MASOMO YA KI-ISLAMU
KITABU CHA NNE
SOMO LA SITA
MATENDO YALIYO HARAMU (II)
(10)
Kupoteza haki:
Hapa kuna maana nyingi, kuna haki za Mwenyezi Mungu, haki za Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
na haki za Waislamu kwa wenzao. Zote hizo ukipoteza moja wapo ni dhambi.
(11)
Kuiba:
Ni dhambi ambayo inajulikana pote ulimwenguni. Mwenyezi Mungu amesema: 'Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, malipo ya yale waliyo yachuma. Ndio adhabu itokayo kwa Mwenyezi Mungu." (Qur'an Sura ya 5 aya ya38).
(12) Ukuwadi na kusaidia katika mambo ya ndoa hata kwa mke wake:
Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Hataingia peponi wala hapati harufu ya peponi." Akaulizwa, "Ni nani huyo
?
Akasema, "Yule mume ambaye anajua vema kwamba mke wake analala na mwanamume mwingine (na haoni aibu).
(13) Kusema uwongo:
Ni haramu, dhambi kubwa sana. Amesema Imam Al-Baqir
: "Hakika Mwenyezi Mungu ameweka kwa kila shari {uovu} kufuli na ufunguo wa makufuli hayo ni ulevi, na uwongo ni ubaya zaidi kuliko ulevi
."
(14) Kuteta na kufitinisha:
Mwenyezi Mungu amesema: "Wala baadhi yenu wasiwaseme wengine. Je! Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa
?" (Qur'an, Sura ya 49 aya ya 12).
Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Hataingia peponi mfitini (mwenye kutangaza maneno ya huyu kwa yule ili atie fitina na kuwagombanisha)
."
(15) Kula riba:
Mwenyezi Mungu amesema: "Wale wanao kula riba................ wakasema, 'Biashara na ni kama riba.' Hali Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba.
" (Qur'an, Sura ya 2, aya ya 275).
Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Mwenyezi Mungu amemlaani mla riba, mtoa riba, na mwandikaji wa riba na mshuhudiliaji hayo
.''
(16) Kuua:
Mwenyezi Mungu amesema:'Na mwenye kumuua Muislamu kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu, humo atakaa milele, na Mwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.
" (Qur'an Sura ya 4a ya ya 93).
(17) Hiyana:
Mwenyezi Mungu amesema: "Hakika, Mwenyezi Mungu hawapendi wafanyao hiyana
. (Qur'an, Sura ya 8, aya ya 58).
(18) Dhuluma:
Mwenyezi Mungu amesema: "Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafirika na haya wanayoyafanya madhalimu. Hakika yeye anawaakhirisha tu mpaka siku ambayo macho yao yatakodolea yatoke nje kwa khofu
." (Qur'an, Sura ya 14 aya ya 42).
SOMO LA SABA
MATENDO YALIYO HARAMU (III)
(19) Kutumia kwa fujo:
Mwenyezi Mungu amesema: "Kuleni na kunyweni. Lakini msipite kiasi tu. Hakika yeye (Mwenyezi Mungu) hawapendi wapitao kiasi (wapindukiao mipaka)
." (Qur'an,Sura ya7 aya ya 31).
(20) Kudharau watu:
Mwenyezi Mungu amesema: "Enyi mlio amini, Wanaume wasidharau wanaume wenzao, huenda wakawa bora kuliko wao, wala Wanawake wasiwadharau wanawake wenzao, huenda wakawa bora kuliko wao." (Qur'ani, Sura ya 49, aya ya 11).
(21) Kuwaudhi watu:
Mwenyezi Mungu amesema: "Na wale wanao waudhi wanaume Waislamu na wanawake Waislamu pasipo wao kufanya kosa lolote, bila shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilizo dhahiri." (Qur'an, Sura ya 33 aya ya 58).
Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Mwislamu ni yule ambaye wamesalimika watu na vitimbi vya mkono na ulimi wake
."
(22) Kutoa siri:
Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Mazungumzo kati ya watu wawili yaliyo zungumzwa ni amana; basi ukiyasema kwa watu huwa si mwaminifu.
" Kwa hiyo kutoa siri ya mwenziwe ni dhambi kubwa (siri ina weza kuwa ni aibu ya mtu au ni jambo lingine, mradi yote ni siri).
(23) Kuficha bidhaa (chakula) ya mahitajio kwa kutaka kuuza kwa thamani kubwa:
Imepokewa hadithi tukufu ya Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Mficha vyakula kalaaniwa na Mwenyezi Mungu
."
(24) Kuwatazama wanawake wasio halali na wanawe:
Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Tazama mtupo wajicho ni mshale wenye sumu katika mishale ya Shetani. Mwenye kuacha kutazama kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, Atampa Mwenyezi Mungu imani na atapata utamu wake moyoni mwake
."
Mwenyezi Mungu anasema katika Qur' an: "Waammbie Waislamu wanaume wainamishe macho yao (wasitazame yaliyo katazwa)
...................Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao
." (Qur'ani, Sura ya 24, aya ya 30).
(25) Kuhudhuria magomani na sinema za haramu:
Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amekataza kuhudhuria mahala popote patendwapo maasi na mambo yaliyo haramishwa. Katika sinema inakuwepo miziki, maneno na matendo ya aibu na matusi; na vitu hivi vimekatazwa sana katika Uislamu, kama ilivyoelezwa humu humu kitabuni.
(26) Kuimba na kusikiliza muziki:
Mtukufu Mtume(s.aw.w)
amesema: "Mpiga zeze atafufuliwa siku ya Qiyama na uso wake hauna nuru, na mikononi mwake zeze la moto, na juu ya kichwa watakuwepo Malaika sabini elfu wa adhabu na mikononi kwa kila Malaika patakuwepo mundu wanampiga kichwani na usoni mwake, na atafufuliwa mwimbaji chongo, bubu, kiziwi, na mzinifu vivyo hivyo, na pia mwenye filimbi za zumari na mpiga dafu
."
SOMO LA NANE
MATENDO YALIYO HARAMU
(27) Kujitoa shahawa kwa mkono:
Ni haramu na dhambi, na pia huleta madhara mengi mwilini.
(28) Kuvunja ahadi:
Katika alama za imani, Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amesema; "Akitoa ahadi hutimiza, basi asiyetimza ahadi yake anatoka katika imani
."
(29) Kuvaa pete ya dhahabu na kujipamba wanaume kwa dhahabu:
Ni haramu kwa mwanaume kuvaa dhabhabu kwa kiasi chochote.
(30) Kuhadaa:
Kuficha aibu au ubaya wa kitu unachomuuzia mtu ni haramu.
(31) Kughushi:
Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Hayuko nasi mwenye kumghushi Muislamu mwenziwe
."
(32) Kupekua (kupeleleza) mambo ya watu:
Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'an: "Enyi mlio amini; Jiepusheni sana na kuwadhania watu dhana mbaya, kwani kuwadhania watu dhana mbaya ni dhambi. Wala msipeleleze habari za watu
." (Qur'an, Sura ya 49 aya yal 2).
(33) Kutukana na kushutumu:
Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
amesema: "Kumtukana au kumshutumu mwenye imani mwenzio ni ufasiki
."
(34) Kenda utupu wanawake kama hali ya sasa:
Mwenyezi Mungu amesema: "Na kaeni (enyi wanawake) majumbani mwenu wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili
(ujinga,ukafiri). (Qur'an, Sura ya 33 aya ya 33).
(35) Kumsaidia mdhalimu:
Mwenyezi Mungu amesema: "Na saidianeni katika wema na utawa, wala msisaidiane katikadhambi na uasi.
" (Qur'an, Sura ya 5 aya ya 3).
(36) Kuhukumu kinyume cha sheria ya Kiislamu:
Mwenyezi Mungu amesema: "Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri
." (Qur' an, Sura ya 5 aya ya 44).
"Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio waasi
." (Qur'an, Sura ya 5 aya ya 47).