UTANGULIZI
Miongoni mwa maswala ambayo bado ni mahali pa tofauti baina ya madhehebu za kiislamu, ni suala la adhana na ibara zinazotamkwa ndani yake, kama vile ibara: As-swalaatu khayrun minan nawm. na huwezi ukafanya utafiti wa mas.ala haya bila ya kujua adhana ilivyowekwa kisheria. Rejea ya vyanzo vya Hadith kwa ma-Sunni inatufichulia idadi kadhaa ya riwaya dhaifu na maqtu.u katika sanad zake, na zingine zaishilia kwenye hali ya kutojulikana, ambazo zatuambia jinsi adhana ilivyowekwa kisheria kupitia mtu mmoja aliyeota, bwana aitwaye Abdalla bin Zayd Al- Answari na Umar bin Al-Khattab, sababu ni kuwa Mtume(s.a.w.w)
alitaka ushauri juu ya adhana. Na zimekhitilafiana baadhi ya riwaya na zingine juu ya kwamba ibara: as-swalatu khayrun minan nawmi ilikuwa sehemu iliyoambatanishwa na kisa hiki kilichotokea wakati wa Mtume(s.a.w.w)
, au mathalan, kuwa yeye(s.a.w.w)
alimuamuru Bilal kutaja ibara hiyo badala ya kutaja (hayya a.laa khayril-a.mal) ambayo imefutwa kwa masunni.
Au ni kwamba Bilal aliitamka ibara hiyo na Mtume(s.a.w.w)
akaiwafiki. Kuungana na ndoto au kuwa amri ya kuzidisha ni kutoka kwa Mtume(s.a.w.w)
ilikuja wakati uliofuata. Kama tulivyoona katika riwaya nyinginezo kwamba kutaja as- Swallaat khayrun minan nawm (Swala ni bora kuliko usingizi) kwamba ilikuwa ni katika ijtihadi ya Khalifa wa pili Umar bin Al-Khattab. Ama tukienda kwenye marejeo ya kisasa kwa wafuasi wa maimamu wa Ahlul-bayt tutaona kwamba aina ya adhana inahitilafiana na kijumla na kiufafanuzi na aina ya adhana kwa watu kwa kutegemea riwaya zilizopokewa na maimmu wa Ahlul-bayt, kutoka kwa babu yao Mtume(s.a.w.w)
.
Riwaya za adhana katika Sahih na Musnad Kabla ya kuingia kwa kina katika ufafanuzi wa masuala haya twaona ni bora kwanza tuonyeshe baadhi ya riwaya zenye kuhusika na tamko la: Aswalaatu hayrun minan nawm.
pamoja na riwaya ambazo hazikutaja na ambazo zimenukuliwa na vitabu vya Sunni pamoja na sanad zao ili ifanye msingi na kigezo cha maongezi na darasa: Ibn Maja: Ametuhadithia Muhammad bin Khalid bin Abdallah Al- Wasiti, amesema: Ametuhadithia baba yangu, kutoka kwa Abdur- Rahman bin Is.hak, kutoka kwa Zahri, kutoka kwa Salim, kutoka kwa baba yake, kwamba Mtume(s.a.w.w)
aliwashauri watu juu ya kitakachowahimiza kwenda kuswali.
Wakataja kuwekwe parapanda. Mtume(s.a.w.w)
hakupendelea hilo kwa kutumiwa na mayahudi. Wakataja kengele. Pia hakutaka kwa kuwa ilitumiwa na manaswara; kisha usiku huo, mtu mmoja katika ma-Answari, aitwaye Abdallah bin Zayd alionyeshwa ndotoni mwito huo na pia Umar bin Al-Khatab. Yule Ansari akamgongea mlango Mtume(s.a.w.w)
usiku, akamweleza, naye Mtume akamwamuru Bilal hivyo; naye akaadhini. Amesema Zahri: .Bilal akaongeza katika adhana ya alfajiri (as-Swalatu khayrun minan nawmi) Mtume(s.a.w.w)
akakubali kwa kuthibitisha
.
Amesema Abu Daud: .Ametuhadithia Musaddid, ametuhadithia Harth bin Ubayd kutoka kwa Muhammad bin Abdul-Malik bin Abi Mahdhurah, kutoka kwa babake, kutoka kwa babu yake, amesema: Nilisema, ewe Mtume(s.a.w.w)
nifundishe Sunna ya adhana. Akasema: akanigusa mbele ya kichwa changu akasema: Utasema: Allahu Akbar (mara nne) kisha utapaaza sauti yako useme: Allahu Akbar. (mara nne), utapaaza sauti yako kisha useme, Ash.hadu anlaa ilaaha illa.llah (mara mbili). Kisha useme: Ash-hadu anna Muhammadan Rasulullah (mara mbili), kisha: hayya a.las-Swalaa (mara mbili), kisha hayya a.lal.falaah (mara mbili), ikiwa ni Swala ya Al-fajiri useme, as-Swalaatu khayrun minn nawm (mara mbili). Kisha useme: Allahu Akbar Allahu Akbar, laa ilaaha illa llaah
.
Na katika Musnad ya Ahmad, ametuhadithia baba yangu, kutoka kwa Is.hak, amesema: Na ametaja Muhammad bin Muslim Az-Zahri, kutoka kwa Said bin Musayyib, kutoka kwa Abdallah bin Zaid bin Abdur-Rabbih, amesema: .Pindi Mtume(s.a.w.w)
alipoataka kuwakusanya watu kwa Swala kwa kutumia kengele, na alichukia kengele kwa kuwaafiki manaswara nilimuota mtu wakati nikiwa nimelala aliyevaa nguo za rangi ya kijani kibichi akiwa ameshikilia kengele mkononi mwake, nikamwambia ee mja wa Mwenyezi Mungu je wauza kengele?
Akasema: Kwani utaifanyia nini?. Nikasema, nitaitumia kukusanyia watu kwenye Swala. Akasema: Je si nikuonyeshe kilicho bora zaidi ya hicho?. Nikaseama, ndio. Akasema: Useme, Allahu Akbar (mara nne), Ash-hadu anlaa ilaaha illa.llah (mara mbili), Ash-hadu anna Muhammadan Rasuuli llah (mara mbili), hayya alas swalaa (mara mbili) hayya alal falaah (mara mbili), Allahu akbar (mara mbili), laa ilaaha illa llaah.
Kisha akasema juu ya kukimu Swala: Utasema, Allahu akbar (mara mbili), Ash-hadu anlaa ilaaha illa.llah (mara mbili), Ashhadu anna Muhammadan Rasuuli.llah (mara mbili), hayya a.las swalaa (mara mbili) hayya alal falaah (mara mbili), Qad qaamatis swalaa (mara mbili), Allahu Akbar (mara mbili) laailaaha illa.llah. Akasema: Kulipokucha nilikwenda kwa Mtume(s.a.w.w)
.
Naye Mtume(s.a.w.w)
akasema: Hakika ndoto hii ni ya kweli inshaallah. Kisha akaamuru kuadhiniwe. Akawa Bilal akiadhini hivyo na Mtume(s.a.w.w)
akilingania kwenye Swala. Anasema: Akaja akalingania usiku mmoja na akaambiwa kuwa Mtume(s.a.w.w)
alikuwa amelala, Bilal akapaaza sauti yake akisema: As-swalaatu khayrun minan nawm.. Akasema Ibun Musayyib: Ndipo neno hilo likaongezwa kwenye Swala ya Alfajiri..
Katika Sunan ya Darmi: Ametuambia Uthman bin Umar bin Faris, ametuhadithia Yunus, kutoka kwa Zahri. Kutoka kwa Hafs bin Umar bin Saad - muadhini, ya kwamba Saad alikuwa akiadhini katika msikiti wa Mtume(s.a.w.w)
.. Amesema Hafs: Amenihadithia ahli yangu kuwa Bilal alikwenda kuadhini kwa Mtume(s.a.w.w)
kwa ajili ya Swala ya Alfajiri. Wakamwambia kuwa Mtume(s.a.w.w)
amelala. Hapo Bilal akanadi kwa sauti yake kubwa, As-swalaatu khayrun minan nawm., nayo ikathibitishwa hiyo katika adhana ya Swala ya Alfajiri
.
Katika Majmauz-Zawaid, ametuhadithia Ahmad bin Muhammad bin Al-Walid Al-Arzaqi, ametuambia Muslim bin Khalid, ametuhadithia Abdur-Rahim bin Umar, kutoka kwa Shihab, kutoka kwa Abdallah bin Umar kwamba Mtume(s.a.w.w)
alitaka kuweka kitu kitakachoweza kuwakusanya watu kwenye Swala, mpaka akaoteshwa mtu mmoja wa ki-Answari aitwaye Abdallah bin Zaid na pia akaoteshwa Umar bin Khattab usiku huo..mpaka aliposema: .Bilal akazidisha katika Swala ya Alfajiri kwa kusema: As- Swalaatu khayrun minan nawm. Na Mtume(s.a.w.w)
akaithibisha hiyo
.
Na kutoka kwa Bilal kwamba alikuwa akiadhini Swala ya Alfajiri akisema hayya a.laa khayril a.mal ndipo Mtume(s.a.w.w)
akaamuru iwekwe mahali pake neno As-walaatu khayrun mina nawm na aache neno hayya a.laa khayril a.mal
.
Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraira, amesema: .Alikwenda Bilal kwa Mtume(s.a.w.w)
ili aadhini kwa Swala ya Alfajiri, akasema: .Muamrisheni Abu Bakr aswalishe watu, akarudi kwake, akaona kwake uzito, akasema: Muamrisheni Abu Bakr aswalishe watu. Akaenda akaadhini, na katika adhana akazidisha neno .As swalaatu khayrun minan nawm.. Mtume(s.a.w.w)
akasema: Ni nini hii uliyozidisha katika adhana yako? Akajibu: Nimekuona una uzito nikataka kukuchangamsha.. Mtume(s.a.w.w)
akasema: Nenda kazidishe katika adhana yako na muamuru Abu Bakr aswalishe watu
.
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kwamba Bilal alikwenda kwa Mtume(s.a.w.w)
wakati wa adhana ya Alfajiri. Akamkuta Mtume(s.a.w.w)
amelala, akamwita akisema: As- Swalaatu khayrun mina nnawm. na Mtume(s.a.w.w)
hakumkataza na akaliingiza - yaani Bilal - neno hilo kwenye adhana, hivyo basi haiadhiniwi Swala kabla ya wakati wake isiokuwa Swala ya alfajiri
.
Imepokewa kutoka kwa Aisha amesema: Alikwenda Bilal kwa Mtume(s.a.w.w)
ili amuadhinie kwa Swala ya Alfajiri, akamkuta amelala, akasema: As-Swalaatu khayrun minan nawm; ikathibitishwa katika adhana ya asubuhi kuwa ndani ya adhana..
Na katika Sunnan Tirmidhi, Hadith ya Ahmad bin Mu.in, ametuhadithia Abu Ahmad Zubeiry, ametuhadithia Abu Israil, kutoka kwa Hakam, kutoka kwa Abdul Rahman Abi Layla, kutoka kwa Bilal, amesema: Ameniambia Mtume(s.a.w.w)
usiongeze kitu katika Swala ila katika Swala ya Al-fajiri..
Amepokea Abu Daud amesema: Ametuhadithia Ubbad bin Musa Al-Khatly, na Ziyad bin Ayyub, na Hadith ya Ziyad imetimia, wamesema wawili hao: Ametuhadithia Hashim kutoka kwa Abu Bashar, amesema Ziyad: Ametuambia Abu Bashar, kutoka kwa Umayr bin Anas kutoka kwa maanswari amesema: Mtume(s.a.w.w)
alikuwa na haja sana ya kufanya namna atakavyowakusanya waislamu kwa Swala. Akaambiwa, weka bendera wakati wa Swala unapoingia. Watu wakiiona wataambiana.
Hilo halikumpendeza. Akasema: Akaambiwa apige parapanda (kama la Wayahudi), hilo pia halikumpendeza. Akasema: Hiyo ni katika mambo ya Wayahudi.. Akatajiwa kengele, akasema: Hilo ni katika jambo la Manaswara.. Akaondoka Abdallah bin Zaid bin Abdur Rabbah, naye huyu akaoteshwa ndotoni adhana, akasema, akaenda mapema kwa Mtume(s.a.w.w)
na akampasha habari hiyo akisema: Nilipokuwa katikati ya kulala na kuwa macho, mara alinijia mwenye kunijia na kunionyesha adhana. Amesema: Na Umar bin Khattab alikuwa ameshaona kabla ya hapo na akalificha hilo kwa siku ishirini, kisha akamwambia Mtume(s.a.w.w)
, naye akamwambia: .Nini kimekuzuia usinieleze?. Akajibu Umar: Abdallah Bin Zaid alinitangulia hivyo nikaona haya kusema.
Hapo Mtume(s.a.w.w)
akasema: Ee Bilal, simama na ufanye analokuamuru Abdallah bin Zaid.. Akasema: Akaadhini Bilal.. Amesema Abu Bashar: Akaniambia Abu Umayr kwamba Answari wanadai kuwa Abdallah bin Zaid lau asingelikuwa siku hizo ni mgonjwa, basi Mtume(s.a.w.w)
angelimfanya kuwa ni muadhini..
Amesema: Ametuhadithia Muhammad bin Mansur Tusi, ametuhadithia Yakub, ametuhadithia baba yangu, kutoka kwa Muhammad bin Is.hak, amenihadithia Muhammad bin Ibrahim bin Harith Taymi, kutoka kwa Muhammad bin Zaid bin Abdu Rabbih amesema: Ametuhadithia Abdallah bin Zaid, amesema: Mtume(s.a.w.
w
)
alipoamuru kengele ipigwe ili kukusanya watu kwa Swala, alikuja kwangu mtu, ilhali nimelala, akiwa na kengele mkononi, nikasema, ee Abu Abdallah je wauza kengele? Waifanyia nini? Nikajibu: Tunaitia kwenye Swala.
Akasema: Je si nikuambie lililo bora zaidi kuliko hiyo kengele?. Nikamwambia, ndio niambie. Akasema: Utasema, Allahu Akbar (mara nne); Ashahdu.. (mara mbili), wa ash-hadu ana.(mara mbili) hay.ya ala-Swalaa.(mara mbili) hayya alal falaah.(mara mbili) Allah Akbar (mara mbili) laa ilaaha ila.llaah (mara mbili). Akasema: kisha hakukawia sana akasema: .Na utapokimu Swala useme, Allahu Akbar (mara mbili), Ash-hadu an.laaillaha ila.llah ..(mara moja), wa ash-hadu ana.(mara moja), hay.ya ala swalaa (mara moja) hay.ya alal falaah.(mara moja), Qad qaamatis swalaa, qad qaamatis swalaa, Allahu akbar (mara mbili), laa ilaaha illa.llah.. Kulipokucha nilikwenda kwa Mtume(s.a.w.w)
nikamweleza niliyoyaona.
Naye akasema: Hiyo ni ndoto ya kweli, inshaallah, simama na Bilal na umwambie uliyoyaona na aadhini kwayo, kwani yeye ana sauti kubwa zaidi kuliko wewe.. Nikasimama na Bilal nikawa namsomea adhana hiyo. Akasema: Umar akasikia hilo akiwa nyumbani kwake akatoka huku akikokota nguo yake na akisema: Naapa kwa yule aliyekutuma kwa haki! Ee Mtume(s.a.w.w)
wa Mwenyezi Mungu! Mimi pia nimeona hayo aliyoyaona.. Mtume(s.a.w.w)
akasema: Shukrani ni za Mwenyezi Mungu..
Amesema Ibn Maja: Ametuhadithia Abu Bayd Muhammad bin Ubayd bin Maymuunul-Madani, amesema: Ametuhadithia Muhammad bin Salama Al-Harani, amesema ametuhadithia Muhammad bin Ishak, amesema: ametuhadithia Muhammad bin Ibrahim Taymi, kutoka kwa Muhammad bin Abdallah bin Zaid kutoka kwa baba yake, amesema: Mtume(s.a.w.w)
alikuwa ana haja ya kutumia parapanda, akaambiwa atumie kengele, akakataa, hivyo Abdallah bin Zaid akaoteshwa usingizini..
Na katika Sunan Tirmidhi: Ametuhadithia Sa.ad bin Yahya bin Said Al-Amawi, ametuhaditha baba yangu, ametuhadithia Muhammad bin Is.hak, kutoka kwa Muhammad bin Ibrahim Taymi, kutoka kwa Muhammad bin Abdallah bin Zaid, kutoka kwa babake, amesema: Kulipokucha, tulikwenda kwa Mtume(s.a.w.w)
na nikamwambia kuhusu hiyo ndoto...Akasema Tirmidhi: Amepokea Hadith hii Ibrahim bin Saad kutoka kwa Muhammad bin Is.hak, akakamilisha Hadith hii kwa urefu.
Kisha Tirmidhi akaongeza: Na Abdallah bin Zaid naye ni Ibn Abdu Rabbih hatujui kwake Hadith ila hii pekee ya adhana..
Kwa muhtasari, riwaya za Hadith hizi zina mambo yafuatayo: Nyongeza ya ziyada ya maneno imekuja upande wa Bilal na Mtume(s.a.w.w)
akaithibitisha, na Abdallah bin Zaid hakuiona ndotoni wala Umar bin Al-Khattab kama vile riwaya za kuhusu adhana zilivyonukuu. Adhana Mtume(s.a.w.w)
alimfundisha Abi Mahdhur na ina neno: As-Swaatu khayrun minnnawm. ndipo likaingizwa kwenye adhana. Na katika riwaya nyingi, Bilal alipaaza sauti yake na huku Mtume(s.a.w.w)
akiwa amelala akasema, As-Swalaatu khayrun minan-nawm. ndipo neno hilo likingizwa kwenye adhana.
Na katika riwaya nyingine: Bilal alikuwa akiadhini kwa Swala ya Alfajiri akisema hayya a.laa khayril amal. na hapo Mtume(s.a.w.w)
akaamuru neno hilo liwe badala ya neno As-Swalaatu khayrun mina-nawm.. Riwaya hizi zilizoandikwa na vitabu vya Sunan na ambazo zinataja suala la neno As-swalaatu khayrun minan nawm. katika adhana, na zingine hazikutaja, hizi hazizingatiwi, kwa sababu kadhaa zifuatazo:
Kwanza, ni upande wa sanad, tunaona kuwa njia zake za upokezi, ama ni dhaifu ama ni zimekatika, ama hazijulikani. Namna adhana ilivyowekwa kisheria inashangaza. Na hivyo ni kwa ajili ya kuwa kinyume na ile misingi ijulikanayo ya kuwekwa hukmu za kidini. Kuwapo tofauti baina ya mafakihi wa kiislamu wa madhehebu manne katika suala la kuongeza neno - Aswalatu khayrun minan Nawmi - katika adhana.
Mosi: Mjadala juu ya riwaya za adhana zilizotangulia kutajwa sanad zake: Tutafafanua hapa zaidi kifungu hiki kuhusiana na sanad za riwaya na tutaangalia kulingana na mapokezi ya Hadith ya kwanza mpaka ya mwisho ili tuone katika hukmu kama ikiwa kutajwa swalaatu khayrun minan nawm. kulikuwapo wakati wa Mtume(s.a.w.w)
ama kulipendelewa baadaye na kuongezwa katika adhana kwa ijtihadi tu:
1.
Muhammad bin Khalid bin Abdallah Al-Wasiti, Jamalud-Din Al- Mazzi anatoa taarifa yake akisema: Amesema: Ibn Muin hana kitu.. Na riwaya yake kutoka kwa baba yake ilikanushwa.
Amesema Abu Hatim: Nilimuuliza juu ya Yahya bin Mu.in, akasema: Huyo ni mtu muovu, muongo na ametaja mambo maovu.. Na amesema Abu Uthman Said bin Umar na Bardai: Nilimuuliza Aba Ara juu ya Muhammad bin Khalid akasema huyo ni mtu muovu. Na Ibn Hayyan katika kitabu At-Thuqaat: akasema, huyo hukosa na
hukhalifu..
Na Shawkani naye amesema baada ya kunakili riwaya: Kuwa katika isnadi yake kuna udhaifu sana
.
2.
Dhahabi amesema: Muhammad bin Abdul Malik bin Abi Mahdhura, kutoka kwa baba yake kuhusu adhana kuwa siyo hoja
. Na katika kitabu Naylul-awtaari cha Shawkani imetajwa: Muhammad bin Abdul-Malik bin Abi Mahdhuurah si mtu maarufu, na Harith bin Ubayda pia kwake kuna maneno
.
3.
Muhammad bin Is.hak bin Yasar bin Khiyar anasema: Kuwa masunni hawazitolei hoja riwaya zake. Amesema Ahmad bin Khushayma: Aliulizwa Yahya bin Mu.in juu yake huyo. Akasema: .Ni dhaifu kwangu, ni mgonjwa na hana nguvu..
Akasema Abul Hasan Al-Maymuni: Nimemsikia Yahya bin Mu.in akisema, Muhammad bin Is.hak ni dhaifu. Na Nasaai amesema: Yeye si mwenye nguvu..
4.
Imekuja katika Sunnan Ad-Darami: Hadith hii isnad yake ni dhaifu kwa sababu ya kuwepo Hafs bin Umar na baba yake, na Malik ametaja kisa hiki katika kitabu chake, Muwattaa kwa isnad yake yenye kukatika katika, ndani ya kitabu cha Swala
.
5.
Muslim Bin Khalid bin Qurrah, ambaye huitwa Jarha alimtaja kuwa ni dhaifu Yahya bin Mu.in. Na akasema Ali Al-Madini: Si chochote. Akasema Bukhari: Hadith ni munkar.. Nasaai naye amesema: mtu huyo hana nguvu katika upokezi.. Naye Abul Hatim akasema kuwa mtu huyo hana nguvu katika upokezi na Hadith yake huandikwa lakini haitolewi hoja, hadith zake zajulikana na zapingwa.
6.
Tabrani amepokea katika kitabu Al-Kabir na pia Abdul Rahman bin Ammar bin Saad ambaye alisema kuwa Ibn Muin ni dhaifu katika Hadith
.
7.
Na pia Abdul Rahman bin Qasit wala sikupata utajo wake
.
8.
Tabrani amepokea katika Al-Awsat, akasema: Mtu mmoja tu alijitenga kwake naye ni Marwan bin Thawban, nikasema, wala sikuona akitajwa mahali.
9.
Tabrani amepokea katika Al-Awsat na Saalih Al-Akhdhar, na wakakhitilafiana juu ya kumtolea hoja, na hakuna hata mmoja aliyemnasibisha ila kwa uongo tu
.
10.
Amesema: Na katika mlango, imepokewa kutoka kwa Abi Mahdhurah, amesema Abu Isa: Hadith ya Bilal hatuijui ila Hadith ya Abu Israil Al-Malai. Na Abu Israil hakuisikia Hadith hii kutoka kwa Hakam bin Utaybah, akasema: Yeye ameipokea kutoka kwa Hasan bin Umaarah kutoka kwa Hakam bin Utaybah, na Abu Israil jina lake hasa ni Ismail bin Is.haqa, huyu si mwenye nguvu miongoni mwa watu wa Hadith..
11.
Riwaya hii ni dhaifu kwa sababu mwisho wake ni kutojulikana kutokana na neno lililomo ndani ya Hadith hiyo, watu miongoni mwa Answari.. Miongoni mwao ni Abu Umayr bin Anas. Ibn Hajar amemtaja na akasema juu yake kuwa amepokea miongoni mwa watu ma-Answari katika maswahaba wa Mtume(s.a.w.w)
juu ya kuona adhana ndotoni. Akasema Ibn Saad: Alikuwa muaminifu lakini mwenye Hadith chache.. Akasema Ibn Abdul Barri: Hajulikani, hachukuliwi kwa kutolewa hoja..
Akasema Jamalud-Din: Hii ndio iliyotokea kwenye maudhui mbili, kuona mwezi na adhana..
12.
Na katika riwaya hii:
A.
Muhammad bin Ibrahim bin Al-Harith bin Khalid At-Tiimi Abu Abdallah, aliyefariki mwaka 120 (A.H.). Amesema Abu Jafar Al-Aqiily: Kutoka kwa Abdallah bin Ahmad bin Hambali, nimemsikia baba yangu akamtaja Muhammad bin Ibrahim At-Taymy Al-Madany, akasema: .Katika Hadith yake kuna kitu.. kwani yeye hupokea Hadith zinazokataliwa..
B.
Muhammad bin Is.hak bin Yasar bin Khiyar: Masunni hawazitolei hoja riwaya zake japokuwa yeye ndiye msingi wa Sirah ya Ibn Hisham Amesema Ahmad bin Abi Khaythama: Aliulizwa Yahya bin Muin kuhusu mpokezi huyu, akasema: .Huyu ni dhaifu kwangu, hana nguvu.. Na akasema Abul-Hasan Al-Maymuni: Nilimsikia Ibn Muin akisema: Muhammad bin Ishak ni mpokezi dhaifu. Na Nasai amesema: Hana nguvu..
C.
Abdallah bin Zaid: .Inatosha kuwa yeye ana Hadith chache.. Amesema Tirmidhi: .Hatujui Hadith yoyote kutoka kwake inayoswihi kutoka kwa Mtume(s.a.w.w)
ila Hadith ya adhana.. Amesema Hakim: Ni sahihi kuwa yeye aliuwawa Uhud na riwaya zake zote zimekatika. Amesema Ibn Adiy: .Hatujui Hadith yoyote kwake itokayo kwa Mtume(s.a.w.w)
ila ya adhana tu..
Amepokea Tirmidhi, kutoka kwa Bukhari amesema: .Hatujui Hadith yoyote itokayo kwake ila ya adhana tu
. Na Al-Hakim amesema: Abdallah bin Zaid ndiye aliyeoteshwa adhana ambayo mafakihi wa kiislamu wamepokezana kwa kuikubali, lakini haikutoka kwenye Sahih Muslim na Sahih Bukhari kutokana na kuhitilafiana wenye kuipokea katika sanad zake
.
13.
Sanad ndani yake muna: Muhammad bin Is.hak bin Yasar na Muhammad bin Ibrahim At-Taymi na umekwishajua hali zao kama vile ulivyojua kuwa Abdallah bin Zaid ambaye alikuwa amepokea riwaya chache tu, na zote zimekatika.
14.
Katika sanad za riwaya hii ameingia Muhammad bin Is.hak bin Yasar na Muhammad bin Al-Harith At-Taymi na Abdallah bin Zaid, na makosa ya wawili hao wa mwanzo umeyatambua na kule kukatika sanad za kila walichopokea kutoka kwa watatu, kwa hivyo hapa ile hali ya sanad yaonekana wazi, angalia kwa makini.