6
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
SOMO LA SITA
HAJA YA ULIMWENGU KUMHITAJI YULE ASIYEHITAJI CHOCHOTE
Kanuni ya usababisho ni ya kawaida na fani zote na msingi wa juhudi zote za mwanadamu, katika kutafuta elimu na katika shughuli zake za kawaida vilevile. Jitihada za wanazuoni kuvumbua sababu za kila jambo, ama liwe la kimaumbile au la kijamii, hutokana na imani kwamba hakuna kitu kinachojianzisha ndani yake, au chenyewe tu bila sababu na asili kuingilia kati.
Utafiti wa wanafikra duniani pote umewapa wao uwezo wa kufahamu vizuri zaidi mpangilio wenye nguvu sana wa maumbile; jinsi wanavyozidi kusonga mbele kwenye mkondo wa maarifa ndivyo wanavyozidi kujifunga kwenye kanuni ya usababisho. Kiungo baina ya sababu na athari, na kanuni kwamba hakuna kitu kitakachotokea chenyewe kwenye uwanja wa uwepo bila sababu, ni miongoni mwa maamuzi yenye nguvu sana ambayo yamepata kufanywa na mwanadamu na kuthaminiwa kama sharti la kimsingi kwa shughuli za kitaalamu. Yanawakilisha kitu ambacho ni kawaida na cha asili, kinachofyonzwa na akili zetu moja kwa moja bila kukwepa.
Hata mwanadamu aliyeishi kabla ya historia kuanza kuandikwa alielekea kugundua sababu za mambo, na kwa kweli, wanafalsafa waliipata dhana hai ya uhusiaino kati ya sababu na athari kutoka kwenye asili yenyewe na silika ya mwanadamu kabla ya kuiweka katika kalibu (chungu) ya kifalsafa. Kufungiwa kama tulivyo kwenye kuta nne mata, hatukabiliani kamwe na kitu chochote cha kutuka chenyewe kwenye uhai, na kwa kweli, hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kamwe kukabiliana, katika historia ya ulimwengu, na kutuka kwa jambo ambalo halitokani na sababu. Kama hali isingekuwa hivyo, tungeweza labda kuwa kisingizio cha kuufikiria ulimwengu kuwa ni kitu cha kutuka chenyewe katika asili yake. Itakuwa ni aina gani ya kutuka kiajali ambako tangu mwanzo wa kuwepo kwa uhai hadi sasa, kumeongoza muingilano huo usiopimika wa vitu vyote, katika mfumo na mtindo wa kushangaza kiasi hicho? Je, inawezekana mpangilio huu tunaoufahamu ukawa ni kuakisi kwa jambo la kutuka na sadifa ya hivi hivi tu?
Kitu chochote kinachoweza kudhaniwa hapa ulimwenguni kilikuwa kimezamishwa kwenye giza la kutokuwepo kabla hakijapata umbile la kiumbe. Hakiwezi kupenya giza la kutokuwepo na kujitokeza kwenye uwanja wa uhai kama kitu kilichopo hadi mkono wa kisababisho wenye uwezo mkubwa uingie kazini.
Uhusianao baina ya chanzo na athari ni uhusiano baina ya vitu viwili vilivyopo, kwa maana kwamba kuwepo kwa kimoja chao kunategemea juu ya kuwepo kwa kile kingine. Kila athari ina uhusiano wa mvuto na uwiano na chanzo chake, kwa kuwa athari hupata kuwepo kwake kutoka kwenye chanzo. Uhusiano huu maalum hauwezi kuharibiwa au kubadilishwa na mwingine.
Wakati wowote unapofikiria asili ya kitu chenye uhusiano wenye kufanana kwa kiumbe hai na kisichokuwa hai, na vyote vikiwa hakuna ambacho ni muhimu kimsingi kwa ajili ya kitu hicho, kitu hicho huitwa 'dharura' kwa maana kwamba hakuna chochote katika asili yake kinachosababisha ama uhai au kutokuwa hai. Kama kitu katika asili yake kinahitaji kutokuwa hai kwake, basi kuwa hai kwake hakuwezekani. Hatimaye, endapo uhai utajitokeza kutoka ndani ya asili ya kitu kwa namna ambayo kwamba akili haiwezi kukiona kwamba ni tegemezi kwa kitu kingine chochote, uhai wa kitu hicho unafanywa kuwa muhimu. Ni kiumbe hai kinachojitegemea, kisichohitaji chochote na kinajikimu kwa njia za asili yake binafsi, kuwepo kwake ndicho chanzo cha viumbe vingine vyote ambapo chenyewe hakitawaliwi na haja au hali yoyote.
Inapaswa kuongezwa hapa kwamba kuwepo kwa maada hakuwezi kupata sifa ya "muhimu" kwa sababu kuwepo kwa kitu chochote cha mchanganyiko wa maada kunategemea kuwepo kwa sehemu zinazokiunda kitu hicho; kinakuwa ni tegemezi juu ya sehemu zake chenyewe kwa ajili ya chanzo na kuendelea kwa uhai wake. Mata ina mielekeo tofauti na ukubwa mbalimbali; yenyewe imetumbukizwa kwenye kiasi na kuongezeka, na inapata ukubwa wake mbali mbali kwa namna ya sifa na tabia. Kiumbe muhimu, kwa kinyume chake, hakihitajii tabia zote hizi.
Vitu vyote ambavyo wakati fulani havikuwepo halafu vikajakuwepo, wakati mmoja vilitawaliwa na dhana ya kufikirika ya uhai na kutokuwa hai. P ale vilipokimbilia kwenye hatua ya uhai, hii ilikuwa ni matokeo ya chanzo ambacho kilivilazimisha mwelekeo huo, kilikuwa ni kichocheo, kipengele cha nje ambacho kilivisukuma vyote kwenye mwelekeo mmoja badala ya ule mwingine. Kwa mneno mengine, kuwepo kwa chanzo ilikuwa ni wakala wa kiumbehai, kama vile kutokuwepo, au kukosekana sababu ni asili ya kutokuwepo kiumbe.
Kwa kawaida, kitu ambacho kinakuja kuwepo kama matokeo ya kuwepo kwa chanzo kamwe hakipotezi asili yake ya kuhitaji, wakati wote kitabia kiumbe chenye kuainishwa na kuhitaji. Kwa sababu hii, haja ya kitu juu ya kuwepo chanzo ni ya kudumu na isiyotanguka, uhusiano wake na chanzo hicho hautakatika japo mara moja. Endapo uhusiano huo ungekatishwa, uhai wa kitu hicho ungesalimu amri mara moja na kutokuwepo, kwa namna ile ile ambayo kwamba, mara jenereta ya umeme inapoacha kufanya kazi, taa zote angavu zilizounganishwa hapo hizimika. Ni kwa sababu hii kwamba chanzo na athari, uhuru kutokana kuhitaji na kutawaliwa na mahitaji ni hali ambazo zinahusiana wakati wote, endapo uhusiano huo ungekatizwa, kusingebakia chochote isipokuwa giza na kutokuwepo uhai.
Hivyo, hakuna jambo linaloweza kuonekana dhahiri hapa duniani mpaka uwezo maalum uwe umewekwa juu yake na kimoja ambacho asili yake iko huru kutokana na kuhitaji na chenyewe ndio chanzo haswa ambacho uhai hububujika kutoka humo. Kama uhai ungekuwa ni sehemu ya asili za vitu, kamwe usingefuata mkondo wa kukoma na kutoweka. Lakini ni ile tabia ya kuhitaji ndio tabia ya msingi kwenye asili zao, ili hata baada ya uhai wao kuanzishwa kwenye mpangilio wa viumbe, sifa yao ya kuhitaji huendelea kuwepo kwa hali yoyote ile. Haviko huru kamwe na kutohitaji chanzo; haiwezekani kwamba athari iweze kupata uhai kwa uhuru kabisa au iendelee kuwepo japo kwa nukta moja bila kutegemea juu ya chanzo. Kwa hiyo inakuwa dhahiri juu yetu kwamba vitu vyote - viumbe hai vyote vinavyoweza kutokea - vinapata wakati wote na kwa kila mara kutoka kwenye asili isiyo na ukomo ambayo ndio hugawa uhai - yaani, ile Nafsi Muhimu, ya Pekee na Muumbaji Muweza - ule uwezo na uhai unaoviruhusu kuwa hai na kubakia kuwepo hai.
Qur'anii Tukufu inasema:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿١٥﴾
"Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujitosha, Msifiwa (Fatir:35:15).
Na tuzingatie pia wito huu wa Qur'ani:
أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ ﴿٣٥﴾
"Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?" ( Tur: 52:35).
أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بَل لَّا يُوقِنُونَ ﴿٣٦﴾
"Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini" (Tur: 52:36).
أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٣﴾
"Au wanae mungu mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametakasika Mwenyezi Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye." (Tur: 52:43).
تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾
"Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu." (Almulku: 67:1).
Chanzo cha viumbe vyote chenyewe hakihitajii kuwa na Asili Wafuasi wa uyakinifu wanatoa uangalifu wa ukosoaji sana kwenye kanuni ya kwamba Mwenyezi Mungu hahitaji kuwa na Asili. Wao wanasema endapo tutadhani Muumbaji ndiye chimbuko la ulimwengu na ndiye anayeweka uhai juu yake, viumbe vyote vikipata vyanzo vyao na uhai wa kuendelea kutoka kwake, ni sababu gani imemuondolea yeye haja ya kuwa na muumbaji, ni kiwakilishi gani kilichosababisha yeye mpaka kuja kuwepo? Katika hotuba iliyotolewa kwenye jumuiya ya 'Londoni Atheist Sosiety,' mwandishi maarufu, Betrand Russell, alisema; "Siku moja, nilipokuwa na umri wa miaka kumi na nane, nilikuwa ninasoma wasifu wa John Stuart Mill. Sentenso moja mahsusi ilinivutia sana: Mill aliandika kwamba siku moja alimuuliza baba yake, ni nani aliyemleta yeye kwenye uhai duniani, na baba yake hakuweza kumjibu." Sababu yake ni kwamba papo hapo aliuliza swali la ni nani aliyesababisha Mwenyezi Mungu kuwepo?
Halafu Russell anaongeza: "Bado ninasadiki kwamba sentenso ile rahisi inadhihirisha ile ghiliba ya chanzo cha msingi. Kwani kama kila kitu lazima kiwe na sababu na chanzo, hali hiyo lazima itumike juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Kama, kinyume chake, kitu kinaweza kuwepo bila ya sababu au chanzo, kitu hicho inawezekana kiwe ama Mwenyezi Mungu au ulimwengu, na mjadala wote unakuwa hauna maana."
Kwa bahati mbaya, wanafalsafa fulani wa nchi za Magharibi ambao wanakubali kuwepo kwa Mwenyezi Mungu wameshindwa kufumbua tatizo hili. Mwana falsafa wa Uingereza Herbet Spencer amesema yafuatayo
kuhusiana na suala hili: Tatizo ni kwamba, kwa upande mmoja, akili ya binadamu hufuata sababu ya kila kitu na, kwa upande mwingine, hukataa fhana zote zisizo na mantiki (kwa vile ukweli wa dhana hizo hauwezi kuthibitishwa bila kurejea kwenye hitimisho). Haitambui wala kuelewa chanzo kisichosababishwa. Mchungaji anapomwambia mtoto kwamba Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu, mtoto huuliza nani aliyemuumba Mwenyezi Mungu?
Mahali pengine mwanafalsafa huyu anasema: "Myakinifu hujaribu kujisadikishia mwenyewe kuhusu dunia ambayo ipo na imetokana na yenyewe, milele bila ya kisababisho. Hata hivyo, hatuwezi kukiamini kitu ambacho hakina mwanzo wala asili. Mwanatheolojia huyo anayapeleka mambo haya hatua moja zaidi nyuma kwa kusema kwamba Mwenyezi Mungu aliuumba ulimwengu. Lakini mtoto anamuuliza swali lisilojibika: Nani aliyemuumba Mwenyezi Mungu?
.
Tunaweza kuleta hasa upinzani kama huo huo dhidi ya wayakinifu na kuwauliza, endapo tukifuata mlolongo wa usababishaji kinyumenyume, hatimaye tutafika penye chanzo cha msingi. Natuseme kwamba chanzo si Mwenyezi Mungu, bali ni mata. Sasa hebu tuambieni ni nani aliyeiumba mata ya msingi. Ninyi mnaoamini katika kanuni ya usababisho, tujibuni sisi swali hili. Kama mata ndio chanzo halisi cha vitu vyote, ni nini chanzo cha mata? Mnasema kwamba asili ya vitu vyote ni nguvu ya mata, ni nini sababu na asili ya nguvu ya mata? Kwa kuwa mlolongo wa usababisho hauwezi kurudi kwenye kutokuwa na ukomo, jibu pekee wanaloweza kutoa ni kwamba mata ni kitu kisicho na wakati na chenye umilele ambacho hakiwezi kuwekewa mwanzo: mata ni kitu kisichoumbwa, hakina mwanzo wala mwisho, kuwepo kwake hutukia ndani ya asili yake yenyewe.
Hii ina maana kwamba wayakinifu wanakiri kuwepo kwa kanuni ya umilele na kukosa chimbuko; wanaamini kwamba vitu vyote vilitukia kwenye maada ya milele na kwamba uhai unatukia kutoka ndani ya asili yenyewe hasa ya maada, bila ya haja yoyote ya muumbaji. Russell anelezea wazi imani hii kwenye hotuba iliyonukuliwa hapo juu. Yeye anasema; "Hakuna uthibitisho kwamba dunia ilipata kuwa na mwanzo kamwe. Hii fikira ya kwamba vitu lazima wakati fulani vilikuwa vina mwanzo inatokana na ufinyu wa fikra zetu."
.
Kwa namna ile ile ambayo Russell anafikiria mata kuwa ni ya milele, wanaomwamini Mwenyezi Mungu wanahusisha sifa ya umilele kwa Mwenyezi Mungu. Imani katika kitu chenye umilele kwa hiyo ni ya shirika, ya kawaida kwa wanafalsafa wa kiyakinifu na kidini. Makundi yote mawili yanaafiki kwamba kuna chanzo cha msingi, lakini wanaomwamini Mwenyezi Mungu wanakiachukulia chanzo cha msingi kama ni chenye hekima, ujuzi wote, na chenye kumiliki uwezo wa kuamua na utashi, ambapo kwa maoni ya wayakinifu, hicho chanzo cha msingi hakina busara wala akili, utambuzi ama uwezo wa maamuzi. Hivyo, kumwondoa Mwenyezi Mungu, kwa hali yoyote ile hakuleti ufumbuzi wa tatizo linaloletwa na suala la kiumbe cha milele.
Zaidi ya hayo, maada ni kituo cha mwendo na mabadiliko, na mwendo wake ni wenye nguvu na imewekwa ndani ya asili yake yenyewe. Sasa, mwendo muhimu hauendani na umilele, na mata na utulivu muhimu ni jinsi mbili ambazo zote ni za kipekee ambazo haziwezi kuunganishwa kwenye kituo kimoja. Chochote kile ambacho kimetulia na hakibadiliki katika asili yake hakiwezi kupokea mwendo na mabadiliko katika asili hiyo.
Ni vipi wenye fikira za ki-Marx, ambao wanaamini kwamba mata inaandamana na tamathali yake yenye dhana ya kutofautiana (tabaini), wanavyoweza kuthibitisha umilele wa maada? Umilele maana yake ni umadhubuti na kutobadilika kwa asili, kutowezekana kwa ukomo, lakini maada katika asili yake ni ufupisho makini wa nguvu na uwezekano; inawiana yenyewe, ikiwa imenasa kabisa katika kuishi na kufariki. Umilele hauendani na mtindo wa uhai uliomo kwenye mata na vipengele na sifa zilizolazimishwa na asili yake. Itikadi ya wale walio na imani juu ya Mwenyezi Mungu kuhusu kanuni isiyobadilika na ya dhahiri inahusika kwa kiumbe ambacho ndani, na, kwa asili yake kinaweza kukubali utulivu na kutobadilika; asili yake hainazo kabisa - na iko mbali nazo - sifa za maada. Asili yenyewe hasa ya maada inakataa kudumu, umilele na uendelevu, kwani kamwe haiwezi kujitenga yenyewe na mwendo, kuwiana na inakataa kuwa chanzo cha msingi au kisichobadilika.
Itakuwa na manufaa hapa kusimulia mazungumzo baina ya Imamu Sadiq
na mmoja wa wayakinifu wa wakati wake. Myakinifu: "Viumbe viliumbwa kutokana na nini? Imamu: "Havikuumbwa kutokana na kitu chochote (yaani kiasili havikuwa viumbe)." Myakinifu: "Sasa vinakua vipi na kujitokeza kutoka kwenye kutokuwa kiumbe?"
Imamu: "Je, sikusema kwamba vitu vyote duniani havikuumbwa kutokana na chochote? Maana yangu ni hii, kwamba viumbe vyote ki-asili havikuwa viumbe, na halafu vikaja kuwepo. Unataka kusema kwamba dunia ni ya milele, lakini fhana hii si sahihi kwa sababu zifuatazo:
"Kwanza, kama dunia hii ya maada ni ya milele, ina maana kwamba kitu chenye umilele lazima kipatwe na kubadilika na ukomo, jambo ambalo haliwezekani.
"Pili: endapo elementi zinazotengeneza dunia ni vya milele kwa sababu ya asili yao, inawezekanaje basi ziingie kwenye mkumbo wa kifo na kutoweka? Na kama, katika kinyume chake, zinakuwa hazina uhai katika asili zao, ni namna gani uhai unavyoweza kuchomoza kutoka ndani yao? Endapo utasema kwamba viumbe hai hutokana na elementi hai na viumbe visivyo hai hutokana na elementi zisizo hai, tunajibu kwamba asili isiyona uhai ndani mwake na utokanao ndani mwake haiwezi kuwa ya milele na haiwezi kuwa chanzo cha uhai." Myakinifu: "Kama maada iko kama vile usemavyo, kwa nini viumbe vinasemekana kuwa na umilele?" Imamu: "Imani katika umilele wa ulimwengu inashikiliwa na wale wanaokanusha kuwepo kwa mtawala na mpangaji wa maumbile, wanawakataa mitume wa Mwenyezi Mungu, wanafikiria vitabu wanavyokuja navyo wajumbe ni ngano za kale, na kubuni itikadi zinazowaridhisha wao wenyewe."
.
Sasa tunasema kwamba, kuwepo kwa kitu hakuwezekani bila ya chanzo cha kitu chenye upungufu, yaani, ambacho majaaliwa yake yamo mikononi mwa chanzo chake na ambacho kudumu kwake kunategemea kuwepo hai kwa chanzo chake. Hali hii haiwezi kutumika kwa kitu ambacho, kinafahamu uhalisi wake na hakioneshi dalili yoyote ya upungufu na ukomo.
Chanzo cha msingi ni chanzo msingi kwa sababu ya kuwa na uhai kamilifu na usiokuwa na kikomo; bila kutawaliwa na asili yoyote, kimeepukana na kuhitaji, mazingira na utegemezi, na hakina dalili ya kugeuka au kubadilika.
Tunapozungumzia kuhusu sababu ya mwanzo na wakati huo huo tunasema kwamba Mwenyezi Mungu ameepukana na haja yote ya kuwa na chanzo, hatuna maana ya kwamba Yeye kwa ujumla anashirikiana na viumbe vilivyoumbwa ile haja ya kuwa na chanzo lakini wakati fulani alikuwa, kama ilivyokuwa, aliondokana na kanuni ya usababisho. Mwenyezi Mungu sio athari kwamba ahitaji chanzo; Yeye si kiumbe kwamba ahitajie muumbaji. Kinyume chake, dalili zote na maajabu ya uhai vinatokana na Yeye, chanzo cha milele cha uhai. Kanuni ya usababisho hutumika kipekee kwenye mazingira ya vile vitu ambavyo kutokuwepo kwao kulitangulia - kabla ya kuwepo kwao.
Vivyo hivyo, maana ya sababu ya mwanzo si kwamba Mwenyezi Mungu alijibuni Mwenyewe, kwamba Yeye alikuwa ndio chanzo chake mwenyewe. Mahitaji ya athari kwa ajili ya chanzo yamo kwenye aina ya uhai ambao kile kilichotangulia kinao; kinakuwepo sio kwa sababu kina uhai kimsingi bali ni kama matokeo ya uhai utokanao na kitu kingine na ulio tegemezi kinaoupata kutoka kwenye chanzo. Lakini kiumbe ambacho asili yake haitawaliwi na hali yoyote na kinaonyesha kutokuwepo kabisa kwa utegemezi na uhusiano umeondolewa kabisa kutoka kwenye mazingira ambamo ile kanuni ya usababisho inafanya kazi.
Endapo kiumbe kwa sababu ya ukamilifu na kutokuhitaji kwa asili yake, kinakuwa hakihitaji chanzo, maana yake ni kwamba hakuna chanzo kilichokiweka katika kiwango maalumu cha uhai na kwamba hakuna sababu inayoweza kuingilia ndani yake. Mlolongo wa kisababisho hauwezi kurefushwa kurudi nyuma bila kikomo, na kukosekana kwa uhusiano ni kwa asili katika dhana yenyewe hasa ya chanzo cha awali. Swali kama: "Hicho chanzo cha awali kilijitokeza lini?" kwa hiyo, huwa halijitokezi; hivyo maswali kama haya hutumika tu juu ya vyanzo vya vitu na tabia zao za kutegemea.
Kuwepo kwa chanzo cha kwanza kunatambulika kwa dhati yake; kuwa kwake chanzo cha kwanza chenyewe, kwa hakika pia kunattmbulikana kwa dhati yake. Tabia zote hizi zinaashiria kujitosheleza, ambapo vitu ambavyo kuwepo kwao kumetokana na vitu vingine huwa vinahitaji chanzo, kwa sababu vinajulikana kwa tabia za kubadilik na kugeuka, kwa kuchipukia kutoka kwenye kutokuwepo na kuingia kwenye kuwepo. Inawezekanaje kudhaniwa kwamba imani katika kuwepo kwa Mwenyezi Mungu ni kukiri kuwepo kwa kuhitilafiana, ambapo imani juu ya asili isiyoanzishwa ya athari kama vile maada iwe haipingani?
Tunaishi kwenye dunia ambayo vitu vyote vimeachwa wazi kwenye kubadilika na kuharibika; ipo dalili ya kutokudumu, kutawaliwa na kufadhiliwa kulikochapwa kwenye kila chembechembe yake. Kuhitaji na kutegemeana kumeota mizizi imara katika uhai wetu na ule wa kila kitu kilichomo duniani na mbinguni. Uhai wetu sio wa kudumu na haukuzuka kutoka ndani ya asili yetu wenyewe; hatukuwa, na halafu tulifunikwa kwenye joho la kuwepo na tukaja kuwa hai. Ili kuweza kuja kwenye uhai, viumbe kama vile sisi lazima tuwe wenye kuomba sana kumfikia mwenye kutoa uhai.
Lakini Yeye Ambaye ni wa milele nawa kudumu, ambaye kuwepo kwake kunatokana ndani ya asili Yake Mwenyewe, na Ambaye kuonekana kwake kuko nje ya wakati, ni wazi kabisas hana haja ya chanzo. Maana ya chanzo katika falsafa ni kile kinacholeta athari kutoka kwenye kutokuwepo kitu hadi kuwepo kwake na kukifunika na vazi la uhai. Uumbaji huu hauwezi kutolewa hoja kwa ajili ya vyanzo vya kimaada, na jukumu moja tu la mata ni kuacha umbile moja ili kuweza kupokea umbo lingine.
Ni kweli kwamba kila kiumbe cha kimaada hupata tabia mpya na iliyo tofauti katika kila nukta kama matokeo ya maendeleo ya ndani kwa ndani. Hata hivyo, usogevu wa kimaumbile wa dunia na mifuatano ya uletaji na uchafuzi inadai mahitaji kudumu ya msaada kwa yule ambaye huumba mwendo, msaada ambao hulea msafara wa haraka wa uhai na kuusukuma kwenda mbele.