MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE 0%

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE Mwandishi:
: SALMANI SHOU
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi: KIMEANDIKWA NA SAYYID MUJTABAA MUUSAWIY LARI
: SALMANI SHOU
Kundi:

Matembeleo: 29171
Pakua: 3421

Maelezo zaidi:

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 28 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 29171 / Pakua: 3421
Kiwango Kiwango Kiwango
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

Mwandishi:
Swahili

11

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA KUMI NA MOJA

KUTOLINGANISHIKAKWA SIFA ZA KI-MUNGU

Katika jitihada zetu za kumwelezea alivyo Muumba na kupata kujua sifa zake, tunahitaji kwa ukamilifu kuwa na dhana na maelezo ambayo yako nje ya uwezo wetu. Yale maneno tunayotumia hayatatuwezesha kufikia lengo letu, maelezo halisi juu ya Mwenyezi Mungu, kwani uchache wa kuelewa kwetu hauwezi kuzingatia utambuzi wa asili hasa ya sifa za Mwenyezi Mungu zisizo na ukomo. Ametukuka juu ya dhana na fikra zote zinazobuniwa na kuundwa na akili ya binadamu.

Mwanadamu, ambaye ameumbwa na kuwekewa mipaka katika kila hali, asitumainie kuwa na uwezo wa kukadiria na kuelezea kitu kisicho cha kimaumbile kwa njia ya sifa na tabia za kimaumbile. Uhakika ambao ni kinyume na viumbe vinavyoweza kutokea na vile vya kawaida, ambao mamlaka yake kamili na elimu isiyo na ukomo vinafunika vitu vyote, ambao kwa maneno ya Qur'ani:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾

"Hakuna kitu chochote mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona." (42:11).

Dhati ya aina hii kwa kawaida haiwezi kujadiliwa kwa haraka kama mada zingine za kawaida. Ali(a.s) Bwana wa wacha-Mungu, alisema: "Yeyote anayemlinganisha na kumchanganya Mwenyezi Mungu na kitu au anakihusisha kwenye asili yake takatifu atakuwa kwa uhakika bado hajamuona Yeye. Chochote anachokijua mwanadamu kuwa ni msingi wa asili Yake ni lazima kiwe kimeumbwa. Mwenyezi Mungu ndiye Muumbaji na Mtengenezaji. Chochote kinachotegemea kitu kingine zaidi ya chenyewe hicho kimesababishwa na kimeumbwa. Ni Mwenyezi Mungu peke Yake tu ambaye ndiye sababu pekee (na sio athari).

Yeye anashughulikia uumbaji bila ya kutumia namna yoyote ya vitendea kazi. Hupima bila msaada wa fikira na tafakuri. Yeye si mhitaji na hapati manufaa kutokana na kitu chochote. Wakati na nafasi haviandamani Naye. Vyombo na vifaa havimsaidii Yeye. Kuwepo kwake hutangulia nyakati zote na ukabla wa umilele Wake ulitangulia mwanzo wote.

"Yeye habanwi na mipaka, kwani ni viumbe ndivyo huwekea mipaka maumbile yao kwa njia ambazo ni maalum kwao, na miili yao ndio inayoonyesha aina zao. Dhati Yake takatifu haikubali dhana ya mwendo na ile ya kutokuwa na mwendo, inawezekanaje kwamba kitu kilichoumbwa ndani ya kiumbe pia kiwepo ndani ya Dhati Yake? Kama pangekuwepo mwendo na kutuama kimya katika Dhati Yake, Angelazimika kukumbwa na mabadiliko na marekebisho; angeweza kugawanyika na kutokuwa na mwanzo kwake kungekanushwa. Yeye ni chanzo cha nguvu zote, kwa hiyo hakuna kiumbe ambacho kingeweza kumwathiri.Mwisho kabisa, Yeye ni Muumba Ambaye habadiliki au kutoweka na Ambaye kamwe hafichikani kwa watu wa ujuzi na umaizi."[33]

Ukweli kwamba sifa za Mwenyezi Mungu zimejitenga kabisa na zile za kwetu na haziwezi kupimwa kwa kulinganishwa na sifa zetu ni kwa sababu sifa za hicho chanzo cha viumbe ni tofauti na sifa za viumbe vingine vyote. Mathalani, sisi tunao uwezo wa kufanya kazi fulani, lakini hii sio sawa na ule uwezo wa Mwenyezi Mungu; kwa upande wetu, sifa ni kitu kimoja na kitu hasa kinachozungumziwa ni kingine. Tunapojivunia elimu zetu, hatuko kitu kimoja na kufanana na elimu zetu. Wakati wa utoto wetu hapakuwapo na dalili ya ujuzi au elimu katika utu wetu, lakini baadaye tulianza polepole kupata kiasi fulani cha elimu kwa kujifunza. Elimu na uwezo vinaunda pembe mbili tofauti za utu wetu, pembe hizi hazifanani na asili yetu na wala kuunganishwa pamoja katika maisha yetu. Sifa ni matokeo ya bahati na asili yetu ndio kiini; kila kimoja hakitemgemei mwenzie.

Lakini suala la sifa za ki-Mungu kimsingi ni tofauti: tunaposema kwamba Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa yote na ni Muweza wa yote, tunachokimaanisha ni kwamba Yeye ndiye chanzo cha elimu na uwezo. Sifa hizo sio kitu kingine mbali na kile inachokielezea ingawaje kifikra vinatofautiana. Kwa hali halisi, sifa Zake zinafanana na Dhati Yake; kwani Dhati Yake haiundwi na kitu ambamo mambo ya kubahatisha yanaweza kushikilia. Yeye ni Dhati halisi, yenye kufanana na elimu, uwezo, uhai, uthabiti na utambuzi; Yeye hatawaliwi na mipaka yoyote ya kiakili au ya kutoka nje au kizuizi.

Kwa kuwa tunalelewa katika kiini hasa cha maumbile, na kwa hiyo tuna uzoefu nayo wakati wote, na kwa kuwa chochote tunachokiona kina kipimo na umbo maalumu, wakati na mahali na sifa zingine zote za miili - kwa ufupi, kwa sababu ya mazoea ya akili zetu kwenye maumbile ya kawaida - tunajaribu kupima vitu vyote kwa kigezo cha maumbile, hata dhana za kiakili na kihekima. Kigezo cha maumbile kwa hiyo, kinakuwa kituo cha kuanza kuondokea cha uchunguzi wote wa kisayansi na kifalsafa. Kuidhania nafsi ambayo haina hata sifa moja ya kimaada na ambayo ni tofauti kabisa ni vile akili zetu zinavyoweza kutambua na kuelewa sifa ambazo hazitenganishiki na dhati hiyo, sio tu kunahitaji usahihi lakini pia kunatutaka tusafishe kabisa akili zetu na mambo ya maumbile.

Ali(a.s) amesema kwa ufasaha kabisa, kwa kina na kwa umuhimu mkub- wa kuhusu jambo hili. Anasisitiza kwamba mwanadamu hawezi kumfunga Mwenyezi Mungu katika maelezo, akisema: "Upwekeshaji halisi wa Mwenyezi Mungu (Tawhiid) na imani halisi vinategemea katika kuacha, kukana na kuondoa kabisa kutoka kwenye asili Yake tukufu, sifa zote za viumbe vilivyoumbwa. Mwenyezi Mungu apishie mbali kwamba Angeweza kuelezwa kwa sifa zozote kama hizo, kwa sababu akielezewa hivyo, itaonekana kama vile kila sifa imejitenga na mwenye sifa hiyo na ni mgeni nayo. Kwa hiyo mtu anayesema chochote katika kumuelezea Muumbaji akimdhania Yeye kuwanazo sifa fulani ambazo zimeongezwa na kukithirishwa kwenye ile dhati, tayari zimemfanya Yeye kuwa mshirika wa kitu fulani na kushauri kwamba anazo sehemu mbili. Jaribio la namna hii la kumwelezea Mwenyezi Mungu husababishwa na kutokujua na kutokutambua."[34]

Dhana za kiakili haziwezi kumwelezea Mwenyezi Mungu kwa kukimbilia sifa zenye ukomo, kwa kuwa na mipaka kwao, basi hazifai kumwelezea Mwenyezi Mungu. Kila sifa, kwa kuhusiana na ile maana maalum inayoiwasilisha, iko tofauti na sifa zingine zote. Kwa mfano; sifa ya uhai ni tofauti kabisa na sifa ya uwezo; hazibadilishaniki. Inawezekana kwamba mifano fulani huenda ikakusanya sifa zote hizi mahali pamoja, lakini kila moja ina maana yake kimsamiati.

Wakati akili ya mwanadamu inapotaka kukipatia sifa kitu fulani, lengo lake ni kuanzisha, katika mfano maalum, aina ya ushirikiano baina ya sifa na kitu inachokielezea. Lakini kwa kuwa sifa kimawazo inatofautiana na kitu chenyewe, akili bila kukwepa inaamuru kwamba vibakie mbali mbali. Njia moja tu ya kujua vitu ni kuvieleza kwa kutumia fikra za kiakili, ambazo kimawazo kila moja imetengana na mwenziwe, na kwa hiyo lazima viwe na ukomo. Dhana hizo haziwezi kwa hiyo, kutumiwa kupatia elimu juu ya ule Uhakika wa Hali ya Juu zaidi. Yeye ametukuka juu ya uwezekano na kujulikana kwa maelezo, na yeyote anayemwekea mipaka Mwenyezi Mungu kwa kutumia sifa fulani, huyo ameshindwa kupata

Kwa kutaja mifano michache tunaweza kuelewa kwa kiwango fulani jinsi ambavyo sifa hazikithirishwi kwenye dhati hiyo. Hebu zingatia kwamba miale ya joto inayotoka kwenye moto inafikisha joto kwenye kila kitu, hivyo kwamba mojawapo ya tabia na sifa ya moto ni kuwaka na kusambaza joto. Je, tabia hii imekalia pembe moja katika mwili wa umbile la moto? Kwa kweli, jibu ni hapana; uhai wote wa moto kwa jumla una sifa ya uwakaji na ugawaji wa joto. Imam Jafar as-Sadiq(a.s) alisema katika kumjibu mtu ambaye alimuuliza kuhusu hali halisi ya Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu ni kitu tofauti kabisa na vitu vingie vyote; ni Yeye peke yake ndiye anayelingana na dhati halisi ya asili ya uhai wote. Yeye si mwili na wala hana umbile. Milango ya fahamu haiwezi kumtambua Yeye na hawezi kutafutwa. Yeye ameepukana na utambuzi aina yoyote wa milango mitano ya fahamu; njozi na dhana havimtambui Yeye. Kupita kwa wakati na kupishana kwa zama havimpunguzi Yeye kwa hali yoyote, na ameepukana na mabadiliko na kigeugeu cha aina yoyote."[35]

UPWEKE WA MWENYEZI MUNGU (TAWHIID)

Wakati suala la upweke wa Mwenyezi Mungu linapojitokeza kwenye mazungumzo ya kidini, linachukuliwa kujumuisha mada nyingi, ikiwemo pamoja na imani ya upweke wa hiyo dhati, hivyo pia mkusanyiko wa sifa na tofauti baina ya dhati na sifa imewekwa pembeni kabisa kuhusiana na umoja wa sifa. Upambanuzi na utofautishaji unatokana na uwekaji mipaka. Kama tunatanguliza tofauti miongoni mwa sifa za ki-Ungu, inakuwa ni halali tu kwa mtazamo wa mawazo na tafakuri zetu za kawaida; ongezeko la mielekeo na sifa zilizokithirishwa haziwezi kuathiri hiyo dhati tukufu

Endapo katika ulimwengu wa maumbile tutatazama kiwiliwili kwa kutumia vipande vya kioo vyenye rangi tofauti; kiwiliwili hicho kitaonekana katika mfululizo wa rangi tofauti. Hivyo hivyo, tunapotafakari dhati tukufu ya kipekee kwa busara zetu, wakati mwingine tunaihusisha elimu na hiyo dhati isiyokuwa na ukomo kwa kuzingatia ukweli kwamba viumbe vyote wakati wote vipo mbele yake; halafu tunasema Yeye ni Mjuzi wa Yote. Wakati mwingine tunatambua uwezo wake wa kuumba vitu vyote, na halafu tunazungumzia juu ya Yeye kuwa Mwenye Nguvu zote. Kwa hiyo, pale tunapotambua kupitia kwenye vipenyo hivi mbali mbali, zile sifa tofauti zinazoonekana kufanana na uhai wetu wenye ukomo, tunajaribu kuzitenga kutoka kwenye dhati Yake isiyo na ukomo. Hata hivyo, bila upendeleo, dhana zote zilizowasilishwa na sifa hizo tofauti zinakuwepo mahali pamoja na unawasilisha ukweli moja, ukweli ambao hauna dosari na upungufu wowote, wenye ukamilifu wote kama vile uwezo, huruma, ujuzi, neema, hekima na ufahari.

Amirul-Muminin Ali(a.s) anasema katika hotuba ya kwanza ya Nahjul- Balagha,"Mwanzo wa dini ni kumtambua, na ukamilifu wa kumtambua ni kumsadiki. Imani ukamilifu wa kumsadiki ni kumpwekesha, na ukamilifu wa kumpwekesha ni kuwa na Ikhlasi Naye, na ukamilifu wa kuwa na Ikhlasi Naye ni kumuondolea sifa, kwa ushuhuda wa kila sifa ni si chenye kusifiwa, na ushuhuda wa kuwa kila chenye kusifiwa sio sifa. Hivyo basi mwenye kumsifu Mungu swt. Amemfanyia mwenzi, na mwenye kumfanyia mwenzi amemfanya kuwa wawili, na mwenye kumfanya wawili amemfanya kuwa mwenye sehemu sehemu, na mwenye kumfanya kuwa mwenye sehemu sehemu anakuwa hamjui, na ambaye hamjui anakuwa amemuashiria, na mwenye kumuonyesha amemuwekea mpaka, na mwenye kumwekea mpaka amemfanya wa idadi. Na mwenye kusema yuko ndani ya nini amemfanya yuko ndani ya; na mwenye kusema yuko juu ya nini amemtoa humo."

Kwa hiyo, kila sifa haina ukomo na inakuwa na uhai mrefu wa pamoja na umilele wa dhati yenyewe. Mwenyezi Mungu ametakasika na kuondokana na sifa zinazoweza kuwa tofauti na nyingine na kutenganishwa na dhati yenyewe. Pindi tutakapotambua kwamba dhati ya Mwenyezi Mungu inatokana na Yeye mwenyewe, hiyo ina maana kwamba kuna nafsi kamilifu isiyopimika katika namna zote. Kama kiumbe hai na kisichokuwa na uhai vyote vinaweza kufikiriwa sawa kwa ajili ya maisha, lazima kipate uhai kutoka kwenye kitu kingine ili kiweze kuwa hai; kitu kujianzisha chenyewe, hata hivyo, haiwezekani. Kwa hiyo, ni dhati kamilifu tu ndio inayoweza kutokana na yenyewe; hali halisi nyingine zote ziko chini yake na zinajulikana tu kwa njia yake. Pindi dhati itakapofanana na uhai wake, inakuwa isiyopimika kuhusu ujuzi, uwezo, kutojianzisha na hali ya kudumu milele, kwani zote hizi ni aina za viumbe na chimbuko ambalo linafanana na asili yake kwa hali yoyote ni lazima kuwa na ukamilifu wote huu kwenye kiwango kikubwa sana.

Upweke wa Mwenyezi Mungu (Tauhiid) ni mojawapo ya sifa Zake za mwanzo kabisa. Dini zote za mbinguni, katika mafundisho yao ya asili na yasiyopotoshwa, yamemlingania mwanadamu kwenye uthibitisho halisi wa upweke wa Mwenyezi Mungu, usiotiwa dosari na kushirikishwa na miungu wenza. Kupachikwa washirika huko, kwa namna zote za miundo na mielekeo ndio kosa baya sana ambalo mwanadamu anawajibika kwalo kisheria. Imetokea katika historia yote kama matokeo ya ujinga, kutokutambua, na kukengeuka toka kwenye mwongozo wa akili na mafundisho ya Mitume.

Kama mwanadamu alimwamini Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa fikra sahihi, uthibitisho wa akili na mwongozo wa mitume, isingewezekana kwa wao kukubali vitu vyovyote vya kubahatisha au vitu vilivyoumbwa, kusimama mahali Pake, na kudhani kwamba kiumbe kingine chochote kinaweza kuwa mshirika wake au kuwa sawa katika kuamuru na kuthibiti hali za dunia, au hata kuwa na sehemu katika uendeshaji wa mpango wa ulimwengu. Kama miungu wengi wangeitawala dunia na kila mmoja wa miungu hawa angefanya anavyotaka na kutoa amri kufuatana na utashi wake, mpangilio wa ulimwengu ungetambukia kwenye uawala huria. Qur'ani inasema:

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٢﴾

"Na (Yusuf) alipofikilia utu uzima, tulimpa hukumu na elimu na hivyo ndivyo tunavyo walipa watendao mema." (12:22)

Kama tunasema kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja, ni kwa sababu Yeye sio mwili. Kuimbe ni mkusanyiko wa mlolongo wa elementi, ambazo kuunganika kwao husababisha kiumbe kuwepo. Kuchanganyika, mgawanyiko na kuzaana zote hizi ni sifa za viumbe na miili inayotegemewa kuweko au kutokea; kwa hiyo tunaiondoa kwenye mfano wa Mwenyezi Mungu na tunathibitisha kwamba chochote ambacho kimekuwepo, kama matokeo ya uchanganyikaji na uzaanaji, wala hakiwezi kuwa Mwenyezi Mungu ama kufanana Naye.

Inawezekana kufikiria juu ya u-wingi ndani ya namna fulani maalum pindi tunapozungumzia mipaka kama vile wingi, ubora na muda. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu habanwi kimipaka na lolote kati ya haya, na kwa hiyo haiwezekani kumfikiria Yeye kuwa na wa kufanana Naye au mwenza. Kama tunajaribu kudhania asili ya maji, bila sifa yoyote ya ukomo au mpaka, na tukalirudia zoezi hili mara kadhaa, hakuna kitakachoongeka kwenye dhana yetu ya awali. Kwa sababu mwanzoni tuliyafikiria maji katika maana yake halisi, bila kuweka ufinyu wowote katika hali, wingi au ubora, haiwezekani kwamba katika majaribio yetu yatayofuata ya kutafakari juu yake, nadharia mpya itajitokeza kwetu sisi.

Lakini tunapoongeza kwenye asili ya maji sifa fulani zenye ukomo ambazo sio za msingi juu yake, aina tofauti na mifano ya maji itatokea na pamoja nayo, ni uwingi. Mifano ya hili ingekuwa maji ya mvua, maji ya chemchem, maji ya mto, maji ya bahari, yote haya yakionekana nyakati na sehemu tofauti hapa na pale. Kama tukiondoa masharti yote haya na kuangalia tena asili ya msingi ya maji, tutaona kwamba yameondokana na aina zote za uwili mchanganyiko na sasa ni asili moja tu.

Lazima tutambue kwamba kiumbe chochote ambacho kinaweza kuwekwa na kuenea kwenye sehemu fulani, basi kwa lazima sana kinaihitaji sehemu hiyo, na kitu chochote ambacho kitakuwa ndani ya wakati fulani, uhai wake yenyewe unategemea mazingira bainifu ya wakati huo: uhai wake utatambuliwa tu ndani ya muundo maalum wa kiwakati ambamo mazingira hayo yanaupata.

Kwa hiyo, tunapokuja kuitambua nafsi ambayo ipo wakati wote na kila mahali na ambayo ina kiwango cha juu sana cha ukamilifu wa kueleweka, na ambayo mbali na hiyo hakuna kitu kingine ambacho ni kikamilifu au halisi na kisicho na walakini, lazima tuelewe kwamba kupachika uwili juu ya dhati ya juu kiasi hicho ni kukifanya kiwe chenye mwisho na ukomo. Hakika Mwenyezi Mungu si mmoja kwa maana ya kimahesabu, hivyo kwamba tunaweza kudhania kwamba Yeye ni wa kwanza wa aina ambayo anafuatiwa na wa pili. Upweke wake ni kiasi kwamba kama tukidhania kuwepo wa pili pamoja Naye, yule wa pili lazima afanane na yule wa kwanza.

Kwa kuwa uongezekaji wa vitu hutokana na mazingira yenye kuweka mipaka ambayo huvitofautisha kimoja na kingine, itakuwa haina mantiki kabisa kuleta nadharia ya wa pili juu ya kiumbe kisichokuwa na mipaka na vifungo. Kuwepo kwa wa pili itamaanisha kwamba wa kwanza alikuwa na mipaka na vifungo, na endapo mipaka na vifungo vikiondolewa, hatuwezi kuwa na viumbe viwili; dhana yetu ya kiumbe cha pili itakuwa ni marudio ya kile cha kwanza.

Mafundisho ya upweke wa Mwenyezi Mungu yana maana kwamba kama tukimchukulia Mwenyezi Mungu peke yake bila kuvihusisha viumbe vingine vyote vinavyotambulika, dhati yake tukufu inathibitika kikamilifu. Vivyo hivyo, endapo tunafikiria kuwepo kwake, pamoja na kuvihusisha viumbe vingine vyote, hapo tena, kuwepo kwake kutakuwa kumethibitika kikamilifu. Lakini kama, kwa kinyume chake, tunaviangalia vitu vinavyotokea bila kutarajiwa bila kumhusisha Mwenyezi Mungu basi vitu hivyo haviwezi kusemekana kwa njia yoyote ile kwamba vipo, kwa sababu kuwepo kwao kunategemea juu ya Muumba kwa ajili ya chimbuko lao na kuongezeka kwao.

Kwa hiyo wakati wowote tunapomwekea Mwenyezi Mungu mipaka na masharti, maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu atakoma kuwepo wakati wowote ambapo mpaka na sharti hilo litakoma kuwepo. Hata hivyo, kuwepo kwa Mwenyezi Mungu hakutawaliwi na sharti au wingi, na kwa hiyo akili haiwezi kuleta nadharia ya wa pili katika namna yake. Hebu natutoe mfano mmoja: Tuchukulie kwamba dunia haina ukomo; haina mipaka na katika upande wowote tutakaoelekea kamwe hatufikii mwisho wake. Kwa fikra kama hii kuhusu dunia ya maumbo, mipanuko yake yote ikiwa haina mwisho, tunaweza kudhania kuwepo kwa dunia nyingine zaidi yake, imma yenye ukomo au isiyo na ukomo. Hakika hatuwezi, kwa sababu dhana ya dunia ya viumbe isiyo na mwisho inalazima kuondoa kuwepo kwa dunia nyingine kama hiyo. Endapo tunajaribu kufikiria dunia nyingine kama hii, ama itafanana na ile ya kwanza au iwe ni sehemu yake.

Kwa hivyo, kufikiri kwamba asili tukufu ni kiumbe kilicho kamilika, kudhania kuwepo kwa kiumbe cha pili kinachofanana na Yeye ni sawa kabisa na kudhani dunia ya pili ya viumbe kuwepo kwa wakati mmoja huohuo na dunia ya viumbe isiyo na mwisho. Kwa maneno mengine, hiyo haiwezekani. Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba maana ya Mwenyezi Mungu kuwa Mmoja sio kwamba Yeye sio wawili; ni kwamba, wa pili hafikiriki kuwepo na kwamba umiliki pekee wa utukufu unalazimishwa na asili Yake. Anakuwa tofauti na mwingine asiyekuwa Yeye Mwenyewe, sio kwa namna ya mpaka wowote bali kwa namna ya asili Yake yenyewe ambayo inaweza kutofautishwa wazi wazi na zingine zote. Viumbe vingine vyote, vinapolinganishwa, hupata ubainishwaji wao, sio kutoka kwenye asili zao bali hasa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Tunaona dhahiri kwamba uhusiano na upatanifu mkubwa unakuwepo miongoni mwa vijenzi vyote vya dunia. Binadamu huzalisha gesi ya asidi ya kaboni ambayo huiwezesha mimea kuvuta hewa hiyo, na miti na mimea, kwa kubadilishana hurudisha hewa ya oksijeni ambayo humwezesha binadamu kuivuta. Kwa matokeo ya kubadilishana hivi baina ya binadamu na mimea, kiasi cha hewa ya oksijeni huhifadhiwa wakati wote; kama isingekuwa hivyo, hakuna dalili za maisha ya mwanadamu yangebaki juu ya duniani.

Kiasi cha joto kinachopokelewa na dunia kutoka kwenye jua huwa kinakubaliana na mahitaji ya viumbe hai kwa ajili ya kupata joto. Kasi ya mbiringiko wa dunia kuzunguuka jua na umbali inaouweka kutoka kwenye chanzo hicho cha nishati na joto vimekadiriwa katika kiwango kinachofanya uhai wa binadamu juu ya dunia uwezekane. Umbali wa dunia kutoka kwenye jua ndio unaoamua kiwango cha nyuzi joto ambacho hasa ndicho kinachokubaliana na mahitaji ya uhai juu ya ardhi. Kama kasi sya mbiringiko wa dunia kuzunguka jua ingekuwa maili 100 kwa saa badala ya maili 1000 kwa saa, kama ilivyo sasa, vipimo vya usiku na mchana wetu vingekuwa mara kumi zaidi kwa urefu, na ukali wa joto la jua ungepanda na kufika kiwango ambacho uhai wote wa mimea ungeunguzwa na usiku wa baridi wa kila siku ya majira ya kipupwe ungegandisha machipu yote mapya ardhini.

Endapo, kwa upande mmoja, miale ya jua ingepunguzwa kwa nusu, viumbe hai vyote vingegandishwa pale vilipo na baridi iliyokithiri sana. Endapo, kwa upande mwingine, miale ya jua ingeongezwa na kuwa maradufu, mbegu ya uhai kamwe isingeweza kufanikisha matunda yake. Kama mwezi ungekuwa mbali sana kutoka duniani, mawimbi ya bahari yangekuwa na nguvu na makali kiasi cha kutosha kuweza kung'oa milima. Inapooonekana kwa mtazamo huu, dunia huonekana kama msafara ambao wasafiri wake wote wameungana pamoja kama viungo katika mnyororo. Sehemu zake zote, kubwa na ndogo zinajitahidi kwa pamoja kusonga mbele kwenye muelekeo mmoja. Katika mfumo wote huu, kila kitu kinatimiza kazi yake mahsusi na vitu vyote husaidiana na kukamilishana. Kiungo kikubwa na kisichoonekana huunganisha kila atomu moja na atomu zingine zote.

Dunia ambayo imejaa umoja kiasi hicho lazima iwe imeunganishwa na chimbuko na kanuni moja. Uhai unatokana na chanzo kimoja, kama ujumla wote wa ulimwengu ni mmoja, muumbaji wake pia lazima awe mmoja. Ule ukweli kwamba muumbaji ameleta umoja katika uwingi wa dunia iliyoumbwa, huo peke yake ni uthibitisho wa kutosha wa Upweke wake, uwezo na hekima Yake.

Qur'ani inasema:

قُلْ أَرَأَيْتُمْ شُرَكَاءَكُمُ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا فَهُمْ عَلَىٰ بَيِّنَتٍ مِّنْهُ بَلْ إِن يَعِدُ الظَّالِمُونَ بَعْضُهُم بَعْضًا إِلَّا غُرُورًا ﴿٤٠﴾

"Sema: mmewaona washirika wenu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Nionyesheni ni sehemu gain ya ardhi waliyoiumba au wanayo shirika katiaka mbingu? Au tumewapa kitabu na wao ambacho kwacho wakawa na dalili za wazi? Lakini madhalimu hawaahidiani wao kwa wao ila udanganyifu tu. Kwa hakika Mwenyezi Mungu huzuia mbingu na ardhi zisiondoke, na kama zikiondoka hakuna yeyote wa kuzizuia baada yake. Bila shaka yeye ni Mpole, Mwingi wa kusamehe." (35:40-41).

Asili yetu ya kimaumbile, ambayo ni kipimo cha msingi wa maisha yetu pia inathibitisha upweke wa Mwenyezi Mungu. Katika nyakati za hali mbaya sana na taabu, matakwa yetu yote huelekezwa mahali pamoja; tunageukia upande mmoja na kukabidhi nyoyo zetu Kwake. Mmojawapo wa wanafunzi wa Imamu Jafar as-Sadiq(a.s) alimwuliza, "Kuna uthibitisho gani juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu?" Imamu alimjibu: "Uthibitisho wa upweke Wake ni uhusianaji mwendelezo wa maumbile yote, mpangilio muhimu wa uhai ambao unatawala juu ya kila kitu. Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qur'ani:

"Angekuwepo muumba mbinguni na katika ardhi, mbali na yule Mungu Mmoja, mpango wao ungetoweka na dunia ingeangamia."[36] Kwa hiyo, utaratibu na uelewekaji wa mpangilio uliotawala vitu vyote unaikanusha ile nadharia ya kuwa panaweza kuwepo na miungu wengine kadhaa, wanaotawala maeneo yale au maeneo mengine tofauti.

Ingawa Qur'ani inasisitiza upweke wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji na hekima, pia inatamka wajibu wa visababisho na njia ambazo zinatekeleza amri ya Mwenyezi Mungu. Inasema:

وَاللَّـهُ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ﴿٦٥﴾

"Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, kwa hakika katika hayo mna mazingatio kwa watu wanaosikia." (16:65)

Pindi tunapofikia kwenye hitimisho kwamba Mwenyezi Mungu peke Yake ndiye anayeshughulika na uumbaji, upangaji na uendeshaji wa ulimwengu wote, na kwamba vyanzo vyote vya athari na uhusiano baina yao viko chini ya utashi na amri Yake, kila kimoja kikiwa na kazi yake maalum ilichopangiwa na Mwenyezi Mungu - pindi tunapofikia uamuzi huo, tunawezaje kudhania kiumbe kingine chochote kuwa katika daraja sawa na Mwenyezi Mungu na kuinama katika kukiabudia mbele yake?

Qur'ani inasema:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾

"Na miongoni mwa watu wako ambao huwafanya miungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini wale walioamini wanampenda sana Mwenyezi Mungu zaidi (2: 165)

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿٣٧﴾

"Na miongoni mwa ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba, ikiwa ninyi mnamuabudu Yeye t u." (41:37).

12

MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE

SOMO LA KUMI NA MBILI

UWEZO WA MWENYEZI MUNGU USIOPIMIKA

Uwezo wa Mwenyezi Mungu Usiopimika,haun uthibitisho wa wazi zaidi kuliko ule unaopatikana kwa njia ya uchunguzi na kuhoji maumbile ya ulimwengu ulioumbwa na mifumo mingi ya mpangilio wa rangi za maumbile ambazo kamwe haziwezi kuelezewa kukamilifu.

Tunapo tazama viumbe wa Mwenyezi Mungu tunajikuta tunakabiliwa na nguvu kubwa mno hivyo kwamba hapana ukomo unaoweza kufikiriwa juu yake. Kutazama uumbaji na mamilioni ya ukweli yaliofichika kwenye maajabu ya maumbile na vina vya ndani vya utu wake mwanadamu mwenyewe kunatoa dalili za wazi kabisa za kipimo cha uwezo wa yule Mmoja Aliyeuumba huo, kwani mpangilio mzito wa uhai na mgumu kuelezeka haukubali maelezo mengine.

Ni uwezo wa Mwenyezi Mungu usiolinganishika ambao humlazimisha binadamu kuinama kwa unyenyekevu mbele ya Muumbaji wa mpango huu mkubwa. Hakuna neno la kuweza kuelezea kadiri ya vipimo vya uwezo Wake, dhati hiyo ya pekee ina uwezo mkubwa mno ambao kwamba wakati wowote Anapolitaka jambo, hutosha kwa ile amri, 'Kuwa' itoke kwake na kitu kilichoambiwa hivyo, kitakuwa. Qur'ani inasema:

إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾

"Hakika amri yake, anapolitaka jambo lolote ni kuliambia tu: 'KUWA' na linakuwa. (36:82).

Sheria iliyofafanuliwa katika Aya hii ni ishara nzuri zaidi ya uwezo Wake usio na mpaka na udhihirisho wa mamlaka wa utukufu Wake usio na mwisho. Inabatilisha mpaka wowote ambao unaweza kuwekwa juu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu na kutangaza kutotoshekeza kwa vigezo vyote na vipimo, vinapokabiliwa na sheria hii tukufu.

Mabingwa wa sayansi ya viumbe, watu wa maabara, licha ya maendeleo yote ambayo wamepata, hawajapata elimu kamili ya siri za ndani kabisa za kiumbe mmoja pekee miongoni mwa viumbe vingi na vyenye kutofautiana vya ulimwengu ulioumbwa. Hata hivyo, ile sehemu ya elimu na yenye dosari ambayo mwanadamu ameipata kuhusu viumbe vichache vilivyopo hapa ulimwenguni inamtosha yeye kutambua kwa nafsi yake yote kwamba ile nguvu kubwa ambayo imeumba aina mbalimbali na nyingi kama hizi hapa duniani lazima iwe haina ukomo.

Fikiria wingi wa viumbe Vyake: viumbe vidogo sana na madubwana yenye sura za ajabu kwa pamoja wakiishi katika vina vya baharini; ndege wanaopendeza wenye sauti za kuvutia wenye mabawa yenye rangi mbalimbali, ambao uzuri wao, wasanii stadi huiga, kama mapambo ya kazi yao; nyota zing'arazo mbinguni na jua lichomozalo na kuzama; alfajiri na mwanga wa mwezi; sayari, galaksi na jamii ya nyota nyingi za mbali sana kila moja yao wakati mwingine kwenye kiini chake huwa na mamilioni ya nyota kubwa sana zing'arazo na kufanya maruweruwe ukosa ukomo wake wa dhahiri.

hivi maumbile kama haya, yanayoshangaza kwa utukufu wake, hayaashirii uwezo usio na ukomo wa mtengenezaji wake? Je, mtu anaweza kudharau uwezo wa Muumbaji Ambaye anatoa mabadiliko mbali mbali kama haya kwenye maisha, akafanya miundo dhahiri, ya mabadiliko hayo, yenye ukomo kujitokeza kwenye mpango wote huu mpana wa matukio. Sasa baada ya ukweli kwamba aina zote hizi za viumbe za kuvutia hatimaye zinachipukia kutoka kwenye atomu, suala la uhai haliwezi kuelezewa isipokuwa kwa kurejea kwenye mamlaka yenye muongozo na yasiyo na ukomo. Ni Yeye Ambaye huvichochea vitu vyote kuelekea kwenye dhana ya muundo wenye kuleta uhai na anao uwezo na akili ya kupanga na kubuni mpango huu mpana na sahihi.

Kubwa na ndogo, ngumu na rahisi ni tabia zinayofungamana na viumbe vyenye ukomo; katika ufalme wa milele wa dhati na sifa za Mwenyezi Mungu, hakuna suala la ukubwa na udogo, nyingi na chache. Unyonge na udhaifu husababishwa na ukomo wa nishati katika haki ya utumiaji wa wakala, kwa kuwepo kipingamizi katika njia yake, au kwa kukosekana njia na vifaa, hayo ni yasiyowazika katika suala la uwezo usio na ukomo. Qur'ani inasema:

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا ﴿٤٤﴾

" Na hakuna kitu kiwezacho kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala ardhini, Bil a shaka yeye ni Mwenye kujua, Mwenye uwezo." (Fatir: 35:44).

Ingawa Mwenyezi Mungu anaweza kufanya vitu vyote, Ameumba ulimwengu kulingana na mpango usahihi na maalum katika mfumo ambao kwamba jukumu lililopangwa maalum, limewekwa juu ya viumbe fulani katika uanzishaji wa vingine. Viumbe hivyo, moja kwa moja na bila shaka yoyote viko chini ya amri Yake wakati vinapotimiza jukumu hilo na kamwe havikiuki amri Zake japo kidogo. Qur'ani inasema:

وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾

"Na jua na mwezi na nyota vimetiishwa kwa amri Yake. Fahamuni kuumba na amri zote na Zake. Amebarikiwa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote. (A'aaraf: 7:54).

Kusema kweli, hapana kiumbe katika mpango wa ulimwengu kinachoweza kuwa udhihirisho wa mamlaka au kuwa na fungu lolote katika utashi na amri Yake, kwani kama vile ambavyo Mwenyezi Mungu hana mshirika katika dhati Yake, vivyo hivyo, pia, hana mshirika katika uwakala Wake. Kama vile ambavyo viumbe vyote duniani vinavyokosa uhuru katika asili zao na vikawa vinamtegemea Yeye, pia vinaukosa vilevile katika kutoa vitendo na athari. Kila kiwakilishi na kisababishi hupata dhati ya uhai wake kutoka kwa Mwenyezi Mungu na pia uwezo wake wa kutenda na kutoa athari.

Kila anapotaka na kukilazimisha, amri ambayo inahusu viumbe vyote hutelekeza wajibu wake, kwani utaratibu huo wenyewe upo chini ya utashi Wake, hata kama uwe wenye thamani na imara vipi. Muumbaji Ambaye ameweka athari mahsusi kwa kila kitu na chanzo, anaweza kuitangua na kuahirisha athari hiyo wakati wowote. Kama vile ambavyo amri moja ilivyosababisha utaratibu wa ulimwengu kuwepo, amri nyingine hunyang'anya maumbile athari zao za desturi.

Hivyo, Qur'ani inasema:

قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ ﴿٦٨﴾ قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿٦٩﴾

"Wakasema; mchomeni (Ibrahim) na muiokoe miungu yenu, ikiwa ninyi ni watu wenye kutenda. Tukasema; Ewe moto! Kuwa baridi na salama juu ya Ibrahim. (21:68-69).

Ingawaje ule mvuto wenye nguvu sana utolewao na jua na ardhi unaenea kwenye nafasi kubwa mno, bado maumbo yote hayo yako chini ya utashi Wake. Mara tu Anapompa ndege mdogo nguvu za lazima, ndege huyo anakuwa na uwezo wa kuzuia mvuto wa ardhi na akaruka zake. Qur'an inasema:

أَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ مُسَخَّرَاتٍ فِي جَوِّ السَّمَاءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا اللَّـهُ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٧٩﴾

"Je, hawawaoni ndege waliotiishwa katika anga la mbingu? Hakuna awazuiaye (wasianguke) isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayo mna mazingatio kwa watu wanaoamini. (16:79).

Kiumbe chochote kinachoweza kufikiriwa kuwepo katika dunia ya maumbile kinakuta mahitaji yake ya riziki na maisha yanatimizwa na Muumbaji. Kwa hiyo, uwezo wowote na nafasi inayoonekana kwenye mpango wa maumbile inabidi lazima kurudi kwenye uwezo usio na kikomo wa Mwenyezi Mungu. Amirul-Mu'minin Ali(a.s) anasema kwenye hotuba iliyoandikwa kwenye Nahju al-Balagha:

"Ee Mwenyezi Mungu, hatuwezi kupenya vina vya ubora utukufu wako. Tunajua kwamba Wewe uko hai daima na unajitosheleza, kwamba wewe huhitajii kula wala kulala usingizi. Hakuna akili inayoweza kukutambua Wewe na hakuna jicho linaloweza kukuona wewe. Bali Wewe unayaona macho yote, Unajua kipindi cha uhai wa kila kiumbe, na Wewe ni Muweza wa kila kitu.

"Ingawa hatujatambua lolote katika uumbaji Wako, tunashangazwa na uwezo Wako na tunakutukuza sana Wewe. Kile kilichofichika kwetu na macho yetu hayawezi kukiona wala fikra na akili haviwezi kukipata, ambacho kimefichwa kwetu kwa mapazia ya ghaib (yasiyoonekana) ni kikubwa zaidi kuliko kile tunachokiona." [37] Mtu anapoamua kujenga kitu - mfano hospitali - hukusanya vitendea kazi muhimu na vifaa vingine ambavyo havina uhusiano wowote muhimu kati ya kimoja na kingine, na halafu anaviunganisha kwa kutumia mlolongo wa uhusiano wa bandia ili kutimiza lengo lake.

Ili aweze kutengeneza uhusianao wa bandia kama huo, hutumia nguvu tofauti tofauti na vitu vingine ambavyo anavikuta tayari vipo. Kazi na shughuli ya mtu huyu ni sehemu ya mfumo wa maumbile, sio shughuli ya ubunifu kwa kusema kweli, bali ni namna ya msogeo tu ambao unafanyika ndani ya vitu vilivyopo. Uumbaji wa ki-Mungu unakuwa na aina tofauti kabisa na ule uzalishaji wa uhusiano wa bandia baina ya vitu visivyo husiana. Mwenyezi Mungu huanzisha vitu vikiwa na tabia zao zote, nguvu, nishati na sifa bainifu.

Tunaposema Mwenyezi Mungu ni mweza wa yote, lazima tuelewe kwamba uwezo wake unavutika au kuitikia tu kwenye vitu vinavyowezekana. Vitu ambavyo haviwezekani kimantiki vipo nje ya nyanja (fani) ya uwezo Wake na kutumia neno 'Uwezo' kuhusiana na vitu ambavyo haviwezekani sio sahihi na haina maana yoyote. Ingawa uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa kweli hauna ukomo, uwezo wa mapokezi wa vitu na uwezo wao wa kutumika kama kituo maalum kwa ajili ya udhihirishaji wa uwezo wa ki- Mungu lazima ufikiriwe. Utekelezaji wa utashi wa Mwenyezi Mungu unasokotana na uhusiano baina ya chanzo na athari, na mfumo mgumu wa sababu na vyanzo usioelezeka kwa urahisi. Ili kitu kiweze kuwa lengo la utashi wa ki-Mungu, lazima kisiwe ni kisichowezekana na lazima, katika asili yake, kiwe na uwezo wa kupokea; utashi wa ki-Mungu unatimizwa kwa njia ya wepesi wa upokeaji vitu vyenyewe. Ni kweli, kwamba nuru ya ki-ungu haina ukomo na wakati wote inazidi kufurika, lakini sehemu inayotakiwa kuipokea nuru hiyo inaweza kuwa na dosari na kwa hiyo inashindwa kufyonza mgawo huo wa kudumu ambao unatolewa na chanzo hicho chenye ukwasi tele.

Bahari ni chanzo kikubwa sana cha maji, chenye maji mengi sana, lakini meli ya kubebea vimiminika ina nafasi ndogo tu ya kuchukua maji yake; kwa kweli ni kiasi kidogo sana cha maji hayo kitakachoweza kupakiwa kwenye meli hiyo. Kwa uwazi wa kutosha kabisa ni kwamba chenye mpaka na kikomo katika mfano huu ni nafasi ya meli, sio maji katika bahari hiyo.

Mtu mmoja wakati fulani alimuuliza Ali, Amirul-Mu'minin(a.s) : "Je, Mola wako anaweza kuijaza dunia yote kwenye yai la kuku?"

Akajibu:Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote, kwa hakika anaweza kufanya chochote, lakini kile ulichouliza ni kitu kisichowezekana." [38] Kwa hiyo ingawa dhati tukufu ya Mwenyezi Mungu ipo huru kabisa kutokana na kutokuwa na nguvu na uwezo, haina maana na mantiki kuuliza kama Mwenyezi Mungu anaweza kufanya jambo ambalo kwa asili haliwezekani.

Mtu ambaye moyo wake hudunda kwa kumpenda Mwenyezi Mungu na ukawa umejawa na imani juu ya Muumbaji wa vitu vyote kamwe hatokata tamaa, kujihisi mpweke na asiye na matumaini hata katikati ya matatizo magumu sana. Tendo lolote analolifanya, anafanya huku akitambua kwamba yupo kwenye kivuli cha ulinzi cha nguvu kubwa ambayo inaweza kumfanya yeye aweze kupata ushindi juu ya matatizo yote. Mtu anayemtambua Mwenyezi Mungu na anajua kwamba anafaidi msaada Wake anaweza kujizuia na kustahamili matatizo ya kila aina. Kwake yeye mtu huyo matatizo ni kama sehemu ya povu iliyomo kwenye povu linalotoweka haraka juu ya uso wa maji. Moto unaowaka ndani mwake huendelea kuwaka na kuangaza zaidi na anatokea kuwa na nguvu zaidi kuliko mwanzo kutoka kwenye kalibu (kikaango) ya mateso.

Wakati wote binadamu wa kazi ngumu anazostahimilia, analiwazwa na kutiwa nguvu na huruma na upendeleo wa Mwenyezi Mungu, hali hii ndiyo inayo tengeneza nguvu ya shughuli yake. Kushindwa hakumzibii njia yake na kusababisha asalimu amri badala yake, kwa nia njema na juhudi za uchapakazi, huendelea kufanya bidii kwake hadi mwishowe anapopata ushindi.

Anaelewa vema kabisa kwamba juhudi zake haziwezi kukosa kuleta matokeo mazuri na kwamba ushindi huenda kwa yule anayestahili. Kila anaporidhia, Mwenyezi Mungu humshika mkono yule aliyeanguka na mwenye kudhulumiwa ambao hawana kimbilio jingine mbali na Kwake na kuwanyanyua na kuwafikisha kwenye kilele cha uwezo. Pia wakati mwingine Mwenyezi Mungu, huzipaka vumbi la udhalilishaji na mabalaa, zile pua za wenye uwezo na madhalimu wenye kiburi ambao huamini kwenye vurugu tu na mantiki ya mabavu na kuwatendea watu kama vile hawana thamani.

Ni madikteta wangapi wenye kiburi wametupwa chini na mabalaa katika historia ya mwanadamu, wakazama na kutoweka katika wimbi la aibu. Mfululizo wa kisa cha mitume wa Mwenyezi Mungu unawakilisha mfano kamili na bora wa maadili mema ya binadamu. Sote tunajua jinsi mitume walivyosimama peke yao dhidi ya nguvu za dhuluma za wakati wao ili waweze kuwaongoza wanadamu kwenye ukombozi, kuibadili jamii yao, na kuwafundisha maadili ya kiwango cha juu. Kwa kufanya hivyo, waliwasha cheche ya kwanza ambayo hatimaye iliangamiza ushirikina.

Majibu yaliyoamshwa na imani zao yalisababisha vurugu ya uhakika hivyo, kiasi kwamba waliweza kubadili sura na mwelekeo wa historia. Waliweka misingi ya ibada ya Mungu mmoja (Tawhiid) na waliasisi kanuni za maadili kwa njia pana zaidi. Ni nani anayeweza kukanusha wajibu waliofanya kwa kujitolea kwao na imani zao katika mapambano yasiyochokesha waliyoyafanya? Ni umbali gani nguvu ya utashi peke yake inaweza kumfikisha wanadamu na kwa kiasi gani itamwezesha kustahamili na kujitolea mhanga?

Uchambuzi wa haraka wa historia ya kujivunia ya maisha ya Mitume unatuwezesha sisi sote kutazama, kwa namna ya dhahiri kiasi iwezekanavyo, ule uaminifu na utiifu waliouonyesha, huruma zao na uvumilivu wao na tamaa yao kubwa ya kuwaongoza na na kuwabadilisha wanaadamu.

Siri yao kuu juu ya mafanikio yao ni ukweli kwamba kamwe hawakujifiria wao wenyewe binafsi hata mara moja, kwa uaminifu walizikana nafsi zao, na kuzifanya wakfu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Halafu Mwenyezi Mungu akajibu kwa kuwajaalia Mitume uhai na umaarufu wa milele daima.