MUANDAMO WA MWEZI

MUANDAMO WA MWEZI 12%

MUANDAMO WA MWEZI Mwandishi:
Kundi: Midahalo na majadiliano kielimu

MUANDAMO WA MWEZI
  • Anza
  • Iliyopita
  • 23 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 63012 / Pakua: 7163
Kiwango Kiwango Kiwango
MUANDAMO WA MWEZI

MUANDAMO WA MWEZI

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

6

7

8

19

MUANDAMO WA MWEZI

SEHEMU YA KUMI NA NANE

KUFUNGWA KWA MASHETANI

MUNASEMA

18. Kufungwa Kwa Mashetani Katika kejeli zake ndugu Juma kwenye hoja za Kidini, hata katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anathubutu kuyaumbua kwa kusema kama ifuatavyo: ((Hoja nyengine - ya mitaani - inasema kwamba Ramadhani inapoingia hupatikana rehema fulani. Miongoni mwa hizo ni kuwa mashetani wote hufungwa kama Bwana Mtume(s.a.w.w) alivyosema: "Ramadhani ikiingia, milango ya mbingu (na katika riwaya ya pili) milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya jahannam hufungwa na mashetani hutiwa minyororo." Na Hadithi nyengine inasema: "Inapoingia siku ya kwanza ya Ramadhani upepo hupiga chini ya Arshi kutoka katika majani ya pepo (kuwapiga upepo huo) Mahuru-Al-ain.)

Maneno kama haya ya kuyakejeli na kuyabeza maneno matukufu ya Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuyafanya kama kwamba ni maneno ya mitaani au kuifanya haki kuwa batil ni katika mambo yanayompelekea mtu kuingia katika kufru. Kitu cha msingi ni vyema kukumbuka kwamba Shaykh Naaswir Bachuu hakuonesha lugha za kashfa na kejeli hata katika yale maeneo ambayo hakukubaliana nayo basi pia alitumia lugha ya kistaarabu.

JAWABU

Kejeli iko wapi hapa? Je mimi niliyaita maneno ya Mtume(s.a.w.w) kuwa ndio hoja ya mitaani au niliita kule Sheikh Nassor Bachoo kutoa hoja kwa Hadithi hio kuwa ndio hoja ya mitaani? Ebu Soma yote niliosema. Nilisema: Hoja nyengine - ya mitaani - inasema kwamba Ramadhani inapoingia hupatikana rehema fulani. Miongoni mwa hizo ni kuwa mashetani wote hufungwa kama Bwana Mtume(s.a.w.w) alivyosema: "Ramadhani ikiingia, milango ya mbingu (na katika riwaya ya pili) milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya jahannam hufungwa na mashetani hutiwa minyororo." Na Hadithi nyengine inasema: "Inapoingia siku ya kwanza ya Ramadhani upepo hupiga chini ya Arshi kutoka katika majani ya pepo (kuwapiga upepo huo) Mahuru-Al-ain."

Tunachojifunza kutokana na Hadithi hizi ni kuwa:

1) Ramadhani ni moja!!!

2) Neema hizo za kufungwa mashetani na nyenginezo hupatikana siku ya mwanzo ya Ramadhani. Sasa je:

a) Rehema hizi watazipata dunia nzima au wale waliouona mwezi tu?!!!

b) "Inapotokea nchi fulani kama Saudia (Makka & Madina) imeingia katika Ramadhani, Tanzania wanangoja mwezi wao.

Je inaaminika kwamba wale mashetani walioko nchini S. Arabia yatakuwa yamefungwa na mashetani yalioko Tanzania watabaki huru bado? Au tudhani mashetani yalioko S. Arabia yatakimbilia huku Tanzania mbio kuja 'kuvunja jungu' kwa kuwa Ramadhani haijaingia huku bado?"

c) Je mtu aliyeanza kufunga S. Arabia siku ya mwanzo, siku ya pili akaja Tanzania wakati bado watu hawajaanza kufunga, vipi ile rehema ya kufungiwa mashetani ataipata, au watafungwa kwa ajili yake tu?!!!

d) Je mtu huyu aliyeanza kufunga Ramadhani S. Arabia kisha alipokuja Tanzania Ramadhani bado je ataambiwa kaja kufunga Ramadhani au kafunga Ramadhani Saudia na kaja kufunga Shaabani huku Tanzania.

e) Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu?!

Masuala haya nimeyanukuu kimaana kutoka katika kitabu cha Sheikh Bachoo , nayo ni masuala ya kuchekesha na kustaajabisha!!! Lau tutakwenda mahala kama Al-azhar au chuo chochote kile kikubwa tukatoa hoja hizi, basi hata yule anayeona kwamba kauli sahihi ni kauli ya kufunga kwa muandamo mmoja basi atacheka sana!!!

Ama kuhusu suala la kwanza kwamba Hadithi hizi zinathibitisha kuwepo Ramadhani moja, Jawabu yake ni kuwa Ramadhani kweli ni moja. Na kwani ni nani kasema kwamba kuna Ramadhani mbili katika mwaka? Ramadhani ni moja katika mwaka isipokuwa inatangulia kuingia katika miji fulani na kuchelewa katika miji myengine, kama vile ambavyo - katika Ramadhani moja hio hio, tunatangulia kufunga katika baadhi ya miji kwa kutangulia kuchomoza alfajiri na tunachelewa kufunga katika miji myengine kwa kuchelewa kuingia alfajiri. Na tunatangulia kufuturu katika miji myengine kwa kutangulia kutua kwa jua na tunachelewa katika miji myengine kwa kuchelewa kutua kwa jua. Na hii haina maana kwamba kuna Ramadhani tano au kumi.

Ramadhani zingelikuwa mbili lau ingelikuwa tunafunga mwezi huo wa Ramadhani, na mwezi mwengine, mathalan tunafunga na mfunguo sita, lakini tunafunga mwezi mmoja, tafauti ni katika kutangulia na kuchelewa tu, basi vipi mtu atatoa hoja kama hio!!! Tazama ukweli kwamba, pia kuna watu wanatangulia kusali Adhuhuri na wengine wanachelewa kwa masaa mengi, wala haisemwi kwamba kuna Adhuhuri tatu au nne. Kwa hivyo, dai hili halina muelekeo kabisa wala halifai kuzungumzwa na wanavyuoni wala wanafunzi, dai hili linafaa kuzungumzwa na watu wasiojua Dalili za Kisharia.

Pili : ni kuwa Hadithi mbili hizo alizozinukuu Sheikh Bachoo hazitoi ushahidi huo kamwe wa kuwa na Ramadhani moja, kwani mantiki ya kusemwa "Ikiingia Ramadhani" ni sawa sawa na kusemwa: "Ikiingia J/tatu" au kusemwa "Ukiingia usiku" na hii haina maana kwamba J/tatu ikianza kuingia sehemu moja huwa imeingia dunia nzima: bali ikianza kuingia sehemu moja - yaani baada ya kutua jua magharibi - sehemu nyengine bado ni J/pili asubuhi. Halkadhalika kusemwa "Ukiingia usiku" kama Allah alivyosema: Usiku ulipomuingilia: haina maana kwamba usiku ukiingia sehemu moja ndio umeingia dunia nzima. Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu.

Ama suala linalosema: "Je mtu huyu aliyeanza kufunga Ramadhani S. Arabia kisha alipokuja Tanzania Ramadhani bado je ataambiwa kaja kufunga Ramadhani au kafunga Ramadhani Saudia na kaja kufunga Shaabani huku Tanzania Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu?!" Jawabu yake ni kuwa: je mtu aliyepanda ndege siku ya J/pili - mathalan - ikamkuta magharibi humo katika ndege katika sehemu fulani ya anga ya dunia akafuturu, kisha baada ya saa moja au mbili akaingia katika anga ya nchi nyengine bado ni saa 9 za jioni ya siku hio hio ya J/pili, funga yake itakuwaje: je ataambiwa kafunga huyu siku ya J/pili au kafunga nusu ya siku hio katika sehemu moja ya dunia na kala katika sehemu nyengine ya dunia?

Tena mara ya pili: je mtu aliyepanda ndege akaanza kusali Adhuhuri humo katika sehemu ambayo jua tayari limetenguka au akasali magharibi katika sehemu ambayo jua tayari limezama na kabla ya kumaliza ikawa ndege imeingia katika sehemu ambayo jua bado halijatenguka au halijazama, je yule aliyesali Adhuhuri ataambiwa kasali Adhuhuri au kasali nusu adhuhuri na nusu Dhuha?! Na yule aliyesali magharibi atakuwa kasali magharibi au kasali sala ambayo nusu yake ni magharibi na nusu yake ni laasiri kipande: yenye rakaa tatu? Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kule. Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga.

Sasa cha muhimu kujua ni kuwa Dini ya Kiislamu imeyagawa mambo katika sehemu nne kuu. Moja ni kitu ambacho kimeelezwa katika Qur-an kwa uwazi. Pili ni kitu ambacho kimeelezwa katika Sunnah (Hadithi) kwa uwazi. Tatu ni kitu ambacho Umma umekubaliana juu ya kitu hicho. Mambo matatu haya hayafai kupingwa: ni lazima tufanye vile vile ilivyoelezwa kwa uwazi. Sasa mambo mengine (ambayo ndio ya nne) ni yale ambayo hayakuelezwa kabisa au hayakufafanuliwa nayo ni kama hayo:

1) Aliyefunga katika nchi fulani kisha akaja katika nchi nyengine watu wako katika Shaabani.

2) Kama tulivyosema: "Aliyepanda ndege siku ya J/pili - mathalan - ikamkuta magharibi humo katika ndege katika sehemu fulani ya anga ya dunia akafuturu, kisha baada ya saa moja au mbili akaingia katika anga ya nchi nyengine bado ni saa 9 za jioni ya siku hio hio ya J/pili ya tarehe hio hio alioiwacha katika nchi alioondoka, funga yake itakuwaje: je ataambiwa kafunga huyu siku ya J/pili au kafunga nusu ya siku hio katika sehemu moja ya dunia na kala katika sehemu nyengine ya dunia?"

3) Aliyesali Magharibi katika ndege baada ya kutua jua kabla ya kumaliza sala yake ndege imeingia katika anga ambayo jua lake bado halijatua, je itakuwaje sala yake.

Mas-ala haya na yalio mfano wa haya hayana andiko maalumu lililo wazi, kwa hivyo huitwa mas-ala ya ijtihadi. Kila aliyefikia daraja ya kuitwa Mujtahid atatoa fikra yake akijiongozea kwa dalili za Kisharia (Qur-an, Sunna, Ijmaa (makubaliano ya Umma) au Qiyas (analogy). Kwa hivyo, utaona kwamba bado tuna tatizo la kutokufahamu tafauti baina ya mas-ala ya ijtihadi na yale yasio ya ijtihadi. Mas-ala ya kutokufata muandamo wa mbali yamethibiti kwa Hadithi ya Mtume (s.a.w.) katika riwaya hio ya Ibn Abbas na Kuraib, kwa hivyo haya si mas-ala ya ijtihadi, lakini furui (matawi) tunazozipata katika mas-ala haya na ambazo hazikuelezwa kwa uwazi, ndizo za kufanyiwa ijtihadi.

Sasa kwa ufupi ni kuwa jawabu ya suala "Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu" aliyefunga Ramadhani S. Arabia na alipokuja Tanzania akakuta watu wanakula bado ni Shaabani, jawabu ya suala hili ni jawabu ya masuala mawili tulioyatoa, nayo ni masuala ya aliyefuturu na aliyesali kwenye ndege. Na hii ni kuwa:

1) Ima aliyesali basi sala yake aliosali mwanzo aitupilie mbali na aanze upya kwani katika sehemu alio bado wakati wa Sala haujaingia. Halkadhalika aliyefuturu. Ukichukua msingi huu, basi na aliyefunga Saudia Ramadhani na alipokuja Tanzania akaikuta Shaabani bado imo, basi saumu yake asiizingatie na aanze upya kwani katika sehemu alio bado wakati wa kufunga haujaingia.

2) Au asirejee tena sala yake kwani kasali kwa mujibu wa wakati sawa huko alikotoka. Halkadhalika aliyefuturu. Basi na huyu aliyetoka Saudia naye aendelee kufunga kwa kuzingatia kwamba kafunga sawa kwa mujibu wa kule anakotoka. Kwa hivyo, chagua jawabu unayotaka katika mas-ala haya mawili ya aliye kwenye ndege, kisha jawabu yako hio utayoichagua ndio jawabu yetu kwako kwa yule aliyefunga S. Arabia na akaja Tanzania hali ya kuwa bado ni Shaabani.

Ama masuala ya kufungwa mashetani hayana uhusiano kabisa na masuala ya kuthibiti muandamo wa mwezi katika miji pasi na kuthibiti katika miji myengine. Na kipi kinatujuilisha sisi kwamba mwezi ukiandama sehemu moja hufungwa mashetani wa dunia nzima au kila mahala hufungwa mashetani kwa mujibu wa muandamo wa mwezi wa mahala hapo? Kipi kitatujuilisha mas-ala haya. Haya ni mas-ala ya ghaibu wala hayatakiwi kabisa kuhusishwa na mas-ala ya dhahiri. Hadithi inatueleza kwamba mashetani hufungwa. Vipi wanafungwa: hakuna ufafanuzi. Na mas-ala haya ni mas-ala ya itikadi haitakiwi kusema kwa ijtihadi na rai wala kwa kusukuma. Bali Hadithi hio inabidi itazamwe, ikiwa ni Hadithi sahihi na ni mutawatir basi tuikubali; ikiwa sahihi lakini ni Ahadi basi tutatazama ikiwa Umma umekubaliana juu ya maana yake, itakuwa imepata nguvu kwa Ijmaa (makubaliano) ya Umma; ikiwa kuna khilafu nayo ni Hadithi Ahadi basi tuiache kama ilivyo, kwani Hadithi Ahadi haijengewi hoja katika mambo ya itikadi, kama Jumhuri ya Umma ilivyosema. Mwisho wa kunuu nilioyasema katika kitabu.

Hayo ndio nilioyasema. Haya nionesheni hapa wapi nimeyakejeli maneno ya Mtume(s.a.w.w) . Mimi ninachokipinga ni kuzichukua Hadithi hizo za kufungwa kwa mashetani kama ni ushahidi wa kuwepo kwa muandamo mmoja: sio kuzikejeli Hadithi hizo. Bali nimesema katika maelezo ya chini: "Ibn Hajar ana maelezo mazuri kuhusu Hadithi ya kufungwa mashetani. Tazama Al-Fat-Hu katika sherehe ya Hadithi na. 1899". Sasa tuseme ndio mumekuwa hamufahamu kiasi hiki au muna lengo lenu?!

Munasema Tukirudi katika mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kufungwa kwa mashetani tunazingatia juu ya kuingia kwa mwezi wa Ramadhaan, kwani maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yamekuja katika matamko yasemayo: (Inapoingia siku ya mwanzo ya Ramadhaan mashetani hufungwa)

Ndugu Juma akiendelea kudai kwamba: (Ikiingia Ramadhani" ni sawa sawa na kusemwa: "Ikiingia J/tatu" au kusemwa "Ukiingia usiku" na hii haina maana kwamba J/tatu ikianza kuingia sehemu moja huwa imeingia dunia nzima: bali ikianza kuingia sehemu moja - yaani baada ya kutua jua magharibi - sehemu nyengine bado ni J/pili asubuhi.)

Hayo ndio kama yale tunayomueleza ndugu Juma kila mara kwamba Suala la kutangulia mchana au usiku sio hoja katika mas-ala ya muandamo wa mwezi. Hilo ni jambo lisilowezekana kutumia "Qiyaas" cha mwezi na jua. Hapawezekani kutumiwa "Qiyaas" cha Swala, kuanza kufutari wakati wa magharibi au nyakati za kula daku kabla ya alfajiri hata katika nchi moja kuna kutafautiana katika kuingia mchana na usiku pia kuna kutafautiana katika kuingia "siku." Tuchukulie mfano Dar es Salaam inaingia katika siku ya Jumapili pale jua linapotua, wakati huo huo Kigoma bado iko katika siku ya Jumamosi jioni. Lakini kumbuka kwamba wanafunga siku moja ya muandamo wa mwezi mmoja. Tukichukua mfano mwengine wa nchi kubwa kama Canada au Urusi, ndani ya nchi hizo kuna tafauti ya masaa mengi kutoka mashariki hadi magharibi zake.

JAWABU

Haya yote nimeshayaeleza - mas-ala ya Qias, mas-ala ya kuwa na nyakati tafauti za kufuturu katika nchi moja yote mumeyakariri mara elfu na tumeshayaeleza sana. Lakini pamoja na hayo, hayana uhusiano na maudhui iliopo hapa. Maudhui ya hapa ni kufungwa kwa mashetani na hili pia nimeshakufafanulieni kwamba si hoja ya kuwa tuwe na muandamo mmoja wala mas-ala hayo hayapo kamwe katika uwanja wa elimu.

MNASEMA

Akiendelea kutoa hoja zake ndugu Juma juu ya kufungwa kwa Mashetani anahoji: (Na kipi kinatujuilisha sisi kwamba mwezi ukiandama sehemu moja hufungwa mashetani wa dunia nzima au kila mahala hufungwa mashetani kwa mujibu wa muandamo wa mwezi wa mahala hapo?) Hapa Ndugu Juma amekuja na dhana kwamba mashetani hufungwa pale tu ilipoingia Ramadhaan. Na sisi tunamuuliza ni wapi ameona kuwa ikiingia Ramadhaan hufungwa mashetani wa sehemu hiyo tu iliyoandama mwezi?

JAWABU

Hilo suala jijibuni wenyewe kwani mimi sijasema hivyo wala sijaja na dhana hio, ingawa nadai kwamba inawezekana ikawa hivi na inawezekana ikawa hivi: hakuna ushahidi wa mkato juu ya vipi mashetani wanafungwa. Na mimi nilichokisema ni hiki: Ama masuala ya kufungwa mashetani hayana uhusiano kabisa na masuala ya kuthibiti muandamo wa mwezi katika miji pasi na kuthibiti katika miji myengine. Na kipi kinatujuilisha sisi kwamba mwezi ukiandama sehemu moja hufungwa mashetani wa dunia nzima au kila mahala hufungwa mashetani kwa mujibu wa muandamo wa mwezi wa mahala hapo? Kipi kitatujuilisha mas-ala haya.

Haya ni mas-ala ya ghaibu wala hayatakiwi kabisa kuhusishwa na mas-ala ya dhahiri. Hadithi inatueleza kwamba mashetani hufungwa. Vipi wanafungwa: hakuna ufafanuzi. Na mas-ala haya ni mas-ala ya itikadi haitakiwi kusema kwa ijtihadi na rai wala kwa kusukuma. Bali Hadithi hio inabidi itazamwe, ikiwa ni Hadithi sahihi na ni mutawatir basi tuikubali; ikiwa sahihi lakini ni Ahadi basi tutatazama ikiwa Umma umekubaliana juu ya maana yake, itakuwa imepata nguvu kwa Ijmaa (makubaliano) ya Umma; ikiwa kuna khilafu nayo ni Hadithi Ahadi basi tuiache kama ilivyo, kwani Hadithi Ahadi haijengewi hoja katika mambo ya itikadi, kama Jumhuri ya Umma ilivyosema.

MNASEMA

Tujuavyo sisi ni kuwa tamko la "Ashshayaattwiinu" kwa hapa lina maana ya mashetani wote dun ia nzima. Tamko lililokuja katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kufungwa kwa mashetani inapoingia siku ya mwanzo ya Ramadhaan yaani, lina "Alif na Laam" ambayo linaonesha ni tamko la umumi ('aam). Neno ni na kawaida ya neno "Ismul-jinsi" linawakilisha maana ya ('aam) yaani linazungumzia "ujumla" au "wote". Baadhi ya vitabu vilieleza kwamba "Ismul-jinsi" kuwa ni ('aam)

Ni vyema kuelewa kuwa msimamo wa Shaykh Naaswir Bachuu katika kitabu chake ni kuwataka Waumini wote wafunge na kufungua kwa "Siku moja" na msimamo wake huo unatokana na Hadiyth sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo na watu wote kwamba: ((Fungeni kwa kuonekana mwezi - muandamo.)) Maneno hayo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yanawajumuisha Waumini wote, popote walipo kama tulivyokwisha elezea hayo katika kurasa zilizopita. Kwa upande wa utekelezaji wa kufunga na kufungua kwa dunia nzima siku moja, uwezekano huo pia upo kama tulivyokwisha elezea kwa urefu.

JAWABU

Madai yenu: "Tujuavyo sisi ni kuwa tamko la "Ashshayaattwiinu" kwa hapa lina maana ya mashetani wote dunia n zima. Tamko lililokuja katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kufungwa kwa mashetani inapoingia siku ya mwanzo ya Ramadhaan yaani, lina "Alif na Laam" ambayo linaonesha ni tamko la umumi ('aam). Madai haya yanaonesha hamujui mukisemacho. Huu sawa ni ujumla lakini kwa mujibu wa qarina (context) ya Hadithi hakuna ulazima wa kuwa iwe ni ujumla wa dunia nzima. Sababu ni kama ilivyo katika Hadithi: "Ikiingia siki ya kwanza ya Ramadhani" na Ramadh ani haiingii dunia nzima kwa wakati mmoja. Bali kuna sehemu imeingia yaani kwa kuingia magharibi na kuna sehemu ni asubuhi - Ramadhani haijaingia. Ni sawa na kusema "Ikiingia J/tatu", J/tatu huwa haiingi dunia nzima wakati mmoja. Kwa hivyo, ujumla uliomo katika mashetani si lazima uwe ujumla wa dunia, bali inawezekana ikawa hivyo, na inawezekana ikawa pale ilipoingia Ramadhani tu, kwani tamko ikiingia siku ya kwanza ya Ramadhani haliuhusu ulimwengu wote. Kwa hivyo, hili ni suala la ghaib na halina ufafanuzi bali lina ihtimalat uwezekano huu na ule. Kwa hivyo, hii si hoja inayokubalika Kisharia.

MNASEMA

Baada ya maelezo kama hayo: Ndugu Juma anatoa hoja za kutokuwepo uwezekano huo kwa kutoa mifano tofauti kama ifuatayo: ((je mtu aliyepanda ndege siku ya J/pili - mathalan - ikamkuta magharibi humo katika ndege katika sehemu fulani ya anga ya dunia akafuturu, kisha baada ya saa moja au mbili akaingia katika anga ya nchi nyengine bado ni saa 9 za jioni ya siku hio hio ya J/pili, funga yake itakuwaje: je ataambiwa kafunga huyu siku ya J/pili au kafunga nusu ya siku hio katika sehemu moja ya dunia na kala katika sehemu nyengine ya dunia? Tena mara ya pili: je mtu aliyepanda ndege akaanza kusali Adhuhuri humo katika sehemu ambayo jua tayari limetenguka au akasali magharibi katika sehemu ambayo jua tayari limezama na kabla ya kumaliza ikawa ndege imeingia katika sehemu ambayo jua bado halijatenguka au halijazama, je yule aliyesali Adhuhuri ataambiwa kasali Adhuhuri au kasali nusu adhuhuri na nusu Dhuha?!))

JAWABU

yetu kwa ndugu Juma ni pale pale kwamba: a). Hayo ni mas-ala ya Ijtihaad kama alivyotaja mwenyewe ndugu Juma kwenye uk 168 wa kitabu chake. Ndio maana hakuna kauli moja ya Wanavyuoni katika mas-ala hayo.

JAWABU

Kwani mimi nilisema hivi kujibu nini. Tafadhali rejeeni mjadala kamili: musikate maneno vipande bila kutimaza maana. Nukta hii ilikusudiwa kujibu kitu maalumu nayo ni kuwa Sheikh Nassor aliuliza masuala haya:

1) Je mtu huyu aliyeanza kufunga Ramadhani S. Arabia kisha alipokuja Tanzania Ramadhani bado je ataambiwa kaja kufunga Ramadhani au kafunga Ramadhani Saudia na kaja kufunga Shaabani huku Tanzania.

2) Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu?!

Hayo ndio masuala yake. Nami nikamjadili kwa kusema: Ama suala linalosema: "Je mtu huyu aliyeanza kufunga Ramadhani S. Arabia kisha alipokuja Tanzania Ramadhani bado je ataambiwa kaja kufunga Ramadhani au kafunga Ramadhani Saudia na kaja kufunga Shaabani huku Tanzania Nini hukumu ya saumu ya mtu huyu?!" Jawabu yake ni kuwa: je mtu aliyepanda ndege siku ya J/p ili - mathalan - ikamkuta magharibi humo katika ndege katika sehemu fulani ya anga ya dunia akafuturu, kisha baada ya saa moja au mbili akaingia katika anga ya nchi nyengine bado ni saa 9 za jioni ya siku hio hio ya J/pili, funga yake itakuwaje: je ataambiwa kafunga huyu siku ya J/pili au kafunga nusu ya siku hio katika sehemu moja ya dunia na kala katika sehemu nyengine ya dunia?

Tena mara ya pili: je mtu aliyepanda ndege akaanza kusali Adhuhuri humo katika sehemu ambayo jua tayari limetenguka au akasali magharibi katika sehemu ambayo jua tayari limezama na kabla ya kumaliza ikawa ndege imeingia katika sehemu ambayo jua bado halijatenguka au halijazama, je yule aliyesali Adhuhuri ataambiwa kasali Adhuhuri au kasali nusu adhuhuri na nusu Dhuha?! Na yule aliyesali magharibi atakuwa kasali magharibi au kasali sala ambayo nusu yake ni magharibi na nusu yake ni laasiri kipande: yenye rakaa tatu? Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kule. Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga. Kwa hivyo, huu ndio mnasaba wa mimi kusema hayo mulioyanukuu. Ama ikiwa hamukujilazimisha kunukuu kitu kwa ukamilifu, mutamfanya msomaji asijue nini hasa kimezungumzwa.

MNASEMA

b). Ndugu Juma anapenda kutumia "Qiyaas" cha Sala na Funga (Swaum) ambapo tumeshaeleza kwamba ni jambo lisilokubaliana kabisa. Hayo tumeyaeleza sana , tatizo sio muandamo mmoja au mingi, hata katika nchi moja inatokea, unaweza kusafiri kwa ndege ukasali katika anga la Dar-es-salaam Adhuhuri ukafika Kigoma bado haijaingia Adhuhuri. Je utasema Dar-es-salaam na Kigoma kila moja iangalie mwezi wake? Au kama utaondoka Dar es Salaam umeshafuturu ukafika Kigoma jua halijatua bado utafanyaje?

JAWABU

Ni kweli: hayo mumeyaeleza sana nami nimekujibuni sana nanyi munakariri yayo kwa yao. Suala la miandamo nimekwambieni haitazamwi nchi moja; inatazamwa tafauti za matalai na umbali wa masafa. Kwa hivyo, hii hoja yenu munayoikariri "Hata nchi moja; hata nchi moja" hii si hoja ya kuzingatiwa, kwani kinachotazamwa ni tafauti za matala na umbali: si nchi moja au nchi tafauti. Ama huyu aliyetoka Dar baada ya kufuturu akafika Kigoma bado jua halijatua, sijui kenda kwa chombo gani, maana Unguja na Pemba kwa ndege - nadhani - haipungui nusu saa; sasa Kigoma yenye tafauti ya dakika 40 kwa mujibu wa maneno yenu na masafa ni marefu mno, sijui kapanda chombo gani!

MNASEMA

Kabla ya kuendelea na ufafanuzi zaidi ni vyema kumnukuu ndugu Juma katika maelezo yake anaposema: (Sasa cha muhimu kujua ni kuwa Dini ya Kiislamu imeyagawa mambo katika sehemu nne kuu. Moja ni kitu ambacho kimeelezwa katika Qur-an kwa uwazi. Pili ni kitu ambacho kimeelezwa katika Sunnah (Hadithi) kwa uwazi. Tatu ni kitu ambacho Umma umekubaliana juu ya kitu hicho. Mambo matatu haya hayafai kupingwa: ni lazima tufanye vile vile ilivyoelezwa kwa uwazi. Sasa mambo mengine (ambayo ndio ya nne) ni yale ambayo hayakuelezwa kabisa au hayakufafanuliwa) Kwa maelezo hayo mazuri aliyoyaeleza ndugu Juma tungependa kumuuliza:

Je suala la kufunga na kufungua kwa muandamo mmoja ataliweka wapi katika mafungu hayo? Bila shaka suala hili litawekwa katika kifungu cha pili. Yaani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelieleza jambo hili kwa uwazi. Riwaya zote zilizokuja katika agizo hili ni sahihi na zenye kukubalika mbele ya Wanazuoni wote wa Kiislamu. Na riwaya zote hizo zimekuja kwa Waumini wote popote walipo watekeleze agizo hilo Mwanachuoni maarufu Al-Jassas katika kitabu chake Ahkamul-Qur-aan J. I uk 305 katika kuielezea kauli hii ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivi:- "Ni jambo linaloeleweka kuwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo: (Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi), ni ya jumla inawahusisha watu wa pande zote za dunia na kwamba haihusu watu wa nchi moja peke yao pasi na wengine."

JAWABU

Tunaendelea kukariri. Suala la kufunga kwa miandamo tafauti limefafanuliwa na Hadithi ya Ibn Abbaas, kilichojificha ni masafa. Ama Hadithi munazosema nyinyi ni Hadithi Aam. Lakini suala ni kuwa je ujmla wenyewe ni ujmla gani. Tumeshakubainishieni kuwa ujmla wenyewe ni kuwa watu wote wanaamrishwa kuwa wasifunge ila kwa kuuona. Ndio maana katika riwaya nyengine ikaja "Musifunge mpaka muuone". Hakuna katika riwaya zote hizo ufafanuzi juu ya suala la kuwa je tufunge kwa muandamo mmoja au kila watu wawe na muandamo wao. Ufafanuzi huu unapatikana katika Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas ambayo munaikimbia: hamuitaki. Kwa hivyo, maneno ya Al-Jassas si sahihi, na kama mulivyosema, maneno ya mwanachuoni hayana kima ikiwa yatakwenda kinyume na dalili. Madai hayo yanaifanya Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas isizingatiwe: iwachwe wakati kanuni ni kutokuliacha andiko lolote litapowezekana kutendewa kazi. Kwa ufupi ni kuwa, hoja hio niliijibu kama ifatavyo: Jambo la pili: la kutazamwa katika Hadithi hii ni kuwa Khitabu (Agizo: kama alivyofasiri Sheikh Nassor Bachoo) ya Hadithi hii ni Aam (ya ujumla), kama Sheikh alivyon ukuu kutoka katika kitabu cha Al-sayyid Saabiq.

Na sisi tunajibu kwa jawabu mbili. Ya kwanza ni kuwa: Ujumla wa agizo hilo, umehusishwa na Hadithi ya Ibn Abbas, na kanuni ya kiusuli inaeleza kwamba Al-khaas (Andiko maalumu au specific) ndio inayotangul izwa kuliko Al-aam (Andiko la ujumla), kwa kuwa kwake (hio Khaas) ni ya uhakika kinyume na Aam hakika yake ni (kitu) cha dhana. Kwa hivyo kanuni hapa inatutaka kuitanguliza Hadithi ya Ibn Abbas. Na natija ni kuwa ujumla jamala uliobakia katika Had ithi "Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi" na ambacho tunachotakiwa sote tukifanye kwa mujibu wa Hadithi hii, ni kuwa sote tufunge kwa kuuona mwezi. Ama je muandamo ni mmoja au kila watu wana muandamo wao, Hadithi hii haitoi jawabu hio.

Jawabu ya pili: ni ile tuliotangulia kuinukuu kutoka kwa Sheikh Ibn Uthaimin aliponukuu jawabu ya wale wenye kusema kwamba kila mji una muandamo wake, ambapo walisema kwamba ujumla uliomo katika Hadithi hio, ni sawa na ujumla uliomo katika Aya inayosema:

﴿ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ ﴾

"Sasa waingiliyeni (wake zenu) na tafuteni kile Allah alichokuandikiyeni, na kuleni na kunyweni mpaka ukubainikieni uzi mweupe kutokana na uzi mweusi wa alfajiri, kisha timizeni saumu hadi usiku."

Je hapa Allah anazungumza na watu wote au na watu maalumu? Je kuzungumza huku na watu wote inamaanisha kwamba alfajiri ya nchi moja ikichomoza watu wa nchi zote wajizuie, au kila watu na alfajiri yao? Jawabu yako hapa ndio jawabu yetu kwa maneno ulioyanukuu kutoka katika kitabu cha Al-sayyid Saabiq kwamba Hadithi hiyo "Fungeni kwa kuuona" ni: "Agizo la ujumla linalojumuisha umma wote (wa Kiislamu) kwa hivyo; yeyote miongoni mwao atakayeuona (mwezi) popote pale; kuonekana huko ku takuwa ni kuonekana kwa wote." Halkadhalika tunajibu ujumla huo kwa Hadithi inayosema:"Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)." Na sisi tunauliza je hapa walikuwa wakiambiwa watu wa Makka tu, au wakiambiwa watu wa nchi zote? Kama walikuwa wakiambiwa watu wa nchi zote, je jua likitua Makka au katika mji wowote ule sote tufuturu? Kwa hakika kila aliyejaaliwa kuwa na mtazamo sahihi, anaona kwamba kujenga hoja kwa ujumla wa Hadithi "Fungeni kwa kuuona" kwamba ni ushahidi wa kuwepo muandamo mmoja, ni kujenga hoja juu ya msingi dhaifu sana. Na kwa maana hio, Ibn Uthaimin (Mwanachuoni wa Kiwahabi) akasema kwamba kauli ya kuwa kila watu wana muandamo wao: "Ina nguvu yake kwa mujibu wa lafdhi (yake) na mtazamo sahihi na Qiyas sahihi vile vile: Qiyas cha wakati wa siku kwa (kuulinganisha) na wakati wa mwezi (month). Mwisho wa kunukuu.

Kwa ufupi ni kuwa, ujumla wa Hadithi inayosema "Fungeni kwa kuuona" ni - kama tulivyotangulia kusema - kwamba watu wote ni lazima wafunge kwa kuuona: si kwa kalenda wala kwa jengine lolote. Huu ndio ujumla unaokusudiwa katika Hadithi hio, au ndio ujumla uliobakia baada ya kuhusishwa au kuvuliwa sehemu ya ujumla huo na Hadithi ya Ibn Abbas na Kuraib.

Jambo la tatu: la kutazamwa katika Hadithi hii, ni kuwa Hadithi hii ni Mutlaq (isiofungamanishwa na kitu) wakati Hadithi ya Ibn Abbas ni muqayyad (iliofungamanishwa). Kanuni ni kuitanguliza muqayyad kuliko mutlaq kama usuli unavyoeleza. Kwa hivyo, kila msingi utaoufata utaona kwamba Hadithi ya Ibn Abbas ndio inayotakiwa itangulizwe.

Ama waliosema kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ukweli ni kuwa wao waliitanguliza rai kuliko kanuni za tafsiri. Walitazama wakaona kuwa mwezi ni mmoja na unakamilisha safari yake mara moja na kwa hivyo muandamo utakuwa mmoja. Lakini tumeona kwamba huu si muandamo wa Kisharia bali ni muandamo wa Kifalaki: muandamo wa Kisharia tunaupata katika kuzijumisha Hadithi tafauti. Pili ni kuwa hio ni rai, na ya Ibn Abbas ni Hadithi; na rai haina uwezo wa kuipinga Hadithi. Kama walivyosema: "Rai haina nafasi mbele ya Andiko."

20

MUANDAMO WA MWEZI

SEHEMU YA KUMI NA TISA

HITIMISHO

19. Hitimisho Kuna milango katika kitabu alichoandika ndugu Juma ambayo hatukupenda kuizungumza, kwani ukichunguza utakuta maneno yake yote yamejengeka katika dhana mbili. Moja ni ile kauli aipendayo kuikariri kwamba (Penye andiko huwa hakuna ijtihadi:) Bila shaka andiko alilokusudia ni ile kauli ya Ibnu 'Abbas (Radhiya Allaahu 'Anhu) alipokataa mwezi wa Sham kwa kusema: (La! Hivi ndivyo alivyotuamuru Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?.) Kwa upande wetu tumejaribu kuilezea kifani kauli hii na tumeonesha kwa kutumia ushahidi mbali mbali juu ya udhaifu unaopatikana katika kuitegemea kauli hiyo katika mas-ala haya.

JAWABU

Ni fani gani mulioitumia kubainisha Hadithi hio? Pili ni kosa kusema kuwa hio ni kauli ikiwa munakusudia kuwa ni ijtihad tu; hio si kauli kwa maana ya ijtihad bali ni Hadithi. Nakukumbusheni maneno yenu muliposema: "Isipokuwa Sahaba akisema: "Tumeamrishwa kadha" au "Tumekatazwa kadha." Jambo hilo hupewa hukumu ya "Rafii" yaani hio inazingatiwa kuwa ni Hadithi ya Mtume(s.a.w.w) . Kwa bahati mbaya, maneno yenu haya - ambayo ni sahihi kwani ndivyo ilivyo katika elimu ya Hadithi - ni kinyume na matendo yenu. Tazama kwamba hamuiti hio kuwa ni Hadithi bali munasema "Kisa" au "Kauli"; wakati muitakayo nyinyi ndio munaita "Hadithi". Hii inaashiria kwamba hamuutaki ukweli bali munataka kulazimisha rai hata kama ni kinyume na fani za elimu.

MNASEMA

Dhana ya pili ya ndugu Juma imejengeka katika msingi dhaifu wala haina nafasi katika uwanja wa fani (kitaalamu) nao ni kule kusukuma kwake juu ya elimu ya Jiografia. Umeonekana udhaifu wake hasa pale alipokuwa akijaribu kuelezea tofauti iliyopo baina ya nchi na nchi katika suala zima la kutofautiana kwa masaa na kuingia kwa usiku na mchana kwa baadhi ya nchi. Kwa upande wa suala hilo pia tumeshalieleza na kulitolea mifano mbali mbali.

JAWABU

Udhaifu munao nyinyi, kwa kudai kwenu kwamba inawezekana kwa ulimwengu mzima kufunga sawa sawa na kwamba wote wanakutana katika usiku na mchana, ilhali kuna sehemu nyingi ambazo zimepishana kwa masaa mengi: huku usiku kule mchana; jua likitua kule huku ni asubuhi. Sasa vipi watafunga sawa sawa na kukutana kwa usiku na mchana. Nyinyi hamuoni haya munavyosukuma kwa kunukuu kanuni za kiusuli halafu hata kuzifasiri hamujui licha ya kuzitumia?! Kanuni nyengine munazinukuu kutolea hoja nazo ni dhidi yenu, yote hayo nyinyi hamuyajui na munasukuma na wenyewe mumeridhia!

MNASEMA

Mwisho tunachukua fursa hii kumuonya ndugu Juma kuwa amuogope Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Akumbuke kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aelewe kwamba ataulizwa juu ya hilo Lingekuwa jambo la busara kama ndugu Juma angalikubali kuuliza na kufanya utafiti zaidi juu ya mas-ala haya kama agizo la Mwenyezi Mungu linavyotutaka.

Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa. (17: 36)

Jawabu

Hii ni nasaha nzuri kwa ndugu kumpa nduguye. Nami nakupeni nasaha yangu kwa udhati: si kwa kukejeli. Tafadhali chukueni vitabu vya fani hususan usulu-fiqhi, usulul-hadith, balagha, nahau na sarfu. chukueni vitabu hivyo, nendeni kwa mtu kama Sheikh Aliyani akusaideni. Au kwa wale walio Pemba nawende kwa mtu kama Sheikh Kabi. Hawa wataweza kukusaidieni kwani wana uwezo mzuri. Vyenginevyo mutakuwa siku zote munasukuma mukinukuu kitu ambacho kukifasiri hamujui wala hamujui mahala pa kukiweka.

Muogopeni Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Kumbukeni kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aeleweni kwamba mutaulizwa juu ya hilo Lingekuwa jambo la busara kama ndugu zetu mungelikubali kuuliza kwani Allah anasema:

﴿ وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ

مَسْئُولًا﴾

Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa. (17: 36)

21

MUANDAMO WA MWEZI

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

MUKHTASARI WA MJADALA

Ndugu msomaji bila shaka umejionea kwamba, katika sehemu zake nyingi, huu si mjadala wa kielimu, bali ni mjadala wa hoja za mitaani safi. Ingawa ndugu zetu wamejaribu kunukuu huku na kule, lakini mara nyingi huwa hicho walichokinukuu hawajui hata tafsiri yake licha ya kujua wapi pa-kukiweka. Sasa baada ya hayo, ningependa kukupa maelezo kwa ufupi kuhusu ikhtilafu hizi za miandamo ya mwezi.

Waislamu wametafautiana juu ya suala la mwezi muandamo: je muandamo mmoja wa mwezi unatosha kwa dunia nzima au kila watu wa matalai fulani wawe na muandamo wao. Wengine wakasema kuwa muandamo mmoja wa mwezi unatosha kwa dunia nzima; wengine wakasema kila watu wa matalai fulani wawe na muandamo wao. Wanaosema kwamba tufunge kwa muandamo mmoja wanatoa hoja kwa Hadithi isemayo: "Fungeni kwa kuuona". Hoja yao katika Hadithi hii ni kuwa Hadithi hii ni ya ujmla: haamrishwi kwayo Muislamu pasi na Muislamu; wala watu wa nchi moja pasi na wengine.

Sisi tunaosema kuwa kila watu na muandamo wao, tumekuwa na jawabu tafauti juu ya maana ya Hadithi hio kama ifatavyo: 1) Ujumla uliomo ndani ya Hadithi hio haurejei katika nchi za dunia; bali unarejea katika uoni wa mwezi muandamo. Yaani maana ya Hadithi ni kuwa watu wote wasifunge ila kwa kuuona mwezi. Huu ndio ujumla uliomo katika Hadithi hio. Ama suala je watu wote wafunge kwa muandamo mmoja au vipi? Hadithi hio haitoi ufumbuzi juu ya suala hilo. Bali hilo linapatika katika Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas.

2) Pili ni kuwa Hadithi hio - katika baadhi ya mazingatio yake - ni 'Aam ya ujumla. Na Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib Khaas. Kanuni ya kufasiria mandiko inasema kwamba Khaas inatangulizwa kabla ya 'Aam.

3) Hadithi hio - katika baadhi ya mazingatio yake - ni mujmal (isiofafanuliwa). Wakati Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib ni mubayyan (iliofafanuliwa). Kanuni ya kufasiria maandiko inasema kwamba mubayyan ndio yenye kutangulizwa kabla ya mujmal; yaani andiko mujmal hurejeshwa katika andiko mubayyan. Tumeiita Hadithi "Fungeni kwa kuuona" kuwa ni mujmal kwa kuzingatia kwamba Hadithi hii haikubainisha je muandamo ni mmoja au kila watu wana muandamo wao? Bali imesema kwa ujumla tu "Fungeni kwa kuuona mwezi" kama Qur-an ilivyosema "Simamisha sala kwa kutenguka jua." Na tumeiita Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas kuwa ni mubayyan kwani - katika qadri hii - imebainisha kwamba muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali.

4) Hadithi hio - katika baadhi ya mazingatio yake - ni mutlaq (isiofungamanishwa na sehemu) wakati Hadithi ya Kuraib na Ibn Abbaas muqayyad (iliofungamanishwa na sehemu pasi na nyengine). Kanuni ni kulirejesha andiko mutlaq katika andiko muqayyad, yaani muqayyad ndio inayotangulizwa. Na kwa hivyo, Hadithi hio ni lazima ifungamanishwe na Hadithi ya Ibn Abbaas ili kufikia maana sahihi. Tumeiita Hadithi hio kuwa ni mutlaq kwa kuwa lafdhi yake haikufungamanishwa na sehemu yoyote, na tukaiita Hadithi ya Ibn Abbaas kuwa ni muqayyad kwani lafdhi yake imefungamanishwa na sehemu moja pasi na nyengine. Kwa hivyo, kwa mujibu wa kanuni zote za tafsiri, natija ni kuwa Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib ni lazima itangulizwe. Jambo jengine ni kuwa ujumla uliomo katika Hadithi hio, ni sawa na ujumla uliomo katika Aya inayosema

﴿أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ

Simamisha sala kwa kutenguka jua .

Hapa pia haamrishwi mtu maalumu, lakini pamoja na hayo nyakati za sala za watu duniani haziungani. Kwa hivyo, ujumla uliopo hapa ni kuwa watu wote kila watu ni lazima wasali adhuhuri kwa kutenguka jua.

Pia ujumla huo, ni kama Hadithi isemayo:"Usiku ukitokeza kutoka hapa na mchana ukaondoka kutokea hapa na jua likatua, basi aliyefunga ameshafungua (au na-afungue)." Na bila shaka ujumla huu maana yake ni kuwa kila watu wafuturu kwa kuzama jua: wala haina maana ya kuungana nyakati za kufuturu. Halkadhalika, ujumla uliomo katika Hadithi: "Fungeni kwa kuuona", utaona - hususan baada ya kuzikusanya dalili zote mbili: Hadithi hio na ya Kuraib - kwamba ujumla uliomo ndani yake ni kuwa watu wote kila watu ni lazima wafunge kwa kuuona: si ujumla wa kuwa watu wote wafunge sawa sawa. Vyenginevyo, itabidi tulitendee kazi andiko moja; na tuliwache jengine na hili ni kinyume na minhaj (methodology) ya tafsiri.

Wanaosema kuwa kila watu na muandamo wao, wanatoa hoja kwa:

1) Hadithi ya Ibn ya Ibn Abbaas na Kuraib isemayo :"Kutoka kwa Kurayb (kasema) kwamba Ummu Al-fadhli bint Al-harith alimtuma Sham (Syria) kwa Muawiya. Akasema: 'Basi nikaenda Sham nikamkidhia haja yake.' Na ukaniindamia (mwezi wa) Ramadhani na mimi niko Sham. Basi nikauona mwezi usiku wa (kuamkia) ijumaa. Kisha nikaja Madina mwishoni mwa mwezi. Basi Abdullahi bin Abbas (r.a.) akaniuliza. Kisha akataja (habari za) mwezi muandamo akasema: 'Lini mumeuona mwezi muandamo?' Nikasema: 'Tumeuona usiku wa (kuamkia) Ijumaa.' Akasema: 'Wewe umeuona?' Nikasema: 'Ndio. Na Watu wameuona na wakafunga na Muawiya akafunga.' Akasema: 'Lakini hakika ya sisi tumeuona usiku wa (kuamkia) Juma Mosi, basi hatuachi kuendelea kufunga mpaka tutimize (siku) thalathini au tuuone.' Nikasema: 'Kwani wewe hutosheki na kuonekana na Muawiya na kufunga kwake?' Akasema: 'Laa' (Sio): Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume(s.a.w.w) ."

Hoja yao humu ni kuwa Ibn Abbaas alipopewa habari za muandamo wa mwezi uliotokea Sham usiku wa Ijumaa, alikataa kuufata na akasema "Hivi (ninavyofanya mimi) ndivyo alivyotuamuru Mtume s.a.w.". Ikafahamika kwa mujibu wa nakala hii kwamba mafunzo ya Mtume(s.a.w.w) ni kutokuuzingatia muandamo wa mbali. Ama wanaosema kuwa tufunge kwa muandamo mmoja wakajibu kwa hoja tafauti, muhimu zao ni hoja sita za Al-Imamu Al-Shawkani ambazo nimezijadili katika kitabu. Na muhimu katika hizo ni kuwa hii ilikuwa ni ijtihad ya Ibn Abbaas. Hoja hii ikajibiwa kwamba Ibn Abbaas katika riwaya hii kasema: "Hivi ndivyo alivyotuamuru Mtume(s.a.w.w) ". Na lafdhi kama hii inaifanya hadithi ihukumiwe kuwa ni marfu'u yaani hukumu yake ni kuwa hio ni Hadithi ya Mtume (s.a.w.). Hivi ndivo elimu ya Hadithi inavyosema.

2) Hoja ya pili ya wale wenye kusema kuwa kila watu na muandamo wao, ni Qiyas cha nyakati za funga na nyakati za Sala na kufuturu kama tulivyoeleza juu. Ubainifu wa hili ni kuwa: a) Wajibu wa Sala umefungamanishwa na kutenguka na kuzama kwa jua - kitu cha kimaumbile (Natural phenomenon). Kwa hivyo mtenguko wa jua ni sababu ya kuwajibika sala.

b) Wajibu wa funga umefungamanishwa na muandamo wa mwezi - kitu cha kimaumbile (Natural phenomenon). Kwa hivyo kuandama kwa mwezi ni sababu ya kuingia kwa wajibu wa funga.

c) Jua - ambalo kutenguka kwake ndio sababu ya kuwajibikiwa na sala - likitenguka katika nchi moja, watu wa nchi nyengine hawawajibikiwi na sala. Kwa hivyo, Qiyas sahihi ni kuwa kuonekana kwa mwezi - ambayo ni sababu ya kuwajibika funga - katika nchi moja isiwe sababu ya kuwajibikiwa na funga kwa watu wa nchi nyengine. Hiki ni Qiyas sahihi kama alivyosema Sheikh Ibn

'Uthaimin. Huu ndio mukhtasar wa suala hili la kuonekana mwezi na anayetaka kwa urefu na arudi katika kitabu Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi cha Sheikh Nassor Bachoo na kitabu Ushahidi Uliowekwa Wazi cha Juma Mazrui. Ahsanteni

Ndugu yenu katika dini

Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui

Tel: 92213669 Al-Qurm, Muscat Oman

E-Mail: jumamazrui@hotmail.com

Jumamazrui@yahoo.com

Tarehe 6/8/2009

MWISHO

14

MUANDAMO WA MWEZI

SEHEMU YA KUMI NA NNE

UFAFANUZI WA AYA ISEMAYO : ATAKAYEUHUDHURIA MWEZI AFUNGE!

MUNASEMA

14.Ufafanuzi Wa Aya Isemayo:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atakayeuhudhuria mwezi afunge!" (2: 185)

Uchambuzi wa neno "shahida" na neno "Shahra"; baadhi ya watu wamedhani kwamba maana ya shahida ni 'kuona kwa macho' na neno Shahra wanadhani kuwa ni 'mwezi - muandamo.' Kwa mujibu wa Wafasirina takr iban wote wamelifasiri neno 'shahida' kwa maana ya "kuwepo" au "kuhudhuria" wala sio maana ya 'kuuona mwezi' hata Shaykh Muhammad 'Aliy Assaabuniy ameona ni makosa kitafsiri kulifasiri neno hilo kwa maana ya "Kuuona mwezi muandamo" kama alivyosema:: 27) "Na wala sio maana ya neno 'shahida' (liliyomo katika Aya hiyo) kwa maana ya kwamba: 'ameuona mwezi." Neno 'shahra' lililomo katika Aya hiyo linaleta maana ya 'mwezi - siku' yaani 'month' kwa lugha ya Kiingereza. Ni mwezi unaoashiria tarehe kuanzia 1 mpaka 29 au 30. Wala neno hilo halina maana ya 'mwezi-sayari' yaani 'crescent' au 'moon' kwa lugha ya Kiingereza.

JAWABU

Kama Shahida ina maana ya kuhudhuria tu, basi maana itakuwa "Atayekuwepo katika mji wa mwezi (month). Na kama ni hivyo, hii ni dalili kwamba kuna miji myengine bado hakuna mwezi (month) kwani Aya imekuja kwa njia ya mafhumu Al-Shati na mafhumu hii ni dalili katika dalili za Kisharia. Na kwa maana hio, itakuwa kuna sehemu mwezi bado haujaonekana; wanaoamrishwa kufunga ni wale ambao mwezi (month) umewaingilia kwa kuuona mwezi (Crecent). Tafsiri yenu inaupa nguvu msimamo wetu: si msimamo wenu. Pili wanavyuoni walioifasiri Aya hio kwa maana ya kuona wako wengi kama nilivyotaja baadhi yao katika kitabu na nitanukuu tena baadae.

MNASEMA

Kitu muhimu ni kuelewa kwamba maneno mawili hayo yaani 'shahida' na 'shahra' yaliyomo katika aya hiyo, yana maana tuliyoieleza hapo juu na ndivyo walivyoeleza Wafasirina wakubwa wote. Ni vyema mtu anapoingia katika mjadala kama huu atoe madondoo sahihi yenye kukubalika sio kuingiza fikra zake tu, hususan katika suala hili la tafsiri. Tukianza kutumia utamaduni huo wa kila mmoja kubuni tafsiri yake mwenyewe na tukaziacha tafsiri za Wanazuoni wenye kutegemewa, jambo hilo litatufanya tuwe na idadi kubwa ya wafasiri 'bandia' ambao sio wafasiri wa kweli.

JAWABU

Wafasirina bandia wamejaa sasa huko Zanzibar, ndio maana ikawa munanukuu kanuni za kiusuli na kuziweka si mwahala mwake bali hata kuzifasiri pia zinakushindeni munafasiri sivyo, halafu munataka kuingia katika mijadala ya elimu kama hii. Pili: Kinachotazamwa si tafsiri za wanavyuoni tu, hususan wasio Masahaba, bali kinachotazamwa ni dalili walizozitoa. Isipokuwa pale walipokubaliana ndio huwa kuna ulazima wa kufata: sio walipotafautiana. Tatu: Kama nilivyosema Wafasirina na Maulamaa wakubwa Mujtahidun walioifasiri Aya hio kwa maana ya kuona wako wengi kama tutavyonukuu maneno yao.

MNASEMA

Vile vile ukizingatia neno 'shahra'﴿ الشَّهْرَ﴾ utaliona katika herufi yake ya mwisho ambayo ni 'Re' imetiwa 'fat-ha' hio haina maana kwamba neno hilo lina maana ya 'mtendwa' kama wanavyodhania baadhi ya watu. Ingaw aje neno hilo limemalizikia 'fat-ha', lakini halina maana ya 'mtendwa' bali neno hilo linaashiria maana ya 'wakati'. Ni muda maalumu kama mfano mtu akisema: "Nitakuja mwezi wa Ramadhaan" hapa hakuna kitu chenye kuonekana bali muda au wakati tu Kinyume na akisema: "Nimeuona mwezi" hapa ndio itakuwa neno 'mwezi' ni 'mtendwa.' Kwa hiyo, wanaotumia Aya hiyo kwa maana ya 'kuuona mwezi kwa macho' sio sahihi kama alivyothibitisha hayo Mwanachuoni - Mufasir katika tafsiri ya 'Al-Kashaaf'. Na vile vile katika kitabu: 'Rawaaiul-Bayaan' yameelezwa hayo hayo.

Kinyume na maneno ya ndugu Juma aliposema: ((Aya hii inawezekana kuchukua tafsiri zote: kushuhudia kwa maana ya kuona na kushuhudia kwa maana ya kuwepo katika mji. Na zote zinakubalika kwa mujibu wa fani za tafsiriInasikitisha sana mar a nyingi kumuona ndugu yetu Juma anavyotoa tafsiri ya baadhi ya Aya za Qur-aan bila kuwapa nafasi Mashaykh wenye kutegemewa katika ulimwengu wa Kiislam. Anachokifanya yeye ni kuingiza fikra zake binafsi katika kufasiri Aya za Qur-aan tukufu. Kitendo ambacho hakikubaliki. Kwani ingekuwa inakubalika hali hiyo bila shaka kusingelikuwa na haja ya kutegemewa tafsiri yoyote, kwani kila mmoja wetu angelikuwa bingwa wa kubuni tafsiri aitakayo mwenyewe - jambo ambalo lingetufikisha pahala pabaya na baya zaidi ni kumsingizia uongo Mwenyezi Mungu katika Maneno Yake Matukufu. Wala hatukusudiwi kwamba hao wafasiri pekee walikuwa kama kwamba wakipata 'Wahyi' na kwamba maneno yao yalikuwa hayawezi kuwa na dosari au kupingwa. La hasha! Kinachokusudiwa ni kuwa anapoingia mtu yeyote katika mjadala wa kutetea hoja juu ya jambo fulani lazima aonyeshe madondoo sahihi yenye kuthibitisha dai lake hilo , sio kutoa fikra zake na zikakubalika. Kinachosisitizwa ni ule umuhimu wa kuonyesha madondoo ya tafsiri ya Aya za Qur-aan alizotegemea sio nafasi ya mtu kutumia akili yake katika maeneo hayo.

JAWABU

Wanavyuoni wa tafsiri hawakukubaliana juu ya suala hili kinyume na munavyodhani nyini. Wako waliosema kwamba neno 'shahra'﴿ الشَّهْرَ﴾ limetiwa fataha kwa kuwa ni dharfu-zaman kama mulivy onukuu nyinyi. Na kuna wengine wengi wanavyuoni wakubwa waliosema kuwa ni 'mtendwa'. Sasa nyinyi ilikuwa mutuoneshe ni ipi kauli sahihi tufate. Anasema Abu Hayyan - baada ya kuitaja hio irabu mulioitoa nyinyi - : "Na wakasema kwamba kunasibika ( kuingia fataha) kwa neno Sha-hr ni kwa kuwa ni (mtendwa). Nayo ni kwa msingi wa kuondoshwa mudhaf na maana ni atayeshuhudia - mtendwa wake akaondoshwa - naye ni mji (misr) au mji (balad)." Na haya yote nilikuelezeni lakini nyinyi hamutazami kilich osemwa: munatazama aliyesema. Kisha Abu Hayyaan akatoa muelekeo mwengine wa neno lililoondoshwa akasema: "Na ikasemwa kwamba kunasibika (kuingia fataha) kwa neno Sha-hr ni kwa kuondoa mudhaf nalo ni neno dukhul". Anasema Mahmud Safi: "(Neno) Al-Shar ni mtendwa, kwa (kukadiria) kuondoshwa mudhaf, na makadirio yake ni dukhulu Al-Shar (kuingia kwa mwezi).

Kwa ufupi ni kuwa wako wanavyuoni waliosema hivi na waliosema vile, tafauti na dhana za ndugu zetu kwamba wanavyuoni wote wamesema kitu kimoja. Na kila tafsiri moja inamuelekeo sahihi. Tafsiri ya kuwa mtendwa hasa ni mudhaf (kaondoshwa), mfano wake ni kama Aya:

﴿وَاسْأَلِ الْقَرْيَةَ الَّتِي كُنَّا فِيهَا وَالْعِيرَ الَّتِي أَقْبَلْنَا فِيهَا ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ

"Kiulize kijiji ambacho tulikuwamo ndani yake" . Sote tunajua kwamba kijiji hakiulizwi wala hakisemi. Hapa mten dwa pia kaondoshwa na asili yake ni : Waulize watu wa kijiji ambacho tulikuwemo ndani yake". Halkadhalika Aya﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ inawezekana ikawa maana yake ni"Ataye shuhudia miongoni mwenu uingiaji wa mwezi" yaani atayekuwepo katika mji wakati mwezi (month) unaingia. Tafsiri hii - kama nilivyosema - inatupa nguvu sisi. Au ikawa maana ni"Ataye shuhudia miongoni mwenu uingiaji wa mwezi" . Na kwa tafsiri hii, neno shahida litakuwa kwa maana ya kuona. Na - kama invyoleweka - kwamba kuweza kujua ni maana gani neno imekusudiwa, ni pale litapokuwa katika sentensi. Na kama neno sh ahida kwa asili halina maana ya kuona; je haliwezi kuwa na maana hio kwa misingi ya kimajazi zikiwepo Qarina?

MNASEMA

Takriban wafasirina wote wa Qur-aan tukufu wameifasiri Aya hiyo kwa maana ya 'atakayekuwa katika mji katika huu mwezi wa Ramadhaan afunge. Hakuna hata mmoja aliye Mwanachuoni wa kweli aliyeifasiri Aya hiyo kwa maana ya 'atakayeuona' au 'atakayeushuhudia' mwezi afunge. Wala hakuna khitilafu katika tafsiri za Wanavyuoni hao juu ya Aya hiyo. Khitilafu iliyopo ni moja tu: Je mwezi ukiandama sehemu moja duniani italazimu kufunga sehemu nyengine zilizobaki au kila sehemu na muandamo wake?

JAWABU

Kwanza: inaonekana hamukuyasoma maandishi yangu kwa makini wala hamujua mimi naeleza nini. Nilichokisema ni hiki: Wanavyuoni wengi wameifasiri Aya hii, kuwa maana yake ni "Atayeuhudhuria mwezi (Month) basi na-aufunge." Kisha wakabainisha kwamba maana ya atayeuhudhuria mwezi, ni atayekuwa katika makazi yake, yaani si msafiri. Nynyi munanijibu "Takriban wafasirina wote wa Qur-aan tukufu wameifasiri Aya hiyo kwa maana ya 'atakayekuwa katika mji katika huu mwezi wa Ramadhaan afunge". Sasa tafauti iko wapi?!

Kisha mukadai yale yale alioyadai Sheikh Nassor kwamba "Hakuna hata mmoja aliye Mwanachuoni wa kweli aliyeifasiri Aya hiyo kwa maana ya 'atakayeuona' au 'atakayeushuhudia' mwezi afunge". Nalo pia ni kosa kwani nakala za wanavyuoni walioifasiri Aya hio kwa maana ya kuona nimekupeni kwa wingi. Nimesema katika kitabu:

1) Abu Al-Suud - katika Maulamaa wa tafsiri - baada ya kuifasiri Aya hio kama alivyosisitiza Sheikh Nassor Bachoo, anasema: "Na ikasemwa kwamba (maana ya Aya hio ni) mwenye kuushuhudia hilala Al-shahri mwezi muandamo wa mwezi (wa Ramadhani) basi naafunge kama kauli yako (unaposema): 'Nimeshuhudia ijumaa yaani Sala yake (Sala ya ijumaa)." Mwisho wa kunukuu. Ni wazi kwamba kwa mujibu wa Abu Al-suud, kuna kauli ya pili juu ya tafsiri ya Aya hii, amba yo wengine wameshikana nayo. Na bila shaka Abu Al-suud hazungumzii watu wa Afrika ya Mashariki.

2) Ibn Al-arabiy. Anasema: "(Aya hii - yaani "Atayeushuhudia mwezi na-aufunge), inafasiriwa kwa kuushuhudia mwezi (month), nako ni kuuona mwezi muandamo, na vivyo hivyo kasema Mtume (s.a.w.): "Fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona." Mwisho wa kunukuu.

3) Ibn Baraka Al-bahlawiy, Al-umaniy, baada ya kuinukuu Aya hio inayosema:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Ataye ushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge." Akasema: "Na kushuhudia kuko kwa namna mbili: kushuhudia katika kuuona (mwezi muandamo) na kushuhudia kwa kujua kama kipofu na yule ambaye uoni wake amepungua kwa sababu ya kufichikana kwa (mwezi) au asiweze kuuona mwezi."

4) Abu Zahra kataja tafsiri ya Aya hio:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Ataye ushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" kwamba maana yake ni:"Atayeushuhudia miongoni mwenu mwezi muandamo wa mwezi (wa Ramadhani)."

5) Ibn Hazm baada ya kuinukuu Aya:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Ataye ushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" anasema: "Atayeuona basi kwa hakika kaushuhudia."

6) Al-Jassas Al-Razi, kaweka mlango aliouita : Babu kayfiyyati shuhudi al-shahri. Hapa Al-imamu Al-jassas, anazungumzia kuandama kwa mwezi ni vipi: nini dhana au mafhum (concept) ya kuandama kwa mwezi Kisheria? Akaanza kwa kunukuu Aya mbili:

Moja : ni Aya inayosema:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" .

Pili : ni Aya inayosema:﴿يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo, sema hivyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na hija" . Kisha akanukuu Hadithi ya Ibn Umar (r.a.), kisha akatoa maelezo mpaka akasema: (Likaonesha hilo kwamba kuuona mwezi muandamo ndio kuushuhudia mwezi (wa siku 29 au 30 yaani month ).

Ni wazi kwamba Al-jassas kaifasiri Aya hii kwa maana ya kuona kwa macho.

Na kabla ya hapa alisema: "Na hukumu zinazopatikana kutoka katika kauli yake (Allah S.W. inayosema):﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" ni kumlazimu kuufunga mwezi yule aliyeshuhudia miongoni mwao. Na kushuhudia kunagawika sehemu tatu: kuujua (kwamba mwezi umeandama), kuwepo katika mji, ..na ikamaanisha pia kwamba aliyeuona mwezi muandamo peke yake basi inampasa kuufu nga." Tazama uzuri maneno haya ya Al-imamu Al-jassas, utaona kwamba kakufasiri kushuhudia kulikotajwa katika Aya kwa tafsiri tatu: moja ya hizo ni kuona.

7) Anasema Al-Imamu Abu Muslim: "Na akauita Allah mwanzo wa mwezi kwa jina la mwezi mzima au pakadiriwe mudhafu (kilichotegemezwa ambacho kimeondoshwa nacho ni Hilal)." Bali Abu Muslim kabla ya hapa kanukuu kauli ya Al-zajjaj akisema "Shahru ni jina la Hilal (mwezi muandamo), ingawa kauli hii Al-imam baadae kaipinga.

8) Sheikh Al-Khalili na Prof Moh'd Bakr Ismail, utaona kwamba dhahiri ya maneno yao katika vitabu vyao ni kuwa Aya hio pia inafasirika kwa maana ya kuona kwa macho, ambapo Sheikh Al-khaliliy anasema hivi: "Na hoja gani basi iliothabiti zaidi na kubwa zaidi kuliko mtu kuuona mwezi muandamo kwa macho yake ambao wajibu wa funga au hukumu ya kufungua zimefungamanishwa nao. Mwenyezi Mungu anasema:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" 9) Ama Prof Moh'd Bakr Ismail yeye anasema kuhusu mtu aliyeuona mwezi peke yake: "Na saumu imemuajibikia peke yake katika hali hii, kwa sababu ya kauli yake Allah (S.W.):﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge".

10) Ibn Uthaimin alipokuwa akielezea tafsiri ya wale wenye msimamo kwamba kila mji na muandamo wake, alisema - kuhusu Aya hio inayosema:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" - maneno haya: "Na inajulikana kwamba haikusudiwi kwa (Aya) hio kw amba kila mtu auone peke yake, basi unatendewa kazi (muandamo huo) katika sehemu (mji) ulioonekana." 11) Al-Sayyid Ahmad Al-Hashimiy, alipokuwa akizungumzia darsa inayoitwa Al-istikhdam katika fani ya balagha, alitoa mfano wa Aya hio:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" kisha akasema: (Makusudio ya mwanzo ya neno Al-shahru (mwezi wa siku 29-30: month, katika Aya hii) ni Al-hilalu (Mwezi muandamo)." Mwisho wa kunukuu.

12) Anasema Dr. Wahbat Al-zuhailiy: "Mfano wa sababu ni kauli yake Allah Mtukufu﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge" (basi) kuuona mwezi muandamo ndio sababu ya uwajibu wa kufunga." Je hao wote si wanavyuoni wa kweli? Ama kauli yenu: "Wala hakuna khitilafu katika tafsiri za Wanavyuoni hao juu ya Aya hiyo. Khitilafu iliyopo ni moja tu: Je mwezi ukiandama sehemu moja duniani italazimu kufunga sehemu nyengine zilizobaki au kila sehemu na muandamo wake". Jawabu ni kuwa khilafu ipo, lakini nyinyi munapenda kudai "Wamekubaliana" au "Maulamaa wote wamesema" n.k. Hili ndio tatizo lenu, na si nyinyi tu bali hata wale wenzenu walioko Saudia huo ndio mtindo wao. Hebu rejeeni hizo tafsiri mulizozitoa, kama ya Abu Suud, Abu Hayyan na wengine, mutazame je hamutooana waliosema kuwa maana ya Aya hio tunayoizungumzia hapa ni﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ "Ataye ushudia kati yune mwezi muandamo (crecent) wa mwezi (wa ramadhani" . Sasa kuushudia mwezi muandamo n i vipi?

MNASEMA

Mantiki hiyo ndiyo aliyotumia Shaykh Naaswir Bachuu kila anapotaja tafsiri ya Aya za Qur-aan tukufu huwa anaonesha pahala alipoitoa tafsiri hiyo. Kwa hivyo hakwenda kinyume na kanuni za kielimu na misingi sahihi ya Dini yetu. Alichosisitiza Shaykh Naaswir Bachuu katika Hadiyth isemayo:

(Fungeni kwa kuuona mwezi - muandamo) Ni kuwa Hadiyth hii ni 'aam - yaani ya ujumla, kwa hivyo popote mwezi utakapoonekana na habari hizo zikathibitishwa usahihi wake, basi watu wote wafunge. K adhalika wafungue kama ni mwezi wa kufungua. Pia Shaykh Naaswir ameonesha msimamo wa Wanazuoni juu ya masimulizi ya Kuraib kwamba hayawezi kuwa "hoja sahihi" katika mas-ala haya.

JAWABU

Ama Sheikh Nassor kenda kinyume na kanuni za elimu katika sehemu nyingi za kitabu chake. Kwanza katoa tafsiri na kupinga tafsiri bila kuonesha kwa mujibu wa kanuni za lugha, usuli na nyengine, usahihi wa tafsiri alioichagua: hakuonesha kifani kwanini kakipinga alichokipinga na kukisapoti alichokisapoti. Kwa hivyo, hakuwa na dalili za kielimu isipokuwa fulani kasema; wakati fulani kasema ni hoja ambayo kila kundi inalo. Kinachotakiwa ni kuonesha kuwa hoja hizi ndio sahihi kwa sababu kadha. Ama Hadithi(Fungeni kwa kuuona mwezi - muandamo), tumeshaielezea sana hatuna haja ya kuikariri mara kwa mara. Pia Hadithi ya Kuraib tumeshaielezea na kutoa majibu juu ya tafsiri sahihi ya Hadithi hio, hatuna haja ya kuikariri mara kwa mara.

MNASEMA

Ndugu Juma yeye amezitaja baadhi ya tafsiri za Quran na baadhi ya vitabu vilivyotaja Aya inayoelezewa:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ Akidhania kuwa tafsiri hizo zimeitafsiri Aya hiyo kuwa:"Atakayeushuhudia mwezi afunge." Ukichunguza vyema utaona kuwa ndugu Juma hakuelewa kinachokusudiwa katika tafsiri hizo. Kwanza utaona kuwa kila anapojaribu kulito lea tafsiri neno﴿ شَهِدَ﴾ 'shahida' huliwacha kama lilivyo kwa kusema 'atakayeushuhudia'. Ni kama kusema:"Atakayeushuhudia" maana yake"atakayeushuhudia."

JAWABU

Maana ya kuliwacha neno hilo kama lilivyo, ni kwa sababu wako waliofasiri Shahida kwa maana ya kuwepo; na wako waliofasiri Shahida kwa maana ya kuona. Kwa hivyo, baadhi ya mwahala - kutegemea nakusudia nini - ndio huliwacha kama lilivyo. Lakini kila aliyesoma kitabu changu kaelewa vyema nini nilichokieleza.

MNASEMA

Hebu na tuangalie Wanavyuoni walivyolifasiri neno shahida: Mwanachuoni Dr. Zuhaily ameeleza yafuatayo: "Kuuhudhuria mwezi wa Ramadhaan ni sababu ya kuwajibika kufunga (Swaum) kama ilivyoelezwa katika Qur-aan Tukufu:" Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhaan) afunge" .

Dr Zuhaily aliendelea kutoa dalili ya kuonesha wajibu wa kufunga kwa kuonekana mwezi - muandamo kwa kuyanukuu maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pale aliposema:(Fungeni kwa kuonekana mwezi - muandamo) Na jambo la kuonekana mwez i japo na mtu mmoja katika Hadiyth hiyo ni la wote ('aam). Wala hakuna Mwanachuoni yeyote aliyesema kuwa Hadiyth hii inaashiria kila pahala pafuate muandamo wake. Kutegemea maneno matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kuk ubalika kifani, huo utakuwa udhaifu.

JAWABU

kwanza : munatabia ya kutotoa marejeo. Ilikuwa ni jambo la busara munapotaja kauli ya mtu muoneshe kutoka wapi.

Pili : ikiwa Dr. Al-Zuhaili, katika sehemu moja kasema hivyo, sehemu nyengine kasema:"Atayeushudia mwezi na aufunge" . Kuuona mwezi muandamo ndio sababu ya wajibu wa kufunga. Kwa hivyo, Dr. Al-Zuhaili pia kaifasiri Aya hio kwa maana ya kuuona kwa macho. Cha kufahamu ni kuwa mwanachuoni anapotoa maelezo kisha akataja Aya au kinyume chake anapotaja Aya kisha akatoa maelezo, basi huwa maelezo hayo ndio anaifasiri Aya hio.

Ama kauli yenu: "Wala hakuna Mwanachuoni yeyote aliyesema kuwa Hadiyth hii inaashiria kila pahala pafuate muandamo wake. Kutegemea maneno matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa udhaifu". Ninasema: munarejea kosa lile lile alililolifanya Sheikh Nassor la kudai hivyo, nami nimekunukulieni ushahidi k uwa wako wanavyuoni waliosema kwamba Hadithi hio "Fungeni kwa kuuona.." ni mahususi kwa watu maalumu nao ni wale waliouona. Anasema Ibn Hajar: (Na w ale ambao hawakuchukua kauli hio, wanasema kwa sababu kauli yake Mtume(s.a.w.w) aliposema:"Mpaka muuone" ni agizo kwa watu maalumu." Anasema Al-san'ani: "Na ikasemwa kwamba (Muandamo wa mbali) hauzingatiwi (mbali), kwa sababu kauli yake Mtume (s.a.w.w) aliposema:"Mukiuona" ni agizo kwa watu maalumu." Maelezo haya nyinyi mumeyafumbia macho kwani hamukuyapenda.

Ama kauli yenu: "Kutegemea maneno matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa udhaifu" inanifanya nisijue mukitakacho. Ninanapokupeni ushahidi wa kifani juu ya tafsiri fulani, munasema Juma Mazrui anafasiri kwa rai yake wala hategemai mael ezo ya wanavyuoni; mukipewa maneno ya wanavyuoni munasema "Kutegemea maneno matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa udhaifu". Sasa munataka vipi, hebu twambieni mutakavyo!

MNASEMA

Shaykh Al-Amin 'Aliy Mazrui: katika kuifasiri Aya isemayo:﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ameeleza yafuatayo: "Basi mwenye kuwemo katika mwezi huu na afunge." Kisha akaendelea kusema: "Muradi wa 'mwenye kuwamo katika mwezi huu' ni ambaye hakuwa sa farini." (uk. 65)[9][9] Mwanachuoni Shaykh Al-Jassas katika kitabu chake Ahkamul-Qur-aan ameweka mlango unaitwa Kayfiyati Shuhudi Shahri "mlango unaolelezea namna ya kuhudhuria mwezi" Shaykh Al-Jassas akaanza kunukuu aya mbili, ya kwanza "Famman Shahida minkum na aya ya pili "Yas-alunaka 'anil-ahilah" Ifuatayo ni tafsiri sahihi ya aya hizo kama ilivyo katika vitabu vya tafsiri, tafsiri ya aya ya mwanzo:"Atakayekuwa katika Mji katika mwezi huu mwezi (wa Ramadhaan afunge" . Tafsiri ya aya ya pili:"wanakuuliza miezi miandamo sema hiyo ni (vielelezo vya) nyakati kwa ajili (ya mambo) ya watu na hija zao" .

JAWABU

Maneno ya Sheikh Al-Amin hayana upinzani. Na - kwa ujumla - maneno hayo na yalio mfano hayo yalikuwa hayana maana kwani mimi katika kitabu changu sijapinga kwamba kuna wanavyuoni walioifasiri Aya hio kwa maana ya kuwa katika mji. Bali nilisema: Wanavyuoni wengi wameifasiri Aya hii, kuwa maana yake ni "Atayeuhudhuria mwezi (Month) basi na-aufunge." Kisha wakabainisha kwamba maana ya atayeuhudhuria mwezi, ni atayekuwa katika makazi yake, yaani si msafiri.

Kwa hivyo, mimi nanachokipinga ni dai lenu kwamba hakuna mwanachuoni aliyefasiri shahida kwa maana ya kuona: wala sijapinga ukweli kwamba kuna wengi waliosema kwamba neno shahida katika Aya ni kwa maana ya kuwepo katika mji. Bali nilisema kwamba tafsi hii ndio yenye nguvu. Nilisema hivi: Tafsiri hii inapata nguvu kwa kutazama kukabiliana kimaana (Muqabala) - kuliopo katika sehemu ya kwanza ya Aya hii na sehemu yake ya pili. Aya hii inasema: "Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu, basi na-aufunge." Neno "Kushuhudia" linatumika kwa maana ya kuhudhuria, na hutumika kwa maana hio na ziada nayo ni maana ya "Kuona" kwani kila muonaji huwa kahudhuria. Sasa "Kuushuhudia" mwezi inawezekana ikawa maana yake ni kuuona kwa macho na inaweza ikawa maana yake ni kuhudhuria kwa maana ya kuwepo katika mji. Sasa ilipokuja sehemu ya pili ya Aya, ikasema:

﴿مَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ

"Na atayekuwa mgonjwa au kuwa safarini, basi (afunge) idadi (ya siku asizozifunga" katika siku nyengine. " Hapa ikawa tumefahamu kwamba makusudio ya Aya inayosema:"Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu, basi na-aufunge" ni "Atayekuwa katika mji: yaani si msafiri." Na kwa tafsiri hii, Muqabala (opposite au kinyume) utakuwa umepatikana, na maana ya Aya itakuwa hivi: "Huyu ni wajibu kufunga kwa kuwa ni mzima na kwa kutokuwa safarini; na (kinyume chake) yule karuhusiwa kula kwa kuwa ni mgonjwa au kwa kuwemo safarini." Msingi huu wa Muqabala, dhahir ndio msingi wa wale walioifasiri Aya hio kuwa maana yake ni: Atayekuwa katika mji: yaani si msafiri" nao ni msingi madhubuti. Hatimae nikakuta katika tafsiri ya Ibn Jariri Al-ttabari akieleza hivyo hivyo Walillahi Al-hamdu.

Sasa munachokipinga ni nini? Inaonesha hamujui mukisemacho. Ama kuhusu Al-Imamu Al-Jassas Al-Razi, nilisema hivi: Al-jassas Al-raziy, kaweka mlango aliouita: Babu kayfiyyati shuhudi al-shahri. Hapa Al-imamu Al-jassas, anazungumzia kuandama kwa mwezi ni vipi: nini dhana au mafhum (concept) ya kuandama kwa mwezi Kisheri a? Akaanza kwa kunukuu Aya mbili:

Moja : ni Aya inayosema:

﴿ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ

Atayeushuhudia mwezi miongoni mwenu na-aufunge).

Pili : ni Aya inayosema:﴿يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo, sema hivyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na hija" .

Kisha akanukuu Hadithi ya Ibn Umar (r.a.), kisha akatoa maelezo mpaka akasema:(Likaonesha hilo kwamba kuuona mwezi muandamo ndio kuushuhudia mwezi (wa siku 29 au 30 yaani month).

Ni wazi kwamba Al-jassas kaifasiri Aya hii kwa maana ya kuona kwa macho.

Nyinyi maneno:(Likaonesha hilo kwamba kuuona mwezi muandamo ndio kuushuhudia mwezi (wa siku 29 au 30 yaani month) , mumeyafumbia macho kama kawaida yenu, na badala yake mukasema: Mwanachuoni Shaykh Al-Jassas katika kitabu chake Ahkamul-Qur-aan ameweka mlango unaitwa Kayfiyati Shuhudi Shahri "mlango unaolelezea namna ya kuhudhuria mwezi" Shaykh Al-Jassas akaanza kunukuu aya mbili, ya kwanza "Famman Shahida minkum na aya ya pili "Yas-alunaka 'anil-ahilah" Ifuatayo ni tafsiri sahihi ya aya hizo kama ilivyo katika vitabu vya taf siri, tafsiri ya aya ya mwanzo:"Atakayekuwa katika Mji katika mwezi huu mwezi (wa Ramadhaan afunge" . Tafsiri ya aya ya pili:"wanakuuliza miezi miandamo sema hiyo ni (vielelezo vya) nyakati kwa ajili (ya mambo) ya watu na hija zao" . Mwisho wa kunukuu.

Bali kabla ya hapo Al-Jassas kasema kuhusu Aya hio kwamba ina maana tatu; moja yao alisema: "Na ikamaanisha kwamba atayeuona mwezi peke yake basi naafunge". Ni wazi kwamba Imamu huyu anakubali kwamba neno hilo au Aya hio pia inabeba maana ya kuona. Na akasema tena: "Na Waislamu wamekubaliana kwamba Aya hii na Hadithi hio kwamba maana yake ni kuuzingatia uoni wa mwezi muandamo". Yote haya nyinyi mumeyafumbia macho, kwani lengo lenu ni kunusuru rai. Kwa ujumla nilichokipinga si kwamba Aya hio ina maana ya kuwepo katika mji: hili sikulipinga bali nililitilia nguvu. Nilichokipinga ni dai kwamba; HAKUNA WANAVYUONI WALIOFASIRI AYA HIO KWA MAANA YA KUONEKANA MWEZI. Hili nililipinga na nikatoa ushahidi wa wanavyuoni wengi kama ilivyotangulia.

MNASEMA

Ufuatao ni ufafanuzi wa aya hizo. Tunaanza na aya ya mwanzo wanazuoni wengi sana wameitafsiri aya hiyo kwa maana iliyo hapo juu. Ingawa ukilichukua neno mojamoja katika aya hiyo na ukaliangalia katika makamusi ya Kiarabu utalikuta lina maana zaidi ya moja, utaratibu huu sio mgeni katika lugha ya Kiarabu, kanuni ya lugha inasema: "Neno halina maana (moja) mpaka liwemo ndani ya sentensi", kwa hivyo neno "Shahida" liliyomo ndani ya aya hiyo lina maana ya "Kuwepo" (sio maana ya kuona). Na neno "Shahri" lina maana ya mwezi siku, sio maana ya mwezi sayari hiyo ndiyo tafsiri sahihi ama kuitafsiri kwa maana ya "atakayeuona mwezi na afunge" hiyo ni tafsiri ya kuilazimisha.

JAWABU

Natukubaliane kuwa hio ndio tafsiri sahihi, japo kuwa hamukuonesha ushahidi wa elimu, tatizo ni kuwa tafsiri hio itawapa nguvu wale wenye kudai kwamba kila watu na muandamo wao. Kwani ikiwa tafsiri ya neno "Shahida" liliyomo ndani ya aya hiyo lina maana ya "Kuwepo" na tafsiri neno "Shahri" lina maana ya mwezi siku" maana itakuwa "Atayekuwepo katika mwezi siku naafunge" hii mufhumu mukhalafa yake - na kwa hapa ina nguvu kwani ni mafhumu Al-Shart - itakuwa yule ambaye hayupo katika mwezi siku basi asifunge - anayeamrishwa ni aliyepo. Na kusema hivi haiwezekani ila iwe kuna sehemu mwezi siku tayari umethibiti; na kuna sehemu bado haujathibiti. Na hili litawapa nguvu wapinzani wenu. Sijui munafahamu au munanukuu tu?!!!

MNASEMA

Ama uchambuzi wa aya ya pili kama ulivyo katika vitabu vingi vya tafsiri, kwanza wameeleza sababu ya kuteremshwa aya hiyo ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameulizwa na kama aya yenyewe inavyothibitisha tokeo hilo Na vilevile Wanazuoni hao wakaeleza kuwa kilichoulizwa hapo ni hali halisi ya mabadiliko ya miezi. Kwa maelezo zaidi rudi katika tafsiri, itakutosha tafsiri ya Dr. Zuhaily. Kwa mantiki hiyo hapa hapazungumziwi kuwepo miandamo mingi wala kuwepo muandamo wa kisheria, wala Aya hii maana ya kuwa kila nchi ifunge na ifunguwe kwa mujibu wa matlai yao , vile vile Aya hii haina maana ya kuwa ni "Khaas" katika zile Hadiyth zilizotaja kwa ujumla kuhusu suala la kufunga na kufungua.

JAWABU

Sasa munaanza kuchanganya mambo. Aya ambayo imesemwa kushuka kwa sababu hio ni Aya "Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo": si Aya:"Atayeushudia mwezi" . Na maudhui yetu hapa ni kuhusu Aya"Atayeushudia mwezi" . Mara mumerukia kwengine. Kwa ufupi, ni kuwa tumeshajibu kwamba wanavyuoni hao wametegemea Hadith maudhui (Hadithi ya kutunga) kwa ushahidi tuliotoa wa sanad na kwa ushuhuda wa wanavyuoni wengine. Nakukumbusheni kaul i yenu muliposema: "Kutegemea maneno, matupu ya mwanachuoni kama ni Khaas bila ya kuonyesha dalili zenye kukubalika kifani, huo utakuwa ni udhaifu". Sasa nyinyi mulitumia fani gani hata mukaitegemea sababu hio ya kutremka Aya ambayo sanad ya riwaya y ake ina wapokezi waongo.

MNASEMA

Alichokisisitiza Shaykh Al-Jassas katika kitabu chake ni ule wajibu wa kufunga na kufungua kwa kuzingatia "Suala zima la kuonekana mwezi" Na ndio maana Shaykh Al-Jassas akanukuu Hadiyth zenye kutaja wajibu wa kufunga na kufungua kwa kuonekana mwezi. Na Hadiyth zote hizo zimetaja jambo hilo kwa njia ya Ujumla, yaani hukumu yake inawaenea Waumini wote popote walipo. Katika kuielezea kauli hii ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Shaykh Al-Jassas anasema: "ni jambo linaloeleweka kuwa kauli ya Mtume(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo:(Fungeni kwa kuonekana mwezi na Fungueni kwa kuonekana mwezi) ni ya ujumla haiwahusishi watu wa nchi moja peke yao pasi na wengine.

Na vilevile msimamo kama huu wa kufunga pamoja ameuweleza Dr. Zuhaily katika kitabu chake Al-Fiqhul- Islamiy.

JAWABU

Hatupingi kwamba kuna wanavyuoni waliosema hivyo, wala mimi katika kitabu chamgu sikupinga hilo; tunachodai ni kuwa hoja zao ni dhaifu ukilinganisha na hoja za kundi lapili. Na Hadithi hio tumeshaielezea, tusikariri yayo kwa yayo mara elfu.


11

12

13

14

15

16