24
TAFSIRI YA QURANI AL-MIIZAAN
SURA QAARIA ( KIYAMA) (NA. 101)
INA AYA 11
Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehemai, Mwenye kurehemu
الْقَارِعَةُ ﴿١﴾
1. Kiyama!
مَا الْقَارِعَةُ ﴿٢﴾
2. Ni nini Kiyama?
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ ﴿٣﴾
3. Na nini lipi lakukujulisha ni nini Kiyama?
يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ ﴿٤﴾
4. Ni siku ambayo watu watakuwa kama panzi waliotawanywa.
وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنفُوشِ ﴿٥﴾
5. Na yakawa majabali kama sufi iliyopurwa.
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾
6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito.
فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾
7. Yeye atakuwa katika maisha yenye kuridhiwa.
وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ﴿٨﴾
8. Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi.
فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ ﴿٩﴾
9. Basi makaza yake yatakuwa ni Hawiya.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ ﴿١٠﴾
10. Na ni lipi la kujulisha wewe nini hiyo ( Hawiya).
نَارٌ حَامِيَةٌ ﴿١١﴾
11. (Hawiya) ni moto uliomkali mno.
UBAINIFU
Sura hii inatoa onyo juu ya Kiyama.Imeshuka Makka.
Aya Ya 1-3
Neno Qari'ah linatokana na Qur'u lenye maana ya kugonga sana, nalo ni mojawapo katika majina ya Kiyama. Imesemwa kuwa Kiyama kimeitwa hivyo, kwa sababu kinagonga nyoyo fazaa na kinawagonga maadui wa Mwenyezi Mungu kwa adhabu.
Aya Ya 4
Yaani siku hiyo ya Kiyama watu watakuwa kama panzi waliotapanyika, kutokana na mfazaiko. Imesemwa kuwa watu siku ya kufufuliwa wamefananishwa na panzi, kwa vile panzi wanaporuka hawaeleki upande mmoja kama desturi ya ndege wengine. Bsi vile vile watu watakapotoka makaburini mwao watakuwa wameshikwa na fazaa; wataelekea pande mbali mbali; au wataelekea sehemu zao mbalimbali za uovu au wema.
Aya Ya 5-7
Inaashiria juu ya uzani wa amal ( Matendo); kwamba kuna matendo mazito ambayo yana daraja mbele ya Mwenyezi Mungu nayo ni iman na twaa (Utii) na kuna yale ambayo hayana uzani wowote nayo ni kufuru na uasi. Kwa hiyo mwenye kuwa na amali zenye uzani uzito atakuwa katika maisha atakayoyaridhia.
Aya Ya 8
Neno Hawiya lenye maana ya kuporomoka ni mojawapo ya majina ya Jahannam; imeitwa hivyo kwa vile mtu atakayeingizwa humo ataporomoka hadi chini ya waliochini; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Kisha tukamrudisha chini ya waliochini, ila wale walioamini
"(95:5-6)".
Kuusifu moto kwa neno Hawiya ni fumbo kama fumbo la kuyasifu maisha ya kuridhiwa kuileta ibara ya makazi kwa neno Ummu lenye maana ya mama, ni kwa sababu ndiyo marejeo ya huyo mwenye uzani mwepesi, kama anavyorejea mtoto kwa mama yake. Imesemwa kuwa makusudio ya Ummu ni Ummur- ra'as yaani fuvu la kichwa chake, kwa maana yakuwa ataangukia kichwa chake katika Jahannam, lakini kauli inawekwa mbali na kubakia dhamiri bila ya mahali inapoashiria katika neno Maahiya inayofasiriwa na aya 11.
Aya Ya 10
Jumla hiyo ni kulifanya kubwa jambo la huo moto.
Aya Ya 11
Moto mkali, yaani wenye kuchomwa sana. Na hilo ni jawabu na tafsiri ya aya 1.
Utafiti Wa Hadith Katika Tafsri ya Qummi katika neno lake Mwenyezi Mungu " Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi". Yaani wepesi katika mambo mema. Na kuhusu Ummu amesema ni fuvu la kichwa chake yaani atatupwa katika Jahannam kichwa- kichwa.
Katika Durril Manthur ametoa Ibn Murdawayah kutoka kwa Abu Ayyub El- Ansari, kwamaba Mtume(s.a.w.w)
amesema: " Hakika nafsi ya muumin inapochukuliwa hukutana na watu wa rehema katika waja wa Mwenyezi Mungu na watu wema kutoka duniani; watasema: Mwaangalieni mwenzenu anastarehe kwani yeye alikuwa katika mashaka makubwa; kisha watamuuliza: fulani na fulani wamefanya nini? Je Fulani ameolewa? Na watakapomuulizia mtu aliyekufa kabla yake, atasema: huyo amekufa kabla yangu. Halafu watasema: " Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Amekwishapelekwa kwenye makazi yake ya Hawiya, ni makazi mabaya na malezi mabaya." Na imepokewa hadith kwa maana haya kutoka kwa Anas bin Malik, na kutoka kwa Hassan na Ash'ath bin Abdalla Ama.
SURA TAKATHUR ( KUTAKA WINGI WA MALI) (NA. 102)
INA AYA 8
Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ﴿١﴾
1. Kumewashughulisha mno kutaka wingi wa mali.
حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ ﴿٢﴾
2. Mpaka mzuru makaburi.
كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣﴾
3. Komeni! Hapo mtajua.
ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾
4. Kisha komeni! Hapo mtajua.
كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ ﴿٥﴾
5. Si hivyo! lau mngejua ujuzi wa yakini (msinge jishughulisha na hayo).
لَتَرَوُنَّ الْجَحِيمَ ﴿٦﴾
6. Hakika mtauona moto.
ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيْنَ الْيَقِينِ ﴿٧﴾
7. Kisha mtauona kwa jicho la yakini.
ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾
8. Lisha mtaulizwa siku hiyo matumizi ya neema mlizopewa.
UBAINIFU
Makaripio makubwa kwa watu kutokana na kujishughulisha kwao kwa wingi wa mali na watoto na kusahau mambo yanayofuatia miongoni mwa hasara na adhabu. Vile vile ni utisho kwamba wao watajua, wataona adhabu na kuulizwa neema waliyopewa ili washukuru, lakini wakabadilisha neema hiyo kuwa kufuru. Sura hii uinaweza kuwa imeshuka Makka au Madina Maelezo zaidi yatakuja katika utafiti wa hadithi kuhusu sababu za kushuka kwake, (Inshallah).
Aya Ya 1-2
Maana ya aya hizi mzunguko ni kuwa: mmeshughulika sana na kuzama katika starehe za dunia na vipambo vyake na kushindana katika wingi wa vitu, jambo ambalo limewafanya muache jambo muhimu la kumtaja Mwenyezi Mungu, mpaka mkafikiwa na kifo. Kughafilika kwenu kumewatia upofu katika maisha yenu yote. Imesemwa kuwa maana yake ni kuwa kumewashughulisha nyinyi kujifaharisha kwa wingi wa watu. Hawa wanasema "Sisi tuna watu wengi zaidi". Na wengine wanasema "Sisi tuna watu wengi hata mlipomaliza kuhisabu waliohai mkaenda makaburini kuwahesabu waliokufa katika watu wenu. Hivyo basi mkashindana pia kuwahisabu wafu wenu".
Maana haya ndiyo yaliyoko katika mpangilio wa yale yaliyopokewa kuhusu sababu za kushuka Sura hii, kwamba makabila mawili katika Ansar yalijifakharisha waliohai na waliokufa. Katika baadhi ya yaliyopokewa ni kwamba hayo yalikuwa Makka kati ya Abdu Manaaf na Bani Sahm. Kitakuja kisa chake katika utafiti wa hadithi (Inshallah).
Aya Ya 3
Makemeo na vitisho kutokana na kujishughulisha na mambo yasiyokuwa na umuhimu wowote.
Aya Ya 4
Kusisitiza yale yaliyotangulia katika aya ya 3. Imesemwa kuwa makusudio ya aya ya 3 ni kwamba watayojua hayo wakati wa kufa, na aya ya 4 kuwa watayajua wakati wa kufufuliwa.
Aya Ya 5
Makemeo baada ya makemeo, kwa kusisitiza. Na 'yakini' ni elimu ambayo haina shaka yoyote. Jawabu la 'Lau' limeondolewa, ambalo makadirio yake ni "Lau mngejua ujuzi wa yakini msingejishughulisha na hayo".
Aya Ya 6
Ni jumla nyengine inayoanza, na wala siyo jawabu la lau ya aya ya 5. Makusudio yake ni kuuona moto kwa moyo kabla ya kuuona kwa macho siku ya Kiyama, kutokana na inavyoonyesha katika neno lake Mwenyezi Mungu: "Na utadhihirishwa moto kwa mwenye kuona
". (79:36).
Aya Ya 7
Makusudio yake ni kuona kabisa kwa macho siku ya Kiyama, kutokana na dalili ya aya ya mbele (Kisha ataulizwa siku hiyo neema zote). Kuna kauli zinazosema: Kuuona kwa kwanza ni kabla ya kuuingia moto na kuuona kwa pili ni baada ya kuuingia. Kauli nyengine inasema, kwanza ni kuujua huo moto na pili ni kuuona. Na imesemwa makusudio yake ni kuuona baada ya kuuona, kwa kuonyesha kuendelea na kudumu. Na mengine zaidi ya hayo yamesemwa.
Aya Ya 8
Mzunguko wote wa maneno, unaonyesha kuwa maneno haya yanaelekezwa kwa watu wote wale ambao neema za Mwenyezi Mungu zimewafanya wamsahau Mwenyezi Mungu. Na binadamu ni mwenye kuulizwa juu ya neema zote alizopewa na Mwenyezi Mungu. Neema-Jambo ambalo linamuafiki yule mwenye kuneemeshwa na kumpa heri na manufaa-inakuwa neema kulingana na yule mwenye kuneemeshwa anavyoitumia. Kinyume cha hivyo, basi itakua ni balaa, ijapokuwa yenyewe nineema. Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuumba mtu na akajaalia makusudio ya kumuumba kwake, ni kumuabudu. Kama alivyosema: "Sikuumba majini na watu ila waniabudu
" (51:56).
Huo ndio utawala wa Mungu kwa mja wake, na Mwenyezi Mungu amemuandalia huyo mja wake, kila linalomnufaisha katika kulifikia lengo ambalo amemuumbia kwalo.
Kwa hivyo kuitumia neema hii katika njia anayoiridhia Mwenyezi Mungu na itakayomfikisha mtu kwenye lengo lake analolitaka, ndiyo njia ya kufikia lengo muhimu ambalo ni twaa (Utii). Kuitumia neema kinyume cha anavyoridhia Mwenyezi Mungu na kusahau lengo lake, ni upotevu na kukosa kulifikia lengo. Mwenyezi Mungu amekwishatoa hukumu ambayo haibadilishwi, kuwa mtu atarudi kwake na kumuuliza juu ya amali (matendo) yake, kisha amuhisabie na kumlipa. Matendo (amali) yake ni matumizi ya neema ya Mwenyezi Mungu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na kwamba mtu hatapata isipokuwa yale aliyoyatenda. Na kwamba matendo yake yataonekana. Kisha atalipwa malipo yaliyo kamili. Na kwamba mwisho (wa kila jambo) unarejea kwa Mola wako
." (53:39-42).
Utafiti Wa Hadithi Katika Majmau imesemwa kuwa Sura hii ilishuka kwa Mayahudi waliosema: "Sisi ni wengi zaidi kuliko ukoo fulani". Na ukoo fulani ni zaidi ya ukoo fulani". Wengine wamesema kuwa ilishuka kwa makabila mawili katika Ansar walipojifaharisha, na imesemwa kuwa imeshuka kwa Maquraish ukoo wa Abdu Manaaf bin Quswai na wa Sahm bin Amr wakajifaharisha na wakahesabu watukufu wao, Abdu Manaaf wakawa wengi. Kisha wakasema twendeni makaburini, tuwahisabu wafu wetu. Wakawa wengi ukoo wa Sahm, kwa sababu wao walikuwa wengi wakati wa ujahili. Katika Tafsiri ya Bur'han kutoka kwa Barqi kutoka kwa baba yake kutoka kwa Ibn Abu Umayr, kutoka kwa Hisham bin Salim naye kutoka kwa Abu Abdillahi, kuhusu neno la Mwenyezi Mungu "Lau mngelijua kujua kwa yakini". Amesema: Nikuona kwa macho. Na riwaya hii inatilia nguvu yale tuliyotangulia kuyaeleza katika maana ya aya". Katika Tafsiri ya Qummi kwa isnadi yake kutoka kwa Jamil naye kutoka kwa Abu Abdillahi
amesema: "Nilimwambia kuhusu mtaulizwa siku hiyo neema zote" akasema: "Utaulizwa uma huu juu ya neema aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kisha kwa Ahlul Bayt wa Mtume(s.a.w.w)
.
Katika Kafi kwa isnadi yake kutoka kwa Abu Khalid El-Kabili amesema: "Nilliingia kwa Abu Jafar
akaniita chakula cha mchana nikala pamoja naye chakula ambacho sijapata kukila kwa uzuri wake. Tulipomaliza kula akasema: "Ewe Abu Khalid umekionaje chakula chetu?" Nikasema, "Sijakula chakula kizuri na kisafi kama hicho, lakini nimekumbuka aya ambayo iko katika kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema: "Kisha mtaulizwa siku hiyo neema zote". Abu Jaffar akasema: "Hakika mtaulizwa yale mliyo na haki nayo
".
Katika hiyo hiyo Kafi kutoka kwa Abu Hamza amesema: "Tulikuwa kundi kwa Abu Abdillahi
akatuita chakula ambacho hatujapata kuona mfano wake, kutokana na ladha yake na kupendeza kwake, na akatuletea tende zilizo nzuri na safi, mtu mmoja akasema: "Mtaulizwa neema hii mliyoneemeshwa nyumbani kwa mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema Abu Abdillahi
: Hakika Mwenyezi Mungu ni mkarimu sana, hawezi kuwalisha chakula kisha awaulize, isipokua atawauliza neema aliyowaneemesha kwa Muhammad na kizazi cha Muhammad(s.a.w.w)
." Zimepokewa riwaya zenye maana haya kwa njia nyengine na ibara zenya kukhitalifiana. Baadhi ya riwaya zinasema kwamba neema ni wilaya (Utawala) wa Ahlul Bait wa Mtume na imetafsiriwa, kuwa ni neema zote alizozineemesha Mwenyezi Mungu.
Ubainifu wa hayo, ni kwamba neema hiyo sio kuwa itaulizwa kama kitu kwa mfano nyama, mkate, tende au maji baridi. Au kwamba neema hiyo ni usikizi, uoni, mkono au mguu. Hapana sio hivyo; isipokuwa itaulizwa neema ambayo Mwenyezi Mungu amemuumbia mtu, kama ameitumia katika njia ya ukamilifu wake na kupata ukaribisho na ibada, na akahimiza kuitumia kwa kushukuru, sio kuikufuru. Neema itaulizwa vipi ilivyotumiwa? Inayoelezea jinsi ya kutumia neema, ni dini aliyokuja nayo Mtume(s.a.w.w)
na kuusimamisha ubainifu wake, na maimamu kutoka katika Ahlul Bayt wake Mtume.
Kwa hiyo kuulizwa neema, maana yake ni kuulizwa amali ya dini katika harakati zote. Na kuulizwa juu ya Mtume(s.a.w.w)
na Maimamu walio baada yake ambao amewajibisha Mwenyezi Mungu kuwatii na akawajibisha kuwafuata katika njia ya kumuendea yeye Mwenyezi Mungu, ambayo njia yenyewe nu kuitumia neema kama ilivyobainishwa na Maimamu. Kuulizwa neema maana yake ni kuulizwa dini, kunaonyeshwa na riwaya ya Abu Khalid inayosema: "Hakika mtaulizwa yale mliyo na haki nayo". Kuulizwa dini maana yake ni kuulizwa juu ya Mtume na Ahlul Bayt wake, hili linaonyeshwa na riwaya mbili za Jamil na Abu Hamza zinazosema. "Atauliza Mwenyezi Mungu umma huu juu ya alivyowaneemesha kwa Mtume wake na Ahlul Bait wake".
Kuna baadhi ya riwaya zinazosema neema ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa watu wa ulimwengu kuwaokoa na upotevu. Na neema ni utawala wa Ahlul Bait, na utawala wa Ahlul Bait, unawajibisha kuwatii na kuwafuata katika ibada. Katika Majmau, imesemwa kuwa neema ni uzima na wasaa juu ya marifa. Riwaya hii inasaidiwa na riwaya iliyopokewa na Ibn Abbas kutoka kwa Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Watu wengi wamehadaiwa na neema mbili, uzima na wasaa".
Katika hiyo hiyo Majmau imesemwa kuwa neema ni amani na uzima. Riwaya hii imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Masud na Mujahid. Katika riwaya nyingine kutoka katika njia ya Ahli Sunnah zinasema: "Neema ni tende, maji baridi, nk. Na katika hadithi nyingine kutoka katika njia hiyo hiyo ya Sunni inasema: "Mambo matatu hataulizwa mtu; kitambaa kinachousitiri uchi wake, kipande cha tonge kinachozuiya njaa yake au nyumba inayomsitiri joto na baridi". Na Mwenyezi Mungu ndie mjuzi zaidi.
SURA ASR (ZAMA) (NA. 103)
INA AYA 3
Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu
وَالْعَصْرِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa zama.
إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾
2. Hakika mwanadamu yumo katika hasara.
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿٣﴾
3. Ila wale ambao wameamini wakatenda amali (matendo) njema, wakausiana (kushikamana na) haki, wakausiaana kusubiri.
UBAINIFU
Sura hii Muhtasari wa maarifa yote ya Kiqur'an na imekusanya makusudio ya Qur'an kwa maelezo mafupi (Muhtasar). Sura hii inawezekana kwa imeshuka Makka na Madina, lakini inavyoelekea imeshuka Makka.
Aya Ya 1
Ni kuapa kwa majira maalum. Na hii ndiyo tafsiri nzuri, kwa vile aya mbili zinazofuatia, zimejumlisha watu wote wa ulimwengu katika kupata hasara, isipokuwa wale waliofuata ukweli na wakasubiri. Sifa hizo ni za waumini wanaofanya mema. Hivyo makusudio ya majira (asr) yanakuwa ni zama za Mtume(s.a.w.w)
ambazo ni zama za kutokeza Uislamu kwa jamii ya watu na kudhihiri haki juu ya batili. Inasemekana pia kuwa makusudio ya Asr hapa ni wakati wa Alasiri ambao ni sehemu ya mwisho katika mchana, kwa kufahamisha mipangilio ya Mungu kwa kuchwa jua na kuja usiku pamoja na kuondoka ufalme wa jua. Na imesemwa kuwa makusudio ya Asr hapa ni swala ya Alasiri ambayo ni swala katikakati na ni bora katika swala za faradhi za kila siku.
Pia inasemeka makusido ya Asr ni usiku na mchana, na imesemwa kuwa makusudio ni zama ndefu za maisha kutokana na matukio ya kiajabu yanayofahamisha uwezo wa Mungu nk Imepokewa kutoka katika baadhi ya riwaya kwamba makusudio yake ni zama za kudhiri Mahdi
kwa kutumia kudhihiri haki juu ya batili.
Aya Ya 2
Yaani hasara ya kupungua raslimali ya mtu.
Aya Ya 3
Mwenyezi Mungu anawatoa katika hasara wale wenye kuvaana na imani na matendo mema, hao ni wenye kusalimika na hasara. Hapa kitabu cha Mwenyezi Mungu kinabainisha kuwa mtu anayo maisha ya milele ambayo hayakatiki kwa kifo, bali kifo ni kugura kutoka ulimwengu mmoja mpaka ulimwengu mwengine, kama alivyosema Mwenyezi Mungu "(Hatutashindwa) kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyingi katika umbo (jengine) msilolijua
".(56:61).
Qur'an inabainisha kwamba sehemu ya maisha hayo ambayo ni maisha ya dunia ni mtihani wa sehemu ya mwisho ya maisha ambayo ni akhera ya milele; kuwa yatakuwa mazuri au mabaya anasema Mwenyezi Mungu: "Na uhai wa dunia kwa mkabala wa akhera si kitu isipokuwa ni starehe ndogo tu
".(13:26).
Na amesema tena: "Kila nafsi itaonja mauti, na tuna kufanyieni mitihani kwa (mambo ya) shari na ya kheri, na kwetu (nyote) mtarejea
" (21:35).
Vile vile inabainisha kwamba kitu cha kukitanguliza katika maisha haya ya dunia kwa ajli ya maisha ya akhera ni itikadi na vitendo. Kwa hiyo itikadi ya kweli na amali njema ndivyo vyenye kumiliki wema wa akhera, na ukafiri na ufasiki utasababisha uovu akhera. Mwenyezi Mungu amesema: "Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyatenda. Na kwamba matendo yake yataonekana. Kisha atalipwa malipo yaliyo kamili
." (41:39-41)
Amesema tena: "Anayekufuru, (madhara) ya kufuru yake ni juu yake (mwenyewe); na wafanyao mema (hao) wanazitengeza nafsi zao
".(44:46). Kwa hali hiyo basi, imebainika kwamba uhai wa dunia ni rasilimali ya mtu, anachuma yale atakayoishi nayo katika maisha ya akhera. Kama akifuata haki katika itikadi na amal (vitendo) basi amepata faida katika biashara yake, amebarikiwa katika chumo lake na amesalimika na shari katika mustakabali wake. Kama akiifuata batili na akaacha imani na matendo mema, basi biashara yake itakuwa na hasara na atazuiliwa heri katika mwisho wake. Hilo ndilo neno lake Mwenyezi Mungu. " Hakika wanadamu wote wako katika hasara, isipokuwa wale ambao wameamini na wakatenda amali njema". Makusudio ya imani, ni kuamini Mwenyezi Mungu na miongoni mwa mambo ya kumuamini Mwenyezi Mungu ni kuamini Mitume yako yote na kuamini siku ya mwisho.
Mwenyezi Mungu ameeleza katika Sura ya (4:150-151), kuwa yule asiyeamini baadhi ya Mitume yake au siku ya mwisho, basi sio muumin. Kukusiana (kushikamana na) haki na kuusiana kusubiri, ni kuusiana watu kushika hiyo haki, kuifuata na kudumu nayo. Dini ya kweli haiwi isipokuwa kwa kuifuata haki kwa itikadi na vitendo. Na kuusiana kushikamana na haki ni kukubwa zaidi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwa sababu kunakusanya itikadi na kuhimiza amali njema.
Kisha kuusiana haki na katika amali njema, na kumetajwa baada ya amali njema kutokana na umuhimu wake. Na kuusiana kusubiri ni katika kuusiana haki, limetajwa neno kuusiana mara mbili kwa ajili ya kusisitiza. Kumetajwa kuusiana baada ya kutajwa iman na amali njema, kwa kuashiria kwanza kwenye uhai wa nyoyo zao na kukunjuka nyoyo zao kwa Uislamu, kisha kuieneza haki hiyo kwa watu wote. Subira imeelezwa kwa ujumla, kama kusubiri juu ya kumtii Mungu, kusubiri juu ya kuacha maasai na kusubiri juu ya misiba inayompata kwa kadari ya Mungu.
Utafiti Wa Hadithi Katka Tafsri ya Qummi kwa isnadu yake kutoka kwa Abdurrahman bin Kathiyr naye amepokea kutoka kwa Abu Abdillahi
katika neno lake Mwenyezi Mungu "Ila wale ambao wameamini" amewavua Mwenyezi Mungu watu wa ikhlas katika viumbe vyake. Katika Durril Manthur, ametoa Ibn Murdawayh, kutoka kwa Ibn Abbas kuhusu neno lake Mwenyezi Mungu: "Hakika wanadamu wote wako katika hasara" anakusudia Abu Jahl bin Hisham. Na kuhusu "Ila wale ambao wameamini na wakatenda mambo mema" ametajwa Ali na Salman.