TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE Juzuu 8

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: tafsiri ya Qurani

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
: HASANI MWALUPA
Kundi:

Matembeleo: 12573
Pakua: 3188


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 17 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 12573 / Pakua: 3188
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE Juzuu 8

Mwandishi:
Swahili

11

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA NANE

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ أُولَـٰئِكَ يَنَالُهُمْ نَصِيبُهُم مِّنَ الْكِتَابِ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوْنَهُمْ قَالُوا أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿٣٧﴾

37. Basi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo au anayezikadhibisha Aya zake? Hao ndio itawafikia sehemu yao waliyoandikiwa. Mpaka watakapowafikia wajumbe wetu ambao ni Malaika, kuwafisha, watasema: Wako wapi mliokuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema wametupotea, Na watajishuhudia wenyewe kwamba wao walikuwa makafiri

قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ كُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَّعَنَتْ أُخْتَهَا حَتَّىٰ إِذَا ادَّارَكُوا فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَاهُمْ لِأُولَاهُمْ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ أَضَلُّونَا فَآتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِّنَ النَّارِ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ وَلَـٰكِن لَّا تَعْلَمُونَ ﴿٣٨﴾

38. Atasema: Ingieni motoni pamoja na umma zilizopita kabla yenu za majini na watu, Kila utakapoingia umma utalaani ndugu zake. Mpaka watakapokusanyika wote humo, wa mwisho wao watawasema wa mwanzo wao: Mola wetu! Hawa ndio waliotupoteza basi uwape adhabu ya moto maradufu, Hawa ndio waliopoteza, Atasema: Itakuwa maradufu kwenu nyote, lakini hamjui.

وَقَالَتْ أُولَاهُمْ لِأُخْرَاهُمْ فَمَا كَانَ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ﴿٣٩﴾

39. Na wa mwanzo wao watawaambia wa mwisho wao; basi nyinyi pia hamkuwa na ubora kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma.

WANAOOGOPA NA KUFANYA MEMA

Aya 35-39

MAANA

Enyi: Wanadamu! Watakapowafikia Mitume kutoka miongoni mwenu, wakawaeleza ishara zangu, basi watakaoogopa na kufanya mema, haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu na kizazi chake na akawawekea njia ya kufuata, akawapelekea Mitume wa kuwafahamisha njia hiyo. Akawafanya Mitume ni jinsi ya wale wanaopelekewa Mitume hao. Kwa sababu hilo lina athari zaidi na ni hoja zaidi. Basi atakayesikia na akatii atasalimika na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake.

Na wale watakaokadhibisha ishara zetu na kuzifanyia kiburi, hao ndio watu wa motoni, watadumu humo.

Mwalimu wetu- Mungu awe radhi naye - alikuwa akiwasomea wanafunzi wake sehemu za Kitab anachofundisha na kuwafafanulia kwa maneno wanayoyafahamu wote. Ikiwa sehemu iko wazi na inaeleweka kwa wote, basi husema “Kufafanua ufafanuzi ni mushkeli zaidi ya mishikeli!”. Hapo huiacha sehemu hiyo na kuendelea.

Basi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo au anayezikadhibisha Aya zake?

Yametangulia maelezo katika Juz, 7 (6:21)

Hao ndio itawafikia sehemu yao waliyoandikiwa.

Hao ni wale waliotangulia kutajwa-ambao wamezusha yasiyokuwapo na wakakanusha yaliyopo. Makusudio ya waliyoandikiwa ni ajali na riziki. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu anawaacha wakadhibishaji wamalize umri na riziki waliyoandikiwa.

Mpaka watakapowafikia wajumbe wetu ambao ni Malaika,kuwafisha, watasema: Wako wapi mliokuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema wametupotea hatujui wako wapi wala hawaji kutuokoa na adhabu.

Na watajishuhudia wenyewe kwamba wao walikuwa makafiri.

Kukiri dhambi kunafaa pale inapowezekana kuificha na kukimbia malipo yake. Lakini baada ya kudhihiri kama jua na wakati wa kutekelezwa adhabu yake, hapo kukiri hakufai chochote.

Baada ya makafiri kujishuhudia wenyewe mahakama itafungwa na kutolewa hukumu ya adhabu ya moto.

Atasema: Ingieni motoni pamoja na umma zilizopita kabla yenu za majini na watu.

Makusudio ya uma ni wale wenye mila za kikafiri. Yaani Mwenyezi Mungu atawaambia wale waliokufuru Utume wa Muhammad(s.a.w.w) : Ingieni motoni ikiwa ni malipo ya kukufuru kwenu; kama walivyoingia waliokadhibisha Mitume kabla yenu.

Kila utakapoingia umma utalaani ndugu zake.

Watalaaniana nao walikuwa ndugu katika dini, nasaba na ukwe. Hivi ndivyo wafanyavyo watu wa hawaa na upotevu, wanapendana wakati wa utulivu na siku ya mutumaini, na kuchukiana na kulaaniana wakati ambapo hakuna matumaini wala matarajio yoyote.

Mpaka watakapokusanyika wote humo.

Yaani wakikutana humo, utaanza ugomvi na malumbanowa mwisho wao watawasema wa mwanzo wao: Mola wetu! Hawa ndio waliotupoteza basi uwape adhabu ya moto maradufu.

Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa makusudio ya wa mwanzo wao ni wa kwanza kuingia motoni, na wa nyuma ni wa nyuma kuingia. Wengine wakasema kuwa makusudio ya wa mwanzo ni viongozi na wa nyuma ni wafuasi. Kauli hii ndiyo iliyo sahihi kutokana na kusema:‘Hawa ndio waliotupoteza.’

Kwa sababu mwenye kupoteza hufuatwa, na mwenye kupotezwa hufuata. Wenye kufuata wanataka kuongezewa adhabu wale waliofuatwa. Kwa vile wao ndio sababu ya kupotea kwao.

Atasema: Itakuwa maradufu kwenu nyote, lakini hamjui.

Yaani nyote mtapata adhabu maradufu, lakini kila kundi halijui kiasi cha adhabu ya kundi jingine.

Na wa mwanzo wao watawaambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora kuliko sisi.

Wafuasi wanataka wazidishiwe adhabu viongozi, Kwa hiyo viongozi nao wanasema: Kwa nini mnataka hayo, nasi sote tuna malipo sawa wala hatutofautiana na chochote, kwa nini basi Mwenyezi Mungu atuongezee sisi adhabu zaidi ya nyinyi? Kisha wataendelea kusema ikiwa ni majibu ya maombi ya kuzidishiwa adhabu:

Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma sisi hatukuwalazimisha mlikuwa na hiyari.

إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ ﴿٤٠﴾

40. Hakika wale waliokadhibisha ishara zetu na kuzifanyia kiburi, hawatafunguliwa milango ya mbinguni, Wala hawataingia Peponi mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano, Na hivi ndivyo tunavyowalipa wakosefu.

لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٌ وَمِن فَوْقِهِمْ غَوَاشٍ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٤١﴾

41. Watakuwa na matandiko ya Jahanamu na juu yao shuka za kujifunika, Na hivi ndivyo tunavyowalipa madhalimu.

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wale walioamini na wakatenda amali njema; hatukalifishi nafsi yoyote ila uweza wake; hao ndio watu wa Peponi, watadumu humo.

وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَـٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللَّـهُ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ وَنُودُوا أَن تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾

43. Na tutaondoa chuki vifuani mwao; chini yao itapita mito. Na watasema: Sifa njema zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu ambaye ametuongoza kwenye haya. Na hatukuwa wenye kuongoka wenyewe kama asingetuongoza Mwenyezi Mungu. Hakika Mitume wa Mola wetu walileta haki. Na watanadiwa kuwa hii ndiyo Pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya.

NGAMIA NA TUNDU YA SINDANO

Aya 40-43

MAANA

Hakika wale waliokadhibisha ishara zetu na kuzifanyia kiburi, hawatafunguliwa milango ya mbinguni.

Ishara za Mwenyezi Mungu zinakusanya dalili za kuwapo Mwenyezi Mungu, Utume wa Mitume yake na kila walilolieleza kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kusema kwake Mwenyezi Mungu: Hawatafunguliwa milango ya mbingu- ni ni fumbo la kukataliwa amali zao na kwamba hazitakubaliwa; kama zikubaliwavyo amali za watu wema.

Mwenyezi Mungu anasema:

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ ﴿١٠﴾

“Kwake hupanda neno zuri na tendo jema huliinua” (35: 10)

Wala hawataingia Peponi mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano.

Hili ni sharti lisilowezekana; sawa na kusema:

إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ ﴿٨١﴾

“Kama mwingi wa rehema angelikuwa na mtoto ningekuwa wa kwanza kumwabudu” (43: 81).

Kupatikana sharti la muhali ni muhali. Waarabu hupigia mfano jambo lisilowezekana kwa kusema: “Sitafanya mpaka kunguru aote mvi!” Au “Mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano!”

Na hivi ndiyvo tunavyowalipa wakosefu.

Yaani tunawalipa kwa kuwazuilia Pepo. Pamoja na kuzuiliwa hukuwatakuwa na matandiko ya Jahanamu na juu yao shuka za kujifunika Yaani Jahanamu itawazunguka pande zote.

Na wale walioamini na wakatenda amali njema; hatukalifishi nafsi yoyote ila uweza wake; hao ndio watu wa Peponi, watadumu humo.

Mwenyezi Mungu alipowapa kiaga waasi kwa adhabu ya Jahanamu sasa anawaahidi watiifu Pepo yenye neema watakayo starehe nayo bila ya kuwa na mwisho.

Ameishiria kwa kauli yake: “Hatukalifishi nafsi yoyote ila uweza wake,” kwamba Pepo kwa kadiri ya ukubwa wake, lakini mtu anaweza kuifikia bila ya mashaka wala uzito wowote.

Na kwamba atakayeingia Jahanam ataingia kwa kutaka kwake na hiyari yake.

Na tutaondoa chuki vifuani mwao; chini yao itapita mito.

Kwa nini iweko chuki? Duniani kulikuwa na chuki husuda, ria, uwongo na unafiki, kwa sababu kulikuwa na mafukara na matajiri, madhalimu na wenye kudhulumiwa na aliye mashuhuri na asiyejulikana, lakini Peponi hakuna ufukara, dhuluma wala umashuhuri baada ya Mwenyezi Mungu kumuweka kila mmoja katika daraja yake anayostahiki na cheo alichojichumia. Kila mmoja katika watu wa Peponi anahisi raha kwa kuokoka na Moto wa Jahanamu wala hamwangalii kabisa aliye juu yake:

فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ﴿١٨٥﴾

“Mwenye kuepushwa na moto akatiwa Peponi, basi huyo amefuzu” Juz.4 (3:185)

Na watasema: Sifa njema zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu ambaye ametuongoza kwenye haya. Yaani kwenye njia ya neema hii.

Na hatukuwa wenye kuongoka wenyewe kama asingetuongoza Mwenyezi Mungu.

Hiyo ni shukrani kwa Mwenyezi Mungu juu ya neema zake.

Hakika Mitume wa Mola wetu walileta haki.

Mitume waliwapa habari ya Pepo wakaamini mambo ya ghaibu. Walipoiona kwa macho yao walifurahi ambapo ghaibu imeonekana.

Na watanadiwa kuwa hii ndiyo Pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya.

Neno “Kurithishwa” kwa sababu ya kufanya amali, linafahamisha kwamba Pepo ni haki ya lazima kwa wanaoifanyia amali; sawa na mirathi. Kwa maneno mengine ni kuwa Aya inafahamisha kwamba thawabu ni haki siyo fadhila.

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ أَن قَدْ وَجَدْنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقًّا فَهَلْ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمْ حَقًّا قَالُوا نَعَمْ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿٤٤﴾

44. Na watu wa Peponi watawanadia watu wa Motoni kwamba tumekuta aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni kweli, Je, nanyi pia mmekuta aliyowaahidi Mola wenu kuwa kweli? Watasema ndio, Basi mtangazaji atatangaza kati yao kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya madhalimu.

الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ كَافِرُونَ ﴿٤٥﴾

45. Ambao wanazulia njia ya Mwenyezi Mungu, Na wakataka kuipotosha, Nao hawaiamini Akhera.

WATU WA PEPONI WATAITA

Aya 44 – 45

MAANA

Na watu wa Peponi watawanadia watu wa Motoni kwamba tumekuta aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni kweli, Je, nanyi pia mmekuta aliyowaahidi Mola wenu kuwa kweli?

Watu wa Peponi wanajua fika kwamba watu wa Motoni wamekuta ukweli waliyoahidiwa na kutishiwa, lakini wao watawaelekezea swali hili kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya aliyowaneemesha na kuwakumbusha yale waliyokuwa wakiyasema yakiwa ni pamoja na dharau na stihzai kwa dini ya haki na wafuasi wake.

Watasema ndio.

Maana hakuna njia ya kukataa.

Basi mtangazaji atatangaza kati yao kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya madhalimu.

Kwa laana hii, mtangazaji atainua sauti siku ya Kiyama akiwataja madhal- imu kwa sifa tatu:

1.Ambao wanazulia njia ya Mwenyezi Mungu. Yaani wanawazuia watu kuifuata haki kwa njia mbali mbali.

2.Na wakataka kuipotosha. Hawataki ukweli na ikhlasi wala msimamo, isipokuwa wanataka uwongo, unafiki na hiyana.

3.Nao hawaiamini Akhera. Hawaogopi hisabu wala adhabu kutokana na makosa yao na madhambi.