12
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KWANZA
AL - BAQARAH (NG’OMBE)
﴿وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴾
58.Na tuliposema: Ingieni mji huu na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na ingieni katika mlango (wake) kwa kunyenyekea na semeni: Tusamehe. Tutawasamehe makosa yenu na tutawazidishia wale wafanyao mazuri.
﴿فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴾
59.Wakabadilisha wale walio dhulumu kauli isiyokuwa ile waliyoambiwa. Na ndipo tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kubwa mbinguni kwa sababu ya ufuska waliokuwa wakiufanya.
INGIENI MJI
Aya 58 - 59
MAELEZO:
Na tuliposema: Ingieni mji huu na kuleni humo maridhawa popote mpendapo.
Mwenye Majmaul-Bayan amesema: Wamekongamana wafasiri kwamba maana ya mji hapa ni Bayitul-Maqdis: na kwamba hilo linatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:Ingieni ardhi takatifu. Na ingieni katika mlango (wake) kwa kunyenyekea.
Yaani ingieni hali ya kuinamisha vichwa kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu.
Katika tafsir Bahrul-Muhit ya Abu Hayan Al-Andalusi anasema: Makusudio ya mlango ni mmojawapo wa milango ya Baitul Maqdis unaoitwa Hitwa (mwanachuoni huyu wa Kihispania alikufa mwaka 754 Hijriya)
Na semeni: Tusamehe
. Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwaamrisha kuingia kwa unyenyekevu, vile vile aliwaamrisha kuambatanisha kunyenyekea na kutamka kauli ya kujidhalilisha, mfano kusema: astaghfirullah, ili kauli na kitendo vilingane; kama unavyotamka: Subhana rabbiyal adhwiimi katika kurukuu na; Subhana rabbiyal aala katika kusujudu.
Ilikuwa si lazima kutamka neno lenyewe Hitwa kwa njia ya kuabudu kama walivyosema wafasiri wengi, wala sio kuwa makusudio ya Hitwa ni amali inayokata dhambi, kama ilivyo katika tafsiri ya Al-Manar kwa kunukiliwa Muhammad Abduh aliposema: Hakika Mwenyezi Mungu hakuwakalifisha kutamka, kwa sababu hakuna kitu rahisi kwa binadamu kama hicho.
Itakumbukwa kwamba Mwenyezi Mungu amewakalifisha waja wake kutamka maneno katika swala, amali za Hijja, kuamrisha mema, kurudisha salam na kutoa ushahidi, bali kuzitoa herufi kwa makhraji yake katika baadhi ya sehemu. Wakabadilisha wale waliodhulumu kauli isiyokuwa ile waliyoambiwa. Yaani: wao waliamrishwa waseme yale yanayostahiki msamaha na thawabu, lakini walikhalifu wakasema yale yanayostahili adhabu na mateso.
Nilishangaa kuona baadhi ya wafasiri wakubwa miongoni mwao ni wanafal- safa wawili! Razi na Mulla Sadra, wameingilia masuala ya kuganda kwenye dua na dhikri, kwamba je, inapasa kuganda kwenye herufi au inajuzu kubadilisha tamko kwa tamko pamoja na kuchunga maana?
Na wala wasiingilie pale walipofasiri wakabadilisha wale waliodhulumu, kuwa inawaelezea wale ambao wameifanya dini biashara, na hali wao ndio waliokabidhiwa dini ya Mwenyezi Mungu, lakini wakafanya hiyana na wakazibadilisha Aya na mapokezi, kama walivyofanya Maquraish.
Tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kutoka mbinguni. Mwenyezi Mungu ameinyamazia aina na hakika ya adhabu yake wala hakutubainisha kuwa ni maradhi ya tauni, kama walivyosema baadhi, au ni theluji, kama walivyosema wengine. Vile vile amenyamazia idadi ya wale walioangamizwa na adhabu. Kuwa je ni elfu sabini, zaidi ya hapo au chini ya hapo? Pia hakueleza muda wa adhabu yenyewe kuwa ni saa au ni siku nzima? Kwa hivyo nasi tunanyamazia yale aliyonyamazia Mwenyezi Mungu, Wala hatutajikalifu, kama wengine, kwa kutegemea kauli dhaifu au Hadith zenye kuachwa.
﴿وَإِذِ اسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ كُلُوا وَاشْرَبُوا مِن رِّزْقِ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴾
60.Na Musa alipowaombea maji watu wake, tukasema: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikabubujika humo chem chem kumi na mbili; kila kabila ikajua mahali pake pa kunywea. Kuleni na kunyweni katika riziki ya Mwenyezi Mungu wala msiasi katika ardhi mkifanya ufisadi.
ALIPOWAOMBEA MAJI
Aya 60
MAELEZO:
NaMusa
alipowaombea maji watu wake.
Hakuna maelezo katika Aya hii, kwani makusudio yake yanafahamika upesi, Razi amesema: Wamesema kwa pamoja wafasiri, kwamba tukio hilo lilikuwa katika jangwa la Sinai. Vyovyote ilivyo ni kwamba Mwenyezi Mungu baada ya kuwafunika na kivuli na kuwalisha Manna na Salwa, vile vile aliwanywesha maji akawapitishia chemchem kumi na mbili kulingana na koo zao, kila ukoo ukawa na chemchem yake ili kusitokee mzozo kwenye maji.
UBEPARI NA UJAMAA
Waisrail walipata kivuli, chakula na kinywaji bila ya taklifu wala mashaka yoyote; hakukuwa na tajiri wala maskini; wala mwenye njaa na mwenye kushiba; wala hakukuwa na mwenye kumiliki nyenzo za uzalishaji, wala hakuna ugawaji. Vile vile hakuna kuwa kila mtu atapata kutokana na nguvu zake; au kutokana na kazi yake. Hakukuwa na chochote isipokuwa usawa katika maisha bila ya kufanya kazi yoyote au kuwa na mali.19 Hilo ndilo taifa la mwanzo na la mwisho kupata kuonekana kwa maisha kama hayo, pamoja na kuwa na umoja katika lugha, maendeleo na historia. Tutathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu alilifanyia taifa hilo mambo maalum kwa ajili yao tu na si kwa watu wote.
* 19 Katika yaliyoelezwa na baadhi ya tafsir na ya kushangaza ni kwamba aliyekuwa mtoto katika wao alikuwa akikua na nguo; yaani kila anavyokua na nguo nayo hukua naye kwa urefu na upana, Hayo yanawezekana, lakini hakuna dalili juu yake. Ikiwa siyo sababu ya kiuchumi au ya kikabila inayoleta chuki na ufisadi, basi kwanini kuleta uharibifu na kumwasi mtoaji nasaha aliye mwaminifu, Musa bin Imran
? Na vipi wachoke na maisha ya usawa katika utajiri na kusema, hatuwezi kungojea bali tunataka baadhi yetu wawaombe wengine; na wakaukabili mfululizo wa neema kwa ukafiri na uasi? Wajamaa wanadai kwamba ubepari ndio kitovu cha uovu, na kwamba ujamaa ndio chimbuko la ubora. Mabepari nao wakasema umuhimu ni kuwa jinsi moja katika akili na sifa za kiroho...
Hitler anasema: Hakuna kitu chochote isipokuwa watu wa aina ya Aria (Arian) Lakini maadui wengi wa Hitler walikuwa (kama yeye) Aria; kisha nadharia yake hiyo ndiyo iliyoyaondoa maisha yake, ikidhalilisha taifa la Ujerumani na ikaangamiza mamilioni ya watu wengine. Pia ndiyo iliyovunja miji na maendeleo kwa ujumla. Ama dola za kijamaa zimepita kiasi kwa kubishana. Mzozo wa Moscow na Beijing ulikata matumaini yote ya maafikiano; na kabla yake, kulikuwako na mzozo wa Stalin na Tito.
Hakika binadamu ana nguvu za ajabu zisizoweza kuhisabika, lakini hali ya mazingira yanayomzunguka kwa nje ni nyingi. Mwenye kujaribu kuyadhibiti hayo atakuwa ametafuta muhali, kila moja ina athari yake na kazi yake, na binadamu yuko kati ya kupwa na kujaa.Kwa hiyo kuchukulia kuwa athari inakuwa katika maada peke yake au katika roho peke yake, si sawa.
Ndio, ni kweli kwamba ufakiri unakaribia kuwa ni ukafiri lakini hata hivyo binadamu akipata anayoyahitajia katika uhai wake, hautatimia kwake utulivu na upole mpaka aamini na kutegemea kwenye dini iliyo sawa itakayomhifadhi na makosa na dhambi.
* 20 Katika mwaka 1936 Edward (VIII) alijiuzulu kiti cha ufalme wa Uingereza, ambao haukuchwewa na jua wakati huo. Alijiuzulu kwa sababu ya mwanamke aitwaye Wallis, ambaye alikuwa amekwishaolewa na kuachwa mara mbili. Akaamua aishi naye kama mkimbizi na kuhangaika katika miji akitafuta kazi. Hiyo yote ni kutokana na kuchukulia maisha yote kuwa ni ya kimaada tu!
KITU KUTOKA KUSIKO NA KITU
Unaweza kuuliza vipi mawe yachimbuke chemchemi? Je,muhali unaweza kuwa? Je, kinaweza kupatikana kitu kutoka kusiko na kitu? Au mtu anaweze kuchimba maelfu ya mita ardhini na yasitoke maji ikiwa hayapo pale palipochimbwa. Sasa vipi yabubujiike maji kutoka katika jiwe lisilo na chemchemi wala athari yoyote ya maji? Hakuna maelezo kutoka katika Sayansi kwa hili kabisa, isipokuwa kwa miujiza tu, ambayo kawaida yake ni kukhalifu ada; na isipokuwa kwa kauli yake ambaye umetukuka uweza wake: Kuwa ikawa; kama ilivyo katika kupasuka bahari na kusimama maji yake kama majabali, kushuka Manna na Salwa kutoka mbinguni na kuujalia moto kuwa baridi na salama kwa Ibrahim
. Vile vile kuzaliwa Isa bila ya baba, kufufua wafu, na kuumba ndege kutokana na udongo na mengineyo mengi.
Kwa hivyo mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na uweza wake atatosheka na haya, na mwenye kukanusha na akafanya inadi, itakuwa hakuna haja ya maneno katika matawi baada ya kukanusha shina. Mimi nina yakini kabisa kwamba wale ambao wanataka maelezo ya kielimu na ya kiundani kwa kila kitu, kuwa katika maisha yao wanapitiwa na matukio kadhaa ambayo hawawezi kupata maelezo yake, isipokuwa katika ghaibu na matakwa ya Mwenyezi Mungu, lakini wao hawajui. Inahakikisha hilo kauli ya Mulla Sadra mwanafalsafa mkubwa, ambaye wakati wake hakukuwa na vipimo vyovyote, aliposema katika kufasiri Aya hii: Hakika asili ya maada haina sura ya kukoma kuendelea, kwa hiyo inawezekana baadhi ya sehemu ya jiwe kugeuka maji.
Ushahidi hapo ni kauli yake Inawezekana kugeuka baadhi ya sehemu ya jiwe kuwa maji. Hii inatilia nguvu nadharia ya kukua na kubadilika (evolution), ambayo ali-
* 21 Mulla Sadra ni katika wanavyuoni wakubwa wa karne ya kumi na sita (A.D.) na Darwin alikuwa mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.
Ibainisha kabla ya Darwin kwa karne tatu ambapo Darwin mwenyewe alihusisha nadharia yake kwa mnyama mwenye viungo tu, ama Mulla yeye amekusanya vitu vyote hata vitu vikavu, kama ulivyoona katika uwezekano wa kugeuka jiwe kuwa maji. Ni ukubwa ulioje wa uvumbuuzi huu. Lau Mulla angelikuwa ni mzungu, basi Einstein asingelikuwa na umaarufu wowote, lakini Einstein ni mtu wa Magharibi tena Myahudi na Mulla Sadra ni wa mashariki tena Mwislamu! Ametangulia mtukufu huyu kuielezea nadharia ya kukua kwa upana. Na nadharia hii ilimzidishia imani juu ya kumwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Ugunduzi wake huu umeleta dalili mpya, kuweko Mwenyezi Mungu ambayo hakuwahi kuielezea yeyote mpaka akaitwa kiongozi wa wataalam wa kuthibitisha Mungu. Na ameleta nguvu ya hoja juu ya ujinga wa Gladstone na mamilioni ya wafuasi wake katika madai yao kwamba kuweko Mwenyezi Mungu, muumba wa ulimwengu huu, kumebatilika kwa nadharia ya kukua. Bali ni kinyume na hivyo.
﴿وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نَّصْبِرَ عَلَىٰ طَعَامٍ وَاحِدٍ فَادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ مِن بَقْلِهَا وَقِثَّائِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَىٰ بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ اهْبِطُوا مِصْرًا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلْتُمْ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴾
61. Na mliposema: Ewe Musa: Hatuwezi kuvumilia kwa chakula cha namna moja tu, basi tuombee Mola wako atutolee vile vinavyooteshwa na ardhi miongoni mwa mboga zake, na matango yake na ngano yake na adesi zake na vitunguu vyake. Akasema: Mnabadili vitu duni kwa vile vilivyo bora? Nendeni kwenye mji, huko mtapata mlivyoviomba.Na ikapigwa juu yao (chapa ya) udhalili na umaskini; na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na hayo ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu na wakiwaua Manabii pasipo haki. Basi haya ni kwa sababu ya kuasi kwao na kupituka mipaka.
NA MLIPOSEMA
Aya 61
Na mliposema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia kwa chakula cha namna moja tu.
Yaani walisema wahenga wenu walipo-kuwa katika kuhangaika, walipochoka kuendelea kula Manna na Salwa, waka-pendelea maisha yao ya mjini. Hakuna kosa hapa katika matakwa yao, kwani kila mtu anapendelea namna mbali mbali ya chakula, hali hiyo ndiyo inayoleta matamanio. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amehalalisha riziki njema kwa waja wake. Kwa hivyo Aya haiko katika mfumo wa kutusi bali ni kustaajabu kukataa kwao maisha yasiyo na tabu na kutaka maisha ya dhiki na usumbufu. Akasema: Mnabadili vitu duni kwa vile vilivyo bora? Herufi ba (kwa) inaingia kwenye kitu bora, sio duni, Tunasema: Usibadilishe shaba kwa dhahabu, hatusemi: Usibadilishe dhahabu kwa shaba, lakini watu hufanya kinyume, kwa vyovyote itakavyokuwa muhimu ni kujua makusudio.Nendeni kwenye mji; huko mtapata mlivyoviomba.Yaani Musa ndiye aliyewaambia hivyo. Kwa dhahiri makusudio ya neno Misri ni mji kwa sababu Mwenyezi Mungu hakubainisha mji maalum.Na tafsiri ya Quran siyo ya kinahw ambayo itasahihishwa na Sibawayh na Naftawayh.
Na ikapigwa juu yao (chapa ya) udhalili na umaskini Walikuwa watukufu walio huru; riziki ikiwajia maridhawa, wakakataa isipokuwa kulima, uhunzi na biashara. Yote hayo yanaleta mashindano na vita ambavyo vinaleta kuhemewa na kukosekana amani.Na wakiwaua Manabii pasipo haki.Kwa dhahiri kuwaua Manabii kunakuwa bila ya haki. Kama kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu (s.w.t.) aliwasuta na kuwambia kwamba kuua, kwao hakukuwa kwa kukosea, bali ni kwa makusudi na inadi tu. Kwa hiyo hakuna geni kwa vitendo vya mayahudi, kwa sababu hiyo ndiyo asili yao.
﴿إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴾
62.Hakika wale ambao wameamini na Mayahudi na Manaswara na Wasabai; yeyote atakayeamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akafanya vitendo vizuri basi watapata malipo yao kwa mola wao, wala haitokuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika.
WAUMINI NA MAYAHUDI
Aya 62
Lugha Makusudio ya neno Hadu ni Yahudi kwa kunasibishwa kwa Yahudha mtoto mkubwa wa Yaqub. Israil ni jina la Yaqub, kama tulivyotangulia kueleza. Naswara ni wenye kunasibishwa na mji unaitwa Naswira katika nchi ya Palestina. Imepokewa Hadith: Hakika wameitwa Manaswara kwa sababu Isa na mama yake Maryam
wanatoka katika kijiji kinachoitwa Naswira katika mji wa Sham, Mara nyingi Bwana Masih
huitwa Naswiri. Wasabai ni watu wanaomkubali Mwenyezi Mungu, siku ya mwisho na baadhi ya mitume, lakini wanaitakidi kuwa baadhi ya nyota zinaathiri heri na shari na uzima na ugonjwa, miongoni mwao wanaishi Iraq hivi sasa.
Neno: Swabia lina maana ya kuchomoza; Yaani kuchomoza nyota. Watu wa kwanza kuabudu nyota ni watu wa Namrud ambao walipelekewa Mtume Ibrahim
; wao ndio watu wa dini ya zamani katika Historia.
MAELEZO
Katika maana ya Aya hii kuna karibu kauli nane za baadhi ya wafasiri. Zilizo sahihi zaidi katika hizo ni mbili:
Kwanza
: Makusudio ya Aya ni kwamba Mwenyezi Mungu anataka kubainisha kuwa Yeye hatilii umuhimu majina kabisa. Ni sawa iwe ni aina ya Mwislamu, Mumin, Yahudi, Naswara au Msabai. Kwa sababu matamko hayadhuru kitu wala hayanufaishi, ispokuwa umuhimu mbele ya Mwenyezi Mungui ni itikadi sahihi na amali njema. Ufahamisho wa Aya ni yale yaliyoelezwa katika hadithi kwamba Mwenyezi Mungu haangalii sura isipokuwa huangalia vitendo. Hapana shaka kwamba maana hii yenyewe ni sahihi, lakini tamko halitoi maana hiyo waziwazi. Wengine wamezowea kujipendekeza kwenye dini nyingine kwa kutolea dalili Aya hii kwamba hakuna tofauti kati ya Waislamu na wengine mbele ya Mwenyezi Mungu, na hali wao wanajua kwa yakini kwamba wao wanakanusha Utume wa Muhammad(s.a.w.w)
bali wanamzulia uongo na wanamnasibishia mambo yanayoweza kuitingisha ardhi.
Maana ya pili, ni kwamba watu ambao hawakumuwahi Muhammad(s.a.w.w)
lakini waliongoka kwenye imani ya Mwenyezi Mungu na wakaacha mambo ya haram; kama uwongo, kunywa pombe na kuzini, miongoni mwao ni Qas bin Saida, Zayd bin Amr na Waraqa bin Nawfal na wengineo; hao wanaitwa wenye kushikamana na dini sahihi.Kwa hiyo muulizaji aliuliza hukumu ya hawa mbele ya Mwenyezi Mungu.Ikajibu Aya kwamba hakuna ubaya kwao. Vile vile Wayahudi, Wasabai na Wanaswara ambao hawakumuwahi Muhammad(s.a.w.w)
kupata ufafanuzi; hakika wote hao hawana hofu kwao, madamu walikuwa na Imani ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na matendo mema.Nasi tunapondokea kwenye maana hii.
Unaweza kuuliza kwamba maana ya Aya hii inafanana kuwa ni maana ya hayo kwa hayo. Kwa sababu kauli yake Mwenyezi Mungu:Mwenye kuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho,
imekuja baada ya kusema:Hakika wale ambao wameamini
. Kwa kujaalia maneno kuwa: Hakika wale ambao wameamini. Mwenye kuamini katika wao ambayo ni sawa na kusema: Hakika Waislamu mwenye kusilimu katika wao na waliosimama mwenye kusimama katika wao basi nini jawabu? Jibu: Swali hilo linaweza kuja ikiwa tutaif-anya herufi man ni ya mubtada (kuanzia) kwa kusema: Yeyote atakayemwamini. Ama tukiifanya ni Badal (badili) ya namna tatu yaani katika Wayahudi,
Wasabai na Manaswara atakayemwamini, basi itakuwa hakuna haja ya swali; yaani itakuwa maana yake ni: Hakika wale ambao wamemwamini Mwenyezi Mungu wasiokuwa Wayahudi, Wasabai na Wanaswara haitakuwa hofu juu yao; vile vile atakayeamini katika Wayahudi, Wasabai na Wanaswara haitakuwa juu yao hofu. Hukumu ya wote ni moja.
﴿وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴾
63.Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu: Shikeni kwa nguvu haya tuliyowapa na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate kumcha (Mungu).
﴿ثُمَّ تَوَلَّيْتُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَكُنتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ﴾
64.Kisha mligeuka baada ya haya. Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Zake, mngelikuwa miongoni mwa wenye kuhasirika.
﴿وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴾
65.Na kwa yakini mmekwisha jua wale miongoni mwenu walioivunja Sabato (Jumamosi). Basi tukawaambia: Kueni manyani wadhalilifu.
﴿فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴾
66.Kwa hivyo tukaufanya (umma huo) ni onyo kwa waliokuwa katika zama zao na waliokuja nyuma yao, na mawaidha kwa wamchao Mwenyezi Mungu.
TULIPOCHUKUA AHADI
Aya 63 66Na tulipochukua ahadi yenu:
Yaani; tulipochukua ahadi kutoka kwa wahenga wenu kufanya amali kwa mujibu wa Tawrat. Walipoivunja ahadi, Mwenyezi Mungu aliwainulia jabali juu yao, akasema fanyeni la sivyo nitawaangushia jabali hili. Wakakubali na wakatubia; likatulia jabali mahali pake, lakini baadaye walirudia kuasi. Ikiwa Wayahudi walikuwa hivi wakati wa Musa
pamoja na kushuhudia waliyoyashuhudia katika miujiza, wala hakuna nguvu ya hoja kuliko kuona, basi si ajabu kwa mayahudi wa Madina kumkanusha Mtume(s.a.w.w)
na kuvunja mkataba naye. Angalia kifungu cha Muhammad(s.a.w.w)
na Mayahudi wa Madina katika tafsir ya Aya 47.
Na lau si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema Zake:
Yaani; lau si kuwahurumia Mwenyezi Mungu, angeliwapa adhabu katika dunia na akhera.
Mulla Sadra anasema: Hakika Aya hii ni katika Aya zinazotoa matarajio zaidi na yenye dalili ya nguvu zaidi ya rehema ya Mwenyezi Mungu na vile asivyopatiliza maovu ya waja wake waasi. Kwa sababu, kauli yake:Lau si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu,
ni baada ya kukithiri uovu wao, ukiwa ni pamoja na kuabudu ndama, kuikufuru neema, kuwakana Mitume na kuwaua, kuvunja ahadi iliyotiliwa mkazo, na mengineyo; inafahamisha ukamilifu wa upole wake na msamaha wake. Kisha akanakili Mulla Sadra, kutoka Kuffal, yale yanayoeleza kwa muhtasari, kwamba baada ya kuwaondolea adhabu ya jabali waliibadili Tawrat wakadhihirisha maasi wakamkhalifu Musa, wakamfanyia kila adha. Mwenyezi Mungu alikuwa akiwalipa hapa duniani ili waweze kuzingatia kiasi kwamba baadhi yao aliwapoteza katika ardhi, wengine akawaunguza kwa moto na wengine wakaadhibiwa kwa tauni. Yote hayo na yasiyokuwa hayo yameandikwa katika Tawrat wanayoikubali, ambayo hivi sasa anaweza kuipata kila anayetaka. Kisha waliofuatia wakafanya makosa kama waliyoyafanya waliopita; wakamkanusha Bwana Masih wakadhamiria kumuua. Kwa hivyo si ajabu kukanusha yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad(s.a.w.w)
. Na kwa yakini mmekwishajua wale miongoni mwenu walioivunja sabato (Jumamosi).
Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kuacha kufanya kazi siku ya Jumamosi (sabato) akawaharamishia kuvua samaki siku hiyo. Wakawa samaki wanakusanyika siku hiyo kwa usalama na utulivu, lakini kundi jengine la Mayahudi lilifanya hila ya kuwazuia samaki siku ya Jumamosi, mahali wasipoweza kutoka na kuwachukua siku ya Jumapili, wakisema: Mwenyezi Mungu ametukataza kuvua samaki siku hiyo, lakini hakutukataza kuwazuia na kuna tofauti kati ya kuzuia na kuvua.
Waongo hawa wenye hila wananikumbusha wale wanaoigeuza dini, ambao wanacheza na matamko; wanazivuruga haki ili waingize uwongo katika mitego yao. Jambo la kushangaza ni kwamba baadhi ya masheikh wametunga vitabu maalum vya kuifanyia hila sheria; kama kwamba Mwenyezi Mungu ni mtoto mdogo anayedanganywa, asiyewajua wakweli na waongo. Kama Mwenyezi Mungu hakuwabadilisha hawa kuwa manyani hapa duniani, kama alivyowafanyia Mayahudi, basi atawafufua kesho kuwa majibwa, manyani na nguruwe. Ikiwa waongo hawakugeuzwa hivi sasa kwa dhahiri, basi wamegeuzwa kwa ndani; na hakuna hoja yenye nguvu zaidi inayofahamisha hilo kuliko vitendo vyao vinavyofahamisha kugeuzwa nafsi zao.
Basi tukawaambia kuweni manyani madhalili
.
Wamehitalifiana wafasiri kwamba je, kugeuzwa manyani kulikuwa kwa uhakika kiasi ambacho sura zao na mili yao ilikuwa ya manyani ama kulikuwa ni kugeuzwa kwa kitabia tu; kama vile alivyosema Mwenyezi Mungu:
﴿خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ﴾
Amepiga muhuri Mwenyezi Mungu juu ya nyoyo zao.
(2:7)
﴿كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا﴾
Au...Kama mfano wa punda anayechukua mizigo?
(62:5)
Ambapo Aya hizi ni za majazi. Wafasiri wengi wamesema kuwa walikuwa manyani wa kikweli kabisa, kwa kuchukulia dhahiri ya Aya ambayo haina haja kuiletea tafsiri nyingine. Kwa sababu kugeuzwa sura na kuwa sura nyingine ni jambo linalowezekana kihakika. Ikija Aya au hadith kuhusu jambo ambalo lawez-ekana, basi tutaipitisha kwa dhahiri yake bila ya kuhitajia tafsiri nyingine (Taawil).
Wafasiri wachache, kama Mujahid na Sheikh Muhammad Abduh wamesema kwamba mabadiliko yalikuwa katika nafsi si katika mwili. Anasema Sheikh Muhammad Abduh katika tafsiri yake ya Al- Maraghi: Hakika Mwenyezi Mungu hambadilishi kila asi kumtoa katika umbile la mtu, kwa sababu hiyo siyo desturi yake katika kuumba kwake, na desturi ya Mwenyezi Mungu ni moja, analolifanya kwa karne ya sasa ndilo alilolifanya kwa karne iliyopita. Sisi tunakubaliana na wale wa kwanza waliosema kwamba mageuzo yalikuwa ya uhakika. Ama kauli ya Abduh ni sahihi kama msingi wa mambo yalivyo na kama kawaida ya vyote, lakini kuna mambo mengine yasiyofuata kawaida ambayo yanatokana na hekima ya Mwenyezi Mungu, kama miujiza na mengineyo katika karama zake Mwenyezi Mungu. Vitendo vya Mwenyezi Mungu pamoja na mayahudi wakati huo, ni katika mambo yasiyofuata desturi, kama itakavyobainika katika kifungu kifuatacho.
MAYAHUDI HAWANA MFANO
Mwenye kuangalia vizuri Aya za Quran tukufu zilizowahusu Waisrail hasa wale waliokuwa katika zama za Musa, atatoka na natija iliyo wazi kama jua. Nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwafanyia mambo yasiyokuwa na mfano wala hayafanani na kitu chochote ambacho watu wamekizowea. Sio mbali kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: Na nikawatukuza kuliko viumbe wengine, ni ishara ya muamala huo mahsusi. Mwenyezi Mungu aliwakomboa kutoka katika ukandamizaji wa Firaun na utaghuti wake kwa kuipasua bahari, sio kwa jihadi wala kujitolea muhanga. Aliwalisha Manna na Salwa na kuwapa maji kwa muujiza bila ya taabu au kazi yoyote. Akawainulia jabali ili waweze kutii na kusikia. Akamfufua mtu wao aliyeuliwa, ili abainike muuaji. Yote hayo na mengineyo yanaonyesha dalili kwamba matatizo ya Mayahudi wakati huo hayakutatuliwa kwa njia ya kawaida iliyozoeleka, bali hata hawakufikiria kufanya kazi ya kuyatatua; kila walipo kuwa wakipata tatizo, basi husema; Ewe Musa tuombee Mola wako afanye hivi na awache hivi, na Musa alikuwa akiwaombea na kukubaliwa.
Kwa hivyo basi inatufahamikia kwamba kukifananisha kizazi cha Waisrail cha wakati huo na vizazi vingine sio mahali pake; na kwamba kauli ya Sheikh Muhammad Abduh (analolifanya kwa karne ya sasa ndiyo analolifanya kwa karne iliyopita) ni sahihi katika watu wote isipokuwa watu hao tu!
* 22 Qur an na Injil zimewalaumu Mayahudi kwamba wao ni maadui wa utu, na historia yao inashuhudia ukweli huu. Kwa ajili hiyo wanajaribu kufanya kila njia ionekane kwamba hakuna tofauti ya ukabila wala ya dini; ndio wakatunga vitabu kwa makusudio hayo na wakaeneza propaganda na wakaanzisha taasis, miongoni mwa hizo taasisi ni ile ya Free Mason ya kimtaifa ambayo wameivika nguo ya ubinadamu. Vile vile inabainika kwamba Mwenyezi Mungu aliwainulia jabali kutaka kuwalazimisha waifuate Tawrat, na kwamba kauli ya Sayyid Tabatabai katika tafsiri Al-Mizan: Hakika kuinuliwa jabali hakufahamishi kulazimisha kwa sababu hakuna kulazimisha katika dini, kauli hii iko mbali na mnasaba wa watu wa Musa ambapo Mwenyezi Mungu aliwafanyia mambo yaliyo mbali na kawaida na desturi. Mimi sina namna yoyote ninayoweza kutegemea kujua hekima ya Mwenyezi Mungu katika hilo. Huenda ikawa siri katika hilo ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alitaka kupiga mfano kwa Mayahudi hao kwamba maisha hayawi mazuri ila kwa kutaabika na kufanya kazi. Na ni kutokana na hali hiyo tu, ndipo mtu anaweza kugundua mambo na kujua siri, na kupanda katika daraja ya juu ya kimaendeleo.
Lau binadamu angeliishi kivivu kwa kutegemea chakula kutoka mbinguni asingeliweza kutofautiana na mnyama aliyefungwa na kulishwa; wala asingelikuwa na haja ya akili na utambuzi. Hakika uvivu ni kuganda na ni mauti, ama ukakamavu ndio uhai. Vyovyote iwavyo, historia ya Mayahudi kwa ujumla inaambatana na historia ya Wayahudi waliokuwa wakati wa Musa, wao ndio waliotangulia halafu ndio wakafuatiwa na wajukuu zao. Kutokana na mazungumzo haya tutadokeza kuhusu jumuiya ya wazayuni wanaoishi Marekani katika mtaa uitwao Brooklyn mjini New York. Jina la jumuia hiyo ni Mashahidi wa Yehova ambayo lengo lake la kwanza na la mwisho ni kuleta vurugu na fitina za kidini katika pembe za ulimwengu hasa Uarabuni.
Wanatoa matoleo mengi sana ya vitabu kwa lugha zote, tena kwa majalada ya rangi ambayo yanamiminika kwa wingi katika miji yetu: Pia wanatoa jarida kwa jina la Mnara wa mlinzi. Miongoni mwa vitabu walivyotoa ni kile kinachomshutumu Mtume Muhammad(s.a.w.w)
na Quran. Jina la kitabu hicho ni Hal-khadama ddinul-Insaniyya (Je, dini inahudumia utu). Vingine ni Liyakunillah-Swadiqan (Mungu awe ni mkweli), Nidhamu dduhurililahiy (Nidhamu ya zama za kiungu), Al-haqqu Yuharrirukum (Haki itawakomboa), Al-Maswaliha (Masilahi), na vingine chungu mzima, ambavyo vyote vimechapishwa Beirut. Serikali ya Misri iliwagundua baadhi ya wanachama wa jumuia ya Mashahidi wa Yehova wakiwa katika mikutano ya siri. Ikawashika na kuwashtaki mnamo mwezi wa April mwaka 1967.
Miongoni mwa mafunzo ya jumuia hii ni kwamba kulikuwa na mzozo mkubwa kati ya Mwenyezi Mungu na shetani, ambao ulidumu kwa muda wa karne sitini; kisha Mwenyezi Mungu akajitoa akamwachia mamlaka shetani afanye vile anavyotaka. Shetani akamwachia Mwenyezi Mungu umma wa Kiisrail. Kwa ajili hii Mwenyezi Mungu akamwambia Shetani: Chukua watu wote na uniachie umma huu. Hivyo ndivyo yalivyotimia maafikiano kati ya Mwenyezi Mungu na Shetani, lakini mambo yatabadilika mwisho. Kwa sababu umma wa Kiyahudi utatawala kuanzia mto Naili (Nile) mpaka Furati (Euphrates) na kwamba Mitume wa Kiisrail watafufuka na kuchukua madaraka ya juu katika dola ya Kiisrail; hatimaye ulimwengu wote utakuwa chini ya dola hii, Shetani atash-indwa na Mwenyezi Mungu atashinda. Kundi hili lina wafuasi na wawakilishi katika Beirut, Oman, Baghdad, Damascus, Cairo, Saudia na Morocco.
Lengo la kuyaeleza yote hayo ni kuwatahadharisha watu na nyoka huyu, na kuwahadharisha na vidole ambavyo vinawatekenya baadhi ya waandishi wa vitabu na magazeti kwa kufanya njama za kuleta vurugu na uharibifu, na kuleta ukabila na fitina za kidini. Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Kwanza 2 Sura Al-Baqara 126