1
HADITHI YA SHUKA
QURAN TUKUFU
Quran tukufu ndio chemchemi ya misingi na mafunzo ya kiislamu na uthibitisho wa kuwa kwake Kitabu cha Allah (ambacho ni muujiza) na pia ni uthibitisho wa utume wa Mtume Mtukufu wa uislamu. Quran tukufu ni neno la Allah, lililofunuliwa kwa Mtukufu Mtume(s.awa.) na kwa kupitia kwake liliwafikia wanadamu. Quran tukufu inawapa wanadamu ujuzi wa kielimu na kivitendo, ambao kwa kuutumia ipasavyo, binadamu anaweza kufanikiwa kuchuma mema, amani na mafanikio humu duniani na huko akhera. Lengo hasa la Quran tukufu ni kuwaongoza wanadamu ili kupata maendeleo na mafanikio. Inawapa wanadamu elimu kwa njia nzuri, nyepesi na ya dhahiri, kuhusiana na itikadi zilizo sahihi, tabia njema na matendo mema ambayo ni muhimu sana katika maisha ya kila mmoja, na vile vile katika maisha ya jamii.
Allah (S.B.) amesema katika Quran tukufu. "Na tumekuteremshia Kitabu hiki kielezacho kila kitu na ambacho ni uongofu na rehma na khabari za furaha kwa wanaojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu) waislamu
" (AN NAHL: 89)
AHLUL BAIT
"Ahlul bait" kilugha kama ilivyo katika kamusi ya kiarabu ni jamii yote ya nyumba" k.m. mke, mwana, binti na watumwa. Yaani wote wanao mtegemea mwenye nyumba. Wengine wamepanua zaidi maana yake ili kuwaingiza pia, jamaa wa karibu k.m. mama, baba, dada, kaka na watoto wake ami na shangazi (dada ya mama) pamoja na watoto wao. Lakini kulingana na Quran tukufu na hadithi za Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
, hizi tafsiri mbili hazitumiki kwa "Ahlul bait" wa Mtume(s.a.w.w)
. Kulingana na hadithi za Mtume(s.a.w.w)
, ambazo zimenakiliwa na wapokezi wengi, "Ahlul bait" ni neno tukufu linalomaanisha watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume, ambao ni Imam Ali(a.s)
Bibi Fatima(a.s)
, Imam Hasan(a.s)
, na Imam Husein(a.s)
. Hawa ndio wale watu watano watukufu - (Ahlul kisaa, yaani watu wa shuka) - ambao, hakuna shaka kuwa ndio "Ahlul bait".
Kwa hivyo, Jamii nyingineyo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.a) haiingii katika maana, ya 'Ahlul bait'. Hata Bibi Khadija(a.s)
mke wa Mtume Mtukufu(s.a.w.w)
. aliye heshimika sana, na aliye kuwa mama yake Fatima(a.s)
, binti mpendwa wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
. Vile vile, Ibrahim mwanawe Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
, pamoja na cheo chake kitukufu, haingii katika 'Ahlul bait'. Bila shaka kulingana na ukweli wa hadithi nyingi ambazo zimekuwa zikinakiliwa na wapokezi wa hadithi mara kwa mara watu watano watukufu - (Yaani watu wa shuka) - na Maimamu tisa watukufu, ambao wanatokana na kizazi cha Imam Husein(a.s)
wanaingia katika 'Ahlul bait'. Na kwa Ibara nyingine ni kuwa "Ahlul bait" ni kumi na wanne, katika idadi, na ndio wanaoitwa "Maasumin kumi na wanne".
Kulingana na aya ya utakaso (Suratul Ahzab 33;33) 'Ahlul bait' wana cheo kitukufu cha ucha Mungu na umaasumu (utakasifu), kwani hawakuwahi Katika hadithi ifwatayo, Mtukufu Mtume ameonyesha utukufu wa 'Ahlul bait juu ua maswahaba wake wote; na kwa maneno na vitendo vyake alifafanua maana ya aya ya utakaso. Alisema ya kwamba "Mimi na Ahlul bait wangu tumetakaswa kutokakana na madhambi." Aliwatangazia watu haya akiwa msikitini. Kila alipokuwa akienda msikitini kwa sala ya alfajiri alikuwa akipita nyumbani kwa Imam Ali(a.s)
na Bibi Fatima(a.s)
na kusema; "Amani ya Allah, rehma na baraka zake ziwashukieni, enyi 'Ahlul bait'. (Wakati wa) swala (umewadia), Allah awarehemuni"
. Kisha alikuwa akifuatilizia kwa aya ya Quran,"Mwenyezi Mungu Anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa."
Kisha aliongeza,"Mimi ni mwenye kumpiga vita kila anayekupigeni vita (na) mimi ni mwenye kumpa amani kila anayekupeni amani"
(Majmauz Zawaid, Juzu yaq, na Tafsirus Suyuti, Juzu ya 5). Katika Sahihu Tirmidhi, Musnadu Ahmad, Musnadu Tialasi, Mustadrakus Sahihain, Asadul Ghaba na katika tafsiri za Tabari, Ibn kathir na Suyuti, Anas bin Malik Khazraji (aliyedai kuwa alibaki katika uswahaba wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
kwa muda wa miaka kumi. Alifariki huko basra akiwa na umri wa miaka tisiini) amenakiliwa akisema ya kwamba, Mtume Mtukufu(s.a.w.w)
alikuwa akipita karibu na mlango wa Fatima Zahra(a.s)
kwa muda wa miezi sita akisema. "Enyi watu wa nyumba! Wakati wa swala umewadia!!" kisha aliongeza kusema, "Enyi watu wa nyumba!
".
Hawa ndio "Ahlul bait" ambao Imam Shafii, mmoja kati ya maimamu wanne wa dhehebu la kisunni katika kuwasifu amesema. " Enyi 'Ahlul bait' wa Mtukufu Mtume (s.a.w.a), kuwapenda ni faradhi iliyofaradhishwa na Mwenyezi Mungu katika Quran tukufu. Kwa hakika yatosha kuwa fakhari kubwa kwenu kwamba asiye waswalia nyinyi (katika swala yake), basi swala yake hubatilika!!" (Almuhaddithul Qummi, Alkuna wal Alqab, Shablanji, Nurul Absar, ukurasa wa 104). Vile vile Zamakhshari na Razi, katika tafsiri zao za Quran tukufu wameinakili hadithi ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w) ifwatayo; Amesema(s.a.w.w)
: "Anayekufa akiwapenda Aali (kizazi) zake Muhammad hufa shahidi. Tambueni kuwa, anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad hufa akiwa amesha samehewa (madhambi yake). Tambueni kuwa, anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad hufa (kifo cha) aliyetubia. Tambueni kuwa anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad, hufa akiwa muumini, aliyekamilika imani (yake) Tambueni kuwa anayekufa akiwachukia Aali zake Muhammad, hufa akiwa kafiri. Tambueni kuwa anayekufa akiwachukia Aali zake Muhammad hatoipata harufu ya pepo"
(Zamakhshari, Tafsirul Kash-shaf juzu ya 4, tafsiri ya sura Ash-shura, 42; 32, na Fakhrud Din Arrazi, Tafsirul Kabir, Juzu ya 26, Ukurasa wa 165 - 166).
Tutamalizia kwa misitari ya shairi moja la mwanashairi maarufu wa kiirani aitwaye Sa'adi."Ewe Sa'adi! Ikiwa watamani kupata furaha ya mapenzi na ukamilifu wa maisha usiokuwa na kikomo, basi yakutosha kumpenda Muhammad na Aali zake Muhammad". Hakuna malipo bora na furaha zaidi ya humu duniani kuliko kuwapenda kidhati "Ahlul bait" na kuwafwata kwa vitendo.
2
HADITHI YA SHUKA
ASILI YA HADITHI KISAA (HADITHI YA SHUKA)
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Jabir bin Abdullah Al-ansari anahadithia kutoka kwa Bibi Fatimatuz Zahra(a.s)
ya kwamba, "Nilimsikia Fatima(a.s)
akisema ya kwamba";Siku moja baba yangu (mpendwa) Mtume wa Allah, alinizuru nyumbani kwangu na kusema; "Amani ya Allah iwe juu yako, ewe Fatima" Nami nikamjibu "Nawe pia amani ya Allah iwe juu yako". Kisha akasema;
"(Mwanangu) ninahisi mwili wangu ni dhaifu" Nikamwambia; "Allah Akulinde kutokana na udhaifu, ewe baba". Akasema, "Ewe Fatima, niletee ile shuka itokayo Yemen, na unifinikie, kwayo". Basi nikamletea ile shuka ya Yemen na kumfunika kwayo
".
Nilipokuwa nikimwangalia niliona kuwa uso wake unameremeta, kama mwezi katika usika wa (mwezi) kumi na tano Baada ya muda mfupi mwanangu Hasan(a.s)
aliingia na kunisalimu :"Amani ya Allah iwe juu yako, ewe mama (mpendwa)" nami nikamjibu, "Amani ya Allah, pia, iwe juu yako ewe kiburudisho cha macho yangu! na tunda la moyo wangu!" Akasema, "Ewe mama, hakika mimi ninapata harufu nzuri sana kutoka kwako, kana kwamba ni harufu ya baba yangu, Mtume wa Allah (Amani ya Mwenyezi iwe juu yake)". Nikamwambia, "Na'am, hakika babu yako yuko chini ya ile shuka
".
Basi Hasan(a.s)
aliikaribia ile shuka, na kusema, "Amani ya Allah, iwe juu yako, ewe babu! ewe Mtume wa Allah. Je unaniruhusu kuingia chini ya shuka niwe pamoja nawe?" Naye akamjibu, "Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe mwanangu!, ewe mwenye kuimiliki hodhi yangu (ya kauthar siku ya Qiyama) nimekuruhusu". Basi akaingia chini ya shuka pamoja naye. Baada ya muda mfupi kupita, naye mwanangu, Husein(a.s)
akaingia na kunitolea salamu. "Amani ya Allah iwe juu yako, ewe mama (mpendwa)"
Nami nikamjibu , "Amani ya Allah pia, iwe juu yako, ewe mwanangu! Ewe kiburudisho cha macho yangu! Na tunda la moyo wangu!". Akaniambia, "Ewe mama! Hakika mimi ninapata harufu nzuri sana kutoka kwako, kana kwamba ni harufu ya babu yangu, Mtume wa Allah". Nikamjibu, "Naam, babu yako na ndugu yako wako chini ya ile shuka". Basi, Husein akaikaribia ile shuka na kusema; "Amani ya Allah, iwe juu yako ewe uliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu (kuwa Mtume wake). Je unaniruhusu kuingia chini ya shuka, niwe pamoja nanyi".
Akasema, "Amani ya Allah, pia iwe juu yako ewe mwanangu! Ewe muombezi wa umma wangu (mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Qiyama). Nimekuruhusu". Basi akainga chini ya shuka, (akawa) pamoja nao. Wakati huo huo, Abul-Hassan Ali bin Abi Talib(a.s)
akaingia na kutoa salamu, "Amani ya Allah iwe juu yako ewe binti ya Mtume wa Allah!".
Nami nikamjibu, "Amani ya Allah, pia, iwe juu yako, ewe babake Hasan! Ewe Kiongozi wa waumini!" Akasema"Ewe Fatima, hakika ninaipata harufu nzuri sana kutoka kwako kana kwamba ni harufu ya ndugu yangu na binami yangu, Mtume wa Allah Nikamwanibia "Na'am, yuko pamoja na wanao chini ya ile shuka"
. Basi, Ali akaikurubia ile shuka na kutoa salamu, "Amani ya Allah iwe juu yako, ewe Mtume wa Allah, je unaniruhusu niwe pamoja nanyi chini ya shuka?"
Akamjibu,"Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe ndugu na wasii wangu na khalifa wangu, na mbebaji wa bendera yangu, nimekuruhusu". Basi Ali akaingia chini ya shuka, kisha mimi nami nikaikurubia ile shuka na kusema, "Amani ya Allah iwe juu yako ewe baba (mpendwa), ewe Mtume wa Allah, Je unaniruhusu niwe pamoja nanyi chini ya shuka?". Akajibu, "Amani ya Allah, pia iwe juu yako, ewe binti yangu, na ewe kipande cha mwili wangu, nimekuruhusu"
. Basi nikaingi chini ya shuka.
Tulipokuwa tumekusanyika sote chini ya shuka, babangu mpendwa, alizishika ncha mbili za ile shuka na kuuinua mkono wake wa kulia, akiulekeza binguni na kusema; "Ewe Allah! Hawa ndio Ahlul bait wangu, wasiri wangu na wasaidizi wangu. Mwili wao ni mwili wangu, damu yao ni damu yangu. Huniumiza kinachow- aumiza na hunihuzunisha kinacho wahuzunisha. Ninampiga vita kila ananyewapiga vita, na ninampa amani kila anayewatunuku amani. Mimi ni adui kwa mwenye kuwafanyia uadui, na humpenda yule awapendaye. Hakika wao wametokana nami, nami nimetok- ana nao. Basi niteremshie amani yako, baraka zako, rehma zako, msamaha wako, na radhi yako, mimi pamoja na wao. Na uwaondolee uchafu na kuwataka sa kabisa kabisa".
Basi, Mwenyezi Mungu, Mshindi na Mtukufu Akasema "Enyi malaika wangu! Enyi wakazi wa mbingu zangu! Hakika mimi sikuiumba mbingu madhubuti wala ardhi iliyotandaa, wala mwezi wenye nuru, wala jua lenye kuangaza, wala sayari yenye kuzunguka, wala bahari yenye mwendo wa mawimbi, wala dau lenye kuelea majini, ila tu kwa kuwapenda hawa watano, walioko chini ya shuka".
Hapa, malaika mkuu, Jibrail akasema, "Ewe Mola wangu! Na ni nani walioko chini ya shuka?" Allah, Mshindi na Mtukufu akamwambia, "Hao ni watu wa nyumba ya utume, na asili ya ujumbe. Wao ni Fatima na babake na mumewe na wanawe". Jibrail(a.s)
akasema, "Ewe Mola wangu! Je unaniruhusu kuteremka ardhini ili niwe wa sita pamoja nao?". Allah Akamjibu na kusema, "Na'am nimekuruhusu".
Jibrail(a.s)
akateremka ardhini na kusema, "Amani ya Allah, iwe juu yako, ewe Mtume wa Allah. Mkuu wa wakuu Anakutolea salamu, na kukustahi na kukutukuza, na Anakujulisha ya kwamba "Naapa kwa Ushindi na Utukufu wanga ya kwamba sikuiu- mba bingu madhubuti, wala ardhi iliyotandaa wala, mwezi wenye nuru, wala jua lenye kuzunguka, wala bahari yenye mawimbi wala dau lenye kuelea majini, ila tu kwa ajili yenyu na mapenzi yenyu".
Na ameniruhusu kuingia pamoja nanyi. Basi, ewe Mtume wa Allah, unaniruhusu kuingia?" Mtume wa Allah(s.a.w.w)
akasema, "Amani ya Allah, pia, iwe pamoja nawe, ewe mwaminifu juu ya wahyi (ujumbe) wa Allah, na'am nimekuruhusu." Basi Jibrail(a.s)
naye akaingia nasi chini ya shuka na kumwambia babangu, (mpendwa). "Hakika Allah amewateremshia wahyi, na kusema, "Hakika Mwenyezi Mungu Anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya utume) na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa".
Ali(a.s)
akamwambia babangu (mpendwa)"Ewe Mtume wa Allah! Hebu nijulishe, kikao chetu hiki chini ya shuka kina fadhila gani mbele ya Allah." Mtume
(s.a.w.w)
akamwambia, "Naapa kwa Yule Aliyeniteua kuwa Mtume, na kunipa ujumbe wenye kuokoa, ya kwamba, itaka- pokumbukwa habari yetu hii, katika hafla yoyote ya watu wa ardhini na ikawa ikati yao kuna shia wetu na wapenzi wetu, basi Allah atawateremshia rehma yake na malaika watawahudhuria na kuwaombea msamaha hadi watakapotawanyika"
. Ali(a.s)
akasema, "Basi wallahi tumefuzu na (pia) shia wetu wamefuzu".
Kisha babangu, Mtume wa Allah (s.a.w.w) akasema,"Ewe Ali! Naapa kwa Yule Aliyeniteua kwa haki kuwa Mtume, na kunipa ujumbe wenye kuokoa, ya kwamba itakapotajwa habari yetu hii katika hafla yoyote ya watu wa ardhini na ikawa kati yao kuna shia wetu na wapenzi, na ikawa kati yao kuna mwenye huzuni, basi bila shaka Allah atamuondolea huzuni yake, na mwenye ghamu, Allah atamuondolea ghamu yake, na mwenye haja, Allah Atamtek- elezea haja yake"
. Ali(a.s)
akasema,"Basi, wallahi tumefuzu na tumebarikiwa na kadhalika shia wetu wamefuzu na kubarikiwa, humu duniani na huko akhera, naapa kwa Bwana wa Kaaba".
Ewe Allah mrehemu Muhammad na Aali zake Muhammad.
DUA
Kwa Jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Ewe Allah! Mrehemu Muhammad na Aali zake katika waliotangulia, na mrehemu Muhammad na Aali zake katika watokaokuja, na mrehemu Muhammad na Aali zake katika wakazi wa mbinguni, mrehemu Muhammad na Aali zake katika Mitume na Wajumbe wako. Ewe Allah! Mpe Muhammad(s.a.w.w)
wasila, na utukufu na fadhila na cheo kikubwa (mbele yako). Ewe Allah! Hakika mimi nilimwamini Muhammad(s.a.w.w)
bila ya kumwona,basi usiniharamishie kumuona siku ya Qiyama, na uniruzuku kuwa pamoja naye, na unifishe katika dini yake, na uninyweshe katika hodhi yake (ya kauthar) kinywaji ambacho kitanifanya nisione kiu tena kamwe. Hakika Wewe ni Muweza wa kila kitu. Ewe Allah! Nijaalie kuzifuata sunna zake na unifufue katika kikundi chake, na unijaalie kuwa miongoni mwa wamfuatao, wala usinizuie kumwona (siku ya Qiyama) na usiniharamishie usuhuba wake, kisha unijaalia kuwa jirani wake (huko peponi) kwa rehma zako, ewe Mbora wa kurehemu.
MWISHO