2
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
KUFARIKI KWAKE KWENYE KUSIKITISHA NA KUHUZUNISHA
Tangu Mtume(s.a.w.w)
alipopewa utume rasmi na kukabidhiwa ujumbe wa kiislaam mpaka kufariki kwake na kuiaga kwake Dunia hii alikuwa akiungwa mkono na wahyi (ufunuo), na Aminul-wahyi Jibraaillu
alikuwa akishuka kwake akiwa na Qur'ani tukufu au akimletea Qur'ani tukufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kidogo kidogo na katika matukio mbali mbali, hadi kitabu hiki adhiim kikakamilika katika muda wa miaka ishirini na tatu (23), na Mwenyezi Mungu akamuamuru kukikusanya na kukipanga kama kilivyo hivi sasa. Ndio, Mtume(s.a.w.w)
alikuwa akipangilia na kuiwekea nidham Dini ya Waislaam na Dunia yao, na alikuwa akiwafundisha kitabu na hekima na akiwabainishia kanuni za ibada na twaa (utiifu) na maingiliano kati yao na uwiano wa kijamii na siasa, uchumi na mengine mengi.
Na baada ya Dini kukamilika- kwa kumtawalisha Ali bin Abi Twalib
Amirul muuminiin na Imam wa wachamungu na khalifa wa Mtume(s.a.w.w)
baada yake na hili kufanyika katika siku ya Ghadiir tarehe kumi na nane (18) ya mwezi wa Dhil-hajjil haraam katika mwaka wa hijja ya kuaga na kumshukia kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ﴿٣﴾
Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini
.
Mtume(s.a.w.w)
aliugua ogonjwa mdogo na wa kawaida tu, lakini maradhi au ugonjwa ule ukawa ukizidi na kuongezeka hadi kuaga Dunia na kurejea kwa mola wake tarehe ishirini na nane (28) ya mwezi wa Safar mwaka wa kumi na moja (11) hijiria, na wasii wake pia khalifa wake baada yake kusimamia jukumu la kuandaa mazishi yake nae ni Amirul muuminiin Ali
na kumzika katika chumba chake kwenye mji mtukufu wa Madina mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake tukufu kwa hivi sasa.
Hakika Mtume(s.a.w.w)
katika hali zake zote na katika maisha yake yote alikuwa ni mfano wa hali ya juu katika uaminifu, utakasifu wa moyo (ikhlaas), ukweli, utekelezaji wa ahadi, uzuri wa tabia, ukarimu, elimu, upole, usamehevu, ulain, ukarimu, ushujaa, uchamungu, zuhudi (kujiepusha na ladha au anasa za kidunia), unyenyekevu, na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na alikuwa ni mwenye kusifika kwa uzuri wa maumbile ya kimwili na alikuwa ni mzuri: uzuri wenye kulingana na umbile lake na unao nasibiana na umbile hilo, uso wake ulikuwa ni wenye kumeremeta na wenye nuru sana kama mbalamwezi yenye kuangaza katika usiku wa ukamilifu wake, kama ambavyo moyo wake mtukufu na roho yake ya hali ya juu na kubwa vilikuwa vimefikia kileleni mwa ukamilifu wa kiroho, kama upatikanao kwenye tabia na maadili, na sira yake pia sunna au mienendo yake ni nyeupe yenye kutoa miali kama jua lenye kuangaza katika nusu ya mchana.
Kwa sura ya ujumla, hakika Mtume(s.a.w.w)
alikuwa amekusanya ubora wote na fadhila zote na alikuwa ndio mahala pa utukufu na ukarimu na kitongoji cha elimu, uadilifu, uchamungu na ubora, na alikuwa ndio ofisi ya mambo ya Dini na Dunia na Dunia na Akhera, hakutokea kuwepo mfano wake kati ya walio tangulia na hata tokea mfano wake hadi milele. Huyu ndie Mtume wa Waislaam na hii ndio Dini ya kiislaam, hakika Dini yake ni Dini bora kuliko Dini zote, na kitabu chake ni bora kuliko vitabu vyote, kwani ni kama vile Mwenyezi Mungu alivyo sema:
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ ﴿٤٢﴾
Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa
.
UIMAM
Na Uimam - kama walivyo uarifisha - ni uongozi wa jumla katika mambo ya Dini na Dunia, na uongozi huo (uraisi) unakuwa ni wa mtu mmojawapo kati ya watu akiwa ni naibu wa Mtume(s.a.w.w)
na Uimam ni wajibu kuwepo kwa hukumu ya akili, kwa sababu Uimam ni (lutfu) huruma ya Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunafahamu kwa yakini ya kuwa watu wanapo kuwa na Raisi mwenye kuwaongoza na kuwaelekeza watu na mwenye kusikilizwa na kutiiwa na anae chukua haki ya mwenye kudhulumiwa kutoka kwa dhalimu na kumzuwia dhalimu kufanya dhulma yake watu hao watakuwa karibu zaidi na maisha mema na saada, na watakuwa mbali zaidi na ufisadi na uovu
.
Na bahthi ya Uimam ni miongoni mwa bahthi zinazo fuatia bahthi ya Utume na ni matawi yake, kwa sababu Uimam ni uendelezaji wa kazi ya Utume na kubakia kwake, na ni wajibu katika Uimam yote yaliyo wajibu kwenye Utume kama Ismah na utwaharifu, na kwamba ni lazima Imam ateuliwe na Mwenyezi Mungu mtukufu kwa Nasi (dalili ya wazi) na kumuainisha kwa jina, na kwa neno moja ni kuwa Imam anashirikiana pamoja na Mtume katika kila kitu isipokuwa wahyi (ufunuo), kwani Imam hatelemshiwi wahyi. Kwa hivyo basi: Kama ambavyo Mwenyezi Mungu mtukufu anavyo wateua na kuwachagua mitume na manabii vivyo hivyo maimam na mawasii wa Mtume na makhalifa wake.
Na kwa hakika alimuainisha na kumteulia Mtume wetu Mohammad(s.a.w.w)
mawasii na makhalifa kumi na mbili (12) na hawa ndio maimam kumi na mbili walio mashuhuri kwa waislaam wote
nao ni hawa wafuatao kwa utaratibu wao.
1.
Imam Amirul muuminiin Ali bi Abi Twalib
mtoto wa ami yake Mtume(s.a.w.w)
na mume wa binti yake Fatuma
.
2.
Imam Hassan bin Ali
na mama yake ni Fatuma binti Mohammad(s.a.w.w)
.
3.
Imam shahidi Hussen bin Ali
na mama yake ni Fatuma bint Mohammad(s.a.w.w)
.
4.
Imam Zainul aabidina: Ali bin Hussen
.
5.
Imam Baaqir
: Mohammad bin Ali
.
6.
Imam Swaadiq: Jaafar bin Mohammad
.
7.
Imam Kaadhim: Mussa bin Jaafar
.
8.
Imam Ridhaa: Ali bin Mussa
.
9.
Imam Jawaad: Mohamma bin Ali (a.s).
10.
Imam Al-hadiy: Ali bin Mohammad
.
11.
Imam Askariy: Hassan bin Ali
.
12.
Imam Mahdiy: Mohammad bin Hassan Al-qaaim (atakae simama) na mwenye kungojewa (Mwenyezi Mungu aharakishe faraji yake na kudhihiri kwake), na hawa maimam ndio hoja wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wote na makhalifa wa Mtume wake(s.a.w.w)
walio barikiwa, nao wote wanatokana na nuru ya Mtume(s.a.w.w)
, na walikuwa kama Mtume(s.a.w.w)
katika elimu, upole, na fadhila, zuhdi (kuitupamkono dunia), uadilifu, Ismah,tabia njema na tabia bora, na sifa zingine njema. Vipi wasiwe na sifa kama hizo? Ili hali wao ni makhalifa wake na mawasii wake na maimamu wake (viongozi) kwa viumbe wake na hoja za Mwenyezi Mungu juu ya viumbe (wanadamu) wote baada yake. Na ufuatao ni muhtasari wa historia ya kila mmoja kati yao
na historia ya binti wa Mtume(s.a.w.w)
mke wa wasii wa Mutme(s.a.w.w)
Fatuma Zahraa
.
BINTI WA MTUME FATIMA ZAHRAA
Yeye ni Fatima Zahraa
baba yake ni Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
Mohammad bin Abdillah, na mama yake ni Sayyidah Mtukufu Khadijah
mama wa waumini, na mumewe ni bwana na wasii wa Mtume Ali Amirul muuminiin, na watoto wake pia wajukuu wake ni maimam watwaharifu
.
Alizaliwa
tarehe (20) ya mwezi wa Jamaddul-akhir mwaka wa (45) tangu kuzaliwa Mtume(s.a.w.w)
na alikufa shahidi akiwa ni mwenye kudhulumiwa tarehe 3 Jamaadul Aakhir
siku ya juma nne mwaka wa kumi (11) hijiria akiwa na umri wa miaka (18) katika umri wa kuchanua maua waridi (yaani katika umri wa ujana wake). Na Amirul muuminiin ndie alie simamia suala la kuandaa mazishi yake na kumzika katika mji wa madina na kulificha kaburi lake kutokana na usia wake ikiwa ni hoja kutokana na dhuluma aliyo fanyiwa na haki yake iliyo porwa na kuchukuliwa kwa nguvu. Na Fatima alikuwa kama baba yake katika ibada na uchamungu na ubora na Zuhdi, na Mwenyezi Mungu aliteremsha aya kadhaa kuhusiana na hadhi yake (kuhusiana nae)
.
Na Mtume(s.a.w.w)
ndie alie muita kwa laqabu (jina mashuhuri) ya (Sayyidatu nisaail aalamiin) Mbora wa wanawake wa ulimwenguni, na kumuita kwa kunia ya Ummu abiiha (Mama wa baba yake) na alikuwa akimpenda sana na kumtukuza sana na kwa kiwango kikubwa, hata ilifikia hatua kwamba anapo ingia kwa Mtume humkaribisha na kusimama kwa heshima yake na kumkalisha mahala pake na pengine alikuwa akiibusu mikono yake na Mtume(s.a.w.w)
alikuwa akisema: Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwa maridhio ya Fatima na anachukia kwa kuchukia Fatima
. Alimzalia Amirul muuminiin
watoto wafuatao: Imam Hassan
na Imam Hussen
na Muhsin
lakini Muhsin mimba yake ilitoka kabla ya muda wake kutokana na maudhi na masaibu yaliyo mfika mama yake, na Sayyidatu Zainab
na Sayyidah Ummu kuluthuum
.
IMAMA WA KWANZA IMAM AMIRUL MUUMINIIN (a.s)
Yeye ni Ali bin Abi Twalib
, na mama yake ni Fatuma binti Asad
nae ni mtoto wa Ami yake Mtume wa Allah(s.a.w.w)
na mume wa binti yake na wasii wake na khalifa wake kwa watu baada yake, Amirul muuminiin na baba wa maimam
. Alizaliwa ndani ya Kaaba tukufu katika mji wa Makkah, siku ya ijuma tarehe kumi na tatu (13) ya mwezi wa Rajab baada ya miaka thalathini (30) tangu kuzaliwa kwa Mtume(s.a.w.w)
na alikufa shahidi usiku wa siku ya ijumaa katika msikiti wa Al-kufa katika mihrab, kwa upanga wa Ibnu Muljim Al-muradiy na bwana huyu alikuwa ni miongoni mwa Makhawariji- na ilikuwa ni tarehe kumi na tisa (19) ya mwezi mtukufu wa Ramadhan na kukutana au kurejea kwa mola wake baada ya siku tatu tangu apate dharuba lile na alikufa shahidi katika usiku wa tarehe (21) akiwa na umri wa miaka sitini na tatu (63), na maimam wawili Hassan na Hussen
ndio walio simamia suala la mazishi yake na kumzika katika mji wa Najaful-ashraf mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake hivi leo na kulificha kaburi lake kutokana na usia wake
, ili liwe katika amani kutokana na mashambulizi ya makhawariji na wenye kulitembelea kaburi lake wasiweze kulifikia na kunufaika kwa kufanya hivyo
kisha imam Swadiq
akalitambulisha kwa watu pia imam Kaadhim
.
Na anazo fadhila na sifa nyingi sana na zisizo hesabika, hakika yeye alikuwa ndie mtu wa kwanza kumuamini Mtume(s.a.w.w)
na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu hata chembe na wala hakusujudia sanamu kamwe na kutokana na hilo ndio maana ikasemwa kuwa linapo tajwa jina lake yasemwe maneno yafuatayo:Karrama llahu wajhahu (yaani Mwenyezi Mungu autukuze uso wake) na ushindi katika vita ulikuwa umefungamanishwa na bendera yake katika vita vyote, mwenye kusimama madhubuti na asie kimbia vitani, hakugeuka nyuma katika vita na wala hakukimbia kamwe na kutokana na hukumu zake nzuri (au uzuri wa utoaji wa hukumu wa Ali Mtume akasema kuhusia nae:
أقضاکم عليّ
Hakimu bora zaidi kati yenu ni Ali
.
Na kutokana na wingi wa elimu yake Mtume(s.a.w.w)
akasema:
أنا مدینة العلم وعليّ بابها
Mimi ni jiji la elimu na Ali ni mlango wake
.
Na kutokana na kushikamana kwake na haki Mtume akasema:
عليّ مع الحق والحق مع عليّ
Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali
.
Na alikuwa ni muadilifu kwa watu wake, akitoa haki kwa sawa, mwenye kujiepusha na mali za kidunia, na alikuwa akija na kuingia kwenye hazina ya Waislaam (Baytul mali) na kuziangalia Dhahabu na Fedha na kusema:
یا صفراء ویا بیضاء غرّي غیري
Ewe mwenye rangi ya manjano (Dhahabu) na ewe mwenye rangi nyeupe (Fedha) mghuri (mdanganye) mwingine tofauti na mimi
.
Kisha kuzitawanya kwa watu na habakishi hata tembe moja, na alikuwa akiwahurumia masikini na akikaa pamoja na mafukara na kukidhi haja za watu na akizungumza maneno ya haki na kweli na kuhukumu kwa uadilifu na kuhukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu.
Na alikuwa akitekeleza hukumu za Mwenyuezi Mungu, na akifuata mwenendo wa Mtume wa Allah(s.a.w.w)
mpaka kheri ikaenea sehemu zote na baraka kutangaa na maisha bora na yenye neema (mazuri) kuwaenea waja wote na katika miji yote.
Kwa ufupi ni kuwa: Yeye
alikuwa kama Mtume(s.a.w.w)
katika sifa zote na mambo yote, isipokuwa katika suala la Wahyi na Utume na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu akamfanya katika aya ya maapizano (Mubahala) sawa na nafsi ya Mtume(s.a.w.w)
.
IMAM WA PILI: IMAM MUJTABA (a.s)
Yeye ni Haassan bin Ali
bin Abi Twalib, na mama yake ni Fatima Zahraa
binti Mohammad(s.a.w.w)
nae ni mjukuu mkubwa wa Mtume(s.a.w.w)
na ni khalifa wake wa pili na Imam wa watu baada ya baba yake Amirul muuminiin
.
Amezaliwa katika mji wa Madinatul munawwarah siku ya juma nne katikati ya mwezi wa Ramadhan mwaka wa tatu wa hijiria, na alikufa shahidi kwa sumu ambayo alitegeshewa na Muawia bin Abi Sufyaan kupitia mkewe Imam Hassan ambae ni Juudah binti Ash'ath na hilo lilifanyika siku ya Al-khamisi tarehe saba (7) ya mwezi wa Safar
mwaka wa (50) hijiria, na alisimamia mazishi yake ndugu yake Imam Hussen
na kumsitiri katika makaburi ya Bakii'i katika mji wa Madinatul munawwarah, mahala ambapo ndipo kilipo kiwiliwili chake kwa hivi sasa (ndipo mahala lilipo kaburi lake) na-kwa masikitiko makubwa - kaburi lake lilivunjwa na Mawahabi pia walivunja kuba la kaburi lake hilo.
Na Imam Hassan
alikuwa ni mfanya ibada kwa wingi kati ya watu wa zama zake na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na mbora na alikuwa ni mwenye kumfanana sana Mtume(s.a.w.w)
, na alikuwa ni mkarimu zaidi kati ya Ahlul bayti wake katika zama zake na alikuwa ni mwenye huruma zaidi.
Na miongoni mwa ukarimu wake
ni kuwa alipewa mafuta uzuri na mjakazi mmoja wapo kati ya vijakazi wake, akasema kumwambia mjakazi yule: Wewe uko huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha akasema: Hivi ndivyo alivyo tuadabisha Mwenyezi Mungu pale alipo sema:
وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ﴿٨٦﴾
Mnapo amkiwa kwa maamkizi basi itikieni kwa maamkizi mazuri zaidi kuliko mliyo amkiwa au rudisheni kwa yale maamkizi mliyo amkuliwa
.
Na miongoni mwa upole wake
ni kuwa mtu mmoja wa Sham alimuona akiwa amepanda mnyama, yule bwana akawa akimlaani Imam na Imam hakumjibu kwa chochote, yule bwana alipo maliza kutoa laana zake na matusi yake Imam Hassan akamwendea na kusema:
Ewe shekh nadhani ni mgeni na huenda umenifananisha, lau unge omba tukuridhishe basi tunge kuridhisha, na lau kama unge tuomba kitu fulani tunge kupatia na lau kama unge taka tukuongoze tunge kuongoza na lau unge tutaka tukubebee mzigo wako tunge kubebea na ikiwa unanjaa tunge kushibisha na kama unge kuwa uchi tunge kuvisha na kama ni muhitaji tutakutajirisha na ikiwa umefukuzwa tutakuhifadhi na kukusitiri na ikiwa unahaja tutaitatua haja yako
.
Yule bwana alipo sikia maneno yale alilia na kusema: Nina shuhudia ya kuwa wewe ni Khalifa wa Mwenyezi Mungu katika Ardhi yake, hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kufahamu vema mahala pa kuuweka ujumbe wake.
IMAM WA TATU: IMAM SHAHIID (a.s)
Yeye ni Hussen bin Ali bin Abi Twalib
na mama yake ni Fatima binti Mohammad(s.a.w.w)
nae ni mjukuu wa Mtume(s.a.w.w)
na Khalifa wake wa tatu na baba wa maimam tisa walio kuja baada yake na ni Imam wa watu baada ya nduguye au kaka yake Hassan
.
Alizaliwa katika mji wa Madinatul-munawwarah tarehe tatu (3) ya mwezi wa Shaaban mwaka wa nne hijiria na kuuwawa kwa dhulma kwa upanga hali ya kuwa ni mwenye kiu, mauaji yaliyo fanya na bani Umayyah kwa amri ya Yazid bin Muawia katika tukio mashuhuri la Ashura, siku ya juma mosi tarehe kumi (10) ya mwezi wa Muharram mwaka (61) hijiria, na jeneza lake pia kiwiliwili chake kitwaharifu na kilicho katwa katwa kwa mapanga pamoja na viwiliwili vingine vya mashahidi walio kufa mashahid pamoja nae vilizikwa baada ya siku tatu tangu kuuwawa kwao wakiwa mashahidi na alaie mzika ni mwanae Imam Zainul aabidiin
na kumzika mahala ambapo ndipo kaburi lake lilipo hivi sasa katika mji mtukufu wa Karbalaa, mji ambao uliangukia mikononi mwa Saddam na kundi lake na Mwenyezi Mungu kuukomboa kutoka mikononi mwao-pamoja na sehemu zingine tukufu zilizoko Iraq.
Na fadhila zake ni nyingi sana kiasi kwamba ni vigumu kuweza kuzitaja zote, kwani yeye ni ua zuri la Mtume(s.a.w.w)
ambae Mtume alisema kuhusiana na yeye:
حسین مني وأنا من حسین
Hussein anatokana na mimi na mimi natokana na Hussen
.
Na pia amesema kuhusiana nae na kuhusu nduguye Hassan
:
هما ریحانتاي من الدنیا
Wao wawili ni maua yangu mazuri duniani
.
Pia amesema(s.a.w.w)
:
الحسن والحسین سیدا شباب أهل الجنّه
Hassan na Hussedin ni mabwana wa vijana wa peponi
.
Pia amesema(s.a.w.w)
:
الحسن والحسین إمامان إن قاما وإن قعدا
Hassan na Hussein ni maimam sawa wakiwa wamesimam au wamekaa
.
Na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na mfanya ibada sana kati ya watu, hakika alikuwa akisali kila usiku rakaa elfu moja kama baba yake Amirul muuminiin
na mara nyingi alikuwa akibeba mfuko wa ngozi wenye vyakula usiku na kuwapelekea mafakiri hadi ilionekana alama na athari yake mgongoni mwake baada ya kuuliwa na alikuwa ni mkarimu, mtukufu, mpole, na alikuwa mkali sana pindi anapo asiwa Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwa ukarimu wake ni pale alipojiwa na bedui mmoja akimuomba na kumuimbia shairi lisemalo: Hakwenda kombo kwa hivi sasa mwenye kukuelekea kwa matarajio na alie bisha mlangoni kwa mara kadhaa, wewe ni mkarimu na wewe ni mwenye kutegemewa, baba yako alikuwa ni muuaji wa mafasiki, lau kama si yule ambae alikuwa mwanzoni mwenu, basi sisi sote tunge enewa na kuzungukwa na moto wa jahannama.
Imam Hussen akampatia dinari elfu nne na akmuomba msamaha kwa kusema: Zichukue hakika mimi nakuomba samahani na fahamu ya kuwa mimi ni mwenye huruma sana kwako, lau kama mwendo wetu kesho ungekuwa ni mwema, na anga letu lingekumiminia kheri nyingi, lakini matatizo ya zama ni ya aina tofauti na yenye kubadilika kwa hivyo na mkono wangu ni wenye kutoa kidogo. Na kwa hakika Imam
kwa kisimamo chake cha kishujaa-na ambacho hakina mfano katika ulimwengu-aliweza kuihuisha sheria ya kiislaam na dini ya babu yake Mtume(s.a.w.w)
bali aliuhuisha ulimwengu wote hadi siku ya kiama, kwa hivyo yeye ni bwana wa mashahidi na ni mtu bora baada ya kaka yake na nduguye Hassan
.