HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU15%

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU Mwandishi:
: AZIZI NJOZI
Kundi: Wanawake

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU
  • Anza
  • Iliyopita
  • 33 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 48297 / Pakua: 5931
Kiwango Kiwango Kiwango
HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

18

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

NDOA YA MUDA (MUT'A)

Moja ya sheria tukufu za Uislamu kwa mtazamo wa sheria ya Ja'fari (Shia) ni kuwa kuna aina mbili za ndoa, ndoa ya kudumu na ndoa ya muda maalumu. Baadhi ya athari zinazotokana na aina hizi mbili za ndoa ni sawa (zinafanana) na nyingine ni tofauti. Kuna tofauti mbili za msingi tu kati ya ndoa hizi mbili. Moja ni kuwa katika ndoa ya muda, mwanaume na mwanamke huingia katika mkataba wa ndoa ya muda maalum. Muda ukiisha wanaweza kuongeza au kuachana.

Tofauti nyingine ni kuwa kuna uhuru mkubwa zaidi wa kuchagua katika ndoa ya muda. Wanaooana wanaweza kuwekeana masharti yoyote wanayopenda. Kwa mfano, katika ndoa ya kudumu mume anawajibika kumtunza mke wake na kumtimizia mahitaji yake ya kila siku. Pia anapaswa kumpatia mavazi, malazi na mahitaji mengine ya lazima kama vile matibabu. Lakini katika ndoa ya muda, kila kitu hutegemea masharti ya mkataba. Inawezekana kuwa mume anaweza kuwa hana uwezo au hayuko tayari kubeba gharana za mke wake, au mke anaweza asipende kutumia fedha za mume wake.

Katika ndoa ya kudumu mke anapaswa kumtambua mume wake kuwa ni mkuu wa familia na kumtii katika mambo ambayo yamo ndani ya mipaka ya familia, lakini katika ndoa ya muda hili linategemea masharti ya mkataba wa ndoa waliyowekeana. Katika ndoa ya kudumu, mke na mume wanarithiana, lakini katika ndoa ya muda hawarithiani.

Hata hivyo, katika ndoa ya muda, baada ya nikaha kusomwa, wanandoa hutambuliwa kuwa ni mume na mke halali na wanaweza kuingiliana lakini kabla ya hapo hawaruhusiwi kabisa kufanya hivyo (tendo la ndoa). Tofauti kuu kati ya ndoa ya muda na ndoa ya kudumu ni kuwa ndoa ya muda huweka masharti (majukumu) machache zaidi kwa wanandoa. Masharti yake hutegemea hiari, matakwa na makubaliano yao wao wenyewe. Kwa asili aina hii ya ndoa huwapa wanandoa uhuru fulani, na huwapa wao uhuru wa kuamua ni muda gani ndoa itadumu.

Katika ndoa ya kudumu si mume wala mke anayeweza kutumia njia za kuzuia mimba bila idhini ya mwenzake, lakini katika ndoa ya muda idhini sio jambo la lazima. Hii ni aina nyingine ya uhuru waliopewa mume na mke. Mtoto anayezaliwa katika ndoa ya muda ana hadhi sawa kisheria na mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa ya kudumu. Mahari: Mahari lazima ipangwe wakati wa ndoa, lakini malipo yake halisi yanaweza kutegemea makubaliano ya wanandoa wote wawili. Mahari ni ya lazima katika ndoa zote mbili ya muda na ya kudumu ingawa kuna tofauti kuwa kutopangwa kwa mahari katika ndoa ya muda huibatilisha ndoa hiyo, lakini kutopangwa kwa mahari katika ndoa ya kudumu hakubatilishi ndoa. Ikiwa mahari haikupangwa wakati wa kufunga ndoa, mke hustahili mahari ambayo imezoeleka eneo hilo.

Katika ndoa ya kudumu, mume amekatazwa kabisa kumuoa mama au binti wa mke wake na mke amekatazwa kuolewa na baba au mtoto wa mume wake. Hali iko hivi pia katika ndoa ya muda. Kama ilivyokuwa hairuhusiwi kutoa pendekezo la kumuoa mke aliyeolewa ndoa ya kudumu, halikadhalika hairuhusiwi kutoa pendekezo la kumuoa mwanamke aliye ndani ya ndoa ya muda.

Mtu akizini na mwanamke aliyeolewa ndoa ya kudumu hiki huwa ni kizuizi cha kudumu cha yeye kutokumuoa mwanamke huyo na halikadhalika mtu akizini na mke wa mtu aliye katika ndoa ya muda huwa amejiwekea kizuizi cha kudumu cha yeye kutokumuoa mwanamke huyo. Baada ya kupewa talaka, katika ndoa ya kudumu mke hupaswa kukaa eda, kipindi ambacho haruhusiwi kuolewa na mwanaume mwingine, halikadhalika katika ndoa ya muda baada ya ule muda waliokubaliana kuisha, mke anapaswa kukaa eda pia. Tofauti pekee ni kuwa kwa mke wa kudumu, eda ni miezi mitatu, ambapo kwa ndoa ya muda eda ni vipindi viwili vya hedhi, au siku 45.

Kuwaoa madada wawili kwa wakati mmoja hairuhusiwi katika ndoa zote mbili, ya muda na ya kudumu. Hii ndio maana ya ndoa ya muda kwa mujibu wa sheria ya Shia. Ni wazi kuwa tunaiunga mkono sheria hii kama itazingatia masharti yake. Ikiwa baadhi ya watu waliitumia vibaya huko nyuma au bado wanaitumia vibaya, hilo ni jambo ambalo liko nje ya sheria. Kufutwa kwa sheria hii, kama inavyopendekezwa na watu wa kisasa (modernist) hakuwezi kuwa na manufaa yoyote kwani kwa kuifuta maovu hayatakoma, isipokuwa tu yatachukua sura mpya. Vile vile, kufutwa kwa sheria hii kutasababisha kuzuka kwa maovu mengine mengi. Kinachotakiwa ni kuwa badala ya kutafuta dosari za sheria hii, watu wanapaswa kusaidiwa wajirekebishe na kuelimishwa.

Sasa hebu tuangalie kwanini ni muhimu kuwa na taasisi ya ndoa ya muda sambamba na ndoa ya kudumu. Ikiwa ndoa ya muda ni muhimu je inakubaliana na hali za sasa na mawazo ya kisasa ya maadili? Tunataka kulijadili swali hili chini ya vichwa viwili. Maisha ya sasa na ndoa ya muda. Dosari na uovu wa ndoa ya muda.

Maisha ya sasa na ndoa ya muda. Kama tulivyojifunza huko nyuma, ndoa ya kudumu huwapa majukumu mazito wanandoa wote wawili, mume na mke. Hata hivyo, hakuna mvulana au msichana ambaye wakati wa kupevuka, ambapo huwa katika shinikizo kubwa la hamu ya ngono, huwa amejiandaa kwa ndoa ya kudumu. Mahitaji ya zama hizi yameongeza urefu wa kitambo kati ya kupevuka kwa asili na kupevuka kijamii, ambapo mtu huwa na uwezo wa kujenga familia. Katika zama za kale, ambapo maisha yalikuwa rahisi, mvulana alikuwa anaweza kuanza kufanya kazi fulani toka kipindi cha awali kabisa cha kupevuka kwake na akaendelea nayo hadi mwisho wa uhai wake.

Lakini sasa hivi hili haliwezekani tena. Mvulana humaliza hatua mbali mbali za elimu akiwa na umri wa miaka 25, ikiwa hakufeli katika hatua yoyote. Hapo ndipo anapoweza kutarajiwa kuwa na kipato chake mwenyewe. Huchukua miaka mingine mitatu au minne ya kujiandaa na kuweza kuoa. Mambo yanakuwa hivi pia kwa msichana anayependa kupata elimu bora maishani. Mabarobaro na mihemko ya ngono.

Leo hii ukimuambia mvulana wa miaka 17, ambaye ndio anakuwa katika kilele cha hamu ya ngono, aoe, watu watakucheka. Hali itakuwa hivyo hivyo kwa msichana mwanafunzi wa miaka 16. Katika umri huu wote, wavulana na wasichana hawawezi kubeba majukumu ya ndoa ya kudumu, sio tu kwao kama mume na mke bali na kwa watoto wao pia watakaozaliwa. Kipi ni bora: utawa wa muda, Ukomonisti wa ngono, au ndoa ya muda? Tunajua maumbile yalivyo, lakini hali hiyo ya maisha katika ulimwengu wa sasa haituruhusu kuoa tukiwa na umri wa miaka 16 au 17.

Maumbile hayako tayari kuchelewesha upevukaji au hamu ya ngono hadi tutakapomaliza elimu yetu. Je vijana wetu wapo tayari kuishi maisha ya ubikra kwa muda hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuoa ndoa ya kudumu? Hata kama kijana mwenyewe yuko radhi kustahamili, je, maumbile yapo tayari kumsamehe asipatwe na shinikizo na hitilafu za neva ambazo kwa kawaida matokeo yake ni kumfanya ajiepusha kutokana na tendo la kawaida la ngono, kama ilivyobainishwa na wataalamu wa kisasa wa sayansi ya akili? Sasa tumebakiwa na njia mbili tu.

Ya kwanza ni kumruhusu mvulana kushirikiana ngono na mamia ya wasichana, na msichana kushiriki katika uhusiano haramu na wavulana wengi, na kisha kutoa mimba nyingi. Hii inamaanisha kuwa kivitendo tunaruhusu Ukomonisti wa ngono. Kwa hakika, tukitoa uhuru usio na mipaka kwa wavulana na wasichana, tutakuwa tunakidhi matakwa ya Azimio la Haki za Binaadamu, kwa sababu kwa maoni ya watu wengi wenye akili finyu, Azimio linataka kuwa, ikiwa wanaume na wanawake wataenda motoni, basi waende pamoja mkono kwa mkono.

Lakini swali ni iwapo itawezekana kwa wavulana na wasichana hawa ambao watakuwa wamefanya ngono zisizo na idadi wakati wa kipindi chao cha masomo, kuishi maisha ya kawaida ya familia. Njia ya pili ni ndoa huru ya muda. Kwa kuanzia ndoa ya muda humpa kila mume mke mmoja kwa wakati mmoja. Ikiwa kila mwanamke ana mwanaume mmoja, ni wazi kila mwanaume atakuwa na mwanamke mmoja, isipokuwa pale ambapo jinsia moja itakuwa kubwa sana kuliko nyingine. Hivyo wavulana na wasichana wanaweza kupita katika kipindi chao cha masomo bila kupata madhara ya kuishi maisha ya utawa wa muda, au kuangukia katika lindi la Ukomonisti wa ngono. Ndoa ya majaribio. Kimsingi inawezekana kwa mwanaume na mwanamke wanaokusudia kuona ndoa ya kudumu wakawa kila mmoja hana imani ya kutosha juu ya mwenzake, hivyo wakaoana kwa majaribio kwa muda fulani.

Wakiwa wameaminiana vya kutosha, huendelea kuishi maisha ya ndoa, vinginevyo wanatengana. (kwa hiyo, tofauti kati ya mtindo wa Kimagharibi wa uhusiano pamoja na mwanamke na Uislamu ni kuwa kwa Wamagharibi hakuna dhana ya mfumo wa ndoa kati ya mwanamke na mwanaume ambapo katika Uislamu wenzi huhesabiwa kuwa mke na mume hata kama ni kwa muda). Nadharia ya Russell ya ndoa ya muda. Katika kitabu chake 'Matrimony and Morals' mwanafalsafa maarufu sana wa Kiingereza, Bertrand Russell, anasema kuwa malaya wanauhifadhi usafi wa kimaadili (kutozini) wa wake zetu na binti zetu. Mtazamo huu ulipotolewa kwa mara ya kwanza na Luckey katikati ya kipindi cha utawala wa Victoria watetea maadili walikereka sana, ingawa hata wao hawakujua kwanini.

Hata hivyo hawakuweza kuzivunja hoja za Luckey. Mantiki ya watetezi wa maadili ilikuwa, kama watu wangefuata maadili yao, malaya wasingekuwepo. Lakini walielewa fika kuwa hakuna aliyezingatia walichosema. Hii ndio kanuni ya kizungu ya kukabiliana na hatari inayoletwa na wanaume na wanawake wasioweza kufunga ndoa ya kudumu, na iliyotajwa hapo juu ni kanuni iliyopendekezwa na Uislamu.

Ikiwa kanuni hii ya kizungu itazingatiwa na jukumu hili likakabidhiwa kwa kundi fulani la wanawake wenye bahati mbaya, je hii itakuwa inaafikiana na heshima ya utu wa mwanadamu na staha ya mwanamke na kiini cha Azimio la haki za Binadamu? Bertrand Rusell, katika kitabu chake, ameingiza sura ya ndoa ya majaribio pia. Anasema kuwa Lindsay, ambaye kwa miaka mingi alikuwa jaji wa Denver, na kwa nafasi yake hiyo alikuwa na nafasi ya kutosha ya kuchunguza ukweli wa mwenendo wa maisha, alipendekeza kuwa iwepo 'ndoa ya wenzi' (companionship marriage).

Lakini kwa bahati mbaya jaji huyu alilazimika kupoteza kazi yake kwa kuwa alikuwa anajali maslahi ya vijana mno kuliko kuwajengea ndani yao hisia ya dhambi. Ili kuhakikisha anafukuzwa, mengi yalisemwa na kanisa Katoliki na Ku Klux Klan, (chama cha siri cha watu ambao hawataki watu weusi kushirikiana na watu weupe - wabaguzi wa rangi nchini Marikani). Ndoa ya wenzi ilipendekezwa na msomi anayependelea kuhifadhi mila za kale kwa nia ya kuweka jambo litakaloleta uimara katika mahusiano ya ngono. Lindsay alibaini kuwa tatizo kubwa la ndoa lilikuwa ni ukosefu wa fedha. Fedha haihitajiki kwa ajili ya watoto watakaozaliwa tu, lakini pia kwa sababu haimuwajibikii mwanamke kubeba gharama za matunzo ya familia. Anafikia hitimisho kuwa vijana wanapasa kufunga ndoa za wenzi (muda) ambazo ni tofauti na ndoa za kawaida katika njia tatu. Kwanza nia ya ndoa hii sio kuzaa watoto.

Pili: kwa vile mwanamke huwa hajazaa mtoto, kuachana muda unapokwisha huwa jambo rahisi. Tatu, katika suala la talaka, mwanamke hustahili kulipwa masurufu baada ya kuwa ameachwa. Hapana shaka kwamba mapendekezo ya Lindsay yanafaa na yanatekelezeka, kama yangekuwa yamekubaliwa kuwa sheria, yengetarajiwa kuwa na matokeo mazuri kwa maadili. Ambacho Lindsay na Russell wanakiita ndoa ya wenzi ni tofauti kidogo tu na ndoa ya muda katika Uislamu, lakini pendekezo hili linaonyesha kuwa wanafalsafa wa fani hii wamebaini kuwa ndoa ya kawaida ya kudumu haikidhi mahitaji yote ya jamii. Ndoa ya muda-II Tayari tumeshaeleza tabia ya ndoa ya muda, ulazima wa kuwepo kwake na ndoa ya kudumu kushindwa kukidhi mahitaji yote ya wanaadamu. Sasa hebu tuangalie upande wa pili wa shilingi na kuona hasara na dosari zake. Kabla ya kujadili hilo hebu tuangalie kitu kimoja.

Historia ya Imani. Katika masomo yote ambayo watu mbali mbali wameyatolea maoni, hakuna lililo tata na gumu kama historia ya mawazo, imani, mila na desturi za mwanadamu. Hii ndio sababu kuwa japo mada hii ni maarufu sana, maoni yaliyo mengi yanayotolewa juu ya hili yamekuwa ni upuuzi. Mtu yeyote mwenye elimu juu ya falsafa, mafundisho ya kumfikia Mungu kwa tafkira, irifan (mysticism) na falsafa ya uanazuoni (schalasticim) wa Kiislamu, na akasoma maandishi ya hivi karibuni katika nchi yetu juu ya masuala yanayohusiana na mada hii ataona kuwa mengi yanaazimwa kutoka kwa wageni au wananukuu na kuiga kila neno lao, pia anaweza kuelewa ninachomaanisha.

Waandishi wetu wa zama hizi wanarudia au kuziegemeza kazi zao na mustashirik, wakati inaonekana kuwa mustashirik hawa na vibaraka wao hawafanyi lolote katika kuyachambua masuala haya kwa kina. Kwa mfano, suala linalofahamika katika mafunzo ya Kiislamu ya irifan (mytcism) kama wahadat al-Wujud (Umoja wa Mwenyezi Mungu) limejadiliwa kutoka katika kila pembe, lakini hakuna jitihada ya maana iliyoelekezwa kufafanua maana halisi ya dhana (neno) hiyo wala kuelezea maoni ya vinara wa mafunzo haya ya irifan (Islamic Mysticism) kama vile Muhyiuddin ibn Arabi na Sadrul Muta'llihin Shiraz.

Hivi karibuni maoni yaliyotolewa juu ya ndoa ya muda katika gazeti la ki-Iran 'Zan-e-Imruz' au "mwanamke wa leo" yamenikumbusha mada ya 'Wahdat al-Wujud' Katika makala haya kila kitu kilizungumzwa juu ya ndoa ya muda, lakini nia hasa ya sheria hii iliachwa. Watu hawajali sheria hii kwa kuwa ni sehemu ya urithi wa Mashariki. Ingekuwa ni zawadi kutoka Magharibi mambo yangekuwa tofauti kabisa. Kama sheria hii ingekuwa inatoka Magharibi bila shaka makongamano na semina yangekuwa yanafanyika kutetea wazo kuwa ndoa ya kudumu haikidhi hali ya maisha ya karne hii na kwamba kizazi hiki hakiko tayari kubeba majukumu mazito ya ndoa ya kudumu.

Kizazi hiki kinataka kuwa huru. Kinataka kuishi maisha ya uhuru. Kinataka ndoa huru ambayo masharti yake yataamuliwa na wanandoa wenyewe. Sasa kwa kuwa tayari sauti zimeanza kupazwa huko Ulaya kuteteta ndoa ya muda na watu mashuhuri kama Bertrand Russel wanaihubiri kwa jina la ndoa ya wenzi inatarajiwa kuwa baada ya muda si mrefu ndoa ya muda itakuwa mashuhuri mno kiasi cha kuwa tutalazimika kuzindua kampeni za kutetea ndoa ya kudumu.

Pingamizi Yafuatayo ndiyo yanayosemwa kuwa ni ubaya na mapungufu ya ndoa ya muda. Msingi wa ndoa unapaswa kuwa wa kudumu tokea mwanzo wa mahusiano ya unyumba, mume na mke wanapaswa kujua kuwa kila mmoja ni mali ya mwenzake kwa kudumu. Wazo la kutengana halipaswi kuingi akilini mwao. Ndoa ya muda sio mkataba wa kudumu kati ya mume na mke. Ni kweli kuwa msingi wa ndoa unapaswa kuwa wa kudumu.

Hata hivyo, pingamizi hili linaweza kuwa sahihi tu kama tutaipinga ndoa ya kudumu na kuhimiza kuwa nafasi yake ichukuliwe na ndoa ya muda. Kama pande mbili zinaweza kuimudu ndoa ya kudumu na kila mmoja ana imani ya kutosha na mwenzake na wakaamua kuwa kwa kudumu kila mmoja awe mali ya mwenzake hapana shaka kuwa wanapaswa kufunga ndoa ya kudumu. Sheria ya ndoa ya muda imewekwa tu kwa vile ndoa ya kudumu peke yake haiwezi kukidhi mahitaji yote ya wanaadamu katika hali zote. Kuruhusu ndoa ya kudumu peke yake kutasababisha tu Ukomonisti wa ngono. Ni wazi kuwa hakuna mvulana au msichana ambaye ana rasilimali za kutosha kwa ajili ya ndoa ya kudumu anaweza kujiingiza katika mahusiano ya muda.

Wanawake na wasichana wa Kiirani, licha ya kuwa Shia, hawalipendi wazo la ndoa ya muda. Wanaliona kama tusi kwao. Hivyo maoni ya jumla ya Shia wenyewe yamelikataa. Tunaweza kujibu kuwa kulichukia wazo hilo kijumla kunatokana na wanaume waasherati kulitumia vibaya. Ni jukumu la serikali kuzuia kutumiwa kwake vibaya. Pili sio jambo la maana kutarajia ndoa ya muda kuwa mashuhuri kama ndoa ya kudumu, kwa sababu ndoa ya muda inakusudiwa kukidhi mahitaji ya wahusika ikiwa wote au mmoja wao hayuko tayari kufunga ndoa ya kudumu. Ndoa ya muda inashusha hadhi na utu wa mwanamke.

Ni sawa sawa na kuukodi mwili wa mtu, na hata kuhalalisha uuzaji wa watu. Ni kinyume na staha ya mwanamke kumuweka kwa ajili ya mwanaume yeyote kwa kubadilishana na fedha. Hili ni pingamizi linalostaajabisha zaidi. Kwanza ndoa ya muda, kama tulivyoeleza hapo awali, haina uhusiano wowote na uuzaji au ukodishaji. Je inaweza kuwa uuzaji au ukodoshaji kwa vile tu muda wa ndoa ni maalum? Je inakuwa ni kukodisha kwa kuwa mahari inapaswa kupangwa?

Tunataka kulijadili suala la mahari tofauti. Mafakihi wamekubaliana kuwa, kwa asili ya mkataba, hakuna tofauti kati ya ndoa ya kudumu na ndoa ya muda. Ni miundo miwili ya ndoa na mikataba yake inaweza kusihi tu kwa kuzingatia kanuni ya ndoa. Ikiwa mkataba wa ndoa ya muda utachukua sura ya uuzaji au ununuaji, basi itakuwa ni batili. Pili, tangu lini ada ya kukodi (kuajiri) watu ilipigwa marufuku? Mafundi cherehani, vionyozi, wapishi, hata wataalamu mabingwa, waajiriwa wote wa serikali kuanzia kwa Waziri Mkuu hadi kwa afisa wa cheo cha chini kabisa na wafanyakazi wote wa viwandani wote ni wa kukodiwa.

Mwanamke ambaye kwa hiari yake anaingia mkataba wa ndoa ya muda na mwanaume fulani sio mwanamke aliyekodishwa na hafanyi jambo la aibu kwa staha yake. Kama unataka kuona wanawake waliokodishwa na waliofanywa watumwa na unataka kujua maana halisi ya mwanamke aliyeajiriwa (kodiwa), unapaswa kwenda Ulaya na Marekani na utembelee makampuni ya filamu. Huko utaona miondoko ya viungo vya mwanamke, ishara zake na mikao ya kingono ikiuzwa. Tiketi za sinema na kumbi za starehe unazonunua ndiyo mishahara ya wanawake waliokodiwa.

Unatambua ni kiasi gani mwanamke anajidhalilisha ili kupata fedha? Analazimika kujifunza kwa miaka mingi sanaa ya kuamsha na kuchochea hamu ya ngono chini ya usimamizi wa wataalamu bingwa wa fani hiyo na wenye uzoefu. Analazimika kuuweka mwili wake, roho yake na haiba yake rehani kwenye makampuni ya biashara ili kuvutia wateja zaidi na zaidi. Ukitembelea mikahawa na mahoteli, unaweza kuona ni heshima gani mwanamke aliyopata, ni jinsi gani analazimika kuuza heshima na utu wake kwa ajili ya fedha kidogo ili kujaza masanduku ya fedha ya mabepari na jinsi gani analazimika kujiuza mbele ya wageni.

Wanawake waliokodiwa ni wale wasichana wa mauzo katika maduka makubwa ambao wanaitoa mhanga heshima na staha yao ili kukidhi tamaa ya waajiri wao. Wanawake waliokodiwa ni wale wasichana wanamitindo wanaoonekana katika TV wakitangaza bidhaa na wanaotumia mbinu zote kuwavutia wateja kwao. Nani asiyejua kuwa leo hii huko Magharibi uzuri wa mwanamke, mvuto wake wa kingono, sauti yake, sanaa yake, mwili wake, roho yake na zaidi ya yote, haiba yake vinatumika kama njia nyenyekevu za kutumikia maslahi ya ubepari wa Ulaya na Marekani?

Ninashangaa ni vipi mwanamke aliyeolewa na mwanaume fulani kwa hiari yake lakini kwa muda maalum anachukuliwa kuwa mwanamke aliyekodiwa (kufanya ngono) wakati mwanamke ambaye katika sherehe ya harusi au kwenye hafla ya jioni, mbele ya maelfu ya macho yenye tamaa ya wanaume, anaimba mpaka koo lake linauma, haonekani kuwa ni mwanamke aliyekodiwa (kufanya mambo machafu).

Kwa kuruhusu ndoa ya muda, Uislamu umemkinga mwanamke dhidi ya kunyonywa na mwanaume. Pia Uislamu umemkataza kutumia njia dhalili ili kujipatia riziki. Je, ni Uislamu uliomdhalilisha mwanamke au Ulaya ya karne hii? Ikiwa siku moja mwanamke atagundua mitego yote ambayo mwanaume wa karne hii ameiweka katika njia yake, bila shaka atapinga kwa nguvu zote uongo na udanganyifu huu. Hapo tu ndipo atakapobaini kuwa mlinzi pekee mwaminifu kwake na kimbilio lake ni Qur'ani.

Siku hiyo haiko mbali sana! Aidha, ndoa ya muda inahalalisha ndoa za mitala, ambazo ni mila mbaya. Kwa hiyo ndoa ya muda haifai. Mwisho wa sura hii tutaeleza ni kwa ajili ya nani sheria hii imewekwa. Na kuhusiana na ndoa za mitala, tutajadili hilo katika sura inayofuata. Ndoa ya muda haidumu. Huwaacha watoto watakaozaliwa wakiwa hawana makazi. Wanakuwa hawana mtu anayewajibika kwao. Wananyimwa uangalizi wa baba na upendo wa mama. Katika ndoa ya kudumu hakuna mwanandoa anayeweza kukwepa jukumu la kuzaa watoto, lakini katika ndoa ya muda, pande zote mbili ziko huru. Ni kweli kuwa mke hapaswi kumzuia mume wake kufurahia jimai, lakini anaweza kuchukua hatua za kuzuia mimba.

Tatizo hili limetatuliwa kabisa kutokana na maendeleo ya njia za kisasa za kuzuia mimba. Hivyo katika ndoa ya muda, ikiwa wote wawili, mume na mke wanapenda wanaweza kuzaa watoto, ikiwa wanalikubali jukumu la kuwalea. Ni wazi kuwa, kwa upande wa upendo wa asili, hakuna tofauti kati ya mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa ya kudumu na yule wa ndoa ya muda.

Ikiwa baba au mama watakataa kutekeleza jukumu lao, ni jukumu la mahakama kuwalazimisha kama vile tu inavyoingilia katika suala la talaka. Ikiwa mume na mke hawataki kuzaa watoto na nia yao ni kukidhi haja zao tu, wanapaswa wajiepushe kuzaa watoto. Kama tunavyojua, Kanisa haliruhusu njia za kuzuia mimba. Lakini kwa maoni ya Uislamu mume na mke wako huru kutumia njia za kuzuia mimba. Hata hivyo mimba ikishaingia hairuhusiwi kuitoa au kuiharibu.

Hili ndilo wanalolimaanisha mafakihi wa Kishia wanaposema kuwa lengo la ndoa ya kudumu ni kupata watoto na la ndoa ya muda ni kukidhi haja ya asili ya jimai. Ndoa ya muda maalum na nyumba ya wake wa mtu Moja ya mada, ambazo nchi za magharibi zinaitumia kama silaha ya kuonyesha uovu wa nchi za Mashariki na ambayo nchi za magharibi zimeandaa filamu na tamthilia kwa ajili yake ni suala la uundaji wa nyumba za wake (harems). Kwa bahati mbaya, mifano hii ni ukweli uliopata kuwepo katika historia.

Maisha ya baadhi ya makhalifa na masultani yanatoa mfano kamili wa muundo wa 'nyumba za wanawake' wao, ambazo huelezewa kuwa ni alama mashuhuri ya uasherati wa mwanaume wa Mashariki. Inadaiwa kuwa uhalali wa ndoa ya muda unafanana tu na uhalali wa nyumba ya wake, ambayo ni nukta dhaifu kwa upande wa nchi za Masharikii na imeleta aibu kwayo. Sio hivyo tu, bali pia ni sawa na kuhalalisha uasherati, miundo yote ambayo inakwenda kinyume na maadili na husababisha kuporomoka na kuangamia. Kitu hicho pia kimesemwa juu ya ndoa za mitala na zimetafsiriwa kuwa ni uhalalishaji wa nyumba za wanawake wengi (walio chini ya mwanaume mmoja). Tutalijadili suala la ndoa za mitala peke yake.

Hivi sasa tunabakia kwenye ndoa ya muda. Suala hili linapaswa kujadiliwa katika pembe mbili: Ni sababu gani za kijamii zilizosababisha uundwaji wa nyumba za wake (wa mtu mmoja) huko nyuma? Je, sheria ya ndoa ya muda ilikuwa na ushawishi katika hali hii? Je sheria ya ndoa ya muda inakusudia kutoa fursa kwa wanaume waasherati kuunda nyumba za wanawake wao? Sababu za kijamii za uundwaji wa nyumba za wake wa mtu (harems).

Kulikuwa na sababu mbili zilizosababisha kuwepo kwa nyumba hizi. Ya kwanza ilikuwa ni uchamungu na staha ya mwanamke. Nyumba hizi zinaweza kuundwa tu katika mazingira ambayo mwanamke hawezi kufanya tendo la ndoa na mwanaume zaidi ya mmoja. Katika hali hiyo mwanaume muasherati hana namna ila kuwakusanya wanawake wengi na kuunda 'nyumba ya wakeze' (harem). Ni wazi kuwa katika mazingira ambayo umuhimu hauwekwi katika staha na wanawake wapo wengi na bure hakuna anayeweza kuchukua taabu ya kuunda 'nyumba ya wake' kubwa kwa gharama kubwa na vifaa vingi. Sababu ya pili ilikuwa ni kutokuwepo kwa uadilifu wa kijamii.

Mazingira yanayofaa kwa uundaji wa 'nyumba za wake' ni kuwa wachache wame bobea katika kila aina ya starehe na raha, ambapo wengine hawawezi hata kupata mlo wa siku, na ambamo kuna wengi ambao hawawezi kumudu kuoa na kuwa na familia. Katika mazingira hayo, idadi ya wanawake ambao hawajaolewa huongezeka na hutengeneza mazingira mazuri ya uundwaji wa nyumba za wake.

Kwa upande mwingine, ikiwa kuna uadilifu wa kijamii na kuna uwezo wa kuunda familia na kuchagua mke/mume kwa wote, basi ni wazi kuwa kila mwanamke ataambatana na mume mmoja na kunakuwa hakuna fursa ya ufisadi na uundaji wa nyumba hizi. Ikiwa kila mtu mzima ana nafasi ya kuwa na mume/mke, ni wazi kuwa hapatakuwa na idadi kubwa ya wanawake wanaobaki kwa ajili ya matajiri kuunda nyumba za wake, kwani idadi ya wanawake kwa kawaida huwa sawa, huzidi au kupungua kidogo kuliko idadi ya wanaume.

Imekuwa ni mila kuwa historia inasimulia hadithi za nyumba hizi za makhalifa na masultani na kuelezea fahari na utajiri wa vitala (makazi na ofisi) vyao lakini hupuuzia kueleza dhiki, shida na taabu ya wale waliokufa katika tawala hizo na ambao hali zao hazikuwa zikiwaruhusu kuwa na mke. Mamia ya wanawake waliomalizia maisha yao katika nyumba hizi walikuwa ni haki ya asili ya wanaume hawa fukara waliolazimika kubakia bila kuoa mpaka walipokufa. Bila shaka katika jamii ambayo staha na usafi wa kimaadili upo na ambapo tendo la ngono haliwezekani isipokuwa ndani ya mipaka ya ndoa, zikiwemo zote mbili, ya muda na ya kudumu, uundaji wa nyumba za wake hauwezekani, hasa inapokuwa matabaka ya kijamii na kiuchumi yameondolewa na haki ya ndoa inapowekwa wazi kwa kila mtu mzima.

Tukiitazama historia kwa haraka haraka tutaona kuwa sheria ya ndoa ya muda haikuwa na ushawishi wowote katika uundwaji wa 'nyumba za wake' hata kidogo. Hakuna khalifa yeyote wa ukoo wa Abbas na masultani wa himaya ya Ottoman ambao hawa ndio walikuwa mashuhuri kwa kuwa na 'nyumba za wake' kubwa, aliyekuwa mfuasi wa Theolojia ya Shia na hivyo haitarajiwi kuwa yeyote kati yao angeweza kuwa alitumia fursa ya sheria ya ndoa ya muda. Masultani wa Kishia, japo wangeweza kuwa waliitumia sheria hii kama kisingizio kamwe hawakupata kufanya hivi kama makhalifa wa Ibn Abbasi na masultani wa himaya ya Ottomani. Hii inaonyesha wazi kuwa nyumba hizi zilisababishwa na sababu nyingine maalum za kijamii.

Je ndoa ya muda imehalalishwa ili kukidhi tamaa ya mwili? Hapana shaka kwamba dini zote za ki-mungu zinazuia kabisa uasherati na ukosefu wa maadili, kiasi cha kufikia baadhi ya wafuasi wake kuamua kuishi maisha ya utawa. Moja ya kanuni za wazi za Uislamu na zinazokubalika ni kupiga vita uzinifu, ambao umelinganishwa na shirki (kwa maneno ya Qur'ani).

Uislamu umemuelezea 'muonjaji' yaani anayetaka kufaidi kila aina ya wanawake, kuwa anashutumiwa na kuchukiwa na Allah. Tulipokuwa tukijadili suala la talaka, tulilizungumzia hili. Moja ya sifa (tabia) za Uislamu ni kuwa unapinga utawa na useja (kutooa) lakini hauruhusu uzinifu, kwa mujibu wa Uislamu, matamanio ya haja zote za asili, ikiwa ni pamoja na haja ya ngono yanatakiwa kukidhiwa ndani ya mipaka ya kisheria tu kwa kiasi cha mahitaji ya asili. Uislamu hauruhusu kuwasha moto wa matamanio na kuubadili kuwa kiu isiyokatika. Uislamu unapinga mambo yote yenye sura ya uasherati na dhulma.

Ni ukweli usio na shaka kuwa kamwe haikuwa nia ya Mtungaji wa sheria hii ya ndoa ya muda kutoa njia kwa washerati ya kukidhi matamanio yao yasiyokatika ya ngono na kuleta maafa na maangamizi kwa mwanamke na watoto wake wasio na hatia. Utiaji moyo mkubwa uliowekwa kwenye wazo la ndoa ya muda maalumu na Maimamu (wa Ahlul Bait) una falsafa maalumu, ambayo tutaieleza kwa kifupi. 'Nyumba za wake' na ulimwengu wa kisasa. Sasa hebu tuangalie jinsi ulimwengu wa kisasa ulivyolishughulikia suala la nyumba hizi. Ulimwengu wa kisasa unazitazana nyumba hizi kwa chuki na mila hii imeshaachwa.

Moja ya vipengele viwili vilivyosababisha kuwepo kwa nyumba hizo kimeshaondolewa. Lakini ni sababu ipi hiyo? Sio ile ya matabaka ya kijamii bali ile ya staha na uchamungu wa wanawake ndiyo imeondolewa. Mwanaume mzinifu wa zama hizi hahitaji tena kutaabika kuunda 'nyumba ya wake' na kubeba gharama kubwa za kuihudumia. Shukrani kwa utamaduni wa Kimagharibi kwamba kwa mwanaume wa karne hii 'nyumba ya wake' ipo katika kila sehemu.

BIli kuwafaidi wanawake wa rangi na mataifa mbali mbali, mwanaume wa sasa hahitaji kuwa na madaraka makubwa na fedha nyingi kama Harun al-Rashid au Fazl Ibn Yahya Barmaki. Anachohitaji ni gari tu na kipato cha elfu kiasi kila mwezi ili kuweza kufaidi ngono kwa kiasi ambacho hata Harun alRashid hakupata kuota.

Hoteli za kisasa, migahawa, na mikahawa mara zote zipo tayari kuhudumia (kutumiwa) kama nyumba za wanawake kwa wanaume. Wakati fulani uliopita kijana wa Kiiran, Adil Kutwali, wazi wazi alikiri kuwa na mabibi (mahawara) 22 wa maumbo na sura mbali mbali kwa wakati mmoja. Shukrani kwa utamaduni wa Kimagharibi kwamba mwanaume wa sasa anafurahia raha zote za nyumba hizi (harem) bila kuwa na hofu ya gharama kubwa ya kuihudumia. Kama shujaa wa 'alfu lela ulela' (masiku elfu moja na moja) angenyanyua kichwa chake kutoka mavumbini na kuona fursa tele za kufaidi ngono na urahisi wa bei pamoja na uwingi wa wanawake, asingefikiri tena haja ya kuwa na nyumba ya wake, na kubeba gharama zote za kuihudumia.

Angewashukuru watu wa magharibi kwa kumuokoa na gharama zote za kuunda nyumba ya wanawake na hapo hapo angetangaza kufutwa kwa ndoa za mitala na ndoa za muda, kwa sababu zinawapa wanaume mzigo wa majukumu juu ya wanawake. Ukiuliza ni nani aliyepoteza katika mchezo huu, kwa kuwa mshindi anajulikana toka zamani, tutasema kuwa kwa bahati mbaya mwanamke ndiye mara zote amekuwa mpotezaji. Kwa sababu ya kuamini kirahisi na kuwa rahisi, alipoteza jana na amepoteza leo.

Khalifa apiga marufuku ndoa ya muda maalum.

Ndoa ya muda inaruhusiwa na sheria ya Shia (Jafaria) peke yake. Madhehebu mengine ya Kiislamu hayaruhusu. Sikusudii kuingia katika ubishani wa Shia na Sunni. Napenda tu hapa kutaja kwa kifupi usuli wa kihistoria wa suala hili. Waislamu wote wanakubaliana kuwa katika kipindi cha awali cha Uislamu Mtukufu Mtume wakati akiwa safarini na ikawa Waislamu walikuwa mbali na wake zao na hivyo wakawa wanapata ugumu, aliwaruhusu kufunga ndoa za muda.

Inakubaliwa pia na Waislamu wote kuwa Khalifa wa pili, katika kipindi cha ukhalifa wake, aliipiga marufuku ndoa ya Mut'a kwa mujibu wa taarifa mashuhuri, alisema kuwa: "Leo ninapiga marufuku vitu viwili ambavyo vilikuwa halali wakati wa Mtume. Ni ndoa ya muda na kuhiji 'Hajj' na Umra kwa ihram mbili tofauti." Baadhi ya Sunni wanaamini kuwa Mtume mwenyewe aliipiga marufuku ndoa ya muda katika kipindi cha mwisho cha uhai wake na Khalifa wa pili alirudia kupiga marufuku ambayo tayari imeshawekwa na Mtume.

Lakini maneno ya Khalifa ambayo yamekuja kwetu yanaonyesha kitu tofauti na hiki. Maelezo sahihi juu ya hili ni yale yaliyotolewa na Allamah Kashif alGhita. Khalifa alipiga marufuku ndoa ya muda kwa sababu alifikiri kuwa jambo hili lilikuwa ndani ya mamlaka yake kikatiba kama Mkuu wa Dola, ambaye angeweza kutumia mamlaka yake maalum kutokana na mahitaji ya wakati. Kwa maneno mengine zuio la Khalifa lilikuwa ni la kisiasa sio la kisheria. Khalifa kamwe alikuwa hafichi wasi wasi wake juu ya kusambaa kwa masahaba wa Mtume katika nchi mpya zilizotekwa na kuchanganyika kwao na Waislamu wapya waliosilimu.

Katika muda wote wa uhai wake, alipinga vikali suala la Waislamu (masahaba) kuhama kutoka Madina. Pia hakutaka damu zao zichanganyike na Waislamu wapya waliosilimu, ambao imani yao ilikuwa bado haijawa kubwa. Ni wazi kuwa hii ilikuwa ni rai ya muda. Waislamu wa wakati ule waliikubali amri yake bila kuonyesha chuki, kwa sababu tu walijua kuwa ilikuwa ni ulazima wa kisiasa na sio sheria ya kudumu. Vinginevyo hailekei kwamba watu wangeridhika, kama wangeona Mtume aliamrisha hivi na Khalifa anaamrisha vinginevyo.

Lakini baadaye ambapo kama matokeo ya maendeleo fulani, maisha ya makhalifa wa mwanzo, hususan makhalifa wawili wa mwanzo, yalichukuliwa kama kiigizo, amri zao zilichukua sura ya sheria ya kudumu. Hivyo ndugu zetu wa kisunni wanapaswa kulaumiwa zaidi kuliko khalifa ambaye aliweka zuio la muda dhidi ya ndoa ya muda kwa sababu za kisiasa (kama ilivyokuwa kwa zuio la tumbaku nchini Iran katika mwanzo wa karne hii) Wengine wasingepaswa kulipa zuio hili sura ya sheria ya kudumu.

Ni dhahiri kuwa Allamah Kashif al-Ghita hakutoa maoni yoyote juu ya kitendo cha khalifa kama kilikuwa kinakubalika au la. Alieleza tu asili ya zuio hili na kwa nini halikupingwa na Waislamu. Hata hivyo ni kutokana na ushawishi huu na haiba (shaksia) ya Khalifa, kwamba watu waliacha kuifuata sheria hii na kwa sababu mila ya Uislamu ya ndoa ya kudumu ilidhaniwa ingeachwa basi ikawa ndoa ya muda imeachwa.

Ni katika hali hii kwamba kwa nia ya kuhakikisha kuwa desturi ya Kiislamu haisahauliki kabisa, Maimamu watukufu wa Ahlul Bait, ambao ni watetezi na walinzi wa imani walihimiza na kuitetea sana. Imam Jafar Sadiq(a.s) alikuwa akisema kuwa ndoa ya muda ni nukta ambayo hawezi kuificha kamwe. Mbali na faida nyingi za ndoa ya muda, jitihada ya kufufua desturi zilizokufa ilikuwa ni sababu nyingine ya Maimamu kuihubiri. Kwa maoni yetu, Maimamu walipowakataza watu kuoa kwa ndoa ya muda, walitaka iwe wazi kuwa ndoa hii haikuwa kwa wale wasioihitaji.

Imam Kadhim(as) alimwambia Ali ibn Yaqtin, 'Unataka ndoa ya muda ya nini? Allah amekuepusha na tatizo la kuihitaji." Alimwambia mtu mwingine kuwa 'ndoa ya muda, ni kwa yule asiye na mke au mwenye mke lakini mke wake yuko mbali." Muongozo na uhimizaji wa umma katika kuoa ndoa za muda ni hatua moja mbele katika "ufufuaji wa mila zilizoachwa" au desturi lakini uhimizaji peke yake kwa wale waliokuwa wakiihitaji haukuwa unatosha kuihuisha tena mila hii tuliyoruhusiwa na Mtume, kama inavyoonyeshwa wazi katika maandiko ya Kishia na vitabu vya hadithi.

Hata hivyo ni ukweli ulio wazi kuwa maana na lengo la Mtunzi wa sheria hii katika kuikuza (kuitetea) na maelezo ya sheria hii na lengo la Maimamu Maasumin la kuihimiza halikuwa na nia ya kuruhusu majaribio ya ngono, matamanio maovu na ujenzi wa nyumba za wake kwa ajili ya watu wenye tabia za wanyama wala kuwakandamiza na kuwatesa wanawake wasio na uwezo na waliokandamizwa pamoja na watoto yatima kwa wakati wowote. Mwandishi wa kimisri, Sheikh Muhammad Abu Zuhra, katika kitabu chake, 'Al-Ahwal al-Shakhsiya, amemnukuu Amirul Muuminina Ali(a.s) kuwa amesema, "Kama nikipata habari kwamba mtu mmoja mwenye mke amefunga ndoa ya muda, nitampiga mawe mpaka afe."

Hadith hii haina sanad (nyororo) ya wasimuliaji inayoeleweka. Hata hivyo usahihi wake unakubalika, inaunga mkono wazo kuwa ndoa ya muda inaruhusiwa tu kwa yule asiye na mke au ambaye mke wake yuko mbali. Kwa kifupi kwa nini tushikilie hadith hii moja ya mwanazuoni wa Kisunni (ambayo chanzo chake hakieleweki) na kuziacha hadithi nyingine nyingi za Amirul Muuminina Ali(a.s) zilizoripotiwa katika vitabu vyote vya kisunni na Kishia katika sura ya Mut'ah. Katika kauli zake nyingi za thamani Imam Ali (a.s), Amiri wa walioamini anasema, "Kama Umar asingeifuta ndoa ya muda, hakuna mtu ambaye angezini, isipokuwa wachache wenye maradhi ya ngono." Hii ni kuwa kama ndoa ya muda isingekuwa imepigwa marufuku, hakuna mtu ambaye angejenga tabia ya kuzini, ni wale tu ambao mara zote wanapenda kufanya mambo yaliyoharamishwa ndio wangefanya hivyo.

8

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

UWILI

Kimwili, mwanaume kwa wastani ana maungo makubwa na mwanamke ana maungo madogo. Mwanaume ni mrefu zaidi na mwanamke ni mfupi zaidi. Mwanaume ana ngozi inayo kwaruza na mwanamke ana ngozi laini zaidi. Sauti ya mwanaume inaparuza na ni nzito, na sauti ya mwanamke ni nyororo na inavutia. Mwili wa mwanamke unakuwa haraka zaidi na wa mwanaume unakuwa pole pole zaidi. Inasemekana hata mimba ya mtoto wa kike inakua haraka ziadi kuliko mimba ya mtoto wa kiume. Mwanaume ana nguvu zaidi kuliko mwanamke, na ana misuli imara zaidi, lakini mwanamke ana uwezo mkubwa zaidi wa kustahimili kuliko mwanaume. Mwanamke huvunja ungo mapema na hufikia umri wa kuacha kuzaa mapema zaidi.

Msichana huwahi kuanza kuzungumza kuliko mvulana. Ubongo wa mwanaume ni mkubwa kuliko ubongo wa mwanamke lakini ukiwianishwa na mwili mzima (ukubwa wake ukigawanywa na ukubwa wa mwili mzima), mwanamke ana ubongo mkubwa zaidi. Mapafu ya mwanaume yanaweza kuvuta hewa nyingi zaidi kuliko mapafu ya mwanamke. Moyo wa mwanamke hupiga haraka zaidi kuliko moyo wa mwanaume.

Kisaikolojia, mwanaume anapenda zaidi mazoezi, kuwinda na maisha ya heka heka nyingi. Hisia za mwanaume ni changamoto na ugomvi ambapo mwanamke ni mwenye kupenda amani. Mwanamume ni mchokozi na mtu wa hima, mwanamke ni mtulivu na mkimya. Mwanamke huepuka mapigano na mambo ya nguvu nguvu na ndio maana kesi za wanawake kujinyonga ni chache zaidi. Hata wakati wa kujinyonga wanaume hutumia njia za hatari kama vile kujipiga risasi, kujinyonga kwa kamba au kujirusha kwenye majengo marefu wakati wanawake hutumia, vidonge vya usingizi, madawa ya kulenya n.k. kwa ajili ya lengo hili.

Mwanamke ana mihemko (jazba, hasira, furaha) ya haraka zaidi kuliko mwanaume na wanasisimka haraka zaidi. Mwanaume ni mtulivu wa akili zaidi. Kwa asili mwanamke anapenda mapambo, manukato, vipodozi na vitu vya mitindo mipya mipya vya nguo, viatu n.k wakati mwanaume hayuko hivyo. Hisia za mwanamke sio thabiti (hazidumu), akili yake huwa inabadilika. Ni mwangalifu na huchukua tahadhari zaidi, ni mshika dini zaidi, mzungumzaji zaidi, muoga zaidi na anafuata taratibu zaidi kuliko mwanaume. Hisia zake ni za mfumo jike mama toka utoto wake.

Hawezi kushindana na mwanaume katika maarifa ya kufasiri mambo yalivyo na masomo mengine makavu. Lakini katika fasihi na sanaa kama kupaka rangi, hayuko nyuma ya mwanaume. Mwanaume ana uwezo mkubwa zaidi wa kuficha siri zake. Anaweza kuficha tukio baya lililomfika likabaki moyoni mwake tu na ndio sababu anakumbwa sana na magonjwa yanayosababishwa na undani (kuficha mambo moyoni). Mwanamke ni mwepesi kuhisi na mwenye moyo laini kuliko mwanaume, anaweza kuamua kulia kirahisi na wakati mwingine anaweza kupoteza fahamu.

Mtazamo linganishi wa kila mmoja Mwanaume ni mtumwa wa matamanio yake; mwanamke ni mtumwa wa mapenzi. Mwanaume humpenda mwanamke aliyempenda, mwanamke humpenda mwanaume aliyeitambua thamani yake (ya mwanamke huyo) na kutamka upendo wake kwake. Mwanaume hutaka kummiliki mwanamke, mwanamke hutaka kuutawala moyo wa mwanaume. Mwanaume hutaka kumzidi nguvu madaraka mwanamke, mwanamke hutaka kupenya katika moyo wa mwanaume. Mwanaume hutaka kumteka mwanamke; mwanamke hutaka kutekwa. Mwanamke hutaka mwanaume awe jasiri na shujaa na anayemjali, mwanaume hutaka mwanamke mwenye sura nzuri na mcheshi.

Mwanamke hutaka ulinzi wa mwanaume, na huchukulia ulinzi huo kuwa ni kitu cha thamani zaidi anachoweza kukimiliki. Anaweza kuyadhibiti matamanio yake. Hisia za ngono za mwanaume ni kali na zenye nguvu za mwanamke ni baridi na zenye kusisimka. Tofauti kati ya mwanaume na mwanamke. Mwana saikolojia wa kimarekani, Profesa Reek amechapisha matokeo ya utafiti wake juu ya mwanaume na mwanamke katika kitabu kikubwa. Anasema: Ulimwengu wa mwanaume ni tofauti kabisa na ule wa mwanamke. Ikiwa mwanamke hawezi kufikiri au kufanya mambo kama mwanaume, ni kwa sababu wanaishi katika dunia mbili tofauti.

Ameendelea kusema kuwa; "Kwa mujibu wa Agano la Kale, mwanaume na mwanamke wametokana na mwili mmoja. Hivyo ni kweli lakini ingawa wametokana na mwili mmoja, wana miili miwili tofauti, ambayo haifanani kabisa katika maumbile yake. Hawana hisia za aina moja na hawaonyeshi mwitikio wa aina moja katika matukio na ajali mbali mbali. Wako kama sayari mbili zinazozunguka katika njia mbili tofauti.

Wanaweza kuelewana na wanaweza kukamilishana, lakini sio kitu kimoja (sawa). Hii ndio sababu wanaweza kukaa pamoja, kupendana na wanaweza wasichokane. Profesa Reek analinganisha roho ya mwanaume na mwanamke na anagundua tofauti nyingi. Anasema; "Inakinaisha (chosha) kwa mwanaume kukaa na mwanamke anayempenda muda wote. Lakini hakuna kitu kizuri kwa mwanamke kuwa karibu na mwanaume anayempenda. Mwanaume mara zote anataka kubaki vile vile.

Lakini mwanamke anataka kuamka akiwa tofauti na mpya kila siku. Sentensi bora kabisa ambayo mwanaume anaweza kumwambia mwanamke ni kuwa 'Mpenzi wangu, nakupenda.' Sentensi nzuri kabisa ambayo mwanamke hupenda kumwambia mwanaume ni, 'Naona fahari kuwa na wewe.' Mwanaume aliyepata kuwa na wanawake wengi katika maisha yake huwavutia sana wanawake wengine. Lakini wanaume hawapendi wanawake waliopata kuwa na wanaume wengine huko nyuma.

Wanaume wanapokuwa wazee hukosa furaha kwa sababu wanapoteza kazi walizokuwa wanazitegemea. Wanawake wazee huwa na furaha kwa sababu, kwa mtazamo wao huwa wameweza kumiliki vitu bora kabisa ambavyo mtu anaweza kutamani, nyumba na wajukuu wachache. Bahati nzuri kwa mwanaume ni kujipatia nafasi inayoheshimika katika jamii.

Lakini kwa mwanamke bahati ni kuuteka moyo wa mwanaume na kubaki nao katika maisha yake yote. Mwanaume mara zote hutaka kumbadilisha mwanamke wa chaguo lake ili afuate dini na utaifa wake. Kwa mwanamke ni rahisi kubadilisha dini yake na uraia kwa ajili ya mwanaume aliyempenda ikiwa ni pamoja na kubadilisha ubini wake baada ya kuolewa.

Kazi bora ya uumbaji Bila kujali swali iwapo kutofanana kati ya mwanaume na mwanamke kunasababisha tofauti ya haki na majukumu yao au la, kutofanana kwenyewe ni moja ya kazi bora kabisa na ya ajabu mno ya uumbaji. Ni suala amabalo humuelekeza mtu katika kumtambua Allah na Umoja wake. Kunathibitisha kuwa mfumo wa dunia hii umepangiliwa kwa busara kubwa sana na ubora usio na mfano. Kunaonyesha kuwa uumbaji sio suala la bahati nasibu. Maumbile sio kazi ya upofu. Haiwezekani kutafsiri mambo ya ulimwengu bila kumtambua 'Msababishaji Mkuu.' Kwa nia ya kuhifadhi jamii ya viumbe, utaratibu mkubwa wa uumbaji umefanya mfumo wa uzazi kuwepo.

Wanaume na wanawake wanazaliwa kila siku. Kwa vile kuendelea kwa jamii ya wanaadamu kunategemea ushirikianao wao, maumbile yakaona mwanaume na mwanamke wanahitaji kuishi pamoja. Kwa ajili ya kusudio hili maslahi binafsi ambayo ni ya lazima kwa kila kiumbe yamebadilishwa na kuwa hisia za upendo, huduma, ushirikianao na uvumilivu.

Ili kuufanya mpango huu uwezekane, na kuhakikisha kuwa miili yao na roho zao zinakubaliana vizuri na kwa raha, tofauti fulani za kiroho na kimwili zimewekwa kwa kila mmoja wao. Tofauti hizi kati ya mwanamke na mwanaume zinawavuta wote kila mmoja kwa mwenzake. Kama mwanamke angekuwa na maumbile sawa kimwili, mihemko sawa na tabia sawa na mwanaume, isingewezekana kwake kumvutia mwanaume, kama ilivyo sasa.

Kama mwanaume naye angekuwa na umbile la kimwili na kifiziolojia kama mwanamke, mwanamke asingemuona kuwa ndio sawa yake, asingefanya chochote kuuteka moyo wake (mwanaume). Mwanaume ameumbwa kuutawala ulimwengu, na mwanamke ameumbwa kumtawala mwanaume. Sheria ya maumbile imepanga kwamba wote mwanamke na mwanaume wahitajiane na watafutane lakini uhusiano wao sio wa asili sawa na ile waliyo nayo kwa vitu vingine wanavyomiliki, uhusiano huo unatokana na ubinafsi.

Wanataka kumiliki vitu kwa ajili ya matumizi yao, na wanavitafuta ili viwe chanzo cha raha na starehe yao. Lakini uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume una maana kila mmoja miongoni mwao anataka furaha na raha ya mwenzake, na hufurahi kujitolea kwa ajili ya mwenzake. Muungano mkubwa zaidi kuliko uchu wa ngono. Inashangaza kwamba baadhi ya watu hawawezi kutofautisha kati ya uchu wa ngono na mapenzi. Wanafikiri kuwa uhusiano kati ya mume na mke umejengwa juu ya tamaa, matamanio na hisia ya unyonyaji. Wanashikilia kuwa uhusiano huu ni wa aina moja na ule alionao mtu kwa vitu anavyoku la, kunywa, kuvaa au kuendesha. Watu hawa hawajui kuwa katika maumbile, mbali na mahusiano hayo yaliyojengwa juu ya maslahi binafsi, kuna mahusiano mengine pia.

Haya ndio mahusiano ambayo yanayoonyesha ubinadamu. Mahusiano haya, kwa kiasi fulani yapo kwa wanyama pia hususani linapokuja suala la majike/madume yao na watoto. Watu hawa wanafikiri kuwa mwanaume mara zote humtazama mwanamke, kama vile mwanaume asiye na mke anavyomtazama mwanamke malaya. Wanaamini kuwa ni uchu na matamanio ya ngono tu yanayoweza kuwaunganisha mwanamke na mwanaume. Kwa kusema kweli muungano wa ndoa ni kitu kikubwa zaidi kuliko uchu wa ngono, na msingi wake ni ule uliotajwa katika Qur'ani:

"Na miongoni mwa dalili zake ni kuwa amewaumbia wenza wenu kutokana na nyinyi ili mpate utulivu kwao na baina yenu ameweka mapenzi na huruma." (Suratul Ruum; 30:21).

Ni kosa kubwa lilioje kuitafsiri historia ya uhusiano wa mwanaume na mwanamke kwa mtazamo wa ajira na unyonyaji au kwa msingi wa kupambana ili uishi. Lakini bado kuna watu wanaofanya hivyo na wanatoa hoja zisizo na msingi kutetea mawazo yao. Kwa kweli tunashangazwa sana kwa msingi wa migogoro na ukinzani, kana kwamba mwanaume na mwanamke ni matabaka mawili tofauti ya kijamii ambayo mara zote yapo katika migogoro.

Kama inawezekana kuielezea historia ya uhusiano wa akina baba na watoto wao kwa msingi wa ajira na unyonyaji, basi hapo itawezekana pia kuielezea historia ya uhusiano wa waume na wake zao kwa msingi huo. Ni kweli kwamba mwanaume amekuwa na nguvu zaidi kuliko mwanamke, lakini sheria ya maumbile imemuamrisha katika namna ambayo kwa silika hajaweza kumtendea vibaya au kwa ukatili mke wake kama ambavyo amekuwa akifanya kwa watumwa wake, walio chini ya cheo chake au miliki yake na wakati fulani hata kwa majirani zake.

Hatukatai kwamba mwanaume hajapata kufanya ukatili kwa mwanamke. Tunachopinga ni jinsi ukatili wake unavyoelezewa katika kipindi chote cha historia, wanaume wamewakandamiza wanawake, lakini pia waliwatendea vibaya watoto wao, licha ya upendo wote waliokuwa nao kwao. Sababu za ukatili huu zilikuwa ujinga, mila na kujipendelea wenyewe lakini sio kwa ajili ya kumnyonya mwanamke. Sababu hizi ndio hizo hizo zinazomfanya hata yeye mwenywe mwanaume ajikandamize na kujidhulumu, sababu hizi ni ujinga, desturi na tabia zilizozoeleka, na upendeleo (chuki) na sio tamaa binafsi zaidi.

Uwili na hisia za mwanamke na mwanaume kwa kumhusu kila mmoja Sio tu kwamba mahusiano ya kifamilia ya mwanaume na mwanamke kwa mwenzake ni tofauti lakini pia hisia na mielekeo ya kila moja kwa mwenzake ni tofauti. Kwa maneno mengine, asili ya uhusiano wa mwanaume kwa mwanamke ni tofauti na uhusiano wa mwanamke kwa mwanaume, ingawa kila mmoja anavutiwa na mwenzake, lakini tofauti na ilivyo kwa viumbe visivyo hai, hapa kitu kidogo hukivutia kitu kikubwa kwake.

Mwanaume ameumbwa kama udhihirisho wa kusubiri kwa hamu, mapenzi na mshughulikaji, na mwanamke kama udhihirisho wa mvuto na kutamanika. Hisia za hawa wawili ni tofauti lakini zinazokamilishana. Mmoja humtafuta mwenzake na mwingine huhitaji kutafutwa. Wakati fulani uliopita, gazeti lilichapisha picha ya msichana mdogo wa kirusi aliyekuwa amejinyonga. Msichana huyu aliacha ujumbe kuwa hakuna mwanaume aliyepata kumbusu hivyo maisha yake yamekuwa hayavumiliki tena. Kwa msichana ni jambo la kukatisha tamaa sana kwamba hakuna mwanaume aliyepata kumbusu. Lakini mvulana mdogo haimsumbui kama msichana hajawahi kumbusu.

Will Durant katika mjadala wake mrefu, anasema msichana ambaye sifa yake kubwa ni elimu na uwezo mkubwa wa kufikiri tu, lakini hana ucheshi wa asili na ujanja wenye akili kidogo, haelekei kufanikiwa kupata mume. Asilimia sitini ya wanawake wenye elimu ya chuo Kikuu hubaki bila waume. Amesema kwamba mwanamke mmoja mashuhuri na msomi alilalamika kuwa hakuna mtu aliyekuwa tayari kumuoa. Alikuwa akisema; "Kwa nini hakuna anayenipenda? Ninaweza kuwa mke bora kuliko wanawake wengine wengi. Lakini bado wanawake wasio na elimu na umuhimu wowote kijamii wanatafutwa na kuolewa lakini mimi sitafutwi."

Inaweza kuonekana hapa kuwa hali ya kuvunjika moyo kwa mwanamke huyu ni tofauti na kwa mwanaume yeyote. Analalamika kwamba kwanini hakuna anayempenda. Mwanaume huvunjika moyo tu pale ambapo anapokuwa hawezi kumpata mwanamke wa chaguo lake au anamtaka lakini anashindwa kumpata. Hisia za mwanaume na mwanamke zimepangwa hivi, kwa makusudio maalumu ya kuufanya muungano wa mke na mume uwe mzuri zaidi, imara zaidi na wenye furaha zaidi.

Katika maisha yao kwa kusema kweli, msingi wa jamii ya watu na malezi ya kizazi kijacho yamejengwa juu ya muungano huu. Mwanasaikolojia wa kike anaandika; "Kama mwanasaikolojia shauku yangu kubwa imekuwa kujifunza juu ya roho (akili) za wanaume. Siku za nyuma huko nilipewa kazi ya kuchunguza sababu za kisaikolojia za mwanaume na mwanamke. Mwisho nilihitimisha kuwa; Wanawake wote wanapenda kufanya kazi chini ya uangalizi wa mtu mwingine. Wanapenda kufanya kazi katika vyeo vya kawaida sio kama bosi.

Wanawake wote wanapenda kuhisi kuwa kuwepo kwao kunatambulika na kunahitajika. Mwanasaikolojia huyu anaeleza maoni yake kuwa; "Ninaamini kuwa mahitaji haya mawili ya kiroho yanatokana na ukweli kwamba wanawake wanaongozwa na mihemko (emotions) wakati wanaume huongozwa na akili. Mara nyingi inaonekana kwamba wanawake sio tu kwamba wana akili sawa na wanaume, bali wakati fulani hata huwazidi (wanaume). Udhaifu wao pekee ni kuwa wana jazba sana (mno). Kufikiri kwa wanaume kunatekelezeka zaidi, wanahukumu vizuri zaidi, wanapanga mambo vizuri zaidi na wanawaelekeza wengine (ni wakurugenzi) vizuri zaidi. Ubora wa roho (akili) ya wanaume (kuizidi ya wanawake) ni kitu kilichopangwa na maumbile yenyewe. Jitihada yeyote mwanamke atakayofanya kubadilisha ukweli huu, itakuwa ni kujisumbua bure.

Wanawake lazima waukubali uhalisia kuwa kwa vile wao wana mhemuko sana wanahitaji usimamizi wa wanaume katika maisha yao. Lengo kubwa la maisha ya mwanamke ni 'Kujihakikishia' hatima yake ya baadaye. Akishalipata, huziambia kwa heri shughuli zake nyingine. Ni mwoga kufanya mambo ya hatari (ambayo haijulikani kama matokeo yake yatakuwa mazuri au mabaya).

Uoga ni hisia za moyoni, na ili kuzishinda mwanamke anahitaji msaada wa mwanaume. Kazi zote zinazohitaji kufikiri muda wote zinamchosha. Harakati za papara (pupa). Harakati za wazungu za kurejesha haki za wanamke zilikuwa ni suala la papara lililofanywa kwa uharaka usio wa lazima. Mpango wenyewe wa mageuzi ulikuwa mzuri, lakini ukweli wa kisayansi haukuzingatiwa katika utekelezaji wa mageuzi haya, na matokeo yake yakawa ni mchanganyiko wa nukta za maana na za ovyo.

Hakuna shaka kwamba mlolongo wa masaibu na taabu za wanawake uliondolewa, walikubaliwa na kupewa haki nyingi na milango sasa kwa ajili yao ikafunguliwa na harakati za haki za wanawake. Lakini wakati huo huo mageuzi haya yalileta mikosi na balaa kubwa. Sio kwa mwanamke tu, bali kwa wanaadamu wote. Kama papara na pupa visingepewa nafasi, haki za wanawake zingekuwa zilirejeshwa kwa namna bora zaidi na kusingekuwa na mayowe na vilio vya wasomi dhidi ya matokeo yake maovu.

Hata hivyo, tunatarajia kuwa ushauri mzuri utashinda na kuenea na katika mageuzi yatakayofuatia, badala ya kuwa na jazba, watayatumia na kutanguliza maarifa (elimu) na uelewa. Maoni ya wasomi yanaashiria wema na heri siku za usoni. Inaonekana kwamba watu wa Magharibi bado wanataabishwa na madhara ya mageuzi haya ambayo yanaonekana kuwasisimua na kuwafurahisha waigaji wao wa nchi za Mashariki (Asia). Mtazamo wa Will Durant. Will Durant, katika kitabu chake, 'Pleasures of Philosophy' anaeleza vizuri kabisa masuala ya kijisia na familia.

Hapa tutachagua baadhi ya mawazo yake ili wasomaji wetu waelewe uelekeo wa mkondo wa fikra miongoni mwa wasomi wa Kimagharibi na kuepuka hitimisho la papara. Chini ya sura ya Love (mapenzi) anasema, 'Utaratibu wa kwanza wa wazi huanza wakati wa kubalehe. Kubalehe kwa kiingereza ni 'Puberty' neno ambalo ni la kilatini lenye maana ya zama za nywele, yaani ni kipindi cha kuota nywele katika miili ya wavulana, hasa kifuani, jambo ambalo huwa ni la fahari kwao, na ndevu huota usoni, ndevu ambazo huzinyoa kila baada ya muda fulani.

Ubora na uwingi wa nywele na vitu vingine unahusiana na nguvu ya uzazi na asili (chimbuko). Nywele huwa katika ubora wa juu kabisa katika zama za kilele cha urijali (nguvu za kiume). Kukua huku kwa nywele, pamoja na sauti kuanza kuparuza, ni sehemu ya tabia za awamu ya pili ya jinsia zinazotokea kwa wavulana wakati wa kubalehe. Kwa upande wa wasichana wakati wa kuvunja ungo, maumbile huifanya tabia mienendo yao kuwa mizuri mno kiasi cha kuwavutia wanaowatazama. Matako yao huanza kuwa bapa ili kurahisisha kubeba mimba. Matiti yao hukua na kuchomoza kwa ajili ya kumnyoyesha mtoto.

Hakuna anayejua kwa yakini kinachosababisha kuonekana kwa tabia za awamu ya pili za jinsia (secondary sex characteristics). Hata hivyo nadharia ya Profesa Starling, katika siku za hivi karibuni imepata wafuasi wengi. Kwa mujibu wa nadharia hiyo seli za via vya uzazi, wakati wa hatua hii ya ukuzi, hazizalishi manii na mayai ya kike peke yake, bali pia huzalisha homoni ambazo huingizwa katika damu na kusababisha mabadiliko ya kimwili, kiroho na mengineyo. Katika umri huu, sio tu kwamba mwili hupata nguvu mpya, bali pia roho, tabia na mwenendo huathirika kwa namna nyingi. Romain Rolland anasema kuwa katika miaka ya mtu, huja wakati ambapo mabadiliko mengi ya polepole ya kimwili husababisha maendeleo zaidi ya mwanaume au mwanamke.

Mabadiliko muhimu kabisa huwa ni ukakamavu na nguvu kwa wanaume na uzuri unaovutia pamoja na ulaini wa ngozi na mwili kwa mwanamke. Damoseh anasema kuwa kwa asili 'wanaume wote ni waongo, walaghai, wanafiki, wana hila, na ni wagomvi; na wanawake wote ni wabinafsi, wanajishaua na sio waaminifu. Lakini kuna kitu kimoja duniani ambacho ni kitukufu na kitakatifu, na kitu hicho ni muungano wa watu hawa wawili ambao sio wakamilifu... kuelekea kwenye ukamilifu.

Taratibu za kutafuta mwenza kwa wakubwa zinakuwa na uanzishaji kwa mwanaume kupata mkono wa kheri, lakini kujiondoa kwa mwanamke kwa ajili ya ushawishi na udanganyifu (kama mambo yalivyo, kuna hali za kipekee). Kwa vile mwanaume, kwa asili ni kama mpiganaji na mnyama anayewinda, matendo yake ni ya hakika na halisi na pia yeye ndiye muanzaji (mchokozi).

Mwanamke kwake (kwa mwanaume) ni zawadi ambayo lazima ichukuliwe na imilikiwe. Kutafuta mke/mwenzi ni juhudi na mapambano na ndoa ni umiliki na utawala, kuwepo kwa usafi thabiti (kutozini) kwa mwanamke husaidia maslahi ya uzazi, kwa vile kujizuia (kuzini) kwa mwanamke kutokana na aibu kunamsaidia mwanamke katika kuchagua mwenzi wake. Usafi (kutozini) huwazuia wanawake kutokuwa waangalifu katika kuchagua wenzi (wanaume) wao, ambao ni baba wa wana wao watakaowazaa. Mwanamke huzungumza kwa maslahi ya wote lakini mwanaume hujizungumzia maslahi yake peke yake.

Mwanamke ana ujuzi zaidi wa kufanya uchunguzi kwa vile matamanio yake sio makubwa kiasi cha kufanya ashindwe kutumia akili yake vizuri. Darwin amegundua kwamba katika jamii za viumbe wengi, majike hayapendi sana kufanya mapenzi. Wanaviumbe wengine wanaochunguza mimea na wanyama, kama Lemberzo, Cash na Kraft Ebing nao pia wana maoni kuwa wanawake wanapendelea zaidi kuonekana wanavutia, pamoja na kupokea sifa za juu juu (wakati fulani za uongo) na za jumla za wanaume, na wanapendelea pia kuona wanaume wanajali mahitaji yao halisi ya ndani kuliko kutaka kufanya ngono.

Lemberzo, na wengine wanasema kwamba 'Msingi wa asili wa mapenzi ya mwanamke ni kuwa mama (na kuwajali watoto) ndio tabia na sifa ya kwanza ya mwanamke, kisha mapenzi ndio yanafuatia. Hisia zote na michomo ya moyoni inayomuunganisha mwanaume na mwanamke haitokani na mahitaji yake ya kimwili lakini inatokana na silika yake ya unyenyekevu (kujiweka chini ya uangalizi wa mwanaume).

Silika hii ina kazi ya kutimiza na kutekeleza majukumu ya nafasi yake halisi. Will Durant katika sura aliyoiita 'Man and woman' (mwanaume na mwanamke), anasema; 'Kazi kubwa ya mwanamke ni kuhakikisha kwamba jamii ya watu inaendelea kuishi na kudumu, na kazi kubwa ya mwanaume ni kuwatumikia mke na watoto wake. Wanaweza kuwa na kazi nyingine pia, lakini kwa misingi ya busara na kuangalia manufaa, hizo kazi nyingine ziko chini ya majukumu haya mawili. Haya ni majukumu mawili ya msingi ya binadamu anayoyafanya bila kujijua, ambayo utekelezaji wake ndio utakaoleta furaha kwa wanaadamu. Mwanamke kwa asili hutaka amani, sio vita.

Inaonekana kwamba katika jamii nyingi za viumbe, mwanamke hana silika ya ugomvi na ukorofi kabisa. Akiamua kupigana, basi ni kwa ajili ya watoto wake. Mwanamke ana subira zaidi kuliko mwanaume ingawa mwanaume ni jasiri zaidi katika kukabiliana na kazi za hatari na matatizo katika maisha. Ana uvumilivu mkubwa zaidi, na anaweza kukabiliana na ugumu na kero ndogo ndogo nyingi tu vizuri zaidi. Roho yake ya kupenda vita au ujasiri inaishia katika kupenda kuiona sifa hii kwa wengine. Anawapenda askari na wanaume wenye nguvu na majabari, kwa sababu hii anaweza kushawishiwa na fikra ya kufurahia au kupata ashiki kutokana na kuumia (masochism) na anaweza kuwa mhanga wa nguvu za kiume.

Moyo wa kupenda nguvu na ushujaa wakati fulani huyafunika hata maslahi yake ya kiuchumi, na wakati mwingine huchagua kuolewa na mtu shujaa (na kumuacha tajiri). Humkubali kwa furaha mwanaume ambaye hutoa amri kwa wengine kwa njia ya haki na uadilifu. Kama wanawake sio watii kiasi hicho siku hizi, tofauti na walivyokuwa zamani, ni kwa sababu wanaume siku hizi ni dhaifu, hawana nguvu kama zamani na mazingira yanayowazunguka. Silika yake humfanya apende desturi za zamani. Kimwili na kiakili hapendi kujaribujaribu vitu kama vile kuzini kabla ya ndoa n.k ingawa baadhi ya wanawake wanaoishi katika miji mikubwa wanaweza kuwa tofauti. Akiamua kufanya mapenzi (ngono) nje ya ndoa, si kwa sababu anataka uhuru katika hilo (ngono), bali ni kwa sababu bado hajapata mume mwaminifu na muwajibikaji.

Ikiwa katika ujana wake alipata kuvutiwa na shughuli za siasa na akawa anatamani kufanya kazi katika fani mbali mbali na tofauti za kazi, kwa kawaida huachana na kazi hizo baada ya kupata mume mwaminifu na mara moja hujiondoa yeye na mume wake katika mambo ya umma. Humkumbusha mume wake kuwa uaminifu na uwajibikaji wake aurudishe nyumbani kwake kwa kuwa mwanamke hahitaji kufikiri sana kujua kwamba mageuzi yote huanzia nyumbani. Anapofanikiwa kumrudisha mwanaume mbunifu na mzururaji nyumbani na kumfanya aiangalie nyumba na watoto wake, basi kusalimika na kuendelea kuishi kwa mwanadamu kunamtegemea yeye.

Kwa asili hahusiki na mambo ya sheria na serikali. Nyumba na watoto ndio vitu anavyovipenda. Akishafanikiwa kuvitazama na kuvitunza vizuri, hajali ni serikali gani inaingia madarakani na ni serikali gani inaondoka madarakani. Maumbile hayajali juu ya sheria za serikali. Vitu vya maana kabisa kwa maumbile (nature) ni nyumba (familia) na mtoto. Yakifanikiwa kuvihifadhi hivi vitu viwili, hayashughulishwi tena na mambo ya serikali, na huwacheka wale wanaojaribu kubadili sheria za msingi.

Kama leo maumbile yanayoonekana kushindwa kuihifadhi familia (nyumba) na mtoto, hii ni kwa sababu mwanamke tangu siku nyingi ameyasahau maumbile. Lakini kushindwa kwa maumbile sio kwa kudumu. Yanaweza kuwapatia mamia ya manufaa yalionayo, yakiruhusiwa na kupewa nafsi ya kufanya hivyo. Kuna mataifa na watu wa rangi nyingi sana kuliko tulivyo na maumbile yanayohakikishia kuendelea kuishi na kudumu kutokana na faida ambazo maumbile yanazo.

9

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

- I MAHARI NA MATUNZO

Ni moja ya desturi za zamani za mahusiano ya kifamilia ya mwanadamu kwamba wakati wa kuoa mwanaume hulipa mahari kwa mwanamke (anayemuoa) au kwa baba yake (huyo mwanamke). Na mbali na hili, hujitolea kugharamia gharama zote za mke wake na watoto katika kipindi chote cha uhai wake. Ni nini msingi wa desturi hii? Ni kwa nini na ni kwa namna gani? Ni nini mantiki ya mahari? Je mahari na matunzo bado ni mambo yanayofaa kuendelezwa hadi sasa, hata kama mwanaume na mwanamke wana haki sawa za kibinadamu na za asili na mahusiano baina yao yamejengwa kwa msingi wa uadilifu na usawa? Au ni mabaki (masalia) yaliyobakia ya enzi zile ambapo mwanaume alimmiliki mwanamke? Je uadilifu na usawa wa haki, hasa katika karne hii unaamrisha kuwa desturi hizi zilizopitwa na wakati zipigwe marufuku? Na kwamba ndoa ifungwe bila mahari? Na mwanamke ajitunze mwenywe? Na kwamba jukumu la kulea watoto (gharama zake) liwe jukumu la kuchangia wote wawili, mke na mume?

Tunataka kujibu maswali haya, na tutaanza na swali la mahari. Hebu tuangalie jinsi hii desturi ilivyoanza, falsafa yake ni nini na jinsi wanasosholojia wanavyoeleza chanzo /asili yake: Historia fupi ya mahari. Inasemekana kwamba zamani kabla ya historia kuanza kuandikwa, mwanadamu aliishi maisha ya kishenzi, yaliyokuwa na muundo wa kikabila. Kwa sababu zisizojulikana ndoa kati ya ndugu wa damu moja ilikatazwa. Hivyo vijana wa kiume wa kabila waliotaka kuoa, walilazimika kuchagua wake zao kutoka katika kabila jingine. Mara nyingi waliyatembelea makabila mengine kwa madhumuni haya.

Enzi hizo mwanaume hakuwa anajua jukumu lake katika kusababisha mimba (yaani hakujua kama tendo lake la ndoa ndilo linalosababisha mimba). Alifikiri kuwa mtoto alikuwa ni mali ya mama kwa asilimia mia moja. Ingawa aliona watoto wakifanana naye sana. hakujua sababu ya kufanana huko. Kwa hali hii watoto nao walifikiri kuwa walikuwa ni mali ya mama yao na sio baba yao. Wakati huo ukoo ulitambulishwa kwa kupitia mfumo jike. Wanaume walionekana kuwa ni wagumba na tasa. Baada ya ndoa, waliishi na watu wa kabila la mke wake kama kiambatanishi tu, kwa sababu mwanamke alihitaji uswahiba wa mume wake.

Kipindi hiki kinajulikana kama kipindi cha mfumo jike (matriarchy). Haikuchukua muda mrefu, mwanaume akagundua jukumu lake katika uzazi (utungaji mimba) na akaamini kwamba kumbe kiuhalisia watoto walikuwa ni wake. Kuanzia wakati huo na kuendelea, alimtawala mwanamke na akajipa cheo cha ukuu wa familia. Hivyo, kipindi cha mfumo dume, kikaanza. Katika kipindi hiki pia ndoa ya ndugu wa damu moja ilikatazwa. Mwanaume alipaswa kuchagua mke kutoka katika kabila (au ukoo) mwingine, na kumleta katika kabila lake. Kwa vile kulikuwa na hali ya kutokuelewana baina ya makabila kutokana na vita vya kikabila, njia pekee ya kupata mke ilikuwa ni kumdaka na kumbeba kwa nguvu binti wa kabila jingine.

Pole pole maelewano na amani yakachukua nafasi ya mapigano na magomvi, na makabila mbali mbali yakaweza kuishi pamoja kwa amani. Katika kipindi hiki mila ya kuwadaka na kuwabeba kwa nguvu wasichana ilipigwa marufuku. Ili kumpata mke aliyempenda, mwanaume alipaswa kwenda kufanya kazi kwa baba wa msichana huyo kwa muda fulani. Kwa kuzingatia kazi alizozifanya hapo ukweni, baba wa msichana alimuozesha kwa huyo mwanaume, naye alimchukua na kwenda naye kwenye kabila lake. Mfumo wa malipo wa fedha ulipoenea, mwanaume aligundua kuwa badala ya kufanyakazi kwa baba wa bibi harusi kwa miaka, ilikuwa ni bora zaidi kupeleka ukweni zawadi maridhawa na kumchukua msichana mara moja. Huu ndio ukawa mwanzo wa mahari.

Kwa mujibu wa nadharia hii, katika siku za mwanzo mwanaume aliishi kama kiambatanisho cha mwanamke na alimtumikia (mwanamke). Katika kipindi hiki mwanamke alimtawala mwanaume. Katika hatua inayofuata, madaraka yalipohamia mikononi mwa mwanaume, aliteka nyara wanawake kutoka katika kabila jingine. Wakati wa hatua ya tatu, ili kumpata mwanamke, mwanaume alikwenda kwa baba wa mwanamke na kumhudumia kwa miaka kadhaa.

Wakati wa hatua ya nne, mwanaume aliwasilisha kiasi cha fedha kwa baba wa mwanamke. Na hivyo ndio desturi ya mahari ilivyoanza. Inasemekana kwamba tangu wakati mtu alipofutilia mbali mfumo jike na kuweka msingi wa mfumo dume, alimpa mwanamke hadhi ya utumwa au zaidi kama mfanyakazi au mtumishi wake. Alimchukulia kama chombo cha uchumi, ambacho kwa njia nyingine ataweza kukidhi matamanio yake vile vile. Hakumpa uhru wa kijamii au wa kiuchumi. Mapato ya kazi ya mwanamke yalikuwa ni mali ya baba au ya mumewe.

Hakuwa na haki ya kujichagulia mume wake, wala kuendesha shughuli yoyote ya kiuchumi kwa ajili yake mwenyewe. Fedha ambayo mwanaume amelipa kama mahari na gharama ambazo anatoa kama matumizi (nafaqah) zilikuwa kabisa zinatokana na pato la uchumi ambalo amelipata kutoka kwa mwanamke katika kipindi cha wakati wa mahusiano ya ndoa. Mahari katika mfumo wa haki wa Kiislamu. Kuna hatua ya tano pia ambayo wanasosholojia na wasomi wengine hawakuisema.

Katika hatua hii mwanaume humpa zawadi mwanamke. Wazazi wote wawili wa mwanamke hawana haki ya kuidai zawadi hiyo. Mwanamke hupokea zawadi, lakini hubaki na uhuru wake wa kiuchumi na kijamii. Humchagua mume kwa hiari yake mwenyewe, bila kulazimishwa na baba wala kaka. Na zaidi ya hayo, si baba wala mume wake mwenye haki ya kumnyonya. Matunda ya kazi na jasho lake ni mali yake binafsi, na hakuna mwenye haki ya kumuingilia juu ya mali hiyo.

Katika masuala ya kifedha hahitaji uangalizi au usimamizi wa yeyote. Mume ana haki moja tu. Anaweza kufurahia tendo la ndoa na mke wake. Katika muda wote wa ndoa yao, mwanaume anawajibika kumtimizia mkewe mahitaji yote ya halali kwa mujibu wa uwezo wake. Hii ndio hatua inayotambuliwa na Uislamu na ambayo juu yake Uislamu umejenga msingi wake wa mahusiano ya ndoa. Aya nyingi za Qur'ani zinasisitiza kuwa mahari ni mali ya mwanamke. Na mbali na mahari, mwanaume anapaswa kumtunza na kubeba gharama zote za mkewe.

Na wakati huo huo chochote anachokipata mwanamke ni mali yake peke yake na sio ya mtu mwingine yeyote, sio ya baba yake wala mume wake. Hapa ndipo suala la mahari na matunzo linapotatanisha kidogo. Maadamu mahari inalipwa kwa baba wa msichana na anakwenda kwenye nyumba ya mume kama mtumwa na mume akawa na mamlaka ya kumnyonya, hapa suala lingekuwa rahisi kueleweka. Mahari ililipwa kama bei ya msichana na alipaswa kutunzwa kama mtumwa mwingine yeyote. Sasa kwa vile baba wa msichana hakulipwa chochote, mume haruhusiwi kumnyonya mke wake, mwanamke ana uhuru kamili wa kiuchumi, na kuhusiana na haki zake hahitaji usimamizi, udhibiti au uangalizi wa mtu yeyote.

Sasa kwa kuwa mambo yako hivi kuna maana gani ya kulipa mahari na kugharamia matunzo? Tuitazame historia kidogo. Ili tuweze kuelewa falsafa ya mahari na matunzo katika hatua hii ya tano, tunapaswa kuitazama kiumakinifu nadharia ya vipindi vinne iliyotajwa hapo juu. Ukweli ni kwamba yote yaliyosemwa juu ya vipindi hivi si chochote zaidi ya nadharia tete iliyojengwa juu ya dhana na makisio tu. Hayana taarifa za kihistoria wala ukweli wa kisayansi.

Hatuna elimu ya uhakika juu ya mwanadamu aliyeishi kabla ya kuanza kuandikwa kwa historia. Yote yaliyosemwa juu ya kipindi cha mfumo jike, akina baba kuwauza binti zao, na wanawake kunyonywa kiuchumi na waume zao, si ya kuaminika sana. Kuna mambo mawili yaliyoisumbua akili juu ya dhana na makisio. La kwanza ni kuwa mtu duni (wa kale) amewakilishwa kama mtu mshenzi, mgomvi na asiyekuwa na hisia za kibinadamu. Jambo la pili ni kuwa mpangilio wa ajabu wa maumbile katika kufikia malengo yake umepuuzwa. Tafsiri hii ya asili ya mwanadamu pengine inaweza kutolewa na watu wa Magharibi na sio watu wa Mashariki isipokuwa wale watu wa Mashariki ambao wanafuata mila za Kimagharibi kwa sababu fulani fulani, mzungu hazifahamu vizuri hisia na mawazo ya kibinadamu.

Hawezi kukiri kuwa ana mchango wa msingi katika historia. Kutokana na uchu wake wa kiuchumi, akili yake yote iko kwenye mkate na siagi. Huitazama historia kama mashine, ambayo huwa haitembei mpaka iwekewe mafuta. Kama mwelekeo wake ni ngono huwaona wanaadamu wote na historia ya mwanadamu, pamoja na utamaduni wao, sanaa, maadili na dini kama miundo iliyorekebishwa ya mchezo wa ngono. Kama maoni yake ni ya kisiasa, basi huiona historia yote ya mwanadamu kuwa ni mfululizo wa vita, umwagaji damu na vitendo vya ukatili. Mzungu aliteswa mno kwa kutumia jina la dini katika zama za kati, ambapo watu mara nyingi walikuwa wakichomwa moto wakiwa hai, kiasi cha kuwa amekuwa na mzio na jina la Mungu, dini na vitu vyote vinavyowakilisha dini.

Hii ndio sababu, licha ya ushahidi wote wa ukweli kwamba maumbile yana makusudio na mfumo wa ulimwengu haufanyi kazi kwa bahati nasibu hajathubutu kukiri kuwepo kwa 'Sababu Sababishi' (yaani Mwenyezi Mungu). Hatuwaombi wafasiri wa historia wa Kimagharibi kukiri kuwepo kwa mitume, waliokuwa wakitokea katika historia yote ya mwanadamu kuja kutangaza ujumbe wa uadilifu na ubinadamu na kupiga vita ufisadi, mambo ambayo waliyafanikisha kwa ukamilifu. Tunachowataka ni angalau wasipuuzie jukumu la utambuzi waliopewa na maumbile.

Hakuna shaka kwamba katika historia ya uhusiano wa mwanaume na mwanamke, kumekuwa na matukio mengi ya ukatili uliopindukia, na mengine yakiwa ni maovu mno, ambayo yamesimuliwa katika Qur'ani pia, lakini hatuwezi kusema kwamba historia yote ya mwanadamu ilikuwa imejaa vitendo vya ukatili na mapigano. Falsafa ya kweli ya mahari Kwa mujibu wa imani yetu, mahari ilikuja kutokana na mipangilio makini, iliyowekwa katika usanifu wa uumbaji ili kuweka sawa uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke. Mahari imetokea (imekuwepo), kwa sababu, kwa asili majukumu ya mwanaume na mwanamke kila mmoja kwa mwenzake yako tofauti. Kwa mujibu wa mafunzo ya dini sheria ya mapenzi na mvuto ipo kila sehemu ulimwengu. Kwa vile kila kitu kimetengenezwa ili kutekeleza kazi maalum, basi majukumu yake ni tofauti na vitu vingine vyote.

Tulipokuwa tukijadili tofauti kati ya mwanaume na mwanamke, tulishaeleza tayari kuwa hisia na shauku zao kuhusiana na kila mmoja, hazifanani. Sheria ya uumbaji imeshaamuru kuwa mwanamke awe na sifa za urembo (uzuri), fahari na kutojali ambapo mwanaume awe na sifa za kubembeleza na kushughulika. Hivi ndiyo udhaifu wa kimwili wa mwanamke ulivyofidiwa, na kwa sababu hii mara zote mwanaume ndiye amekuwa akimtaka mwanamke pamoja na kutoa pendekezo la kuoa.

Kama tulivyoona huko nyuma kwa mujibu wa wanasosholojia katika vipindi vyote vya mfumo jike na mfumo dume, ni mwanaume ndiye amekuwa akimtaka mwanamke. Wanasayansi wanasema kwamba mwanaume ana uchu (tamaa) zaidi (ya ngono) kuliko mwanamke. Baadhi ya hadithi za Kiislamu zinasema kuwa mwanaume hana tamaa (uchu) zaidi. Ilivyo, mambo ni kinyume chake lakini mwanamke ana uwezo zaidi wa kujizuia. Kivitendo, maoni yote mawili yanaleta kitu kimoja.

Hata hivyo, ni jambo la hakika kwamba mwanaume ana uwezo mdogo zaidi wa kujizuia. Sifa hii imemuwezesha mwanamke asimfuate (asianze kumtaka) mwanaume, wala kujipeleka kwake kirahisi. Silika ya mwanaume humlazimisha kumwendea na kumtaka mwanamke, na huchukua hatua kadhaa ili ampate. Moja ya hatua hizi ni kumpa zawadi. Wanaume mara zote wamekuwa wakichuana kumpata mwanamke (msichana). Wamekuwa hata wakipigana ili kufikia lengo hili.

Lakini wanawake kamwe hawajapata kuonyesha umakini na shauku kama hii ya kumpata mwanaume. Mambo yako hivi kwa sababu majukumu ya mwanaume na mwanamke kila mmoja kwa mwenzake sio sawa. Mwanaume mara zote humfukuzia mwanamke wakati mwanamke humuonyesha hali fulani ya kutokumjali. Mahari yanahusiana sana na staha na usafi wa kimaadili (hususan kutozini). Mwanamke anafahamu kwa silika kuwa heshima na staha yake vinataka asijitoe bure kwa mwanaume.

Hivi ndivyo mwanamke alivyo, licha ya udhaifu wake wa kimwili aliweza kuwapigisha magoti wanaume, kuwalazimisha kuchuana vikali na kuwafanya akina Romeo kuwakimbilia akina Juliet. Mwanamke anapokubali kuolewa na mwanaume, hupokea zawadi kutoka kwa huyo mwanaume kama ishara ya urafiki, furaha na dhamira njema. Inasemekana kwamba miongoni mwa makabila ya kishenzi, msichana alipokuwa na waposaji zaidi ya mmoja alikuwa akiwashawishi wapigane mapigano rasmi ili kutetea hadhi yao. Aliyeshinda au kumua mwenzake (mpinzani wake) alionekana ndiye anayefaa kumuoa msichana huyo.

Kulikuwa na habari kwenye gazeti kwamba msichana mmoja katika mji wa Tehran aliwashawishi wavulana wawili kupigana ili kutetea hadhi yao mbele yake. Kwa wale wanaofikiri kuwa nguvu ni mabavu ya kikatili na wanashikilia kuwa historia ya uhusiano wa mwanaume na mwanamke haina chochote zaidi ya vitendo vya ukatili na unyonyaji, si jambo linaloaminika kwamba jinsia dhaifu na ya kike inaweza kuwashawishi watu wawili wa jinsia yenye nguvu kushambuliana/kupigana.

Lakini kwa wale wenye elimu kidogo juu ya nguvu ya ajabu ambayo maumbile yamempa mwanamke, hapa hakuna kitu cha ajabu. Mwanamke ana ushawishi mkubwa sana kwa mwanaume. Ushawishi wa mwanamke kwa mwanaume umekuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa mwanaume kwa mwanamke. Mwanaume anamhitaji sana mwanamke, na pia anauhitaji sana ucheshi wake, usafi wake wa kimaadili na staha ili apate mafanikio katika sanaa na medali za ujasiri.

Sifa ya kujenga watu wenye haiba kubwa na wenye vipaji vikubwa inamrudia yeye. Mwanamke anamjenga mwanaume na mwanaume anaijenga jamii. Mwanamke akipoteza sifa ya usafi wa kimaadili, staha na kujizuia, na akajaribu kufanya majukumu ambayo ni ya mwanaume, kwanza mwanamke huyu anaweza kujishushia hadhi, kisha mwanaume anaweza kupoteza uanaume wake, na mwisho wa safari jamii inaweza kuangamia.

Ustadi ule wa mwanamke, umemuwezesha kudumisha haiba yake katika kipindi chote cha historia, kumlazimisha mwanaume kwenda katika mlango wake, kama mchumba, kumshawishi mwanaume kuingia katika uadui na hata kupigana kwa ajili yake, kudumisha staha na usafi wa kimaadili kama nembo yake ya ubora, kuuficha mwili wake usionekana kwa wanaume, kumhamasisha mwanaume apende kufanya matendo magumu ya kishujaa, kama rasilimali takatifu, kufanya vizuri katika mambo ya kiakili na matendo ya ubunifu, kuimba nyimbo za mapenzi na kunyenyekea mbele ya jinsia dhaifu kwa unyenyekevu mkubwa.

Kwa hiyo tabia hii imemlazimisha mwanaume kutoa zawadi kwa bibi harusi wakati wa ndoa kama mahari. Mahari ni sehemu ya sheria ya maumbile, ambayo imeanzishwa na maumbile yenyewe. Mahari katika Qur'ani Muundo wa mahari ulioelezwa hapo juu kuhusiana na hatua ya tano sio ubunifu wa Qur'ani. Qur'ani ilichokifanya ni kuurejesha katika muundo wake wa asili na mzuri kabisa. Qur'ani inasema kwa ufasaha:"Wapeni wanawake mahari yao, hali yakuwa ni hadiya (ziwadi) " (Suratul Nisa 4:4).

Hii ina maana kwamba mahari ni haki ya wanawake (hao wanaoolewa) na ni zawadi wanayopewa wao moja kwa moja. Haiwahusu baba na kaka zao. Katika sentensi hii fupi Qur'ani imetaja nukta tatu za msingi: Kwanza: imetumia nenoSaduqatihinna (yaani ukweli na uaminifu) badala ya neno mahari. Hivyo mahari ni alama ya ukarimu na wema wa mwanaume anayeilipa. Nukta hii imeelezwa na wafasiri mbalimbali mashuhuri wa Qur'ani Tukufu, kama vile Zamakhshari, mwandishi wa tafsir mashuhuri ya Qur'ani iitwayo Kashshaf. Halikadhalika mwanasayansi wa asili na maendeleo ya lugha, Righib Isfahani amesema katika kamusi yake ya Qur'ani kuwa mahari imeitwa Saduqah kwa sababu ni alama ya uaminifu wa imani.

Pili: ni dhahiri kutokana na Aya hiyo ya Qur'ani kuwa mahari inapaswa kulipwa kwa mwanamke moja kwa moja, na wazazi wa mwanamke hawapaswi kudai chochote katika mahari hiyo. Mahari sio fidia ya jitihada walizozifanya wazazi katika kumlea binti yao.

Tatu: ni dhahiri pia kuwa mahari si chochote zaidi ya hadiya na zawadi. Sifa ya hisia (za kimapenzi) miongoni mwa wanyama. Sheria ya mahusianao ya kimapenzi haiwahusu binadamu peke yao bali hata wanyama. Ingawa jinsia zote mbili zinahitajiana, jinsia ya kiume huhisi haja kubwa zaidi kwa ajili ya mwanamke, na huanzisha jitihada za kumpata. Hii ndio sababu mwanaume/dume huwa hatumii vibaya nguvu nyingi alizonazo (kumuonea mwanamke /jike), na huonyesha wema kwa mwanamke.

Zawadi katika mahusiano haramu Hata mwanaume na mwanamke wanapotaka kufurahia ngono katika mahusiano haramu (nje ya ndoa), ni mwanaume ambaye humpatia mwanamke zawadi. Wanapopata chai, kahawa au chakula pamoja ni mwanaume ambaye huona kuwa ni jukumu lake kulipa bili. Mwanamke huona kuwa ni matusi kutakiwa kumlipia mwanaume. Baadhi ya watu hudai kuwa mvulana anahitaji uwezo wa kifedha ili kujiingiza katika zinaa ambapo kwa msichana hiyo ni njia ya kujipatia zawadi. Mila hizi ambazo tunazikuta katika mahusiano halali (ya ndoa) na haramu (ya nje ya ndoa) zinatokana na kutofautiana kwa hisia za mwanaume na mwanamke za kila mmoja kwa mwenzake. Mzungu ana mahusiano ya asili zaidi katika kufanya mapenzi ya haramu kuliko katika ndoa.

Katika nchi za Magharibi ambako hali za kifamilia zimeharibiwa kwa jina la usawa wa haki za binadamu, na jitihada inafanyika kugawa majukumu sawa ya kazi za ndani (kama kupika, kudeki n.k) lakini bado mwanaume anatekeleza majukumu yake ya asili katika mahusiano ya nje ya ndoa. Katika mahusiano ya nje ya ndoa, bado mwanaume hutoa zawadi kwa mwanamke na hubeba gharama za huyo mwanamke, lakini katika ndoa, sio tu kwamba hakuna mahari, lakini mwanamke pia hubeba mzigo mkubwa wa gharama za matumizi ya nje ya nyumbani. Hii ina maana kuwa kwa wazungu mapenzi nje ya ndoa ni ya asili zaidi kuliko mapenzi ndani ya ndoa ya kizungu. Mahari ni mfano unaoonyesha kuwa mwanaume na mwanamke wameumbwa kwa vipaji tofauti na sheria ya maumbile imewapangia haki za asili zisizofanana.


6

7

8

9

10

11

12

13