MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO0%

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO Mwandishi:
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

Mwandishi: AYATULLAHI: SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY
Kundi:

Matembeleo: 9441
Pakua: 3585

Maelezo zaidi:

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 9441 / Pakua: 3585
Kiwango Kiwango Kiwango
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

Mwandishi:
Swahili

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY

HUKUMU ZA KIISLAAM PAMOJA NA USUULUD-DIN- FURUUD-DIN- UBORA WA QUR'ANI TUKUFU- MFUMO WA UTAWALA KATIKA UISLAAM- MAMBO YA WAJIBU- HARAAM- MAADILI NA MAS'ALA MAPYA

KWA MUJIBU WA FAT'WA ZA AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY (Mungu amzidishie uhai)

Ni wajibu kwa mukallaf kujifunza mas'ala ambayo anayahitajia sana katika maisha yake ya kila siku. (Mas'ala 12)

UTANGULIZI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu. Sifa zote njema ni za Allah mola wa viumbe wote na sala na salam ziwe juu ya mbora wa viumbe wote, Mohammad Mustafa na kizazi chake kilicho twahara, na laana iwe juu ya maadui zao wote milele na milele. Amma baad: Inampasa kila muislaam asitosheke katika uislaam wake kwa kuwa na jina pekee la Uislaam (kwa kusema mimi ni Muislaam) na katika Qur'ani asitosheke kwa kusoma na kuwa na maandishi ya Qur'ani pekee, bali ni vema kwake kuufanyisha kazi Uislaam na kutekeleza hukumu za Qur'ani katika maisha yake yote na katika mambo yake yote, (yawe ni mambo yake binafsi, kimajii, kiuchumi, na kisiasa na mengineyo), ili awe Muislaam kwa maana halisi ya neno Uislaam, awe mtu mwema na mwenye kufaulu katika dunia na mwenye kufuzu na mwenye kuneemeka katika Akhera.

Na ni jambo lililo wazi kuwa saada ya Dunia na kufaulu katika Akhera, vitu hivi havipatikani kwa kushikamana na jina pekee na wala havipatikani kwa maombi pekee (Dua) bali jambo liyafanikishalo na kuyathibitisha kwa Muislaam ni kufanya matendo kwa mujibu wa mafunzo ya kiislaam na kutekeleza hukumu za Qur'ani za sawa na zenye kuleta maendeleo-baada ya kuwa na itikadi madhubuti ya Usulud-dini (misingi ya dini) ya kiislaam itikadi za kweli na za haki.

Kutokana na haya inamlazimu kila Muislaam anae taka kuishi maisha mema na yenye mafanikio katika Dunia na anataka mafanikio na awe ni mwenye kufaulu na mwenye neema katika Akhera- na sisi sote tunayataka ahayo-afanye juhudi za kujifunza itikadi zilizo sahihi na za haki za Uislazam na kuyatambua pia kuyaelewa mafunzo ya hali ya juu na mazuri ya Uislaam na kuzifahamu vema hukumu za Qur'ani zilizo madhubuti na za kiwango cha juu, kisha kuitakidi kimadhubuti kabisa itikadi ya kweli na kutekeleza matendo kwa wakati wote kwa mujibu wa mafunzo ya kiislaam na kutekeleza kiukamilifu hukumu za Qur'ani, hadi kufikia hatua ya kukusanya au kuoanisha kati ya jina na mwenye jina, na hivyo kuwa waislaam wenye kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na kwa Mtume wake(s.a.w.w) na tuwe ni wenye kuridhiwa kwa Ahlul bayti wake Mtume walio Maasuuminiin(a.s) na ili tuwe miongoni mwa watu wenye saada katika Dunia na wenye kufaulu katika Akhera.

Na ufuatao ni utangulizi ubainishao mambo ambayo ni wajibu kwa Muislaam kuyafahamu katika uwanja huu, na kwa muhtasari tunasema kama ifuatavyo: Hakika mafunzo matukufu na ya kiwango cha juu kabisa ya Uislaam na hukumu zenye kupea za Qur'ani yanagawanyika kwa muhtasari katika makundi matatu yafuatayo:

1. Usulud-din (Misingi ya dini)

2. Furuud-din (Matawi ya dini)

3. Maadili (Tabia Akhlaaq na adabu za kiislaam).

Kwa hivyo basi mwenye kuitakidi Usuulud-din na kufanya matendo yake kwa mujibu wa Furuud-din na kujipamba kwa maadili na adabu za kiislaam, atakuwa ni mtu mwenye saada katika nyumba mbili (Duniani na Akhera), na atapata faida katika sehemu mbili hizo na ataishi hali ya kuwa ni mwema na mwenye saada na kufa hali ya kuwa ni mwenye kusifiwa, na ufuatao hivi sasa ni ufafanuzi kwa ufupi wa kila moja kati ya makundi matatu haya tuliyo yataja.

1

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

AYATULLAHIL- UDHMAA SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY

KIFUNGU CHA KWANZA

USULUD-DIN (MISINGI YA DINI)

1. TAWHIID (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu)

2. AL-ADLU (Uadilifu wa Mwenyezi Mungu)

3. AN-NUBUWWATU (Utume)

4. AL-IMAMATU (Uimamu)

5. AL-MA'AAD (Marejeo ya kiama)

1. TAWHIID (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu)

Tawhiid: ni mwanadam kufahamu ya kuwa ulimwengu unae muumba alie uumba na kuufanya uwepo baada ya kuto kuwepo na ni mwenye kila kitu.. kama uumbaji, utoaji wa riziki na utoaji wa neema na mzuiaji mwenye kuhuisha na kufisha na mwenye kutoa swiha na ugonjwa , yote hayo yako chini ya utashi wake. Amesema mwenyezi Mungu mtukufu:

إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾

(Hakika si jambo jingine pindi atakapo jambo au kitu chochote huliambai kuwa na likawa).

Na dalili juu ya kuwepo kwa Mwenyezi mungu mtukufu: Ni vitu tuvionavyo mbingu na vilivyomo ndani ya mbingu hiyo, kama jua lenye kuangaza na mwezi wenye kutoa nuru na nyota zenye kumeremeta na mawingu, pepo na mvua. Pia Ardhi na vilivyomo ndani yake, kama Bahari, Mito, Matunda, Miti, madini ya aina tofauti na yenye thamani kama Dhahabu na fedha na Zamrad na mengineyo.

Na katika aina tofauti za wanyama wenye kupaa angani na wenye kuogelea majini na watembeao nchi kavu (yaani juu ya ardhi), wakiwa ni wa aina tofauti na wenye sauti zenye kutofautiana na ukubwa wenye kushabihiana (kufanana) na usio shabihiana. Na mwanadamu wa ajabu mwenye hisia tofauti au mwenye viungo tofauti vya kuhisia kama kusikia, kuona, kunusa, kuonja, na kugusa na kuwazia na mwenye viungo vingi vingine, kama macho, masiko,ulimi, moyo, mikono miguu, afya, ugonjwa, maridhio, ghadhabu, huzuni, furaha na mengi mengineyo. Yote hayo ni dalili juu ya kuwepo kwa mola mwenye hekima na mjuzi, tunamuitakidi na kumuabudu na kumtegemea kutupa usaidizi na kutawakali kwake.

MWENYEZI MUNGU MTUKUFU NA SIFA ZAKE NJEMA

Mwenyezi Mungu alie takasika anazo sifa nyingi kama:

ELIMU : Yeye ni mwenye kufahamu kila kitu, kikubwa na kidogo na anayafahamu yaliyomo ndani ya nyoyo.

UWEZO : Yeye ni mwenye uwezo juu ya kila kitu, ana uwezo wa kuumba, kutoa riziki, kufisha na kuhuisha na mengineyo.

UHAI : Yeye yu hai hafariki.

UTASHI : Yeye hukitaka kitu ambacho kina maslahi ndani yake na wala hakitaki kitu ambacho ndani yake kuna ufisadi au uharibifu.

KUDIRIKI : Yeye hukiona kila kitu na husikia kila sauti hata kama itakuwa ni kwa kunong'onezana masikioni au wahm (kufikiria).

UTANGU : Yeye Mwenyezi Mungu pekee ndie wa tangu na tangu na ndie wa milele, yaani yeye alie takasika alikuwepo kabla ya kila kitu kisha akaviumba vitu vyote na atabakia kuwepo baada ya vitu hivyo hadi milele na ulimwengu wote huu ni miongoni mwa uumbaji wake, au ni viumbe vyake, viumbe hivyo ni vyenye kumuhitajia si katika kupatikana kwake pekee bali katika kubakia kwake na kuendelea kuwepo kwa vitu hivyo pia, na kila kilicho umbwa basi kitu hicho ni chenye kuzuka, kwa hivyo basi hakuna wa tangu na tangu isipokuwa Mwenyezi Mungu mtukufu.

KUZUNGUMZA : Yeye Mwenyezi Mungu ni mwenye kuzungumza, humsemesha amtakae katika waja wake wema walio takasika na kutakaswa, mitume wake na malaika wake.

UKWELI : Yeye ni mkweli katika yale ayasemayo na hakhalifu ahadi zake (yaani haendi kinyume na ahadi zake), kama ambavyo yeye alie tukuka ni muumba, mtoaji wa riziki, muhuishaji, mtoaji, mzuiaji, mwenye huruma, msamehevu, mtukufu, mbora na mkarimu , n.k

MWENYEZI MUNGU AMETAKASIKA NA SIFA MBAYA

MWENYEZI MUNGU ALIE TAKASIKA NA KUTUKUKA AMEEPUKIKA NA SIFA ZA UPUNGUFU

Mwenyezi Mungu si mwenye kiwiliwili na wala si murakkab (yaani hakuunganika kwa sehemu tofauti) hana sehemu wala mahala maalum. Na haiwezekani kumuona Mwenyezi Mungu mtukufu, si katika Dunia wala Akhera, na wala hatokewi na mabadiliko, hapatwi na kiu, hashikwi na njaa, hazeeki hamaliziki, hashikwi na mghafala wala kulala. Na hana mshirika wala mwenza, bali yeye ni mmoja na wa pekee, mmoja mwenye kutegemewa, hana mke wala mtoto. Na sifa zake ndio dhati yake yenyewe, hakuna uwili kati yake na sifa zake, yeye ni muweza mjuzi hadi mwisho wa sifa zake njema kuanzia tangu na tangu, si kama sisi, kwani tulikuwa ni wajinga kisha tukajifunza na hatukuwa ni wenye uwezo kisha tukawa ni wenye uwezo. Na yeye ni ghanii (tajiri na mwenye kujitosheleza) na hakihitajii chochote na yeyote, hahitaji ushauri wa yeyote, au msaidizi au waziri, au askari na mfano wa hayo.

2. UADILIFU WA ALLAH

Maana yake ni kuwa: Mwenyezi mungu ni muadilifu hamdhulumu yeyote na hafanyi mambo yaliyo kinyume na hekima, kwa hivyo uumbaji wote, na utoaji wa riziki, utoaji na uzuiaji, vyote hivyo vimefanyika kutokana na maslahi au hufanyika kwa maslahi hata kama hatuyajui maslahi hayo, kama ambavyo Daktari anapo mtibu mtu fulani kwa kumpatia dawa fulani hufahamu ya kuwa dawa hiyo inamanufaa hata kama hatukufahamu maslahi yenyewe yaliyomo kwenye dawa hiyo. Kwa hivyo basi tutakapo ona ya kuwa Mwenyezi Mungu amemtajirisha mtu fulani au mtu fulani amemtia ufukara, au mtu fulani amemfanya kuwa mtukufu (sharifu) na mwingine hakumfanya hivyo, au amemtia ogonjwa mtu fulani na hakumfanya mtu mwingine kuwa mgonjwa, na mfano wa hayo, nilazima kuitakidi ya kuwa yote hayo yamefanyika kutokana na maslahi na hekima hata kama hatufahamu hekima yake na maslahi yake.[1]

Na imepokelewa katika hadithi kuwa: Mussa(a.s) alimuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amfahamishe na kumtambulisha sehemu fulani ua uadilifu wake kati ya mambo ambayo dhahiri yake ni mushkeli (ni tatizo kuyaelewa), Mwenyezi Mungu akamuamrisha aende kwenye kisima chenye chemchem jangwan, ili akaangalie ni kitu gani kitafanyika huko, pindi Mussa(a.s) alipo toka alimuona mpanda farasi akija na kufika kwenye kisima hicho na kutelemka kutoka juu ya farasi wake na kukidhi mahitaji yake sehemu hiyo, na baada ya kumaliza alianza safari na kuondoka na kusahau mfuko wake wa pesa sehemu hiyo, kisha baada ya muda fulani akaja mtoto mdogo aliekuwa mumayyizi (yaani mwenye kutambua mambo) mtoto yule aliuona mfuko ule ukiwa umedondoka chini pembezoni mwa kisima kile, akauokota kwa furaha kubwa na kuondoka kwa haraka kurejea aliko toka, kisha baada ya muda akaja kipofu kwa ajili ya kutawadha kwenye kisima kile, ghafla yule mpanda farasi akarudi na kufika mahala pale huku akitafuta mfuko wake wa pesa, baada ya kuutafuta na kutouona akamtuhumu yule kipofu ya kuwa ndie alie chukua na kukapita mvutano kati yao, mvutano ulio pelekea yule bwana kumuua kipofu na yule mpanda farasi kujificha na hapo Mussa akastaajabu kutokana na yale aliyo yaona na kushangaa sana, Mwenyezi Mungu mtukufu akamtelemshia wahyi kwa mambo yaliyo ondoa mshangao wake, kwani alimwambia: Mpanda farasi alikuwa ameiba mali ya baba wa yule mtoto, kwa hiyo ile mali tukairudisha kwa mrithi ambae ni yule mtoto ambae umemuona, na yule kipofu alikuwa ni muuaji wa baba wa mpanda farasi, kwa hiyo mrithi akachukua haki yake na kulipiza kisasi kwa kipofu yule.[2]

Na hivyo ndivyo hukumu ya Mwenyezi Mungu inavyo kuwa na uadilifu wake japokuwa kwa mtazamo wa juu juu jambo hilo liko mbali na kanuni.

3. UTUME

Mwenyezi Mungu alie takasika alipo muumba mwanadam, alimtakia mwanadam huyo saada na kheri katika Dunia na neema pia pepo katika Akhera na haya hayathibiti na kupatikana isipokuwa mwanadam huyu atakapo kuwa na mipango au program inayo kwenda sambamba na akili yake na maumbile yake na awe na mfumo unao wiana na roho yake na kiwiliwili chake, na program hiyo au mpango huo uziguse na kuyahusu mambo yote au mahitaji yote ya akili na maumbile, na uwe ni mfumo ulio kamili na wenye kukidhi matakwa yote ya kiroho na kimwili, haiwezekani kuwekwa kanuni hiyona mtu mwingine isipokuwa na muumba wa huyu mwanadam mwenye ujuzi wa matakwa na mahitaji yote ya mwanadam na vitu avipendavyo.

Na kutokana na ukweli kuwa ni Mwenyezi Mungu alie mtakia mwanadam saada wakati alipo muumba, basi ilikuwa ni juu yake kuipanga program na kuuweka mpango huo unao zihusu na kuzigusa sehemu zote za mwanadam (kiroho na kimwili) na kuweka mfumo ulio kamili uwezao kumfikisha mwanadam kwenye saada hiyo, kisha mfumo na program hiyo kuituma na kuifikisha kwa watu kupitia kwenye mikono ya watu waaminifu kati ya viumbe wake na waja wake walio hifadhiwa na utendaji wa makosa au kukosea na kusahau na walio twahirishwa kutokana na aibu mbalimbali na madhambi, nao si wengine bali ni manabii na mitume. Kwa msingi huo: Nabii ni mtu ambae Mwenyezi Mungu humtelemshia wahyi (humletea ufunuo kutoka kwake) kwa maana hiyo ni kuwa Nabii au Mtume hutoa habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu bila kuwepo kiunganishi cha kiumbe yeyote, na manabii wamegawanyika makundi mawili:

1. Nabiyyun mursal: (Nabii alie tumwa): Huyu ni yule Nabii alie tumwa kwa ajili ya kuwaokoa watu, kutoka kwenye kiza hadi kwenye nuru na kuwatoa kwenye batili hadi kwenye haki na kuwatoa kwenye mambo ya kupanga yasiyo na ukweli wala uhakika na kuwafikisha kwenye uhakika wa mambo, na kuwatoa kwenye ujinga na kuwafikisha kwenye elimu.

2. Nabiyyun ghayri mursali: (Nabii asie tumwa) Nae ni yule ambae hutelemshiwa wahyi kwa ajili yake mwenyewe na hakuamrishwa kufikisha hukumu kwa watu.

Na idadi ya mitume ni laki moja na ishirini na nne elfu (124000) na kati ya hao walio tumwa kufikisha hukumu kwa watu ni wachache. Na Mtume wa kwanza ni Aadam(a.s) na wa mwisho wao ni Mohammad(s.a.w.w) . Na manabii walio tumwa kufikisha ujumbe wamegawanyika makundi mawili:

1- Ulul-azmi

2- Wasio Ulul-azmi. Ulul-azmi: ni wale ambao walitumwa na Mwenyezi Mungu mtukufu katika ardhi hii kuanzia mashariki hadi magharibi na kwa watu wote, nao ni watano.

1. Ibrahiim(a.s) .

2. Nuhu(a.s) .

3. Mussa(a.s) .

4. Issa(a.s) .

5. Mohammad(s.a.w.w) .

Na Mayahudi ni miongoni mwa wafuasi wa Mussa(a.s) , Wakiristo ni miongoni mwa wafuasi wa Issa(a.s) na Waislaam ni wafuasi wa Mohammad(s.a.w.w) .

Lakini Uislaam ulifuta Dini zote zilizo tangulia, kwa hivyo basi haijuzu kuendelea kufuata Dini hizi bali ni lazima kwa watu wote kufuata mafunzo ya Uislaam kama Mwenyezi Mungu mtukufu alivyo sema:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri[3] .

Kwa hivyo basi Uyahudi na Ukiristo ni batili, na Uislaam unabakia kuwa ndio sheria ya Mwenyezi Mungu hadi siku ya kiama na haitafutwa kamwe milele na milele. Na Mitume wasio ulul-azmi: ni wale ambao walitumwa na Mwenyezi Mungu mtukufu kwenye sehemu maalum na nchi fulani au sehemu fulani tu na kwa watu maalum.

MTUME WA MWISHO(s.a.w.w)

Hakika umekwisha fahamu ya kuwa Mohammad(s.a.w.w) ndie Mtume wa mwisho na kwamba dini yake- ambayo ni Uislaam- imefuta Dini zilizo tangulia na kwamba sheria yake itaendelea kuwepo na itabakia hadi siku ya kiama na kwamba ndio sheria pekee yenye uwezo wa kumfikisha mwanadamu kwenye saada na kuyathibitisha matarajio yake na matamanio yake katika maisha ya Dunia na Akhera kama ambavyo Mtume(s.a.w.w) ndie pekee ambae ni kigezo cha wanadamu na kigezo kilicho kamili katika upande wa kheri na mambo ya fadhili (ubora) kwa waislaam wote bali kwa ulimwengu wote ikiwa watajitakia kheri wao wenyewe, kwa kuifuata sera yake na kujipamba kwa tabia yake(s.a.w.w) na kuifahamu sehemu fulani ya historia yake(s.a.w.w) ni lazima kutaja baadhi ya sifa na mwenendo wake [4] . Yeye ni Mohammad bin Abdallah(s.a.w.w) na mama yake ni Aamina binti wahab. Alizaliwa katika mji wa Makkatul mukarramah, siku ya ijumaa tarehe kumi na saba (17) mwezi wa Rabiiul-awwal (mfungo sita) baada ya kuchomoza Al-fajiri mwaka wa tembo katika zama za mfalme muadilifu[5] (Kisraa)

KUPEWA UTUME KWA MTUKUFU MTUME (s.a.w.w)

Mtume(s.a.w.w) alipewa ujumbe wa kiislaam mnamo tarehe (27) mwezi wa Rajabul murajjab baada ya kutimiza miaka (40) katika umri wake mtukufu, kwani alishukiwa na jibrilu(a.s) ambae ni malaika mtukufu na alie karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu na wakati huo Mtume(s.a.w.w) alikuwa katika pango la (Hiraa) nao ni mlima ulioko kwenye mji wa Makka na alitelemka kwake akiwa na aya tano za suratul Alaq kama zifuatazo:

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu[6] .

Baada ya tukio hilo Mtume(s.a.w.w) alisimama kwenye mlima wa Swafa na katika masjidul-haraam na katika makundi ya watu na katika sehemu za makutanio ya watu, kwa ajili kufikisha ujumbe wa mola wake na kuwaita watu na kuwaongoza kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na kumuamini huku akisema:

أَیُّهَا النّاسُ قُولُوا لا اِلهَ الاّ اللّه تُفْلِحُوا

Enyi watu semeni hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mungu mmoja mtafaulu [7] .

Na kutokana na ukweli kuwa watu wa Makkah walikuwa ni washirikina na maraisi (viongozi) wao walikuwa wakiona maslahi yao binafsi yako kwenye shirki na kwa kuogopea maslahi yao wakawa wakimfanyia shere (wakimfanyia istihzaa na kumkebehi pia kumuudhi), na Mtume kila alivyo kuwa akiendelea na kazi yake ya wito wa kuwaongoza washirikina, pia wao waliendelea na kuzidisha maudhi yao kwa Mtume(s.a.w.w) mpaka akafikia hatua ya kusema:

ما أوذی نبي مثل ما أوذیت

Hakuudhiwa Mtume yeyote kama nilivyo udhiwa mimi (au hakuna Mtume yeyote aliepata maudhi mfano wa maudhi niliyo yapata mimi)[8] .

Na hawakumuamini isipokuwa watu wachache, wa kwanza wao akiwa Amirul muuminiin Ali bi Abi Twalib(a.s) na katika wanawake Khadijah binti Khuwailid(a.s) .

Na pindi mashinikizo ya washirikina kwake yalipo kithiri akaamua kuhamia kwenye mji wa Madinah, na kuhama huko au hijira hiyo ndio mwanzo wa tarehe ya Waislaam. Na huko ndiko Waislaam waliko ongezeka na kukithiri na nguvu yao kuongezeka, na kwa ubora wa wafunzo ya hali ya juu ya Mtume na kutokana na sheria ya Uislaam iliyo nyepesi na yenye hekima, wakawa ni mifano bora kabisa katika tabia, maadili na utu, na wakawa ni mifano bora katika utamaduni na wakawa wananchi bora, na kutokana na mafunzo hayo wakawapita na kuzivuka au kuzipituka tamaduni zote za ulimwengu na Dini zote za mbinguni na zisizo za mbinguni.

Na Mtume(s.a.w.w) wakati akiwa katika mji wa Madinatul Munawwarah alitokewa na vita pia mapigano mbalimbali, na vita vyote hivyo vilikuwa ni vita vya kujihami na kujibu uchokozi wa Washirikina, Mayahudi na Wakristo waliyo kuwa wakiyaelekeza kwa Waislaam, na Mtume(s.a.w.w) katika vita vyote akiangalia sana upande wa amani, huruma, usamehevu na ubora (fadhila), kwa hivyo ndio maana utakuta kwamba walio uwawa kati ya pande mbili hizo Waislaam na Washirikina katika vita vyake vya kujihami ambavyo vilifikia Thamanini na zaidi hawakuwa zaidi ya elfu moja na mia nne (1400), kama historia zilivyo nukuu na kusajili kwenye kumbukumbu zake.

2

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

KUFARIKI KWAKE KWENYE KUSIKITISHA NA KUHUZUNISHA

Tangu Mtume(s.a.w.w) alipopewa utume rasmi na kukabidhiwa ujumbe wa kiislaam mpaka kufariki kwake na kuiaga kwake Dunia hii alikuwa akiungwa mkono na wahyi (ufunuo), na Aminul-wahyi Jibraaillu(a.s) alikuwa akishuka kwake akiwa na Qur'ani tukufu au akimletea Qur'ani tukufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kidogo kidogo na katika matukio mbali mbali, hadi kitabu hiki adhiim kikakamilika katika muda wa miaka ishirini na tatu (23), na Mwenyezi Mungu akamuamuru kukikusanya na kukipanga kama kilivyo hivi sasa. Ndio, Mtume(s.a.w.w) alikuwa akipangilia na kuiwekea nidham Dini ya Waislaam na Dunia yao, na alikuwa akiwafundisha kitabu na hekima na akiwabainishia kanuni za ibada na twaa (utiifu) na maingiliano kati yao na uwiano wa kijamii na siasa, uchumi na mengine mengi.

Na baada ya Dini kukamilika- kwa kumtawalisha Ali bin Abi Twalib(a.s) Amirul muuminiin na Imam wa wachamungu na khalifa wa Mtume(s.a.w.w) baada yake na hili kufanyika katika siku ya Ghadiir tarehe kumi na nane (18) ya mwezi wa Dhil-hajjil haraam katika mwaka wa hijja ya kuaga na kumshukia kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ﴿٣﴾

Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini[9] .

Mtume(s.a.w.w) aliugua ogonjwa mdogo na wa kawaida tu, lakini maradhi au ugonjwa ule ukawa ukizidi na kuongezeka hadi kuaga Dunia na kurejea kwa mola wake tarehe ishirini na nane (28) ya mwezi wa Safar mwaka wa kumi na moja (11) hijiria, na wasii wake pia khalifa wake baada yake kusimamia jukumu la kuandaa mazishi yake nae ni Amirul muuminiin Ali(a.s) na kumzika katika chumba chake kwenye mji mtukufu wa Madina mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake tukufu kwa hivi sasa.

Hakika Mtume(s.a.w.w) katika hali zake zote na katika maisha yake yote alikuwa ni mfano wa hali ya juu katika uaminifu, utakasifu wa moyo (ikhlaas), ukweli, utekelezaji wa ahadi, uzuri wa tabia, ukarimu, elimu, upole, usamehevu, ulain, ukarimu, ushujaa, uchamungu, zuhudi (kujiepusha na ladha au anasa za kidunia), unyenyekevu, na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na alikuwa ni mwenye kusifika kwa uzuri wa maumbile ya kimwili na alikuwa ni mzuri: uzuri wenye kulingana na umbile lake na unao nasibiana na umbile hilo, uso wake ulikuwa ni wenye kumeremeta na wenye nuru sana kama mbalamwezi yenye kuangaza katika usiku wa ukamilifu wake, kama ambavyo moyo wake mtukufu na roho yake ya hali ya juu na kubwa vilikuwa vimefikia kileleni mwa ukamilifu wa kiroho, kama upatikanao kwenye tabia na maadili, na sira yake pia sunna au mienendo yake ni nyeupe yenye kutoa miali kama jua lenye kuangaza katika nusu ya mchana.

Kwa sura ya ujumla, hakika Mtume(s.a.w.w) alikuwa amekusanya ubora wote na fadhila zote na alikuwa ndio mahala pa utukufu na ukarimu na kitongoji cha elimu, uadilifu, uchamungu na ubora, na alikuwa ndio ofisi ya mambo ya Dini na Dunia na Dunia na Akhera, hakutokea kuwepo mfano wake kati ya walio tangulia na hata tokea mfano wake hadi milele. Huyu ndie Mtume wa Waislaam na hii ndio Dini ya kiislaam, hakika Dini yake ni Dini bora kuliko Dini zote, na kitabu chake ni bora kuliko vitabu vyote, kwani ni kama vile Mwenyezi Mungu alivyo sema:

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ ﴿٤٢﴾

Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa[10] .

UIMAM

Na Uimam - kama walivyo uarifisha - ni uongozi wa jumla katika mambo ya Dini na Dunia, na uongozi huo (uraisi) unakuwa ni wa mtu mmojawapo kati ya watu akiwa ni naibu wa Mtume(s.a.w.w) na Uimam ni wajibu kuwepo kwa hukumu ya akili, kwa sababu Uimam ni (lutfu) huruma ya Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunafahamu kwa yakini ya kuwa watu wanapo kuwa na Raisi mwenye kuwaongoza na kuwaelekeza watu na mwenye kusikilizwa na kutiiwa na anae chukua haki ya mwenye kudhulumiwa kutoka kwa dhalimu na kumzuwia dhalimu kufanya dhulma yake watu hao watakuwa karibu zaidi na maisha mema na saada, na watakuwa mbali zaidi na ufisadi na uovu[11] .

Na bahthi ya Uimam ni miongoni mwa bahthi zinazo fuatia bahthi ya Utume na ni matawi yake, kwa sababu Uimam ni uendelezaji wa kazi ya Utume na kubakia kwake, na ni wajibu katika Uimam yote yaliyo wajibu kwenye Utume kama Ismah na utwaharifu, na kwamba ni lazima Imam ateuliwe na Mwenyezi Mungu mtukufu kwa Nasi (dalili ya wazi) na kumuainisha kwa jina, na kwa neno moja ni kuwa Imam anashirikiana pamoja na Mtume katika kila kitu isipokuwa wahyi (ufunuo), kwani Imam hatelemshiwi wahyi. Kwa hivyo basi: Kama ambavyo Mwenyezi Mungu mtukufu anavyo wateua na kuwachagua mitume na manabii vivyo hivyo maimam na mawasii wa Mtume na makhalifa wake.

Na kwa hakika alimuainisha na kumteulia Mtume wetu Mohammad(s.a.w.w) mawasii na makhalifa kumi na mbili (12) na hawa ndio maimam kumi na mbili walio mashuhuri kwa waislaam wote[12] nao ni hawa wafuatao kwa utaratibu wao.

1. Imam Amirul muuminiin Ali bi Abi Twalib(a.s) mtoto wa ami yake Mtume(s.a.w.w) na mume wa binti yake Fatuma(a.s) .

2. Imam Hassan bin Ali(a.s) na mama yake ni Fatuma binti Mohammad(s.a.w.w) .

3. Imam shahidi Hussen bin Ali(a.s) na mama yake ni Fatuma bint Mohammad(s.a.w.w) .

4. Imam Zainul aabidina: Ali bin Hussen(a.s) .

5. Imam Baaqir(a.s) : Mohammad bin Ali(a.s) .

6. Imam Swaadiq: Jaafar bin Mohammad(a.s) .

7. Imam Kaadhim: Mussa bin Jaafar(a.s) .

8. Imam Ridhaa: Ali bin Mussa(a.s) .

9. Imam Jawaad: Mohamma bin Ali (a.s).

10. Imam Al-hadiy: Ali bin Mohammad(a.s) .

11. Imam Askariy: Hassan bin Ali(a.s) .

12. Imam Mahdiy: Mohammad bin Hassan Al-qaaim (atakae simama) na mwenye kungojewa (Mwenyezi Mungu aharakishe faraji yake na kudhihiri kwake), na hawa maimam ndio hoja wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wote na makhalifa wa Mtume wake(s.a.w.w) walio barikiwa, nao wote wanatokana na nuru ya Mtume(s.a.w.w) , na walikuwa kama Mtume(s.a.w.w) katika elimu, upole, na fadhila, zuhdi (kuitupamkono dunia), uadilifu, Ismah,tabia njema na tabia bora, na sifa zingine njema. Vipi wasiwe na sifa kama hizo? Ili hali wao ni makhalifa wake na mawasii wake na maimamu wake (viongozi) kwa viumbe wake na hoja za Mwenyezi Mungu juu ya viumbe (wanadamu) wote baada yake. Na ufuatao ni muhtasari wa historia ya kila mmoja kati yao (a.s) na historia ya binti wa Mtume(s.a.w.w) mke wa wasii wa Mutme(s.a.w.w) Fatuma Zahraa (a.s) .

BINTI WA MTUME FATIMA ZAHRAA(a.s)

Yeye ni Fatima Zahraa(a.s) baba yake ni Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) Mohammad bin Abdillah, na mama yake ni Sayyidah Mtukufu Khadijah(a.s) mama wa waumini, na mumewe ni bwana na wasii wa Mtume Ali Amirul muuminiin, na watoto wake pia wajukuu wake ni maimam watwaharifu(a.s) .

Alizaliwa(a.s) tarehe (20) ya mwezi wa Jamaddul-akhir mwaka wa (45) tangu kuzaliwa Mtume(s.a.w.w) na alikufa shahidi akiwa ni mwenye kudhulumiwa tarehe 3 Jamaadul Aakhir[13] siku ya juma nne mwaka wa kumi (11) hijiria akiwa na umri wa miaka (18) katika umri wa kuchanua maua waridi (yaani katika umri wa ujana wake). Na Amirul muuminiin ndie alie simamia suala la kuandaa mazishi yake na kumzika katika mji wa madina na kulificha kaburi lake kutokana na usia wake ikiwa ni hoja kutokana na dhuluma aliyo fanyiwa na haki yake iliyo porwa na kuchukuliwa kwa nguvu. Na Fatima alikuwa kama baba yake katika ibada na uchamungu na ubora na Zuhdi, na Mwenyezi Mungu aliteremsha aya kadhaa kuhusiana na hadhi yake (kuhusiana nae)[14] .

Na Mtume(s.a.w.w) ndie alie muita kwa laqabu (jina mashuhuri) ya (Sayyidatu nisaail aalamiin) Mbora wa wanawake wa ulimwenguni, na kumuita kwa kunia ya Ummu abiiha (Mama wa baba yake) na alikuwa akimpenda sana na kumtukuza sana na kwa kiwango kikubwa, hata ilifikia hatua kwamba anapo ingia kwa Mtume humkaribisha na kusimama kwa heshima yake na kumkalisha mahala pake na pengine alikuwa akiibusu mikono yake na Mtume(s.a.w.w) alikuwa akisema: Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwa maridhio ya Fatima na anachukia kwa kuchukia Fatima [15] . Alimzalia Amirul muuminiin(a.s) watoto wafuatao: Imam Hassan(a.s) na Imam Hussen(a.s) na Muhsin(a.s) lakini Muhsin mimba yake ilitoka kabla ya muda wake kutokana na maudhi na masaibu yaliyo mfika mama yake, na Sayyidatu Zainab(a.s) na Sayyidah Ummu kuluthuum(a.s) .

IMAMA WA KWANZA IMAM AMIRUL MUUMINIIN (a.s)

Yeye ni Ali bin Abi Twalib(a.s) , na mama yake ni Fatuma binti Asad(a.s) nae ni mtoto wa Ami yake Mtume wa Allah(s.a.w.w) na mume wa binti yake na wasii wake na khalifa wake kwa watu baada yake, Amirul muuminiin na baba wa maimam(a.s) . Alizaliwa ndani ya Kaaba tukufu katika mji wa Makkah, siku ya ijuma tarehe kumi na tatu (13) ya mwezi wa Rajab baada ya miaka thalathini (30) tangu kuzaliwa kwa Mtume(s.a.w.w) na alikufa shahidi usiku wa siku ya ijumaa katika msikiti wa Al-kufa katika mihrab, kwa upanga wa Ibnu Muljim Al-muradiy na bwana huyu alikuwa ni miongoni mwa Makhawariji- na ilikuwa ni tarehe kumi na tisa (19) ya mwezi mtukufu wa Ramadhan na kukutana au kurejea kwa mola wake baada ya siku tatu tangu apate dharuba lile na alikufa shahidi katika usiku wa tarehe (21) akiwa na umri wa miaka sitini na tatu (63), na maimam wawili Hassan na Hussen(a.s) ndio walio simamia suala la mazishi yake na kumzika katika mji wa Najaful-ashraf mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake hivi leo na kulificha kaburi lake kutokana na usia wake(a.s) , ili liwe katika amani kutokana na mashambulizi ya makhawariji na wenye kulitembelea kaburi lake wasiweze kulifikia na kunufaika kwa kufanya hivyo[16] kisha imam Swadiq(a.s) akalitambulisha kwa watu pia imam Kaadhim(a.s) .

Na anazo fadhila na sifa nyingi sana na zisizo hesabika, hakika yeye alikuwa ndie mtu wa kwanza kumuamini Mtume(s.a.w.w) na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu hata chembe na wala hakusujudia sanamu kamwe na kutokana na hilo ndio maana ikasemwa kuwa linapo tajwa jina lake yasemwe maneno yafuatayo:Karrama llahu wajhahu (yaani Mwenyezi Mungu autukuze uso wake) na ushindi katika vita ulikuwa umefungamanishwa na bendera yake katika vita vyote, mwenye kusimama madhubuti na asie kimbia vitani, hakugeuka nyuma katika vita na wala hakukimbia kamwe na kutokana na hukumu zake nzuri (au uzuri wa utoaji wa hukumu wa Ali Mtume akasema kuhusia nae:

أقضاکم عليّ

Hakimu bora zaidi kati yenu ni Ali [17] .

Na kutokana na wingi wa elimu yake Mtume(s.a.w.w) akasema:

أنا مدینة العلم وعليّ بابها

Mimi ni jiji la elimu na Ali ni mlango wake [18] .

Na kutokana na kushikamana kwake na haki Mtume akasema:

عليّ مع الحق والحق مع عليّ

Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali [19] .

Na alikuwa ni muadilifu kwa watu wake, akitoa haki kwa sawa, mwenye kujiepusha na mali za kidunia, na alikuwa akija na kuingia kwenye hazina ya Waislaam (Baytul mali) na kuziangalia Dhahabu na Fedha na kusema:

یا صفراء ویا بیضاء غرّي غیري

Ewe mwenye rangi ya manjano (Dhahabu) na ewe mwenye rangi nyeupe (Fedha) mghuri (mdanganye) mwingine tofauti na mimi [20] .

Kisha kuzitawanya kwa watu na habakishi hata tembe moja, na alikuwa akiwahurumia masikini na akikaa pamoja na mafukara na kukidhi haja za watu na akizungumza maneno ya haki na kweli na kuhukumu kwa uadilifu na kuhukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu.

Na alikuwa akitekeleza hukumu za Mwenyuezi Mungu, na akifuata mwenendo wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) mpaka kheri ikaenea sehemu zote na baraka kutangaa na maisha bora na yenye neema (mazuri) kuwaenea waja wote na katika miji yote.

Kwa ufupi ni kuwa: Yeye(a.s) alikuwa kama Mtume(s.a.w.w) katika sifa zote na mambo yote, isipokuwa katika suala la Wahyi na Utume na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu akamfanya katika aya ya maapizano (Mubahala) sawa na nafsi ya Mtume(s.a.w.w) [21] .

IMAM WA PILI: IMAM MUJTABA (a.s)

Yeye ni Haassan bin Ali(a.s) bin Abi Twalib, na mama yake ni Fatima Zahraa(a.s) binti Mohammad(s.a.w.w) nae ni mjukuu mkubwa wa Mtume(s.a.w.w) na ni khalifa wake wa pili na Imam wa watu baada ya baba yake Amirul muuminiin (a.s) .

Amezaliwa katika mji wa Madinatul munawwarah siku ya juma nne katikati ya mwezi wa Ramadhan mwaka wa tatu wa hijiria, na alikufa shahidi kwa sumu ambayo alitegeshewa na Muawia bin Abi Sufyaan kupitia mkewe Imam Hassan ambae ni Juudah binti Ash'ath na hilo lilifanyika siku ya Al-khamisi tarehe saba (7) ya mwezi wa Safar[22] mwaka wa (50) hijiria, na alisimamia mazishi yake ndugu yake Imam Hussen(a.s) na kumsitiri katika makaburi ya Bakii'i katika mji wa Madinatul munawwarah, mahala ambapo ndipo kilipo kiwiliwili chake kwa hivi sasa (ndipo mahala lilipo kaburi lake) na-kwa masikitiko makubwa - kaburi lake lilivunjwa na Mawahabi pia walivunja kuba la kaburi lake hilo.

Na Imam Hassan(a.s) alikuwa ni mfanya ibada kwa wingi kati ya watu wa zama zake na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na mbora na alikuwa ni mwenye kumfanana sana Mtume(s.a.w.w) , na alikuwa ni mkarimu zaidi kati ya Ahlul bayti wake katika zama zake na alikuwa ni mwenye huruma zaidi.

Na miongoni mwa ukarimu wake(a.s) ni kuwa alipewa mafuta uzuri na mjakazi mmoja wapo kati ya vijakazi wake, akasema kumwambia mjakazi yule: Wewe uko huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha akasema: Hivi ndivyo alivyo tuadabisha Mwenyezi Mungu pale alipo sema:

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ﴿٨٦﴾

Mnapo amkiwa kwa maamkizi basi itikieni kwa maamkizi mazuri zaidi kuliko mliyo amkiwa au rudisheni kwa yale maamkizi mliyo amkuliwa[23] .

Na miongoni mwa upole wake(a.s) ni kuwa mtu mmoja wa Sham alimuona akiwa amepanda mnyama, yule bwana akawa akimlaani Imam na Imam hakumjibu kwa chochote, yule bwana alipo maliza kutoa laana zake na matusi yake Imam Hassan akamwendea na kusema:

Ewe shekh nadhani ni mgeni na huenda umenifananisha, lau unge omba tukuridhishe basi tunge kuridhisha, na lau kama unge tuomba kitu fulani tunge kupatia na lau kama unge taka tukuongoze tunge kuongoza na lau unge tutaka tukubebee mzigo wako tunge kubebea na ikiwa unanjaa tunge kushibisha na kama unge kuwa uchi tunge kuvisha na kama ni muhitaji tutakutajirisha na ikiwa umefukuzwa tutakuhifadhi na kukusitiri na ikiwa unahaja tutaitatua haja yako[24] .

Yule bwana alipo sikia maneno yale alilia na kusema: Nina shuhudia ya kuwa wewe ni Khalifa wa Mwenyezi Mungu katika Ardhi yake, hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kufahamu vema mahala pa kuuweka ujumbe wake.

IMAM WA TATU: IMAM SHAHIID (a.s)

Yeye ni Hussen bin Ali bin Abi Twalib(a.s) na mama yake ni Fatima binti Mohammad(s.a.w.w) nae ni mjukuu wa Mtume(s.a.w.w) na Khalifa wake wa tatu na baba wa maimam tisa walio kuja baada yake na ni Imam wa watu baada ya nduguye au kaka yake Hassan (a.s) .

Alizaliwa katika mji wa Madinatul-munawwarah tarehe tatu (3) ya mwezi wa Shaaban mwaka wa nne hijiria na kuuwawa kwa dhulma kwa upanga hali ya kuwa ni mwenye kiu, mauaji yaliyo fanya na bani Umayyah kwa amri ya Yazid bin Muawia katika tukio mashuhuri la Ashura, siku ya juma mosi tarehe kumi (10) ya mwezi wa Muharram mwaka (61) hijiria, na jeneza lake pia kiwiliwili chake kitwaharifu na kilicho katwa katwa kwa mapanga pamoja na viwiliwili vingine vya mashahidi walio kufa mashahid pamoja nae vilizikwa baada ya siku tatu tangu kuuwawa kwao wakiwa mashahidi na alaie mzika ni mwanae Imam Zainul aabidiin(a.s) na kumzika mahala ambapo ndipo kaburi lake lilipo hivi sasa katika mji mtukufu wa Karbalaa, mji ambao uliangukia mikononi mwa Saddam na kundi lake na Mwenyezi Mungu kuukomboa kutoka mikononi mwao-pamoja na sehemu zingine tukufu zilizoko Iraq.

Na fadhila zake ni nyingi sana kiasi kwamba ni vigumu kuweza kuzitaja zote, kwani yeye ni ua zuri la Mtume(s.a.w.w) ambae Mtume alisema kuhusiana na yeye:

حسین مني وأنا من حسین

Hussein anatokana na mimi na mimi natokana na Hussen [25] .

Na pia amesema kuhusiana nae na kuhusu nduguye Hassan(a.s) :

هما ریحانتاي من الدنیا

Wao wawili ni maua yangu mazuri duniani [26] .

Pia amesema(s.a.w.w) :

الحسن والحسین سیدا شباب أهل الجنّه

Hassan na Hussedin ni mabwana wa vijana wa peponi [27] .

Pia amesema(s.a.w.w) :

الحسن والحسین إمامان إن قاما وإن قعدا

Hassan na Hussein ni maimam sawa wakiwa wamesimam au wamekaa [28] .

Na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na mfanya ibada sana kati ya watu, hakika alikuwa akisali kila usiku rakaa elfu moja kama baba yake Amirul muuminiin(a.s) na mara nyingi alikuwa akibeba mfuko wa ngozi wenye vyakula usiku na kuwapelekea mafakiri hadi ilionekana alama na athari yake mgongoni mwake baada ya kuuliwa na alikuwa ni mkarimu, mtukufu, mpole, na alikuwa mkali sana pindi anapo asiwa Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwa ukarimu wake ni pale alipojiwa na bedui mmoja akimuomba na kumuimbia shairi lisemalo: Hakwenda kombo kwa hivi sasa mwenye kukuelekea kwa matarajio na alie bisha mlangoni kwa mara kadhaa, wewe ni mkarimu na wewe ni mwenye kutegemewa, baba yako alikuwa ni muuaji wa mafasiki, lau kama si yule ambae alikuwa mwanzoni mwenu, basi sisi sote tunge enewa na kuzungukwa na moto wa jahannama.

Imam Hussen akampatia dinari elfu nne na akmuomba msamaha kwa kusema: Zichukue hakika mimi nakuomba samahani na fahamu ya kuwa mimi ni mwenye huruma sana kwako, lau kama mwendo wetu kesho ungekuwa ni mwema, na anga letu lingekumiminia kheri nyingi, lakini matatizo ya zama ni ya aina tofauti na yenye kubadilika kwa hivyo na mkono wangu ni wenye kutoa kidogo. Na kwa hakika Imam(a.s) kwa kisimamo chake cha kishujaa-na ambacho hakina mfano katika ulimwengu-aliweza kuihuisha sheria ya kiislaam na dini ya babu yake Mtume(s.a.w.w) bali aliuhuisha ulimwengu wote hadi siku ya kiama, kwa hivyo yeye ni bwana wa mashahidi na ni mtu bora baada ya kaka yake na nduguye Hassan(a.s) .