Fadak

Fadak0%

Fadak Mwandishi:
: DR. MUHAMMAD KANJU
Kundi: Faatima (a.s)

Fadak

Mwandishi: Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
: DR. MUHAMMAD KANJU
Kundi:

Matembeleo: 6170
Pakua: 2898

Maelezo zaidi:

Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 2 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 6170 / Pakua: 2898
Kiwango Kiwango Kiwango
Fadak

Fadak

Mwandishi:
Swahili

FADAK FADAK

MWANZO WA KITABU

Kimeandikwa na:

Ra'isu 'l-Muballighin Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Bilal Muslim Mission of Tanzania

P.O. Box 20033

Dar es Salaam TANZANIA

ISBN: 9987 620 39 6

Kimetolewa na Kuchapishwa na:

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA S.L.P. 20033

DAR ES SALAAM TANZANIA

Kimetafsiriwa na:

Dr. Muhammad Kanju

Toleo la kwanza:

Zilqa'ad 1424 / Januari, 2004 Idadi: Nakala 2000

e-mail: bilal@cats-net.com

DIBAJI

Tunamshukuru Allah (s.w.t.), kwa Baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Watukufu Ahlul~Bait (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki "Fadak".

Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya moja ya ma'andishi vya Al-Marhum Ra'isu 'l-Muballigh?n ?yatullah Allamah al-Haj Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a.), Kitabu hiki kimekuwa maarufu katika ulimwengu wa Ki- Islamu na kilitafsiriwa na kuchapishwa na Taasisi mbali mbali kwa lugha ya Ki-Urdu, Ki- Hindi na Ki-Gujrati.

Sababu iliyoifanya Bilal Muslim Mission isimamie kazi hii ni kama ile za mwanzo, ambayo inatokana na maombi ya watu wengi kutoka Afrika ya Mashriki kutaka kujua kadhia ya muhimu na ya maana sana katika historia ya Uislamu, kadhia ya Fadak. Hii ilitufanya tutafsiri na kuchapish kitabu hiki kwa lugha ya kiswahili ili watu wazungumzao kiswahili wa weze kuelewa na kufahamu dhuluma na maonevu yaliyotendwa kwa Ahlul Bayt (a.s.) watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.).

Mimi binafsi sikusita kumuomba ndugu yetu Dr Muhammad Kanju kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake ya lugha ya Kiingereza, Namshukuru Dr Kanju kwa kukubali ombi langu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja.

Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote ambao kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi mwao na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine katika kazi zetu za Tabligh, Tunamuomba Allah (s.w.t.) awalipe malipo mema hapa Duniani na baadaye huko, Akhera.

20 Decemba, 2003

Sayyid Murtaza Rizvi Dar es Salaam Bilal Muslim Mission

FADAK

Fadak ni kadhia ya muhimu na ya maana sana katika historia ya Uislamu. Fadak iko kaskazini ya Madina, umbali wa safari ya siku 2 au 3, ilikuwa ni ardhi yenye rutuba sana, kwa mujibu wa Ibn Abi Hadid, vijisitu vya tende havikuwa vidogo kama vile vya Kufa katika karne ya 13 1 na ambazo pato lake lilikuwa kati ya 24,000 dinar 2 ilikuwa inakaliwa na kabila la Mayahudi.

Katika mwaka wa 7 A.H., Mtume alipigana vita dhidi ya Mayahudi wa Khaibar, kwa sababu walivunja mkataba na Waislamu. Baadhi ya ngome zao zilichukuliwa; mbili au tatu zilizingirwa. Mwishowe walipendekeza mpango ambao maisha yao, dini , heshima yao 1 Ibn Abil-Hadid, Sharh Nahjul-Balagha, J. 16, uk. 236; Halab Publishing House, Cairo.

2. Ibn Tawus, Kashful-Mahajjah, uk. 94 nk. itakuwa salama, na wataondoka katika ngome na kufanya kazi za shamba kwa ajili ya Waislamu. Mapatano yalifikiwa; Mayahudi waliruhusiwa kufanya kazi kwenye mashamba kwa niaba ya Waislamu na mazao yaligawanya kati ya Mayahudi na Waisalmu nusu kwa nusu.

Kwa mujibu wa aya ya Qur'an (8:41) moja ya tano ya ngome na ardhi alipewa Mtume kama Khums, na nne ya tano iliyobakia ilikwenda kwa Waislamu.

Wakati Mayahudi wa Fadak waliposikia vita ya Khaibar na matokeo ya makubaliano, walianza kufikiria kuhusu wao wenyewe. Wakati huo huo akaja mjumbe kutoka Madina, akawalingania Uislamu. Walikataa kukubali Uislamu, lakini kwa matakwa yao wenyewe, walikubali amani kwa masharti yafuatayo:

a) Watatoa nusu ya ardhi yao kwa Mtume nusu iliyobaki iwe kwenye miliki yao.

b) Watafanya kazi katika ardhi ya Mtume na kugawana mazao yake.

c) Mtume atakuwa na mamlaka ya kuwafukuza kutoka Fadak wakati wowote atakao, lakini itampasa kuwalipa malipo kamili ya mgao wao wa ardhi na mali yao.

Mtume alikubali masharti yao.3 Baadhi ya Waislamu walifikiri kwamba Fadak ilikuwa vile vile mali ya ya Waislamu kama Khaibar. Lakini ni kutokuelewa kwao, kwa sababu zamani kabla ya hilo, katika suala la Banu Nazir, sheria ilitangazwa rasmi kwamba cho chote kinachokuja kwa Mtume bila ya kupigana vita, kitakuwa ni mali binafsi ya Mtume, kwa ajili ya matumizi yake au kugawa kwa atakaeona inafaa, na Qur'an inasema:

"Na mali aliyoleta Allah kwa Mtume Wake hamkuyakimbilia mbio kwa farasi wala ngamia. Lakini Allah huwapa mamlaka Mitume Wake juu ya wowote awatakao, na Allah ana uwezo juu ya kila kitu." (59:6)

3. Yaqut Al-Hamawi, Mu'jamul-Buldan; Ibn Abil Hadid, Sharh Nahjul-Balagha J.16 uk.210; al-Tabari, Annals, J. Uk. ; Ibnul Athir, Tarikhul Kamil. Banu Nazir walifukuzwa kutoka Madina mwanzoni mwa mwaka wa tatu hijiriyya. Waliruhusiwa kuchukuwa cho chote kile kinachowezwa kubebwa na ngamia wao isipokuwa silaha.

Katika kuwasili kwake Madina, Mtume alifanya uhusiano wa kindugu, akimfanya Muhajir ndugu wa Ansar na kila Ansar aligawa mali yake yote nusu kwa nusu na ndugu yake Muhajir, kiasi kwamba kama mirathi ya Ansar ilikuwa ikigawanya miongoni mwa kaka na dada zake, ndugu Muhajir alijumuishwa ndani yake.

Abu Bakar alifanywa ndugu na Kharijah bin Zayd; Umar na Utban bin Malik Ansari walifanywa ndugu, kama walivyofanywa Uthman na Aws bin Thabit Ansar, na kadhalaika.4 Ali peke yake aliachwa nje ya undugu huu, Mtume alitangaza kwamba Ali ni ndugu wa Mtume mwenyewe. 5 .

4.. Tarikh Abul Fida, J. 1 uk. 127

5. Samhudi, Khulasatal-wafa', J. 1 uk. 109; Ibn 'Abdil Birr, al-Isti'ab, Hyderabad J. 2, uk. 473 Alipopata mali ya Banu Nazir, Mtume kwa matakwa yake mwenyewe aliamua kuigawa miongoni mwa Muhajirin na akawaondolea Ansar mzigo huu. Alifanya hivyo, na akawajumuisha katika orodha Ansar wawili masikini sana - Abu Dajjanah na Sahl ibn Haniif.6 .

Hivyo Muhajirin wote, wakiwemo Abu Bakar, Umar na Uthmani walipata mgao wao kutoka kwenye ardhi hiyo na ikawa mali yao binafsi. Haikuwa kwa ajili ya "kujikimu" tu. Katika njia hiyo hiyo Fadak ikawa mali ya binafsi ya Mtume na aliisimamia yeye mwenyewe7 Kisha aya nyingine ya Qur'an ilikuja:

"Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake" (17:26)

6. Tafsir Ad-Durr'l-Manthur, J. 6 uk. 187-190

7. Ar-Razi, Tafsir Kabir, Az-Zamakhshari, Tafsir Al- Kashshaf Mtume alimuuliza Jibril maana ya aya hii. Akasema: "Mpe Fatimah Fadak; itakuwa ni chanzo chake cha mapato na watoto wake.8 Mtume akampa Fatimah Fadak; na alikuwa akiitumia kama mali yake mwenyewe; wakala wake alikuwa kule akiangalia maslahi yake. Hii iliendelea mpaka Mtume alopofariki na Abu Bakar akachukuwa umiliki wa Fadaka kwa nguvu.

Sasa Fatimah anapinga dhidi ya uporaji huu wa mali yake, akisema kwamba Mtume alimpa yeye. Abu Bakar akamuambia alete mashahidi kuthibitisha jambo hili.

Sasa Fatimah alikuwa tayari katika umilki wa mali hii; na kwa mujbu wa kanuni za ki- Islamu, umiliki wenyewe ni uthibitisho wa kutosha wa umilikaji. Kama Abu Bakar alidai mali ile kwa ajili yake mwenyewe au kwa ajili ya taifa la ki-Islamu, basi ni yeye, kama mdai

8. Suyuti, Ad-Durrul-Manthur, J. 4, uk. 177; Suyuti, Lubabun-Naqul, imechapishwa katika pambizo la Tafsir al-Jalalain, J. uk. 19.

ambaye alipaswa kuleta mashahidi kuunga mkono madai yake. Lakini aliweka dhima ya kuthibitisha juu ya Fatimah, akipuuza Sheria ya ki-Islamu. Tena, kwa vile alikuwa mdai, hakupaswa kuhukumum kesi yeye mwenyewe. Lakini hakujali mambo ya undani ya kimahakama ilimradi tu madhumuni yake yametekelezwa. Hata hivyo, Fatimah alimleta Ali na Umm Ayman (mjane wa Zaid bin Haritha). Abu Bakar akasema lazima kuwe na amma wanaume wawili au mwanaume mmoja na wanawake wawili kama mashahidi.9 .

Sasa, katika masuala ya familia - zawadi ya baba kwa bint yake ni suala la familia - shahadi mmoja tu anatosha; lakini Abu Bakar kwa urahisi alilisahau hili. Vile vile Uislamu hukubali shahidi mmoja aliye ungaunisha na kiapo cha mdai kama uthibitisho wa kutosha.1 0.

9. Fakhuruddin Ar-Razi, Tafsir Kabir, J. 8, uk. 386.

10. Kanzu'l-'Ummal, J. 3 uk. 178-9 Fatimah alilazimika kuleta mashahidi wengine, miongoni mwao ni watoto wake wawili, Hasani na Huseini na mwanamke mmoja, Asma bint Umais (mke wa Abu Bakar mwenyewe).

Sasa kulikuwa na mashahidi zaidi kuliko kiwango cha chini kilichotakiwa. Hivyo Abu Bakar alianza kushusha sifa za mashahidi wote:

a) Ali, Hasani na Huseini walikuwa mume na watoto, na inawezekana wao kushawishiwa na maslahi binafsi.

Kumbuka kwamba Fatimah, Ali, Hasani na Huseini walikuwa watu pekee ambao walichanguliwa na Mtume kuthibitisha ukweli wake dhidi ya Wakristo wa Najrani - ambao walitakiwa waseme "Amin" kwa maombi ya Mtume ya kutaka laana ya Allah "dhidi ya waongo."

Walikuwa ni watu pekee wanao ishi wakati huo ambao walitakaswa na Allah kutokana na dhambi na makosa yote. Na hakuna Mwislamu hata mmoja katika ulimwengu ambaye anaweza kusema kwamba wanaweza kusema uwongo, Lakini Abu Bakar alikataa ushahidi wao kwa uwazi akisema kwamba ushahidi wao ulishawishiwa na maslihi binafsi - kwa maneno mengine walikuwa waongo!!

b) Asma bint Umais zamani alikuwa ameolewa na Ja'far, kaka yake Ali; na kwa hiyo, angeunga mkono madai ya Bani Hashim.

Alisahau kwamba alikuwa mke wake na hivyo ushahidi wake dhidi ya maoni yake ulikuwa ni wa maana zaidi. Na hata hivyo, je, lazima kwamba shahidi hapaswi kuwa rafiki wa upande wa yule ambaye anahudhuria (mbele ya mahakama) - kwamba ushahidi unaotolewa tu na adui ndio lazima ukubaliwe?

Umm Ayman alikuwa sio Mwarabu na hakuweza kuongea kiarabu fasaha. (Umm Ayman alikwa msichana wa kitumwa wa Abdullah - baba yake Mtume,. Mtume alimrithi, akamuozesha kwa zayd bin Haritha, (na kwa mujibu wa Mtume alikuwa miongoni mwa "watu wa Peponi").

Je, ina maana kwamba ni watu tu wanao ongea kiarabu ndio wanao weza kukubaliwa kama mashahidi? Au ni Waarabu tu ndio wakweli na waaminifu?

Ukatili huu wa Khalifa ulizuia watu wengune kujitokeza mbele na kuota ushahidi kwa niaba ya Fatimah. Ikiwa Khalifa hana kusita kokote katika kumtweza na kumtukana Ali na watoto wake, vipi watakuwa na uhakika kwamba heshima yao haitaharibiwa kama wakijitokeza kumuunga mkono Fatimah?

Madhumuni ya ushahidi ni kuthibitisha ukweli au vinginevyo wa madai. Kama mtu ameridhishwa kwa ukweli wa madai, idadi ya mashahidi inakuwa ni ada tu, ambayo katika baadhi ya masuala ilitolewa hata na Abu Bakar mwenyewe. Abdallah Ansari, Sahaba wa Mtume, alidai kwamba Mtume alimuahidi kiasi fulani kutoka kwenye kodi ya Bahrain. Abu Bakar alikubali madai hayo bila kutaka shahidi yeyote 1 1.

Hata hivyo,wakati Fatima alipoona kwamba Abu Bakar amekusudia kuichukuwa Fadak kutoka kwake, alisema kwamba kama sikupewa kama zawadi, basi Fadak ilikuwa yake kwa urithi.

Sasa, Abu Bakar akaja na jibu la ubunifu. Akasema: "Nimemsikia Mjumbe wa Allah akisema: 'Sisi kikundi cha Mitume, haturithiwi; cho chote tunachokiacha huwa ni Sadaka.'"

Sasa, usemi huu wa kubuni anao husisha nao Mtume ni dhidi ya aya nyingi za Qur'an na kanuni zote zinazokubaliwa za Uislamu, kama Fatimah mwenyewe alivyo onesha katika hotuba yake, ambayo kwayo anasema - pamoja na mambo mengine:

11. Bukhari, Sahih, Muslim, Sahih, kitu kama hicho kilitokea kwa Sahaba mwingine, kama inavyo simuliwa katika Knzul-'Ummal. "Na sasa unakataa kwa kutumia uwongo kwamba sina urithi kutoka kwa baba. Je, unataka desturi za (siku za) ujahiliyya? 1 2. Na ni nani bora kuliko Allah, katika kutoa sheria, kwa ajili ya watu ambao wanaamini? Je, hujui?

Kwa hakika ni wazi kwako kama jua la mchana kwamba mimi ni bint wake (Mtume). Je, mimi ningezuiwa juu ya urithi wangu? Ewe mtoto wa Kahafa ! Je, imo kwenye Kitabu cha Allah, kwamba wewe unapaswa kurithi kutoka kwa baba yako, na mimi nisingemrithi baba yangu? Kwa hakika wewe umeleta kitu cha uzushi kabisa.1 3 Je, ni kwa makusudi kwamba umekiacha Kitabu cha Allah na kukitupa nyuma ya mgongo wako? Kama Allah anavyosema:

"Na Sulaiman alimrithi Daudi'. 1 4. na alisema,

12. Bara Arabu kabla ya Uislamu mwanamke alikuwa hana haki ya kurithi; yeye mwenyewe alikuwa akichukuliwa kama mali ya kurithi. Tazama Ameer Ali, Mohammedan Law, J. 2.

13 Kama bint anazuiwa kurithi kutoka kwa baba yake, ni uzushi. 14. Qur'an, 27:16; hapa Mtume anarithi na mali nyingine inarithiwa. Hivyo, hadithi inayozaniwa ni manifesto dhidi ya Qur'an. akisimulia majilio ya Yahya bin Zakariya: "Alipomuita Mola wake wakati aliposema:

'Ewe Mola wangu! Hakika mifupa yangu imedhoofika na kichwa kinameremeta kwa mvina hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu, na mke wangu ni tasa, basi nipe mrithi kutoka Kwako, ambaye atanirithi na kurithi kutoka katika ukoo wa Yaquub 1 5 na alisema: na ndugu wa damu wana haki zaidi juu ya wao kwa wao katik a Kitabu cha Allah' 1 6 Na alisema: 'Allah anakuusieni juu ya watoto wenu, fungu la mwanamume ni kama la wanawake wawili' 1 7 Na alisema:

'Mmeandikiwa mmoja wenu anapo fikiwa na mauti, kama akiacha mali afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri 15 Qur'an, 19:3-6. inasemwa kwamba Zakariya alimaanisha urithi wa utume. Kama ni hivyo, basi nini maana ya kuogopa kwake ('na hakika naogopa kizazi changu baada yangu')? Je, alikuwa akiogopa kwamba kizazi chake atakuwa Mtume baada yake? 16 Qur'an, 8:75 17 Qur'an, 4:11 inayopendeza, ni wajibu haya kwa wamchamungu.1 8

Na sasa unakataa kiwerevu kwamba mimi sina haki wala urithi wowte kwangu mimi kutoka kwa baba yangu. Vyema, je, Allah ameteremsha aya yoyote maalum kwa ajili yako, na ambayo kwayo baba yangu ameondolewa? Au unasema kwamba watu wa dini mbili tofauti hawarithiani wenyewe kwa wenyewe? 1 9 Baba yangu na mimi si watu wa dini moja? Au wewe una elimu zaidi ya ukamilifu na kauli ya jumla ya Qur'an kuliko baba yangu na binamu yangu (Ali)?"

Hoja hizi zilikuwa hazikanushiki na bado hazikanushiki, lakini Khalifa hakuzijali. Hapa lazima mtu ataje nukta chache kabla ya kuendelea zaidi:

18 Qur'an, 2:180

19 Katika Uislamu asiye Mwislamu harithi kutoka kwa Mwislamu. Anauliza kama wanadai kwamba yeye au baba yake, muasisi wa Uislamu, hakuwa Mwislamu. Hadithi inayodhaniwa (ya kutunga) ilikuwa dhidi ya aya nyingi mno za Qur'an (baadhi ya hizo zimetajwa punde tu hapo juu).

Sasa tumekubali wote pamoja hadithi ya Mtume kwamba: "Hakika wametokea wengi ambao husema uwongo na kuuhusisha nami; hivyo wakati hadithi iliyohusishwa kwangu ikija kwenu, irejesheni kwenye Kitabu cha Allah; na ile iliyo katika kuafikiana na Kitabu cha Allah, ikubalini na ile iliyo dhidi yake itupeni kwenye ukuta.

Abu Bakar alikuwa mdai, na alitoa hadithi ambayo mpaka wakati huo hakuna Sahaba wa Mtume aliye wahi kuisikia. Kwa vile alikuwa mwenye kupenda sana ada na taratibu, kwa nini asitoe mashahadi wawili wanaume kuthibitisha hadithi yake? Hebu natukubali kwa ajili ya hoja, kwamba ilikuwa hadithi sahihi. Sasa, nani ambaye angepaswa kuifahamishwa na Mtume, wale ambao watakuwa warithi wake (bint, wakeze, ami, binamu nk,) au mgeni ambaye kamwe hangefikiria kurithi chochote kutoka kwa Mtume?

Akili za kawaida husema kwamba ni watu wa familia ambao walipaswa kuelezwa na Mtume kwamba, "Tazameni, wakati nikifa, vyote vile ambavyo ninaviacha vinakuwa Sadaka, hamtarithi chochote kwa sababu mimi ni Mtume na Mitume hawarithiwi.

Hivyo, kuwenu waangalifu kutoa Sadaka mali yangu yote ya kidunia." Ilikaje kwamba hakumuelza yeyote katika wale ambao wangekuwa warithi wake na akamuambia Abu Bakar, ambaye hadai chochote katika urithi wake? Kwa nini aliwaweka katika giza bint yake, wake zake, na ami yake, na hivyo kuanzisha mgogoro mkali kati ya Khalifa na jamaa wa familia yake?

Hata wakati madai ya Fatimah yalikataliwa kwa msaada wa hadithi hii ya kutunga, wake za Mtume walimtuma Uthmani kwa Abu Bakar wakiomba mgao wao wa urithi wa Mtume katika Khaibar.2 0 Inaonesha wazi kwamba 20 Yaqut Al-Hamawi, Mu'jamul-Buldan (Baadae hadithi ilihusishwa na Aisha ambayo kwayo anamuunga mkono baba yake) wake za Mtume hawakuiamini hadithi hiyo, wala Uthmani hakuiamini (ambaye baadaye alikuja kuwa Khalifa wa tatu); vinginevyo, asingeuchukuwa ujumbe ule na kuupeleka kwa Abu Bakar.

Mtu anaweza kushangaa kwanini hakukubali hoja za Fatimah zisizokanushika? Kwa dhahiri isingemletea madhara yoyote kama angelikubali madai ya Fatimah. Sababu ya kwanza na ya msingi ilitajwa na Ibn Abi'l-Hadid katika Sharh yake ya Nahju'l- Balagha: "Nilimuuliza Ali bin Fariqi, mwalimu katika Madrasah Gharbiyah huko Baghdad, 'Je, Fatimah hakuwa mkweli mno?' akasema, 'kwa hakika alikuwa!' Nilisema: 'Basi kwanini Abu Bakar asirudishe Fadak kwake wakati anajua kwamba alikuwa mkweli mno?'

Mwalimu alitabasamu na akasema: 'Lau angeitoa Fadak leo kwa sababu tu ya madai yake, angelirudi kesho yake na kudai ukhalifa kwa ajili ya mume wake, na kumuondoa katika nafasi yake; na kisha hatakuwa na sababu, kwani atakuwa ameshakubali kwamba ni mkweli mno katika madai yake, kwa hali yoyote itakayo kuwa, bila haja ya uthibitisho au mashahidi."21 Hii huafikiana na kutokurudishwa kwa mali hii.

Lakini kwanza kabisa kwa nini waliipora? Imamu Ja'far Sadiq (as) alimueleza mwanafunzi wake, Mufadhal bin Umar: "Wakati Abu Babakr alipokuwa Khalifa, Umar alimshauri amnyime Ali na familia yake kutoka kwenye Khums, ngawira na Fadak, "Kwa sababu kama wafusi wake watalijua hili watamucha na watakufuata wewe, kwa masilahi ya dunia." Ni kwa sababu hii kwamba Abu Bakar aliwanyima wote haki zao. 22

22 Haidar Al-'Amidi, Al-Kashkul. Ni rejea pekee ya Shi'a katika makala hii. 21 Ibn Abil Hadid, Sharh Nahjul-Balagha, J.16, uk. 284 Inashangaza kuona kwamba Fadak ina hali ya kisheria sawa na ile ya ardhi ya Banu Nazir ambayo walipewa Muhajirun (akiwemo Abu Bakar na Umar.) Lakini wakati ambapo Fadak ilichukuliwa kutoka kwa Fatimah, mali ya Muhajirun haikuguswa.

Vyo vyote iwavyo. Ukiburi uliotumika katika suala hili, hukanusha kabisa urithi wa vitu viwili ambavyo Mtume (saww) ameviacha nyuma kwa mwongozo wa Ummah. Amerudia mara nyingi ktika hotuba zke: "Ninakuachieni miongoni mweni vizito viwili, Kitabu cha Allah na watu wa familia yangu ambao ni kizazi changu, kadiri mtakavyoshikamana navyo hamtapotea, na havitatengana vyenyewe kwa vyenyewe mpaka vinifikie katika hodhi ya Kauthar.

Lakini Abu Bakar na Umar waliharibu kuaminika kwa vyote: 1. Walimtweza mtoto wa Mtume mbele ya macho ya watu. Watu waliona kwamba pamoja na aya zote za Qur'an na hadithi za Mtume zinazo tukuza ubora wa Ali , Fatimah, Hasani na Huseini, bado wana uzito kidogo katika macho ya Khalifa kuliko Masahaba wa kawaida wa Mtume, kama Jabir Abdallah na Khuzaima bin Thabit.

2. Wameuharibu utukufu na ukubwa wa Qur'an, na kuifanya kufaa kutumika kwa manufaa ya mtawala, mfumo uloanzishwa ambao maneno ya Khalifa yameweza kubadili/kufuta hukumu za wazi za Qur'an. Kwa njia hii wameunyima Ummah mwongozo wa Qur'an na wa Ahlul'l-Bayt daima, na viwili hivi hulinda salama dhidi ya kupotea.

Ilikuwa ni kwa sababu ya kuviacha vitu vizito viwili hivi Ahul'l-Bayt na Qur'an, katika utaratibu ambao kwamba sheria za mirathi, maarifa ya sheria na ushahidi vilipotoshwa, kwamba Fatimah aliwakasirikia sana watu hawa wawili. Bukhari na Muslim wamesimulia: "Hakika Abu Bakar alikataa kutoa chochote kwa Fatimah, hivyo alimkasirikia kuhusu suala hili, alimtelekeza na hakuzungumza naye mpaka kifo chake. 2 3

Maelekezo kwa urefu yanaweza kuonekana katika Sharh Nahju'l-Balagha ya Ibn Abi'l- Hadid, J. 16; Siratun-Nabi ya Al-Halabi, al-Imamah was-Siyasa ya Ibn Qutaibah; Wafa'ul-Wafa ya Ali Al-Samhudi na vitabu vingi vya hadithi na historia. Fadak cha Sayyid Mohammed Hasan Al-Musawi Qazwini, anatupa mwanga juu ya vipengele vyote muhimu vya kadhia hii katika sura fupi.

Ilichapishwa na an-Najah Publishers, Cairo, mwaka wa 1397 A.H. (1977 C.E.) na maelezo chini ya kurasa ya Baqir Muqaddasi na utangulizi wa Profesa Abdul-Fattah. 23 Bukhari, Sahih, Babu Farzil Khums (Kiarabu na tarjuma ya Kiingereza) Beirut, n.d. J. 4, uk. 208 Muslim, Sahih, J. 5, uk. 154.

VITABU VYETU VYA KISWAHILI 1. Ahlul Kisaa

2. Bibi Mwenye Nuru

3. Bustani ya Elimu

4. Bwana Abu Taalib (a.s.)

5. Biblia Neno la Mungu

6. Fadhail za Seyyidna Ali (a.s.)

7. Fitina za Wahhabi zafichuliwa

8. Familia katika Uislamu

9. Fadak

10. Historia ya Kiislamu

11. Historia ya Chanzo cha Mawahhabi

12. Haja ya Dini

13. Huu ni Ushia

14. Hatimaye Nimeongoka

15. Imam Ali (a.s.)

16. Imam Hassan (a.s.)

17. Imam Hussein (a.s.)

18. Imam Ali bin Hussein (a.s.)

19. Imam Muhammad Al-Baqir (a.s.)

20. Imam Jaffar As-Sadiq (a.s.)

21. Imam Mussa Al-Kazim (a.s.)

22. Imam Ali Reza (a.s.)

23. Imam Muhammad Taqi (a.s.)

24. Imam Ali Naqi (a.s.)

25. Imam Hassan Askari (a.s.)

26. Imam Mehdi (a.s.) Anayengojewa

27. Imam Zamana (a.s.)

28. Imam Mehdi (a.f.t.)

29. Imam Hassan na Imam Hussain 27. Waokoaji wa

Uislamu

30. Jibu la Jibu

31. Kitabu cha Sala

32. Kwa nini Mashia husujudu juu ya Udongo

33. Kitabu cha Saumu

34. Kwa nini Uislamu Umeruhusu Kuoa Wake wengi?

35. Kwa Nini Mtume alioa wake wengi?

36. Kitabu cha Tajwid

37. Kanuni za Ibada

38. Mungu wa Uislamu

39. Mtume wa Amani

40. Muhammad (s.a.w.) Ni Nabii wa Mwisho

41. Madhehebu ya Kishia

42. Maana na Chanzo cha Ushia

43. Mafunzo ya Awali ya Uislamu I

44. Mafunzo ya Awali ya Uislamu II

45. Mafunzo ya Salaa

46. Muhimu wa Hijabu

47. Mambo yampasayo Mwislamu.....

48. Mambo yanayomhusu Maiti

49. Muhimu wa Qur'an

50. Mahojiano baina ya Mlahidi na 48. Imam Jafar As-

Sadiq (a.s.)

51. Mawahhabi na Wauwaji wa Imam Hussein (a.s.)

52. Maombolezo ya Kifo cha Imam Hussain (a.s.)

53. Mashairi ya Masaibu ya Kerbala

54. Maana na Chanzo cha Ushia

55. Nyama ya Nguruwe

56. Ili Niwe pamoja na wakweli

57. Ndoa Katika Uislamu

58. Qasida

59. Risaalatul Huquq

60. Shia na Qur'an

61. Shia na Hadith

62. Shia na Sahaba

63. Sayyid wa Vijana wa Peponi

64. Swali na Jibu

65. Sahifat-e-Sajjadiya

66. Siku ya Kiyama

67. Siku ya Kuzaliwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

Lazima Ikumbukwe

68. Taqiyah ni Nini?

69. Tangazo la Ghadiir

70. Uadilifu wa Mungu

71. Uislamu

72. Uislamu ni nini?

73. Uimamu

74. Ulul-Amri Ni Nani?

75. Utetezi wa Sheria za Ki-Islamu

76. Uchunguzi juu ya Uwahabi

77. Ujumbe wa Nahjul Balagha

78. Ushindi Usiozuilika

79. Utume

80. Ujumbe wa Imam Khomein

81. Uharamisho wa kamari

82. Utakaso wa Roho na usafi wa mwili

83. Uislamu na Ukristo

84. Wasia wa Imam Khumaini

85. Waulizeni Wanaofahamu

MWISHO

YALIYOMO

FADAK FADAK 1

MWANZO WA KITABU 1

DIBAJI 1

FADAK 2

VITABU VYETU VYA KISWAHILI 1. Ahlul Kisaa 9

MWISHO 12