5
VAZI LA MWANAMKE
EWE MUME MWEMA
Jukumu lako ewe mume kuhusu suala la ndoa ni muhimu sana mbele ya Mwenyezi Mungu, kwani unawajibika kutengeneza na kurekebisha mwenendo na tabia ya mkeo. Mwenyezi Mungu amekufanya uwe msimamizi wa mkeo na kion-gozi wake. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema: "Wanaume ni walinzi juu ya wanawake kwa sababu Allah amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya mali zao walizozitoa." 4:34 Na Mwenyezi Mungu anasema: "Enyi mlioamini jiokoeni nafsi zenu na watu wenu kutokana na moto ambao kuni zake ni watu na mawe" 66:6 Na ili uweze kutekeleza wajibu wako kisheria na majukumu yako ya dini kama alivyoamuru Allah s.w.t na Mtume Wake, ni lazima uambatanishe mafunzo na maelekezo ya Ki-Islamu kwa vitendo kama ifuatavyo.
Hijabu liwe ni jambo la mwanzo: Unalazimika kumuamuru mkeo avae Hijabu kama alikuwa havai, na pia umuoneshe dalili za kutosheleza na kukinaisha kuhusu Hijabu. Hii ni kwa sababu atakapovaa awe anafahamu na kuelewa umuhimu wa kanuni hii ya Ki-Islamu. Endapo utashindwa kumkinaisha kimaelezo basi fuatana naye hadi kwa Sheikh ambaye ataweza kumfahamisha kwa maelezo yatakayoonesha umuhimu wa falsafa inayopatikana katika Hijabu. Na ikiwa kuna njia nyignine ya kumfahamisha kama vile kumtafutia vitabu ajisomee yeye mwenyewe ni bora kumpa-tia.
Imam Ali
anasema kumuusia mwanawe Muhammad Al-Hanafiyya:
39
Imam Ali anamaanisha kwamba, mume asimtambulishe mkewe kwa wanaume wasiomuhusu mkewe, kwa kuwa jambo hili hus-ababisha fitna. Jambo la pili; Tahadhari na sherehe zenye mchanganyiko: Ewe mume mwema, epukana na mahafali na sherehe zenye mchanganyiko wa wanaume na wanawake. Usimpeleke mkeo sehemu hizo, muepushe mbali kabisa na mikesha ya nyimbo na magoma. Kumpeleka mkeo, katika majumba ya sinema kunachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mwenendo wa mkeo na pia hali hii itasaidia kumfanya asiwe na aibu na heshima yake ita-toweka. 39Nahjul Balaghah.
Mume anayempeleka mkewe sehemu zenye sherehe zenye mchanganyiko wa wanawake na wanaume, au anayemuingiza mkewe katika majumba ya sinema, mume huyu ni haini wa kwan-za dhidi ya mkewe. Yeye ndiye dhalimu atakayekuwa mfundisha-ji wa mwelekeo mbaya wa mkewe. Dhoruba la uovu atakalolianzisha mume huyu dhidi ya mkewe, bila shaka litaanza kumpiga yeye mwenyewe, ili ayaone matunda ya kazi yake hiyo mbaya. Dhoruba hili si jingine, bali ni pale mkewe atakapofanya hiyana ya kuanzisha uhusiano na watu wengine. Hivyo ni wajibu wako wewe mume kumuepusha mkeo kutokana na maeneo ya uovu na mengineyo machafu. Asiyakaribie maeneo hayo licha ya kwenda ili uishi kwa amani na nafsi iliyotulia.
Jambo la tatu: Usimtii mkeo: Inakulazimu uishi maisha ya muongozo wa dini ya Mwenyezi Mungu na hukumu zake na uta-hadhari na kila mwelekeo mbaya na wa kupotosha. Kwa kuwa utulivu wa nafsi yako hupatikana toka kwa mkeo, basi huenda akataka umfanyie jambo ambalo Mwenyezi Mungu kali-haramisha. Iwapo hali hii itajitokeaza kwa mkeo, jaribu kumuleza kwa upana hukmu ya Mwenyezi Mungu kuhusu ombi lake hilo ili atambue ubAya wa jambo hilo. Haifai kabisa kumtii mkeo (hata mtu mwingine) katika mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu s.w.t kwani hapana twaa ya kumtii kiumbe katika kumuasi Muumba.
Hivi sasa soma hadithi ifuatayo: Mtume
anasema;
Mtume
akaulizwa huko kumtii mke ni namna gani? Mtume akasema;
40 40Al Kafi juz 5 uk 517.
Kwa hiyo basi, usimruhusu mkeo kuhudhuria sherehe au harusi zenye mchanganyiko na usimkubalie kuvaa mavazi mepesi mbele ya wanaume wengine kwa kuwa yote haya hayamridhishi Mwenyezi Mungu. Jambo la nne: Kuwa na wivu kwa mkeo: Huna budi ewe mume kuwa na wivu kwa mkeo, kwani imekuja hadithi kutoka kwa Imam Jaafar Sadiq
kwamba;
41 Kwa ajili hiyo basi ni lazima umuhifadhi mkeo na binti zako kitabia, pia mavazi ili msijefikwa na balaa na ghadhabu za Allah (s.w.t). Amesema Imam Jaafar
kwamba;
Na amesema tena Imam Jaafar
42
Na katika kuonesha kuwa una wivu, ni kutomwacha mkeo au mmoja kati ya watu wa nyumba yako, wakiwemo mabinti zako wakatoka nje hali ya kuwa wamejitia manukato na madawa ya kujirembesha na mapambo mengine. Hapana shaka kwamba jambo hilo huwa linatishia heshima yako na yao ndani ya jamii, na matokeo ya hali hiyo ni mabaya mno.
Mtume
amesema;
41 Al Kafi cha Shaikh Al islam Al Kulaini juz 5 uk 535. 42 Al Kafi juz 5 uk 537.
Na ikiwa mke huyu atatoka nyumbani mwake hali kajipamba na kutia manukato na mumewe akawa radhi, mumewe atajengewe nyumba ndani ya moto kwa kila hatua moja atakayotembea mkewe.43 Bwana Mtume
anasema kuwa;
. Miongoni mwa hao kumi Bwana Mtume alimtaja Duyuth, na akaulizwa, ni nani huyo Duyuth? Akasema ni yule mwanaume asiyekuwa na wivu kwa mkewe.44
Imetokea zaidi ya mara moja, kwangu mimi kumuona mtu anaku-la chakula ndani ya mgahawa au hoteli hali ya kuwa na mkewe na watu wengine wakiwa wanamuangalia mtu huyo na mkewe. Cha ajabu ni kwamba bwana huyo anapokuwa katka mazingira hayo anakuwa yuko huru bila wasiwasi kabisa. Hajali kama kuna sitara yoyote au hapana, na wala hana hata habari juu ya kuwa mkewe kavaa Hijabu au hapana.
Kama ambavyo sasa hivi iko wazi kabisa kule kuwako kwa mabustani na maeneo ya matembezi yanayotembelewa na watu wengi wake kwa waume. Kwa hakika jambo hili bila kificho ni jambo baya mno linalohatarisha usalama wa jamii. Kuna Mkurugenzi wa mgahawa mmoja aliniambia kuwa; "Wako baadhi ya watu wanakataa kula chakula ndani ya vyumba maalum vilivyotengwa kwa ajili ya watu wenye familia, na wanaona ni bora wale chakula mahali pa wazi hali ya kuwa wamefuatana na familia zao!" Kama hali ni hii, uko wapi basi wivu wa wanaume kwa wake zao enyi Waislamu?
Mfundishe mkeo Surat An-nur. Inapendekezwa kwako ewe mume kumfundisha mkeo surat Annur na tafsiri yake, kwa kuwa ndani yake mna Aya nyingi zinazozungumzia mas'ala ya wan awake. 43 Biharul An war juz 103 uk 249. 44Al mawaidhatu Al adadiyyah uk223.
Aya hizo zimedhibiti mambo mengi ambayo yanamlazimu mwanamke ayafahamu ili aishi maisha bora ya Ki-Islamu na awe mbali na maovu. Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: "Wafundisheni wanawake surat An-nur kwani ndani yake mna mawaidha mengi (kwa wanawake).45 Usimuweke mkeo katika chumba cha barabarani. Bwana Mtume
amekataza kuwaweka wawnawake katika vyumba vya barabarani akasema; "Musiwaweke wanawake katika vyumba vya barabarani." Makusudio halisi ya hadithi hii ya Bwana Mtume
ni kuwaonya wanaume juu ya kuwaweka wake zao katika vyumba vinavyotazamana na barabara.
Zaidi ya hapo ni lazima tufahamu hata vyumba vinavyotazamana na masoko na maeneo mengine yenye msongamano wa watu ni hatari kuwaweka wanawake ndani ya vyumba hivyo. Imekuja katika hadithi kwamba, miongoni mwa hatua ambazo Imam Mahdi (a.s.) atazichukua katika kurekebisha hali ya Umma pindi dola yake itakaposimama, ni kuondosha madirisha yanayoelekea barabarani.46
Pengine utajiuliza kwamba ni ipi hekima ya jambo hilo? Jawabu lake ni hili lifuatalo: Hapana shaka kwamba madirisha yanay-otazama barabarani ni kichocheo kikubwa katika kuleta uharibifu ndani ya ndoa za watu na pia kuvuruga familia. Na sababu yake ni kwamba dirisha hilo huwa ni nyenzo ya kumfanya mtu aone ni kitu gani kilichomo ndani ya chumba na hasa katika majengo ya ghorofa kadhaa. Majengo haya huwa yanaonesha kila kilichomo ndani ya chumba hicho kwa wapita njia na hata watu wanaoshi mkabala na majengo hayo. 45Alkafi juz 5 uk 516. 46Biharul An waar juz 52 uk 339.
Sasa basi uharibifu wa familia na ndoa za watu unaweza kuja kutoka katika moja ya pande mbili, yaani upande wa mwanamke aliyemo ndani ya jengo hilo au yule mwanaume mpita njia. Kwa mfano mwanamke ikitokezea akachungulia njiani kwa kupitia dirishani na kwa bahati mbaya mmoja kati ya wapita njia akimuona na moyo wake ukaingia namna fulani ya kumpenda huyo mwanamke, basi hapo ndipo unapoanzia ule msiba wa maovu. Na pengine mwanaume naye anaweza kuwa amesima-ma dirishani na mara akamuona mwanamke kwenye ghorofa lililoko mkabala na na ghorofa analoishi yeye, basi kutokana na mazingira ambayo hayapingiki ni kuwa bila ya shaka mwanamke huyo atakuwa hakujisitri kwa kutambua kuwa yumo ndani mwake. Katika hali kama hii tunataraji matokeo gani baina ya wawili hawa ikiwa hawatamuogopa Mwenyezi Mungu? Hapana shaka kwam-ba Bwana Mtume
amesema kuwa:
.47
Hekima inatwambia kwamba: "Kinga ni bora kuliko tiba." Hali ina-jieleza wazi kwamba, ni mara nyingi tiba imekuwa ni jambo lisilo na mafanikio, wakati ambapo kinga imekuwa ni dhamana yenye nguvu. Kwa hakika miongoni mwa mambo yanayohuzunisha ni kuona kwamba jamii kwa jumla inaishi nje ya mafunzo haya ya Ki-Islamu yenye ulinzi madhubuti. 47Biharul An war juz 104 uk 38/ Iqabul-A'maal cha Sheikh Saduq
Utamuona mwanamke anatoka barazani hali ya kuwa kavaa nguo zinazostahili kuvaliwa ndani, kisha katika hali kama hiyo anaani-ka nguo kwenye kamba. Au utamkuta mwanamke anachungulia njiani katika hali ile ile huku akiwa amejisahau kwamba kwa kufanya hivyo anajiletea msiba na huzuni yeye binafsi na familia yake. Basi ni juu yako ewe mume mwema uzindukane na ushika-mane na mafunzo bora ya Ki-Islamu, na pia uyatumie ndani ya maisha yako ya ndoa na familia yako kwa jumla mpaka ifikie hali ya maisha yako na familia yako kuwa maisha mema yenye kuepukana na fedheha za duniani na udhalili wa huko akhera.
Mafunzo ya Ki-Islamu. Ndugu Mwislamu pokea baadhi ya mafundisho ya Ki-Islamu ambayo Mwenyezi Mungu ametuamr-isha kuyatumia katika maisha yetu ya kijamii. Mafunzo haya yanalenga kumhifadhi mtu kutokana na uovu pia kumlinda asiteleze na kuingia makosani. Kwanza: Usimuangalie mke asiyekuhusu.48 Kumtazama mwanamke asiyekuhusu ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye uharibifu wa tabia na ndiyo ufunguo wa shari na kuteleze-sha watu. Katika kumtazama mara moja hutokea ukavutika na kuongeza mtizamo wa pili, na hatimaye watatu na mwisho hus-ababisha nia mbaya katika nafsi.
Mshairi mmoja anasema: Kutazama ndiyo hatua ya mwanzo, tabasamu hufuatia, kisha salamu. Kinachofuata ni mazungum-zo, na hatimaye ahadi hufungwa na mwisho wa yote kitendo hutimia.
48Jambo hili kwa upande wa pili, haipaswi kwa mwanamke kumuangalia mwanaume asiye-muhusu. Na inaposemwa kuwa mke asiyekuhsu makusudio ni wale wanawake ambao kishe-ria unaweza kuwaoa, au kwa lugha fupi wasiyo Maharimu wako. Ili kuwafahamu zaidi unaweza kurejea Qur'an sura ya nne Aya 23 mpaka 24.
Kwa sababu kama hizi, Uislamu kwa kutaka kukata mizizi ya fiti-na umekataza jambo hili. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha kumtazama mke asiyekuhusu, na akaonya kwa onyo kali. Isitoshe Mwenyezi Mungu amewaamuru Waumini wa kiume wainamishe macho yao wasiwatazame wanawake wasiowahusu Akasema: "Waambie Waumini wanaume wainamishe (chini) macho yao na wazilinde tupu zao, kwani kufanya hivyo kuna utakaso kwa ajili yao. Na hakika Mwenyezi Mungu anafahamu wanayotenda. " 49
Hapana shaka kwamba tabia ya kibinaadamu ni tabia inay-opelekea mvuto baina ya jinsiya mbili hizi , yaani ya kiume na ile ya kike kwa sababu tu ya kila mmoja kumtazama mwenzake. Kwa hiyo basi, ni lazima tabia hii iwekewe mipaka kwa mujibu wa she-ria ya Ki-Islamu, vinginevyo matokeo ya maisha ya jamii ya wanaadamu yataingia ndani ya ufisadi na matokeo ya ufisadi huo ni mabaya. Imam Jaafar As-sadiq
amesema:
.
" Hadithi hii inatufunza kwamba, mwanzo wa uzinifu hupatikana kwa njia ya kuangalia kulikoharamishwa na sheria. Jambo hili liko wazi kwa kuwa, uzinifu haupatikani ila baada ya mwanaume kumkazia macho mwanamke, na ndiyo maana tukaambiwa ndani ya ile hadithi iliyotangulia hapo kabla kwamba: 49Qur'an 24 : 30.
50 Bila ya shaka kinachokusudiwa hapa ni kuwa: Ima muangaliaji atakuwa ni mwanaume kamuangalia mwanamke kwa kumkazia macho, au mwanamke kumuangalia mwanaume kwa kumakazia macho. Sote tunafahamu vilivyo matokeo ya hali hii na namna inavyosababisha uharibifu katika jamii. Lakini ni nani yuko tayari kuiepuka tabia hii? Hakuna ila wachache.
"Kuangalia kulikoharamishwa ni mjumbe wa uzinifu." Kwa maele-zo haya ndugu msomaji, wala hakuna haja ya kuuliza juu ya athari mbaya zinazojitokeza kutokana na uzinifu ikiwemo marad-hi mabaya yanayosababishwa na tendo hilo chafu. Isitoshe hali hiyo, bali kuna uharibifu mkubwa mno ndani ya jamii. Na kila ukichunguza utakuta kuwa uzinifu ndiyo chanzo cha misiba hii, na ambayo chimbuko lake ni kumuangalia mwanamke asiyekuhusu kwa mujibu wa sheria. Nabii Yahya ibn Zakariyya
aliulizwa kuhusu chanzo cha uzinifu akasema: "Ni kumuangalia (mwanamke asiyekuhusu) na nyimbo."
Siyo jambo la ajabu kuwa, sheria imekuja kuyakataza kwa mkazo sana mambo haya, na wala siyo jambo la kushangaza kuwa, huko akhera kutakuwa na adhabu kali na ngumu kwa watendao matendo haya. Imekuja ndani ya hadithi tukufu ya Mtume
kwamba:
51
Hadithi nyingine nayo inasema kuwa: "Yeyote mwenye kuyajaza macho yake kwa kuanglia vitu vilivyoharamishwa, Mwenyezi Mungu atayajaza macho yake siku ya kiyama kwa misumari ya moto, isipokuwa kama atatubia."52 Miongoni mwa athari za kuwaangalia wanawake wasiyokuhusu ni kujiadhibu wewe mwenyewe nafsi yako na kujisababishia mawa-zo mengi bila sababu ya msingi. Imam Ali
anasema: 51I'qabul A'maal cha As Saduq. 52Lialaail Akhbar juz 5 uk 195.
"Yeyote mwenye kuliachilia jicho lake (likawaangalia wanawake wasiomhusu) mtu huyo hujisababishia majonzi mengi."53 Na kasema tena Imam Ali
:
54 Mtu anayeishi maisha yanayoruhusu macho yake kuangalia kila anayemtaka na anachokitaka, hapana shaka kwamba mtu huyu huishi maisha yenye majonzi mengi na huiadhibu nafsi yake mwenyewe, na huwa mwenye mawazo yasiyo na kikomo. Yote haya yatampata kwa sababu moyo wake utakuwa umefung-wa kwa huyo aliyemuona na akamtamani kisha asimpate. Akili yake ataishughulisha akifikiria namna ya kumpata, na huwenda akakosa raha na hata usingizi.
Hadithi hii iliyotaja hatari za kuangalia, na kisha kumsababishia taabu na majuto mwenye tabia hiyo, inahusisha mambo mengi ambayo haipaswi kuyaangalia, lakini moja wapo na muhimu ni hili la kuwaangalia wanawake wasiokuhusu, bali tunaweza kusema kuwa hilo ndilo makusudio. Na kwa ajili hiyo basi Imam Jaafar
akibainisha hatari za kumuangalia mwanamke asiyekuhusu anasema: "Kumtazama mwanamke asiyekuhusu ni mshale wenye sumu miongoni mwa mishale ya iblisi, na ni mara nyingi kumtazama mwanamke asiyekuhsu limekuwa ni jambo lenye kuleta majuto ya muda mrefu.55" 55Kitabu Al Kafi juz 8 Khutbatul Wasilah.
56 Kitabu Jamiul Akhbar uk 93. Tabia ya kumuangalia kila mwanamke apitaye au umuonaye kwanza: Ni tabia mbaya mno, na hapana shaka sote tunakubaliana kwamba mtu mwenye tabia hii huwa na majuto kila wakati kwa sababu hutamani kila akionacho na kwa hakika siyo rahisi kukipata kila anachokitamani. Kutokana na kutokuwepo uwezekano wa kupata kila ana-chokitamani, matokeo yake mtu huyo hubakia kuwa ni mwenye majuto na majonzi yasiyok-wisha. Ni kwa nini hasa mtu ajiadhibu kiasi hiki wakati Mwenyezi Mungu ametupatia fursa ya kuoa mke zaidi ya mmoja? Siyo siri kwamba wanawake ni wengi mno kuliko idadi ya wanaume. Kwa hiyo oa badala ya kubakia unajiadhibu hapa duniani kwa majuto yasiyok-wisha na kesho akhera unasubiriwa na adhabu kali kutokana na wewe kuyajaza macho yako kwa misumari ya motoni. Mtarjumi 57Biharul Anwar juz 104 uk 40.
Ewe ndugu yangu bila shaka unafahamu jinsi mshale unavy-oweza kuingia mwilini na kupasua mishipa iliyoko mwilini. Hebu fikiria namna mshale usiokuwa na sumu unavyoweza kuleta mad-hara pindi uingiapo mwilini, sasa je itakuwaje hali ya mshale wenye sumu ukiingia mwilini? Bila shaka madhara yake ni makubwa zaidi ambayo yanaweza kupelekea mauaji kwa mtu. Hali ni kama hiyo kwa mtu mwenye tabia ya kuangalia wanawake wasiomhusu, kwani kuangalia huko ni sawa na mshale wenye sumu, mshale huo hujitengenezea njia mpaka ndani ya moyo ili kumnyima mtu huyo raha na utulivu na kumuachia majuto ya muda mrefu. Ewe ndugu yangu mpendwa! Ili uweze kujitakasa na kuwa mbali na mawindo ya shetani, napenda kukufahamisha pia kwamba Uislamu unachukizwa na tabia ya kuwaangalia wanawake.
Mimi naamini kwama kuna baadhi ya watu wasiofuata mafundisho ya dini wanapokutana na wanawake, wakishakupishana nao basi huwaangalia nyuma hali ya kuwa wanatizama kwa mtazamo wa kutaka kufahamu namna wanawake hao walivyo au wanavyotembea, pia maumbo yao. Kwa hakika hii ni tabia mbaya mno haifai kabisa. Inasimuliwa kwamba Abu Basir alimuuliza Imam Jaafar
.57 56Lialil Akhbar juz 5 uk 196. 57Qur'an 28: 26.
Nabii Shuaibu alipoyasikia maneno ya Binti yake alimuuliza akasema: "Huyu Musa ni mwenye nguvu na hii ni kwa sababu umemuona akilinyanyua jiwe kwenye kisima, sasa je, huu uamini-fu wake umeufahamu vipi?" Yule Binti akajibu kwa kusema: "Ewe Baba mimi nilikuwa natembea mbele yake, mara Musa akani-ambia, tembea nyuma yangu na iwapo nitapotea njia basi wewe utanielekeza, kwani sisi ni watu tusiyowaangalia wanawake kwa nyuma.58
Katika tafsiri ya neno la Mwenyezi Mungu lisemalo kuwa:
Imamu Muhammad Al Baqir
anasema: "Kijana mmoja wa Kiansari alikutana na mwanamke fulani katika vichochoro ya mji wa Madina, na huyu kijana akamkazia macho yule mwanamke. Walipopishana kijana huyu akageuza shingo yake na akaende-lea kumuangalia yule mwanamke huku anakwenda hali ya kuwa kageuza shingo yake akimuangalia. Basi ghafla alijikuta ame-jigonga ukutani na damu zikaanza kumchuruzika. Kijana yule kuona hivyo akasema: Ni lazima niende kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikamueleze juu ya kisa hiki. Kijana yule alipofika mbele ya Mtume
hali damu zikiendelea kumto-ka, Mtume alimuuliza umepatwa na nini? Yule kijana akasimulia yaliyomfika, na mara Malaika Jibril
alishuka akiwa na Aya inayowaamuru Waumini wanaume wainamishe macho yao."59 Kipo kisa kingine kinasimuliwa kuhusu hali kama hizi na kinase-ma kuwa: "Kuna mtu mmoja ambaye kazi yake ilikuwa kuteka maji na kupeleka ndani ya nyumba ya Sonara fulani kwa muda wa miaka thelathini. 60Lialil Akhbar juz 5 uk 196. 61Al Kafi juz 5 uk 521.
Bila shaka kuna wakati yule hakuwako nyumbani kwa mke wa sonara alikuwa akija kumfungulia mlango yule mchota maji ili apate kumimina maji mahala panapostahili. Kipindi chote hiki yule mchota maji hakuwahi kufanya hiyana yoyote dhidi ya mke wa sonara japo kumuangalia kwa jicho la hiyana. Siku moja wakati yule mama anamfumngulia mlango yule mchota maji, mara ghafla aliunyoosha mkono wake na kumvuta yule mama na akambusu!! Kwa bahati nzuri mwanamke huyu aliuvuta mkono wake kwa nguvu kisha akapiga makelele na hapo hapo akamfukuza yule mchota maji kutoka mule ndani.
Baadaye huyu mama alianza kufikiria huku akishangazwa na hali ile iliyojitokeza. Imekuwaje mchota maji yule kufanya hiyana ile baada ya kuwa muaminifu kwa muda wa miaka thelathini?!! Mumewe aliporudi nyumbani mkewe akamuuliza: 'Je leo kuna jambo gani limetokea huko dukani kwako?' Yule mume akajibu kwa kusema: 'Leo kuna mwanamke alikuja dukani kwangu kununua bangili, basi nilipom-funua mikono yake ili apate kuvaa bangili zile, nilimshika mkono wake kisha nikambusu.'!! Basi pale pale mkewe alipiga makelele akasema: 'Allahu Akbaru!' 60 Baada ya hapo alimsimulia mumewe mambo yaliyotendwa na yule mchota maji."61
Naam chochote atakachokifanya mtu kuwafanyia wenziwe na wake wa wenzake, basi na yeye yatamfika hivyo kwa mkewe, mama yake, dada yake na binti yake. Ndani ya hadithul Qudsi inasemwa kuwa: "Vile uwatendeavyo wenzako, basi na wewe utatendewa hivyo hivyo." Maana yake ni kwamba: Iwapo utawatendea wema wenzako basi na wewe utatendewa wema, na iwapo wewe utawatendea ubaya wenzako fahamu wazi kuwa na wewe utatendewa ubaya. " Maana yake: Mungu ni Mkubwa. Tamko hili licha ya kuwa ni utajo wa Mwenyezi Mungu, pia hutumika kama tamko la kuonesha mshangao au kustushwa na kitu fulani kilichotokea bila kutarajia. 61Lialil Akhbar juz 5..
Ewe msomaji mpendwa: Narudia tena kuzungumzia suala la kumuangalia mwanamke asiyekuhusu na ninasema; Hapana shaka kwamba Uislamu ni dini yenye mafunzo yanayokuhama-sisha kutenda mema, na wakati huo huo inayo mafunzo ya kukuonya usiyaendee maovu. Ndiyo maana utaiona Qur'an Tukufu pindi Mwenyezi Mungu anapoitaja pepo na neema zake, hapo hapo hufuatisha kuelezea habari za moto na adhabu zake. Yote haya lengo lake ni kumfanya mtu awe katika mazingira ya kutumainia neema na thawabu, na pia awe na khofu ya moto na adhabu kwa upande wa pili. Hivi punde tu umesoma baadhi ya hadithi tukufu zilizosimulia kuhusu adhabu za kumuangalia mwanamke asiyekuhusu na pia matokeo mabaya yanayoletwa na tabia hiyo mbaya.
Hivi sasa umefika wakati wa kuzungumzia hadithi zinazoelezea malipo mema aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya wale watakaojiepusha na mambo ya haramu. Kadhalika hadithi hizo zitaelezea athari njema zinazopatikana kutokana na tabia njema za kujiepusha na mambo aliyoyakataza Mwenyezi Mungu. Bwana Mtume (s.a.w).w anasema: "Kuyatazama mapambo ya wanawake wasiokuhusu ni mshale miongoni mwa mishale ya ibilisi iliyo na sumu, atakayeliacha jambo hilo kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu (s.w.t) basi Mwenyezi Mungu atamuonjesha ladha ya ibada itakayomfurahisha.62
"Katika hadithi nyingine Mtume
anasema;
"63 62 Mustadrak Al wasail juz 2 uk 554. 63 Biharul An waar juz 104 uk 42.
Bwana Mtume anaendelea kutufunza anasema kwamba: "Yainamisheni macho yenu, kwa kufanya hivyo mtaona maajabu (makubwa).64 Hapana shaka kwamba Mwenyezi Mungu humfunika mtu huyo kwa wingi wa baraka kutokana na kitendo chake cha kuinamisha macho na kutowaangalia wanawake wasiomhusu. Imam Ja'far Sadiq
anasema:
65 Anasema tena Imam Ja'far
:
66Sasa hivi kumebakia kitu cha mwisho ambacho ni:
Je! Ni namna gani basi mtu anaweza kuepukana na jambo hili la haramu, wakati sote tunafahamu kwamba, gonjwa hili la kansa ya wanawake kuvaa nusu Hijabu na kutokujisitiri kwa mujibu wa she-ria limeenea? Na kwa bahati mbaya sana hata katika nchi zetu za Ki-Islamu gonjwa hili limo. Hivi kweli kwa hali tuliyonayo mtu anaweza tena kuinamisha macho yake na ni vipi ataiona njia? Jawabu la suali hili ni kama ifuatavyo: Sina shaka umesoma baadhi ya Aya na hadithi tulizozitaja. Kinachotakiwa ni kuinamisha macho siyo kuyafumba, na hii ndiyo maana iliyokusudiwa, yaani uangalie chini. 64Biharul An waar juz 104 uk 30 65Safinatul Bihari juz 2. 66Biharul Anwaar juz 104 uk 41
Anachopswa mtu kukifanya wakati anapomuona mwanamke asiyemhusu, haraka sana ateremshe macho yake chini au aan-galie upande mwingine. Kwa hakika Mwenyezi Mungu hawezi kupoteza malipo yake. Usimpe mkono mwanamke asiyekuhusu: Ndugu Mwislamu, Mwenyezi Mungu ameharamisha kumpa mkono mwanamke asiyekuhusu. Mtume Muhammad
amesema:
67
Usimtanie mwanamke asiyekuwa mkeo: Miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu amekukataza na kukuharamishia ewe ndugu Mwislamu, ni kufanya utani na mwanamke asiyekuhusu kisheria, kwani jambo hili mara nyingi hukaribisha uovu na pia husaidia kwa kiasi kikubwa kuamsha hisia za maumbile zilizokuwa zimejificha katika pande mbili hizi. Bwana Mtume
anasema:
67 Biharul Anwaar juz 103.
Kwa hakika Mwenyezi Mungu amemuumba mtu na akamuwekea matamanio ya kijinsiya, na akayafanya kuwa ndiyo matamanio yenye nguvu kuliko mengine yote. Kwa matamanio hayo Mwenyezi Mungu akafanya kuwa ndiyo njia ya kukidumisha kizazi cha wanaadamu, na akafanya kuoa ndiyo njia ya pekee kuy-atosheleza matamanio haya. Kwa hiyo kuoa ndiyo njia nzuri na tukufu na ndiyo ufumbuzi wa pekee uliopo kisheria kuhusu tatizo hili la kijinsiya.
Ukweli ulivyo ni kwamba, kuchelewa kuoa kunamfanya mtu akumbwe na mambo mawili. Kwanza: Katika kushindana na matamanio yake kutamfanya aiumize nafsi yake na kupata taabu kubwa ya kuvumilia katika muda huo. Pili: Huenda hatimaye akaingia katika haramu ikiwa ni pamoja na njia isiyo ya kawaida katika kuyatosheleza matamanio yake, au akajikuta anafanya mambo machafu zaidi ambayo ni kinyume na maumbile. Au huenda akafanya uzinifu na matokeo yake ni kuvunja heshima yake au heshima za watu wengine. Na kutokana na hali halisi ilivyo, kila jambo moja katika hayo lina hatari kubwa kwa mtu yeye mwenyewe na heshima yake na utu wake. Kwani kuzuia matamanio na kuyadhibiti kunasababisha kuiadhibu roho na matokeo yake huleta athari mbaya mwilini na hasa katika akili.
Hali hii husababisha kuingia katika dhambi na hatimaye mtu ndipo hujikuta akifanya ambalo hakulitarajia, hapo utu wake huporomoka na mwisho hupata akahukumiwa kwa kosa la jinai na kuingia gerezani na kuishi humo sawa na wezi na wanyang'anyi.
BASI NINI UFUMBUZI WA TATIZO HILI?
Ufumbuzi wa tatizo hili ni kuoa, kitu ambacho Uislamu unakitan-guliza mbele na hata akili inakubaliana kabisa na ukweli huu, kwa kuwa kuoa ndiyo dawa pekee ya kutibu maumbile haya. Kuoa kunatimiza furaha ya kiroho kwa mtu na kuiliwaza nafsi na kuya-pamba mazingira na tabia ya mtu. Kwa jumla ladha ya maisha na starehe vimo ndani ya ndoa, na kwa upande mwingine kuoa kunazuia mtu kuyaingia maovu na madhambi. Zaidi ya hapo ni kwamba, Mwenyezi Mungu hakumuumba mtu ili aishi maisha ya ujane na upweke, bali amemuumba aishi na mkewe aliye Muumini bega kwa bega ili wajenge familia na jamii bora hasa katika malezi ya watoto. Kwa hakika ujane ni miongoni mwa mambo yanayomchukiza Mwenyezi Mungu, pia Uislamu unapin-ga kwa nguvu zake zote jambo hili na hata Mawalii wa Mwenyezi Mungu wanachukizwa na ujane. Bwana Mtume (s.a.w.w) anase-ma: "Waovu miongoni mwenu ni wajane, (wasiyooa au kuolewe) nao ni ndugu wa shetani."68 Na akasema tena: "Watu wengi wa motoni ni wale wajane ( wasiyooa au kuolewa)."69
Imesimuliwa kutoka kwa al-Ukaaf al-hilali anasema: "Nilikwenda kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akaniambia 'ewe U'kaafu unaye mke?' Nikamwambia, Hapana sina mke. Mtume akaniambia: 'Je unaye mjakazi?' Nikasema: Hapana sina. Bwana Mtume akasema: 'Je wewe ni mzima na mwenye uwezo (yaani unao uwezo wa mali na unalimudu tendo la ndoa)? 68Mustadrak al Wasail Kitabun Nikah.. 69Wasailus Shia juz 7 uk 8.
'Nikamjibu: Ndiyo tena namshukuru Mwenyezi Mungu. Bwana, Mtume akasema: 'Ikiwa unayamudu hayo na hujaowa, basi kwa kweli wewe ni miongoni mwa ndugu wa mashetani, au basi utakuwa miongoni mwa mapadri wa ki-Kristo na kama si hivyo, fanya kama wanavyofanya Waislamu kwani miongoni mwa mi la zetu ni kuowa.' Mtume aliendelea kunionya na kusisitiza suala la kuowa mpaka akafikia hatua ya kuniambia: 'Ole wako ewe U'kaafu, owa hakika wewe ni miongoni mwa waovu ( ikiwa hukuowa).' Nikamwambia Bwana Mtume: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu niozeshe kabla sijaondoka ha pa." Bwana Mtume akamuozesha Bwana huyo kabla hajaondoka.70
Na katika kulitilia mkazo suala la kuoa na kuhimiza watu waowe, Bwana Mtume
anasema:
Na akasema tena: "Kijana yeyote anayeowa katika umri wake wa mwanzo katika ujana, shetani huchukia na kusema; Lo nimepata hasara theluthi mbili za dini yake kijana huyu amezikinga kutokana na uovu wangu." Kisha Mtume akamuusia kijana wa aina hii akasema: Na amuogope Mola wake kijana huyu katika theluthi iliyobaki."71
Makusudio ya maelezo haya ni kuonesha kwamba kuoa kunahi-fadhi theluthi mbili ya dini, kwa hiyo mtu anatakiwa awe mchamungu katika theluthi iliyobakia. Na kama hali ni hii, umuhimu wa kuoa katika maisha ya mtu ni jambo ambalo linayo nafasi ya pekee na tukufu, na pia mwanaadamu anatakiwa ali-patie nafasi kubwa ya kulitekeleza katika mipango yake. 70Mustadrak al Wasail Kitabun Nikah. 71Mustadrak al Wasail Kitabun Nikah.
Tukamilishe mazungumzo juu ya kuowa kwa hadithi ya Mtume
inayosema kuwa:
"72
MAKAZI YA MWANAMKE ASIYEJISITIRI
Ni yapi makazi ya mwanamke asiyevaa Hijabu wala hajisitiri KiIslamu huko akhera? Sote tunafahamu kwamba, Mwenyezi Mungu ameweka adhabu kali kwa wale wanaokiuka maamrisho yake na wanaamua kuyain-gia mambo ya haramu. Je ni adhabu gani atakayoadhibiwa mwanamke asiyejisitiri kwa vazi la Ki-Islamu na akaona ni bora kuutembeza mwili wake wazi kinyume na sheria inavyomtaka avae? Jawabu lake ni kama ifuatavyo: Kwa mwanamke asiyejsi-tiri hujisababishia laana na kujiweka mbali na rehma na radhi za Muumba wake. Pia hujiingiza mwenyewe katika unyonge na adhabu za Mwenyezi Mungu. Bwana Mtume (s.a.w.w) anasema: "Katika zama za mwisho watakuja watu katika umati wangu ambao wanawake zao nusu wamevaa na nusu wako uchi. vich-wani watasuka mafundo ya nywele na kuyaacha wazi bila kuya-funika.
Basi sikilizeni (niwaambieni) kuweni wenye kuwalaani wanawake hao kwa kuwa wamekwisha kulaaniwa, wala hawataipata harufu ya pepo na iko mbali nao kwa masafa ya mwendo wa miaka mitano."73 Naye Imam Ali
amesema:
. 72 Wasailus Shia juz 7 uk 6. 73 Musnad Ahmad, Hayatul Hayawan cha Ad Dumair.
Wanawake wa aina hii watakuwa wametoka katika dini na watain-gia katika fitna, watapenda starehe na mambo ya fahari na wata-halalisha mambo ya haramu. Wanawake hawa malipo yao ni kuingia motoni, basi angalieni sana kipindi hicho ni kibaya kuliko vyote." Kuna hadithi nyingine kutoka kwa Bwana Mtume
inay-oelezea adhabu za wanawake wasiojisitiri kwa mujibu wa sheria ya Ki-Islamu. Hadithi hii tunainakili kwa kifupi. Imam Ali
anasema: "Mimi na Fatma
tuliingia nyumbani kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu tukamkuta analia sana. Nikamwambia ni kitu gani kinakuliza? Mtume akasema: 'Ewe Ali, usiku niliopelek-wa mbinguni niliwaona wanawake katika umati wangu wakiad-hibiwa vikali.
Nilihuzunishwa na hali yao hiyo na nikalia kutokana na adhabu kali wanayoadhibiwa.' Kisha Bwana Mtume
akaanza kueleza aliyoyaona katika usiku huo wa Miraji akasema: 'Nilimuona mwanamke amefungwa kwa nywele zake kwenye moto na ubongo wake unatokota. Na nikamuona mwanamke mwingine amening'inizwa kwa ulimi wake huku moto ukimiminwa kooni mwake. Pia nikamuona mwanamke anakula nyama ya mwili wake hali yakuwa chini yake panawaka moto mkali, na mwingine amefungwa mikono yake na miguu kwa pamoja, kisha amezungukwa na mojoka mengi na nge wanamuuma. Pia nilimuona mwanamke kiziwi tena kipofu halafu hawezi kusema akiwa ndani ya moto ubongo wake unavuja kupitia puani, mwili umeenea vidonda mithili ya mgonjwa wa ukoma. Na kuna mwanamke mwingine anakatwa nyama za mwili wake kwa mikasi.
Bibi Fatma
akasema kumwambia baba yake: 'Baba hebu nifahamishe ni matendo gani waliyoyatenda wanawake hao hapa duniyani?' Mtume
akajibu:
.
Na yule mwanamke aliyefungwa mikono na miguu kwa pamoja na akawa anaumwa na majoka na nge, huyu alikuwa mchafu hana udhu nguo zake chafu na alikuwa hakogi janaba wala hedhi na alikuwa akipuuza kuswali. Ama yule kipofu, kiziwi na hawezi kusema alikuwa akizaa watoto wa zinaa ( nje ya ndoa) na kisha humpachikia mumewe na kudai kwamba ni watoto wa mumewe. Na huyu wa mwisho ambaye alikuwa akikatwa nyama za mwili wake kwa mikasi, alikuwa Malaya, akiitoa nafsi yake kwa kila mwanaume."74
Kwa hiyo imetudhihirikia wazi katika hadithi hii aina mbali mbali za mateso na adhabu alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa wanawake wasiozingatia kanuni ya Hijabu kwa maana zake zote. Miongoni mwa adhabu hizo ni kufungwa kwa nywele zake nwanamke na kutokota ubongo baada ya kupata adhabu ya moto unaowaka pande zake zote. Kwa hivyo basi, ina maana kila mwanamke atakayeshindwa kusitiri mwili wake na akauacha wazi kwa kila mtu, hapana budi ataadhibiwa kwa adhabu kali inay-oumiza, kama zilizotajwa ndani ya hadithi.
Lakini ikiwa mwanamke mwenye sifa hizi zilizotajwa katika hadithi atatubia kwa Mwenyezi Mungu na kuacha kabisa makosa hayo aliyokuwa akiyatenda, kisha akavaa kama sheria ya KiIslamu inavyomtaka avae kwa ukamilifu, bila shaka Mwenyezi Mungu atakubali toba yake na atamsamehe. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:"Ni yeye Mwenyezi Mungu ambaye anakubali toba za waja wake (wanapotubia) na anasamehe makosa na anafahamu mnayoyatenda"75 Na anasema tena Mwenyezi 74 Biharul Anwaar juz 103 uk 245 75 Qur'an 42: 25.
Mungu (s.w.t.): "Nami kwa hakika ni mwingi wa kusamehe kwa yule anayetubia na akaamini na kutenda mema kisha akaoongo-ka"76 Hijabu Isiyokamilika: Kuna baadhi ya dada zetu ambao utwaona wamavaa Hijabu, lakini Hijabu yao hiyo siyo kamilifu kwa mujibu wa sheria ya Ki-Islamu. Kina dada hao utawaona wamejistiri sehemu fulani tu ya kichwa, na au sehemu fulani ya mwili na hala-fu sehemu nyingine za mwili ziko wazi mbele ya kila mtu. Wakati mwingine wanaweza kujisitiri vizuri kichwa chote, lakini utaona mikono au miundi iko wazi au ikawa haikusitiriwa ipasavyo.
Kwa hakika Hijabu kama hi moja kwa moja ni Hijabu isiyokamilika ni Hijabu pungufu isiyoweza kutimiza lengo la Hijabu linalokusudiwa. Wakati huo huo, uvaaji kama huo si uvaaji ulioko juu ya msingi wa kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Hali kama hii ya uvaaji usiokamili iliwahi kutokea katika zama za Bwana Mtume
, ambapo walikuwako wanawake ambao hujistiri sehemu ya kichwa na kuacha sehemu nyingine bila kuisi-tiri ikiwa ni pamoja na masikio.
Tendo kama hili Mtume
alilikemea na akawaamuru wanawake wajisitiri kikamilifu kwa mujibu wa sheria. Kumbuka ndugu msomaji ile hadithi ya Mtume aliposema: "Nusu wamevaa na nusu wako uchi." Hadithi hii ina-maanisha kwamba, wanawake watakuwa wanajisitri sehemu ya maungo yao na sehemu nyingine hawajisitiri. Kama hali ndiyo hii tuliyonayo, lengo la Mtume
ni kuwafahamisha wanawake wanaovaa hivyo kwamba wasidhani kuwa wamevaa Hijabu, bali inawapasa watambue kwamba uvaaji huo siyo kamili na haukubaliki kisheria. 76Qur'an 20:82
NENO LA MWISHO
Wasomaji wapendwa imetudhihirikia katika yale tuliyoyataja ndani ya kitabu hiki kwamba, Hijabu ni vazi la Ki-Islamu na siyo fashion,77 na ni kanuni iliyojaa hekima nyingi. Hijabu inalinda heshi-ma ya mwanamke na inaitakasa familia na jamii nzima. Zaidi ya hapo ni amri ya kidini na hukumu ya sheria za Ki-Islamu, Mwenyezi Mungu ameithibitisha na kuitaja ndani ya Qur'an Tukufu. Naye Bwana Mtume
na watu wa nyumba yake wamesisitiza na kuitilia mkazo sheria hii. Kinyume cha maagizo haya na faida zilizomo ndani ya Hijabu, tayari tumekwishakuona wazi kwamba jamii huwa inaharibika na mwanamke kuangamia na ndipo familia inapotengana.
Zaidi ya hapo kutokuchunga mipaka ya mavazi, hasa Hijabu kwa wanawake ni uasi wa amri ya Mwenyezi Mungu, na maamuzi yake pia ni kinyume na maslahi ya wengi. Kwa hiyo ni wajibu wetu sote kufanya kila linalowezekana ili kuona sheria hii inafanya kazi na kuieneza baina ya wanawake waliomo katika jamii zetu, majumbani, mashuleni, maofisini na kila mahali. Kwa kufanya hivyo, tutapata radhi za Mwenyezi Mungu, pia huu utakuwa ni wema kwa ajili ya nafsi zetu hapa duniani na kesho akhera.
'7Fashion/Mtindo: Kwa kawaida mtindo ni kitu ambacho hupita na kuja kingine badala yake, lakini siyo Hijabu, kwani yenyewe ni vazi la mwanamke kisheria na anapaswa kulivaa wakati wote anapokuwa ndani ya mazingira husika kama ilivyokwisha kuelezwa kitabuni. Mtarjumi.
HABARI MOTOMOTO
AL- AZHAR YASEMA: WANAWAKE WA KI-ISLAMU WALIOKO UFARANSA WANAWEZA KUVUA HIJAB KAMA WAKILAZIMISHWA
1.
Cairo, Desemba 30, 2003 (IslamOnline, net): Imamu Mkuu wa Al-Azhar Sheikh Mohammad Sayed Tantawi siku ya jumanne, Desemba 30, 2003 alisema kwamba: Wanawake wa ki-Islamu wanaoishi Ufaransa wanaweza kuvua Hijab zao kama wakilazimishwa kwa shida, alikuwa akirejea kusudio la sheria ya kupiga marufuku Hijab katika shule za serikali. Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy (aliyekuwa anaizuru Misir), Tantawi alisisitiza kwamba Hijab "ni sharti la ki-Mungu kwa mwanamke wa ki-lslamu... Hakuna Mwislamu yey-ote, awe yeye ni mtawala au mtawaliwa, awezaye kulipinga hilo."
Lakini alihoji kwamba Ufaransa wana haki ya kupiga marufuku Hijab katika shule za serikali, akaongeza kwamba chombo cho-chote cha ki-Islamu au nchi ya ki-Islamu haina haki ya kulipinga hilo, kwa sababu Ufaransa sio nchi ya ki-Islamu. "Hijab ni wajibu kama mwanamke anayeishi katika nchi ya ki-Islamu. Kama anaishi katika nchi isiyo ya ki-Islamu, kama Ufaransa, ambayo watawala wake wanataka kufuata sheria inay-opinga Hijab, ni haki yao," alisema Imamu mkuu huyu wa Al-Azhar, mwachuoni aliyeteuliwa na serikali.
Alisema kwamba iwapo mwanamke wa ki-Islamu atafuata sheria za nchi isiyo ya ki-Islamu (kwa kuvua Hijab yake), basi Uislamu humchukulia kama aliyelazimishwa kwa shida. Sheikh Tantawi alitetea maoni yake hayo kwa kusoma Aya Tukufu, ambayo inasema: "Mmeharamishwa (kula) nyama mfu na damu na nyama ya ngu- ruwe, na kilichosomewa jina lisilo la Mwenyezi Mungu...Lakini mwenye kusongeka kwa njaa, pasipo kuelekea kwenye dhambi, wala kupituka mipaka - basi Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe mwenye kurehemu."
"Nasisitiza na kukazia: Ni haki yao na siwezi kuipinga... sisi, kama nchi ya ki-Islamu, hatuwezi kumruhusu mtu yeyote kuingilia katika mambo yetu ya ndani," alisema akisherehesha juu ya upi-gaji marufuku wa Ufaransa ulio na majadala. "Mimi mwenyewe, katika wadhifa wangu kama Imamu Mkuu wa Al-Azhar, siwaruhusu watu wasio Waislamu kuingilia katika mambo yetu ya ndani, na kwa mantiki hiyo hiyo, siwezi nikaruhusu nafsi yangu kuingilia katika mambo ya ndani ya nchi isiyo ya ki-Islamu," aliongeza Sheikh Tantawi.
Rais wa Ufaransa Jacques Chirac siku ya jumatano, 17 Desemba, 2003 aliunga mkono kusudio juu ya utungaji mpya wa sheria ya kupiga marufuku uvaaji wa Hijab katika shule za serikali. Waziri wa sheria wa zamani wa Ufaransa, Bernard Stasi, ambaye aliongoza kamati ya serikali juu ya mazingira ya kilimwengu na dini, alipendekeza mapema katika mwezi huo kuwekwa sheria ya kupiga marufuku Hijab, misalaba mikubwa na vikofia vya ki-Yahudi. Hatua hiyo iliyopendekezwa, imepangwa kuwakilishwa mbele ya Bunge la Ufaransa mwezi Februari 2004, na inatarajiwa kuanza kutumika katika mwezi wa Septemba 2004.
{Kwa mujibu wa fatwa za wanachuoni wengi pamoja na Mkuu wa Mamlaka kubwa ya ulimwengu wa Waislamu-Mashi'a, Ayatollah Mkuu Sayyid Seestani (HA); hairuhusiwi kwa msichana wa ki-Islamu kuvua Hijab yake Shuleni, na kama akilazimishwa kuvua, basi asihudhurie Shuleni hapo.]78
KUJIFUNIKA KICHWA NA UHURU WA DINI
2.
Nchi kadhaa za Ulaya zinachochea sheria za kupiga marufuku au kuzuia uvaaji wa mitandio ya kichwa kwa wanawake wa ki-Islamu. Sheria hizo huzua maswali kwenye misingi ya kuvumiliana na usawa katika jamii ambayo hupigania mfumo wa kutambua mawazo, misimamo mbali mbali na uhuru wa dini.
Hivi sasa Ufaransa inafikiria kupiga marufuku uvaaji wa Hijab (shela) mashuleni, wakati ambapo katika nchi ya Ujerumani, majimbo mawili yamependekeza itungwe sheria ambayo itapiga marufuku moja kwa moja uvaaji wa ushungi (Hijab) katika taasisi za elimu.
Makala hii inazungumzia suala la Hijab, adabu ya kufunika kichwa kwa wanawake wa ki-Islamu, na vile vile na desituri za Wayahudi na Wakristo za uvaaji wa shela na ushungi. Hijab na shela? Baadhi ya watu katika nchi za mahgaribi (yaani, Ulaya na Amerika) hufikiria adabu ya kufunika kichwa inayofuatwa na wanawake wa ki-Islamu kama alama kubwa ya ukandamizaji wa wanawake na utumwa. Je, ni kweli kwamba hakuna desturi zina-zo fanana katika mila za Mayahudi-Wakristo? 78Msimamo unaopaswa kuoneshwa na Waislamu ndiyo huu. Hatuko tayari kumfurahisha Jacques Chirac wa Ufaransa na wakati huo huo tumchukize Mwenyezi Mungu.
Hebu ngoja tuiweke rikodi hii sawasawa. Kwa mujibu wa Rabbi Dr. Menachem M. Brayer (Profesa wa Biblical Literature, Yeshiva University) katika kitabu chake, 'The Jewish woman in Rabbinic Literature,' ilikuwa ni desturi ya wanawake wa ki-Yahudi kutoka nje wakiwa na shungi (nguo ilyofunika kichwa), ambayo wakati mwingine, hufunika hata uso wote na kuachilia jicho moja tu nje.79 Anawanukuu baadhi ya Marabbi wa zamani wakisema, "Haifanani kwa mabinti wa Israeli kutembea bila kufunika vichwa" na "Laana iwe juu ya mwanaume ambaye anaruhusu nywele za mkewe zionekane...mwanamke ambaye anaonesha nywele zake kwa ajili ya kujirembesha huleta ufukara."sheria za ki-Yahudi hukataza usomaji wa dua za kuomba baraka au maombi (yoyote) mbele ya mwanamke aliyeolewa akiwa kichwa wazi, kwa vile kutokufunikwa kwa nywele za mwanamke huchukuliwa kama 'uchi'.80
Dr. Brayer vile vile anataja kwamba ,"wakati wa kipindi cha utawala wa Marabi (wanachuoni wa dini ya ki-Yahudi) kushindwa kwa mwanamke wa ki-Yahudi kufunika kichwa kulichukuliwa kama tusi kwa heshima yake. Akiwa hakufunika kichwa chake anaweza kupigwa faini ya zuzim mia nne kwa kosa hili." Dr. Brayer vile vile anaelezea kwamba shela ya mwanamke wa ki-Yahudi haikuchukuliwa wakati wote kama alama ya adabu. Wakati mwingine, shela huashiria hali ya ubora na anasa kuliko adabu. Shela huupa utu heshima na ubora wa wanawake watuku-fu. Vile vile huwakilisha kutokuwezekana njia yeyote ya kumuen-dea mwanamke kama miliki ya mume iliyotakaswa. 81 ' Menavhem M. Brayer, Mwanamke wa ki-Yahudi katika fasihi ya ki-Rabbi: A Psychosocial Perspective ( Hoboken, n.J: Ktav Publishing House, 1986) uk. 239 80 Ibid., uk. 316-317. vile vile tazama Swidler, op. cit., uk. 121-123. 81 Ibid., uk. 139
Shela huonesha kujiheshimu kwa mwanamke na hadhi ya kijamii katika jamii. Wanawake wa daraja za chini mara kwa mara huvaa shela ili kutoa picha ya daraja la juu. Ukweli kwamba shela ilikuwa ni alama ya utukufu, ilikuwa ndio sababu ya makahaba kutoku-ruhusiwa kufunika nywele zao katika jamii ya ki-Yahudi ya zamani. Hata hivyo, makahaba mara kwa mara walivaa mitandio maalum ili waonekane wa heshima.82 Wanawake wa ki-Yahudi huko Ulaya waliendelea kuvaa shela mpaka karne ya kumi na tisa wakati maisha yao yalipokuwa yameingiliana zaidi na utamaduni wa kisekula ulioyazunguka. Shinikizo la nje la maisha ya Kizungu katika karne ya kumi na tisa liliwalazimisha wengi wao kutoka nje vichwa wazi. Baadhi ya wanawake wa ki-Yahudi waliona inafaa zaidi kubadilisha shela yao ya asili kwa kuvaa wigi (nywele za bandia) kama muundo mwingine wa kufunika nywele. Leo, wanawake wachamungu zaidi wa ki-Yahudi hawafuniki nywele zao isipokuwa katika Hekalu.83 baadhi yao, kama vile madhehe-bu za Hasidic bado wanaendelea kutumia wigi. 84
Vipi kuhusu mila ya Ukristo? Inajulikana sana kwamba watawa wa Kanisa Katoliki wamekuwa wakifunika vichwa vyao kwa mamia ya miaka sasa, lakini hiyo sio mwisho. Mt. Paulo katika agano jipya ameandika maelezo ya kuvutia sana kuhusu shela: Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanaume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanaume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. Kila mwanamume asalipo, au anapohutubu, naye amefu-nika kichwa yuaabisha kichwa chake. Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaabisha kichwa chake; kwa maana ni sawa sawa na yule asiye nyolewa. Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele.
82 Susan W. Schneider, Jewish and Female (New York: Simon &Schuster, 1984) uk.237. 83 Ibid., uk. 238-239 84 Alexandra Wright, "Judaism", in Holm and Bowker, op. cit., uk. 128-129.
Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe. Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunika kichwa, kwa sababu yeye ni mfano wa utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume. Kwa hiyo imempasa mwanamke awe dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika. 1Wakorintho 11:3-10 Mantiki ya Paulo ya kuwavisha wanawake shela ni kwamba, shela huwakilisha alama ya utawala wa mwanaume, ambaye ni mfano na utukufu wa Mungu juu ya mwanamke, ambaye ameumbwa kutokana na mwanaume na kwa ajili ya mwanaume. Mt. Tertullian katika tasnifu yake mashuhuri, 'On the veiling virgins' ('Juu ya kuwavisha wanawali shela), anaandika hivi: "Wanawake vijana, mnavaa shela zenu nje mitaani, hivyo ni lazi-ma mzivae mkiwa kanisani, mnazivaa mkiwa pamoja na wageni, basi zivaeni mkiwa pamoja na kaka zenu...
"Miongoni mwa sheria za kanisa Katoliki za sasa, kuna sheria inayowataka wanawake kufunika vichwa vyao wakiwa kanisani.85 Baadhi ya madhehebu ya Kikristo kama vile Amish na mennon-ites kwa mfano, wanawavalisha wanawake wao shela hadi sasa. Sababu ya kuvaa shela, kama inayotolewa na viongozi wa Kanisa ni kwamba, "Kufunika kichwa ni alama ya mwanamke kuwajibika kwa mwanaume na Mungu," ambayo ni mantiki ile ile iliyotolewa na Mt. Paulo katika Agano Jipya.86 Kutokana na ushahidi wote huo hapo juu, ni wazi kwamba Uislamu haukubuni ushungi. Hata hivyo, Uislamu umeuthibitisha. 85 Clara M. Henning, "Cannon Law and the Battle of exes" in Rosemary R. Ruether, ed., Religion and Sexism: Images of woman in Jewish and Christian Trraditions (new York: Simon and Schuster, 1974) uk. 272, 86Donald B.Kraybill, The riddle of the Amish Culture (Baltimore: Johns Hopkins University Press, 1989) uk. 56.
Qur'an inawahimiza wanaume waumini na wanawake waumini kuangusha macho yao chini na kulinda tupu zao, na kisha huhimiza wanawake waumini kuteremsha shungi zao ili kufunika shingo na kifua: "Waambie waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao, bila shaka Mwenyezi Mungu anazo habari za yale wanayoyafanya.
Na waambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waan-gushe shungi zao juu ya vifua vyao, na wasioneshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au watoto wa kaka zao, au watoto wa dada zao, au wanawake wenzao, au wale waliomilikiwa na mikono yao, au wafuasi wanaume wasio na matamanio (kwa wanawake) au watoto ambao hawajajua siri za wanawake. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapam-bo waliyoyaficha. Na tubieni nyote kwa Mwenyezi Mungu enyi wenye kuamini ili mpate kufaulu." Qur'an...24:30-31
Qur'an iko wazi kabisa kwamba shela ni muhimu kwa ajili ya adabu, lakini kwa nini adabu ni muhimu? Qur'an bado iko wazi: Ewe Nabii! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wake wa waumini: Wateremshe juu yao shungi zao. Kufanya hivyo inaelekea zaidi wajulikane na wasiudhiwe, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu. Qur'an...33:59 Hii ndiyo nukta yote, adabu imeamriwa ili kuwakinga wanawake kutokana na usumbufu au kwa lugha nyepesi, adabu ni kinga. Hivyo, dhumuni pekee la Hijab katika Uslamu ni kinga.
Hijab, tofauti na shela ya mila ya Kikristo,sio alama ya mamlaka ya mwanaume juu ya mwanamke, wala sio alama ya mwanamke kuwajibika kwa mwanaume. Hijab, tofauti na shela iliyoko katika mila ya ki-Yahudi, sio alama ya anasa na ubora wa baadhi ya wanawake watukufu walioolewa. Katika Uislamu Hijab ni alama ya adabu ambayo hulinda salama uadilifu binafsi wa mwanamke. Qur'an inasisitiza kwa nguvu sana kuhifadhi heshima ya mwanamke, na kuwahukumu wanaume kuadhibiwa vikali kama kwa uwongo wanashutumu wanawake kwa uchafu: Na wale wanaowasingizia wanawake waaminifu kisha hawaleti mashahidi wanne, basi wapigeni mijeledi themanini na msi-wakubalie ushahidi wao kabisa, na hao ndio mafasiki. Qur'an 24:4 24:4
Baadhi ya watu, hususan katika nchi za magharibi, wamezowea kudhihaki hoja yote ya adabu kwa ajili ya kinga. Hoja yao ni kwamba, kinga bora ni uenezaji wa elimu, tabia za kistaarabu na kujizuia. Tungesema: Vema, lakini haitoshi. Kama ustaarabu ni kinga ya kutosha, basi kwa nini wanawake katika Amerika ya Kaskazini hawathubutu kutembea peke yao katika mitaa yenye giza - au hata kukatisha sehemu iliyotupu ya kuegeshea magari? Kama elimu ni ufumbuzi, basi kwa nini vyuo vikuu vyetu vina 'huduma ya kusindikizwa nyumbani' kwa wanafuzi wa kike katika kampasi (eneo la chuo)? Kama kujizuia ni ufumbuzi, basi kwa nini taarifa za unyanyasaji wa kijinsia katika sehemu za kazi huripotiwa kwenye vyombo vya habari kila siku? Mfano wa wale walioshutumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia, katika miaka michache iliyopita, ni pamoja na: Mabaharia maofisa, Mameneja, Maprofesa wa vyuo vikuu, Maseneta, Mahakimu wa Mahakama Kuu, na Rais wa Amerika! (Clinton).
Ifuatayo ni takwimu iliyochapishwa katika kipeperushi kilichotole-wa na mkuu wa kitengo cha wanawake katika Queen's University ya Canada: Nchini Canada mwanamke anashambuliwa kijinsia kila baada ya dakika 6, mwanamke mmoja katika wanawake watatu nchini Canada atakuwa ameshambuliwa kijinsia wakati fulani katika maisha yake. Mwanamke mmoja katika wanawake wanne wako katika hatari ya kubakwa au kujaribiwa kubakwa katika maisha yake. Mwanamke mmoja mmoja katika wanawake wanane watakuwa wameshambuliwa kijinsia wakati wakuhudhuria vyuo au vyuo vikuu, na utafiti umegundua kwamba wanaume 60% wenye umri wa kwenda chuo kikuu wamesema wangeweza kufanya shambulio la kijinsia kama watakuwa na uhakika kwamba hawatashikwa.
Kukabiliana na ushambuliaji wa wanawake, mabadiliko makali ya msingi katika muundo na utamaduni wa maisha ya jamii ni ya muhimu kabisa. Utamaduni wa adabu ni wenye kuhitajika sana, adabu katika mavazi, katika kuongea, na katika tabia za wote wanaume na wanawake, vinginevyo takwimu za kutisha huelekea kuongezeka , na kwa bahati mbaya mwanamke peke yake ndiye mwenye kulipa gharama hiyo. Kwa hakika, tunateseka, lakini kama alivyosema K. Gibran:"...kwa mtu ambaye anapigwa ngumi sio sawa sawa na yule ambaye anazihesabu."87
Jamii kama ya Kifaransa ambayo inawafukuza wasichana kutoka mashuleni kwa sababu ya mavazi yao ya adabu, mwishowe ina-jidhuru yenyewe. Ni moja ya kejeli kubwa ya dunia yetu ya leo kwamba ushungi ule ule uanaoheshimiwa kama alama ya 'utukufu' wakati ukivaliwa na watawa wa Kanisa Katoliki, unakejiliwa na kushutumiwa kama alama ya 'ukandamizaji wa wanawake' wakati ukivaliwa na wanawake wa ki-Islamu kwa madhumuni ya adabu na kinga. 87 Khalil Gibran, Thoughts and Meditations (New York: Babtam Books, 1960) uk. 28. Wasala Llahu ala Sayyidina wa Nabiyyina Muhammadin wa Alihit-taahiriina. Wal hamdulilahi Rabbil-alamin. Mwandishi: Muhammad Ibrahim Kaadhim Al-Qaz-wini. Mtarjumi: Msabah Sha'ban Mapinda. 27 Muharram 1412 -9 August, 1991
MWISHO