIYOMO
ABU HURAIRAH 1
ABU HURAIRAH NA HADITH 1
ABU HURAIRAH 4
WAPOKEZI WA HADITHI 4
ABU HURAIRAH 10
HALI YAKE KIAKILI NA KIMWILI 10
ABU HURAIRAH KUPATA FAHAMU YA AJABU 13
SHARTI YA KUCHAPA 14
MWISHO WA KITABU 14
YALIYOMO 15