4
VAZI LA MWANAMKE
UISLAMU SIYO DINI YA NADHARIA
Mara nyingi tunasoma katika baadhi ya magazeti kwamba, baad-hi ya watu waliohadaika na wasiojuwa chochote kuhusu Uislamu, eti wanajaribu kutoa fikra zao katika kukosoa baadhi ya kanuni za sheria ya Ki-Islamu. Miongoni mwa kanuni ambazo wamekuwa wakijaribu kuzikosoa kwa kutumia kalamu zao ni hili vazi la Hijabu. Waandikapo husema; "Mimi sioni umuhimu wa Hijabu, kwani Hijabu katika maoni yangu sio lazima kwa kuwa inarudisha nyuma maendeleo." Au hupata wakasema kuwa; "Kuna ubaya gani wanaume na wanawake kuchanganyika pamoja?" Na mengine mengi wanasema lakini kifupi ni hayo. Sisi tunawajibika kuwaambia watu hawa na wengine mfano wa hao kwamba; "Ninyi ni kina nani? Ninyi ni kina nani hasa mpaka mnathubutu kutoa maoni yenu dhidi ya desturi na mila ya Mbinguni?
Na mna utuku-fu gani mbele ya maamuzi ya MwenyeziMungu na sheria nzima ya Ki-Islamu? Na je Uislamu ni dini ya fikra za kinadharia mpaka mumediriki kuusemea kwamba mimi naona kadhaa, au mtazamo wangu katika sheria ya Ki-Islamu naona hivi au vile.? Kisha nawauliza hawa wanaosema maneno haya; "Je, ninyi kweli ni Waislamu? Ikiwa wao ni Waislamu wanawajibika kuwa watiifu katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake, pia washikamane na sheria za Ki-Islamu ambazo miongoni mwake ni Hijabu. Na kama ninyi siyo Waislamu basi, hamna haki ya kuingilia mambo ya Ki-Islamu, wala hamna haki ya kutoa maoni yenu potofu mbele ya Umma wa Ki-Islamu.
Mpaka hapa ndugu msomaji nashangazwa na ujeuri wa watu hawa dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na ni kwa misingi gani viumbe hawa dhaifu wamejasirika na kufikia kiasi cha kukosoa hukmu na kanuni za Mwenyezi Mungu? Je wanasahau kwamba Mwenyezi Mungu anasema katika sura al-maidah katika Aya tatu mfululizo: "Na wale wasiyohukumu ( kwa sheria) aliyoi-teremsha Mwenyezi Mungu basi watu hao ni makafiri, madhal-imu, mafasiki.29 Watu hawa mbele ya Mwenyezi Mungu watabeba mzigo mzito kwa makosa yao ya kuhamasisha watu kuvunja amri za Mwenyezi Mungu na kutenda machafu yaliyo katazwa. Malipo (adhabu) yao pia ni mazito kutokana na maneno yao hayo, kwa adhabu kali watakayoadhibiwa kutokana na wao kuunga mkono maasi na kuyatia nguvu yatendwe.
Mimi naamini kuwa, watu hawa hawasemi kutoka katika nafsi zao, bali wao wanatumwa na maadui wa Uislamu wanaoupiga vita Uislamu kupitia nyuma ya pazia. Lengo lao ni kuiangamiza maana nzima ya Uiislamu, na kisha kuwapotosha wasichana na wavulana wa Ki-Islamu. Jambo la kusikitisha na kuhuzunisha ni kwamba, kauli kama hizi zimekuwa zikirudiwa mara kwa mara na katika nyakati tofauti, ima ndani ya magazeti na majarida na au katika mikutano mbali mbali. Kuna lugha nyingi zinazotumika katika kampeni hii ikiwemo lugha ya Kiarabu ambayo inawaun-ganisha Waislamu wa dunia nzima kama lugha ya dini yao.
Yote haya ndugu Waislamu, ni majaribio ya makusudi kabisa yenye lengo la kuivuruga na kuipoteza jamii takatifu ya Ki-Islamu. Kinachotakiwa kwa Waislamu wenye uchungu na dini yao ni kun-yanyuka na kuyapinga magazeti haya kwa kuwa yenyewe ndiyo sauti ya vita vya kuutokomeza Uislamu na Waislamu. Kwa hakika wajibu wa kisheria unamtaka kila Mwislamu kupambana na majaribio haya hatari kwa uwezo wake wote kinadharia na kivi-tendo, hadi lengo la maadui hawa lisitimizwe katika nchi zetu tukufu za Ki-Islamu na jamii za Ki-Islamu popote zilipo duniani. 29Suratul Maidah Aya No 44, 45 na 47.
Kadhalika kukabiliana na maadui hawa dhidi ya njama zao za kutaka kugeuza nchi zetu kuwa ni mapori ya wanyama kufuatia mila zao wanazokusudia kuturithisha.Watu hawa madhalimu, katika nchi zao wamebadilika kutoka katika mila ya wanaadamu na wamekuwa na tabia za wanyama, kiasi kwamba mwanamke na mwanaume wanakidhi matamanio yao mabarabarani kama wafanyavyo wanyama bila kuwa na hisiya zozote za kuona haya wala kuogopa kwamba wao ni viumbe teule na watakatifu kwa kuumbwa kwao kama wanaadamu.
VIPI WAMEFAULU KUTUPOTOSHA?
Sasa tuangalie namna gani watu hawa wamefanikiwa kutupoto-sha, kwa kuwavua binti zetu na wake zetu mavazi ya Ki-Islamu. Pia ni kwa vipi wamefaulu kututeka kwa kupitia anuani ya kutetea uhuru wa mwanamke. Ili kupata ufumbuzi wa suala hili hatuna budi kufanya ziyara ya uchunguzi katika nchi za magharibi na kuiangalia jamii yao, na ni vema pia kufuatilia magazeti yao na majarida ili tuyaone mazingira mabaya wanayoishi wanawake wasio na Hijabu huko kwao. Kwa watu wa magharibi mambo hayaishii kwenye kukosa Hijabu na kutembea kichwa wazi na miundi nje basi. Bali hali yao inakwenda mbele zaidi kiasi kwamba kifua nacho huwa wazi, na wanawake hao kadhalika huvaa nguo nyepesi inayodhihirisha rangi ya mwili hadi kufikia kufanana na mtu aliye uchi kabisa.
Matokeo ya mavazi haya ni umalaya au kutekwa nyara na baa-daye kubebeshwa mimba za haramu kisha kuingia katika kufanya mauaji pindi wanapotaka kuzitoa mimba hizo. Linalojitokeza hapa ni kudhulumu kiumbe hicho kinachotolewa kwa nguvu au muhusika kukumbwa na kifo wakati wa zoezi hilo.
Hali hii ndiyo iliyoko kwenye nchi zinazoitwa zimeendelea. Nchi zetu za Ki-Islamu na Waislamu kwa jumla kwa sasa wanakabili-wa na tishio la hatari hii inayokuja kwa kasi ya ajabu kutoka kwenye hizo nchi za mashariki na magharibi. Kinachotakiwa kwa Waislamu ni kuwa na tahadhari kubwa na kuikabili kasi hii ya hatari inayokuja kutoka katika nchi hizo za mashariki na magharibi. Kwa hakika wameeneza uovu wao katika jamii yetu chini ya kivuli cha utaalamu na elimu. Idadi kubwa ya makosa ya jinai yanayotokea katika nchi zinazo-daiwa kuwa zimeendelea ni mengi mno, ukilinganisha na matukio kama hayo yanayotokea katika nchi zetu za Ki-Islamu. Tofauti hii ni kwa sababu Uislamu unahimiza na kutilia mkazo watu wawe na maadili mema, tabia nzuri na waepukane na kila tabia chafu.
Pamoja na hali hii ambayo kwa kiasi fulani inaone-sha tofauti baina ya nchi za Ki-Islamu na hizo za magharibi, Ni lazima kwa Waislamu kuchukua tahadhari, wasihadaike na hali waliyonayo, kwani hatari inakuja na shari zinaandaliwa dhidi yao, na ni wajibu wa kila Mwislamu kuwa na tahadhari. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayotendeka katika nchi ambazo ndizo zina-zoongoza katika kupiga vita utamaduni wa Ki-Islamu.
1.Nchini Uingereza peke yake karibu filamu 10 zinazohusu mambo machafu hukamilika kutengenezwa kila wiki na kutumwa nchi za nje. Kwa hali hii basi kila mwaka filamu zisi-zopungua 500 hutengenezwa nchini Uingereza na zote ni za kuonesha mambo ya aibu tupu na uchafu ambao jamii yetu inapotea na kuangamia kutokana na yaliyomo ndani ya filamu hizi. 2.Mwaka 1961 polisi wa Uingereza walijaribu kuwaangamiza wanawake wapatao laki moja, ambao kazi yao ilikuwa umalaya na machafu mengineyo, lakini baadaye walitangaza kushindwa kwa jaribio hilo.30
3.Mjini Rome kuna majumba yapatayo mia tano ya malaya, humo ndani mna maelfu ya wanawake ambao kazi yao ni kusubiri wanaume.31
Gazeti la " The Gurdian" liliandika kwamba takwimu za polisi zinaonesha kuwa, makosa ya jinai ya kubaka yanaongezeka mwaka hadi mwaka. Katika mji wa Washington peke yake kila baada ya dakika kumi na tano huwa kuna tukio la kubaka. Na katika mji mkuu wa Ungereza (London) yalitokea matukio 2095 ya kubaka wanawake na wasichana mwaka 1970 peke yake. Haya ni machache katika mengi ambayo tungeweza kukuorodheshea.
EWE DADA WA KI-ISLAMU
Ewe dada wa ki-Islamu nakuomba uyafanyie mazingatio baadhi ya mafunzo ya Ki-Islamu ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu kwetu Tanzania Serikali imejaribu mara kadhaa kuwaondoa mitaani wasichana na wanawake wanaofanya umalaya hadharani, lakini bila mafanikio. Kuna wakati sisi tunajiuliza hivi kweli serikali imedhamiria kupiga vita tabia hizi chafu au la? Swali hili linakuja pale tunapoyaona na kuyasikia makongamano mbali mbali ambayo yanahusu kuitahadharisha jamii kutokana na ugonjwa hatari wa ukimwi. Hivi ni kweli tutaweza kupambana na janga hili kwa mikutano na semina zisizokwisha wakati mitaa yetu kila inapofika jioni wasichana wetu na wanawake wetu wanatoka barabarani wak-isubiri wanaume? Pamoja na hali hiyo, mavazi wanayovaa wanawake na wasichana hao pindi wanapofuatilia mawindo yao, ni mavazi hatari ambayo bila kuuliza ni kichocheo kikubwa kwa wanaume kunasa katika mtego huo.
Binafsi yangu ninaingiwa na mashaka makubwa juu ya lengo na madhumuni ya semina, mikutano pamoja na mabango yanayoitahadhrisha jamii kuhusu janga la ukimwi. Haiwezekani kabisa kuupiga vita UKIMWI wakati vyanzo vyake viko huru ikiwemo kuwahamasisha Watanzania kuwa wazinifu kwa kuwaambia wavae kondom. Hapana shaka sote tunafahamu kwamba, njia kuu ya maambukizo ya ugonjwa huu ni uzinifu. Hivyo basi, ni wazi kwamba kwa utaratibu huu hatuwezi kushinda vita dhidi ya UKIMWI.
31Majumba hayo kwa hapa kwetu yanajulikana kwa jina la madanguro. Imani yangu ni kwamba madanguro hayo yanajulikana fika, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa na jamii au vyombo husika kuyaondosha majumba hayo ili kuisalimisha jamii yetu kutokana na tabia hizi za kinyama. Je, huku nako sikuupalilia UKIMWI uzidi kushamiri katika jamii yetu? Iko wapi hapa dhamira ya kupiga vita UKIMWI? Mtarjumi.
amekupangia ili uweze kufanikiwa duniani na akhera. Mafunzo hayo ni mafunzo mema yatakayo kupandisha daraja ya ubora, imani, na utukufu. Na sina shaka kwamba utafanikiwa na kupata kheri nyingi mno, lakini sharti uyatumie na kushikamana nayo maishani mwako. Hijabu kabla ya mambo mengine: Hijabu pekee ndiyo kinga yako ya kuaminika ambayo itakulinda kutokana na maovu na waovu, na ni hifadhi madhubuti dhidi ya kila aina ya uchafu na wahusikao na uchafu huo. Vazi la Hijabu ewe dada wa Ki-Islamu, ni ujumbe rasmi wa Mwenyezi Mungu kwako, basi mtii Mola wako na tekeleza amri yake. Hakika Hijabu ni kwa faida yako na umewekewa kwa ajili ya kulinda hadhi yako wewe mwenyewe. Dada mpendwa, Muumba wako ni mpole kwako naye anakwambia katika Qur-an,
"Na wala msioneshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za jahiliya." Q. 33:33 Na anasema tena Muumba wako. "Wanawake wateremshe (vizuri) shungi zao hadi vifuani mwao na wala wasioneshe mapambo yao." 24:31 Maelekezo ya Mola wako ndiyo haya, ole wako ukiyapa mgongo utaangamia duniani na akhera.
Dada mpendwa, ufunguo bora wenye thamani kubwa utakaoweza kufungua milango ya dini yako, dunia yako na heshi-ma yako umo ndani ya Hijabu, hebu jitahidi kufuata amri ya Mola wako ili uupate ufunguo huo. Pia fahamu kwamba uzuri wako, thamani yako na heshima yako vimo ndani ya Hijabu. Ole wako kama utaiacha Hijabu, basi uzuri wako na heshima yako vita-poromoka. Ningependa pia ufahamu kwamba, njia ya wewe kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuingia peponi imo ndani ya Hijabu. Kwa hiyo radhi za Mola wako na pepo utavikosa iwapo utaitupa Hijabu. Kadhalika dada mpendwa fahamu kwamba, njia inayoelekea kwenye ghadhabu za Mwenyezi Mungu na motoni inapitia kwenye kuvua Hijabu na kutoitekeleza. Basi ole wako usi-jeanguka ndani ya kina kirefu cha moto wa Jahanam.
Imamu Ali
amesema:
Basi ni juu yako ewe dada ujifahamu thamani yako. Usiruhusu mwili wako na mapambo yako yachezewe na kila mtu, isipokuwa mumeo tu. Katika kumsifu mwanamke mchamungu, Bwana Mtume
anasema;
Dada yangu katika Uislamu, angalia sana usije ukawa mfano wa bidhaa zilizotandazwa sokoni, au bidhaa za dukani kila mmoja huangalia na kuzikamata kamata apendavyo.33
32 Al kafii juz 5 uk 324.
33 Makusudio ya usemi huu ni kwamba: "Mwanamke muovu ni yule ambaye mwili wake hauna hifadhi popote pale, ndani au nje, akiwa na mumewe au hata mbele ya wanaume wengine." Kwa hiyo mwanamke huyo ni sawa na bidhaa iliyoko sokoni au dukani inatafuta na au inan-gojea wanunuzi waione. Endapo wataipenda watainunua na wasipoipenda wataiacha. Na kawaida ilivyo ni kwamba, bidhaa inapokuwa sokoni au dukani, basi wanunuzi wana uhuru mkubwa katika kuchagua bidhaa wanayoitaka na hapo ndipo mtu huikamata bidhaa hiyo na kuigeuza kila upande ili tu aone kama itamfaa au la. Bwana Mtume
anamtahad-harisha mwanamke asiwe ni kiumbe kinachokamatwa na kila mtu kama bidhaa iliyoko sokoni, ni lazima aulinde uwanamke wake na utu wake. Mtarjum
Usitumie vifaa vya kujirembesha na manukato ila unapokuwa nyumbani mwako na nduguzo wanaokuhusu kisheria. Tahadhari tena tahadhari sana na tabia ya kujirembesha kisha ukatoka barabarani, jambo hili ni hatari unaweza ukafanyiwa maovu, pia litakusababishia ghadhabu na laana za Mwenyezi Mungu. Bwana Mtume
amesema
Bwana Mtume
amesema:
34 Ewe dada mpendwa, usipeane mkono na mwanamume asiye kuhusu, japo kuwa yeye ni mion-goni mwa jamaa zako, kama watoto wa ami zako au watoto wa mjomba. Iwapo mwanaume atanyoosha mkono wake kwako mwambie; "Dini yangu na Mola wangu ananizuia kupeana nawe mkono.
Usimuogope mtu ikiwa atachukia au kukasirika kwani radhi ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko radhi za watu. Na kuogopa kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu ni bora kuliko kukasirikiwa na watu. Imesimuliwa ya kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia Mtume Isa
; "
"35 Usione haya kuvaa Hijabu, bali shikamana nayo kila inapokuwa. Ni lazima popote pale japo iwe ni katika jamii isiyovaa Hijabu, au hata kama umo ndani ya shule au chuo ambacho wengi wao hawana Hijabu wala hawataki kuvaa. Inakupasa uwe na msi-mamo wa dini yako sawa sawa kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika Qur'an; 34 Al kafi juz 5 uk 552 35 Al kafi juz 8 uk 138 "Uwe imara (na msimamo) kama ulivyoamrishwa. 11:112 Mwenyezi Mungu amesema tena.
"Hakika wale waliosema Mola wetu ni Allah kisha wakawa na msimamo (katika dini yao) huteremkiwa na malaika (wakati wa kutoka roho zao na wakawaambia) msiogope wala msi-huzunike na furahini kwa pepo mliyokuwa mkiahidiwa." 41:30 Usijali kelele za wapinzani, sawa sawa wakiwa ni wanawake au wanaume, bali waambie kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Ikiwa ninyi mnatukejeli basi na sisi tutawakejeli kama mnavyotukejeli." Hud:38 Hapana shaka kwamba tabia ya wapinzani wa sheria za Mwenyezi Mungu siku zote imejaa kejeli na dharau dhidi ya
Waumini na Watu Watakatifu. Yote hayo wanayafanya kwani wao hawana utu, na wala hawana dalili wala hoja ya kutetea upinzani na upotofu wao. Na kwa ajli hiyo basi wao hutegemea zaidi njia za kutukatisha tamaa ili tu wapate kufanikisha maovu na maasi yao. Hapana shaka kwamba njia hizi za upinzani ulioshindwa dhidi2 yetu, ndizo hizo hizo walizokuwa wakizitumia kupambana na Mitume wa Mwenyezi Mungu na watu wema na waumini tangu hapo zamani katika historia ya ulimwengu. Mwenyezi Mungu anasema: "Na hapana Mtume yeyote aliyewafikia isipokuwa wao wal-imfanyia kejeli." Al-Hijr: 15:11 Na anasema tena Mwenyezi Mungu: "Hakika wenye kutenda maovu walikuwa wakiwacheka walioamini. Na wanapopita karibu yao wanakonyezana." 83:29-30 "Na pindi wanapowaona husema kuwa hakika hawa wame-potea.83:32
Ewe dada yangu katika Uislamu, je unafahamu kwamba mwenda wazimu hujiona kuwa yeye pekee ndiye mwenye akili na wengine wote ni wenda wazimu, wakati ukweli hauko hivyo?36 Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Basi leo Walioamini watawacheka wale waliokufuru." 83:34 Hapana shaka kwamba, iko siku Mwenyezi Mungu na waumini watawakejeli wapinzani hawa wanaozicheza shere sheria na kanuni za Mwenyezi Mungu. Mwenyzi Mungu anasema; "Mwenyezi Mungu atawalipa kejeli zao na watapata adhabu kali." 9:79 Anasema Mwenyezi Mungu; "Yakawazunguka wale waliyofanya mzaha miongoni mwao, yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha." 6:10 Huu ni mfano mzuri sana kwa hao wanaopinga sheria na muongozo wa Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu anasema tena: "Moto utababua nyuso zao nao watakuwa humo wenye kukenya (meno yao kwa adhabu). (Waambie) Je hamku-somewawa Aya zangu na ninyi mkazipinga? Watasema; Mola wetu! Uovu wetu ulituzidi na tukawa ni watu wenye kupotea." 23:104-106 Maneno haya ya Mwenezi mungu yanaonesha namna watakavyokiri watu hao wenye kejeli kwamba wao katika ulimwengu huu walikuwa waovu, wenye kupoteana kutangatan-ga. Lakini Mwenyezi Mungu atawajibu kwa jawabu kali;
"Atasema (kuwaambia watu hao): Dhalilikeni humo motoni na wala msinisemeshe. (Kumbukeni kwamba) Bila shaka kulikuwa na kundi katika waja wangu likisema; Mola wetu tumeamini basi utusamehe na utuhurumie kwani wewe ndiwe Mbora wa wanao-hurumia. Lakini ninyi mliwafanyia mzaha hata wakakusahaul-isheni kunikumbuka na mlikuwa mkiwacheka. Hakika leo nime-walipa (wema) kwa sababu ya kusubiri kwao, bila shaka hao ndiyo wenye kufuzu." 23:108-111 Kwa hiyo jione mwenye fahari kwa kuvaa Hijabu, kwani umo katika hali ya kuonesha utiifu wako kwa Allah (s.w.t), na unapata thawabu kila hatua yako moja utembeayo. Kilichoko kwa Allah (s.w.t.) ni bora na ni chenye kudumu Basi Je, Hamfahamu?" 28:60."
"Na radhi za Mwenyezi Mungu ni kubwa." 9:72 Kinyume chake katika thawabu ni, yule mwanamke asiye na Hijabu, kwa kuwa anapata madhambi kwa kila hatua yake moja anayotembea. Wapo wanawake wasemao; "Mimi najiamini nafsi yangu siwezi kufanya maasi na maovu, hivyo sioni sababu ya kunilazimisha kuvaa Hijabu." Jawabu la fikra kama hii ni hili lifu-atalo. Kwanza: ni lazima ifahamike kwamba vazi la Hijabu ni jambo la wajibu juu yako kwa mujibu wa sheria kati hali yoyote ile iwayo, sawa sawa ukiwa unajiamini au la. Pili: Kujiamini peke yake hakutoshi kwa sababu.
"Hapana shaka kwamba nafsi ni yenye kuchochea maovu isipokuwa ambayo Mola wangu ameirehemu. "12:53 Kuna wasichana wengi wameteleza na wakajikuta wameingia ndani ya maovu kwa sabau ya kuacha Hijabu. Tatu: Kuishi bila sitara ya Ki-Islamu kunasababisha kuamsha hisia za kimaumbile kwa wanaume wanaokutazama, pia inaweza kuwa sababu ya kukufanyia uchafu bila wewe kutarajia. Je! hili hali-wezekani? Hali kama hii ikikufika, huko kujiamini kwako kutaku-saidia na au kunaweza kuizuwia hali kama hii isitokee? Ewe msichana na mwanamke wa Ki-Islamu, usihadaike na fikra poto-fu, maadui wa Uislamu ndiyo hao hao maadui wa mwanamke, wanaipiga vita Hijabu kwa njia nyingi. Huna budi kuzinduka na kuepuka kampeni hizo sizizo na hekima. Wala usidanganyike na mitego yao iliyomo ndani ya mtizamo wao. Kwa kukuzindua ni kwamba; maneno wayasemayo huenda yakawa yanavutia hasa yanapokuja kwa lugha ya kutaka eti kukukomboa. Maneno yao haya ni sawa na asali tamu lakini ina sumu ukiila itakudhuru. Angalia iwapo utahadaika utakuwa umeiuza nafsi yako na dini yako kwa maadui wa Mwenyezi Mungu, pia fahamu ya kwamba utakuwa umeshawauzia kwa thamani ya kukuangamiza wewe mwenyewe.
Hebu jitahidi kuwa Mwislamu kwa ulimi wako na vitendo vyako. Wachana na nyendo za kiulaya, kwani miongoni mwa malengo yao ni kumtumia mwanamke kama chombo cha kutangaza biashara hali ya kuwa hana sitara. Jilinde kwa Mwenyezi Mungu akuepushe na nyendo zao ambazo nia yake ni kuichafua jamii ya
Ki-Islamu na kuiangamiza. Fahamu ewe dada mpendwa kwam-ba, maendeleo na uungawana kwa mwanamke ni kuwa na sitara inayokubaliana na mazingira na hali yake kama mwanamke. Dada wa Ki-Islamu, utamaduni na uhuru wa kweli unapatikana ndani ya Uislamu na kanuni zake toka mbinguni.
Elewa pia kwamba, uovu na fedheha vitakupata iwapo utakwen-da kinyume na kanuni za Ki-Islamu. Ni wajibu wako kutangaza na kuelimisha hekima ya Hijabu na falsafa yake kwa nduguzo, jamaa na marafiki. Kazi hii ifanye popote, ikiwa nyumbani, shuleni, chuoni, ofisini na sehemu nyinginezo unazoweza kufanya hivyo katika muda wote wa uhai wako. Kufanya tabligh siyo kazi ya wanaume peke yao, bali na wanawake inawahusu kikamilifu. Mtume
anasema;
Historia inatuonesha kwamba Bibi Fatma
alikuwa akifafan-ua mambo yanayohusu sheria kwa wanawake wa Madina. Bibi Zainab binti Ali bin Abi Twalib alikuwa akifundisha tafsiri ya Qur'an kwa wanawake wa mji wa Al-Kufah huko Iraq. Fahamu ya kwamba Mwenyezi Mungu atakulipa thawabu nyingi kwa kila msichana au mwanake atakayefuata nasaha yako ya kuvaa Hijabu na akaongoka kupitia mkononi mwako.
Imesimuliwa ndani ya hadithi kwamba, Mwenyezi mungu alimpelekea ufunuo Nabii Musa
akamwambia; "Ewe Musa ikiwa utamrejesha mlangoni kwangu mtu amabaye ni mwenye kuniasi au ukamrejesha uwanjani kwangu mtu aliyepotea, ni bora mno jambo hilo kwako kuliko ibada ya miaka mia moja ambayo mchana utakuwa umefunga saumu na ukasimama usiku ukisali. "37 37 Biharul Anwar juz 2 uk 4.
Hapana shaka kwamba mwanamke asiyevaaa Hijabu ni muasi anayeziasi kanauni zitokazo mbinguni. Basi mtu kama huyu akirudi kwenye uwanja wa Mwenyezi Mungu kisha akashika-mana na Hijabu kutokana na juhudi zako na maelekezo yako, hapana shaka utapata malipo yaliyomo ndani ya hadithi iliyotajwa hapo juu Kwa hakika hayo ni malipo makubwa mno na ni thawabu nyingi. Hivyo basi ifanye nafsi yako iwe miongoni mwa watu wa tabligh hasa kuhusu Hijabu na elekeza tabligh yako baina ya wasichana wenzio na wanawake wenzio.
Usikatae kuolewa: Dada mpendwa endapo atakuja mtu kuku-posa, tafadhali chunguza vitu muhimu na vya msingi. Vitu hivyo ni kama vile Dini yake na tabia yake. Iwapo mtu huyu kakamilika sawasawa kwa sifa mbili hizi usibabaike baina ya kuolewa au hapana. Kwani Dini na tabia ndiyo msingi wa mafanikio ya maisha yako ya ndoa. Usichunguze shahada yake au jinsi yake (utaifa) wala usiangalie suala la mahari kwamba ni kiasi gani anachotoa. Pia nakusihi acha visingizio vya eti mpaka nikamilishe masomo yangu ili nipate shahada ya juu, na sababu zingine zisizokuwa na maana ambazo huenda zikakusababishia kuharibikiwa na Mwenyezi Mungu hatakuridhia. Mtume
anasema:
Kuolewa ni sawa na kiota cha dhahabu ambacho ukikipata utat-ulia na kustarehe ndani yake, na ukweli ulivyo kitakulinda na kuyadhibiti maumbile yako. Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanamke ili aishi maisha ya ujane na upweke, bali amemuum-ba aishi na mume bega kwa bega ili wajenge familia na jamii bora katika kuendeleza kizazi cha wanaadamu. Kwa maelezo haya elewa jambo jingine muhimu nalo ni kuwa: Kuchelewa kuolewa ni makosa na ni hatari, chukua tahadhari ya jambo hili.
"Mtume
anasema:
Baada ya Mtume kumaliza kusema maneno haya, alisimama mtu fulani akasema: 'Tumuoze nani basi?' Mtume akajibu: 'Wanaume wanaostahiki kuwaowa.' Yule mtu akauliza ni kina nani hao? Mtume akajibu;
38
Ama ikiwa mchumba atakayekuja ni muasi wa Dini yake au kuna kitu kibaya katika tabia yake, kwa mfano asiyeswali, mlevi na mengineyo, huyu mkatae wala usitishike kwa mali yake au cheo chake. Maisha ya upweke ni bora kuliko kuishi na Mume muasi wa Mungu au mwenye tabia mbaya, japo awe na mali au cheo kikubwa. Ewe dada yangu wa Ki-Islamu, muombe Mwenyezi Mungu akukadirie upate mume mwema ambaye ni muumini aliyekusanya sifa za uzuri wa sura, Dini na tabia njema, kwani Yeye Mwenyezi Mungu anasema: "Niombeni nami nitakujibuni maombi yenu." 40-60 38 Al kafi juz 5 uk 337, Biharul Anwar juz 103 uk 371.