TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO Juzuu 5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: tafsiri ya Qurani

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
: HASANI MWALUPA
Kundi:

Matembeleo: 17915
Pakua: 2617


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 14 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 17915 / Pakua: 2617
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA TANO Juzuu 5

Mwandishi:
Swahili

10

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA TANO

﴿وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴾

125.Ni nani mwenye dini nzuri kuliko yule aliyeusalimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu na akawa mwema na akafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahim kuwa rafiki mwandani.

﴿وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطًا ﴾

126.Na ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kukizunguuka kila kitu.

NANI MWENYE DINI NZURI

Aya 125 - 126

MAANA

Na ni nani mwenye dini nzuri kuliko aliyeusalimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye akawa mwema.

Makusudio ya kusalimisha uso ni kusalimu amri, Maana ni kuwa, mkamilifu ni yule ambaye anamtarajia Mwenyezi Mungu wala hamtarajii asiyekuwa Mwenyezi Mungu na anafuata desturi alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa viumbe vyake katika maisha haya.

Ni kwa hivi tu ndio mja atakuwa karibu na Muumba wake. Ama mwenye kuwanyenyekea waungu wa dunia kwa tamaa ya mali waliyonayo na jaha, basi hana chochote kwa Mwenyezi Mungu: hata kama atasimama kwa ibada usiku na kufunga mchana.

Na akafuata mila ya Ibrahim mwongofu

Yaani akamfuata Ibrahim(a.s) ambaye ameachana na kila yasiyokuwa ya Mwenyezi Mungu aliyewaambia watu wake:

﴿قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانِ وَلَا أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ﴾

"Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu na hali yeye ameniongoza? Wala siogopi wale mnaowashirikisha naye" (6: 80)

Unaweza kuuliza : Kwa nini Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na akafuata mila ya Ibrahim na wala asiseme mila ya Muhammad?"

Jibu :Kwanza : mila ya Ibrahim na Muhammad ni kitu kimoja

﴿إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴾

"Hakika watu wanaomkurubia zaidi Ibrahimu ni wale waliomfuata, na Mtume huyu na walioamini pamoja naye. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa waumini" (3:68)

Pili : Utume wa Ibrahim umeafikiwa na dini zote, sio uislamu peke yake. Kwa hiyo kuutolea hoja kwa wasiokuwa waislam kutakuwa na nguvu zaidi, kama sikosei.

Na Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwandani. Mwenyezi Mungu amemhusu Ibrahim kwa cheo kikubwa kinakurubia kuwa zaidi ya unabii na utume. Imam Jafar as-Sadiq(a.s) anasema:"Hakika Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahim ni mja wake kabla ya kumfanya Nabii na akamfanya nabii kabla ya kumfanya mtume na akamfanya mtume kabla ya kumfanya rafiki mwandani."

Na ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini.

Yeye ni mwenye kumiliki kila kitu mwenye kukiendesha kila kitu na mwenye kukizunguuka kila kitu.

Unaweza kuuliza : kuwa maana haya yamekaririka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu mara nyingi, je kuna siri gani?

Jibu : Siri ni kumzindua binadamu na kubaki daima kukumbuka kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye kuendesha ulimwengu, na kwamba amri yake ni yenye kupita humo na yeye binadamu daima yuko kwenye ujuzi wa Mungu, uweza na hekima yake. Nafsi itakapotambua hakika hii, itafanya matendo kulingana na aliyeiumba, kwa kufuata njia zake na kutii amri zake.

Zaidi ya hayo, kukaririka kunakuja kwa mnasaba unaohitajia, ambao mara nyingine wafasiri wanaweza kuutambua na mara nyingine wasiutambue. Nao hapa ni kwamba baadhi wanaweza wakafikiria kwamba Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahim rafiki; kama vile sisi tunavyowafanyia marafiki.

Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akaondoa tuhuma hii, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Muumbaji mwenye kumiliki kila kitu na kwamba Ibrahim yuko chini ya milki yake, lakini yeye ni mja aliyechaguliwa, si kama waja wengine.

﴿ وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِهِ عَلِيمًا﴾

127.Wanakutaka fatuwa kuhusu wanawake, waambie Mwenyezi Mungu anawapa fatuwa kuhusu wao na yale msomewayo humu Kitabuni kuhusu mayatima wanawake, ambao hamuwapi walichoandikiwa, na mnapenda kuwaoa, na walio dhaifu katika watoto, na muwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na heri yoyote muitendayo basi Mwenyezi Mungu anaijua

WANAKUULIZA KUHUSU WANAWAKE

Aya 127

MAANA

Mwanzoni mwa Sura Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja kidogo hukumu ya mwanamke na yatima, akafuatilia kwa kuwataja watu wa Kitabu, wanafiki na vita.

Kisha akarudi tena kutaja mwanamke na yatima na kutaja baadhi ya hukumu zao kwa kukamilisha hukumu ya familia, aliyoianzia Sura. Hii ndiyo njia ya Qur'an kuelezea jambo kisha kuingiza jambo jingine tena kurudia jambo la kwanza kwa makusudio ya kuathiri katika nyoyo na mengineyo yanayohitajia hekima na kuwachukulia upole waja.

Wanakutaka fatuwa kuhusu wanawake.

Fatuwa ni kubainisha mushkeli. Yaani wanakutaka wewe Mtume wa Mwenyezi Mungu uwabainishie hukumu ya wanawake katika urithi, ndoa n.k.

Waambie Mwenyezi Mungu anawapa fatuwa kuhusu wao.

Hii inafahamisha kwamba kuweka sharia ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake; Mtume hana zaidi ila kufikisha, Imethibiti kwamba Mtume alipokuwa akiulizwa jambo ambalo hajateremshiwa wahyi alikuwa hajibu mpaka ateremshiwe wahyi.

Na yale msomewayo humu Kitabuni kuhusu mayatima wanawake.

Yaani Mwenyezi Mungu anawapa fatwa kuhusu wanawake vile vile Qur'an inawapa fatwa kuhusu hao wanawake.

Unaweza kuuliza : kuwa kufutu Qur'an ni kufutu kwa Mwenyezi Mungu hasa. Kwa hiyo kuunganisha kati ya mawili hayo ni kuunganisha kitu chenyewe.

Jibu : Makusudio ya kufutu kwa Qur'an hapa ni yale yaliyotangulia kubainishwa mwanzo wa Sura.

Na makusudio ya kufutu Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni yale aliyoyabainisha hapa kukamilisha yaliyotangulia. Kwa dhahiri ni kuwa kuunganisha kunafaa ikiwa kutakuwa na tofauti za mwelekeo fulani kama vile kutofautiana wakati au mahali pa jambo moja.

Ambao hamuwapi walichoandikiwa.

Yaani Mwenyezi Mungu na Qur'an inawabainishia hukumu ya wanawake ambao mliwazuilia fungu lao la urithi na mahari. Waarabu wakati wa ujahiliya walikuwa wakimdhulumu mwanamke na kumfanya kama bidhaa au mnyama.

Na mnapenda kuwaoa.

Mwanamume katika wao alikuwa akijichukulia yatima akiwa mzuri amempendezea humuoa, na kuila mali yake akiwa hakumpendezea humzuia asiolewe mpaka afe na achukue mali yake, mara nyingine humuua kwa lengo la kuchukua mali.

Na walio dhaifu katika watoto.

Yaani anawatolea fatwa pia kuhusu watoto wadogo ambao hamuwapi fungu lao la mirathi; na walikuwa hawamrithishi ila anayeweza kushika silaha. Ndipo Mwenyezi Mungu akalikataza hilo na akafanya fungu la mwanamume ni mara mbili zaidi ya mwanamke. Kwa hiyo hii ni kutilia mkazo ubainifu uliotangulia mwanzo wa Sura.

Na muwasimamie mayatima kwa uadilifu.

Yaani pia anawapa fatwa ya kuwasimamia mayatima kwa uadilifu wao wenyewe na mali zao, Kumpa kila mmoja katika wao haki yake kamili, awe mwanmume au mwanamke mdogo au mkubwa.

Na heri yoyote muitendayo - kuwatendea mayatima na wananwake - basi Mwenyezi Mungu anaijua.

Kwa ufupi maana ya Aya ni kuwa waislamu walimtaka Mtume kuwabainishia hukumu ya wanawake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwambia Mtume wake: waambie Mwenyezi Mungu amewabainishia sehemu ya hukumu hii na sasa anawabainishia sehemu nyingine, la muhimu kwenu ni kufanya uadilifu na kuitumia hukumu hiyo. Kisha akawabainishia Mwenyezi Mungu (s.w.t), katika Aya inayofuatia hukumu ya mwanamke, anayehofia unashiza wa mumewe na kuachana na mumewe.

﴿وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا وَالصُّلْحُ خَيْرٌ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴾

128.Ikiwa mke atahofia mumewe kuwa nashiza au kumtelekeza, basi hapana vibaya juu yao kusikilizana kwa suluhu; Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa mbele uchoyo. Na mkifanya wema na mkajihifadhi, basi Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa myatendayo.

﴿وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ وَإِن تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا﴾

129.Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wanawake hata mkikamia. Basi msipondokee kabisa kabisa, mkamwacha (mwingine) kama aliyetundikwa. Na mkisikilizana na mkamcha Mungu, basi Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu

﴿وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغْنِ اللَّـهُ كُلًّا مِّن سَعَتِهِ وَكَانَ اللَّـهُ وَاسِعًا حَكِيمًا ﴾

130.Na watakaptengana, Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja kwa wasaa wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye hekima.

UNASHIZA WA MUME

Aya 128 - 130

MAANA

Ikiwa mke atahofia mumewe kuwa nashiza au kumtelekeza.

Unashiza unaweza kuwa kwa mke kwa kumnyima unyumba mumewe au kutoka nyumbani bila ya idhini ya mume.Yametangulia maelezo ya unashiza wa mke katika kufasiri Aya ya 34 ya Sura hii.

Pia unashiza unaweza kuwa kwa mume kwa kumuudhi mke na kuacha kumpa matumizi au kumnyima siku akiwa na mke zaidi ya mmoja. Aya hii inaelezea hofu ya mke kwa unashiza wa mumewe au kumtelekeza. Makusudio ya kutelekeza ni kumwepuka kwake kunakoonyesha kumchukia. Ama kwenda kwenye shughuli zake na matatizo yake, lazima mke amvumilie na kumstahmilia madamu hamchukii.

Basi hapana vibaya juu yao kusikilizana kwa suluhu.

Ikiwa mke anahofia kuwa unashiza wa mumewe utasababisha talaka au kuwa katika hali ya kufungika - si kuwa na mume wala kuachwa, basi hapana ubaya kwa mume wala kwa mke kuafikiana wenyewe au kupitia kwa mtu. Waafikiane na kusikilizana, kuwa mume aache kumnyima haki zake, ili abakie katika hifadhi yake na waishi maisha ya utulivu.

Na suluhu ni bora kuliko kutengana na talaka. Kuna Hadith isemayo:"Halali inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni talaka." Ni vizuri tueleze kuwa anachokitoa mke kwa ajili ya talaka si halali ila kwa kuridhia nafsi yake. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿فَإِن طِبْنَ لَكُمْ عَن شَيْءٍ مِّنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَّرِيئًا﴾

"Kama wakiwatunukia kitu katika hayo mahari, basi kuleni kwa raha na kunufaika" (4:4)

Na nafsi zimewekewa mbele uchoyo.

Yaani uchoyo daima uko mbele katika nafsi haumwep uki hata wakati wa kutoa, ile hali ya jakamoyo anayoihisi mtoaji na kuificha wakati wa kutoa ndio uchoyo wenyewe na makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu "na nafsi zimewekewa mbele uchoyo." Mke haiachi haki yake kwa urahisi wala mwanamume hasamehi badali, Tusisahau kuwa Aya tukufu imezungumzia matatizo ya unyumba. Ama ikiwa unyumba hauna matatizo hakuna lolote la kuwajibisha kutoa kitu bali hakuna kati ya mume na mke anayeona kuwa kitu ni chake.

Na mkifanya wema na mkajihifadhi basi Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa muyatendayo.

Huu ni mwito kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa mume na mke kufanya kila juhudi amfanyie wema mwenzake na ajichunge na sababu za kukosana na kutengana.

Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wanawake hata mkikamia. Kufanya uadilifu baina ya wake kuko aina mbili: Kuna kule kunakowezekana, kama kufanya usawa katika matumizi na mazungumzo mazuri. Na kuna ambako kuko nje ya uwezo wa binadamu, kama vile mapenzi ndani ya moyo na hata kujamii pia. Mume anaweza kusisimuliwa na mke, kiasi ambacho yule mwingine hamsisimui vile.

Uadilifu baina ya wanawake unaotakiwa ni katika matumizi ambao uko chini ya uwezo. Ama uadilifu katika mapenzi na mfano wake, mtu hakalifishwi nao. Na hii ndiyo inayotofautisha baina ya Aya hii na ile Aya ya tatu katika Sura hii isemayo: "Na kama mkihofia kutofanya uadilifu, basi ni mmoja"

Imam Jafar as-Sadiq(a.s) anasema: "Ama kauli yake Mwenyezi Mungu: Mkihofia kutofanya uadilifu anakusudia kutoa matumizi; na ama kauli yake; 'Hamtaweza' anakusudia mapenzi." Na sisi ni katika wale wanaoamin i kabisa kuwa hakuna kitu kigumu kukipata kuliko uadilifu.

Kwa hakika yake hasa na kiini chake ni kujikomboa na matamanio; kama ilivyoelezwa katika baadhi ya Hadith kwamba mwadilifu ni yule mwenye kuhalifu mapenzi yake na akamtii Mola wake. Wala hawi na haya ila aliyejitakasa.

Basi msipondokee kabisa kabisa.

Kwa mke mnayempenda na mwingine mkamnyima haki zake.Mkamwacha (mwingine) kama aliyetundikwa akawa si mke aliyeolewa anayepata haki zake, wala si mtalikiwa anayeweza kuolewa na mwingine anayemtaka.

Na watakapotengana, Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja kwa wasaa wake.

Inatakikana kabla ya chochote mume na mke wajaribu kuondoa tofauti zao na mambo yanayosababisha kutengana. Kwa sababu suluhu ni bora. Ikiwa haiwezekani, basi talaka ni bora kuondoa madhara zaidi; na fadhila ya Mwenyezi Mungu na riziki yake itawaenea wote, wawe pamoja au watengane. Mwenyezi Mungu anaweza kumpa mtalikiwa mume bora kuliko wa kwanza; na anaweza kumpa mtaliki mke bora kuliko wa kwanza.

Kwa ufupi ni kwamba yote yaliyotangulia yanazunguuka kwenye mzunguuko mmoja tu ambao ni"kushikana kwa wema na kuachana kwa wema." Kushikana ni bora ikiwa hakuna ufisadi na kuachana ni bora ikiwa kuna ufisadi; kama ambavyo Mwenyezi Mungu ameumba dawa ya kuponesha magonjwa ya mwili, vile vile ameweka dawa ya maradhi ya kijamii.

﴿وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّـهَ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَكَانَ اللَّـهُ غَنِيًّا حَمِيدًا ﴾

131.Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na hakika tuliwaamrisha waliopewa Kitabu kabla yenu na nyinyi kwamba, mcheni Mwenyezi Mungu. Na kama mkikufuru, basi ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Mwenyezi Mungu ni mkwasi mwenye kusifiwa.

﴿وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا﴾

132.Na ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyo ardhini, na Mwenyezi Mungu atosha kuwa mlinzi.

﴿ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ أَيُّهَا النَّاسُ وَيَأْتِ بِآخَرِينَ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرًا ﴾

133.Akitaka atawaondolea mbali, enyi watu alete wengine. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa hilo .

﴿مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ ثَوَابُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴾

134.Anayetaka malipo ya duniani, basi yako kwa Mwenyezi Mungu malipo ya duniani na akhera na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kuona.

NI VYA MWENYEZI MUNGU VILIVYOMO MBINGUNI NA VILIVYOMO ARDHINI

Aya 131 - 134

MAANA

Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Katika juzuu ya kwanza na juzuu hii, tumezungumzia kuhusu kukaririka katika Qur'an. Sasa tutazungumzia kukaririka kwenye Aya hasa hii , kwa sababu ni Aya iliyotajwa na kurudiwa zaidi katika Qur'an

Kisha tutadokeza kukaririka kwa namna maalum ambayo imetajwa kwa kunakiliwa mara mbili katika Aya moja na kurudiwa mara ya tatu katika Aya inayoifuatia moja kwa moja bila ya kuweko kati kitu kingine.

Ama sababu za kukarika kwake kwa ujumla ni kwamba maudhui yake ni ulimwengu ambao pamoja na vilivyomo ndani yake unatolea dalili kuwapo Mwenyezi Mungu na sifa zake; kama elimu, uweza, matakwa na hekima. Ni dalili inayokusanya aina za dalili zote na vyenye kutolewa dalili. Kwa hiyo kukumbuka Aya hii ni kukumbuka kuwapo Mwenyezi Mungu na utukufu wake.

Ama kutajwa kwake hapa mara tatu, ni ishara ya faida tatu:

Kwanza : Mwenyezi Mungu katika Aya iliyotangulia amesema: "Atamtosheleza kila mmoja kwa wasaa wake" Kwa hiyo dalili hii imenasibiana na wasaa huu kuwa ni vyake vilivyomo mbing uni na ardhini.

Pili : Amesema:Kama mkikufuru basi ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Yaani yeye hamhitaji mwenye kukufuru kwa sababu vilivyomo mbinguni na ardhini ni vyake.

Tatu : Amesema Mwenyezi Mungu:Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na Mwenyezi Mungu atosha kuwa mlinzi. Akitaka atawaondelea mbali, enyi watu na alete wengine.

Makusudio ni kwamba Yeye ni muweza wa kuwamaliza waasi na kuwaleta watiifu; kwa sababu ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini. Kwa hiyo kila moja katika mara hizo tatu ina sababu yake na kukutanishwa na faida mpya.

Anayetaka malipo ya duniani, basi yako kwa Mwenyezi Mungu malipo ya duniani na akhera.

Yaani malipo ya duniani na akhera yanawezekana kupatikana pamoja na imani na takua. Mwenye kudhani kuwa malipo ya duniani hayawi pamoja na takua, basi huyo amekosea.

Kwa sababu hakuna kitu chochote kinachotengeneza vizuri maisha ya hapa duniani ila kitakuwa kinakubaliwa na dini bali kinaamrishwa na kuhimizwa na hiyo dini, lakini kwa sharti moja tu; kuwa kufanikiwa kwake kusiwe ni uovu kwa mwingine na utukufu wake usiwe ni utwevu wa mwingine.

Kwa hivyo malipo ya duniani na akhera hayagongani; isipokuwa kugongana kunatokea baina ya dhulma na malipo ya akhera - baina ya ghushi, hadaa na unyang'anyi na vilevile radhi za Mwenyezi Mungu, neema zake na pepo yake.