1
HAJA YA DINI
DINI, MABADILIKO NA MAENDELEO
Inasemekana kuwa "Mabadiliko na maendeleo", vimethibitisha kuwa hakuna ulazima wa kuwepo Mwenyezi Mungu katika utaratibu wa Ulimwengu.
Ingawa jambo hili lafaa kuzungumziwa katika sehemu ya pili (Mungu wa Uislamu) ya masomo haya, ningependelea kutoa maoni machache ili mwanafunzi ayafikirie.
Kwanza
: ni lazima ieleweke wazi kuwa, sizungumzii kuhusu ukweli au uongo wa maelezo yahusuyo mabadiliko na maendeleo, kwani hapa sio mahali pafaapo kulizungumzia zaidi jambo hili.
Pili
: ni lazima ieleweke kuwa mabadiliko tu yatokeayo kwa viumbe asili vyenye uhai si 'Mabadiliko ya maendeleo'.
Kitabu cha maarifa yote kijulikanacho kwa jina la "World Book Encyclopaedia" cha 1966 kimeandikwa yafuatayo: "Ufafanuzi wa 'Mabadiliko na maendeleo ya viumbe vyenye uhai hujumlisha mawazo haya matatu yafuatayo:
1. Viumbe vyenye uhai hubadilika kizazi hadi kizazi vikitoa vizazi vyenye tabia zitofautianazo na zile za wahenga wao.
2. Tendo hili limetendeka kwa muda mrefu sana hata likazalisha vikundi vyote na aina zote za viumbe viishivyo sasa, na vile vilivyoishi zamani, ambavyo vimekwisha kufa au vimekwisha potea.
3. Hivi viumbe tofauti tofauti vyenye uhai vina uhusiano wa kiasili kati yao.
Tatu
: ieleweke kuwa, ingawa kuna thibitisho hizo, maelezo kuhusu "Mabadiliko na maendeleo', bado ni makisio (theory) tu, wala sio ukweli (fact).
"Ukweli" kama Kamusi la Lugha ya Kiingereza lijulikanalo kwa jina la "Websters Third New International Dictionary", liufafanuavyo ni "Tukio halisi, katika muda au nafasi", ni "Habari zilizothibitishwa".
Hivi kuna uthibitisho gani juu ya maelezo haya ya 'Mabadiliko na Maendeleo?'
Mtaalamu mmoja wa 'Mabadiliko na Maendeleo' aliyejulikana sana, Bwana W. Le Gros Clark, ameandika katika kitabu chake kiitwacho "The Fossil Evidence for Human Evolution" hivi.
"Uwezekano wa kupata mabaki ya zamani ya miili ya wajenga halisi, au hata mfano tu wa Kikundi cha kijiografia cha mahali maalum, ambavyo ndivyo vilivyotoa wahenga hasa ni wa kubuniwa tu, kiasi ambacho haustahili hata kidogo kuufikiria ukweli wake.
"Ufafanuzi wa ushahidi kuhusu 'Maendeleo na mabadiliko' ya binaadamu wa zamani sana ulitokana na uchimbuzi wa sehemu walizoishi binaadamu wa zamani, ambao wameelezwa katika sura iliyopita ni ufafanuzi wa muda tu, kwa sababu ya kutotimilika kwa ushahidi huo haiwezekani kuwa vinginevyo zaidi ya hivi".
Gazeti liitwalo "Science News Letter" la mwaka 1965 lilisema hivi: "Kuna ugomvi baina ya wanasayansi kuhusu tu, jinsi mwanadamu alivyobadilika na kuendelea: ni lini alifanya hivyo na alivyokuwa kabla."
Bwana Clark tuliyemtaja hapo juu aliandika hivi, "Ni nini chanzo asili cha mwanaadamu?....Kwa bahati mbaya, majibu yo yote yawezayo kutolewa hivi hapa kuhusu maswali kama haya yanategemea ushahidi usio wa dhahiri kabisa, na kwa hivyo mengi ya majibu hayo ni makisio tu."
Rais wa zamani wa "Shirika la Umarikani Ia Maendeleo ya Sayansi aliandika katika gazeti liitwalo "Science Magazine" haya yafuatayo ili 'kuunga mkono' mabadiliko na Maendeleo:
Hebu njoo sasa, kama unaweza, katika safari ya kukisia ya nyakati za zamani sana zisizo na kumbukumbu za kuaminika. Tufikirie wakati ambao jamii ya viumbe vyenye akili vimetokea kutokana na aina ifananayo na.....; fanya hima katika muda wa maelfu ya miaka, muda ambao habari za sasa zautegemea, kwa ajili ya sehemu kubwa ya makisio ya ufafanuzi wa wakati wa kwanza wa kumbukumbu zilizoandikwa, ambazo kutokana nazo, uhakika fulani fulani waweza kuokotezwa."
Mwanasayansi mmoja wa Kiingereza, Bwana L. M. Davies wakati fulani alisema hivi:
"Imekisiwa kuwa, vifungu vya maneno visivyopungua 800 katika maneno yaonyeshayo wazo Ia kukisia (maneno kama vile "Tuchukulie tu," au Tunaweza kudhania kuwa" n.k) vinaonekana kati ya majalada ya kitabu cha Bwana Darwin kiitwacho "Origin of Species" (Asili ya viumbe vyenye asili moja), peke yake."
Ukivifikiria vifungu vya maneno tulivyoviandika hapo juu, na hasa maneno yale tuliyoyapigia mistari, utaamua kuwa "Mabadiliko na maendeleo si ukweli uliodumishwa ila ni maelezo tu miononi mwa maeIezo mengi yaliyokuwepo tangu mwanzoni mwa binaadamu, ili kuieleleza asili ya ulimwengu, Mengi ya maelezo ya namna hii, sasa yamedharauliwa, lakini hapo mwanzoni yalikuwa na nguvu akilini mwa watu kama yalivyo haya maelezo ya mabadiliko na maendeleo hivi sasa. Na nguvu zake hizi, katika akili ya watu, hazifanyi mawazo haya kuwa ya ukweli zaidi.
Hakika, mwanasayansi mmoja, Dakta T. N. Tahmisian, ambae ni mtaalamu wa mambo ya viumbe vyenye uhai, wa Tume ya Nguvu za Atomiki, alisema, "Wanasayansi waendao huku na huku na kufundisha kuwa maelezo kuhusu mabadiliko na maendeleo ni ukweli uliothibitika wa masiha ni wadanganyifu wakuu na hadithi watoazo kuyaeleza mabadiliko na maendeleo, hazina ukweli hata kidogo. Aliuita uelezaji wa mabadiliko na maendeleo kuwa ni "fumbo la mchezo wa mchanganyiko wa dhana na mazingaumbwe ya matumizi ya nambari."
Mwanasayansi mwingine aliyekuwa mkuu wa idara ya sayansi katika chuo kimoja, Bwana J. W. Klotz, alisema mnamo mwaka 1965 Masihiya kwamba, "kuyakubali maelezo ya mabadiliko na maendeleo bado kunategemea tu, kuwa ni imani zaidijuu yajambo hilo.
Na juu ya hapo maelezo haya mpaka sasa yanawajibikiwa kutafuta ushahidi utoshao kuyaunga mkono. Basi vipi maelezo haya yawezavyo kutumika kupinga maelezo ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu?
Mwisho kabisa, hata wanamabadiliko na maendeIeo wenyewe wanakubali kuwa kunahitajika kuwepo, "Mwenyezi Mungu Mwenye kuishi milele, Mjuzi wa yote, Mwenye nguvu zote." Katika utaratibu wa Ulimwengu kama inavyoelezwa katika maelezo ya "Mabadiliko na maendeleo."
Lakini, hapo mwanzo wanasayansi walikukataa kuwepo Mwenyezi Mungu; na kuzihusisha sifa njema hizi na "Asili", wanasema kuwa "Asili" ilichukua kile, na "Asili" ilifanya kile.
Hata hivyo hebu tutazame hii 'Asili' ni nini? Asili ni wazo la kuwazika tu, lililo katika ubongo wa watu, baada ya kujifunza kwa makini tabia za vitu. Asili yaweza kuonekana katika vitu; lakini si yenye kuishi yenyewe. Na kwa hali yoyote, hakunia kumbukumbu ya mkutano wo wote uliofanyika kuhusu asili za vitu mbali mbali; ili kuamua kuhusu jinsi ya kupatanisha kazi zao. Maua hayafanyi kazi pamoja na nyuki ili kutafuta ushirika wa nyuki katika uzalishaji wao, na kuwapa nyuki asali kama ujira wao. Bali twajua wazi kuwa nyuki hawawezi kuishi hata kwa siku moja tu, bila ya maua, na kuwa maelfu ya maua yangelipotea kama si sababu ya nyuki.
Hivyo basi, unaona kuwa wana mabadiliko na maendeleo wanatambua umuhimu wa Mtengenezaji na "Msanii". Lakini kimafundisho, wanafundisha kwa kurudia rudia kuwa, huyo Mtengenezaji na Msanii alikuwa ni "Asili" (fundisho ambalo ni oni la kuwazika tu) au "Jauhari" ambayo ni kitu kisicho na "Akili wala Uhai".
HOJA IJULIKANAYO KAMA "HOJA YA PASCAL
Hadhrat Amiirul Mu'miniin Ali bin Abi Talib alisema:
Wanajimu na waganga husema kuwa wafu hawatafufuliwa kamwe, "Nikasema: Haya shikilieni maoni yenu hayo. Kama oni lenu litakuwa sahihi, sitapata dhara lolote (kutokana na imani yangu, ya kuiammi sika ya Hukumu); lakini iwapo imani yangu itakuwa sahihi basi mtakuwa wakosefu (katika siku hiyo kwa kutoiamini siku ya Hukumu)".
Allama Abu Hamid Al Ghazali (Aliyefariki mnamo mwaka 1111 Masihiya) aliandika katika kitabu chake kiitwacho "Mizanul Aamal" kuwa "Ali (Mwenyezi Mungu amteremshie baraka zake) alimwambia mtu mmoja aliyekuwa akibishana naye sana kuhusu Akhera akisema: Kama ukweli ni huo unaoufikiria (kuwa hakuna maisha ya Akhera); basi ninyi wote mtaokoka; lakini iwapo ukweli ni kama hivi nilivyokwisha kueleza (kuwa kuna maisha ya Baadaye), basi ninyi mtalaaniwa na mimi nitaokolewa." Huo ndio ukweli uliopo. Thibitisho tuzipatazo sisi wenyewe tuvionapo viumbe vilivyomo humu duniani, zaunga mkono imani ya kuwepo Mwenyezi Mungu Muumba, na kuwepo kwa siku ya Hukumu.
Kisha Mwanachuoni huyo, Bwana Al-Ghazali alieleza kuwa, Hadhrat Ali
hakuitoa hoja hii ili kuficha mdhihiriko wa kuwepo kwa maisha ya Akhera, ila aliitoa kwa kutaka kuwahakikishia watu jambo hili kwa maelelezo ya kihoja.
Miaka elfu moja, baada ya Hadhrat Ali bin Abi Talib
alitokea mtaalamu wa hesabu maarufu sana Bwana Pascal ambaye alifariki mnamo mwaka 1662 Masihiya; pamoja na "Parido Pascal" (Hoja ya Pascal) yake maarufu, ambayo allitumia ili kulihakikishia kundi la watu wa aina hiyo hiyo, jambo hilo hilo. Hoja yake hiyo, yaweza kuelezwa kwa kifupi zaidi kwa maneno yafuatayo:
"Kama unaamini kuwepo maisha ya Akhera, utapata kila kitu kama kweli maisha hayo yapo kweli, na hutapata hasara yoyote kama maisha hayo hayapo. Hivyo basi ni afadhali kuyakinisha kuwa, hakika siku hiyo ipo." (Habari hizi zinatoka katika UK. 439 wa kitabu kiitwacho "Pascal", kilichoandikwa na Bensees na kutayarishwa Bwana Y. Brunchirey huko Paris - Ufaransa mnamo mwaka 1912 Masihiya).
Je huu ni ulinganifu tu? Au Pascal alipata wazo la (Pari) imani yake kutokana na Uislamu?
Bwana Asin Palalcios anaamini kuwa Bwana Pascal alisoma hoja hizi katika kitabu kiitwacho "Ihya-ul-Uluum" cha Mwanachuoni Al-Ghazali.
Lakini, Bwana Al-Ghazali mwenyewe anaeleza katika kitabu hicho Mizanul-Aamal tulicho kitaja hapo juu kuwa, Hadhrat Ali bin Abi Talib
ndiye asili ya hoja hii.
Hivyo basi, inatubidi tuziweke sifa hizi pale zipasikapo kuwapo na kukubali kuwa Bwana Pascal (ingawa yeye binafsi hakutueleza kazipata habari hizi kutoka kwa Hadhrat Ali bin Abi Talib
.
SIFA ZA DIN
Mpaka sasa nimeeleza umuhimu wa dini kwa ujumla.
Sasa hebu ngoja nizitaje sifa za lazima kwa dini kuwa nazo, ili itimize mahitaji ya dini niliyoyataja hapo juu.
1) Kwanza kabisa dini ni lazima ipatane na akili na udadisi wa mtu.
Hakika zipo dini zenye kuwataka wafuasi wake waamini kwanza kisha ndipo waelewe. Kusema kweli dini kama hizi huzirudisha nyuma fikara za mwanaadamu na ni haki ziitwe (na kwa hakika zinaitwa) dini zisizopatana na fikara za Mwanaadamu.
Uislamu kama unavyofafanuliwa na imani ya madhehebu ya Shia Ithna-sheria, hutoa nafasi ya mbele zaidi kwa akili za binadamu na hoja zake. "Akili" ni moja wa misingi minne ya Sheria ya Shia Ithna-Asheria. Sio hivyo tu, bali vile vile imani hii inahimiza kuwa mafundisho ya dini ni lazima yaeleweke kwa mwenye kuiamini dini hiyo.
2) Ni lazima dini ifundishe na ifanye kwa vitendo, hekima ya mwanaadamu.
Ziko dini ambazo huwataka wafuasi wake wasujudie picha au sanamu za watu fulani fulani au wanyama fulani fulani au vitu vingine ambavyo havina uhai.
Dini kama hizi hushusha sana heshima za wafuasi wao, na ni haki zilaumiwe kwa jambo hilo. Baadi ya dini hufundisha ubora wa watu wa taifa fulani au kudharau watu wa ukoo mwingine.
Uislamu tu ndio uliokuwa na bado ni kiongozi wa usawa wa binaadamu na ambavyo, kwa mara ya kwanza katika historia ya dini, umefundisha na ukafanya kwa vitendo, udugu, usawa na haki kwa binadamu na ukaonyesha heshima ya Mwanadamu kiasi cha kuweza hata kuyashangaza macho ya watu wote.
3) Dini ni lazima iwe mwongozo ulio kamili wa kumwendeleza mwanadamu kimwili, kiakili na kiroho kwa ujumla.
Zipo baadhi ya dini ambazo hutilia mkazo zaidi katika mambo ya kiroho na kuachilia mbali mwili na akili; na zipo nyingine ambazo huzungumzia tu kuhusu maendeleo ya kimwili, au ya kiakili lakini haziyafanyi kimatendo mambo hayo.
Dini za aina hii haziwezi kuwachukua wafuasi wake mbali sana kwa sababu maendeleo yafundishwayo na dini hizo yamekwenda kombo.
Ni Uislamu tu, kama unavyofundisha na Madhehebu ya Shia Ithnaasheria, ambao humwendeleza mtu kimwili, kifikara na kiroho kwa ujumla.
4) Ni lazima dini iwe na mkusanyiko wa sheria zihusuzo maisha ya binaadamu.
Dini ambazo hufundisha tu kuwa "wapende jirani yako" bila ya kuonyesha jinsi ya kufanya hivyo, ni dini zisizo na faida yo yote wakati zikaribiwapo na suala la kulifanya jambo kimatendo.
Uislamu unao mkusanyiko timamu wa sheria za maisha ya mwanaadamu ambazo humwongoza mtu sawa sawa katika maisha yake ya kifamilia, kijamii, kiuchumi, kitabia za kiutu na kiadilifu.
5) Ni lazima dini iafikiane na asili ya mwanaadamu.
Zipo dini zinazojaribu kuiepuka asili ya mwanaadamu. Kwa mfano, baadhi ya dini zinafundisha utawa. Wanaamua kwa matendo yao (kama si kwa maneno mengi) kuwa Mwenyezi Mungu alikosea alipoumba hamu ya tendo la mke na mume katika mwili wa mwanaadamu. Vile vile wanasahau (au wanajifanya kusahau) kuwa silika za kiasili haziwezi kuharibiwa na kuwa silika hizi zisizo za kiasili zinamwongoza mtu kwenye undanganyifu wa kisiri.
Na sijui, ni nini kingelitokea kuhusu kuwepo kwa mwanaadamu hapa duniani, iwapo watu wote wangelikuwa wafuasi wa kimatendo wa dini hiyo. Hakika watu wote wangelimalizika katika muda wa miaka kati ya arobaini na hamsini hivi.
Bila ya kusema kuwa dini kama hii haiwezi kuwaongoza watu kwenye ustawi, kwa sababu kufuatana na asili yake, dini hii ni kinyume na mdumisho wa kuwepo kwa wanadamu hapa duniani.
6) Ni lazima dini isitumike kama zana mikononi mwa wadhalimu, ili kuudhulumu umma.
Dini nyingi zinalaaniwa na makafiri kwa kuwa silaha ya makabaila kwa ajili ya kuudhulumu umma unaoonewa na kuzifunika sauti za walalamikaji.
Dini kama hizi, kwa mfano zile zilizofundisha mawazo ya "Kudra". Hivyo basi, umma ulilazimishwa kuamini kuwa matendo yote mabaya, udhalimu, na uovu wa watawala ulikuwa ni Penzi la Mwenyezi Mungu; hivyo basi vitu kama hivi ni lazima vivumiliwe bila ya malalamiko yo yote.
Dini kama hizo hazina nafasi katika karne iliyoendelea kama hii yetu. Ni Uislamu peke yake, kama ulivyoelezwa na madhehebu ya Shia Ithna-asheria ambao ulisema kuwa imani kama hiyo ilikuwa upuuzi mtupu; kuwa kila mtu ana madaraka kamili ya matendo yake na kuwa madaraka yake yasihusishwe na Mwenyezi Mungu.
Itadhihirika wazi, kutokana na kanuni ya hapo juu kuwa, miongoni mwa dini nyingi sana za duniani, ni Uislamu tu (Imani ya Shia Ithna-asheria) ambao Unatimiza masharti haya ya lazima ya dini ya kweli, na yenye maarifa mengi.
SHARTI YA KUCHAPA
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini
ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
MWISHO WA KITABU