3
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
IMAM WA NNE: IMAMA SAJJAD (a.s)
Yeye ni Imam Ali bin Hussen
na mama yake ni Shahri banuu binti wa mfalme Yazdjard na Imam huyu
alikuwa akiitwa Mtoto wa wateule wawili, kutokana na kauli ya Mtume(s.a.w.w)
:
Hakika mwenyezi Mungu ana wateule wawili katika waja wake, mteule wake katika waarabu ni Quraishi na katika waajemi (wasio waarabu) ni Mfursi. Na kwa kuyazingatia maana ya maneno haya Abul Aswad akaimba shairi lifuatalo:
Hakika mtoto alie zaliwa kati ya Kisraa na Haashim ni mkarimu zaidi ya watoto wote walio vishwa hirizi shingoni mwao.
Amezaliwa
katika mji wa Madinanatul-munawwarah siku ya Alikhamisi mwezi mtukufu wa Shaaban
mwaka (38) hijiria na kufa shahidi kwa sumu siku ya juma mosi tarehe (25) mwezi wa Muharram
mwaka (95) akiwa na umri wa miaka (57), na mwanae Imam Baaqir
ndie alie simamia suala la mazishi yake na kumzika karibu na kaburi la Ami yake Imam Mujtaba
katika mji wa madinatul-munawwarah.
Na alikuwa ni wa aina yake (kwa maana ya kuwa hakuwa na mfano) katika zama zake katika suala la elimu, ibada, fadhila, uchamungu, kuwasaidia watu wenye kuomba misaada na wenye kutaka usaidizi na mengineyo, na maulamaa wengi pia mafaqihi wamepokea riwaya nyingi sana na zisizo hesabika kutoka kwake na kuhifadhi kutoka kwake dua na mawaidha mengi na karama mbalimbali na mengine mengi yasiyo hesabika. Na alikuwa akitoka usiku wa kiza na kubeba mfuko mabegani mwake ukiwa na Dinari na Dirham napengine alikuwa akibeba mgongoni mwake mfuko wa vyakula, au kuni na kupita mlango mmoja mmoja akibisha hodi na kumpatia kila atokae kwenye nyumba hizo pesa hizo, na alikuwa akifunika kichwa chake ili mafakiri wasimfahamu, na pindi alipo fariki watu wa madina wakafahamu na kuelewa ya kuwa yeye
ndie ambae alikuwa akibeba mfuko na kuwapatia vyakula.
Pamoja na hayo akipendezewa sana kula pamoja na mafukara au kuhudhuria kwenye chaku chake mayatima na mafakiri na kula pamoja nae. Na miongoni mwa tabia zake njema
ni kuwa katika kila mwezi alikuwa akiwaita wahudumu wake na kusema: Mwenye kutaka kuolewa kati yanu nitamuoza, au akitaka kuuzwa nitamuuza, au akitaka kuachiwa huru nitamuachia huru. Na pindi alipokuwa akijiwa na muombaji husema: Karibu wewe ambae huibeba akiba yangu ya akhera.
Na kutokana na uchaji mwingi wa mola ni kuwa alikuwa akisali kwa usiku na mcana wake rakaa elfu mmoja na anapo kuwa kwenye sala ngozi yake husinyaa na kukunjamana na rangi yake kubadilika na kuwa ya njano na kutetemeka kama kuti la mtende, na miongoni mwa laqabu zake ni Dhuthafanaati (mwenye sugu au magamba), kutokana na athari za sajda katika paji lake la uso na vitanga vyake pia magotini mwake. Mtu mmoja alimtusi na kumtolea maneno machafu na mabaya na yeye
akiwa kimia hazungumzi wala kasema chochote na baada ya muda Imam
akamwendea, waliokuwa wamehudhuria wakadhania ya kuwa anataka kumfanya kama alivyo fanya yeye, mara akasoma aya ifuatayo:
وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾
Na wenye kuvunja ghadhabu na kuwasamehe watu na Mwenyezi Mungu anawapenda watu wema
.
Kisha akamsimamia bwana yule na kusema: Ewe ndugu yangu hakika wewe ulisimama kwangu (ulinisimamia) muda ulio pita na kusema uliyo yasema, ikiwa umeyasema kwangu hayo uliyo yasema, basi mimi nina muomba Mwenyezi Mungu msamaha na ikiwa umesema mambo ambayo siko nayo, Mwenyezi Mungu akusamehe
.
IMAM WA TANO: IMAM BAAQIR (a.s)
Yeye ni Imam Mohammad bin Ali Al-baaqir
na mama yake ni Fatuma binti Hassan
alizaliwa katika mji wa madina siku ya Ijumaa mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Rajab
mwaka (57) hijiria.
Na yeye ndie mtu wa kwanza katika kizazi cha Ali alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi hicho cha Ali, na ni mtu wa kwanza wa kizazi cha Haashim alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi cha Haashim, na ni mtu wa kwanza alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi cha Fatuma, kwani yeye ndie wa mwanzo alie kusanya kati ya kizazi cha maimamu wawili Hassana na Hussen
na alikufa shahidi kwa sumu siku ya juma tatu tarehe (7) Dhul hajjil haraam mwaka (114) hijiria akiwa na umri wa miaka (57) na mwanae Imam Swaadiq
ndie alie simamia suala la maandalizi ya mazishi yake na kumzika pembezoni mwa kaburi la baba yake Imam Sajjad
na Ami wa baba yake na babu yake Imam Mujtaba
katika makaburi ya Baqii'i kwenye mji wa Madinatuil munawwarah. Na alikuwa ni mwenye fadhila kubwa mkarimu na mwenye kushikamana na dini na alikuwa ni mwenye elimu nyingi na kubwa na mpole sana, pia mwenye tabia njema na mwenye kufanya ibada sana, mwenye unyenyekevu, ukarimu, ukunjufu na alifikia kwenye kilele katika tabia zake njema, mkiristo mmoja alimwambia: Wewe ni mfunguzi na mpasuaji! Imam akasema: Mimi ni Mfuinguzi.
Akasema wewe ni mtoto wa mpishi. Imam akasema:Hiyo ni kazi yake
. Akasema: Wewe ni mtoto wa mtu mweusi na mbaya. Imam
akasema:
Ikiwa umesema kweli Mwenyezi Mungu amsamehe na ikiwa umesema uongo Mwenyezi Mungu akusamehe
. Yule Mkiristo akasilimu.
Na katika elimu alikuwa kama Bahari yenye mawimbi mengi, akijibu kila mas'ala na swali lolote analo ulizwa bila kusita.
Na Ibnu Atwaa Al-makiy amesema: Sija wahi kuona kamwe wanazuoni na maulamaa kwa mtu yeyote alie kuwa mdogo zaidi kuliko nilivyo waona kwa Baaqir
hakika nilimuona Al-hakam bin Utaybah-pamoja na utukufu wake na heshima yake kati ya watu-akiwa mbele yake kama mtoto akiwa mbele ya mwalimu wake, na Mohammad bin Muslim amesema: Sikujiwa na fikra yoyote isipokuwa nilimuuliza Mohammad bin Ali
mpaka nilimuuliza hadithi elifu thalathini (30).
Na Imam
alikuwa ni mwenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wakati wote, mpaka Imam Swaadiq
akasema: Baba yangu alikuwa ni mwenye kumtaja sana Mwenyezi Mungu, nilikuwa nikitembea pamoja nae hali ya kuwa akimtaja Mwenyezi Mungu na alikuwa akizungumza na watu na lisimshughulishe hilo kunako kumtaja Mwenyezi Mungu
.
Na Imam alikuwa ni mwingi wa tahajjud (sala za usiku) na ibada, mwenye kulia sana na mwenye mazingatio.
IMAM WA SITA: IMAM SWAADIQ (a.s)
Yeye ni Jaafar bin Mohammad As-swaadiq
na mama yake ni Fatuma alie kuwa akiitwa kwa kunia ya (Ummu farwah) alizaliwa
katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarehe (17) mwezi wa Rabiiul Aawwal (mfungo sita) siku ya kuzaliwa Mtume(s.a.w.w)
mwaka (83) hijiria na kufa shahidi kwa sumu siku ya juma nne tarehe (25) mwezi wa Shawwal (mfungo mosi) mwaka (148) hijiria akiwa na umri wa miaka (65), na mwanae Imam Kaadhim kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika katika makaburi ya Baqii'i pembezoni mwa kaburi la baba yake Imam Baaqir
na babu zake wawili: Imam Sajjad na Imam Mujtaba
.
Na alikuwa na Fadhila nyingi zisizo hesabika kama elimu, fadhila, hekima, fiqhi, zuhdi, uchamungu, ukweli, uadilifu, ubora, furaha na utoaji, ukarimu, ushujaa na fadhila zinginezo.
Na kwa hakika Mufiid alisema (Mwenyezi mungu autukuze utajo wake): Na maulamaa hawakunukuu kwa yeyote kati ya Ahlul bayti wake kama walivyo nukuu kutoka kwake na hakuna yeyote kati ya watu wakusanyao hadithi na wakusanyaji wa habari, mfano wa Jaafar bin Mohammad As-swaadiq
hakika walikusanya majina ya wapokezi kutoka kwake kati ya watu waaminifu pamoja na kutofautiana kwao kirai na itikadi, na walikuwa ni watu elfu nne (4000)
. Hadi mwisho wa maneno yake.
Na Abu hanifa Imamu wa madhehebu ya hanafi alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wake moja kwa moja, kama ambavyo maimam wengine wa madhehebu za Ahli sunna walikuwa ni wa wanafunzi wake pia
lakini si moja kwa moja bali kwa kupitia wanafunzi wake na kwamba elimu nyingi na mpya kama vile Kemia, Fizikia na elimu ya maumbo na nyota na elimu ya ugunduzi wa madini na kuchimbuaji wa hazina zilizoko ardhini na zinginezo nyingi ambazo Imam ndie alie weka misingi yake na kuwaongoza watu kwenye elimu hizo.
Hakika Imam
alitumia fursa iliyopatikana ya ugomvi kati ya bani Abbas walio fanya mapinduzi dhidi ya bani Umayyah na kati ya bani umayya walio kuwa mbioni kuanguka na kutoweka dola lao, alitumia fursa hiyo kuanzisha Madrasa kubwa ya kielimu na kujishughulisha na kazi ya ulezi wa wanafunzi na watafutaji wa elimu na kuwabainishia mafunzo ya kiislaam na uzuri wa sheria zake na kuwafafanulia fikra za batili na mbaya zilizo ingia kwenye Uislaam na kubatilisha shubha zitolewazo, mpaka misingi ya sheria ikaimarika na ubainifu wa Uislaam kudhihiri na kubainika wazi na akafahamika
kama Raisi na kiongozi wa Madhehebu ya Jaafaria, kama ambavyo wafuasi wake
walifahamika pia kwa jina la Shiatu Jaafar (wafuasi wa Jaafar au mashia wa Jaafar).
Na miongoni mwa uongofu wake
ni kuwa yeye alikuwa akila siki na mafuta na kuvaa kanzu ngumu na nzito napengine alikuwa akivaa nguo yenye viraka na alikuwa akifanya kazi zake mwenyewe kwenmye mabustani na mashamba yake.
Na miongoni mwa Ibada zake ni kuwa alikuwa akisali sana na pengine alikuwa akizimia katika sala na kuitwa watu wa kumsaidia usiku, Mtumishi wake anasema: Nilikwenda mlangoni kwake na nikamkuta katika chumba chake cha faragha akiwa ameweka shavu lake juu ya udongo hali akiomba kwa kuinua vitanga vyake na huku kukiwa na athari ya mchanga usoni mwake na kwenye shavu lake.
Na Imam
alikuwa ni mwingi wa kutoa, mwenye tabia njema, mwenye maneno laini, mwenye vikao vizuri na mwenye bashasha kwa kila mwenye kukutana nae na alikuwa na muashara mzuri kwa kila anae kutana nae.
IMAM WA SABA: IMAM KAADHIM (a.s)
Yeye ni Imam Mussa bin Jaafar Al-kaadhim
na mama yake ni Hamidah Al-muswaffah, alizaliwa
katika sehemu iitwayo (Ab'waa) nayo ni sehemu iliyoko kati ya Makka na Madina siku ya juma pili tarehe (7) mwezi wa Safar mwaka (128) hijiria na aliiaga Dunia akiwa na umri wa miaka (55) kwa kulishwa Sumu na kufa shahidi katika jela ya Haroun baada ya kumfunga kwa muda mrefu kwa muda wa miaka (14) kwa dhuluma na uadui, na alifariki siku ya Ijumaa tarehe (25) ya mwezi wa Rajab mwaka (183) na mwanae Imam Ridhaa
kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika mahala lilipo kaburi lake tukufu kwa hivi sasa katika mji wa Kaadhimiyyah huko Iraq.
Na Imam alikuwa ndie mwenye elumu zaidi kati ya watu wa zama zake na mbora wao na mkarimu zaidi kati yao na shujaa zaidi na amwenye tabia njema, mwenye umbile bora na mororo, mwenye kudhihiri juu yake fadhila, elimu na mwenye hadhi tukufu, mwenye kufanya sana ibada na mwenye kurefusha sijda zake, na kutokana na kuvunja kwake ghadhabu na kuto kasirika akaitwa Al-kaadhim, na kutokana na wema wake na utukufu wake alikuwa akiitwa Al-abdus swalih (mja mwema). Na kutokana na elimu yake nyingi aliweza kudhihirisha elimu za aina tofauti, elimu ambazo ziliwashangaza watu, na kati ya elimu hizo ni hadithi ya (Burayha)
mkuu wa Wakiristo alie mashuhuri alie shindwa na Imam na kukosa la kusema mwishowe kusilimu na kuwa muislaam safi.
Na miongoni mwa ukarimu wake
ni kuwa: fakiri mmoja alimuomba Dinari mia moja na Imam kwa kutaka kumjaribu akamuuliza mas'ala au swali moja ili kujua kiwango cha maarifa yake, yule fakiri alipo jibu mas'ala yale Imam akampatia Dinari elfu moja. Na Imam
alikuwa ni mwenye sauti nzuri sana pindi anapo soma Qur'ani na alikuwa ni mfanya ibada sana kati ya watu na kusoma sana Qur'ani, na alikuwa ni mwenye kurefusha sana sijda na rukuu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na mwenye kulia sana na mwenye mazingatio, na alifikiwa na shahada hali ya kuwa yuko kwenye hali ya kusujudu (yaani akiwa ni mmwenye kusujudu).
IMAM WA NANE: IMAM RIDHAA
Yeye ni Imam Ali bin Mussa Ridhaa
na mama yake ni Sayyidah Najmah, alizaliwa
siku ya Al-khamisi tarehe (11) mwezi wa Dhulqaadatul-haraam, mwaka (148) hijiria katika mji wa Madina na kufa shahidi kwa sumu siku ya Ijumaa mwishoni mwa mwezi wa Safar, mwaka (203) na mwanae Imam Jawaad
kusimamia suala la maandalizi ya mazishi yake na kumzika katika sehemu ya khorasani sehemu ambayo ndiko liliko kaburi lake tukufu. Na Imam
alikuwa mashuhuri sana kwa elimu nyingi, fadhila, ukarimu, mwingi wa kutoa, mwenye tabia njema, mnyenyekevu, na mwenye kufanya ibada sana.
Maamun-kutokana na vitimbi na hadaa-alimuita Imam Ridhaa
kutoka Madinah hadi Khorasani (Iran) na kumtaka achukue ukhalifa wa kiislaam-badala yake-lakini Imam alikuwa amejiweka kando na kuyapa mgongo mambo ya kidunia (yaani alikuwa ni mwenye zuhdi) na hakukubali, kwani alifahamu matokeo ya maombi hayo, kuwa ni vitimbi na hadaa, kama ambavyo babu yake Amirul muuminiin
alivyo kataa Ukhalifa-katika shura-wakati Ibnu Auf alipo mpatia Ukhalifa huo kwa sharti kwamba afuate sera ya mashekhe wawili walio mtangulia, (Abubakar na Omar), kwani Imam aliona ya kuwa Ukhalifa wakati huo ulikuwa umesimama juu ya jambo moja wapo kati ya mambo mawili, na mambo yote mawili hayo ni ya uongo na si yenye kukubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu: Ama jambo la kwanza ni kuwa Imam
akubali sharti kisha asilitekeleze -kama alivyo fanya Othumani - na huo ni uongo wa kikauli na wenye kuchukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Ama jambo la pili ni kuwa: Imam akubali sharti na atekeleze, maana yake ni kuwa aridhie sera ya mashekhe wawili pamoja na kuwa hakuwa na ridhaa na hakuridhishwa na matendo yao na huo ni uongo wa kimatendo na ni wenye kukemewa mbele ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo basi Imam hakuona njia yenye kuridhiwa na Mwenyezi Mungu tofauti na kukataa na kupinga na kuto kubali
.
Na baada ya Imam Ridhaa
kuukataa Ukhalifa, Maamun alishikwa na butwaa na kunyongea sana kwani aliona ya kuwa mpango wake ambao kwa ajili yake alimuita Imam umeshindwa na kufeli, hapo alimtaka achukue wilayatul ahad - cheo cha waziri mkuu- na kumlazimisha kukubali
lakini Imam
alimuwekea sharti ya kuwa hato ingilia katika jambo lolote kati ya mambo ya dola na kukubali cheo hicho kwa sharti hilo. Imam
alikuwa ni mrithi wa baba zake watukufu
katika elimu na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
na elimu yake ilionekana na kudhihiri kiasi kidogo kuhusiana na mambo ya dini na Madhehebu fikra na Itikadi-katika kikao cha majadiliano ambacho kiliandaliwa na Maamuun-na yaliyo jitokeza kwenye hadithi ya Rukbaan.
Vile vile katika ibada alikuwa
akikesha katika masiku mengi kwa ibada na kuhitimisha Qur'ani kwa muda wa siku tatu na mara nyingi alikuwa akisali usiku na mchana rakaa elfu moja, na mara nyingi alikuwa akisujudu kwa muda mrefu, pengine alichukua masaa kadhaa kwenye sijda na alikuwa ni mwengi wa kufunga. Na Imam
alikuwa ni mwingi wa kutenda mema, na akitoa sana sadaka na sadaka nyingi alikuwa kizitoa kwa siri na hasa kwenye usiku wa kiza.
Na miongoni mwa tabia zake na adabu zake
ni kuwa hakumuudhi mtu yeyote kwa maneno kamwe na wala hakumfanyia ukali mtu yeyote katika kauli, na hakuwa akiegemea kukiwa kuna watu wamekaa mbele yake na hakuwahi kucheka kwa sauti kubwa na ya juu kamwe, na hakuwahi kutema mate mbele ya yeyote kamwe, na chakula kilipo kuwa tayari mezani huwaita ahli zake wote na wahudumu wake na kula pamoja nao.