3
HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W) PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)
HARAKISHENI KUOA
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Kwa hakika bikira ni kama matunda ya mtini; matunda hayo yanapokomaa na kama hayakuchumwa, basi mwanga wa jua una waharibu na upepo unawatawanya. Hivyo bikira wapo katika hali hiyo hiyo. Na pale wanapo tambua kile anachohisi mwanamke, basi hakuna dawa yao yoyote isipokuwa kuolewa na bwana. Iwapo wao hawataozwa, basi hawataweza kuepukana na uchafuzi, kwa sababu wao ni binaadamu, vile vile. (kwa sababu wao pia wanahisia na matakwa kama binaadamu wengineo)"
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Kijana yeyote anayeoa mwanzoni mwa ujana wake, Shaytani wake analia na kujuta kabisa kuwa yeye ameikomboa sehemu mbili ya tatu ya imani yake kutoka kwa Shaytani."
Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 221.
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Ewe kijana! Iwapo kuna yeyote miongoni mwenu anayeweza kuoa, basi afanye hivyo, kwa sababu ni vizuri kwa macho yenu (msiwachungulie wanawake wengine) na inahifadhi sehemu zenu za siri (ili muendelee kubakia wacha Allah swt)"
Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 14, Uk. 153.
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Allah swt ameharamisha hali ya kutokuoa, na amewaharamishia wanawake kutokujitenga bila kuolewa (hivyo lazima na wanawake pamoja na kuwa wacha Allah swt lazima waolewe)"
Mustadrak Al-Wasa'il- ush-Shiah, J. 14, Uk. 248
KUWASAIDIA NA KUINGILIA KATIKA NDOA ZILIZO HALALI
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Yeyote yule anayefanya jitihada za kuwaunganisha Waislam wawili katika ndoa iliyo halali ili waweze kuoana kwa sheria takatifu za Allah swt, basi Allah swt atamjaalia kwa ndoa hiyo Hur ul-'Ain mwenye macho meusi katika Jannat, na atamjaalia thawabu za ibada za mwaka mmoja kwa kila hatua atakayochukua au neno atakalolizungumza."
Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 221.
AMESEMA AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB
Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
:
"Ibada bora kabisa ni kule wewe kuingilia kati ya watu wawili kwa ajili kuoana ki halali kwa mujibu wa amri za Allah swt"
At-Tahdhib, J. 7, Uk. 415 na Al-Kafi J. 5, Uk. 331.
AMESEMA AL IMAM MUSA AL-KADHIM
Amesema Al Imam Musa al-Kadhim
:
"Katika siku ya Qiyamah, ambapo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha rehema za Allah swt, basi kutakuwa na aina tatu ya watu ambao watapewa kivuli hicho cha 'Arish ya Allah swt: Mtu yule aliye sababisha kusaidia kufunga ndoa ya Mwislamu mwenzake, au yule ambaye amemhudumia, au yule ambaye amemfichia siri zake kwa ajili ya suala lake hilo"
Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 356.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
Amesema:
"Yeyote yule anayewaunganisha wasioolewa katika ndoa basi wao watakuwa miongoni mwa wale watu ambao Allah swt atawatazama kwa rehema Zake siku ya Qiyamah"
At-Tahdhib, J. 7, Uk. 404
Amesema Al Imam Musa al-Kadhim
:
"Katika siku ya Qiyamah, kutakuwa na kivuli maalum cha Allah swt ambamo hakutakuwapo na wengine isipokuwa Mitume
au vizazi vyao, au Muumin anayemfanya huru mtumwa, au Muumin anayelipa deni la muumin mwingine, au Muumin ambaye anawaunganisha waumini ambao katika ndoa (waumini ambao hawajaoana"
Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 356.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Yeyote yule anayejaribu kuwaunganisha Waislam wawili katika ndoa kwa mujibu wa sheria za Allah swt, basi Allah swt atampatia Hur ul-'Ain elfu moja (wahudumu wanaokaa Jannat wakiwa na macho meusi makubwa) katika ndoa na ambapo kila mmoja wao atakuwa katika ngome ya Malulu na Almas na Rubi"
Wasa'il ush- Shi'ah, J. 20, Uk. 46.
MWANAMKE NA MAHARI
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Ubashiri mbaya wa mwanamke ni kuwa mahari yake ya juu kabisa na ghadhabu zake"
Bihar al- Anwaar, J. 58, Uk. 321.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
Amesema
"Waizi huwa wa makundi matatu: La kwanza wale wanaozuia kutoa sadaka; pili wale wanao jiwekea mahari ya mwanamke na kujihalalishia kwa ajili yao wenyewe; tatu wale wanaochukua mikopo na hawajaamua kurudisha mikopo hiyo kwa ajili ya kulipa madeni yao"
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
Amesema:
"Kwa hakika moja ya baraka za Allah swt kwa mwanamke ni mahari yake kutokuwa juu, na moja ya maovu ya mwanamke ni kuwa na mahari kubwa"
Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 387.
AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB
Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
:
"Msifanye mahari ya wanawake ikawa nzito, kwa sababu hiyo inaleta uhasama na uadui"
Wasa'il ush-Shi'ah, J. 21, Uk. 253.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
:
"Kuna madhambi maovu kabisa ya aina tatu: Kuwatesa wanyama wakati wa kuwachinja, Kuchelewesha na kutokulipa mahari ya mwanamka, na Kutokulipa mishahara ya wafanyakazi"
Bihar al-Anwaar, J. 64, Uk. 268.
AFADHALI MAHARI NDOGO
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Ndoa ile imebarikiwa ambayo ina gharama ndogo"
Kanz-ul- 'Ummal, J. 16, Uk. 299.
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Wanawake bora kabisa katika umma wangu ni wale ambao nyuso zao ni zenye urembo na mahari yao huwa ni ndogo"
Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 236.
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Oeni hata kama mtakuwa na pete ya chuma (kama mahari".
Kanz-ul- 'Ummal, J. 16, Uk. 321.
. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Yeyote yule anayetoa hata kiasi cha tonge moja ya nafaka au tende kama mahari (kwa kukubaliwa na mwenzake), basi kwa hakika ndoa yake ni halali na sahihi kabisa".
Kanz-ul- 'Ummal, J. 16, Uk. 321.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
:
"Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alitoa mahari ya Zirah moja yenye thamani ya Dirham thelathini katika ndoa ya binti yake Fatimah az- Zahra
akiwaolewa na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
"
Wasa'il ush-Shi'ah, J. 21, Uk. 251.
NDOA KWA KUJALI IMANI NA UAMINIFU
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
bila kujali daraja la kizazi cha mtu, amesisitiza na kusema:
"Mtu yeyote anapokuletea habari za kutaka kukuoa na wewe kwa kuridhika unakubalia, kwa adabu zake na dini yake, basi ungana naye kwa ndoa. Na iwapo hutafanya hivyo, basi wewe utakuwa umesababisha fitina na ufisadi mkubwa kabisa juu ya ardhi"
At-Tahdhib, J. 7, Uk. 394.
AL IMAM JAWAD
Al Imam Jawad
ameandika katika barua:
"Mtu yeyote akutakaye wewe katika ndoa anayetaka kukuoa na wewe unakuwa umeridhika na dini na uadilifu wake, basi ungana naye kwa ndoa"
Al-Kafi J. 5,Uk.347 na Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 393 na At-Tahdhib, J. Uk. 394.
Siku moja mtu mmoja alimwambia Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib
kuwa:
"Yeye alikuwa na binti wake na alimwuliza Imam
kuwa yeye amwoze binti wake kwa nani, kwa hayo Imam
alimjibu: Muoze binti wako kwa yule ambaye ana imani na ni mcha Allah swt: Kwa sababu atampenda na kumheshimu huyo binti wako, na iwapo yeye atakuwa mkali juu ya binti yako, basi hatamdhuru"
Al-Mustadrak, J. 2, Uk. 218.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Yeyote yule atakaye muoza binti wake kwa mtu ambaye si mcha Allah swt basi kwa hakika amevunja uhusiano wake pamoja naye"
Al- Muhajjat-ul-Baidha, J. 3,Uk. 94.
AZMA YA MWANAMME KATIKA NDOA
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa urembo wake tu (bila ya kujali imani yake), basi yeye hataambulia kile alichokitaka; na yeyote anayeoa mwanamke kwa ajili ya mali na utajiri wake (basi Allah swt atampa hiyo mali na utajiri tu peke yake.) Kwa hivyo ni juu yenu nyie kutafuta mwanamke aliye katika dini na mcha Allah swt"
At-Tahdhib, J. 7, Uk. 399.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
amesema:
"Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa matarajio ya utajiri, basi Allah swt anampa utajiri na mali peke yake"
Al-Kafi J. 5, Uk. 333.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amesema:
"Yeyote anayeoa mwanamka kwa utajiri wake, Allah swt humwachia hayo tu; na yeyote anayeoa mwanamke kwa ajili ya urembo wake na uzuri wake, basi yeye atayaona yale ndani ya mwanamke yale asiyoyapenda; lakini yule anayeoa mwanamke kwa misingi ya imani na dini yake, basi Allah swt atamjazia kila aina ya sifa ya mambo hayo kwa ajili yake"
At-Tahdhib, J. 7, Uk. 399
. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amesema,:
"Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa ajili ya urembo wake tu, basi Allah swt atamjaalia uzuri wake na uzuri wa mwanamke huyo utamdhuru na kumletea matatizo huyo mwanamme."
Wasa'il ush- Shi'ah, J. 20, Uk. 53.
AMESEMA AL IMAM ZAYNUL 'ABEDIIN
Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin
:
"Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt, na kuungana naye kwa wema basi Allah swt atamjaalia taji la heshima na ufanisi"
Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 385.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Msioe wanawake kwa ajili ya urembo wao tu kwa sababu urembo wao unaweza kusababisha wale wasiwe wacha Allah swt wala si kwa ajili ya mali yao kwa sababu mali yao inaweza ikawasababisha wakawa wasiwe watiifu; lakini muwaoe kwa misingi ya imani ya dini yao"
Al-Muhajjat-ul-Baidha, J. 3, Uk. 85.
KUTAFUTA RIZIKI
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA(S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Amelaaniwa, amelaaniwa yule ambaye hawajali wale anaotakiwa kuwalisha ambao wanamtegemea, kwa hakika amelaaniwa kwa mara nyingi"
Man la Yahdharul Faqih, J. 3.Uk. 168.
Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) Amesema:
"Mwanamme yule ambaye anafanya subira kwa hasira mbaya za mke wake, na anatafuta ile subira kwa Allah swt, basi Allah swt anamjaalia thawabu na ujira mkubwa sana kwa wale wenye kushukuru"
Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 16.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
Amesema:
"Yeyote yule anayevumilia taabu za kutafuta pesa kwa ajili ya kumtimizia haja ya mke wake, ni sawa na yule anayepigana vita vya Jihadi katika njia ya Allah swt"
Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 168 na Al-Kafi, J. 5, Uk. 88.
. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
:
"Ni dhambi moja kubwa kabisa inamtosheleza mtu yule ambaye anawapuuzia wale wanaomtegemea yeye kwa kuwapatia riziki. (Dhambi hili kubwa linaweza kumteketeza huyo mtu)"
Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 168.
Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema:
"Mtu mwenye furaha ni yule ambaye anasimamia na kuratibu maswala ya mke na watoto wake"
Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 168.
WAKE KUWAWIA WEMA WAUME ZAO
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura Ar-Rum, 30, Ayah ya 21 kuwa:
﴿وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴾
Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alipopata habari kutoka kwa Ummi Salama kuhusu Uthman ibn Mazu'un, basi aliondoka kuelekea wafuasi wake na huku akiwaambia kuwa, Bihar:
"Je nyie mnajitenga na wake zenu ? Kwa hakika, mimi mwenyewe huwaendea wanawake, huwa ninakula chakula nao mchana, na kulala nao usiku. Kwa hakika yeyote yule anayejitenga na maisha ninavyoishi mimi basi hatakuwa miongoni mwangu yaani atakayeipa mgongo"
al-Anwaar, J. 93, Uk. 73.
AMESEMA AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
:
"Yeyote yule anayeikataa ndoa na kuipuuzia kwa hofu ya gharama itakayo mfikia, basi anaondoa imani yake juu ya Allah swt kwani inamaanisha kuwa yeye hamwamini Allah swt."
Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 385.
AL IMAM 'ALI AR-RIDHA
Imeripotiwa kutoka kwa Al Imam 'Ali ar-Ridha
kuwa:
"Al Imam Ja'afer as-Sadiq
kwa kumjibu wa mwanamke ambaye alikuwa hataki aolewe ili abaki bila kuolewa, kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu " usifanye hivyo, kwa sababu iwapo ndivyo ingekuwa ni kutukuka huko, basi Bi Fatimah az-Zahara
angekuwa ni mwanamke wa kwanza kutokuolewa kuliko wewe (kwa sababu yeye alikuwa na wadhifa mmoja mkubwa sana akiwa ni binti wake Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
, na kwa hakika hakuna mwanamke yeyote duniani ambaye anaweza kuwa na utukufu zaidi ya Bi Fatimah az-Zahara
"
Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 219.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
ameripotiwa kusema kuwa:
"Wanawake watatu walimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
na kusema kuwa waume zao wamekataa kula nyama au kutumia manukato au kuwakaribia wake zao. Na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
(Akikaripia matendo yao) alikwenda haraka juu ya Mimbar na baada ya Kumhimidi Allah swt alisema: Je wamekuwaje baadhi ya watu kuwa hawataki kula nyama, na wala hawataki kutumia manukato, na wameacha kuwakaribia wake zao?"
Al- Kafi J. 5, Uk. 496.
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
Amesema:
"Kuwa wakati mke wa Uthman ibn Mazu'un, alipomwelezea Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
kuwa bwana wake daima amekuwa akifunga saumu siku za mchana na kusali wakati wa usiku alikuwa hajali maisha yake na wala alikuwa hamjali mke wake pia, kwa kusikia hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliondoka akaenda moja kwa moja nyumbani kwake na akamkuta yuko anasali. Wakati Uthman alipomaliza sala zake, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alimwambia: "Ewe Uthman, Allah swt hakunituma mimi kuwa Ruhbani (Kuwa kama Mapadre kwa kikirsto) bali amenituma mimi kwa ajili ya dini iliyo rahisi ambayo inalinda haki za mwili na roho. Mimi hufunga saumu, huwa nikidumisha sala, na huwa nikichanganyikana na kujumuika pamoja na familia yangu kwa ukamilifu. Na yeyote yule anayependa Sunnah yangu na mwenendo wangu basi lazima afuate mwenendo wa maisha yangu, na Sunnah yangu; Na kwa hakika ndoa ikiwa ni mojawapo ya Sunnah zangu"
Al-Kafi J. 5, Uk. 494.
KUWAHESHIMU WAKE ZENU
AL IMAM 'ALI AR-RIDHA
Al Imam 'Ali ar-Ridha
amenakili kutoka kwa baba yake hadi kufikia kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Amelaaniwa mwanamke yule ambaye anamfanya mme wake akasirike, na mwanamke mwenye furaha ni yule ambaye humridhisha bwana wake kwa furaha"
Bihar al-Anwaar, J. 8, Uk. 310.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Yeyote yule aliye na wanawake wawili na kama hawawii kwa haki kwa nafsi na mali yake miongoni mwao, basi siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa amefungwa kwa minyororo na nusu ya mwili wake hautakuwa wima hadi kule atakapo tumbukizwa Jahannam."
, Bihar al- Anwaar, J. 7, Uk. 214.
IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR
Imam Muhammad al-Baqir
Amesema:
"Yeyote yule anayeoa mwanamke lazima amheshimu kwa heshima zote, kwa sababu mwanamke kwa mtu yeyote anamaanisha raha na mustarehe, kwa hiyo yeyote anayemwoa mwanamke asimharibu wala kumdhalilisha yeye (Kwa kutojali haki zake zinazostahili)"
Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 224.
AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB
Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
:
"Kwa hali yoyote ile na katika sura yoyote ile lazima mpatane na wake zenu, na muongee nao vyema kwa kutumia maneno mema mazuri, na hivyo matendo yao yatakuwa mema na watabadilika kuwa wake wema na wazuri kwa ajili yenu"
Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 223.
AL IMAM MUSA AL-KADHIM
Amesema Al Imam Musa al-Kadhim
kwa kumnakili baba a.s. yake ambao wamemnakili Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) akisema:
"Kiasi chochote cha imani cha mtu kitakachoongezeka basi na kumjali kwa mke wake pia kutaongezeka"
Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 228.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
kuwa:
"Kutokana na vitu vya duniani, mimi huwajali wanawake na manukato zaidi, lakini ibada ni nuru ya macho yangu, (mapenzi na ibada ya Allah swt)"
Al Khisal, Uk. 183 na Bihar al-Anwaar, J. 76, Uk. 141.
MWANAMKE KUMRIDHISHA MUME WAKE
AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR
Al Imam Muhammad al-Baqir
amesema:
"Siku ya Qiyamah mwanamke hataokolewa na hatapata uokovu wowote kutoka kwa Allah swt bila ya idhini ya bwana wake"
Bihar al-Anwaar, j.81, uk 385.
AL IMAM 'ALI AR-RIDHA
Al Imam 'Ali ar-Ridha
ameripoti kutoka kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
ambaye amesema:
"Bora wa wanawake miongoni mwenu ni yule ambaye ana sifa tano Mwanamke asiye na matatizo, Mtiifu, Mnyenyekevu, Mwenye matumizi madogo Mvumilivu wakati bwana wake anapokasirika Mshiriki mwema na msaidizi wakati wa shida, Mpaji wa hima kwa bwanake anapokuwa amezongwa na mawazo na shida Mtunzaji wa mhifadhi wa nyumba ya bwana wake anapokuwa hayupo. Kwa hivyo mwanamke kama huyo ni wakala wa mawakala wa Allah swt na kwa hivyo mawakala wa Allah swt hawatakuwa wenye hasara (yeye anapata matumaini sahihi".
Al-kafi, j5, uk.324.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
amesema:
"Mwanamke yeyote yule anayepitisha usiku ambapo mume wake amemkasirikia na kumghadhibikia, ibada zake hazikubali hadi pale huyo mwanamke atakuwa amemridhisha bwana wake"
Al-Kafi, J.5,Uk.507.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amesema:
"Haki za bwana kwa mke wake ni kuziwasha taa, kutayarisha na kupika chakula na kumpokea mume wake anapokuja mlangoni kwa maneno mazuri na kamwe asimkatalie mume wake anapomhitaji yeye binafsi ( kujamiiana) isipokuwa anapokuwa sababu zake "
Makarim-ul-Akhlaq,J.2, Uk. 246.
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Mwanamke kamwe hatatekeleza haki za Allah swt hadi yeye ametekeleza haki za mume wake"
Mustadrak-Al-Wasa'il-ush-Shiah, J.14, Uk. 257.
AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR
Amesema Al Imam Muhammad al-Baqir
:
"Siku moja mwanamke mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
na kumwambia: 'Ewe Mtume wa Allah swt ! Je bwana haki gani kwa mke wake ?' Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alimjibu: Mwanamke amtii mume wake na wala asimuasi"
Wasa'il ush-Shi'ah, J.10, Uk. 527.
TALAKA NA ATHARI ZAKE
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Amesema:
"Kwa hakika Allah swt hapendi kabisa au humlaani mwanamme au mwanamke yeyote ambaye anakuwa na nia ya talaka au anaoa kwa ajili ya kustarehe tu." Na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ameirejea kauli hii mara tatu kusisitiza kuwa mwanamme yeyote yule anayempa mke wake talaka kwa ajili ya kuoa mwanamke mwingine na kutaka kustarehe starehe za ndoa mwanmke mpya na vile vile mwanamke yeyote yule anayeomba talaka kwa sababu kama hizo hizo na kuolewa na mwanamme mwingine, basi wote hawa wanajitumbukiza katika laana za Allah swt"
Al-Kafi, J. 6, Uk. 54.
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Wanawake katika umma wangu ambao wanafuata sunnah nne (mambo mema manne) basi wataingizwa Jannat: Iwapo yeye atalinda utukufu wake, Anamtii mme wake, Anatimiza sala zake tano, na Anafunga saumu katika mwezi wa Ramadhani"
Bihar al-Anwaar, J. 104, Uk. 107.
KUPELEKA MACHO CHINI NA KULINDA HESHIMA
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Allah swt anatwambia katika Qur'an Tukufu, Sura An Nuur, 24, ayah ya 30:
﴿قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ﴾
Waambieni waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Allah swt anazo khabari za wanayo yafanya.
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
anatuambia:
"Kutazama kiharamu kwa wale walio haramishwa kwetu ni sawa na mshale kutoka upinde wa Shaytani ambayo imejaa sumu. Yeyote anayejiepusha naye kwa ajili ya Allah swt, na wala si kwa sababu zinginezo, basi Allah swt atampa imani ambamo yeye ataipata furaha ndani mwake"
Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 18.
Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
:
"Zinaa ya macho ni kuangalia yale yaliyo haramishwa, kwa mtazamo wa matamanio, Zinaa ya midomo ni kuwabusu wale walio haramishwa (wasio maharimu), na Zinaa ya mikono ni kuwagusa (mikono na sehemu zingine za wale walio haramishwa Wasio-maharimu ) bila kujali iwapo atakuwa na hamu au hatakuwa na hamu ya kujamiiana"
Al-Kafi, J. 5, Uk. 559.
AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR
Amesema Al Imam Muhammad al-Baqir
:
"Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amemlaani yule mtu ambaye anaangalia sehemu za siri za mwanamke ambaye si halali kwake, na vile vile ememlaani yule mtu ambaye anafanya khiyana pamoja na mke wa ndugu yake, na vile vile yule mtu ambaye anachukua rushwa kwa watu kwa msaada wanaohitaji kutoka kwake"
Al-Kafi, J. 5, Uk. 559.
MWANAMKE NA KUJIPAMBA
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA(S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Neno asemalo mwanamme kumwambia mke wake: 'Nakupenda basi kamwe halitatoka moyoni mwa mke wake"
Wasa'il ush- Shi'ah, Volume 14, Uk. 10.
Amesema Al Imam Muhammad al-Baqir
:
"Haijali chochote au vyovyote vile mwanamke ajirembavyo kwa ajili ya bwana wake"
Al-Kafi, J. 4, Uk. 119.
AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB
Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
:
"Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameharamisha kujiremba kwa mwanamke kwa ajili ya mwanamme mwingine mbali na mume wake mwenyewe na akasema: 'Na kama atafanya hivyo, basi ni haki ya Allah swt kumchoma moto katika Jahannam. (Hadi hapo atakapofanya Tawba)"
Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 6.
Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
:
"Yeyote yule anayezidisha mapenzi yetu (Ahlul Bayt a.s) basi na atazidisha mapenzi yake kwa mke wake vile vile"
Wasa'il ush-Shi'ah, J. 14, Uk. 11.
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Bora katika wake zenu ni yule ambaye ni mcha Allah swt na mtiifu kwa mume wake katika mapenzi na kujirembesha (lakini sio kuwavutia wanaume wengine)"
Wasa'il ush- Shi'ah, J. 20, Uk. 30.
ZINAA NA ATHARI ZAKE MBAYA
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Imeandika katika Tawrat: Mimi ni Allah swt, muuaji wa wauaji na muadhibu wa wazinifu"
Al-Kafi, J. 5, Uk. 554.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
:
"Ziko athari sita za zinaa, tatu ambazo zinapatikana humu duniani na tatu zitapatikana huko akhera. Zile zitakazoonekana duniani: Itaondao heshima ya mtu na kumdhalilisha; Itamfanya mtu awe maskini; na Itafupisha umri wa maisha yake (yaani atakufa haraka
Na zile zitakazo patikana Akhera ni: Adhabu za Allah swt, Hali ngumu kabisa katika utoaji wa hesabu, na Kutumbukizwa katika Jahannam kwa ajili ya milele"
Al-Kafi, J. 5, Uk. 541.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Kutokea Tawrat kuiwa:"Enyi watu msizini kwa sababu mkifanya hivyo wake zenu pia watafanya vivyo hivyo. Kile mkipandacho ndicho mtakacho kivuna. (kila ufanyavyo na wewe utafanyiwa hivyo".
Al-Kafi, J. 5, 554.
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Yeyote yule amkumbatiaye m wanamke, ambaye ameharamishiwa kwake, basi atafungwa kwa minyororo ya mioto pamoja na Shaytani na wote kwa pamoja watatupwa katika Jahannam"
Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 14.
AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ
Al Imam Ja'afer as-Sadiq
wakati mmoja aliulizwa na 'Amar ibn Mussa kuhusu kufanya tendo la kujamiiana pamoja na wanyama au kujitoa manii kwa mkono au kwa kutumia sehemu zinginezo za mtu mwenyewe, na Imam a.s. alimjibu:
"Hali yoyote katika hizi na vyovyote vile ambavyo mwanamme humwaga maji yake, inachukuliwa kuwa ni zinaa (na imeharamishwa"
Al-Kafi, J. 5, Uk. 541.
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Amelaaniwa! Amelaaniwa yule mtu ambaye anafanya tendo la kuwaingilia wanyama"
Al-Kafi, J. 2, Uk. 270.
MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
:
"Zinaa miongoni mwa jamii moja) mwanamme kwa mwanamme au mwanamke kwa mwanamke (ni zinaa".
Kanz-ul- 'Ummal, J. 5, Uk. 316.
ULAWITI
AL-IMAM AS- SADIQ
Amesema al-Imam as- Sadiq
katika Al-Kafi :
"Kuingiza (uume) mwanzoni mwa nafasi ya haja kubwa ni dhambi kubwa kabisa hata kuliko kuingizia katika sehemu ya mbele ya siri ya mwanamke. Kwa hakika Allah swt ameangamiza ummah mzima wa Mtume Lut
kwa sababu wao walijiingiza katika laana ya ulawiti. Allah swt kamwe hakumteketeza hata mtu mmoja kwa dhambi za zinaa"
MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w)
,Wasa'il al-Shiah :
"Mtu yeyote anayetenda ulawiti pamoja na kijana wa kiume atapatwa na janabah (uchafu) ambao hautaweza kutakasishwa hata kwa maji ya dunia nzima. Allah swt atamghadhabikia na kumlaani vikali. (Yaani Allah swt atazichukua rehema na baraka kutoka kwake na kumlipa Motoni i.e. Jahannam). Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa ! Pepo (Jannah) zitakuwa zimemkasirikia mno. Na mtu ambaye anakubali kulawitiwa kwa nyuma, basi Allah swt humweka ukingoni mwa Jahannam (motoni penye moto mkali kabisa) na atamweka huko hadi hapo atakapo maliza kuwahoji watu wote. Hapo ndipo atakapo mwamrisha kuwekwa Motoni. Atapitia adhabu moja baada ya pili hadi kuzimaliza adhabu zote za Jahannam na hadi atakapofikia daraja la chini kabisa. Na kamwe hataweza kutoka hapo"
AL-IMAM 'ALI IBN ABI TALIB
Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
amesema katika Al-Kafi:
"Ulawiti ni moja ya Madhambi Makuu na inaadhibu pale mtu mmoja anapompanda mtu bila ya kumwingilia. Na iwapo atamwingilia kwa nyuma basi hiyo itakuwa ni kufr (ukafiri)"
AL-IMAM AS- SADIQ
Hudhaifa ibn Mansur anasema :
"Mimi nilimwuliza al-Imam as- Sadiq
kuhusu Dhambi Kuu?
al-Imam as- Sadiq
akajibu: "Kubana kwa sehemu za kiume baina ya mapaja mawili kwa njia isiyoruhusiwa."
Nikamwuliza tena, "Je ni mtu gani anayetenda dhambi la ulawiti ?" Al-Imam as- Sadiqe
alinijibu :
"Yule ambaye amekufuru kwa Allah swt kwa yale aliyoteremshiwa Mtume Muhammad
(Qur'an tukufu )"
Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
kwa kumjibu Abu Basir kuhusu Qur'an Tukufu, Surah Hud, 11, Ayah 82, isemayo :
﴿فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ﴾
'Basi ilipofika amri yetu, Sisi tuliibinua (mji) juu chinii, na kuwateremshia mvua ya mawe magumu ya udongo uliopikwa, tabaka juu ya tabaka'
Al-Imam as- Sadiqe
alimjibu:
"Yupo mtu ambaye anaiaga hii dunia huku akisadiki kuwa ulawiti ni halali, lakini Allah swt anampiga kwa jiwe moja ambalo liliwadondokea watu wa Mtume Lut
Walivyoadhibiwa Umma wa Mtume Lut
Qur'an tukufu imeelezea aina tatu za adhabu zilizoteremshiwa umma wa Mtume Lut
"Sauti kubwa ya kutisha na mayowe ya kusikitisha na makubwa mno "Kupigwa kwa kutupiwa mawe juu yao " Kupindua ardhi juu chini"
Baada ya kutaja adhabu hiyo ya tatu, imeelezwa katika Sura Hud,11, 83:
﴿ مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ وَمَا هِيَ مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ﴾
'Mawe hayo ya udongo uliopikwa) yalikuwa yametiwa alama (za adhabu) za Mola wako; Na wala haipo (maangamizo ya miji) mbali kutoka wadhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya'.
AL IMAM 'ALI AR-RIDHA
Al Imam 'Ali ar-Ridha
amesema : katika Fiqh-i-Ridha
"Jiepusheni na ulawiti na zinaa, na huu ulawiti ni chafu na mbaya kabisa kuliko zinaa. Madhambi haya mawili ndiyo vyanzo vya mabaya sabini na mbili ya humu duniani na Aakhera."
Qur'an tukufu imetumia neno 'utovu wa adabu, uchafu' kwa ajili ya zinaa kwa njia ambayo imetumika vile vile kwa ajili ya ulawiti. Twaambiwa katika Surah A'araf, 7, : Ayah 80 - 81
﴿وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ﴾
'Na (Sisi tulimpeleka) Lut, wakati alipowaambia watu wake:"Je ! Mwatenda jambo chafu ambalo halikutendwa na yeyote kabla yenu katika ulimwengu'
"Nyinyi mnawaendea wanaume kwa hamu (ya kufanyiana uchimvi) badala ya wanawake; Ama nyinyi ni watu wafujaji.'
. Kumtazama kijana mdogo wa kiume kwa macho ya ashiki au uzinifu ni Haraam kabisa, hususan kijana ambaye bado hajaota nywele za usoni mwake. Madhara na adhabu za mtazamo wa ashiki au uzinifu vinazungumziwa kwa mapana na marefu katika maudhui yanayozungumzia zanaa.
Vile vile Mtume Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w)
katika Wasa'il al-Shiah
"Jiepusheni na kuwatazama kwa macho ya ashiki au uzinifu vijana wa matajiri na watumwa, hususan wale ambao hawajaota hata ndevu. Kwa sababu uchokozi unaofanywa kwa mitazamo ya aina hiyo ni mbaya kabisa kuliko uchokozi wa kuwatazama hivyo wasichana wadogo walio katika hijabu."
NI HARAAM KUMBUSU KIJANA WA KIUME KWA KUASHIKI
AL-IMAM AS- SADIQ
Amesema Al-Imam as- Sadiq
katika Al-Kafi kwa; kumnakili Mtume Muhammad(s.a.w.w)
:
"Iwapo mtu atambusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki, basi Siku ya Hukumu (Siku ya Qiyama), Allah swt atamfunga mdomoni mwa mtu huyo hatamu ya moto"
AL-IMAM AR-RIDHA
Al-Imam ar-Ridha
amesema katika Fiqh-i-Ridha:
"Wakati mtu anapombusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki (mapenzi au nyege) basi Malaika wa mbinguni na Malaika ardhini , Malaika wa Rehema na Malaika wa adhabu wote kwa pamoja humlaani huyo mtu. Na allah swt humtolea hukumu yake kwenda Motoni (Jahannam). Loh ! mahala pakutisha mno"
MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)
Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w)
katika Mustadrakul Wasail:
"Allah swt atamwadhibu Motoni (Jahannam) kwa maelfu ya miaka mtu ambaye anambusu kijana wa kiume kwa ashiki au matamanio ya mapenzi."
Wanazuoni wanasema kuwa wanaume wawili kulala pamoja chini ya blanketi au shuka moja bila mavazi kunawapa adhabu kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu, navyo pia ni miongoni mwa madhambi makuu.
Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w)
, Wasa'il al-Shiah:
"Tengenezeni vitanda vya kulalia tofauti kwa ajili ya watoto wenu wanaozidi umri wa miaka kumi. Ndugu wawili wa kiume au ndugu wawili wasichana au ndugu na dada yake wasilazwe pamoja katika kitanda kimoja"
Kwa mujibu wa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
"Mtu aliyetenda dhambi kama hili, mwili wake uchomwe moto hata baada ya kuuawa kwa njia nyingine. Yaani akishauawa kwa adhabu atakayoiamua Qadhi, basi baada ya kuuawa mwili wake uchomwe moto.
Tunakuleteeni hadith ya Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
aliyoisema:"Mtu yeyote anayestahili kuuawa mara mbili kwa kupigwa mawe basi huyo ni mlawiti"
Ni lazima ujilikane wazi wazi kuwa mwanamme yeyote anayemlawiti kijana wa kiume (anamwingilia sehemu za haja kubwa), basi wafuatao watakuwa wame haramishwa kwake:
" mama wa kijana huyo, " dada na " binti yake huyo kijana kwa maisha yake yote. " Yaani, mtu huyu (mlawiti) kamwe hataweza kumwoa mama yake, au dada au binti ya huyo kijana.
AL IMAM JAAFER SADIQ
Al Imam Jaafer Sadiq
amesema:
"Allah swt ameweka adhabu sita kwa wale watendao zinaa ambapo adhabu za aina tatu wanazipata humu humu duniani na zinazobakia hizo tatu wanazipata huko Akhera. Adhabu hizo zilizowekewa humu duniani ni: "Wanapoteza nuru " Wanakuwa maskini Maisha yao yanakuwa mafupi. Adhabu tatu zilizowekewa Akhera ni:- " Allah swt atakuwa amewakasirikia mno "Watahesabiwa siku ya Qiyama kwa Sharia kali " Wataishi milele Jahannam.
MTUME MTUKUFU (S.A.W.W)
Mtume Mtukufu(s.a.w.w)
amesema:
"Manukato ya Jannat yataweza kusikika hadi umbali wa miaka. Hata hivyo yule mtoto ambaye amekanushwa na wazazi yaani wazazi wamesema sio mtoto wao tena, na mtu yule ambaye haonyeshi huruma kwa jamaa zake na yule mtu mzee anafanya zinaa, hao ndio watu hawataweza kusikia manukato ya Jannat." Iwapo mwanamme aliyebaleghe atafanya Ulawiti na kijana wa kiume, basi mama, dada na binti wa mtoto huyo atakuwa haramu kwa ajili yake. Na Sharia kama hii itatumika wakati ambapo mtu ambaye amelawitiwa ni mwanamme mtu mzima, au wakati mtu anayelawiti ni kijana ambaye hajabaleghe. Lakini iwapo mtu atakuwa na shaka iwapo kikofia cha uume wa mwanamme umeingia katika sehemu za haja kubwa au haikuingia, basi katika sura hiyo mwanamke katika kikundi cha hapo juu hawatakuwa haramu kwa ajili yake. Iwapo mwanamme atamuoa mama au dada wa kijana mvulana, na akamlawiti huyo mvulana baada ya ndoa kwa misingi ya tahadhari hao watakuwa ni haramu kwa ajili yake.