5
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
SOMO LA TANO
KUONEKANA MWENYEZI MUNGU KATIKA MAUMBILE
Dunia ya maada na maumbile, inayochukuliwa kama kitu kizima kilichoumbwa, ndio ushahidi mzuri sana, wa dhahiri na ulioenea sana, bila upinzani, juu ya ujuzi wa Mwenyezi Mungu. Utashi wenye busara ya Kanuni ya Milele unaweza kugundulika kutoka kwenye kutendeka huku hasa kwa mabadiliko ya vitu. Ni dhahiri kwamba miale Yake ya milele inatoa uhai na mahitaji kwa viumbe vyote, na kwamba viumbe wote wanapata uhai na maendeleo yao kutoka Kwake.
Kuchunguza viumbe tofauti ulimwenguni, siri za kitabu cha uumbaji, kurasa ambazo zote zina shahidilia kwenye shughuli za akili ya juu sana katika uumbaji wake, hutoa, halafu ushahidi ambao wakuegemeza elimu na imani juu ya Muumba mwenye hekima, Ambaye uwezo wake huonekana kidogo tu kwenye mpangilio wa viumbe kwa utukufu wao wote na ukubwa wao. Zaidi ya haya, ni uthibitisho ulio rahisi na kueleweka kwa urahisi ambao unakosa utata na uzito mkubwa wa ushahidi wa kifalsafa. Ni njia ya uchunguzi na tafakuri ambayo ipo wazi kwa wote; kila mtu anaweza kunufaika nayo, wanafikra na wanazuoni na umati wa watu wa kawaida.
Kila mtu, kwa kadiri anavyoruhusiwa na uwezo wake na upeo wa kuona kwake, anaweza kuona katika jambo zima la uumbaji dalili za uunganikaji, utulivu, umasukusudi wa dhati kabisa, na kukuta katika kila moja ya chembechembe zisizo idadi za maumbile, uthibitisho thabiti wa kuwepo kwa chanzo cha viumbe. Marekebisho kamili ya kila aina ya mnyama kufuatana na hali za maisha yake ni ishara kubwa ya Mwenyezi Mungu; kila aina imeumbwa pamoja na vifaa vyote muhimu vinavyohitajika katika hali ya maisha yake. Musa, (amani iwe juu ya Mtume wetu pamoja na yeye), ambaye alizungumza na Mwenyezi Mungu, alitumia ushahidi huu ili aoneshe kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa Firauni. Yeye Firauni akawaambia Musa na nduguze:
قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَا مُوسَىٰ ﴿٤٩﴾ قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ ﴿٥٠﴾
"Ni nani Mola Wenu ewe Musa? Akasema "Mola Wetu ni yule aliyekipa kila kitu umbo lake. ." (20:49-50).
Vivyo hivyo Imam Sadiq
alimwambia Mufadhal, "Tazama kwa uangalifu lile umbo la maumbile ya ndege; uone jinsi alivyoumbwa mwepesi na mdogo katika ujazo ili kumwezesha kuruka. Ndege alipewa miguu miwili tu badala ya minne ambayo wanyama wengine wamepewa na vidole vinne tu kati ya vitano ambavyo wanavyo katika kila mguu. Ndege wana vifua nyembamba vilivyochongoka, ili waweze kuelea hewani na kuruka kwa urahisi kuelekea kila upande. Miguu mirefu ya ndege imekaa vizuri chini ya mkia wake na mabawa yake, na mwili wake wote umefunikwa na manyoya ili hewa iweze kupenya humo na kumwezesha kuruka. Kwa kuwa chakula cha ndege ni pamoja na mbegu na minovu ya wanyama ambavyo wanavila bila kutafuna, basi hawana haja ya meno.
Badala yake, Mwenyezi Mungu amewambia ndege mdomo mgumu na wenye ncha kali ambao hauwezi kuvunjiki wakati unaponyofoa nyama au kuumia wakati wa kukusanya nafaka. Ili kumuwezesha kiumbe huyu kukisaga chakula ambacho hakukitafuna, amepewa mfumo wa kusagia chakula wenye nguvu na mwili wenye joto. Zaidi ya hayo, ndege huzaana kwa kutaga mayai ili waweze kubakia wepesi kiasi cha kutosha kuwawezesha kuruka; endapo watoto wao wangekuwa wakulie matumboni mwao, wangekuwa wazito sana kuweza kuruka."
Halafu Imam akarejea kwenye kanuni ya jumla, akisema,"Kwa hiyo upekee wote wa umbile la ndege huendana na mazingira yake na namna ya maisha yake."
Suala la lugha ya wanyama - ile njia ambayo kwamba wanyama wanawasiliana wao kwa wao - ni dalili nyingine ya ki-ungu. wanyama wanayo aina maalumu ya lugha ambayo huwawezesha kuwasiliana wao kwa wao.
Qur'ani Tukufu inaelezea kisa cha mdudu chungu akiongea na Nabii Suleiman
:
قَالَتْ نَمْلَةٌ يَا أَيُّهَا النَّمْلُ ادْخُلُوا مَسَاكِنَكُمْ لَا يَحْطِمَنَّكُمْ سُلَيْمَانُ وَجُنُودُهُ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١٨﴾
"Akasema mdudu chungu: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Suleiman na majeshi yake, hali hawatambui." (Naml: 27: 18).
Wanasayansi wa sasa wamegundua mtandao changamano wa mawasiliano miongoni mwa wanyama ambao ni mgumu zaidi na uliosahihi kuliko mfumo wetu wenyewe wa mawasiliano. Crissy Morrison anaandika: "Kama tukimweka nondo jike karibu na dirisha la chumba chetu, hutoa ishara nyororo ambazo nondo dume huzipokea kutoka kwenye umbali wa kuangaza na kutuma ishara zake mwenyewe katika kujibu. Kwa kiasi chochote utakachoweza kutaka wewe kuvuruga mawasiliano haya, hutaweza Mwenyezi Mungu na sifa zake 51 kufanya hivyo. Je, kiumbe huyu mnyonge anabebea aina fulani ya transimita, au huyu nondo dume anacho kinasio kilichojificha kwenye kipapasi chake?
"Senene husugua miguu yake kwa pamoja, na sauti inaweza kusikika kwa umbali wa kilomita moja wakati wa usiku wa kimya na mtulivu. Ili aweze kumwita mwenzi wake, nondo dume huweka tani sitini za hewa katika mwendo na senene jike hupeleka jibu la kusisimua kwa kuposa kwake kwa kwa njia ya kimwili, pamoja na kwamba inavyoonekana hakuna sauti inayosikika kutoka kwake. "Kabla ya kuvumbuliwa kwa radio, wanasayansi walidhani kwamba wanyama waliwasiliana wao kwa wao kwa njia ya harufu. Endapo dhana hii ingekuwa kweli, bado ingekuwa ni jambo la muujiza, kwa sababu harufu ingekwenda kupitia hewani ili iweze kufika kwenye pua za mdudu jike. Hali hii ni mbali kabisa na suala la ama upepo unavuma au hapana na jinsi gani mdudu jike angeipata harufu na kutambua inatoka wapi, na kumwezesha kujua mwenzi wake aliko.
"Leo hii, shukrani kwa njia changaman za hali ya juu za kitaalamu, tumepata uwezo wa kuwasiliana na kila mmoja wetu kwa masafa marefu sana. Radio ni uvumbuzi wa kipekee kabisa, unaotuwezesha kuwasiliana mara moja. Lakini matumizi ya uvumbuzi huu hutegemea waya na sisi kuwepo mahali fulani. Nondo bado yupo mbali sana na sisi kwa mbele yetu."
Kuchagua sayansi za kimajaribio kama njia ya kuchunguza miujiza ya dunia isiyo na kikomo kuna manufaa mengine ndani yake zaidi ya kuwa karibu na kila mtu. Ni ule utambuzi wa maajabu ya maumbile na utaratibu uliomo ndani yake ambao kwa kawaida humuunganisha mwanadamu na Mwenyezi Mungu Ambaye ameuumba; utambuzi wa aina hii humuonesha binadamu sifa za ukamilifu, ujuzi na uwezo usio na kikomo ambao humuainisha Muumba na Chanzo cha viumbe wote.
Mpangilio huu ulio sahihi unaashira lengo fulani, mpango, hekima pana na kubwa. Ubunifu gani, uwezo gani, ujuzi gani ambao Yeye Ameuwekeza katika dunia yote ya uhai, katika udogo kabisa na ukubwa kabisa wa uumbaji wake wenye kulandana - katika ardhi, katika angahewa, katika maumbile ya ki-mbinguni, katika moyo wa mawe, na kwenye viini vya chembehai! Tunapozungumzia juu ya 'Mpango' lazima ieleweke kwamba fikira hii ya mpangilio inatumika kwa kitu ambapo sehemu zake mbali mbali kwa namna fulani zinahusiana kwa namna ambavyo kwa ulinganifu zinafuatia lengo maalum; ushirikiano wa sehemu hizo lazima pia uwe umezingatiwa. Ingawa wale wanaokanusha kuwepo kwa mpangilio katika ulimwengu kwa ujumla hawakatai kuwepo kwa chanzo hai (kwa vile wanakubali kanuni za usababisho), kinachomaanishwa na kanuni ya ujuzi wa pande mbili katika maumbile ni ile sababu ya msingi, na hii - ikimaanisha kama ifanyavyo kuingilia kati kwa lengo na makusudi kwenye jambo asilia - wao hukataa.
Kwenye Ayah zake nyingi sana, Qur'anii Tukufu inamualika binadamu kutafakari kuhusu mpangilio wa uumbaji ili kwamba watu walio wengi waweze, kwa njia rahisi iwezekavyo, kutambua kuwepo kwa Muumba wa Pekee. Hizi ni baaadhi ya Ayah husika:
إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿١٦٤﴾
"Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kuhitilafiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini pamoja na viwafaavyo watu, na maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo ishara kwa watu wenye kuzingatia." (Baqarah: 2:164).
اللَّـهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى يُدَبِّرُ الْأَمْرَ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُم بِلِقَاءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ ﴿٢﴾
"Mwenyezi Mungu aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnazoziona; kisha akatawala kwenye Arshi, na akalitiisha jua na mwezi, kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliowekwa. Yeye ndiye anayeliendesha kila jambo, na anazipambanua Ayah ili mpate kuwa na yakini kukutana na Mola wenu." (Rad: 13:2).
وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٣﴾
"Na ndiye aliyeitandaza ardhi na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya dume na jike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika haya zimo Ishara kwa wenye kufikiri." (Rad; 13:3).
Endapo tunakubali na kukimbilia kila nadharia ambayo imewekwa na wataalam na watafiti, hata ile nadharia ya mabadiliko kuhusu kutokeza kwa spishi za aina mbali mbali zinazoonekana duniani, hakuna hata nadharia moja itakayoeleweka bila kuwepo kwa nguvu kamili, uingiliaji kati wa utashi, utambuzi, na lengo na makusudio ya mwisho. Uumbaji wa pole pole katika mpangilio wa maumbile pia unaonesha kwa uwazi uingiliaji kati kwa utashi na utambuzi katika utaratibu wake; hatua zote katika mwendo na maendeleo ya maumbile zimetegemezwa kwenye chaguo na azimio sahihi kabisa, na maumbile kamwe hayajatofautiana kwenye njia yake yaliyowekewa hata kidogo katika mamilioni ya miaka.
Ni kweli kwamba katika hatua za mwanzo za kupata uthibitisho wa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kutoka kwenye mpangilio wa ulimwengu zimetumika kumbukumbu za majaribio, na kwamba sehemu za hoja zimejengwa kwa msaada wa hisia, uchunguzi wa maumbile na uchunguzi wa majaribio. Hata hivyo, kwa kweli hoja hiyo si ya majaribio lakini hasa zaidi ni ya kimantiki, ambayo inatuongozea nje ya maumbile na kutuelekeza kwenye ukweli ulio nje ya uwezo wa binadamu ambao uko mbali na maumbile. Uthibitisho wa majaribio unahusu uhusiano baina ya sehemu mbili za maumbile, ambazo kila moja lazima iwe ya utambuzi wa kihisia ili kuruhusu uhusiano baina ya sehemu hizo mbili kuanzishwa.
Tunapokisia kiwango cha ujuzi na utambuzi wa mtu kwa kupima kazi zake na mafanikio yake, hatupo katika uvumbuzi wa majaribio, kwani kiwango cha ujuzi na akili za mtu sio kitu chenye wingi wa kugusika kwa ajili ya sisi kutegemea majaribio moja kwa moja upande wetu sisi.Bila shaka, mtu moja kwa moja anapata utashi, akili, na fikira ndani ya nafsi yake mwenyewe, lakini huwa hana utambuzi kama huo wa kuwepo kwa vitu hivyo kwa wengine; hawezi kuvifikia.
Tunatambua kuwepo kwa akili na fikira ndani ya watu kwa kuangalia kazi zao na mafanikio yao, ingawaje hakuna uthibitisho wa kimajaribio juu ya kuwepo kwa vitu hivyo ndan ya watu hao. Sasa ugunduzi wa akili ndani ya watu wengine kwa njia ya kazi zao na mafanikio yao, upo kwenye ushahidi wa kimantiki, sio matokeo ya majaribio kwa maana ya akili na kazi zake kuwa vyenye kuvutika moja kwa moja kwenye uchunguzi wa moja kwa moja ili kwamba uhusiano wao uweze kugundulika. Ugunduzi huu pia haupo kwenye ulinganishaji wa kimantiki kwa maana ya kuonesha utambulisho baina ya mtu mmoja na wengine wote.
Ikiwa basi, kwamba utambuzi wa fikira na akili ndani ya watu haufanyiki kwa njia ya uthibitisho wa kimajaribio, ni dhahiri kwamba hoja ya mpangilio katika ulimwengu na uhusiano wake na chimbuko la ki-Mungu pia haipo katika jamii ya uthibitisho wa kimajaribio.
Kutoka kwenye mtazamo mwingine, kwa kuwa mwanadamu siye muumbaji wa maumbile bali yeye ni sehemu yake, matendo yake katika dunia ya maumbile yanawakilisha kuanzishwa kwa uhusiano baina ya sehemu tofauti za dunia hiyo. Lengo na madhumuni yanayotafutwa na mwanadamu katika ukusanyaji wa mlolongo wote wa elementi za kimaada (kwa mfano, katika kujenga jengo, kutengeneza motokaa, au kiwanda) kuna husiana na nafsi yake mwenyewe, ni kusema kwamba, lengo na makusudio ya mwisho ni mtengenezaji mwenyewe, sio kile kitu kilichotengenezwa. Uhusiano baina ya sehemu ya vile vitu vilivyotengenezwa, kwa hiyo ni uhusiano ambao si wa kimaumbile; kwa kuthibitisha uhusiano huo, mtengenezaji anataka kutimiza malengo yake mwenyewe na kukumbukia mapungufu yake mwenyewe, kwani juhudi zote za mwanadamu ni msongo wa kutoka kwenye uwezekano na kwenda kwenye hali halisi na kutoka kwenye mapungufu kwenda kwenye ukamilifu.
Hata hivyo, sifa hizi mbili hazitumiki katika uhusiano baina ya vitu vilivyoumbwa, na yule muumbaji - Mwenyezi Mungu. Uhusiano baina ya seheMwenyezi mu tofauti na kazi za Mwenyezi Mungu ni wa kimaumbile, na lengo la kiumbe kilichoumbwa halina uhusiano na Muumbaji. Yakiwekwa mbalimbali, makusudio ya matendo ya Mwenyezi Mungu yote yanahusiana na matendo yenyewe, si kwa Wakala, kwa kuwa hekima ya Mwenyezi Mungu inalazimu kwamba Yeye apaswe kusababisha viumbe wote kufikia ukamilifu wao.
Wakati wa kutengenezwa hoja ya mpangilio wa ulimwengu tunajaribu kuthibitisha kuwepo kwa mtengenezaji afananaye na mtengenezaji binadamu, mtengenezaji wa ki-Mungu, kwa kweli, pia atakuwa kiumbe kilichoumbwa kwa kiwango cha mwanadamu; kuthibitisha kuwepo kwa mtengenezaji kama huyo ni jambo tofauti kabisa na kuthibitisha kuwepo kwa Mtengenezaji na Muumbaji wa viumbe wote. Kwa mtazamo wa kisayansi, kujianzisha mwenyewe kwa jambo hakuwezekani; ile nadharia ya ki-Marx kwamba dunia ya kimaada wakati wote anabadilika na kuelekea kwenye hali za juu zaidi ni dhahiri inapingana na kumbukumbu za kisayansi na ukweli wa kimaumbile. Mielekeo yote na misongo katika nyanja ya madini ninatokana ama kwa sababu ya kuingilia kati kwa utashi nje ya vitu au mvutano, kubadilishana, na ukusanyikanaji na maumbo mengine.
Katika ulimwengu wa mimea, maendeleo, kukua na kuongezeka hutokea kama matokeo ya kunyesha mvua, mwanga wa jua na kupata yale madini muhimu kutoka kwenye udongo. Hali ni ile ile kwa ulimwengu wa wanyama. Hali ni ile ile kwa ulimwengu wa wanyama, isipokuwa kwamba hapo kipengele cha mwendo wa hiari kuelekea kile chenye manufaa na muhimu lazima kiongezwe. Katika mifano yote iliyotajwa hivi punde, kuna ushirikiano wa wazi baina ya vitu na viumbe, kwa upande mmoja, na mambo yaliyopo nje yao kwa upande mwingine. Kwa mujibu wa sifa pekee za asili ndani ya kila kiumbe na sheria na kanuni ambazo zinakitawala, haziwezi kukiuka amri ambazo zimepigwa mhuri katika umbile lake.
Ukweli wa kwamba mwanadamu hutambua kwa hisia zake una sifa fulani za pekee. Tunatambua wazi kwamba viumbe katika dunia hii vinapatwa na mabadiliko ya mara kwa mara na hali ya kutokudumu. Kakita kipindi chote cha kuwepo kwake, kiumbe chochote cha kimaada ama kinakwenda kwa kupitia mkondo wa kukua na kuendelea au kuelekea kwenye kuoza na kudhoofika. Kwa ufupi, hakuna kiumbe cha kimaada katika hatua ya uhai wake kinabakia kama kilivyo na hakibadiliki.
Kuwa na kikomo ni sifa nyingine ya uhai wa kihisia. Kutoka kwenye chembechembe ndogo sana hadi kwenye kundi kubwa la nyota, vitu vyote vinahitaji nafasi na muda; ni kawaida kwamba vitu fulani huchukua nafasi kubwa zaidi au muda mrefu zaidi; na vingine, huchukua muda mfupi zaidi na nafasi ndogo zaidi. Zaidi ya hayo, viumbe vyote vya kimaada vina uhusiano kwa mtazamo wa kuwepo kwao na pia sifa vilivyonazo; sifa yoyote ile kama vile uwezo, utukufu, uzuri na hekima ambazo tunazozitoa kwa vitu, tunafanya hivyo kwa kulinganisha na vitu vingine.
Kutegemea na hali ya kimasharti pia ni miongoni mwa sifa za viumbe hivi. Kuwepo kwa kiumbe chochote tunakowezakutambua kunategemea na ni kwa masharti ya vipengele vingine, na kwa hiyo, kinakuwa kwenye kuvihitajia vipengele hivyo. Hakuna kiumbe kinachoweza kuonekana duniani ambacho kinajitegemea chenyewe tu, ambacho hakina haja na kitu kingine chochote isipokuwa chenyewe tu. Kuhitaji na kutegemea, kwa hiyo, huvizingia viumbe vyote.
Akili na fikara ya mwanadamu vinaweza kuvuka mapazia ya muonekano wa nje, tofauti na hisia zake, na kupenya vina na kadiri za ndani zaidi za kiumbe; vitu hivyo haviwezi kukubali kwamba uhai lazima uwekewe mipaka kwenye viumbe vyenye uhusiano, kikomo, mabadiliko na utegemezi. Kinyume chake, uwezo wa kufikiri kwa dhahiri hutambua umuhimu wa kuwepo, nje ya uwezekano wa kuchunguzika, ukweli thabiti, usiopingika na wenye kujitosheleza ambao juu yake viumbe vingine vinatumainia na kutegemea. Ukweli huu upo wakati wote na mahali popote, endapo haungekuwepo, ukamilifu wa dunia ungekoma kuwepo na ungepoteza ulingano wote wa uhai.
Mara tunapoona utegemezi wa dunia iliyoumbwa na kutambua kwamba hakuna kitu kinachoweza kuwepo bila ya kusaidiwa, tunahitimisha kwamba kuna "Kilichopo kwa Lazima," kwani tunalazimika kuhoji, "ni juu ya kitu gani ambacho kila kiumbe hatimae hutegemea?" Endepo tutajibu, "Hutegemea kiumbe kingine," halafu lazima tuulize, "kiumbe hicho na chenyewe hutegemea nini?" endapo basi jibu litatolewa "Hutegemea kitu ambacho sisi hatujui asili yake," swali linajitokeza, "Je kitu hicho ni cha peke au changamani?"
Kama jibu litakuwa "changamani" halafu tunajibu kwamba changamani pia ni tegemezi juu ya sehemu zake, kwani kwanza kabisa hizo sehemu lazima ziwepo ilihiyo changamani itokee kuwepo. Kwa kuwa maumbile ni changamani, hayawezi kuwa ndiyo 'Kilichopo kwa Lazima.' Kwa hiyo, tunalazimika kusema kwamba kisababisho cha kwanza lazima kiwe peke. Pia lazima kiwe ndani ya mpaka au maana moja na kile 'Kilichopo kwa Lazima,' kwani mlolongo wa kisababisho hauwezi kuendelea bila mpaka.
Ujumla wa dunia, kwa hiyo, unahitaji ukweli ambao unajitegemea na ambao humo ndimo vitu vyote vyenye masharti, ukomo na uhusiano vinamotegemea. Vitu vyote vinauhitaji ukweli huo ili kuvijaza uhai, na viumbe vyote vyenye uhai vinakuwa na dalili ya uhai wake wa milele, ujuzi, uwezo na hekima. Kwa hiyo, vinaturuhusu sisi kupata ujuzi wenye manufaa kuhusu ukweli huo na kumwezesha kila mtu aliye na akili, mdadisi kufasiri kuwepo kwa Muumbaji.
Kutegemeana kwa pande mbili kwa maada na kanuni za uhai kwa namna yoyote ile hakuelekezi kwenye kujitegemea kwa vitu vya kimaada. Kinyume chake, mambo tofauti yanayotokea kwenye maada, pamoja na uhusiano wao wa karibu, yanaonesha kwamba maada, katika namna yake ya maisha, hulazimika kukubali na kufuata kanuni fulani na desturi ambazo huyasukuma kwenye utaratibu na uelewano. Uhai unategemea juu ya vipengele viwili muhimu. Maada na utaratibu, ambavyo vinahusiana kwa karibu sana na huzaa dunia inayoeleweka na yenye utulivu. Baadhi ya watu huchukulia maada kama yenye kujitegemea na hudhania kwamba yenyewe imepata uhuru huu na kufafanua zile kanuni ambazo zinaitawala. Lakini ni vipi wanaweza kuamini kwamba haidrojeni na oksijeni, elektroni na protoni, zipaswe kwanza kujizalisha zenyewe, halafu ziwe chanzo cha viumbe vingine vyote, na hatimaye kuamuru kanuni zinazojirekebisha zenyewe na ulimwengu wote wa maada?
Uyakinifu unadhania kwamba vitu duni ndio chanzo cha kutokeza vitu vya hali ya juu bila ya kusumbuka kuhakikisha kama kile kitu cha hali ya juu kwa kweli, kinakuwepo katika kiwango cha kile duni. Kama mata ya kiwango duni haiwezi - hata katika kiwango cha juu sana cha maendeleo yake yaani fikra na tafakuri - ama kujiumba yenyewe au kukiuka mojawapo ya kanuni ambazo hutawalia juu yake, kwa hiyo ina maana isiopingika kwamba haiwezi kuumba viumbe vingine na kanuni zinazovirekebisha. Ni vipi, basi inaweza kuaminika kwamba mata duni ingejishughulisha katika uumbaji na uanzishaji wa viumbe vya hali ya kiwango cha juu au kuwa na uwezo wa kutoa uhai kwa vitu vya juu sana? Katika sayansi mpya ya mifumo, kanuni imethibitisha kwamba mifumo yenye elementi zenye uhai ambazo zina lengo au mifumo iliyopangika kwa nje kwa msingi wa programu iliyowekwa, zinaweza kuendelea kwenye mwelekeo wa kupanuka, utaratibu mkubwa zaidi na uboreshaji. Hata hivyo, mifumo yote, ama ya peke au changamani, inahitaji kusaidiwa na, na kuhusishwa na vipengele vya nje yao yenyewe, haziwezi kujijenga zenyewe. Hakuna mfumo au kitu humu duniani kitakachoweza kuumba au kutia utashi kwenye kiungo kinachotembea na kukua isipokuwa kiwe kina kiwango fulani cha dhamira na ufahamu.
Yakiwa yametegemezwa kwenye kanuni ya uwezekano, matokeo ya hamasa huru ya fani zote yanaweza kuwa tu ya mtawanyiko na vurugu, yakielekea kwenye kifo cha namna moja. Kanuni ya uwezekeano pia inakanusha wazi wazi kutokea kwa dunia kwa njia ya kubahatisha, na kuiona kuwa haina mantiki na haiwezekani. Hata makadirio yaliyofanywa kwa msingi wa kanuni ya kimahesabu ya uwezekano yanathibitisha umuhimu wa mwongozo ulio sahihi na upangaji kwa ajili ya dunia, kwa kukubaliana na programu iliyo sahihi na dhamira ya fahamu.
Kwa kweli kanuni ya uwezekano inatoa pigo la uhakika kwa wale wanaoamini nadharia ya kutokea kwa dunia kwa bahati. Endapo tutajaribu kutumia nadharia ua ajali kwenye mfumo wa kawaida au tarakimu ndogo, utumikaji wake ni wenye kuwezekana, ingawaje hauelekei kabisa. Lakini haieleweki kwamba mtu aweze kubahatisha kamwe kwa njia ya ajali ya kijometri kuelezea mpangilio imara na wenye utulivu uliopo kwenye mfumo changamani wa dunia. Mabadiliko ya kiasi na ya kawaida kwenye mpangilio wa maisha pia hayawezi kuuelezea mgeuko wa dunia; muungano wa elementu zilizo tofauti, na mchanganyiko wa chembechembe za asili kuunda mchanganyiko unaowiana.
Ikiwa kama wakati fulani maumbile yalijishughulisha kwa kujitawala katika kazi za sanaa na utengenezaji, kwa nini sasa hayaonyeshi hatua yoyote katika mwelekeo wa kujibadilisha yenyewe zaidi ya hapo; kwa nini hayaonyeshi tena mabadiliko makubwa yanayojiendesha yenyewe? Hata matukio madogo na ya kawaida hapa duniani husababishia uumbikaji wa sura za kipekee ambazo zinawiana na kuafikiana na lengo la maumMwenyezi bile.
Hii peke yake, yenyewe ni dalili ya ule ukweli kwamba nyuma ya mabadiliko yote makubwa, kuna nguvu makini na yenye uwezo mkubwa inayojishughulisha katika kuumba na kuzalisha mpangilio wa maajabu ya ulimwengu: inatoa umbo kwenye udhahiri wa kipekee wa dunia ya maumbile na kuashiria mpango na utaratibu wa uhai.
Uwiano na upatanishikaji wa mamilioni ya vitu vya maumbile na uhusiano wao kwenye uhai unaweza kuelezwa juu ya msingi wa nadharia moja tu - yaani kwamba tunamtambua kuwepo kwa Muumbaji juu ya mfumo huu mpana Ambaye ameasisi chembe zinazotofautiana za uhai juu ya duniani hii kwa njia ya uwezo usio na mipaka na ukomo na kutayarisha programu kwa ajili ya kila mojawapo ya chembechembe hizo za uhai. Nadhari hii ni kwa kulingana na uhusiano mtulivu ambao tunaouona umewekwa ndani ya viumbe.
Kama hatutakubaliana na nadharia hii, upo uwezekano gani kwamba utulivu wa aina hii ungetokea - ki-ajali na bila madhumuni - miongoni mwa taratibu nyingi za uhai? Ingeaminikaje kwamba mata yenyewe iwe chanzo cha mamilioni ya sifa na tabia na kwa hiyo kuwa inayolingana na Muumbaji mwenye madhumuni, hekima na mjuzi wa yote? Endapo dunia ya uhai isingekuwepo, pamoja na maajabu yake ambayo yanastaajabisha akili na uzuri ambao ujuzi wa mwanadamu hauwezi kufahamu kikamilifu, na endapo ulimwengu ungekuwa na kiumbe cha seli moja tu hai, bado uwezekano kwamba kitu kidogo na kisichokuwana thamani, pamoja na mpangilio uliopo juu yake na hali ya lazima na vifaa kingekuja kuwepo kama bahati tu, uwezekano, ajali, uwezekano kama huo unaashira, tarakimu ndogo sana ambayo haiwezi kueleweka kimahesabu, kwa mujibu wa bingwa wa baiolojia Mswisi aitwaye Charles Unguy.
Chembe zote za viumbe hai, katika maumbo yao ya ndani na uhusiano wao, zinategemea mpangilio ulioimarika. Kujengeka kwao na uhusuano uliopo baina yao ni wa namna ambayo husaidiana zenyewe ili ziendelee kwenye njia zao husika hadi kwenye malengo yaliyoko mbele yao. Zikinufaika kutokana na uhusiano zilionao kwa viumbe vingine hai na kutokana na kuambukizana athari kwao kama livyodhamiriwa na uundwaji wao wenyewe, zina uwezo wa kuelekea kwenye malengo na mwisho wa safari yao.
Mafanikio makubwa ya sayansi ya maada ni kutambua sura na sifa za nje za dunia; kutambua asili na mumbile hailsi ya viumbe vilivyoumbwa na matukio kupo nje ya upeo wa uelewa wa sayansi hizo. Mathalani, mafanikio makubwa sana ambayo mnajimu anaweza kupata, ni kujua kama mabilioni ya matufe kule angani hayabadiliki wa kusogea kwa sababu ya kani-pewa au kama yanaendelea kubiringika ambapo nguvu ya uvutano huyazuia yasigongane na kudumisha utulivu wao. Inaweza pia kupima umbali wao kutoka hapa ardhini na kasi ya mwendo wao na ukubwa kwa njia ya zana za kisayansi. Hata hivyo, hatima ya matokeo ya ujuzi huu wote na majaribio hayavuki upeo wa tafsiri ya nje na ya juujuu ya vipengele vya maumbile, kwani mnajimu (bingwa wa elimu ya anga) hawezi kutambua asili halisi ya nguvu ya mvutano, chimbuko la kani-pewa au namna ya jinsi zilivyo na ule mfumo ambao zinauatumikia vilivyojitokeza kuwepo.
Wanasayansi wanaweza kutafsiri mashine bila kutambua tafsiri ya hiyo nguvu mwendo. Sayansi asilia vivyo hivyo hazina uwezo wa kutafsiri na kuchanganua mamilioni ya mambo ya ukweli ambayo yamewekwa katika maumbile na ndani ya mwanadamu. Mwanadamu amechimba kwenye kiini cha chembe lakini ameshindwa kupata ufumbuzi wa miujiza migumu na iliofichika ya chembe hai moja. Kwa ufupi, ni ngome hizi za miujiza ambazo mabingwa wa sayansi asilia wamekuwa hawana uwezo wa kuzishinda.
Mojawapo ya maajabu ya maumbile ni ule uwiano wa maafikiano uliopo baina ya vitu viwili ambavyo sio vya wakati mmoja. Ulinganifu huu ni wa hali ambayo kwamba mahitaji ya kitu ambacho bado hakijatokeza na kuwepo, tayari yameandaliwa kwenye umbile la kitu kingine. Mfano mzuri wa aina hii ya uwiano unaweza kuonekana kwenye uhusiano baina ya mama na mwana. Miongoni mwa binadamu na mamalia wengine, mara mwanamke anapobeba mimba na jinsi kilenge kinavyokua ndani ya nyumba ya uzazi, tezi ambazo hutengeneza maziwa - aina nzuri na changamani ya lishe - huanza kufanya kazi kwa mvuto wa homoni maalumu. Jinsi kilenge kinavyoendelea kukua, ndivyo lishe hii yenye virutubisho inavyoongezeka wingi wake ili kwamba pindi kilenge kinapokuwa kwenye mlango wa kizazi na kipo tayari kuingia katika dunia hii pana isiyo na mipaka, kirutubisho hiki kinachohitajiwa na mtoto na kinachofaa kwa mahitaji yake yote ya kimwili kinakuwa kipo tayari.
Kirutubisho hiki kilichokwishatengenezwa tayari, kimepatanishwa kabisa na mfumo ambao bado mchanga, wa kusaga chakula wa mtoto. Kimehifadhiwa kwenye ghala iliyofichika - titi la mama, ghala ambayo alipewa mama miaka mingi kabla kichanga hakijapata umbo. Ili kuwezesha ulishaji wa mtoto alliyezaliwa mara, vijitundu vidogo na laini vimewekwa kwenye chuchu za titi lenyewe - kwa kipimo kinacholingana na mdomo wa mtoto - ili maziwa yasitiririke moja kwa moja kwenye mdomo wa mtoto ambaye kwa wakati huo hana uwezo wa kuyameza mwenyewe. Badala yake mtoto anayapata riziki ya kila siku anayoihitaji kutoka kwenye hazina hiyo kwa njia ya kunyonya.
Jinsi mtoto aliyezaliwa anavyozidi kukua, ndivyo mabadiliko yanavyofanyika kwenye maziwa ambayo yanaunganishwa na umri wake. Ni kwa sababu hii kwamba madaktari wa tiba wanaamini kwamba kunyonyeshwa mtoto mchanga aliyezaliwa punde na mama mwingine ambaye siye aliyemzaa, wakati mwingine si jambo la busara kushauriwa. Hapa swali linajitokeza; si kweli kwamba mahitaji ya kiumbe kutengenezwa kwenye umbile la kiumbe kimoja, kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kiumbe kingine ambacho bado hakipo, ni jambo ambalo kimepangwa na kutabiriwa kwa msingi wa hekima na usahihi? Je, sio kwamba matayarisho haya kwa ajili ya siku zijazo, uhusiano huu wa kistadi na wa kushangaza baina ya viumbe viwili, ni kazi ya nguvu yenye uwezo na hekima isiyo na mfano? Si kwamba hii ni dalili ya wazi ya kuingilia kati kwa nguvu isiyo na kikomo, mbunifu na mpangaji mkuu, ambaye makusudio yake ni kuendeleza uhai na kukua kwa vitu vyote kuelekea kwenye ukamilifu? Tunatambua vizuri kwamba mahesabu sahihi tunayoyaona kwenye misingi ya mashine zote na zana za viwandani ni matokeo ya vipaji na fikra zilizoingizwa kwenye usanifu na utengenezwaji wao. Vivyo hivyo, kwa kutegemea uchunguzi wetu wa busara tunaweza kufikia uamuzi wa jumla wa kifalsafa kwamba popote pale ambapo mpangilio na ukusanyaji unaotegemea uwiano na makadirio unapotakiwa kufuatwa, dhamira, akili na mawazo lazima pia vitafutwe.
Usahihi huo huo ambao unaweza kuonekana kwenye mashine za viwandani ndio utakaoonekana katika kiwango cha juu zaidi na kipekee katika viumbe asili na uumbwaji wao. Hakika kiwango cha maandalizi na mpangilio unaoonekana kwenye maumbile upo katika daraja ya juu sana hivyo kwamba usahihi alioumaliza mwanadamu katika ubunifu wake hauwezi kwa hali yoyote ile kulinganishwa nacho. Wakati bila kusita, tunapotambua kwamba utaratibu wetu wa viwanda ni matokeo ya fikira na mawazo, hatupaswi sisi kuutambua utendaji wa akili isiyo na kikomo, dhamira na ujuzi uliopo kwenye mpango sahihi wa maumbile?
Katika zama hizi, elimu ya madawa imefika katika kiwango cha maendeleo ambacho kinakiruhusu kuondoa figo kutoka kwenye mwili wa binadamu na kuipandikiza kwenye mwili wa mtu ambaye figo zake zimekwama kufanya kazi na ambaye anakaribia kufa. Maendeleo haya kwa uhakika si matokeo ya juhudi ya daktari moja pekee; hii inatokana na urithi wa milenia kadhaa. Shughuli ya upandikizaji sasa ndio hatua ya mwisho katika mlolongo mrefu ambao hatua zake za mwanzo zilikamilishwa na wanasayansi wa siku za mwanzo; mawazo na utambuzi wa wanasayansi yalikuwa yakusanywe kwa miaka elfu kadhaa kabla ya kupandikiza figo kuweza kutokea.
Je, inawezekana kwamba matokeo haya yaweze kupatikana bila ujuzi? Bila shaka hapana: akili za binadamu uwezo mkubwa zililazimika kufanya kazi kwa miaka elfu kadhaa ili upandikizaji wa figo upate kuwezekana. Sasa na tuulize swali jingine. Ni lipi linahitaji ujuzi mwingi na akili zaidi: ni kubadilisha tairi kwenye gurudumu la gari - kazi ambayo inahitaji kiasi fulani cha ufundi stadi - au utengenezaji wa tairi lenyewe? Kazi ipi iliyo ya umuhumu: kutengeneza tairi au kubadilisha tairi? Ingawaje kupandikiza figo ni kazi muhimu katika tiba, inafanana na kubadilisha tairi kwenye gurudumu la motokaa; kazi hii inakosa umuhimu ikilinganishwa na ile ya kutengeneza umbo la figo yenyewe na ile miujiza, ustadi na mahesabu iliyonayo.
Mwanasayansi gani halisi, aliyetawaliwa na uaminifu katika kutafuta ukweli anayeweza kudai leo hii kwamba, wakati ambapo upandikizaji wa figo ni matokeo ya mfululizo wa utafiti wa majaribio ya kisayansi ya karne nyingi, umbo la figo yenyewe halioneshi dalili ya akili bunifu na dhamira, kuwa ni matokeo ya maumbile tu - maumbile yasiyo na ujuzi zaidi au utambuzi kuzidi mwanafunzi wa shule ya chekechea?
Haitakuwa na mantiki zaidi kuweka nadharia ya kuwepo kwa akili, dhamira na maandalizi katika uumbaji na utaratibu wa ulimwengu kuliko kuhusisha uumbaji kwenye mata kitu ambacho hakina akili, mawazo, umakini na uwezo wa kuanzisha mambo mapya? Imani juu ya kuwepo kwa muumbaji mwenye hekima bila shaka ina mantiki zaidi kuliko kuamini katika ubunifu wa mata, kitu kisichokuwa na ama utambuzi, umakini wala uwezo wa kupanga, hatuwezi kuzihusisha kwamba zitokane kwenye maada, tabia na sifa zote za akili tuzionazo hapa duniani na utashi wa mpangilio inaouonyesha.
Mufadhal alimwambia Imam Sadiq
: "Bwana! baadhi ya watu hudhani kwamba huu utaratibu na usahihi tuuonao hapa duniani ni kazi ya maumbile." Imamu akamjibu:"Waulize kama maumbile hufanya kazi zake zote zilizokadiriwa kwa usahihi kwa mujibu wa elimu, mawazo na uwezo wake yenyewe. Kama watasema kwamba maumbile yana elimu na uwezo, kuna kitu gani kinachozuia wao kupinga lile chimbuko la milele la ki-ungu na wakakiri kuwepo kwa hiyo kanuni kuu? Endapo kwa upande mwingine watasema kwamba maumbile hufanya kazi zake kwa kawaida na kwa usahihi bila matumizi ya ujuzi na utashi basi kinachofuata ni kwamba shughuli zote za hekima na zilizo sahihi, sheria zilizopangwa vizuri ni kazi ya muumbaji mjuzi na mwenye hekima. Kile ambacho wao wanakiita maumbile, kwa kweli, ni sheria na kawaida zilizowekwa na mkono wa uwezo wa ki-mungu ili zitawale maumbile."
Ustadi wa maumbile.
Mfikirie mbu wa malaria. Hakuna haja ya kutumia darubini; unaweza kutambua mpangilio sahihi na changamano uliomo kwenye kiumbe kile kisicho na thamani kwa matumizi ya kawaida ya jicho tupu. Ndani ya kiumbe hiki dhaifu mnakuwemo na seti kamili ya viungo na milango ya fahamu, ya kipekee kwa usahihi wao: mfumo wa kusaga chakula tumboni, mfumo wa mzunguko wa damu, mfumo wa neva, mfumo wa kupumua. Mbu anayo maabara iliyoandaliwa kwa vifaa: kwa usahihi na kasi ya ajabu, itengeneza vitu vyote anavyovihitaji. Mlinganishe mbu na maabara ya kisayansi: pamoja na nguvu zote za kibinadamu na kiuchumi zilizomwagwa juu yake, maabara hiyo haiwezi kamwe kupata kasi, umakini na usahihi wa maabara inayodharaulika ya mbu. Ni muda kiasi gani, tafakuri na akili vinavyohitajika, kwa mfano, kutengeneza tiba kwa ajili ya ule uumaji wa mbu tu!
Wakati ambapo upangaji mwingi, mawazo na usahihi vinahitajika kwa mtu kufanya kazi kama hii, hivi huu ustadi, usahihi na utaratibu unaoonekana duniani, sio uthibitisho wa chimbuko linalotokana na akili, maandalizi bunifu na busara ya kiwango cha juu ya huyo muumbaji? Hivi inawezekana hata kidogo kufikiria jometri yote sahihi, utendaji wa mwendo wa ulimwengu kuwa ni matokeo ya mata, na kukosa elimu kwake? Tunatamka kwa dhati kabisa kwamba jambo la maumbile linaonyesha mpangilio na utaratibu; haya hayatangazi kutokuwa na lengo, vurugu na machafuko.
Endapo nyakati fulani tunaona dalili za dosari katika maumbile hii haina maana ya kuwepo kwa upungufu au kasoro kwenye kitabu kikubwa cha uumbaji. Fikira na utambuzi wetu haviwezi kupaa na kuruka angani na uwezo wa akili zetu ni mfupi mno kuweza kuelewa miujiza na vitendawili vyote vya ulimwengu. Akili zetu haziwezi kuvumbua azma na malengo yote ya uhai. Kama hatuwezi kuelewa kazi ya skrubu ndogo kwenye mashine kubwa, sasa basi, hali hii inatupatia sisi haki ya kumshutumu na kumlaani mbunifu kwamba ni mbumbumbu? Au ni kwamba upeo wetu wa kukodoa macho ni mfinyu mno kuweza kuelewa lengo na madhumuni halisi ya mashine hiyo?
Bahatisho haliwezi kufanya kazi ya elimu, elimu, ambayo zaidi ya hayo, haikuchanganyika na ujinga kwa hali yoyote ile. Ikiwa, kama wayakinifu wanavyodhani, dunia ya maumbile haikutokana na elimu na utashi (licha ya dalili za uumbaji na ubunifu unaoonekana wazi katika kila kiumbe) halafu, mwanadamu pia ili aweze kufanikisha malengo yake atalazimika kuacha maendeleo yake kwenye mkondo wa elimu na kujifunga mwenyewe kwenye ujinga ili aweze kutenda kufuatana na kule kutokujitambua kwa maumbile yenyewe. Ile hali halisi inayoongoza na kuelekeza utendaji wa dunia kwa utaratibu na mpangilio wa namna hiyo una lengo, madhumuni na dhamira, mambo ambayo hayawezi kukanushwa. Haiwezi kudhaniwa kwamba mlolongo wa utendaji usiokatika na athari zake huendelea kuelekea upande maalum bila uingiliaji na uangalizi wa akili fulani.
Baada ya miaka mingi ya maandalizi yaliyofanywa kwa uangalifu na kazi ya kuchosha mabingwa wa sayansi ya biokemia wamefaulu katika kugundua mfumo fulani wa majaribio katika kiwango cha kawaida na cha chini ambao kutoka humo dalili zote za uhai zinakosekana. Ushindi huu wa kisayansi ulionekana kuwa na manufaa sana na ulipokelewa kwa shauku kubwa katika duru za kisayansi, na hakuna mtu aliyedai kwamba uumbaji huu wa maabara wenye upungufu mkubwa na wa kiwango cha chini sana uliotokeza kuwepo kama matokeo ya bahati, bila ya mwelekeo, maandalizi na usahihi.
Hali ikiwa ni hivi, wale wanaohusisha viumbe vyote viliyomo kwenye mfumo mpana wa ulimwengu, pamoja na sifa zake changamani na za kimwujiza kwenye nguvu povu na zisizo na fahamu za mata, kwa kweli wanaifanyia vurugu na udhalimu mantiki na akili ya binadamu na kuendesha vita vya wazi dhidi ya ukweli. Weka mazingatio yako kwa dakika moja tu juu ya mtayarishaji wa chapa kwenye kiwanda cha uchapishaji. Yeye anachukua hadhari na uangalifu mkubwa anapozipanga herufi zinazotakiwa kwa ajili ya ukurasa mmoja wa kitabu, lakini anapoirudia kazi yake, anakutana na makosa madogo madogo yatokanayo na kukosa umakini kidogo tu. Mtayarishaji wa chapa angekuwa achukue herufi chache kiganjani na kuzisambaza kwenye bamba badala ya kuzipanga kwa uangalifu katika mistari, je, itawezekana kwa vyovyote vile kwamba ukurasa utakaotokea uweze kuwa sahihi katika maudhui na kutokuwa na kosa lolote?
Itakuwa bado ni upumbavu zaidi kudai kwamba kila mia moja za risasi iliyoyeyushwa, ikashindiliwa kwenye tyubu, itatokeza katika hali ya herufi ambazo zimetengenezwa tayari; na kwamba dhoruba kali iweze kuzichukua herufi hizo na kuzipanga kwenye mpangilio na utaratibu maalum unaokubalika, kwenye maelfu ya mabamba ya chuma, na kwamba mabamba haya yaishie kwenye kuchapishwa kitabu chenye kurasa elfu moja chenye maudhui nyingi sahihi za kisayansi na maelezo ya kuvutia na kushawishi, yote haya yafanyike bila hata kosa dogo kutokea. Kuna mtu yoyote anayeweza kuiunga mkono nadharia hii?
Wayakinifu ambao hukanusha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu wana nini cha kusema kuhusu kutokeza kwa maumbo tofauti ya herufi za maumbile na uhusiano ulio sahihi na changamani ambao hudhibiti viumbe vya mbinguni, maumbile asilia na vitu vyote vya kimaada? Je, herufi za maumbile (yaani atomu na chembechembe zinazoziunda) zinaweza kuwa hazina maana kuliko herufi zitumikazo katika uchapishaji? Inawezekana kukubalika kwa namna yoyote ile kwamba hizi herufi zenye mpangilio na maana, jometri hii iliyo sahihi na iliyoandaliwa vizuri maumbo ya kushangaza yanayofafanuliwa kwenye kitabu cha uumbaji, iwe ni kazi ya kijinga na isiyo na malengo? Kwamba nguvu kuu na yenye hekima, kanuni ya mpangilio ya kimwujiza, isiwepo kwenye muonekano wenyewe wa dunia? Je, mambo yote sio kwamba yanachipukia kutokana kudhihiri kwa ufahamu, utambuzi na uwezo?
Endapo uwezo uliofichika kwenye vina vya mata hautokani na akili ya fani zote, ni jambo gani linauongozo kwenye ufafanuzi wa maumbile, kwenye utaratibu na uwiano wa kushangaza? Ikiwa uwezo huo ni wakala asiye na akili na fahamu, kwa nini basi haujaangukia kamwe kwenye vurugu, na kwa nini mchanganyiko wake wa mata kamwe hausababishi mgongano na maangamizi? Hapa ndipo ambapo imani ya kuwepo kwa muumbaji inaleta maana juu ya maada yote na hujaalia dunia kuwa na maana na kutosheka. Wale wenye mtazamo wa mbali na fikra safi za wazi hutambua dhahiri kwamba uwezo usio na ukomo ndio unaohakikisha utunzaji wa mpangilio wa dunia kwa njia ya usimamizi ulio madhubuti na mamlaka kamili.
Zamani, kila mtu alikuwa akimwongoza na kumdhibiti mnyama wake wa kipando, na vile vile alikuwa na desturi, katika zama zote, ya kumuona mmiliki au msimamizi anayesimamia sehemu ya rasilimali, kila kipande cha ardhi isiyotumika, kila kundi au chama. Sasa mambo yamebadilika. Mwanadamu wa kisasa anaweza kutengeneza setilaiti inayoendeshwa toka mbali, ala za elektroni na ndege zisizo na rubani, vyote hivi vikiwa vimetayarishwa kwa vifaa vinavyojiendesha vyenyewe. Kila mtu anajua kwamba inawezekana kutengeneza mashine yenye vifaa vyote ambayo inaweza kufanya kazi kwa namna nyingi zinazofaa kwenye hali yoyote itakayojitokeza, bila mtengenezaji wa chombo hicho kuwepo au kuonekana. Kwa hiyo, hatuna tena haki ya kukataa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa ukaidi tu kwa sababu mkono Wake hauonekani haufanyi kazi kwa kuonekana katika mambo ya uumbaji - kwa kuonekana, yaani kwa uelewa na elimu yetu yenye upungufu.
Kwa kweli, ungekuwa ni ufananishaji wenye upungufu mkubwa endapo tungemlinganisha mtengenezaji setilaiti au roketi bandia, ambaye ameketi kwenye kituo chenye vifaa vyote hapa ardhini na kwa msaada wa vifaa changamani anaongoza na kudhibiti njia na mwendo wa chombo cha angani. Lakini kama uingiliaji kati wa mkono wa Mwenyezi Mungu kwenye mpangilio wa maumbile hauonekani kwa jicho letu la kawaida na utambuzi wetu (ingawaje tunaweza kuona dalili na ishara ambazo zinafanana na mwale unaoendelea kutoka kwenye fahari ya utukufu wake) tunaweza kwa sababu hiyo kutotilia maanani kuwepo kwa mpangaji na mwendeshaji ambaye peke yake ndiye elimu ya dhati, uwezo na utashi halisi, kwa sababu tu kwamba hawezi kudhibitiwa ndani ya mfumo finyu wa muda na nafasi.
Ni kweli kwamba uwezo wetu wa kuelewa nafsi ambayo haifanani wala haina mfano na chochote katika himaya ya hisia na ambayo lugha ya kibinadamu haiwezi kuieleza kikamilifu na kwa usahihi ni mfinyu sana. Taa ya akili zetu hutoa mwanga mdogo kwenye uwanda huu usio na ukomo, au - kwa lugha nyingine tofauti - unakabiliana na kuta za mipaka. Wakati huo huo uhusiano wetu katika dunia hii upo juu ya matukio; lile ambalo litajiingiza lenyewe kwenye akili zetu linakuwa na miali ambayo hugunduliwa na kaida za dunia yenye busara. Lakini katika kuitambua dunia hiyo, tatizo la kuidhania linaondolewa kwetu; hakuna kipingamizi kilichopo baina ya fikira zetu na kile kiasi muhimu cha ufahamu.
Hata hivyo, watu fulani wenye kushuku ambao wameutelekeza mtindo thabiti wa fikra ambao unatokana na asili ya msingi ya mwanadamu na ambao wamekuwa, kimipaka kabisa, na mazoea ya uhai wenyewe hasa wa maumbile wakati wote wakingojea kutokea muujiza kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambao utavunja utaratibu uliopo wa muumbo ili kufanya zawadi kwao ya itikadi na imani, na kufanya kuwepo Kwake (Mwenyezi Mungu) kueleweka na kukubalika bila kusita. Hata hivyo, watu hao hawatilii maanani kwamba dalili na ishara zozote mpya za Mwenyezi Mungu zinazoweza kutokea zitasababisha msisimko mashaka ya muda tu, na kwa kupita muda, yatakuwa mambo ya 'kawaida' na hayatavuta nadhari tena.
Ingawa mambo yote sasa yamejumuishwa kwenye muundo wa mpangilio wa maumbile, yalianza kwa kuvunja mpango wa asilia, na kwa kuwa viumbe vyote vimerudiwa katika hatua za dunia tangu kudhihiri kwa mara ya kwanza, sasa vinaonekana kuwa vya kawaida na kuzoeleka. Kinyume chake, kiumbe kisichoweza kutambulika kihisia - kiumbe, ambacho zaidi ya hayo kimejaa fahari na utukufu na kilichojaa utakatifu na ukuu - kila mara kitavutia roho za wanadamu. Mazingatio yao kwa kiumbe kama hicho, kwa kweli kila wakati utaongezeka na wakati wote watakiangalia kwa kuhitajia.
Ni kutawaliwa na nafsi ya ukaidi, ya uamuzi uliotengenezwa kwenye mantiki isiyopatana, ambayo huifungia fikira ya kibinadamu kwa mipaka. Kwa kila kiumbe katika mpangilio wa kuwepo ni uthibitisho unaotosha kwa ajili ya wale wanaobana na kuweka tupu akili zao za ukaidi na sababu za ukanushaji.