8 UKWELI WA USHIA
KUTAWASSALI KUPITIA KWA MAWALII WA MWENYEZI MUGNU
Salaamun alaykum.
Oh..ni akina nani hawa makafiri na mazindikiwanao jiita
kuwa ni waislaam. Jihadharini.. kutokana na watu hawa.
Unawakusudia watu gani?
Hawa Mashia.
Usiwatukane, na wala usiwanasibishe katika ushirikina, kwani wao ni Waislaam.
Watu hawa ni bora zaidi kuuwawa kuliko hata makafiri.
Ni ghadhabu gani hii isiyo kuwa na hisia za ubinadamu uliyo nayo, kwa nini wao wawe washirikina?
Hakika wao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu na kumuwekea waungu wengine, na wanamuabudu Mungu mwingine asie kuwa Allah asie wadhuru wala kuwanufaisha.
Wanamshirikisha vipi Mwenyezi Mungu?
Wao wanafanya tawassuli kupitia kwa Mitume, maimam na mawalii wa Mwenyezi Mungu ili awakidhie haja zao na wanasema: Ewe Muhammad ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ewe Ali, ewe Husein, ewe Swahibuz-zaman)
na mengineyo wakidai ya kuwa mawalii hawa wanauwezo wa kukidhi haja zao. Na hili si jambo lingine bali ni ushirikina wa wazi kabisa na ukafiri, na ni kumuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu.?
Nina mazungumzo kiasi ni ruhusu tuweze kuzungumza.
Sema unacho taka kukisema.
Mimi nilikuwa ni miongoni mwa watu walio kuwa wakiwabebesha na kuwatwisha Mashia aina tofauti za matusi na shutuma, na nilikuwa sikai chini wala kusimami isipokuwa nitawatukana na kuwatuhumu, na yote nikiyafanya nikiwa mbali nao, mpaka safari ya hija ilipo nikutanisha na mmoja wa Mashia, na nilipo zungumza nae nilikuwa mkali na nikizungumza kwa ukali na nilito aina zote za matusi na maneno mabaya yaliyo kuwa yakinikera kifuani mwangu kutokana na ghadhabu niliyo kuwa nayo kwa miaka mingi, na Shia yule hakuna alicho kifanya isipokuwa alikuwa na subira kwa yale niliyo kuwa nikiyasema, na kuyanyamazia, na huku akinicheka, na bashasha au furaha ndiyo iliyo kuwa ikionekana na kudhihiri usoni mwake, na mimi kila nilivyo kuwa nikizidisha matusi kwake ndivyo alivyo zidisha ukunjufu usoni mwake na akinipoza kwa lile harara nililo kuwa nalo kwa tabasamu ambazo zilikuwa hazikatiki midomoni mwake, tabia ile njema ilizima moto na harara nililo kuwa nalo la kuwafanyia uadui na kuwatukana.
Na mimi nilipo nyamaza, akanielekea kwa maneno akisema: Ewe ndugu yangu katika dini..Muhammad je unaniruhusu nizungumze nawe maneno kadhaa? Kisha akasema, nami nikasema, akasema..nami nikasema, akasema..nami nikasema..hadi ikanibainikia na kunidhihirikia ya kuwa wana haki katika maudhui mengi sana ambayo tuliyazungumzia. Na miongoni mwa maudhui niliyo yaona kuwa wanahaki katika maudhui hayo ni maudhui ya kutawasuli kupitia kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu.
Je uliathirika na uongo wao, hadaa zao na ushirikina wao..ni kwa kiasi gani umekosa muongozo katika dini, na ni kwa kiasi gani umekosa maarifa ya kiislaam!
Kwa hakika mimi kwa hivi sasa niko tayari kujadiliana na wewe kuhusu maudhui ya kutawasali kupitia kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu, kwa mujibu wa Qur'ani yenye hekima, na Sunna tukufu na Mwenendo wa Watu wema kati ya waislaam.
Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu ni mpole sana kwa waja wake kuliko viumbe wengine, na hakuna kizuizi chochote kati yake na waja wake, kwa hivyo basi ni juu ya kila mja kufanya mawasiliano na Mwenyezi Mungu mtukufu- moja kwa moja bila ya kuwa na wasila wa aina yoyote kwa muda wowote ule, na katika sehemu zote, yaani afanye mawasiliano na Mwenyezi Mungu moja kwa moja na atawasali kwake yeye mwenyewe, kwani haijuzu kutawasali kupitia kwa yeyote asie kuwa Mwenyezi Mungu vyovyote cheo chake kitakavyo kuwa kikubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, hata kama atakuwa ni Mtume au Imam au mfalme au mja mwema na wengineo.
Kwanini haijuzu kufanya hivyo?
Kwa sababu mwanadamu anapo fariki anakuwa ametoweka na kumalizika, na alie kwisha toweka na kumalizika haiwezekani kufaidika nae, sasa vipi utatawasali na mtu alie toweka na kumalizika?
Utasemaje kuwa mauti ni kumalizika, nani anae itakidi na kusema hivyo?
Imam Muhammad bin Abdul wahhab amesema: Kutawasali kupitia watu wema walio fariki ni sawa na kukizungumzia kitu kilicho toweka na kumalizika na kisicho kuwepo, na tendo hilo ni tendo baya kiakili. Na imenukuliwa kutoka kwa mmoja wa wafuasi wake au ilimfikia habari na kuiridhia ya kuwa (Fimbo yangu hii ni bora kuliko Muhammad, kwa sababu hufaidika nayo kuulia nyoka na nge na mfano wa hivyo na Muhammad amekufa na hana manufaa tena)
- Kwa hivyo haya na mengineyo yanatujulisha juu ya ubaya wa kutawasali kupitia kwa maiti hata kama atakuwa ni Nabii au Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Ukweli ni kinyume na unavyo sema, kwani mwanadamu anapo kufa hufunukiwa na kuona ulimwengu zingine ambazo hazikuwa ni zenye kumfunukia kabla ya kufariki kwake. Mwenyezi Mungu mtukufu anasema:Tumekuondolea pazia lako na kuona kwako leo kuwa kukali. suratul-qaf aya 22. Pia amesema Mwenyezi Mungu mtukufu (Wala msiseme kwamba wale walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai lakini nyinyi hamtambui). Suratul-baqarah aya ya 154. Na pia anasema (Wala usidhani wale walio uliwa katika njia ya Mwenyeezi Mungu kuwa ni wafu, bali ni hai wanaruzukiwa kwa Mola wao) suratu Al-imraan aya 169.
Na katika Bukhari
imepokelewa kuwa Mtume
alifika kwenye shimo Walilo zikiwa washirikina walio uwawa katika vita vya Badri na kuwazungumzia washirikina kwa maneno yafuatayo: (Hakika sisi tumepata tuliyo ahidiwa na Mwenyezi Mungu na tumekuta kuwa aliyo tuahidi ni kweli, je ninyi mmeyakuta aliyo waahidi mola wenu ni ya kweli) akaulizwa je unawauliza watu walio kufa? Mtume
akasema: (Hakika nyinyi si wenye kusikia zaidi kuliko wao)
. Hakika mwanadamu sawa awe muumini au kafiri anapo kufa hawi kama kitu kisicho na hisia kisicho ona wala kusikia. Na Ghazaliy
nae akiwa ni mmoja kati ya maimamu wa madhehebu ya Shafiiy amesema: (Baadhi wakidhania kuwa kifo ni kutoweka kabisana hii ndio rai ya walahidi (wasio muamini Mungu..).
.
Imam Ghazaliy anaona kuwa kauli ya kutoweka kabisa kwa mwanadamu kupitia kifo ni Ilhadi (kufru)? Hayo ameyasema wapi?
Ameyataja katika kitabu chake kiitwacho ( Ihyaaul-uluum)
rejea kitabu hicho, utaipata nassi ya haya tuliyo yasema na kuyataja.
.
Maneno haya ni ya ajabu kutoka kwa mtu kama Ghazaliy!
Hilo si jambo la ajabu kutoka kwa Ghazaliy bali la ajabu ni hili litokalo kwako ya kuwa huyafahamu hayo. Je hukusikia Mtume
alivyo wazungumzia washirikina katika kisima cha badri, na lau kama wangekuwa wametoweka kabisa kwa kufa kwao, hawasikii wala kufahamu, Mtume
asinge wazungumzisha, pamoja na kuwa Mtume
alisema: (Nyinyi si wenye kusikia zaidi kuliko wao).
Hiyo ina maana kuwa wao wanasikia kama msikiavyo, na wanafahamu kama mnavyo fahamu. Je umekinaika na haya?
Ndio nimekinaika. Lakini mimi ninatahayari ni vipi mimi katika muda wa miaka yote hiyo sikuwa ni mwenye kudadisi na kuiangalia kwa makini aya hii ili niweze kuyafikia maana haya?! Ni vipi sikuisikia hadithi hii ya Mtume
, na kauli hii ya Imam (Ghazaliy)?
Je hadi hivi sasa umeamini nusu ya kauli za Mashia ya kuwa: Mtu hatoweki kabisa kwa kufariki? Au bado unashaka?
Hapana..hakuna shaka yoyote niliyo bakia nayo katika hilo, lakini mimi ninautata katika jambo lingine!
Ni utata gani huo?
Utata wenyewe ni kuwa, inakuwaje ibnu Abdul-wahhab anaitakidi ya kuwa mtu anatoweka kabisa kwa kufariki, pamoja na kuwa Ghazaliy anasema ya kuwa hayo ni maneno ya walahidi? Pamoja na kuwa Mtume
anasema wazi ya kuwa mtu alie fariki (mfu) anasikia kama asikiavyo mtu alie hai na hakuna tofauti kati yao? Kisha nivipi ibnu Abdul-wahhab na wengineo wanasimama kwa ushupavu bila woga na kusema: (Fimbo yangu hii ni bora kuliko Muhammad, kwani fimbo hii inamnufaisha mtu, na Muhammad hamnufaishi mtu kwa chochote) ?!
Haya ndio yaliyo nifanya nitahayari.
Usitahayari. Kwa hakika sisi inatulazimu kuwafahamu watu kutokana na kufuata kwao misingi ya dini, kwa maana kila mtu ambae kauli zake na matendo yake yanawafikiana na Qur'ani na Sunna na sira ya waja wema walio tangulia (As-salaf-s-swalih) huyo ndio muumini, si kuifahamu dini kupitia watu fulani, kwani sisi tutakapo mfahamu fulani mtoto wa fulani kwa mfano ya kuwa ni muumini mwenye ikhlasi haijuzu kuzihesabu kauli zake na matendo yake kuwa ni sehemu ya Uislaam, hata kama tutayaona na kufahamu waziwazi ya kuwa yanapingana na kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake
na sira ya waja wema walio pita, na kwamba hiyo ni kufru na ilhadi, bali lililo wajibu kwetu, wakati tunapo ona upotovu kwa mtu yeyote vyovyote atakavyo kuwa cheo chake ni wajibu kwetu kujitenga nae na kuwa mbali nae, na kuifuata haki iliyo tudhihirikia na kuiona.
Maneno yako ni sahihi..na mimi ni miongoni mwa waumini walio kuwa na imani kubwa kwa mtu huyu, na hivi sasa umenionyesha na kunifahamisha makosa makubwa ya mtu huyu, ambayo huzingatiwa kuwa ni ilhadi na kufru katika dini, kwa hakika imani yangu kwake imetoweka, na sinta mzingatia kuwa ni mwanazuwoni ambae anafaa kuchukua kutoka kwake hukumu za kiislaam.
Achana na kumzungumzia Ibnu fulani, ili tuweze kuzungumzia mambo mengine.
Ndio..ni kweli kuwa maiti hatoweki na wala hamaliziki kabisa kwa kufariki kwake, lakini inajuzu vipi kutawasali kupitia kwake ikiwa ni Mtume au Imam au ni katika watu wema? Pamoja na kuwa tunafahamu ya kuwa kuna watu waizingatiao tawassuli kupitia kiumbe ni shirki na ni kutoka katika dini?.
Je inajuzu kutawasuli kupitia kwa mtu alie hai, na kumuomba haja fulani, au kumuomba dua na mengineyo, kwa mfano kusema: Ewe Baaqir, au Ewe Jaafar, au Ewe Ridhaa au Ewe fulani..nipatie Dinari, au niombee kwa Mwenyezi Mungu anisamehe, au nishike mkono hadi msikitini na mengineyo yasiyo kuwa haya?
Ndio inajuzu kufanya hivyo.
Kwa hivyo baada ya kuthibiti ya kuwa maiti anasikia kama asikiavyo mtu alie hai, ni kizuizi gani kizuiacho kutawasali kupitia kwa maiti baada ya kufariki kwake, na kumuomba haja fulani? Waliid aliinamisha kichwa chake na kufikiria ..kisha akainua kichwa chake na kusema: Ndio ni kama usemavyo ewe Muhammad, maneno yako ni sahihi.
Ni nani alie tawassali kupitia kwa Mtume
baada ya kufariki kwake?
Ifuatayo ni baadhi ya mifano hai ya watu walio fanya hivyo: Amepokea Baihaqiy
na Ibnu Abi Shaibah kwa sanadi sahihi. Kama ilivyo pokelewa kutoka kwa Ahmad bin Zainiy Dahlan ya kuwa: Watu walipatwa na ukame katika zama za utawala wa Omar, Bilal bin Haarith akaja kwenye kaburi la Mtume
na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu waombee umma wako wanyeshewe na mvua kwa hakika wameangamia
Lau kama kumuomba Mtume na kutawasuli kupitia kwake ni shirki, Bilal asinge fanya hivyo- Bilal ambae alifuatana na Mtume kwa muda mrefu- na kuchukua hukumu mbali mbali kutoka kwenye kinywa cha Mtume
na masahaba wengine wange mzuwia. Na hii ni dalili yenye nguvu sana juu ya kujuzu kutawassuli kupitia kwa Mtume
.
Na Baihaqiy amepokea
kutoka kwa Omar ni Khattab, amesema: Amesema Mtume
: Adam alipo tenda makosa alisema:Ewe Mola ninakuomba unisamehe kwa haki ya Muhammadhadi mwisho wa hadithi. Lau kama kutawassuli kupiti kwa Mtume kunge kuwa ni haram na shirki basi Nabii Adam
asinge fanya hivyo. Na imepokelewa ya kuwa
Mansour Dawaniqiy ali
po hiji, na kuzuru kaburi la Mtume (s.a.w) alimuuliza Imam Maalik
(Imam wa madhehbu ya Maalikihhay) na kumwambia: Ewe Aba Abidillahi, Nielekee kibla na kuomba, au nimuelekee Mtume wa Mwenyezi Mungu? Imam Maalik akasema: (Kwa nini huuelekezi uso wako kwake wakati ambapo yeye ni wasila wako na wasila wa baba yako Adam kumuelekea Mwenyezi Mungu, bali muelekee yeye, na Muombe shafaa atakuombea Shafaa, Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:
.
. Na katika kauli ya Maalik: Yeye ni wasila
wako na wasila wa baba yako Adam kwa Mwenyezi Mungu
kuna dalili ya wazi juu ya kujuzu kufanya tawassuli au kutawasali, bali kuna dalili ya kuwa ni sunna pia kufanya hivyo.
Na bwana Daarimiy pia amepokea
katika sahihi yake
kutoka kwa Abil-jawzaai, amesema: Watu wa madina walipatwa na ukame mkali, wakamshitakia Aisha, Aisha akasema: Liangalieni kaburi la Mtume na lifanyeni kuwa ni wasila wenu kuelekea mbinguni ili kusiwe na kizuizi kati ya kaburi hilo na mbingu. Wakafanya vile, na mvua ikanyesha hadi nyasi zikaota.
Na kuna mamia ya ushahidi juu ya hilo, utaupata kwenye vitabu vilivyo yaelezea kwa upana mambo haya, sasa ikiwa kutawasali kupitia kwa Mtume
inajuzu na si haram, wala shirki, kutawassuli kupitia kwa Maimam, Malaika na watu wema miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu pia ina juzu. Kwani kutawassuli ikiwa ni shirki ni wajibu iwe haram hata kama kutawassuli huko kutakuwa ni kupitia kwa Mtume
Na kama inajuzu basi si kutawassuli kupitia kwa Mtume pekee bali hata kupitia kwa watu wote wema kati ya waja wa Mwenyezi Mungu.
Hadithi hizi ulizo zinukuu ni za ajabu sana kwangu, kwa hakika sija iona hata hadithi moja kati ya hadithi hizo!
Kama unge rejea kwenye vitabu vya hadithi bila shaka unge ona mamia ya ushahidi uthibitishao kutawassuli kupitia kwa Mtume (s.a.w), na mawaliii wa Mwenyezi Mungu walio wema, na unge ona ya kuwa hadithi hizi nilizo kunukulia si chochote bali ni kama tone katika bahari
na inaonekana ya kuwa si mwingi wa kusoma vitabu vya hadithi na sira ya watu wema walio tangulia?
Wingi wa shughuli zangu na kazi nilizo nazo ndizo zinizuiazo kupitia vitabu vya hadithi na sira, pamoja na kuwa nina shauku kubwa sana ya kufanya hivyo.
Sasa ikiwa ni mwenye maarifa machache ya hadithi vipi unathubutu kuwatukana Mashia- bali inakuwaje unathubutu kuwatukana waislaam wote- na kuwanasibisha kwenye shirki kwa sababu tu ya kauli ya Muhammad bin Abdil-wahhab wakati hufahamu chochote katika hadithi? Kwa hivyo si sahihi wala si sawa, na ninakuomba uniruhusu nikueleze kiuwazi na kwa upana zaidi.
Kwa tabasamu lako na ukunjufu wa uso wako, sema kila ulicho nacho moyoni mwako ewe Muhammad, hakika sisi ni marafiki, kwa hakika nimeanza mazungumzo haya ili nipate nuru ya elimu yako, na niweze kufaidika kutoka kwako.
Kwa hakika mfano wako ni sawa na mfano wa makafiri wa kikuraishi bila tofauti yoyote, makafiri walio kuwa wakiyaabudu na kuyasujudia masanmu yao, kwa hoja ya kuwa:
.
Kwanini Mwenyezi Mungu anawakemea? Kwa sababu wao pindi walipo kuwa wakiona haki walikuwa hawaisikilizi haki hiyo, ili waweze kufahamu ni sahihi au laa? Na wakabakia wakiyasujudia na kuyaabudu masanamu yao.
Na wewe ndugu yangu Waliid usiwafuate baba zako ufuataji wa kipofu, bali kuwa ni mwenye kufuata nuru na mwenye kufanya utafiti kuhusu ukweli ili uweze kuipata au kuifikia na kuyajenga maisha yako juu ya haki hiyo, lau kama ungepekua na kufungua vitabu vya hadithi ungekuta kwamba wayasemayo watu fulani ya kuwa haijuzu kutawassali kupitia kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake, na kwamba kufanya hivyo ni shirki ..ni maneno waliyo kubaliana madhehbu zote za waislam na makundi yao yote kinyume na hivyo, je unge amini hivyo?
Ndio..kwa sababu inadhihiri ya kuwa Mashia wako na haki na waislaam wengine wako kwenye haki pia katika hilo, lakini nifanye nini kuhusiana na suala la kuwatukana kwangu Mashia?
Muombe msamaha na maghafira Mwenyezi Mungu, na wakati wote utafute ukweli, huenda Mwenyezi Mungu akakusamehe, na wakati wote unapo sikia itikadi yoyote ya Shia ifanyie utafiti, hadi uufikie ukweli, na achana na asabia, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu
amesema: Mwenye kuwa na asabia au akafanyiwa asabia kwa hakika amevuliwa na kutolewa imani shingoni mwake (yaani amevuliwa imani).
Nitayafanya yote hayo na ninakushukuru sana