2
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
SOMO LA PILI
UNDANI WA NAFSI YA MWANADAMU HUMLAZIMISHA KUMTAFUTA MWENYEZI MUNGU
Nje ya mfumo wa hisia za mwili wake, mwanadamu anayo maeneo makubwa mno na muhimu ambayo kwa hali yoyote ile hayakufungiwa katika utaratibu wa mwili wake. Ili kuweza kugundua vipengele hivyo na hatua zilizo nje ya muundo wa mwili na ukubwa wa kiwiliwili chake, mtu lazima atafute muundo wa ndani na wa kiroho wa binadamu na kufahamu ule upeo mpana wa asili yake yenye mambo mengi, pamoja na udhihiri nyeti na wa kiungwana wa hisia na silika zake.
Mlolongo wa namna maalumu za ufahamu zinakuwemo katika nafsi ya binadamu ambazo zimejiotea mizizi ndani yake zenyewe, zinachomoza kutoka kwenye namna hasa ya hulka ya mwanadamu, na na kuchomoza kwao hakupasiki na jambo lolote la nje ya mwili wake. Miongoni mwa tambuzi hizi ni hisia za kuwajibika kwenye amana, haki, kuwa mkweli na mwaminifu. Kabla hajaingia kwenye uwanja wa sayansi na ujuzi na vyote vinavyohusika navyo, mtu ana uwezo wa kutambua ukweli fulani kwa njia ya utambuzi huu wa asili. Lakini baada ya kuingia kwenye eneo la sayansi na falsafa na kuujaza ubongo wake na shuhuda mbali mbali na tasfiri ya mambo, anaweza akasahau tambuzi zake za kawaida na za asili au akaanza kuzitilia mashaka. Ni kwa sababu hii kwamba binadamu anapokwenda kinyume na tabia yake ya asili kufafanua imani kwa maneno, tofauti huanza kujitokeza.
Kuelekea kwenye dini na kumuamini Mwenyezi Mungu, katika hatua zake za mwanzo huvutia kwenye sababu za kisilika na tambuzi za asili, lakini halafu huendelea kukua na kugeuka kwa msaada wa mantiki na tafakari. Mizizi ya hisia asili katika silika za mwanadamu imekwenda ndani mno na wakati huo huo, huonekana wazi na dhahiri sana hivyo kwamba endapo mtu anatakasa akili yake na roho yake kuhusu fikira za kidini na zisizo za kidini na halafu akajiangalia mwenyewe na dunia ya viumbe, kwa wazi kabisa ataona kwamba anasonga kuelekea upande fulani akiwa na msafara mzima wa viumbe. Bila ya utashi wowote au hiari upande wake, huanza maisha yake mahali fulani, na halafu tena bila hiari yake husonga mbele kwenda mahali pengine ambapo hapajui. Na ukweli huu huu unaweza kuonekana juu ya viumbe vyote vya asili, vikijiendesha kwa namna ya usahihi na kwa mpango.
Endapo mtu anayeona vizuri, akiwa bado yu katika hali ya kimaumbile, atayaangalia mazingira yanayomzunguka, kwa wazi kabisa atahisi kuwepo kwa nguvu kuu ambayo inamzunguka yeye na dunia yote. Katika umbile lake mwenyewe, ambalo ni sehemu ndogo sana ya dunia kubwa, ataona ujuzi, nguvu na utashi wa kuishi, na atajiuliza ni vipi ujuzi, nguvu na utashi havingeweza kuwepo katika dunia kwa jumla. Ni huu mpango uliofanyiwa mahesabu kwa ustadi mkubwa na mwendo wa dunia ambao humlazimisha mwanadamu kukubali kuwepo kwa uwezo wa akili ya fani zote ambayo, ikiwa ipo nje ya dunia ya kimaumbile, lakini hata hivyo inaisanifu na kuiamuru, isipokuwa kwa kukubalika hili, mpangilio huu wa dunia hauwezi kuelezeka. Mtu yeyote anaye tathmini nafasi yake hapa duniani anaweza kutambua kwamba kuna nguvu inayomuumba yeye, ikamleta yeye hapa, inayomtia usongefu ndani mwake, na halafu tena humwondoa, bila ya ruhusa au msaada wake kutakiwa kwa ajili ya lolote katika haya.
Kiongozi mkuu wa mashahidi, Hussein bin Ali
alisema katika dua yake ya siri kwa Muumba wake; "Inawezekanaje kufasiri kuweko Kwako kutoka kwenye kitu ambacho kinakutegemea Wewe kwa kuwepo kwake? Kwa nini huna hali ya kudhihirika kama wengine wasio wewe waliyonayo, ili kwamba iweze kukufanya Wewe uwepo dhahiri? Ni lini ulifichika kamwe kutoka kwenye jicho la ndani ili labda uweze kuhitaji uthibitisho uwe kama mwongozo wa kuelekea kwako Wewe? Ni lini ambapo ulikuwa kamwe mbali na sisi hivyo kwamba ishara na dalili Zako labda zingeweza kutusogeza karibu na Wewe? Limepofuka jicho ambalo halikuoni Wewe unapolitazama kulilinda na kuliongoza!
"Ee Mwenyezi Mungu, Wewe ambaye umejidhihirisha Mwenyewe kwa ufahari wako, unawezaje kuwa umefichika ambapo unaonekana na kudhihirika? Unawezaje kuwa haupo ambapo kwa kuonekana kwako kusiko na ukomo unawaangalia waja Wako?"
Hapana mahali popote na wakati wowote ambapo kitu kimetengenezwa bila mtengenezaji wake kuonekana, wala tendo bila mtendaji. Utafutaji wa kiungo baina ya chanzo na athari hujitokeza kutokea kwenye silika ya ndani ya mwanadamu; utambuzi wa uhusiano hauwezi kuondolewa kutoka kwa mtu yeyote.
Vivyo hivyo, hisia za kidini, kumtafuta Muumba, pia haiwezekani kuondolewa kutoka kwa mtu yeyote. Hata mtoto ambaye hana uzoefu wa dunia, wakati wowote asikiapo sauti au aonapo msongo, ki-silika atageuzia nadhari yake kwenye chanzo cha sauti au msongo. Misingi yote ya maisha halisi na ujuzi inasimama kwenye kukubali sababu kwa kila athari. Kanuni ya uhusiano, kwa kweli ni dhahiri kabisa ambayo haitoi mwanya wowote. Jiolojia, fizikia, Kemia, elimujamii, uchumi - katika hizi na elimu zingine, utafiti una lengo la kubainisha sababu na mambo yanayoamua uhusiano. Kwa ufupi, ni dhahiri kwamba elimu na ujuzi si lolote zaidi ya utafutaji wa vyanzo; maendeleo na kusonga mbele katika mambo ya binadamu hutokana na uchunguzi unaofanywa na wasomi kuhusu vyanzo vya mambo.
Kama ingekuwa inawezekana sisi kugundua kutoka kwenye kiumbe kimoja au pembe moja ya ulimwengu alama ya kujianzisha au kujiumba chenyewe kikamilifu, tungeridhika katika kueneza mfano huo moja kwa mpangilio wote wa viumbe. Kama mambo yalivyo, si muhimu kwamba kanuni ya usababisho kila mara ijioneshe kwetu katika miundo inayojulikana. Aina mbalimbali na wingi wa vyanzo viko kiasi kwamba mtafiti anayejihusisha na jambo moja tu labda atashindwa kupambanua visababisho vyote. Hata hivyo, katika mambo yote ya mwanadamu, maalum na ya kawaida, yaliyopita na yajayo, katika mazingira ya mtu mmoja au ya jamii, hakuna nukta hata moja inyoweza kuonekana kuwa ya bahati mbaya.
Si tu kwamba upo mpangilio mahususi ambao ni wa asili katika kuumbwa kwa kila kitu peke yake; pia kunakuwepo na ya kuonekana katika uhusiano wa kila jambo na jambo jingine, vile vile na uhusiano wa kila kitu na mazingira ambamo kinakuwemo, utaratibu stadi uliokokotolewa vizuri sana. Mathalani, katika kuukuza mti, kanuni za anga na ardhi zinafanya kazi katika uelewano kamili na muundo wa mizizi na matawi yake. Pia upo uhusiano wa wanyama na mti ule kwa vile wanapata chakula kutoka humo. Inawezekanaje kwamba pawepo na bahati mbaya katika asili ya utaratibu wa uhusiano wa aina hiyo?
Endapo jambo lingepata umbo katika ngazi fulani katika muundo wa kiumbe, bila kufahamu na katika misingi ya kubahatisha, hali hii ingetoa maandalizi mazuri sana kwa ajili ya kutoweka na kuangamia kwa dunia. Kwa sababu hitilafu ndogo sana katika usawa wa vitu asili na dosari ndogo sana katika kanuni angavu za ulimwengu ingetosha kusababisha vitu kukosa amari zao na viumbe vya angani kugongana, na kutokea kwa mlipuko mkubwa na kuangamia kwa dunia. Kama asili ya dunia ingeegemea kwenye kuweko bahati mbaya, kwa nini nadharia hata za wapenda anasa za dunia zimetegemewa kwenye kufikiria kupanga, mpangilio uliopangwa, kukosekana hali ya bahati mbaya? Kama dunia yote ni matokeo ya kubahatisha na bahati mbaya, ni kitu gani kile ambacho hakikutokea kwa msingi wa kubahatisha? Endapo kitu kilichopo sasa kilikuja kuwepo kama kiumbe si kwa sababu ya kubahatisha, ni sehemu gani muhimu na sifa zake zake ambazo zinazokibainisha na je zinaweza kutumika katika vitu vingi na vya namna nyingi mbali mbali vya ulimwengu?
Sasa kwa kuwa kubahatisha kunapingana na mpangilio na upatanifu, inaonekana kwamba kitu chochote kinachokuwa na mabaki ya upangaji, ubunifu na ukokotozi kitakuwa hakitangamani vizuri na hakiendelei, kwa sababu dhana za upangaji, usanii na mpangilio mzuri zimepingana na kubahatisha na hali ya uwezekano. Kudhani kwamba mfumo wa kubahatisha ndio muundombinu kwa ajili ya ulimwengu na kanuni yake inayotawala haitegemei uthibitisho wowote wa kimantiki au ushahidi wa kisayansi haiwezi kukubaliwa kuwa ni ufumbuzi wa uhakika kwenye jiometri ya muundo wa maumbile.
Wakati ambapo sayansi za majaribio zinaonyesha kwamba elementi na vipengele vya asili haviwezi kutoa mvuto wowote wa kujitegemea na havina uumbaji; ambapo uzoefu wetu wote, hisia zetu za fahamu na mafuhum zetu za kimantiki yanaelekeza kwenye maamuzi kwamba katika maumbile hakuna kinachotokea bila ya sababu na chanzo na kwamba vitu vyote vimetengenezwa kwenye mfumo madhubuti na kanuni maalum - ikiwa yote haya ndio hali halisi yenyewe, inashangaza kuona watu wengine wanageuzia migongo yao kwenye kanuni za kisayansi, mafuhum muhimu na mapendekezo yaliyo egemezwa kwenye tafakuri, na kukataa kuwepo kwa Muumba.
Elimu na vipengele vya kimazingira ni miongoni mwa sababu ambazo ama huzuia fahamu za asili za binadamu zisijioneshe, au kinyume chake, kuziimarisha. Kila chenye kujionyesha chenyewe kutoka kwenye chanzo cha silika hufanana katika mpangilio wake na mlolongo wa asili. Wale ambao wameachwa huru na kufuata mwelekeo wa asili wa maumbile yao bila ya kufungwa na mazoea na ambao tabia yao ya kina zaidi haikupambwa na maneno na muonekano, wanaweza kusikiliza vizuri zaidi wito wa nafsi zao za ndani zaidi na kuweza kupambanua baina ya matendo mema na mabaya, imani za kweli na za uongo. Kutokuwa na maadili ya dini, hali ambayo kwa kweli ni kuipa kisogo asili ya maumbile, kwa hiyo, ni nadra sana kuonekana miongoni mwa watu kama hao.
Endapo mtu anawaambia kwamba dunia haina mpangilio wenye kukaa ndani na kwamba inatokana na hali ya kutukia (isiyo ya uhakika), akiyapamba maneno yake kwa istilahi za kifalsafa, hatakuwa na athiri juu ya watu kama hao, kwa sababu watazikataa nadharia zake kwa ajili ya asili yao ya kimaumbile. Watu ambao wamenasa katika mitandao ya sayansi wanaweza kuwa mateka wa shaka na utatanishi kama matokeo ya istilahi zenye ushawishi. Elimu finyu ambayo hutia msukumo wa kiburi kwa binadamu ni kama mfano wa kipande cha kioo kilichopakwa rangi ka kuwekwa mbele ya kiupenyo cha akili na maumbile ya asili; yeyote mwenye akili hii huona dunia imetiwa rangi kidogo na ujuzi wake na elimu yake. Hudhania kwamba ukamilifu wa ukweli ni ule anaouona kupitia kwenye kipenyo chembamba cha fahamu zake na akili ambavyo ni nyara rahisi ya rangi. Kama hali ilivyo, hatuna maana kwamba binadamu aache kuendeleza akili yake ili ajiepushe na upotovu. Hata hivyo, asije akawekewa mipaka na ujuzi wake na elimu yake au asijigambe kwa hiyo elimu na ujuzi wake wenye kikomo.
Watu walio wengi, badala ya kufanya maarifa na ujuzi wao kuwa ngazi ya kunyanyua uwezo wa akili zao ili waweze kufikia kiwango cha juu zaidi, wanabaki wametulia na kufungiwa kwenye uzio wa kuta nne za dhana na masharti. Hali ya asili ya mwanadamu, pindi anapohisi hatari, haraka hukimbilia kwenye msaada wake. Mtu anapobanwa na shida na matatizo makubwa sana, wakati mambo ya kilimwengu yanapompa kisogo, anapokuwa hana njia yoyote ya kuzifikia rasilimali za kimaisha na anazama kama bua kwenye machafuko ya mabadiliko na kifo kipo karibu sana naye - ndipo dhamira ya kutoka moyoni humwongoza kisilika na kumwelekeza kwenye chanzo cha msaada kisichokuwa cha kilimwengu. Hutafuta msaada kutoka kwa yule ambaye uwezo wake upo juu ya uwezo wowote ule, na huelewa kwamba ni yule Muumba mwenye huruma na mwenye nguvu zote ambaye anaweza kumsaidia kwa kutumia uwezo wake usio wa kawaida na kumwokoa.
Kwa sababu ya utambuzi wake, kwa nguvu zake zote binadamu hutafuta msaada wa yule aliye mtakatifu sana ili amwondoshe kwenye hatari na kwenye faragha ya moyo wake, anahisi uwezo na nguvu ya muweza huyo zikifanya kazi kwqa ajili ya mwokovu wake. Mtu mmoja wakati fulani alimuomba Imamu Sadiq
amwongoze kuelekea kwa Mola wake Mlezi, akasema kwamba maneno ya wapinzani yalimtatanisha. Imamu akamuuliza, "Umewahi kusafiri kwa meli? Akajibu, "Ndio."
Imamu: "Je, imewahi kutokea kwamba meli ikaingiza maji na hapakuwepo na mtu wa kuwaokoeni ili msizame kwenye mawimbi ya tufani ya bahari?"
Jibu: "Ndio." Imamu: "Wakati huo wa hatari na katika hali hiyo ya kukatisha tamaa, je, ulikuwa na hisia kwamba nguvu isiyopimika na yenye uwezo mkubwa ingeweza kuwakuokoeni kwenye balaa lenu la kutisha?"
Jibu: "Ndio, hivyo ndivyo ilivyokuwa."
Imamu:"Ni Mwenyezi Mungu Mwenye uwezo ambaye ndio chanzo cha mategemeo na kwake Yeye watu ndiko wanakotazamia kwa matumaini pale ambapo milango yote inapokuwa imefungwa."
Hata watu waasi na wapenda dunia wenye uwezo ambao hawautambui uwezo usio na kikomo wa Mwenyezi Mungu, wanapofurahia utawala wao, hubadilika wanaponasa kwenye mtego wa kushindwa na kuangamia. Husahau kumkana kwao Mwenyezi Mungu ambako madhehebu yao ya mazingira na ya kianasa za dunia ulivyojipandikiza ndani yao na kwa moyo mkunjufu kabisa hugeukia kwenye asili ya viumbe vyote na chanzo cha nguvu zote.
Historia imeorodhesha mifano mingi sana ya watu kama hao ambao walipata kuwa waathirika wa matatizo na hali za mitihani hivyo kwamba vumbi la upotofu liliondolewa ghafla kutoka kwenye tabia zao za asili na kutoka kwenye vina vya nafsi zao na wakarejea kwa Muumba asiye na kifani. Kwa kuongezea kwenye rasilimali za ndani ambazo ni za asili katika nafsi ya binadamu na humsaidia yeye kugundua ukweli hivyo kwamba, akiwa huru kutokana na dhana na vikwazo vya kiakili husonga mbele akifuata njia ya tabia yake ya asili, na kiwango cha nje cha mwongozo na maonyo pia ni muhimu kwa ajili ya kumwelekeza njia na kuimarisha hali yake ya asili. Ni mwongozo ndio unaorekebisha sifa za ki-uasi na kuilinda akili na tabia ya asili kutoka kwenye upotovu na utiifu kwa miungu wa uwongo. Mitume walipelekwa kwa madhumuni ya kuwafanya watu wajihadhari na utambuzi wenye utatanishi, wa tabia zao za asili, ili kuufanya mwelekeo wao wa ki-Mungu ufuate mkondo unaostahili, na kuyanyanyua matarajio yao makubwa.
Amirul-Mu'minina
amesema:"Mwenyezi Mungu aliwatuma Wajumbe Wake miongoni mwa watu ili waweze kuwahoji kuhusu ahadi yao na Mwenyezi Mungu, kuwakumbusha watu kuhusu neema za Mwenyezi Mungu zlizosahaulika, kuzungumza nao kwa namna ya kuwaonya, kuzindua hekima iliyojificha ndani mwao, na kuwaonesha ishara za uwezo wa Mwenyezi Mungu."
Mwongozo na nasaha za aina hiyo kwa jinsi yoyote ile haimaanishi kuzimwa kwa nuru ya dhamira endelevu ya mwanadamu kumnyima uhuru na uwezo wake wa kufikiri na kuchagua. Hii, kinyume chake, ni aina ya msaada kwenye mielekeo na silika bayana, kuziwezesha kukua na kuendelea. Ni kupitia mwongozo na nasaha ambapo wanadamu wanaondolewa kwenye vifungo na kuwezeshwa kunufaika kutokana na mpanuko wote wa maumbile yao ya asili na kusitawi pamoja na viumbile wenzao wote. Qur'anii inasema:
وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾
". . Anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomuamini yeye, na wakamtukuza, wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu."
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ﴿٢٤﴾
"Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuiteni kwa yale yatakayokupeni uzima."
يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ ﴿٥٧﴾
"Enyi watu! Yamekufikieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, pozo la yale yaliyomo vifuani, .
Watu wa kwanza waliokubali wito wa Mitume walikuwa watu wenye mioyo safi na dhamira zilizoongoka. Safu za washindani wao zilikuwa na wale waliotegemea juu ya mamlaka bandia na utajiri au walijawa na kiburi kwa sababu ya ujuzi wao mdogo na wenye mapungufu, akili zilizochafuliwa na udanganyifu, kwa namna ambayo kwamba jeuri yao isiyo na msingi, ilizuia uwezo wa kina na matamanio yao kustawi.
Mwanazuoni fulani amesema hivi: "Katika mambo ya kiroho, pia kanuni ya usambazaji na kuhitaji huwepo. Kama haja ya dini isingekuepo katika tabia ya asili ya binadamu, mahitaji yaliyotolewa na Mitume yangepotea bure. Tunaona kwamba ugawaji wa Mitume ulipata wateja; mawazo yao yenye mipango mingi, yasiyo na shaka na sahihi kabisa yalipata wafuasi na waunga mkono wengi. Huu ni uthibitisho kwamba haja ya dini inakuwepo ndani ya mwanadamu na dhamiri yake ya kina kabisa."
Kwa kweli, mafundisho ya msingi ya Mitume wote yalikuwa wito wa kumwamini Mwenyezi Mungu mmoja, sio ya kuthibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Walibatilisha thamani ya masanamu, jua, mwezi na nyota kuabudiwa, ili kwamba kiu ya ya mwanadamu ya kina na ya kimaumbile kwa ajili ya ibada isitoshelezwe na kuvikimbilia vitu vya maumbo ya nje kama hivi na wanaweza, badala yake, kutafuta malengo na maadili yao kwenye safina imara na kupanda kwenye madhumuni halisi ya ibada. Mioyo yao inapaswa ifungamane na ulinzi usio na kikomo, na kwa imani ambayo daima inapanda, wao wanapaswa wakati wote kusonga mbele kuelekea kwenye chanzo cha maadili yote na wema, hatimaye kufikia kwenye malengo yao.
Aina zote za kuabudu miungu wengi za ukana dini - mfumo wa kale ambao ni kuabudu masanamu namuundo ulioendelea, wa kisasa, ambao tamaa ya anasa - ni matokeo ya kukengeuka asili ya maumbile. Maendeleo ya elimu kuhusu uzoefu wa kidini ambayo yanatokea pote duniani yamesababisha ugunduzi mwingi ambao unaruhusu maamuzi muhimu ya uhakika yaweze kufikiwa.
Ikiegemezwa kwenye takwimu nyingi kiasi zilizokusanywa na wataalamu wa sosholojia, wanaakiologia (wachambuzi wa elimu ya kale), wana anthropogia (elimu ya asili ya binadamu), historia ya dini sasa ina changanua silika ya kidini, pamoja na uanzishwaji, imani, desturi na vipengele ambavyo vinaijenga jamii, kwa namna mpya ambayo inatofautiana sana na maelezo yaliyotolewa kabla ya hapo. Sasa hivi kuna wimbi la fikra ambalo kwa muda wote linaendelea kuwavutia wafuasi wapya kutoka kwenye madhehebu mbali mbali wanaosema kwamba hisia za kidini ni kijenzi cha msingi, cha asili na madhubuti cha roho ya binadamu na kwamba ni njia ya asili ya kutambua yaliyo ghaibu. Mnamo kama mwaka wa 1920, mwanafalsafa wa Kijerumani aitwaye Rudolf Otto aliweza kudhibitisha kwamba sambamba na dalili za kiakili na maadili ndani ya mwanadamu, pia zipo dalili za kimantiki ya hali ya juu sana ambazo hujenga hisia za kidini. Sifa zinazomhusu Mwenyezi Mungu kama vile uwezo, ukuu na zenye kuvuka mipaka zina madhumuni ya kusisitiza kwamba utakatifu hauwezi kurahisishwa kuwa dhana nyingine. Hii ni namna inayojitegemea ambayo haiwezi kupatikana kutokana na namna nyingine na haiwezi kuhusishwa na dhana nyingine yoyote, kimantiki au vinginevyo.
Mojawapo ya upekee wa zama hizi kwa kweli, ni utafutaji wa kipimo cha nne katika dunia ya asili kiitwacho "Wakati". Kama vilivyo vipimo vingine, ni lazima kiingiliane na miili, na kwa hiyo hakuna mwili uliopo katika duniani ambacho kimeepukana na wakati ambao unatokana na msongo na mabadiliko. Vivyo hivyo ni sifa ya zama hizi kwamba tafiti za wanachuo zimeongozea kwenye ugunduzi wa 'kipimo cha nne' cha nafsi ya mwanadamu - hisia za kidini
.
Vipimo vingine vitatu au hisia vinakuwa na hisia ya dadisi, hisia ya maadili na hisia ya ubora. Hisia ya kidini au dhana ya utakatifu, ni kipimo cha nne na cha msingi zaidi cha hisia. Kihulka kila mtu anao mvuto na mwelekeo kwa kile kilichoko nje ya maumbile, tofauti na huru kutokana na zile hisia zingine tatu. Kwa kugunduliwa kwa hisia ya kidini, jela ya nafsi yake, yenye nyuso tatu, iliporomoka na ikathibitika kwamba mielekeo ya kidini ya mwanadamu imeota mizizi kwa kujitawala kabisa ndani ya utu wake. Ilijitokeza yenyewe hata nyakati zile ambazo watu walikuwa wanaishi ndani ya misitu na mapangoni.
Licha ya ubora wake, kujitawala na kufaa kwa hisia za udadisi, maadili, ubora na nafasi zilizoichukua katika kutokeza kwa elimu, maadili na ujuzi, ilikuwa ni hisia ya kidini iliyoandaa mazingira kwa ajili ya utendaji wa hisia hizi tatu, ikizisaidia kusonga mbele katika njia yao na kugundua siri za ulimwengu ulioumbwa. Kwa mtazamo wa muumini, dunia imesanifiwa katika msingi wa kanuni na mpango sahihi uliokusudiwa vizuri. Imani hii kwa Mwenyezi Mungu mwenye kuamuru na mwenye hekima huzindua hisia ya udadisi kwa lengo la kutafuta na kugundua kanuni na siri za maumbile ambazo zimeegemea kwenye mlolongo wa sababu namotokeo yake. Mchango wa hisia ya kidini katika kukuza na kuendeleza tabia tukufu kabisa za binadamu, katika kurekebisha hisia zake na kurutubisha silika zake za maadili na wema, haupingiki. Wale wanaofuata maamrisho ya dini wanauona kama mmoja wa wajibu wao muhimu sana wa kidini, kudhibiti silika zao na kupata sifa nzuri za hali ya juu. Fikra ya kidini pia imekuwa kipengele chenye kulea hisia za kisanaa. Watu wa kale walitengeneza kazi zao za kisanaa endelevu sana ili kuwatukuza miungu wao. Mahekalu ya ajabu ya China, mapiramidi makubwa ya Misri, masanamu ya aina ya kipekee ya Mexico, usanifu majengo ulioboreshwa na wakustaajabisha ya Mashariki ya Kiislamu -yote haya yalitegemea sana kwenye hisia ya kidini.
Wanasaikolojia wanaamini kwamba upo uhusiano baina ya hali ya balehe na kujitokeza kwa ghafla kwa hisia za kidini. Katika kipindi hiki cha maisha, hata kwa watu ambao siku za nyuma hawakujali mambo ya dini, hisia ya kidini inachukua mkazo maalum. Hapana shaka kwamba, wito wa ndani hujionyesha kwa jinsi ambayo kwamba hakuna kizuizi kinachoweza kuzuia njia yao. Hata hivyo vipengele fulani kama vile propaganda za upinzani vinaweza kupunguza hisia za ndani kwa ndani na fikra sahihi, ingawa vishawishi kama hivyo haviwezi kuishia kwenye ung'oaji kabisa wa uwelekeo huo. Endapo vikwazo kama hivyo vitaondolewa, hisia zilizo imara huanza tena utendaji wao na kujionesha kwa namna ya jitihada zao endelevu za ndani kwa ndani.
Tunafahamu kwamba zaidi ya nusu karne imepita tangu mapinduzi ya kikomunisti ya Jumuiya ya Kisovieti, lakini mizizi ya dini ipo hai kwenye vina virefu vya nafsi za watu wa Sovieti. Licha ya juhudi zote ambazo zimefanywa katika kipindi hiki kirefu na watawala za kuifuta dini, wameshindwa kuondoa hisia ya kidini kutoka kwa watu.
Kuwapo kwa fikra za maslahi ya kidunia, kwa hiyo, hakupingani na ukweli kwamba kumwamini Mwenyezi Mungu ni jambo la kawaida kwa mwanadamu. Endapo madhehebu fulani itaondoka kwenye mkondo wa maumbile ya asili na hapo ikajifanya ya kipekee kusuiana na madhehebu zingine, kwa dunia ya sasa na katika nyakati zilizopita, hali hii haiwezi kufikiriwa kama ni kukanusha ile hoja kwamba kumwamini Mwenyezi Mungu ni kawaida kwa binadamu; tofauti inakuwepo katika nyanja zote. Kile ambacho historia inakionesha na kwamba madhehebu ya tamaa za kidunia ilianzishwa mnamo karne ya sita na saba kabla ya Yesu Isa
.