1
VAZI LA MWANAMKE
BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE
Bibi Fatimah
ni mwanamke anayezingatiwa kuwa ni mwanamke wa kutolea mfano katika dini ya ki-Islamu, na pia ni kiigizo chema kwa kila mwanamke anayetafuta mafanikio katika maisha yake. Bibi Fatimah binti Muhammad
ndiye mwanamke bora ulimwenguni aliyezaliwa na kupata malezi katika nyumba iliyokuwa ikishuka ndani yake Wahyi kutoka mbingu-ni.
9 Hadithi hii imenukuliwa kutoka ndani ya kitabu kiitwacho Tuhaful- Uquul. Katazo hili linajumuisha mambo mengi na khususan mambo yote ambayo Mwenyezi Mungu hayaridhii na yanatendwa na maadui wa Mwenyezi Mungu. Mwislamu inamuwajibikia kujiepusha nayo vinginevyo hapatakuwa na tofauti kati ya Muumini na adui wa Mwenyezi Mungu. Mtarjumi.
Si hivyo tu bali Bibi Fatimah alihitimu mafunzo ya Uislamu katika madrasa ya Utume, na kutokana na mafunzo hayo aliweza kufikia daraja ya juu na tukufu. Katika kuthibitisha ubora wa Bibi Fatimah, Mtume
amepata kusema,
10 Kwa ajili ya daraja kubwa aliyonayo Bibi Fatimah katika Umma wa Nabii Muhammad
imekuwa ni wajibu kwa kila mwanamke duniani kuiga mwenendo wa Bibi huyu katika maisha yake, ajing'arishe kwa nuru yake nzuri na afuate nyayo zake ambazo zitamuelekeza kwenye mafanikio na utukufu. Hakika Bibi Fatimah
, ni mfano wa kila utukufu na kila jema. Mwanamke yeyote atafanikiwa iwapo ataamua kufuata mwenendo wa Bibi Fatmah (
, na kinyume chake ni kuwa, kila mwanamke ataangamia iwapo ataamua kujichagulia mwenendo wake au kuiga usiyokuwa mwenendo wa Bibi Fatimah. Pia Fatimah
alikuwa Mchaji Mungu na mwenye kutekeleza vilivyo maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Pia ile maana nzima ya Hijabu aliifahamu vema na kuitekeleza kama ilivyoamriwa na Mwenyezi Mungu.
Hivyo utekelezaji wake katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu ulikuwa wa hali ya juu, kwani hakupata kutoka nje ila huwa amevaa vazi la kumsitiri mwili wake wote tangu kichwani hadi miguuni. Isitoshe alikuwa akiichukia mno tabia ya wanawake kutoka majumbani mwao bila kujisitiri kisheria. Bibi Fatimah alichukizwa na tabia hiyo kwa sababu Mwenyezi Mungu pia anaichukia tabia ya kutokujisitiri na hasa kwa kuwa kukosa sitara ya kishera kwa wanawake ni ufunguo wa kuyaendea maovu na ni miongoni mwa vitangulizi vinavyosababisha watu kuteleza, bali wanaaanguka kabisa. 10Mustadrak Alhakim juz 3 uk , Al isabah ya Ibn Hajar Al asqalani juz 4 uk. 10 Sasa hivi tunawaletea baadhi ya mafundisho kuhusu Hijabu na tutaona pia utukufu wa Bibi Fatimah katika mafunzo hayo.
NI KITU GANI KILICHO BORA KWA MWANAMKE?
Inasimuliwa katika historia kwamba, Mtume
siku moja aliwauliza Masahaba suali lifuatalo:
Masahaba walinyamaza kwa kuwa jibu la mkato na sahihi hawakulifahamu, ikawa kama kwamba akili zao zinahangaika baina ya kuwa kilicho bora kwa mwanamke ni mali, uzuri wake, kuolewa au kitu gani? Kipindi chote hiki Bibi Fatimah alikwisha lisikia swali hilo, na baada ya kimya cha kukosekana jibu, Bibi Fatimah alimtuma mtu aende kwa Mtume
aka-toe jibu sahihi la swali hili nalo ilikuwa;
11
Baada ya jibu la bibi Fatimah Masahaba walikuwa wakisubiri jibu la Mtume atasema nini kuhusu jawabu alilotoa Binti yake. Mtume
akasema "Amesema kweli Fatimah." Na akaongeza kusema,
Maana ya maneno ya Mtume yalimaanisha kwamba hilo ndilo jawabu sahihi na hiyo ndiyo imani. Kutokana na jawabu hili, Bwana Mtume
akawa ameitangazia dunia nzima kwamba; Utu, heshima, utukufu, na wema wa mwanamke unapatikana ndani ya Hijabu, na kinyume chake ni uovu na shari, isitoshe hasara hum-fika mwanamke anapoitupa Hijabu. 11Hapana shaka makusudio yaliyomo ndani ya jawabu la bibi Fatimah
ni kwamba, waw-ili hawa yaani mwanamke na mwanaume ni wale wasiokuwa na uhsiano wa kisheria. Watu wenye uhusiano kisheria ni kama hawa wafuatao: Mama, dada, shangazi na au Baba, kaka, mjomba na wengine ambao wametajwa katika vitabu vinavyohusika na sheria. Ama mume na mke, wawili hawa uhusiano kati yao hauna haja ya kutolewa maelezo. Mtarjumi.
MAZUNGUMZO YA KUSTAAJABISHA
Historia inaendelea kutufahamisha kwamba Bibi Fatimah
alikuwa amekaa na baba yake ambaye ndiye Mtume
, mara alibisha hodi Sahaba Abdalla ibn Ummi Maktum ambaye alikuwa kipofu. Kabla Sahaba huyu hajaingia Bibi Fatimah
alisimama akaondoka mahali hapo. Baada ya kwisha mazungumzo baina ya Mtume na Sahaba huyu, Sahaba Abdallah ibn Ummi Maktum aliondoka. Bibi Fatima alirudi na akaendelea kuzungumza na Mtume
Bwana Mtume
.wakamuuliza Binti yake sababu ya kuondoka wakati alipoingia Sahaba Abdallah ibn Ummi Maktum hali kuwa anafahamu kabisa kwamba yule ni kipofu haoni.12
Bibi Fatimah alijibu kama ifuatavyo
Mtume
alifurahishwa mno na jawabu la Binti yake ambalo linaonyesha kipimo cha Uchamungu na utukufu unaotoka kwa Binti yake Mwenye hekima. Isitoshe kwa jawabu hilo, Bwana Mtume hakumlaumu binti yake kutokana na mkazo huu mkali unaohusu Hijabu, bali furaha ya Mtume iliendelea kwa upeo mkubwa na akaunga mkono kwa dhati kabisa kisha akasema;
13.
12 Ni vyema ikaeleweka wazi kwamba Bwana Mtume
alimuuliza Binti yake suali hilo hali ya kuwa yeye mwenyewe anajua wazi kuwa Sahaba yule alikuwa haoni, lakini lengo la Bwana Mtume (s.a.w) kuuliza suali hilo alitaka aone namna Binti yake atakavyo toa jawabu la suali hilo ili historia ipate kusajili mazungumzo haya ya kiimani na ubakie kuwa ni mfano mzuri wa kuigwa siku zote.
13 Mustadrak Al-Wasail Kitabun-Nikah. Biharul-An-Waar juz 104 uk 38.
TUKIO MUHIMU NDANI YA MSIKITI WA MTUME (S.A.W.W.)
Siku moja Bibi Fatimah
alitaka kutoa mhadhara ndani ya msikiti wa Mtume
Kabla ya kuanza kuhadhiri aliten-genezewa sitara humo Msikitini, akakaa yeye na Waumini wengine wakike upande mmoja na Waumini wanaume wa Kiansari na Muhajirina nao wakakaa upande wa pili. Sitara hii aliyotengenezewa Bibi Fatimah
ilikuwa ina maana nyingi ndani yake. Kwanza ilikuwa ni kutekeleza sheria inayohusu Hijabu katika sura ya kuweka kizuizi, ambapo pande mbili hizo zilitenganishwa. Pili, hali hiyo ilikuwa ni kuonesha kutokuukubali kwa vitendo mchanganyiko wa wanaume na wanawake, jambo ambalo maadui wa Uislamu wanatumia kila mbinu kulihalalisha kwa kuli-tolea hoja batili.
Sasa nakutazama ewe dada yangu wa ki-Islamu, nikitarajia umeiona mifano hii mitatu inayohusu maisha ya Bibi Fatimah
ambaye ni mwanamke bora kuliko wanawake wote duniani, na ni mwanamke anayestahiki kuigwa katika Uislamu. Inafaa uige na ujifunze kwake ili upate kupambika kwa umbile la kike ( yaani kuwa na haya) na utukufu, kadhalika ifanye nafsi yako iwe ya mwanamke Mchamungu mwenye kushika mafunzo ya ki-Islamu na hukmu za Qur'an. Ewe dada wa ki-Islamu hebu shikamana na mafunzo ya ki-Islamu ambayo Mwenyezi Mungu amekupa ili ufanikiwe duniani na akhera. Mafunzo haya yatakupandisha kwenye daraja tukufu la wenye imani na mafanikio. Fahamu kwamba hutafanikiwa isipokuwa uwe umeshikamana na kuyatu-mia mafunzo hayo kwa kuyatekeleza maishani mwako.
KUJIHESHIMU NDIYO PAMBO LA MWANAMKE
Bwana Mtume
amesema,
Hapana shaka kwamba pambo limegawanyika sehemu mbili: Pambo lisilo halisi na pambo halisi. Ama pambo lisilo halisi ni lile ambalo linaloonekana wazi, na ni lenye kubakia kwa muda maalum, kisha hutoweka bila hata ya kumuongezea kitu muhusi-ka katika utu wake. Ama lile pambo halisi, ni lile ambalo hubakia muda wote na pia humfanya mwanamke aupate ule utu wake kamili na kumfikisha kwenye daraja ya ukamilifu. Ukweli usiokuwa na shaka ni kuwa, pambo halisi ndilo lenye umuhimu mno kuliko lile jingine, bali ndilo lengo analopaswa kulishughulikia kila mtu. Endapo mtu atakosa kuwa na fungu fulani katika pambo hili halisi, basi pia huwa hana faida yoyote ndani ya lile pambo la dhahiri.
Hapana shaka kwamba kujiheshimu ndilo pambo pekee linalom-faa mwanamke kama alivyosema Bwana Mtume
. Pambo hilo humjengea mwanamke utu, heshima na utukufu hapa duniani na kesho akhera. Ama madawa ya kujirembesha, manukato na mengineyo miongoni mwa mapambo, yote hayo ni mapambo ya nje tu na hayana maana yoyote khususan mwanamke mwenyewe atakapokuwa si Mchajimungu; Mwenyezi Mungu apishe mbali.
Hijabu ndiyo alama pekee inayoweza kutambulisha Uchaji Mungu wa mwanamke na pia heshima yake na utu wake. Wakati huo huo tabia ya kutokuwa na Hijabu huchafua heshima ya mwanamke na kuacha maswali chungu nzima kuhusu Uchaji Mungu wake na kujiheshimu kwake kwa jumla. 14Kalimatur-Rasuli uk 110 cha Sayyid Shirazi.
Yote haya yanakuja kwa sababu yeye mwenyewe kauweka mwili wake kuwa maonesho mbele ya maelfu ya watu siku zote. Kutokana na hali kama hiyo, hata huwezi kutambua ni mikono mingapi iliyowahi kuushika mwili wake kwa kuuacha wazi na kutokujisitiri kwa mujibu wa sheria!! Hivi unadhani watu wa kale na hata wa leo hii, nyoyo zao zitasal-imika vipi katika mazingira hayo ya wanawake kuicha wazi miili yao? Kamwe hawatasalimika kabisa, kwani wanawake wanapoiacha wazi miili yao ni jambo linalopelekea tuhuma mbaya kwa wanawake. Imam Ali
anasema
15
Hapana shaka kwamba, mwanamke asiyekuwa na Hijabu huwa anaidhuru nafsi yake mwenyewe kwa sababu; Kwanza, huwa anapata hasara mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Pili, heshi-ma yake ndani ya jamii huwa inaporomoka. Hasara anayoipata mwanamke huyo mbele ya Mwenyezi Mungu inakuja kwa sababu mwanamke huyo huwa amekwenda kinyume na kanuni za mbinguni na kukosa utiifu kwa Mwenyezi Mungu. Baadaye tutaeleza adhabu za huko akhera atakazozipa-ta mwanamke asiyejali kujisitiri kwa mujibu wa sheria ya KiIslamu.
Ama hasara atakayoipata mwanamke kutoka na na heshima yake kuporomoka ndani ya jamii, hali hiyo inasababishwa na yeye mwenyewe kutokana na tabia yake ya kuyaacha wazi maungo yake yaonekane kwa kila mtu, hali ambayo humuingiza ndani ya kila aina ya uovu na ufisadi na hatimaye akadhalilika vibaya. 15 Al-kafi juz uk 152. Miongoni mwa dhana mbaya atakayodhaniwa mwanamke asiyejali sitara ya kisheria ni kuwa, wakati wote huonekana yuko tayari kufanya ufisadi. Kama si hivyo, amtazamaye hushawishika kumtendea uovu. Mtarjumi.
Na tukirejea kwa mwanamke mwenye kujisitiri kwa mujibu wa sheria ya ki-Islamu, huyu hupata faida za aina mbili kwa pamoja: Faida aipatayo mbele ya Mwenyezi Mungu ni kwamba, yeye huwa ni mwanamke mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na Malaika wake pamoja na Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Utukufu huu anaupata kwa kuwa amemtii Mola wake, ametekeleza maamrisho yake na ameyasitri maungo ambayo Mwenyezi Mungu ameamrishsa yasitiriwe. Na kwa ajili hii basi, mwanamke kama huyu kamwe hatonyanyua unyayo wake bali rehma za Mwenyezi Mungu huwa ziko pamoja naye, pia radhi za Mwenyezi Mungu humbatana naye, na wakati huo huo Malaika wa Mwenyezi Mungu wanamuombea msamaha. Mwenyezi Mungu anasema; "Kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na ni chenye kubakia." 16 Ama faida atakayoipata ndani ya jamii, ni pale mwanamke huyo anapokuwa ni mwenye kuheshimiwa na kutukuzwa, yote haya anayapata kwa kuwa yeye amejipamba kwa pambo la kuji-heshimu na kuuhifadhi utu wake, kisha akausitiri uzuri huo aliopewa na Mwenyezi Mungu.
MAJADILIANO NA MSICHANA WA KIKRISTO
Msichana mmoja wa Kikristo alikwenda kwa mwanachuoni wa ki-Islamu na kumwambia. "Mimi nimefahamu mambo mengi kuhusu Uislamu na kwa hakika dini hii imenishangaza sana kwa kanuni zake na miongozo yake, na nimeupenda Uislamu kwa mapenzi ya kweli. Lakini kanuni moja tu kwangu mimi imekuwa ni kikwazo kuingia katika Uislamu. Nimewauliza watu wengi kuhusu kanuni hiyo, mpaka sasa sijapata jawabu la kunitosheleza. 16 Qur'an 42:36.
Iwapo wewe Sheikh utaweza kunibainishia hekima iliyomo ndani ya kanuni hii, basi nakuthibitishia kuwa nitaingia katika Uislamu." Yule Mwanachuoni akasema, "Ni ipi kanuni hiyo?" Msichana aka-jibu. "Kanuni ya kuvaa Hijabu, ni kwa nini Uislamu haumuachi mwanamke akatoka nje apendavyo kama ilivyo kwa wanaume.?" Mwanachuoni yule wa ki-Islamu akasema, "Je umepata kumuona sonara ameweka dhahabu na johari nyinginezo katika sanduku la kioo, kisha akalifunga sanduku hilo kwa kufuli? Msichana akajibu, "Ndiyo." Sheikh huyu akamwambia tena yule msichana, "Je, ni kwanini sonara hakuziacha johari hizo zikawa zinashikwa na kila mtu ajaye kutaka kununua? Kwa nini amezihifadhi ndani ya sanduku la kioo lililofungwa?" Msichana akasema; "Amefanya hivyo ili azilinde johari zake kutokana na wezi na mikono yenye khiyana." Yule Mwanachuoni akamwambia msichana; "Hii ndiyo hekima ya Hijabu, fahamu kwamba mwanamke ni johari ya thamani ambayo ni lazima kuilinda kutokana na waovu na wahaini.
Pia ni wajibu kumhifadhi mwanamke kutokana na macho ya watu waovu ndani ya kitu ambacho kitamsitiri barabara kama inavy-olindwa lulu katika kola lake, ili asije akaangukia mikononi mwa watu hao na kumgeuza kuwa ngawira yao." Hakuna njia bora isipokuwa Hijabu, hicho ndiyo kizuwizi na ni mlinzi wa mwanamke. Kwa hakika mwanamke mwenye Hijabu huwa sala-ma kutokana na shari. kwa kuwa mwili wake umesitirika, na mapambo yake nayo hayaonekani mbele ya kila mtu.
Hali ya kuvaa Hijabu inawafanya watu wasimtamani mwanamke huyo kwa kuwa hakuna wakionacho cha kuwafanya wamtamani. Kutokana na hali hiyo huwa wanamuepuka, wala hakiwageuzi kitu chochote cha kuwafanya wamuangalie mwanamke huyo, bali humuogopa na kumuheshimu. Mwisho wa yote watu humuogopa na kumpa heshima yake kama anavyostahiki. Yote hayo yatap-atikana kwa ajili ya kuvaa Hijabu, na hali hii inamaanisha kwam-ba, Hijabu ndiyo mlinzi wako na ni hifadhi ya heshima, na utuku-fu wako. Ewe msichana huu ndio upande mmoja wa falsafa ya Hijabu."
Baada ya maelezo hayo ya Sheikh, msichana yule wa Kikristo alionesha furaha na akaridhishwa na maelezo ya Sheikh kisha akasema, "Sasa nimetosheka na falsafa iliyomo ndani ya kanuni hii ya ki-Islamu, na pia nimefahamu hekima iliyomo na ninapen-dezwa kuingia katika Uislamu." Baada ya hapo msichana akatoa Shahada mbili na akawa Muislamu. Majadiliano haya mazuri ya kidini yanatubainishia kwamba Uislamu unakusudia kuihifadhi hehsima na utukufu wa mwanamke, pia Uislamu unataka kuilinda jamii. Na kwa sababu hizo basi, Uislamu umewajibisha Hijabu kama sharti la msingi kuweza kutimiza malengo hayo.
TOFAUTI YA MWANAMKE MWENYE HIJABU NA ASIYE NA HIJABU
Mmoja wa marafiki zangu alinisimulia tukio la kufurahisha lililom-tokea Muumini mmoja wa ki-Islamu. Tukio hili lilikuwa kama ifu-atavyo. Siku moja Muumini huyo alikuwa akitembea pamoja na mkewe aliyekuwa kavaa Hijabu. Matembezi hayo yalimfikisha katika moja ya bustani zinazotembelewa na watu wa aina tofauti. Ghafla Muumini huyo alijiwa na mtu fulani ambaye naye alikuwa na mkewe. Mke wa mtu huyu hakuwa amevaa vazi la Hijabu na hivyo basi kwa dharau na kejeli alimwambia yule Muumini. "Kwa nini umemvalisha mkeo Hijabu, kwa nini hukumuacha akatoka bila Hijabu kama jinsi alivyo mke wangu? Hijabu ina faida gani?" Jawabu alilotoa Muumini yule lilikuwa la kushangaza na la kishu-jaa. Alimwambia.
"Je unafahamu tofauti ya mwanamke mwenye Hijabu na asiyekuwa na Hijabu? Bwana yule mwenye kejeli akasema "Nini tofauti yake?" Yule Muumini akajibu kwa njia ya kuuliza, je, kuna tofauti gani baina ya taxi na gari ambalo mtu hulitumia yeye binaf-si? Yaani kwa matumizi yake pekee yake." Bwana yule akajibu akasema, "Taxi hutumiwa na kila mtu, wakati ambapo gari maalum linamuhusu mwenyewe peke yake. Hii ndiyo tofauti iliyopo." Basi yule Muumini akasema, "Hali hiyo ndio iliyopo baina ya mwanamke aliyevaa Hijabu na yule asiye na Hijabu.
Mwanamke asiye na Hijabu ni sawa na taxi ambayo kila mtu anaweza kuikodisha na kuitumia. Mwili wa mwanamke huyo huwa wazi na kuonesha mapambo yake na uzuri wake, na kuwafanya watu wavutike kutokana naye, jambo ambalo linaweza kusababisha kutendewa maovu, kama ambavyo mara kwa mara hali hii inavyowapata wanawake wa aina hii. Ama mwanamke aliyevaa Hijabu yeye ni bibi aliyemtukufu, ni maalum kwa ajili ya mumewe, mapambo yake na uzuri wake havionekani kwa kila mtu. Pia watu wenye nyoyo chafu na dhaifu hawamuangalii, na uso wake na mapambo yake havikutani na macho yenye khiana, kwa kuwa amehifadhiwa ndani ya Hijabu.
Kwa hiyo utukufu wa mwanamke huyu na mwili wake vimo ndani ya hifadhi bora, pia bibi huyu hupendwa na kupendeza mbele ya mumewe na kum-fanya mume kuwa na imani na mkewe, kwa sababu ya hifadhi hiyo inayomkinga kuwa na mahusiano na watu wengine kwa njia mbaya." Baada ya maelezo yaliyotolewa na yule Muumini wa kiIslamu, bwana yule mwenye kejeli aliona haya na akaanza kumwambia yule Muumini, "Najuta kwa kukuudhi, kwani maneno yako ni ukweli mtupu, na mifano uliyonipa ni sawa kabisa naom-ba samahani kwa haya niliyokutamkia na pia natubia kwa Mwenyezi Mungu kwa kitendo nilichokitenda na sasa...Kabla bwana huyu hajamaliza kujieleza mkewe alimkatiza na kusema. "Naam; naapa maneno haya aliyosema bwana huyu ni sawa na mfano aliotoa ni mzuri sana, kwani kabla ya leo nilikuwa sijasikia mawaidha kama haya. Mfano huu umeniingia moyoni nami pia natubia kwa Mwenyezi Mungu."
Baadaye yule mume akarudia kukamilisha usemi wake akasema, "Na mimi sasa naiamini Hijabu na kuanzia leo mke wangu atain-gia katika uwanja mtukufu kwa kuvaa Hijabu. Kamwe sikubali mke wangu atoke bila Hijabu, kwani ndiyo vazi la amani na imani. Nafsi yangu haipendi kabisa kumuona mke wangu akidhihiri mbele za watu kama kwamba yeye ni kwa ajili ya kila mtu."
NI LIPI LENGO LA WANAOPINGA HIJABU?
Baada ya kuusoma Uislamu kwa undani, maadui wa Uislamu wameandaa mikakati ya kuuangamiza Uislamu na Waislamu kidogo kidogo, bila Waislamu kuigundua hali hii isipokuwa wachache. Na miongoni mwa mikakati yao ya kishetani katika kutilia mkazo kuiondoa Hijabu, wametumia na bado wanatumia kila njia za kuvutia na madai batili kutimiza lengo lao hilo. Kuna mambo mengi machafu wanayoyaeneza katika jamii ya Waislamu, chini ya kiza kinene chenye ibara zinazovutia na kam-peni ambazo matokeo yake ni mabaya.
Kwa kutumia mbinu za kimaendeleo na utaalamu, wamefaulu kuwapotosha Waislamu, na wakasambaza uovu mwingi. Kwa madai hayo hayo ya maen-deleo na kupigania uhuru na haki za binadamu., uchafu wao umeenea ndani ya jamii zetu za ki-Islamu. Kwa hakika wamefaulu kuzinyang'anya jamii zetu maumbile ya kuwa na haya na heshi-ma. Ibara hizi zimewahadaa Waislamu wengi, wake kwa waume.
Masikini Waislamu hawa wamekuwa wafuasi wa itikadi hizi zenye sumu kali inayovuja kuelekea kwenye maovu na maangamio. Wanawake wa ki-Islamu na mabinti wa ki-Islamu wanafanya upin-zani hadharani dhidi ya vazi hili la ki-Islamu. Wametoka katika nyumba ya utukufu na imani na kuingia katika nyumba ya kiza na upotovu.
Wanawake wetu na wasichana wetu wameathiriwa na mavazi ya Kiyahudi na Kikristo yatokayo kwa wapinzani wa kimagharibi na makafiri wa mashariki. Maadui na wavamizi hawa wamefanikisha kwa kiasi kikubwa lengo lao, kwa kuwa sasa hivi jamii ya ki-Islamu imekwisha tumbukia na kuzama katika dimbwi la matendo machafu. Jamiii ya ki-Islamu ambayo asili yake ni adil-ifu na yenye muruwa, leo imegeuka na kushika bendera ya maovu ya kila aina.
Matukio ya kubaka,17 kupora, udanganyifu, dhulma, kutoa mimba na mengineyo, yameivamia jamii yetu tukufu. Watu hawa wa Ulaya magharibi na mashariki yake, hawali wakashiba wala hawalali wakapata usingizi, ila mpaka watimize lengo lao la kutu-achisha utamaduni wetu wa ki-Islamu. Ni wazi kabisa kwamba watu hao wanaomtaka mwanamke wa ki-Islamu avue Hijabu lengo lao wanataka wamuone mwanamke huyu anafanya ufisadi kwa kumlazimisha akae uchi. Nia yao ni kumuangamiza na kuipotosha jamii kwa jumla. Kumtaka mwanamke asivae Hijabu ni kumuondolea heshima yake na uchamungu wake.
Ewe msomaji wangu, iwapo utataka kuyafahamu vizuri maneno yangu, muulize mzee yeyote katika wazee wa makamo na mababu ambao bado wanayo kumbukumbu ya hali ya mambo ilivyokuwa hapo zamani. Waulize kwa kusema, "Hivi maovu haya yaliyopo sasa hivi ya kuwavunjia heshima wanawake na kuwaba-ka, na watu kudhulumia, mambo haya yakulikuwepo hapo zamani kabla ya miaka ishirini au thelathini iliyopita?" Watakujibu kwa nguvu zao zote, kwa kusema, Hapana kabisa hayakuwako."
17 Kwa asili mia kubwa wakazi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba, pwani ya Kenya inay-ojumuisha Mombasa, Lamu n.k, Visiwa vya Ngazija na miji mingi ya Tanganyika (Tanzania bara) kwa kipindi kirefu imekuwa ni miji ya amani na utulivu. Mazingira haya mazuri yali-jengeka kutokana na wakazi hao kuwa ni wafuasi wa dini ya ki-Islamu iliyowajenga katika maadili mema ya ki-Islamu. Ni ukweli usiyopingika kwamba hapo zamani hapakuwa na matukio ya kuwavunjia heshima wanawake kama tunavyoyashuhudia mambo hayo leo hii ndani ya miji yetu. Misamiati ya kufadhaika na kubaka haikuwako hapo zamani. Utoaji mimba na kutupa watoto ni mambo mageni kwetu hayakuwako. Ujambazi, utapeli na kutokuaminiana ni misamiati mipya. Lakini haya yote ni mipango ya maadui wa dini ya ki-Islamu, na kwa bahati mbaya Waislamu wamehadaika na mbinu za kikafiri na kujikuta wanapoteza dini yao na hata hiyo dunia waliyopambiwa imewatupa mkono hawana nayo asilani. Msiba uliyoje kwa Umma wa Ki-Islamu!! Mtarjumi.
Sasa yametoka wapi mambo haya maovu na matukio ya kuhuzu-nisha? Watakuambia, "Hali hii imetokana na mambo mengi, mion-goni mwake ni wanawake wenyewe kutembea mabarabarani bila sitara ya kisheria." Hili ndilo jibu sahihi kwa matatizo kama haya ya ubakaji ambayo takwimu zake zinaongezeka kila siku. Iwapo utataka uhakika zaidi, waulize wakazi wa miji michache ambayo wakazi wake bado wanashikamana na sheria za ki-Islamu na imani zao zingali hai na uwaambie, "Hivi katika miji yenu kuna matukio maovu ya kubaka na unyang'anyi kama inavyotokea katika miji mikubwa?" Bila shaka watakujibu hapana. Sababu kubwa ya kutokuwepo maovu kwa wingi katika sehemu hizo, ni kwa kuwa jamii bado inauheshimu na kuulinda Uislamu na kanuni zake zenye hekima.
Maovu mengi zaidi yanajitokeza katika miji au sehemu ambazo zinadai kuwa zimeendelea. Miji hiyo imehusika kwa kiwango kikubwa na ongezeko la maovu ambayo yanakithiri kwa kasi ya kutisha, licha ya serikali zao kutoa adhabu kali kwa wanaohusika kila wanapobainika na kukamatwa.18
Hali hii inaonyesha wazi kwamba kanuni peke yake hazitoshelezi, wala hazinufaishi katika kuirekebisha jamii, bali kinachotakiwa ni kuing'oa mizizi ya maovu kwanza, ili maovu hayo yapate kunyau-ka yenyewe. Kwa kawaida kila kitu kina asili yake, na asili ya maovu yaliyozikumba jamii zetu sasa hivi, ni hizi picha za video wanazooneshwa vijana wetu, 18 Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimekumbwa kwa kiasi kikubwa na matatizo ya mmomonyoko wa maadili, na zinatungwa sheria kali kila leo ili labda? itawezekana kureke-bisha hali hii, lakini bila mafanikio. Tunachokiona ni ongezeko la maovu ambayo yanatende-ka wazi wazi na kila mtu anayashuhudia wakiwemo hao wanaokaa na kutunga sheria hizo kwa matumaini ya kukomesha maovu. Hakuna njia inayoweza kukomesha hali hiyo isipokuwa ni kushikamana na mafunzo bora ya ki-Islamu. Ni muhimu kwa viongozi wetu wakatambua mambo yanayochangia uharibifu wa mwenendo wa jamii na kuhakikisha kuwa wanaing'oa mizizi yake. Mtarjumi.
picha ambazo huwa zinaonesha hali ya maumbile ya siri, isi-toshe huonesha pia matendo ya jinsiya baina ya mke na mume bila kuona aibu wala huzuni kuuchezea na kuudhalilisha uanadamu ambao ni kitu cha thamani, kutokana na kuwa na uwezo wa kutambua nini cha kufanya na nini si cha kufanya. Kitu kingine kinachochangia ni nchi zetu zinaporuhusu uingizaji wa magazeti na majarida yanayochapisha picha zinazoonesha sehemu za siri na kisha magazeti hayo na majarida yanasam-bazwa katika jamii. Maadam asili ya maovu bado ipo kama mifano ya picha za video na majarida tuliyoyataja hapo kabla, basi maovu na matukio machafu yataendelea kutokea siku hadi siku, na kamwe hayataondoka kwa kutegemea kanuni hizi za kidunia.