Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Misingi mikuu ya Dini

UTAMBUZI JUU YA SUALA LA UIMAMU NDANI YA RIWAYA

UTAMBUZI JUU YA SUALA LA UIMAMU NDANI YA RIWAYA

UTAMBUZI JUU YA SUALA LA UIMAMU NDANI YA RIWAYA MEZANI HALISI YA KULIELEWA SUALA LA UIMAMU Hakuna shaka kua kuna hadithi nyingi zilizoelezea sifa za Maimamu (a.s) sifa ambazo zimesababisha kuwatia wasiwasi baadhi ya watu, kwani sifa hizo zimegusia baadhi ya sifa ambazo ni sifa za Mweny enzi Mungu na kuzinasibisha sifa hizo kwa Maimamu (a.s). Kiasi ya kwamba kumetokea baadhi ya watu waliowapandisha cheo Maimamu (a.s) na kuwapa cheo cha Uungu, limetokea hili baada ya pale watu hawa walipoziona zile Hadithi zinazozungumzia sifa kubwa kubwa za Maimamu (a.s), na watu hawa hawahesabiwi kua ni Waislamu ndani ya dini yetu ya Kiislamu na wastahiki kulaaniwa kwani hao ni washirikina waliomshirikisha Mola wao, na kuna wengine walidai kua Mwenye enzi Mungu amewapa Maumamu kazi za Uungu!, nao hao pia wako katika upotofu vilevile na Maimamu (a.s) wako mbali na watu kama hawa, na kuna wele wengine waliobirukia upande wa pili nao ni wale wenye kudai kkua Maimamu (a.s) ni sawa na watu wengine hawana tofauti yeyote na wayu wengine,nao hawa si waumini wa kweli, ama kuna lile kurupu la watu walio katika njia ilionyooka nao ni wale wenye kuamini kua Maimamu (a.s) ni watu maalumu alioteuliwa na Mola wao ili kuuongoza umma huu nao wenye sifa kamili za kuuongoza umma huu na uadilifu wa Mwenye enzi Mungu hudhihirika kwa kupitia kwao na sifa tofauti za Mwenye enzi Mungu hudhihirika kwa kupitia kwa Maimamu (a.s). na pia Maimamu (a.s) ni watu kama watu wenge isipokua wao ni wateuliwa wa Mwenye enzi Mungu nao si Miungu.

Ufafanuzi

MTIZAMO WA MTUME (S.A.W.W) JUU YA SUALA LA UONGOZI

MTIZAMO WA MTUME (S.A.W.W) JUU YA SUALA LA UONGOZI MTIZAMO WA MTUME (S.A.W.W) JUU YA SUALA LA UONGOZI Suala hili linatakiwa kuangaliwa kwa makini kiakili, kwani iwapo tutaliangalia suala hili kimadhehebu tunaweza kupotea njia kayika kusimamisha dalili juu ya suala hili, basi iwapo mtu wa madhehebu ya Kishia ua ya Kisunni atajivua umadhehebu wake na kuliangalia suala hili akiwa nje ya dhehebu lake, na badala yake awe ni mwenye kutumia hoja zilizoegemea kwenye akili safi, hapo ndipo atapoweza kua ni hakimu mzuri katika suala hili. Tukiliangalia kwa ufupi juu ya mtizamo wa Mtume (s.aw.w) katika suala la uongozi, tutaona kua suala hili alilipa uzito mkubwa kabisa na hakua ni mwenye kulipuzia suala hili na kuwaachia watu wafanye watakavyo wao katika kuteua anayefaa kua kiongozi wao, sfikirii kua inayumkini kuwepo mmoja miongoni mwetu anayeweza kusafiri na kuicha nyumba na familia yake bila ya kufikiria kua ni nani anyeweza kumteua ili azishike zile nyadhifa muhimu za familia yake. Na iwapo atakuwepo mtu wa aina hiyo, basi mtu huyo hatothaminiwa na jamii yake, basi vipi Mjumbe wa Alla leo tunasema kua ameuacha umma huu bila la kumteuwa kiongozi atakayeshika nafasi yake baada kuondoka kwake? Leo kila mwenye Dhehebu lake anaamua kulitetea Dhehebu lake bila ya kufahamu kua dini si kuyashangiria yale yaliomo ndani ya Dehebu fulani bali dini kuyafuata yale alio yakweli. Wengine wanadai kua Mtume amemchagua Abuu Bakar kua ndio kiongozi baada ya Mtume (s.a.w.w), na wengine wanadai kua Mtume (s.a.w.w) hakumchagua mtu kua kiongozi baada yake, bali aliwaacha watu wajichagulie wenyewe kiongozi wao! Basi ukweli ni upi kwenye msokotano huu? Basi anza kuutafuta ukweli na kuupima kwa akili yako huku ukizisikiliza hoja za pande zote mbili ili uweze kutoa hukumu isio na dosari, kwani hii ndiyo njia pekee ilio na usalama katika dini yako pamoja na dunia yako.

Ufafanuzi

JAMII KUHITAJIA IMAMU

JAMII KUHITAJIA IMAMU JAMII KUHITAJIA IMAMU Baada kufahamu mitizamo tofauti katika suala la uimamu, sasa kuna haja ya kulijibu suala hili:- Kuna umuhimu gani ya kuwepo Imamu kama Mashia wanavyoitakidi, hali ya kua sisi tuna Qur’ani na tuna Sunna vile vile? JAMII KUHITAJIA IMAMU Baada kufahamu mitizamo tofauti katika suala la uimamu, sasa kuna haja ya kulijibu suala hili:- Kuna umuhimu gani ya kuwepo Imamu kama Mashia wanavyoitakidi, hali ya kua sisi tuna Qur’ani na tuna Sunna vile vile? Kuna dalili nyingi zimetajwa katika umuhimu wa kuwepo Imamu (a.s), lakini tutataja dalili moja:- Kama ilivyokua jamii inahitajia Mtume basi jamii hiyo inahitajia Imamu baada ya kuondoka Mtume, kwa sababu Uislamu ni dini ya mwisho, na Mtume (s.a..w.w) ni Mtume wa mwisho, kwa hiyo dini hii inatakiwa kuyatatua matatizo yote ya waislamu hadi kufikia siku ya Kiama, na kama inavyoeleweka kua Qur’ani imeelezea misingi mikuu ya dini kiujumla bila ya kufafanua, na mfafanuaji wa misingi hiyo alikua ni Mtume (s.a.w.w), na bila ya shaka Mtume (s.a.w.w) aliifafanua misingi hiyo kwa jinsi hali na mahitajio ya jamii ya zama zake, kwa hiyo basi kila zama zinahitajia Imamu atakayeyatatua matatizo ya watu wa zama hizo na kuifasiri Qur’ani kwa jinsi ya zama zake zilivyo.

Ufafanuzi

UIMAMU KWA MTIZAMO WA KISUNNI NA KISHIA

UIMAMU KWA MTIZAMO WA KISUNNI NA KISHIA UIMAMU KWA MTIZAMO WA KISUNNI NA KISHIA UIMAMU Suala la mwanzo lililoleta utata ndani ya jamii changa ya kiislamu baada ya kuondoka Mtume (s.aw.w), ni suala la ukhalifa, kundi fulani ambalo lilitegemea rai za baadhi ya masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w), lilimkubali Abuu Bakar, na kundi jengine liliitakidi kua nafasi hii ni ya Ali (a.s) kwa chaguo la Mtume (s.a.w.w), na baada ya kupita zama fulani, kundi la kwanza likajulikana kwa jina la (Sunni), na kundi la pili likajulikana kwa jina la (Shia). Kitu muhimu cha kukiashiria hapa, ni kua malumbano na tofauti baina ya Shia na Sunni, si katika suala la kua ni nani atakaeshika nafasi ya Mtume (s.a.w.w) baada ya kufa kwake, bali tofauti za makundi haya mawilili zipo katika kulifasiri neno (imamu), pamoja na nafasi ya neno hili, hapo ndipo kila moja kati ya makundi haya mawili linapotafautiana na jenziwe. Neno uimamu katika lugha lina maana ya kuto kutanguliwa (yaani kuwepo mbele kuliko wote waliobakia), na Imamu ni yule mtu mwenye kuliongoza kundi fulani katika njia na misingi maalum, na neno hili katika dini ya kiislamu, limefasiriwa katika maana tofauti.Kwa mtizamo wa madhehebi ya Kisunni, uimamu ni cheo cha kidunia na wala si cheo maalum cha Mwenye enzi Mungu ambacho humpa mja wake anayestahiki, na kwa kutokana na kwamba kila jamii inahitajia kua na kiongozi, basi jamii ya kiislamu vile vile baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.w) inatakiwa kujichagulia kiongozi atakayeyasimamia mambo yao, na kwa kutokana na kua hakujawekwa njia maalum ndani ya uislamu katika kumchagua kiongozi, basi kunaweza kukatumika njia tofauti katika suala hili, kama vile kuzisikiliza rai za walio wengi, au kuwasikiliza wakubwa wanasemaje, au kufuata wasia wa makhalifa waliopita, au hata kupitisha mapinduzi kama itawezekana.

Ufafanuzi

UFAFANUZI JUU YA UIMAMU NDANI YA QURANI NA HADITHI

UFAFANUZI JUU YA UIMAMU NDANI YA QURANI NA HADITHI UFAFANUZI JUU YA UIMAMU NDANI YA QURANI NA HADITHI Katika riwaya mbalimbali limeelezewa suala la kua Maimamu (a.s) ni watambuzi wa mambo yaliopita na yajayo, na kumesisitizwa vilevile kua elimu na utambuzi huu walionao ni yenye kutokana na Mwenye enzi Mungu (a.s), naye ndiye aliyewapatia elimu hii na Wao hawana uwezo wowote mbele ya Mola wao na yote wayafanyayo ni kwa uwezo wa Mola wao, na Gheibu walionayo maimammu (a.s) sio Gheibu ya kujua kila kitu bali ni baadhi mambo tu, kwani hawana habari ya kua siku gani Kiama kitasimama, kwani mjuzi wa siku hii Mwenye enzi Mungu tu peke yake. ELMU GHAIBU YA MAIMAMU (A.S) Elimu ya Mwenye enzi Mungu iko katika namna mbili: Elimu ambayo hakuna aijuayo ila Yeye tu peke yake, na hata Malaika na Mitume (a.s) hawana habari nayo, na sehemu ya pili ya elimu ni ile elimu ambayo huwafunulia Malaika wake na Malaika nao huifikisha elimu hiyo kwa mitume wanaohusika, kama vile ilivyomfikia elimu hiyo Mtume wetu (s.aw) yeye pamoja na kizazi chake (Ahlul bait) (a.s) , ili elimu hiyo ibakie milele hadi siku ya Kiama kwa kupitia kizazi chake, na Mwenye enzi Mungu (s.w) ameliashiria suala hili katika Qurani akisema: (Yeye ni mjuzi wa yale ya ghaibu (asiotambulikana) na yale yalio dhahiri (yenye kujulikana au kushuhudiwa, naye hayadhihirishi yaliofichika (yale ya ghaibu) kwa mtu yeyote yule, isipokua huwadhihirishia wale aliowaridhia miongoni mwa mitume).

Ufafanuzi

AHLUL BAIT NI AKINA NANI?

AHLUL BAIT NI AKINA NANI? AHLUL BAIT NI AKINA NANI? Swali muhimu kabisa ambalo tungependa kulijibu sasa ni Ahlul Bait ni akina nani? Au Ahlul Bait ni wepi? Hapa pia tutatoa majibu kutoka katika vitabu vya Sunni tu. 1- Muslim anasimulia katika Sahihi yake kutoka kwa Safiya bint Shaibah ambaye aliripoti kuwa: "Siku moja Aisha bint Abubakar alisema: "Siku moja Mtume wa Allah alikuwa amejifunika KISAA (blanket kubwa), kisha akaja Imam Hassan (a.s) na Mtume akamuita na kumfunika na Kisaa. Kisha akaja Imam Husayn (a.s) na pia Mtume akamfunika. Kisha akaja Fatima (a.s) na Mtume akamfunika kwa Kisaa. Kisha akaja Imam Ali (a.s) na Mtume pia akamfunika kwa Kisaa. Kisha akasema: "INNAMAA YURIIDULLAHU LIYUDH'HIBA ANKUMUR RIJSA AHLAL BAYTI, WA YUTAHHIRUKUM TATHIIRA". Maana yake ni kwamba "Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul Bayt na anataka kukutakaseni mtakaso ulio bora kabisa". (Suratul Ahzab 33:33). Hadithi hii inaonyesha waziwazi kuwa Ali, Fatma, Hassan na Hussein ndio Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambao wameteuliwa na Mtume kuwa viongozi wetu, Angalia Sahih Muslim, (Jz. 5, Uk. 287). 2- Katika Sahihi Muslim imeripotiwa kuwa: "Aya ifuatayo iliposhuka nayo inasema hivi: "Na atakayebishana nawe baada ya kukujia elimu, basi mwambie: Tuwaite watoto wetu na watoto wenu, wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, na kisha tuombe kwa unyenyekevu laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo (Aya ya Mubahilah, Aali Imran 3:61); Mtume aliwaiita Ali, Fatima, Hassan, na Hussein na akasema: "ALLAHUMAA HAA'ULAAI AHLII" - Ewe Mwenyezi hawa ndio watu wa nyumbani kwangu, Ahlul Bayt". (Tazama Sahih Muslim, Jz. 5, Uk. 268).

Ufafanuzi

USHAHIDI WAHADITHI YA SAFINA (JAHAZI)

USHAHIDI WAHADITHI YA SAFINA (JAHAZI) USHAHIDI WAHADITHI YA SAFINA (JAHAZI) 5- USHAHIDI WAHADITHI YA SAFINA (JAHAZI) Katika kitabu cha Kisunni : kiitwacho Mustadrak Sahihein kimeeleza kua imesimuliwa na Hakim kupitia kwa Hanash Al- Kanani ambaye alisema: Nimemsikia Abudhar Al-Ghafari akisema wakati ambapo alikuwa ameushika mlango wa Ka'ba Tukufu: "Enyi watu, wale wanaonijua mimi ni nani hawanahaja ya kupewa habari kwa wao wananijua, lakini wale wasionijua na wajue kuwa mimi ni Abudhar (Sahaba wa Mtume). Nimemsikia Mtume (s.a.w.w) akisema: "Mathalu AHLULBAYTII FIIKUM MATHALI SAFIINATIN NUUH, MAN RAKIBAHA NAJAA, WA MAN TAKHALLAFA ANHA GHARIKA". - "Mfano wa Ahlul Bayt wangu ni kama Jahazi ya Nuuh (a.s). Kila aliyeipanda aliokoka, na kila aliyejiepusha nayo aligharikishwa (alizama)". Mwanachuoni wa Kisunni Hakim amesema kwamba hadithi hii ni Sahihi. Pia hadithi hii ya Safiina imesimuliwa na mamia ya wanazuoni wa Kisunni katika vitabu vyao. Umewahi kumsikia mwanazuoni yeyote wa Kisunni akiizungumzia hadithi hii kwenye hotuba yake? Kama hujawahi , basi wanazuoni hao wanaificha. Lakini unaweza kurejea vitabu vifuatavyo vya Kisunni na utaipata hadithi hii: • Al-Haakim katika kitabu chake Mustadrak, Juz. 2, Uk. 343. Sawaiq Muhriqah, Uk. 153. Faraid Simtein, Juz.4,Uk. 149. Mustadrak Sahihein, Juz.3, Uk. 343. Nuurul Absaar, Uk. 126, na vitabu vingine vingi tu.

Ufafanuzi

HADITHI YA UMMU SALAMAH

HADITHI YA UMMU SALAMAH HADITHI YA UMMU SALAMAH HADITHI YA UMMU SALAMAH KATIKA MAPOKEZI YA BUKHARIY Katika Mustadrak As-Sahihain amepokea Al-Hakim kwa Isinadi yake kutoka kwa Hanashi Al-Kinaaniy, amesema: " Nilisikia Abudhar anasema akiwa ameshika mlango wa Ka'aba: Enyi watu anayenijua basi mimi ni yule mnayemjua na asiyenijua basi mimi ni Abudhari, nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema mfano wa Ahlul-baiti wangu kwenu ni kama mfano wa jahazi la nuhu atakayelipanda amenusurika na atakayeacha kulipanda ameghariki" .13 Vilevile katika Mustadrak As-Sahihain kwa Isnad yake kutoka kwa Ibunu Abbas: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) "nyota ni tumaini kwa watu wa ardhini kutokana na kughariki, na Ahlul-baiti ni tumaini kwa umma wangu kutokana na Ikhitilafu, kama kabila katika waarabu litawakhalifu basi watakhitalifiana na kuwa kundi la Iblisi". 14

Ufafanuzi

UTUME WA NABII MUHAMMAD (S.A.W.W)

UTUME WA NABII MUHAMMAD (S.A.W.W) UTUME WA NABII MUHAMMAD (S.A.W.W) Kupewa Utume Nabii Muhammad (saw) Lilikuwa Tukio Muhimu katika Historia ya Mwanadamu Kiongozi Mauadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema kuwa kubaathiwa na kupewa utume Nabii Muhammad (saw) lilikuwa tukio muhimu katika historia ya mwanadamu na akaongeza kuwa haja kubwa zaidi ya jamii ya Kiislamu hii leo ni kutekeleza ujumbe wa kubaathiwa Mtume, kuipa umuhimu akili na mantiki, kueneza maadili mema na kuheshimu sheria na nidhamu katika jamii. Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo katika hadhara kubwa ya viongozi wa mfumo wa Kiislamu na matabaka mbalimbali ya wananchi waliokwenda kuonana naye kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya kupewa utume na kubaathiwa Nabii Muhammad rehma na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na Aali zake. Amesisitiza kuwa wadhifa wa wasomi na shakhsia wakuu wa jamii ni mkubwa na wenye umuhimu zaidi katika uwanja huo.

Ufafanuzi

MDAHALO NA AHMAD DEEDAT

MDAHALO NA AHMAD DEEDAT MDAHALO NA AHMAD DEEDAT Ulimwengu wa Kiislamu ulipata taarifa nzito za kuondokewa na mmoja wa wanaharakati wake mashuhuri Sheikh Ahmed Deedat wa Afrika Kusini. Deedat ni mwanazuoni mashuhuri katika fani ya Mlingano wa dini, Compatarative Religion. Alisafiri huku na kule duniyani katika harakati za kutowa mihadhara na kushiriki katika midahalo baina yake na wawakilishi wa imani ya Kikristo. Katika mihadhara na midahalo hiyo aliweza kuwavutiya mno wasikilizaji kwa ule umahiri wake wa kujenga hoja pamoja na ufasaha wa lugha ya Kiingereza. Aidha sheikh Deedat ameandika vitabu vingi vyenye mada na maudhuwi mbalimbali. Kwa pamoja mihadhara, midahalo na vitabu vyake vimeleta athari kubwa ulimwenguni. Mbali na watu wa imani nyingine kuuona ukweli wa imani ya Kiislamu, piya vimetowa changamoto kwa Waislamu wengi duniani ambao wamerithi kazi yake. Kwa hali hii, licha ya kufikwa na umauti, Deedat ataendeleya kuwa hai kutokana na kazi hizo muhimu alizozifanya. Sote lazima tutoweke duniani lakini wapo waja wa MwenyeziMungu ambao watabakizwa hai na yale waliyoyafanya. Sheikh Deedat ni mfano wa waja hao. Tunamuomba MwenyeziMungu aikubali juhudi yake, amghufiriye upungufu wake na amkutanishe na waja wema Peponi-Inna lillahi wainna ilaihi rajiuun. Katika makala haya tunarejeleya moja ya maandiko yake: Majibizano ya Waislamu na Wakristo: Mdahalo katika televisheni-1983 (Na Ahmed Deedat)

Ufafanuzi

UIMAM

UIMAM Utangulizi: Bila shaka kila mtu anatambua kuwa serikali iliyoundwa nchini kwa lengo la kuyashughulikia masuala ya wananchi haiwezi kujiongoza yenyewe. Iwapo watu wanaofaa na wenye ujuzi hawatajitokeza kutekeleza shughuli zake basi bila shaka serikali hiyo haitadumu wala kuwahudumia wananchi. Hali yo pia inahusika na taasisi nyinginezo katika jamii ya Mwanadamu kama vile taasisi za kiutamaduni,za kiuchumi,za kielimu na kadhalika.Daima taasisi kama hizi huwategemea wakurugenzi wanaofaa na waaminifu,la sivyo zitaanguka au huanguka na kufungwa katika kipindi.Hii ni hakika iliyokuwa wazi ambayo inaweza kuonekana hata kwa mtazamo wa kaiwada tu.Uzoefu mwingi pia unaelezea ukweli na hakika hii.Hivyo si lazima na haihitaji mtu uwe na maelimu mengi sana ili kutambua hakika hii na ukweli huu! Ikiwa hili litathibiti,basi kutakuwa hakuna shaka kwamba taasisi ya Dini ya Kiislaam ambayo naweza kusema ni taasisi kubwa sana duniani, nayo hufuata mfumo huu.Taasisi hii ya Dini ya Kiislaam huwategemea wasimamizi na viongozi ili iendelee kudumu.Daima huwatafuta watu wanaofaa kwa lengo la kuwapa mafundisho ya Kiislaam na kutekeleza sheria katika jamii ya Kiislaam na pia kutoacha nafasi au fursa yoyote ya uvunjaji sheria katika kuulinda Uislaam.

Ufafanuzi

ABUU BAKAR ANAMPA UKHALIFA JAMAA YAKE

ABUU BAKAR ANAMPA UKHALIFA JAMAA YAKE BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM ABUU BAKAR ANAMPA UKHALIFA JAMAA YAKE      Abubakr anampa ukhalifa jamaa yake Umar, na anakhalifu maandiko yaliyo wazi kuhusu jambo hilo. Amesema Imam Ali (a.s) kuhusiana na suala la Ukhalifa: "Ama Wallahi ameuvaa (Ukhalifa) mtoto wa Abu Quhafa hali ya kuwa anajua kabisa kwamba nafasi yangu katika huo Ukhalifa ni kama nafasi ya mpini ulioko kwenye jiwe la kusagia nafaka." Akielezea kwa njia ya kinaya Imamu (a.s.) anasema: "Hububujika kutoka kwangu fadhila kwa vile Mungu alinienzi kwa kuniweka karibu na materemkio ya wahyi, hivyo basi nilijizuia nikakaa mbali nao, nikawa nafikiri kati ya kuingia vitani hali nikiwa mikono mitupu, au nivute subira katika giza lililoshona hakika mtu mzima huzeeka, na mtoto huwa kijana. Muumini atataabika kwa juhudi kubwa kubakia na imani safi katika hali hiyo mpaka akutane na Mola wake." Anaendelea kusema, "Niliona kusubiri ni bora na ni hekima, basi nikasubiri hali katika macho kuna tongo tongo na shingoni kuna mwiba umenasa, naouna urithi wangu nimenyang'anywa. Wa kwanza akaenda kisha akampasia mtoto wa Khatab baada yake, ajabu ilioje kwamba yeye (Abubakr) alitaka kujitoa katika ukhalifa alipokuwa hai na ampasie mwenzake ashike baada ya kifo chake ili kudhibiti walichokigawa nusu mbili, kila mmoja akawa mgumu hagusiki na anajikwaakwaa akitaka udhuru."

Ufafanuzi

MA'AD {UFUFUO}

MA'AD {UFUFUO} MA'AD {UFUFUO} Assalaam Alaikum. Ma'ad ni moja kati ya Nguzo Kuu tatu za dini tukufu ya kiislaam na mojawapo ya mambo muhimu katika dini hii tukufu.Tunatambua wazi kuwa kila Mtu anaweza kutofautisha kati ya vitendo vizuri na vibaya kwa kutumia maumbile aliyopewa na na eliyemuumba (yaani Mwenyeezi Mungu -s.w-).Utakuta kila mtu anauchukulia wema (hata kama yeye binafsi hafanyi wema) kuwa ni jambo zuri na lenye kupaswa kutekelezwa na kwamba vitendo vibaya na viovu (hata kama yeye binafsi ni mtenda maovu) ni jambo baya sana na linalopaswa kuachwa. Bila shaka yoyote,ubaya na uzuri na wema pia,yote haya yanatokana na mitazamo ya matokeo na pia malipo ya sifa hizi mbili.Vile vile kila mtu atakubaliana na mimi katika kauli hii kwamba hakuna hata siku moja mtenda matendo mazuri akakosa kupata malipo ya matendo yake mazuri na mtenda matendo maovu akakosa kupata malipo ya matendo yake maovu.Lakini hapa mtu anaweza kuuliza swali hili:Mbona kila tukichunguza kwa jicho kali sana tunatakuta watenda mema huishi katika mashaka na matatizo na wakati huo huo watenda maovu na mabaya walio wengi ambao huhusika kikamilifu na uhalifu na ukatili na unyama pamoja na kuwa na tabia zote mbaya na khabithi wanaishi katika hali ya furaha na saada?.!

Ufafanuzi

KUTHIBITISHA KUWEPO KWA MUUMBA.

KUTHIBITISHA KUWEPO KWA MUUMBA. SOMO LA PILI. Mwanadamu pindi anapozitumia hisia zake halisi hupata dalili nyingi katika kila pembe ya dunia za kuthibitisha kuwepo kwa Muumba wa Ulimwengu huu.Kwa kutumia hisia hizo huweza kutambua vyema kuwa viumbe vyenye uhai ambavyo kwa hiari au bila hiari hufuata njia makhsusi na baada ya kipindi fulani huviachia viumbe vingine nafasi yavyo,kwani haviwezi kuwa vimejipa uhai venyewe.Njia hiyo yenye utaratibu huo maalum ambayo hufuatwa na viumbe hivyo haikuumbwa na viumbe hivyo.Viumbe hivyo havina hata uwezo mdogo wa kuchangia katika uumbaji wala kuratibu njia ya maisha yavyo.Na hii ni kwasababu mwanadamu hakujichagulia uwanadamu wake wala sifa zake bali ameummbwa tu na kupewe sifa hizo za uwanadamu.Kwa njia hiyo hiyo maumbile safi ya mwanadamu hayakubali kuwa kuna kitu kimejiumba au kimetokea hivi hivi chenyewe kighafla kighafla na hayakubali pia kuwa mfumo wa maisha yake hayana lengo lolote(maumbile ya mwanadamu hayakubali fikra ya namna hii).

Ufafanuzi

MAANA YA UIMAMU KILUGHA NA KIISTILAHI

MAANA YA UIMAMU KILUGHA NA KIISTILAHI MAANA YA UIMAMU KILUGHA NA KIISTILAHI UIMAMU KIISTILAHI Maana ya pili:Ni maana khaasi na ambayo ni Istilahi ya Kisheria, au kwa ibara nyingine tunaweza kusema kwamba Imam kiistilah ni yule aliyeteuliwa na Mwenyeezi Mungu (s.w) kuwa Imam na Imam Kilugha ni yule yeyote ambaye kuteuliwa kwake hakunasibishwi kwa Mwenyeezi Mungu (s.w). Hivyo mtu yeyote na kitu chochote ambacho ni kiongozi au ambacho kinafuatwa,kilugha huitwa Imam,sawa sawa awe Mtu,au Kitabu au kitu chochote kile. Katika Qur'an Tukufu maana hii ya Imam kilugha pia imetumika.Kwa mantiki hiyo,Watu na hata Kitabu,vitaitwa au vitatumia (yaani vitu hivi viwili) jina la Imam.Na watu,ni neno linalo jumuisha watu wazuri na watu wabaya,katika kundi la watu wazuri ambao kuteuliwa kwao kunanasibishwa katika upande wa Mwenyeezi Mungu (s.w) au ukitaka sema:(walioteuliwa na Mwenyeezi Mungu s.w),kwa mtazamo wa kilugha watu hao wataitwa (Maimam) au watatumia jina la Imam.Na vile vile kundi la upande wa pili,yaani watu wabaya (au hata kama si wabaya) ili mradi tu ikithibitika kuwa wamefanikiwa kujipatia uongozi,lakini kuchaguliwa kwao au uteuzi wa watu hao si kutoka kwa Mwenyeezi Mungu (s.w) bali kutoka kwa asiyekuwa yeye (s.w),kwa mtazamo wa kilugha pia watu hao wataitwa Maimam au watatumia jina la Imam.

Ufafanuzi

UKHALIFA

UKHALIFA UKHALIFA JAWABU KWA SHEIKH MAZRUI Baada ya kifo cha mtume Suala la Ukhalifa ni suala nyeti sana, sina budi kabla ya kumjibu Bwana Juma Mazrui niwaletee habari muhimu zilizotokea kabla ya tukio la Ukkhalifa na kama zilivyoelezwa na Hadithi sahihi na masimlizi ya Historia katika Vitabu tunavyovitegemea: Sina budi kumshukuru Bwana Juma Mazrui kwa jitihada zake za kutaka kuwaelewesha watu kuwa Seyyidna Ali hakuwa Khalifawa Kwanza wa Waisilamu, pia nawaomba wasomaji pia wawe na subira katika kusikiliza Upande wa pili wa maoni ya Waisilamu Huru usiotaka kushutumu yo yote kati ya Shia na Sunni juu ya suala hili. Kwanza kabisa, Mtume Muhammad alikufa mwaka 632 AD, alikufa kutokana na ahadi yake kufika na baada ya kupewa sumu kule Khaybar baada ya kuiteka ngome ya wayahudi wa Khaybar. Mtume Muhammad (s) baada ya ushindi wake dhidi ya Mayahudi wa Khaybar alikubaliana nao na kuwapa sharti ya kulipa jizya, walilipa nusu ya mazao wanayovuna hapo Khaybar kwa Dola ya Kiislamu ya Madina. Baada ya kufa kwa Mtume Muhammad (s) mayahudi waliobakia Khaybar waliondolewa na kufukuzwa kutoka madina na Khalifa wa pili Omar Bin al-Khattab.

Ufafanuzi

UTAKASO WA MAIMAMU NO.3

UTAKASO WA MAIMAMU NO.3 UTAKASO WA MAIMAMU (A.S) NO.1 ISMAT IMAMU. Moja katika sifa na sharti muhimu zinazomuwajibikia Imam kuwa nazo ni ismati, (ismati yaani kuepukana na maovu na kutofanya madhambi). Imamu anatakiwa kuwa ni mwenye elimu ya hali ya juu ili aweze kuwaongoza wengine, na kwa sababu mbili hizi (yaani kutokufanya madhambi na kuwa na elimu ya hali ya juu) Imamu hujizuia na kuitakasa nafsi yake na maovu, na kujiepusha kufanya madhambi, basi kwa vile Imamu ni mwenye kuelewa na kufafanua masuala ya dini, yeye ndie anayefahamu vipi tunatakiwa kuyafanyia kazi masuala hayo, na huyapambanuwa yale yenye kuleta maslahi na yenye kuleta ufisadi na upotovu katika jamii ya kiislamu. kwa maelezo zaidi unagana nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

UTAKASO WA MAIMAMU NO.2

UTAKASO WA MAIMAMU NO.2 UTAKASO WA MAIMAMU (A.S) NO.1 ISMAT IMAMU. Moja katika sifa na sharti muhimu zinazomuwajibikia Imam kuwa nazo ni ismati, (ismati yaani kuepukana na maovu na kutofanya madhambi). Imamu anatakiwa kuwa ni mwenye elimu ya hali ya juu ili aweze kuwaongoza wengine, na kwa sababu mbili hizi (yaani kutokufanya madhambi na kuwa na elimu ya hali ya juu) Imamu hujizuia na kuitakasa nafsi yake na maovu, na kujiepusha kufanya madhambi, basi kwa vile Imamu ni mwenye kuelewa na kufafanua masuala ya dini, yeye ndie anayefahamu vipi tunatakiwa kuyafanyia kazi masuala hayo, na huyapambanuwa yale yenye kuleta maslahi na yenye kuleta ufisadi na upotovu katika jamii ya kiislamu. kwa maelezo zaidi unagana nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

UTAKASO WA MAIMAMU NO.1

UTAKASO WA MAIMAMU NO.1 UTAKASO WA MAIMAMU (A.S) NO.1 ISMAT YA IMAMU. Moja katika sifa na sharti muhimu zinazomuwajibikia Imam kuwa nazo ni ismati, (ismati yaani kuepukana na maovu na kutofanya madhambi). Imamu anatakiwa kuwa ni mwenye elimu ya hali ya juu ili aweze kuwaongoza wengine, na kwa sababu mbili hizi (yaani kutokufanya madhambi na kuwa na elimu ya hali ya juu) Imamu hujizuia na kuitakasa nafsi yake na maovu, na kujiepusha kufanya madhambi, basi kwa vile Imamu ni mwenye kuelewa na kufafanua masuala ya dini, yeye ndie anayefahamu vipi tunatakiwa kuyafanyia kazi masuala hayo, na huyapambanuwa yale yenye kuleta maslahi na yenye kuleta ufisadi na upotovu katika jamii ya kiislamu. kwa maelezo zaidi unagana nami mpaka tamati mwa makala hii.

Ufafanuzi

FAIDA ZA KUTOWEKA IMAMU MUOKOZI NO3

FAIDA ZA KUTOWEKA IMAMU MUOKOZI NO3 FAIDA ZA KUTOWEKA IMAMU MUOKOZI NO.1 Kutoweka kwa Imam kunaleta faida gani katika dunia?. Ni zaidi ya miaka mia sasa walimwengu wamekutwa na msiba wa kutomuona Imam. Na kwa upande wa Waislamu imekuwa ni msiba mkubwa zaidi kwani hawakumuona Imam wao na kufaidika na neema za mtu huyo. Hivi kupotea Imam machoni mwa watu kunaleta faida gani kwa watu na jamii kwa ujumla? Baadhi ya watu wanasema kwa nini Imam Mahdiy (a.s) asingelizaliwa karibu na wakati wa kudhuhuru kwake ili wafuasi wake wakaondokana na msiba huu waliokuwa nao sasa?.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini