6
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
AINA YA UTAWALA NA NAMNA YA KUTAWALA
Swali
: Je katika utawala wa kiisalam kuna suala la uchaguzi na utoaji wa maoni na upigaji wa kura na je kuna bunge la wawakilishi wa watu na vikao vya manispaa na mikoa na mfano wa hayo?
Jawabu
: Ndio yote hayo yamo ndani ya Uislaam- hasa katika zama zetu hizi ambazo Imam Mahdiy
yuko mafichoni (katika Ghaiba) - lakini kwa mfumo wa kiisalaam, kwa mfano: Bunge jukumu lake ni kutekeleza na kufuatisha au kutekeleza kanuni za ujumla kwenye sehemu zake na maswaadiki zake, na jukumu lake si kuweka sheria mpya na kutunga sheria mpya, kwa sababu utungaji wa sheria na kanuni kwanza kabisa hiyo ni haki ya Mwenyezi Mungu mtukufu na pili ni kuwa hakuna upungufu katika hukumu za kiislaam na wala hakuna kasoro wala upungufu, mpaka tuhitaji kutunga sheria mpya na kutunga kanuni zingine, kwa mfano imepokelewa katika hadithi kwamba:Hakika Uislaam umetubainishia hukumu za kila kitu hata hukumu ya dia (fidia) ya mkwaruzo)
(yaani mtu akimkwaruza mwenziwe kuna hukumu yake) na imepokelewa katika hadithi nyingine ya kuwa: (Halali ya Mohammad(s.a.w.w)
ni halali hadi siku ya kiama na haramu yake ni haramu hadi siku ya kiama)
.
Kwa hivyo basi: Mtu yeyote hana haki ya kuharamisha jambo fulani na kuhalalisha jambo lingine bali haki yake ni katika kutekeleza na kutenda, kwa mfano: Uislaam umehukumu ya kuwa biashara katika nchi ni haki ya watu na wafanya biashara, kwa hivyo bunge halina haki ya kubadilisha sheria hii au kuibadilisha kwa kuifungamanisha au kuihusisha na watu fulani tu au kuihusisha tu na serikali, wakati ambapo Uislaam haukuhukumu ya kuwa utembeaji bara barani na majiani uwe kwa upande wa kulia au upande wa kushoto, kwa hiyo katika sehemu kama hizi ni haki ya bunge kuainisha kuwa iwe ni upande wa kulia au kushoto, na imekuwa hivyo kwa sababu Uislaam umeamrisha kuwepo nidhamu na kuto kuwa na fujo na kila mtu kufanya atakavyo, na suala la kuainisha upitaji wa mabarabarani au njiani iwe ni upande wa kulia kwa mfano ni kutekeleza nidhamu ambayo imehukumiwa na Uislaam na kuweka sheria yake na hali ni hiyo hiyo katika mambo mengine mfano wa hilo.
Swali
: Sasa kwa nini hivi leo tunaona katika nchi za kiisalam upungufu na matatizo na utungaji wa sheria na kanuni?
Jawabu
: Hakika nchi hizo ni nchi za kiisalaam kwa jina tu na kwa alama na si zaidi ya hivyo na Mwenyezi Mungu mtukufu amekwisha sema:
وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ ﴿١٢٤﴾
Na mwenye kujiepusha na utajo wangu (Qur'ani) hakika mtu huyo ana maisha ya taabu na siku ya kiama tutamfufua akiwa kipofu.
Kwa hivyo yule ambae anachukua jukumu la kutunga sheria na kuacha au kujiepusha na hukumu za Mwenyezi Mungu anayafanya maisha yake kuwa finyu na ya dhiki - kama maisha ya nchi za kiislaam yalivyo kuwa finyu-na mtu huyo katika Akhera ana aibu na moto.
MAJUKUMU YA UTAWALA WA KIISALAAM
Swali
: Ni lipi jukumu la utawala wa kiisalaam kuuelekea Umma?
Jawabu
: Jukumu lake ni kuhifadhi na kulinda uadilifu kati ya watu- ndani ya nchi na nje ya nchi-na kuyafanya maisha yaendelee na kuondoa mahitaji kwa kukithirisha mahitaji ya watu: kuwapatia riziki, mali, kuwapatia elimu na kuwapatia elimu za juu na kuhifadhi Amani na usalama wao na utulivu wao.
Swali
: Ni kanuni ipi ambayo hutekelezwa na dola la kiislaam?
Jawabu
: Ni kanuni itokanayo na kitabu na Sunna za Mtume(s.a.w.w)
na Ijamaa na Akili.
Swali
: Ni nani mwenye kuweka kanuni ili ziweze kutekelezeka?
Jawabu
: Huwekwa na mafaqihi (maulamaa wa fiqhihi) walio waadilifu ambao ndio marejeo ya Umma yaani wanazuoni wa mambo ya dini na Dunia, ambao watu hurejea kwao katika taqliid.
Swali
: Je katika Uislaam kuna makundi mbali mbali ya kisiasa?
Jawabu
: Hakuna shaka kuwepo kikundi ambacho kiko chini ya uangalizi wa maulamaa ambao ndio marejeo ya watu, ikiwa kikundi au chama hicho ni utangulizi wa kuunda bunge la wananchi amabalo ndio linalo takiwa kutekeleza na kufuatilia utekelezaji wa sheria, ama kikundi ambacho kitakuwa ni utangulizi wa kusimamia utungaji wa sheria hakifai kuwepo na hilo linatokana na ukweli kuwa utungaji na uwekaji wa sheria hilo ni jukumu maalu tu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu alie takasika.
UCHUMI WA KIISLAAM
Swali
: Je katika Uislam kuna mfumo maalum wa kiuchumi?
Jawabu
: Ndio na ulio bora zaidi kuliko mifumo iliyo wahi kujulikana katika ulimwengu huu.
Swali
: Je mfumo wa kiuchumi wa kiislaam ni wa kibepari (Capitalism), au kijamaa? au ni wa Makomonisti au ugawaji kwa sawa?
Jawabu
: Hakuna Ubepari wala ujamaa katika Uislaam,- kwa maana ifahamikayo hivi leo - na wala si wa kikomonisti wala ugawaji.
Swali
: Basi mfumo wa kiislaam uko je?
Jawabu
: Uchumi wa kiislaam unaheshimu umiliki wa mtu mmoja mmoja na unaukiri kwa sharti kwamba umiliki huo usitokane na mali ya haramu, na nisharti kutekeleza na kutoa haki zake za kisheria
.
Swali
: Basio dola (serikali) linapata vipi mapato yake?
Jawabu
: Dola linapata mapato yake kwa kukusanya haki za kisheria zilizo thibitishwa ndani ya Uislaam.
Swali
: Ni zipi hizo haki za kisheria zilizo wajibu?
Jawabu
: Haki hizo ni nne: Khumsi, Zaka, Kodi za Ardhi, na Jizya (mali ichukuliwayo kutoka kwa Mayahudi na Wakiristo walio wekaeana mikataba na dola la kiisalaam kwa ajili ya kuwalinda).
VYANZO VYA MAPATO KATIKA UISLAAM
Swali
: Tufafanulieni haki hizi ambazo ndio vyanzo vya mapato katika Uislaam kama mlivyo taja hapo kabla?
Jawabu
: "Khumsi" ni mali au pesa ichukuliwayo na mtawala wa kiislaam (Haakim) nayo ni asilimia (20%) katika faida zote za kisheria na katika Madini, Mali iliyo fichwa chini ya ardhi, na Mali itolewayo baharini kwa kuzamia, na Mali ya halali iliyo changanyika na haramu na Mali iliyo patikana kwenye vita kati ya Waislaam na Makafiri na sehemu fulani ya Ardhi. Na "Zaka" ni mali ichukuliwayo na mtawala wa kiisalaam moja ya (40) na moja ya (100), na Zaka huchukuliwa katika Mbuzi, Ng'ombe, Ngamia, Dhahabu, Fedha, Tende, Zabibu, Shairi na Ngano. Na "Kharaaj" Ni kodi zichukuliwazo na mtawala wa kiislaam kutoka kwa wakulima, katika ardhi zilizo kombolewa bila mapigano au bila kutumia nguvu. Na "Jizya" ni mali ichukuliwayo na mtawala wa kiisalaam kutoka kwa Mayahudi, Wakiristo na Majusi walio wekeana mikataba, na makafiri wengine kwa ajili ya kuwahami na kuwalinda au kwa ajili ya dhimma fulani.
Swali
: Je katika Uislaam kuna Mabenki?
Jawabu
: Ndio lakini mabenki ya kiislaam hayana riba wala nyongeza, kwani riba katika Uislaam ni sawa na kumtangazia vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake, pamoja na kutekeleza sheria zake zote za kiislaam za mali na mambo ya wafanyakazi huendeshwa na mapato mengine na ikiwa hayakutosheleza, basi hukamilishwa kutoka katika hazina (baytul mali) ya dola la kiislaam:
Swali
: Je dola au serikali huchukua mali zingine kutoka kwa watu tofauti na hizo zilizo tajwa, kati ya mafungu yaliyopo hivi sasa?
Jawabu
: Hapana, kwani dola la kiislaam halina haki ya kuchukua zaidi ya mafungu manne yaliyo tajwa - kamwe-na imepokewa katika hadithi kama ifuatavyo: (Mwenye kuchukua mali kwa yeyote bila ya ridhaa yake, Mwenyezi Mungu ataichukua mali hiyo siku ya kiama kutoka kwake, badala ya kila Dirham atachukua sala mia saba kati ya sala zake zilizo kubaliwa na kumpatia mwenye mali).
BAYTUL- MAALI YA WAISLAAM (HAZINA YA WAISLAM)
Swali
: Dola la kiislaam, huzifanyia nini pesa au mali lizichukuazo na kuzikusanya kutoka kwa watu?
Jawabu
: Kwa hakika katika dola la kiislaam kuna idara au Wizara kwa istilaha ya kisasa ijulikanyo kwa jina la (Baytul mali) katika wizara hii hukusanya mali yote ikusanywayo kutoka kwa watu na mali hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kutatua mahitaji yote ya Waislaam, pamoja na kuwa dola husimamia mipango yote ya kimaendeleo ujenzi na maendeleo mengine ya nchi, pia hutenga fungu fulani la mali na kumpatia kila fakiri kiasi cha pesa kimtoshelezacho kuendesha mambo yake ya kimaisha, ili asibakie fakiri katika nchi (kwa maana kuwa huweka mpango wa kupiga vita ufukara nchini) na hukidhi haja ya kila muhitaji, kwa mfano mwenye kutaka kuoa, au mtaji wa kuanzisha biashara, au kujenga nyumba na kuanzisha duka, au kwa ajili ya matibabu, au kwa mwenye safari ya lazima kutokana ya haja au tatizo, au humpatia mtu alie katikiwa na matumizi akiwa safarini na hakuwa na pesa ya kumrudisha nyumbani kwake, au kuwasaidia wanafunzi wanao hitajia pesa katika masomo yao kama kulipia karo, na mfano wa hayo kwa kurejea kwenye baytul mali- na kuithibitishia-kwa njia za kawaida, kama kuleta mashahidi, au kuapa- ya kuwa anahaja ya kitu fulani na hana pesa, wakati huo baytul mali humpatia kiwango kinacho tosheleza kukidhi haja yake kulingana na hadhi yake na chenye kumtosheleza, na kwa msingi huu hakutabakia katika dola la kiislaam fakiri au muhitaji-kamwe-.
Swali
: Je haki na pesa hizo za aina nne zilizo tajwa zinatosheleza mahitaji yote hayo?
Jawabu
: Ndio, inatosha ukiongezea mapato liyapatayo dola la kiisalaam kutokana na ghanima (Ngawira) na imepokelewa katika hadithi ya kuwa: (Lau kama pesa hiyo haikutosheleza basi Mwenyezi Mungu angeongezea katika kiwango chake) (yaani angeongeza katika kiwango kinacho takiwa kutolewa)
.
UCHACHE WA WIZARA NA WAFANYA KAZI
Swali
: Vyanzo vya mapato vilivyo tajwa na ambavyo ni vichache, vinatosheleza vipi wakati tunaona ya kuwa hivi leo kuna vyanzo vikubwa na vingi vya mapato na bado havitoshelezi mahitaji ya serikali na watu?
Jawabu
: Vinatosheleza kutokana na uchache wa muundo wa dola na uchache idara (Wizara) na wafanya kazi wake kuwa waaminifu na mambo kuwaachia watu wenyewe, kwa mfano: Wafanya kazi katika dola la kiislaam ni wachache sana, kwa sababu idara au wizara nyingi dola la kiislaam halina haja nazo, kisha ni kuwa kazi nyingi ambazo husimamiwa na dola na serikali-kwa hivi sasa-husimamiwa na watu binafsi katika dola la kiisalaam na hakubakii katika majukumu ya dola na serikali ya kiislaam isipokuwa kazi chache kiasi kwamba dola linakuwa na uwezo wa kuzitekeleza kwa haraka sana na kwa urahisi zaidi kadri iwezekanavyo na ni jambo lililo wazi kuwa: pindi idadi ya wafanya kazi inapokuwa chake na mishahara kupanda na mambo ya watu kuwaachia watu wenyewe na wasimamizi kuwa waaminifu hapo mali hukithiri na kuwa nyingi
.
Swali
: Je walio staafu kazi hupewa pensheni?
Jawabu
: Ikiwa ni fakiri asie jiweza hupewa kulingana na mahitaji yake, si kwa kiwango maalum-kama ijulikanayo katika serikali na madola mbali mbli ya siku hizi
.
7
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
DHAMANA YA KIJAMII KATIKA UISLAAM
Swali
: Je katika Uislaam kuna dhamana ya kijamii?
Jawabu
: Ndio na ni bora kabisa kati ya aina ya dhamana za kijamii na za kiwango cha juu kabisa.
Swali
: Je mnaweza kutubainishia na kutufafanulia sehemu fulani ya dhamana hiyo ya kijamii katika Uislaam?
Jawabu
: Dhamana ya kijamii katika Uislaam inatokana na shauku na mapenzi ya kibinadamu na kiutu tena ya kiwango cha juu kabisa kwa maana hiyo hakika Uislaam una anzia kwenye nukta ya utu au ubinadamu, na huitoa dhamana hii ikiafikiana na hali ya kibinadamu na kiutu na ikilenga kwenye upeo wake na katika nyanja zake za ubora na kwa kusisitiza hilo historia haikuwahi kushuhudia kabla ya Uislaam na historia haikunukuu utamaduni wa aina yoyote baada ya Uislaam hadi hivi leo dhamana ya kijamii yenye kina kilicho sawa na kina cha dhamana ya kijamii katika Uislaam.
MIFANO YA DHAMANA YA KIJAMII YA KIISLAAM
Hakika dhamana ya kijamii katika Uislaam inasema yafuatayo:
1.
Hakika kila mtu anae kufa hali ya kuwa na madeni, au ameacha familia bila msimamizi na mtu wa kuitunza familia yake, ni juu ya Imam wa Waislaam kulipa madeni yake, kama ambavyo ni juu yake kuitunza na kuilea familia yake.
2.
Kila anae fariki hali ya kuwa ana mali, mali yote ni ya warithi wake.
3.
Pamoja na hayo, huduma za kimali ambazo hutolewa na Baitul mali ya Waislaam kwa kila mtu katika umma wa kiislaam, ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya mwanzo na kwa ajili ya kujipatia maisha mema.
Je unadhani-pamoja na yote hayo- unadhani kunadhamana kama hii ambayo imo ndani ya Uislaam, hata kama ni katika utamaduni ulio endelea na wenye kina kikubwa zaidi? Kwa hakika na bila shaka yoyote hakuna kitu kama hicho, bali ukweli ni kuwa mifumo mingine ya utawala ya kiulimwengu na ya kijahili iliyo kuwepo kabala ya Uislaam vilevile mifumo ya ulimwengu inayo dai kuwa imeendelea na iliyo kuwa na maendeleo ya kielimu na iliyo staarabika katika zama zetu hizi huwajibisha kutoa mapato makubwa kwenye urithi, kama ambavyo wao hawalipi deni la yeyote na wala hawabebi jukumu la kuitunza familia ya marehemu na hakuna shaka hapa kutaja baadhi ya mifano ya kiislaam juu ya jambo hili.
MFANO WA KWANZA
Katika Nusuus (dalili) za kisheria za kiislaam, kuna dalili nyingi zinazo tilia mkazo juu ya haya tuliyo yataja ya dhamana ya kijamii ya kiislaam na dalili hizo bila shaka zinatujulisha juu ya namna Uislaam unavyotilia mkazo na hima juu ya jamabo hili na katika upande huu wa kibinadamu na kijamii ulio mkubwa, kiasi kwamba imekaririwa kwa mara kadha zikinukuliwa dalili juu ya suala hilo kutoka kwa Mtume wa Uislaam(s.a.w.w)
na maimam wa kizazi kitwaharifu cha Mtume(s.a.w.w)
. Kwa mfano imepokelewa kutoka kwa Abi Abdillah Jaafar bin Mohammad As-swaadiq
Imam wa sita wa Ahlul bayti
, ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
amesema:
أنا أولی بکل مؤمن من نفسه وعلي أولی به من بعدي
Mimi ni bora kabisa au mwenye haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake na Ali (a.s) ni bora zidi na mwenye haki zaidi kwa kila muumini kuliko nafsi yake baada yangu
.
Akaulizwa: Nini maana ya maneno hayo? Akasema: Kauli ya Mtume(s.a.w.w)
:Mwenye kuacha deni, au familia basi ni juu yangu mambo hayo na mwenye kuacha mali basi ni ya warithi wake
.
MFANO WA PILI
Ali bin Ibrahiim katika tafsiri yake ametoa hadithi, kwa sanadi yake iliyo tajwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
ya kuwa yeye alikuwa akisema:
Hakuna mdai yeyote alie kwenda na mdaiwa wake kwa mtawala kati ya watawala wa kiislaam na ikabainika kwa yule walii ya kuwa ni tajiri na mwenye uwezo, isipokuwa humuokoa yule fakiri kutokana na deni lake, na deni hilo kuhamia kwenye dhima ya mtawala yule wa Waislaam kutokana na mali iliyoko mikononi mwake kati ya mali za Waislaam
.
Amesema Imam Swadiq
baada ya kunukuu hadithi hii kutoka kwa Mutme(s.a.w.w)
: Na hakukuwa na sababu ya kusilimu Mayahudi wote isipokuwa baada ya kusikia kauli hii kutoka kwa Mtume(s.a.w.w)
na kwamba wao walipata tumaini juu ya nafsi zao na juu ya familia zao
.
MFANO WA TATU
Shekh Mufiid (Quddisa sirruhu) ametoa hadithi katika kitabu chake Al-majaalis, kwa sanadi yake kutoka kwa Imam Abi Abdillah As-swadiq
ya kuwa alikuwa akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
alipanda kwenye Mimbari, vitukuta vyake vikabadilika na rangi yake kumeremeta, kisha akageuza uso wake na kusema:Enyi waislaam! Hakika si jambo jingine mimi nimetumwa na kiama, kama vitu viwili hivi- hadi akasema- enyi watu! Mwenye kufariki na kuacha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake na mwenye kuacha deni au familia bila muangalizi, ni juu yangu na hurejeshwa kwangu
.
Pia ametoa hadithi kutoka kwa Abi Abdillah As-swadiq
ya kuwa amesema: Yeyote atakae kuwa na mali (yaani atakae chukua deni) kwa mtu fulani na hakuitumia mali hiyo vibaya (kwa israfu), au katika maasi, na ikamuwia vigumu kulipa deni hilo, ni juu ya mwenye mali kumpa muhula (muda) mpaka Mwenyezi Mungu amruzuku na aweze kulipa deni hilo na ikiwa Imam muadilifu yupo, ni juu yake kumlipia deni hilo, kutokana na kauli ya Mtume(s.a.w.w)
:Yeyote atakae acha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake na mwenye kuacha deni au familia, ni langu na ni juu yangu na ni juu ya Imam kuchukua dhamana aliyo ichukua Mtume
(s.a.w.w)
.
MFANO WA NNE
Hakika Uislaam - kwa ubora wa mfumo na nidhamu yake uliyo nayo ya Baytil mali ya Waislaam na dhamana ya kijamii ya kiislaam- imeufanya umma wa kiislaam kuwa tajiri na ufakiri katika dola hilo umekaribia kuwa sawa na khabari ya kana (khabari iliyo kuwa) kutokana na dola la kiislaam, ambalo lemeenea kila mahala, na lenye ardhi kubwa na pana na zilizo mbali, ardhi ambayo takariban zaidi ya tatu ya nne ya ardhi hiyo ni yenye kukaliwa na watu, na yenye wakazi wengi. Ndio, hakika Shekh Hurrul Amiliy ametaja katika kitabu chake maarufu: (Wasaailu-shia) kisa kifuatacho akisema: Hakika Imam Amirul muuminiin Ali bin Abi Twalib
alikuwa akitembea katika mitaa na vichochoro vya mji wa Al-kufa, ghafla akamuona mtu mmoja akiomba watu misaada: akastaajabu sana kutokana na mtu huyo na akawageukia walio kuwa pembezoni mwake akijiuliza: Ni kitu gani hiki?
Akajibiwa: kuwa ni Mkiristo amezeeka na kuwa na umri mkubwa na hana tena uwezo wa kufanya kazi na hana mali ya kumuwezesha kuishi, kwa hivyo ndio maana anawanyooshea watu mkono kwa kuomba. Imam
akasema hali ya kuwa ni mwenye ghadhabu: Mmemfanyisha kazi wakati akiwa kijana mpaka alipo fikia utu uzima na uzee mkamtelekeza na kumuacha? Kisha Imam
akaamuru atengewe fungu yule Mkiristo katika baytul mali ya Waislaam litakalo mfanya aishi maadamu bado yuko hai
.
Hakika kisa hiki kinatufahamisha ya kuwa ufukara ulikaribia kutokuwa na nafasi katika dola la kiislaam, hadi ilifikia Imam Amirul muuminiin
akimuona fakiri mmoja hushangaa na kustaajabu na kuliona tukio hilo kuwa ni tukio lisilo la kawaida na hali isiyo ya kawaida na halinasibiani na jamii ya kiislaam na dola au nidhamu ya kiislaam, kisha wakati huo akamuwekea fungu litakalo mfanya aishi maisha mazuri na yenye furaha pamoja na kuwa ni Mkiristo na hafuati dini ya kiislaam, na alifanya hivyo ili kusiwe katika nchi ya kiisalaam mfano au tukio moja linalo onyesha hali ya ufukara na kutokuwa na kitu na ili ulimwengu ufahamu hali waliyo nayo Waislaam: Ya kuwa serikali ya kiislaam inampango wa kuangamiza janga la ufukara na kuinua hali ya maisha ya mafakiri na masikini na si kwa mustawa wa Waislaam pekee yao, bali inaupiga vita ufukara hata kwa Makafiri maadamu wako chini ya uangalizi wa dola la kiislaam.
MFANO WA TANO
Shekh Kulayni ametoa hadithi kwa sanadi yake iliyo tajwa kutoka kwa Hassan amesema: (Hakika Ali alipo washinda Twalha na Zubayri) katika vita vya Jamal na katika vita vyake alivyo pigana pamoja na wapingaji (Naakithiin) watu walirejea wakiwa wameshindwa, na wakampitia mwanamke mmoja alie kuwa mja mzito njiani, na alipo waona akashikwa na fazaa na mshutuko mkubwa na ikawa ni sababu ya kutoka kwa kilicho kuwa tumboni mwake kikiwa hai na kutatizika hadi akafariki, kisha mama wa mtoto huyo nae kafariki baadae, Imam Ali
akampitia mama huyo yeye na maswahaba zake hali ya kuwa mama yule akiwa amelala chini na mwanae akiwa njiani, akawauliza kuhusiana na kilicho msibu mama huyo? Wakasema: Hakika alikuwa ni mja mzito na akashikwa na fazaa na mshutuko wakati alipo ona mapigano na namna walivyo shindwa.
Akasema: Akawauliza: Ni yupi alifariki kabla ya mwengine? Akajibiwa: Hakika mwanae ndie alie fariki kabla ya mama.
Akasema: Imam
akamuita mumewe baba wa mtoto alie fariki akampa theluthi ya fidia kama urithi wa mwane, kisha akamrithisha mama yake theluthi nyingine ya fidia, kisha akamrithisha mume vilevile kutoka kwa mkewe nusu ya fidia ambayo aliirithi kutoka kwa mwanae na kuwarithisha jamaa au ndugu wa mke alie fariki fidia iliyo bakia, kisha akamrithisha mume pia katika fidia ya mkewe alie fariki nusu ya fidia nayo ni: Dirhamu elfu mbili na miatano na jamaa za mwanamke alie fariki akawarithisha nusu ya fidia nayo ni:Dirhamu elfu mbili na mia tano na alimpa kiasi hicho kutokana na kutokuwa na motto mwingine tofauti na yule alie toka kutokana na fazaa iliyo mshika.
Akasema: Na Imam
alitoa mali yote hiyo kwenye Baytul mali ya Basrah
.
Ndio, hivi ndivyo Uislaam ulivyo weka Baytul mali ya Waislaam kwa ajili ya manufaa ya Umma na kutatua matatizo yao na kuwapa haki zao, kwani - kama ilivyo pokelewa katika hadithi tukufu -(Haki ya muislaam haipotei)
na katika hadithi nyingine imepokewa ikisema:Damu ya Muislaam haimwagiki bure
na kwa dalili hizo Uislaam ukauwekea Umma wa kiisalaam mahitaji yenye kumtosheleza kupitia mpango wake wa dhamana yake ya kijamii yenye uadilifu.