3
QURANI MUUJIZA WA MILELE
MWENYE KUIJUA QUR'ANI NA ASIFUATE AMRI ZAKE
Imepokelewa kutoka kwa Mtume
katika Hadithi[43] ya kuwa amesema: Mwenye kujifunza Qur'ani na hakufuata wala kutekeleza Amri zake na kuathirika na mapenzi ya dunia na mapambo yake, atawajibikiwa na ghadhabu ya Mwnyezi Mungu na atakuwa katika daraja moja pamoja na Mayahudi na Wakiristo ambao walikiweka kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa kutaka umashuhuri na kwa kuitaka dunia, siku ya kiama atakutana na Mwenyezi Mungu uso wake ukiwa ni mifupa mitupu usio kuwa na nyama na Qur'ani kumrusha kinyumenyume hadi kwenye motoni na kuangukia kwenye moto huo pamoja na walio ingia humo, na mwenye kusoma Qur'ani na hakutekeleza amri zake Mwenyezi Mungu atamfufua siku ya kiama akiwa kipofu na atasema:
[44] Atasema:
[45]
Na hapo itatolewa amri ya kumtupia motoni, na mwenye kusoma Qur'ani kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kuzama katika kuifahamu dini, atakuwa na thawabu mfano wa walizo pewa malaika, Manabii na Mitume, na mwenye kujifunza Qur'ani akitaka kujionyesha na kuwa mashuhuri na ili ajigambe kwa Qur'ani hiyo mbele ya wajinga na kujifakharisha kwa maulamaa na kuitafuta dunia kwa Qur'ani hiyo, Mwenyezi Mungu ataitenganisha mifupa yake siku ya kiama na hakutakuwa ndani ya moto mtu mwenye adhabu kali zaidi kuliko mtu huyo na hakuna aina yoyote ya adhabu isipokuwa ataadhibiwa nayo kutokana na ukubwa wa ghadhabu hiyo na chuki yake, na mwenye kujifunza Qur'ani na kuwa mnyenyekevu kwenye elimu na kuwafunza waja wa Mwenyezi Mungu huku akiyataka malipo ya Mwenyezi Mungu hakuta kuwa ndani ya pepo mwenye thawabu nyingi zaidi kuliko yeye na hakutakuwa na kitu kizuri isipokuwa atakuwa na hisa yake kubwa kwenye kitu hicho na atakuwa na mahala au nyumba tukufu zaidi.[46] Na imepokelewa kutoka kwa Mtume
amesema:
.[47]
Na imepokelewa kutoka kwa Abil-ashhab An-nakh'iy amesema: Amesema Ali bin Abi Twalib
:
[48] Na imepokelewa kutoka kwa Mohammad bin Ali bin Hussein amesema: Amesema Abu Abdillah
: Wanawake msiwaweke vyumbani na wala msiwafundishe kuandika na wala msiwafundishe surat Yuusuf bali wafundisheni kusokota sufi na surat Nuur- Hadithi.[49] Anasema muandishi : Makusudio ya kukataza ni yale matendo ambayo ndani yake kulikuwa na fitina.
KUWA NA QUR'ANI WAKATI WOTE
Imepokelewa kutoka kwa Muawia bin Ammar[50] kutoka kwa Aba Abdillah
katika usia wa Mtume
kwa Ali
amesema: Ni juu yako kusoma Qur'ani wakati wote. Na imepokelewa kutoka kwa Zuhriy amesema: Nilimuuliza Ali bin Hussein
:
[51] Na imepokelewa kutoka kwa Hafs amesema: Nilimsikia Mussa bin Jaafar
akisema: katika Hadithi: Hakika daraja za pepo ziko sawa na kiwango cha aya za Qur'ani huambiwa msomaji, soma na upanda daraja moja, hapo basi atasoma kisha atapanda juu daraja moja.[52]
Na imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Sulaiman, kutoka kwa Abi Jaafar
amesema:
(50) na mwenye kuisoma sehemu nyingine tofauti na sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi mema kumi (10). [53]
Na imepokelewa kutoka kwa Bashiir bin Ghaalib Al-asadiy kutoka kwa Hussen bin Ali
amesema: Mwenye kusoma aya moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu alie takasika katika sala yake hali ya kuwa ni mwenye kusimama, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi mema mia moja, na ikiwa ataisoma sehemu nyingine tofauti na kwenye sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi mema kumi na ikiwa ataisikiliza Qur'ani humuandikia kwa kila herufi jema moja, na ikiwa ataihitimisha Qur'ani usiku, malaika humtakia rehma hadi asubuhi na ikiwa ataihitimisha mchana husaliwa na kutakiwa rehma na malaika walinzi mpaka imfikie jioni, na maombi yao kwake hujibiwa na hilo ni bora kwake kuliko yote yaliyomo mbinguni na ardhini, nikauliza:
[54]
4
QURANI MUUJIZA WA MILELE
MWENYE KUSIKILIZA QUR'ANI
Imepokelewa kutoka kwa Mohammad bin bashiir [55] kutoka kwa Ali bin Hussen
na ameipokea hadithi hii kutoka kwa Abi Abdillah
amesema: Mwenye kusikiliza herufi moja ya kitabu cha Mwenyezi Mungu bila ya kusoma, Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja na kumfutia kosa moja na kuinuliwa daraja moja, na mwenye kusoma kwa kuangalia bila ya kusali Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi jema moja na kumfutia kosa moja na huinuliwa daraja moja, na mwenye kujifunza herufi moja ya dhahiri ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humuandikia mema kumi na kumfutia makosa kumi na kuinuliwa daraja kumi, akasema: Si semi kwa kila aya lakini kwa kila herufi sawa iwe baa au faa au mfano wa hizo, akasema: Na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amekaa kwenye sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi hiyo mema khamsini, na kumfutia makosa khamsini, na kumuinua daraja khamsini, na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amesimama kwenye sala yake, Mwenyezi Mungu humuandikia mema mia moja na kumfutia makosa mia moja na kumuinua daraja mia moja, na mwenye kuihitimisha, maombi yake ni yenye kukubaliwa, sawa yachelewe au yawahi akasema: Nikasema: Niwe fidia yako mwenye kuihitimisha yote? Akasema: Mwenye kuihitimisha yote. [56]
Na imepokelewa kutoka kwa Is'haq bin Ammar, kutoka kwa Abi Abdillah
amesema:
.[57] Na imepokelewa kutoka kwa Anas amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu
:
[58]
SURATUL FAATIHA NA FADHILA ZAKE
Imepokelewa kutoka kwa Hassan bin Ali Al-akariy kutoka kwa baba zake
(katika hadithi) amesema: Hakika Faatihatul kitaab (yaani Al-hamdu) ni bora zaidi kuliko vilivyomo kwenye arshi (hadi akasema) fahamuni ya kuwa mwenye kuisoma kwa makusudi kabisa kwa ajili ya kumtawalisha Mohammad na Aali zake Mwenyezi Mungu atampa kwa kila herufi aisomayo ya sura hiyo jema moja na kila jema moja ni bora kwake kuliko dunia na yaliyomo ndani ya dunia hiyo kati ya mali za aina tofauti na kheri zake, na mwenye kumsikiliza msomaji akiisoma atakuwa na thawabu mfano wa msomaji, basi ni vema kila mmoja wenu kujilimbikizia kheri hizi zilizo nyingi.[59]
Na mepokelewa kutoka kwa Fudhaili bin Hassan At-twabrasiy (katika majmaul bayan) kutoka kwa Mtume
amesema: Ibada bora kabisa ni kusoma Qur'ani.[60] Na imepokelewa kutoka kwake (a.s) ya kuwa amesema (katika hadithi):
[61]
Na imepokelewa kutoka kwake
ya kuwa amesema: Ataambiwa mwenye Qur'ani: Soma na upande juu na soma kwa tartiil kama ulivyo kuwa ukisoma duniani, hakika daraja yako ni mwisho wa aya uisomayo.[8] Na imepokelewa kutoka kwake
amesema:
.[62] Na imepokelewa kutoka kwa Ahmad bin Fahdi (katika kitabu Uddatud-daaiy) kutoka kwa Mtume
amesema: Amesema Mwenyezi Mungu alie takasika: Mwenye kuacha kuniomba na kujishughulisha na kusoma Qur'ani nitampa thawabu bora zaidi za watu wenye kushukuru.[63]
MWENYE KUSOMA QUR'ANI KISHA AKAISAHAU
Imepokelewa kutoka kwa Abi Baswiir [64] amesema: Amesema Abu Abdillah
mwenye kusahau sura moja ya Qur'ani itamtokea ikiwa katika sura nzuri yenye kupendeza na itamjia ikiwa na sura ya daraja la juu kabisa peponi, pindi atakapo iona atasema: wewe ni nani? Uzuri ulioje ulio nao? Laiti unge kuwa wangu mimi, nayo itasema je hunifahamu? Mimi ni sura fulani na fulani na lau kama usinge nisahau ninge kuinua hadi mahala hapa. Na imepokelewa kutoka kwa Yaakuub Al-ahmar, amesema: Nilimuuliza Aba Abdillahi
: hakika mimi nina madeni mengi na hakika nimeingiwa na mambo ambayo huenda Qur'ani ikanikimbia na kunitoka, Abu Abdillah
akasema:
.[65]
Na imepokelewa kutoka kwa yaakub Al-ahman amesema: Nilimwambia Aba Abdillah
Niwe fidia yako hakika nimepatwa na mambo na hima, hakukubakia kheri yoyote isipokuwa sehemu fulani imeniponyoka na kunikimbia hata Qur'ani hakika sehemu yake fulani imeniponyoka na kunikimbia, akasema: basi akahuzunika na kufazaiaka kwa wakati huo pindi alipo taja Qur'ani kisha akasema: Hakika mwenye kusoma sura moja ya Qur'ani itamjia siku ya kiama na kumuangalia ikiwa kwenye daraja mojawapo kati ya daraja za peponi na itasema:
[66]
Na imepokelewa kutoka kwa Said bin Abdallah Al-aaraj amesema: Nilimuuliza Aba Abdillahi kuhusiana na mtu mwenye kusoma Qur'amni kisha akaisahau, kisha akaisoma na kuisahau, je kuna tatizo juu yake kwa kufanya hivyo? Akasema hapana.[67] Na riwaya iliyo pokelewa kutoka kwa Hussein bin Zaidi kutoka kwa Swaadiq
katika (hadithi ya makatazo) ya kuwa Mtume
alisema:
[68]