HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)0%

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S) Mwandishi:
Kundi: Vitabu mbali mbali

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

Mwandishi: ASIYEJULIKANA
Kundi:

Matembeleo: 37601
Pakua: 4019

Maelezo zaidi:

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 37601 / Pakua: 4019
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

Mwandishi:
Swahili

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W) PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Ameripoti riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa amesema:"Enyi wenye shida na masikini! Tunzeni heshima zenu na mpeni Allah swt furaha ya mioyo zenu ili kwamba Allah swt awalipe mema kwa ufukara na shida zinazo wakabili na kama nyie hamtafanya (isije mkakufuru na kuvuka mipaka kwa sababu ya kukosa subira na hikima) hivyo basi mtambue kuwa mtapata adhabu na gadhabu za Allah swt."

Imenakiliwa riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema kuwa:"Itakapo tokea miongoni mwenu mtu akazingirwa kabisa kwa hali mbaya, basi inambidi awajulishe jamaa na ndugu zake na asiiweke nafsi yake katika shida."

AL IMAM 'ALI BIN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) amesema katika Nahaj -ul - Balagha kuwa:"Mtu yeyote atakayemwambia mahitaji yake dharura zake kwa muumin basi ajue kuwa ameweka habari zake hizo kwa Allah swt, na yeyote yule atakayeleta dharura na mahitajio yake kwa kafiri basi ajue kuwa amekwenda kinyume na maamrisho ya Allah swt."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Katika hali tatu tu ndipo kunapo ruhusiwa kuomba ama sivyo hairuhusiwi

"Kwanza: katika kujinusuru mtu mwenyewe,

"kujinusuru na hasara kubwa kabisa ya mali na

"tatu: iwapo kwa kutokuomba kutakuja kumpatia udhalilisho wa hali ya juu sana. Yaani mtu katika vitu hivyo vitatu kujiokoa na hali hizo tatu mtu anaweza kuomba msaada kwa wengine"

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) anasema kuwa:

"Mtu mmoja alimwijia Al Imam Hassan ibn 'Ali bin Abi Talib(a.s) na kuomba chochote: Kwa hayo Imam(a.s) akamwambia haistahiki kuomba isipokuwepo hizo sura tatu.

" Kwanza: ama kuzuia umwagikaji wa damu,

" pili: ama mtu akiwa na shida ya hali ya juu kabisa au " kujizuia kuja kudhalilika vibaya sana. Sasa hebu wewe niambie wewe upo katika sura ipi kati ya hizi tatu? Yeye akasema 'Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Katika sura tatu ulizozitaja ipo mojawapo. Basi bila kusita kwa haraka sana Al Imam Hassan ibn 'Ali bin Abi Talib(a.s) akamtolea dinar elfu hamsini na kumpa, na Al Imam Hussein ibn 'Ali bin Abi Talib(a.s) akampa dinar elfu arobaini na tisa na 'Abdulah bin Ja'afar akampa dinar elfu arobaini na nane."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema:

"Heshima ya muumin ni kule kuamka kwa ajili ya sala za usiku, na vile vile heshima yake ni kule kutokuwa mwombaji wa watu." Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. kuwa amesema: "Wewe lazima uwe na moyo wa kuishi vyema na watu na kuwaheshimu na kutosheka nao. Na kuishi nao vyema ni kule kuongea nao kwa upole na utamu na uwe na uso wenye tabasamu na uishi nao vile kwamba kila wakuonapo uwe ukionyesha furaha usoni mwako na hivyo utakuwa umejiwekea heshima katika jamii."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) anasema:

"Iwapo kutatokezea miongoni mwenu anayemtegemea Allah swt azikubalie kila dua zake anazoziomba basi awe akiishi na watu wote kwa wema na kamwe asimtegemee mtu yeyote isipokuwa Allah swt peke yake na atakapo jiona kuwa yeye kwa hakika anao moyo kama huo basi atambue wazi kuwa chochote kile atakachomwomba Allah swt atampatia na kumjaalia."

AL IMAM ZAYNUL 'ABEDIIN BIN HUSSEIN BIN 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali ibn Abi Talib(a.s) anasema kuwa:

"Iwapo mtu atataka wema wote kwa ajili yake ni kwamba yeye ajiepushe mbali na tamaa za kila aina ya kutamani yale waliyonayo watu, na kama yeye ana matamanio yoyote au maombi yoyote basi asiwategemee hawa watu bali zote azielekeze kwa moyo mkunjufu na halisi kwa Allah swt na lazima Allah swt atazikubalia dua na maombi yake na atamtimizia."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Abul A'ala bin A'ayan anasema kuwa; mimi nimemusikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) akisema:

"Enyi watu nyie mtajidhuru pale mtakapo peleka maombi yenu na mahitaji yenu kwa watu, na kwa hakika inafukuzia mbali heshima na adabu. Mkae na watu katika hali ya kuridhika na kuwa na uhusiano nao mzuri na kwa hakika hiyo ndiyo kwa ajili ya usalama. Kwa hakika tamaa yenu ndiyo dalili ya ufakiri wenu."

AL IMAM 'ALI AR-RIDHA (A.S)

Ahmad bin Muhammad bin Abi Nassr anasema kuwa yeye siku moja alimwambia Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) :

"Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Ninaomba uniandikie barua moja kwa Ismail bin Daud, ili kwamba niweze kupata chochote kutoka kwake. Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) akamwambia iwapo mimi kitu unachokitaka au cha kukutosheleza wewe ningekuwa nimekukataa, ndipo ningekuandikia, ama sivyo uchukue kile nilicho nacho mimi kwangu na ukitegemee hicho.".

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

"Kwa hakika yale waliyonayo watu katika uwezo wao na kuridhika nayo ndimo humo kuna heshima ya muumin ya imani yake, je nyie hamjaisikia kauli ya Hatim? Hatim alisema kuwa pale mtakapoona nafsi zenu zimevutiwa kwa mali za watu wengine basi muelewe kuwa shida na taabu ziko zinawakaribia, na kwa hakika tamaa ni ufakiri ulio dhahiri."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Abdullah Bin Sinan anasema kuwa; yeye amemsikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) akisema:

"Kwa ajili ya muumin mapendezi ya dunia na akhera yako katika mambo matatu. Kwanza ni sala katika sehemu ya mwisho wa usiku, kutokuvutiwa na kutokuwa na husuda na mali na miliki wanayomiliki watu wengine na kuwa mwaminifu na mtiifu kwa ukamilifu wa Ahlul Bayt a.s. na mapenzi yao."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

"Alikuwapo mtu mmoja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na akamwuliza, 'Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! naomba unionyeshe unieleze jambo moja nilifanye jambo ambalo Allah swt atakuwa radhi pamoja nami. Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimujibu: Udumishe amani na upendo katika utamaduni wa dunia, jambo ambalo kimatokeo utapata mapenzi ya Allah swt na usiwe na kijicho na wivu wala tamaa kwa mali na miliki za watu jambo ambalo litahifadhi heshima yako machoni na mioyoni mwao."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Ja'bir bin Yazid ananakili riwaya kutoka kwa Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) kuwa amesema:

"Usiwe na wivu choyo wala tamaa kwa mali za watu kwa hakika ni jambo jema kabisa kwa kuitakasisha nafsi yako kuliko hata kutoa mhanga wa mali. Vile vile wakati wa shida na dhiki fanya subira. Kuhifadhi heshima yako na utakatifu wako, mambo haya ni afadhali hata kuliko kugawa mali kwa watu. Kwa hakika kuwa na imani kamili juu ya Allah swt na kutotaka kutovutiwa kutokuwa na wivu au kijicho au tamaa kwa mali waliyonayo watu wengine ndio hayo mambo yaliyo bora kabisa katika maisha ya mwanadamu.".

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema kuwa; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa akisema:

"Allah swt amechukia hafurahishwi na sifa sita na vile vile mimi sizifurahii hizo sifa sita na ndio nimefanya usia kwa mawasii na waumini wote kuwa vitu hivyo sita wajiepushe navyo na mojawapo ni kule baada ya kutoa sadaka mtu akaanza kumsema na kuvisema."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Baada ya kutenda mema mtu atakapovizungumzia hayo basi atayateketeza mema yake yote."

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa:

"Allah swt hakupendezewa na mambo sita na mimi vile vile katika kizazi changu Maimam wote sikupenda kutokezee sifa hizo, na vile vile Maimam pia nimewahusia kuwa wasizipende sifa hizo ziwepo katika muumin. Hivyo kila muumin anabidi ajiepushe na sifa hizo. Katika sifa hizo sita mojawapo ni ile baada ya kumfanyia mtu wema mtu anaanza kuyazungumzia huku na pale."

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) anasema kuwa; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Allah swt hapendi sifa sita na hizo sifa sita mimi sikupendezewa kwa ajili ya mawasii watakao nifuata na waumini wote watakaonifuatia. Kwanza kusali isivyo kwa makini, pili katika hali ya saumu kujamiiana na mwanamke, tatu baada ya kutoa sadaka kutangaza na kuonyesha. Nne kuingia msikitini katika hali ya Janaba, kuwa na shauku ya kutaka kujua mambo ya watu majumbani mwao kunatendeka na kunaendelea nini, na sita kucheka makaburini mtu anapokuwa baina ya makaburi mawili."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kwa mamlaka yake amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa:

"Mtu yeyote atakaye msaidia muumin ndugu yake na baadaye akaja akamwambia kuhusu wema huo akausema basi Allah swt hulirudisha tendo hilo halikubalii. Basi mtoaji atabakia na uzito juu yake na kwa lile jema alilolitenda hana malipo yoyote kutoka kwa Allah swt."

Na Imam a.s. aliendelea kusema: "Kwa sababu Allah swt anasema kuwa yeye ameiharamisha Jannat kwa ajili ya yule anayesema baada ya kutenda tendo jema na bahili na mchonganishi. Muelewa wazi kuwa yule mtoa sadaka, hata anayetoa kiasi cha Dirham moja, basi Allah swt humlipa zaidi ya ukubwa wa mlima wa Uhud kwa neema za Jannat na yeyote yule atakaye saidia kufikisha hiyo sadaka kwa yule ambaye anahitaji basi Allah swt atamlipa mema hayo hayo, na kamwe hakutakuwa na punguzo lolote katika neema za Allah swt kwa ajili ya wote hao."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika hotuba yake alisema:

"Yeyote yule atakaye tenda wema na kuwawia wema ndugu wenzake, na akaanza kutanganza mema aliyoyafanya basi matendo ya watu kama hawa yatatupiliwa mbali na hayatakuwa na maana yeyote. Allah swt amewaharamishia Jannat watu wafuatao: " Kwanza ni wale wanao tangaza mema waliyowafanyia watu wenzao, na " Wale wanaowapotosha watu wengine, " wafitini, " wanywaji wa pombe, " wale wanao tafuta makosa ya watu na aibu za watu, " wale wenye tabia mbaya, " wale walio makatili kwa wenzao na vile vile " wale watu wanao watuhumu watu wengine kwa tuhuma za kuwazushia maovu."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amenakili riwaya kutoka kwa mababu zake kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Allah swt amewazuieni nyinyi kwa matendo maovu takriban ishirini na manne na mojawapo ni jambo lile ambalo baada ya kutoa sadaka mtoaji anamwambia maneno aliyempatia."

Bwana Abu Zahar Al Ghafar amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa:

"Kuna aina tatu ya watu ambao Allah swt kamwe hatazungumza nao siku ya Qiyama. Kwanza ni yule mtu ambaye hatoi kitu chochote bila ya kumsema au kumwambia yule anayempa, na pili ni yule ambaye hachukui jukumu wala haoni umuhimu wa kuficha zehemu zake za siri na wa tatu ni yule ambaye anauza mali yake na kutaka faida kupindukia kiasi."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mtu yeyote baada ya kumsaidia muumin atamuudhi kwa kumwambia au kwa kumsengenya kiasi kwamba roho yake ikaumia basi Allah swt huibatilisha sadaka na wema kama huo."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

"Aina tatu ya watu kamwe hawataingia Jannat(poeponi). Moja ni yule ambaye wazazi wake wamemfanya Aak, wa pili mnywaji wa pombe (daima anakunywa pombe) na tatu ni yule baada ya kufanya mema huanza kusema na kutangaza."

AL IMAM 'ALI BIN ABI TALIB (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema kuwa: Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) siku moja alimtumia mifuko mitano ya Tende za Baqi' (Jannatul Baqi', ipo Madina ). Mtu huyo alikuwa muhtaji (mwenye shida) na daima alikuwa akitegemea msaada kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) , na kamwe alikuwa harefushi mikono yake kwa wengine kwa ajili ya kuomba kwa watu wengineo. Mtu mmoja alipo yaona hayo basi alimwambia Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) :

"Kwa kiapo cha Allah swt, huyu mtu hajakuomba chochote wewe kwa hivyo badala ya kumpa mifuko mitano mfuko mmoja tu ulikuwa ukitosha, na kwa hayo Al Imam 'Ali bin Abi Talib(a.s) akamwambia: "Allah swt asiongezee idadi ya muumin kama wewe humu duniani! Wewe mtu wa ajabu sana, mimi ndiye ninayempa lakini ubahili unaufanya wewe! Kumbuka kuwa mtu mwenye shida na anaye kutegemea wewe hakuombi, Je ni haki kuwa mwenye shida asipoomba basi asisaidiwe mpaka lazima aombe? Basi hapa inaonyesha heshima yake. Uso ule ambao unawekwa juu ya udongo kwa ajili ya ibada ya Allah swt katika hali ya sujuda itakuwa basi mimi nimeubadilisha ule sura badala ya kumwangukia Allah swt utakuwa umeniangukia mimi ! Na jambo ambalo silitaki mimi na wala silifanyi hivyo."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Kwa hakika uwema ni ule ambao mtu anamsaidia mtu kabla hajaombwa, na kumpa baada ya kujua hali yake inamaanisha umempa baada ya kujua hivyo. Inawezekana maskini huyo mtu usiku kucha akawa anatapatapa iwapo atafanikiwa au hatafanikiwa, huku akiwa amejawa mawazo niende kwa nani nisiende kwa nani, na hatimaye moyo ukiwa unadunda mwili ukiwa unatetemeka na akiwa amejawa na aibu kubwa anatokezea mbele yako."

AL IMAM MUSA AL-KADHIM (A.S)

Yas'ab bin Hamza anasema kuwa: "Mimi siku moja nilikuwa pamoja na Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) , watu walikuwa wamekaa huku wamemzunguka, yaani watu wengi walikuwapo. Watu walikuwa wakiulizia masuala ya halali na haramu, na mara tukaona akaingia mtu mmoja mrefu na akaanza kusema, "Iwe salamu juu yako ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Mimi ni mpenzi na mfuasi wako wewe na baba na mababu zako, na hivi nimerudi kutoka Hijja Tukufu. Mimi nimeibiwa mali yangu yote na hivyo sitaweza kufika nchini kwangu (yaani nyumbani). Mimi naomba nisaidiwe sadaka kiasi kwamba niweze kufika nyumbani kwangu, na mimi nitakapo rudi katika mji wangu kiasi hicho cha fedha nitakitoa nigawe katika kuwasaidia wengine kama sadaka.

Imam(a.s) akamwambia:

"Naomba ukae kidogo upumzike, Allah swt akurehemu. Na Imam(a.s) aliendelea na mazungumzo yake pamoja na umati uliokuwa pale katika kuulizana na kueleweshana kuhusu maswala mbalimbali. Hatimaye mimi Khaysama na Suleiman Al-Ja'afari ndio tuliokuwa tumebakia na hapo Imam(a.s) kwa kuniangalia mimi akasema:"Je unaniruhusu mimi niende chumbani kwangu?" Suleiman akasema "Allah swt aiendeleze amri yako". Hapo Imam(a.s) aliinuka na kuelekea katika chumba chake baada ya muda si mrefu akatoka nje akafunga mlango na mwenyewe akasimama nyuma ya mlango na akatoa mkono tu nje huku akisema:je huyo msafiri kutoka Khurasan yuko wapi?"

Hapo mimi nikamjibu: "Ya Imam(a.s) ! Mimi niko hapa." Na kwa hayo Imam(a.s) akamwambia""Nimekupa hizi Dinar mia mbili ambazo zitakusaidia wewe katika gharama na matumizi ya safari yako na vile vile napenda nikujulishe kuwa hakuna haja tena ya hizi pesa kuzitolea sadaka ufikapo nyumbani kwako, asante na unaweza kuendelea na safari yako na itakuwa vyema tusitazamane nyuso.

Msafiri huyo akachukua hizo pesa na kuondoka zake." Seleiman Al-Ja'afar akauliza: "Niwe fidia juu yako ewe Mwana wa Mtume(s.a.w.w) ! Kwa hakika wewe umefanya wema na ihsani mkubwa sana wenye huruma, lakini pamoja na hayo kwa nini umejificha?"

Kwa hayo Imam(a.s) akamjibu:"Hakuna sababu nyingine ila sikutaka kuona uso wa mwombaji ukiwa umeingiwa na aibu na unyonge sababu ya kuomba. Je wewe hujaisikia hadith ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) ambamo amesema: kwa yeyote yule anayeficha wema hulipwa thawabu za Hijja sabini na yeyote yule baada ya kutenda maasi na madhambi anatangaza basi daima hubakia dhalili. Na yeyote yule anayeficha madhambi na maovu basi Allah swt humsamehe".

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Kwa hakika uwema ni ule ambao mtu anamsaidia mtu kabla hajaombwa, na kumpa baada ya kujua hali yake inamaanisha umempa baada ya kujua hivyo. Inawezekana maskini huyo mtu usiku kucha akawa anatapatapa iwapo atafanikiwa au hatafanikiwa, huku akiwa amejawa mawazo niende kwa nani nisiende kwa nani, na hatimaye moyo ukiwa unadunda mwili ukiwa unatetemeka na akiwa amejawa na aibu kubwa anatokezea mbele yako."

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Jambo jema kabisa linalonisaidia mimi katika kufanya wema katika kuwasaidia ni mkono ambao unawafikishia na mkono mwingine unashirikiana naye. Na kwa hakika hao wanaokuja kuomba wanakuja na maombi yao ndipo wanapokuwa karibu nami zaidi. Kwa hakika nimeona kuwa wale wanao sahau waliyoyatenda mema kabla na baada ya kuurudisha mkono wao nyuma huonekana kuwa wao wanaanza kuyasahau mema yote. Kwa hakika moyo wangu kamwe haukuniruhusu kuwafukuza na kuwakatalia waombaji. Na baada ya hapo Imam(a.s) alisoma mashairi ifuatayo:

Wakati unapokuijia mtihani kwako kwa heshima zako pia inabidi uombe, Basi uende kwa mtu mmoja aliye mkuu na aliye Sharifu kwa ajili ya kuomba kwake. Kwa hakika, huyo mtu Sharifu na mkuu atakapokusaidia basi humo ndani hakutakuwa na maonyesho wala masengenyo, na badala yake ndani kutakuwa na unyenyekevu na kuhuzunika pamoja nawe. Kumbuka wakati utakapotaka kupima katika mzani uombaji na utoaji sadaka na mema basi utaona sahani ya mzani ya uombaji utakuwa daima ni mzito kuliko nyingine yote."

Warram bin Abi Faras ameandika riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuwa:

"Wenye imani dalili zao ni nne, kwanza nyuso zao huwa zina bashasha, ndimi zao zinakuwa zenye ukarimu na mapenzi, nyoyo zao zinakuwa zimejaa huruma, na wanakuwa na mkono wenye kutoa mkono unaopendelea kutoa sadaka na misaada nk."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa akisema:"Kila aina ya wema na huruma ni sadaka."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) akitafsiri neno Ma'arufu katika Qur'an Tukufu, Surah Nisaai, 4, Ayah 114:

﴿لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا﴾

Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa Sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhai ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) aliesema kuwa:

"Kwa ma'arufu kuna maanisha kule mtu kutimiza wajibu wake aliofaradhishiwa."

Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) aliwasaidia waombaji watatu na wa nne alipokuja hakumpa chochote. Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) akasema:

"Iwapo mtu atakuwa na Dirham elfu thelathini au arobaini na zote akazigawa kwa kusaidia au sadaka bila ya kubakiza chochote kwa ajili ya wana nyumba wake basi huyo mtu atakuwa mmoja miongoni mwa watu watatu ambao dua zao hazikubaliwi na Allah swt. Na katika watu hawa watatu: mmoja ni yule ambaye bila kutimiza wajibu wake anagawa mali yote kama sadaka au kusaidia, na baada ya hapo anakaa akiomba dua: "Ewe Allah swt naomba unipe riziki." Basi hapo atajibiwa, "Je mimi nilikuwa sikukufanyia njia ya kujipatia riziki?"

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Bora ya sadaka zote ni ile kufanya wakati mtu anapofanya katika hali unapokuwa sawa."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Hisham bin Al Muthanna anasema: "Kuna mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuhusu tafsiri ya ayah Surah An A'Am, 6, Ayah 141:

﴿وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ كُلُوا مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ وَلَا تُسْرِفُوا إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ﴾

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala mstumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) alimjibu:

"Katika Ansaar alikuwako mtu mmoja (aliwapa jina lao) ambaye alikuwa ana shamba. Pale mazao yake yalipokuwa yakiwa tayari yeye alikuwa akigawa yote katika sadaka, na alikuwa hawapi chochote watoto na wana nyumba yake; na kwa tendo lake hili Allah swt alikuwa akimhesabia yeye kama ni mfujaji na mbadhirifu."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Baada ya mtu kujitolea kile kiasi alicho na dharura nacho kwa mujibu wa mahitaji yake na baadaye katika kiasi kinachobaki akitoa sadaka basi hiyo sadaka ni bora kabisa."

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) anasema: "Mojawapo katika Nasiha na Mawaidha ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ilikuwa ni:

"kila aina ya wema ni sadaka mojawapo, na sadaka iliyo bora kabisa ni pale kutoa wakati mtu ameshajitimizia wajibu wake na ametosheka, na mkumbuke kuwa muwape wale ambao kwao nyie mnawajibika kuwatimizia mahitaji yao. Mkono wa mtoaji ni afadhali kuliko mkono wa mpokeaji. Kwa hakika mtu ambaye anachuma kwa uwezo wake na kutumia kwa ajili yake na kuwatimiza mahitaji yao basi Allah swt kamwe hatamlaumu."

Mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kumlalamikia kuhusu njaa: "Basi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimtuma mmoja wa wake zake naye alipowaendea wakamwambia kuwa wao walikuwahawana chochote isipokuwa maji ya kunywa tu, na kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akamwambia:je kuna yeyote yule atakaye mchukua mtu huyu kuwa mgeni wake kwa usiku huo?" Na kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema:

"Ewe Mtume wa Allah swt ! Mimi nakubali kumchukua huyu kama mgeni wangu kwa usiku wa leo." Na walipofika nyumbani kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Imam(a.s) alimwuliza Bi. Fatimah az-Zahra(a.s) "Je nyumbani kuna chakula chochote?" Kwa kusikia hayo Bi. Fatimah az-Zahra(a.s) akasema, tuna chakula kiasi cha kuwalisha watoto wetu tu lakini na mgeni pia ana haki yake." Na hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) akasema "Wewe walaze watoto, na uizime taa."

Asubuhi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alipokuja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akamwelezea kisa kilivyotokea na wakati bado akiwa anaelezea kisa hicho ayah ifuatayo iliteremshwa: Surah Al Hashri, 59, ayah ya 9:

﴿وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴾

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Muhammad bin Yaqub Al-Kuleiyni amenakili riwaya kutoka kwa Abu Nasar kuwa; yeye amesoma barua ambayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alimwandikia Abu Ja'afar (Mutawakili, mtawala wa Ki Abbasi). Humo kulikuwa kumeandikwa:

"Ewe Abu Ja'afar ! nimepata habari kuwa wewe unapotoka nje wakati umekaa juu ya usafiri wako basi wafanyakazi wako wanakutoa nje kwa kupitia mlango mdogo, ili kwamba yule ambaye ana shida na mwenye kuuhitaji msaada wako asiweze kufaidika hivyo.

Mimi kwa kiapo cha haki yangu ninakusihi kuwa kutoka kwako na kuingia kwako uwe kupitia mlango mkubwa na uwe na wingi wa dhahabu, fedha na mali ili atakapo tokezea mbele yako mwombaji mwenye shida uweze kumsaidia. Wajomba zako wanapokuomba uwape Dinar hamsini na wake zao wanapokuomba uwape Dinar ishirini na tano na usiwape chini ya hapo kama utawapa zaidi basi hilo ni shauri lako. Na hii nakuambia kwa sababu iwapo wewe utafuata hivyo basi Allah swt atakuwia wema, hivyo utumie na usiwe na shaka katika ahadi na neema za Allah swt mmiliki wa malimwengu yote."

AL IMAM 'ALI AR-RIDHA (A.S)

Safwan anasema kuwa siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) alimwuliza mmoja wa wahudumu wake:

"Je leo mmetoa chochote katika njia ya Allah swt ?" Naye alijibu hapana, leo sijatoa chochote bado." Kwa hayo Imam(a.s) alisema"Sasa usipotoa hivyo unategemea Allah swt atupe baraka kwa misingi gani? Lazima utoe kwa njia ya Allah swt hata kama itakuwa ni Dirham moja.