TASHAHHUD
BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI.
TASHAHHUD
Tashahhud (Tahiyatu) : Baaa ya sijda ya pili ukae na usome: Ash- hadu al laa ilaaha illallaahu wahdahu laa shariika lah, wa ash- hadu anna Muhammadan `abduhu wa rasuluh Allaahumma swalli `alaa Muhammadin wa Aali Muhammad Nashuhudia kwa hapana Mola ila Allah, aliye wa pekee asiye na mshirika. Na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja na mtume wake. Ewe Mola, mtakie rehma Muhammad na Aali zake. Ikiwa unaswali Swala ya Al-Fajr (Alfajiri), wacha mengine na uende kwenye maelezo ya sehemu ya Mwisho.
Ikiwa unaswali Swala ya Dhuhr (Adhuhuri), ya`Asr (Alasiri), ya Maghrib (Magharibi), au ya`Isha (Usiku), endelea kwa kusimama kwa rakaa ya tatu huku ukisoma Bihawlillahi…kama ilivyoelezwa kwenye mwisho wa sehemu ya Rakaa ya kwanza.
Rakaa ya tatu
At-Tasbihat ul-Arba`ah (Tasbihi nne) :
baada ya kuinuka na kusimama wima, hapo, aidha utasoma Surat al-Fatiha, au utasoma al-Tasbihat ul-Arba`ah mara tatu, kama ifuatavyo:
Subhaanallaahi wa'l hamdu lillaahi wa laa ilaaha illallaahu wallaahu akbar Utakatifu ni wa Mwenyezi Mungu, Shukrani zote ni za Mwenyezi mungu; hapana Mola apasaye kuabudiwa ila Allah, naya ni Mkuu.
Utarukuu, simama kwa muda mfupi, kisha utasujudu. Hii ni kama ilivyoelezwa katika sehemu ya maelezo ya Rakaa ya kwanza. Ikiwa unaswali Swala ya Maghrib (Magharibi), utasoma Tashahhud baadaye. Kasha wacha mengine na uende kwenye maelezo ya sehemu ya Mwisho.
Ukiwa unaswali Swala ya Dhuhri (Adhuhuri), ya`Asr (Alasiri), au ya `Isha (Isha), utaendelea kwa kusimama kwa rakaa ya nne huku ukisoma Bihawlillahi…. kama ilivyoelezwa katika mwisho wa sehemu ya maelezo ya Rakaa ya kwanza.
Rakaa ya nne
Hii ni kama rakaa ya tatu. Baada ya kusujudu endelea na kukaa, na usome Tashahhud.
Mwisho
Baada ya kusoma Tashahhud ya Rakaa ya mwisho, soma Taslim (Salaam) ambayo itakamilisha Swala yako, nayo ni:
Assalaamu `alayka ayyuhan nabiyyu wa rahmatullaahi wa barakaatuh
Assalamu `alaynaa wa `alaa `ibaadillaahis swaalihiin
Assalamu `alaykum wa rahmatullaahi wa barakaatuh
Amani iwe juu yako ewe Nabii na pia ziwe juu yako rehma za Allah na baraka zake.
Amani iwe juu yetu na juuya waja wako wema.
Amani iwe juu yenu (nyote) na pia rehma na baraka za Allah ziwashukie.
Kisha baadaye (ukipenda) soma Takbir mara tatu.
"…na mtakapopata amani (mkawa katika salama, hakuna vita) basi simamisheni Swala (kama kawaida). Kwa hakika Swala kwa Wanaoamini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalum." (Qur'an: Sura 4, Aya 103)
Jinsi ya kuswali Swala za kila siku
Ni wajibu kuswali Swala tano zifuatazo kila siku kwa nyakati zilizowekwa:
" Salat al-Fajr (Swala ya Alfajiri), ambayo ina rakaa mbili
" Salat al-Dhuhr (Swala ya Mchana) yenye rakaa nne
" Salat al-`Asr (Swala ya Alasiri) ambayo ina rakaa nne
" Salat al-Maghrib (Swala ya Magharibi) yenye rakaa tatu
" Salat al-`Isha ( Swala ya Usiku) yenye rakaa nne.
Kuswali Swala tano za kila siku kulingana na madhehebu ya Shia Ja'fariyya ni kuswali kulingana na utaratibu (tartib) na kuzifuatanisha, pasi na kuchelewa kati yazo (muwalat). Mwenye kuswali anahitajika kwanza ajitoharishe ( kwa ghusl, ikibidi, au kwa wudhu) na anahitajika kufanya mengine ya msingi yanayohitajika kabla ya Swala.
Matayarisho
Simama wima ukielekea Qiblah (kuelekea Makka) kisha uadhini (adhan) na usome iqama. Na fahamu ya kwamba visomo vyote utavyosoma wakati wa Swala viwe ni kwa lugha ya kiarabu. Japokuwa namna ya kutamka imeelezwa hapo chini kwa kila kisomo, ni vizuri kujaribu kusoma maandishi na matamshi ya kiarabu.
Niyya :
Tia nia kwa maneno haya akilini mwako: "Naswali Swala hii ____ (taja Swala unayoiswali), yenye rakaa ____ (taja ni rakaa ngapi) kwa kutaka ukaribu wa Mwenyezi Mungu."
Rakaa ya kwanza
Takbiratul Ihram : Inua mikono yote miwili juu kufikia masikioni na useme:
Allaahu akbar Mungu ni mkuu Neno hili, la Takbir, litarudiwa mara kwa mara wakati wa Swala.
Qiyam :
Uendelee kusimama wima wakati utaposoma kwenye hatua nyingine ya Qira'ah.
Qira'ah :
Mwanzo, soma Sura ya kwanza katika Qu'an tukufu, Surat al-Fatiha
Bismillaahi'r-Rahmaani'r-Rahiim
Al-hamdu lillaahi rabbil-`aalamiin
Arrahmaanir rahiim
Maaliki yawmid-diin
Iyyaaka na`budu wa iyyaaka nasta`iin
Ihdinas-swiraatwal-mustaqiim
swiraat al-ladhiina an`amta `alayhim
ghayril maghdhuubi `alayhim
wa la'dhwaal-lliin
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu. Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu Mwenye mamlaka siku ya malipo; Ni wewe tu ndiye tunayekuabudu na ni wewe tu ndiye tunayekuomba msaada. Tuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale uliowaneemah, sio ya wale uliowakasirikia, wala waliopotea. Kisha, soma Sura kamili nyingine ya Qur'an tukufu (hapa tumechagua Sura fupi, Sura ya 112, Surat al-Ikhlas). Bismillaahi'r-Rahmaani'r-Rahiim Qul huwallwaahu ahad
Allwaahus swamad
Lam yalid walam yuulad
Wa lam yakullahu kufuwan ahad.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu Sema: Yeye ni Allah mmoja, Allah anayekusudiwa na waja (kwa kumuomba na kumtegemea), Hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana anayefanana naye hata mmoja.
Rukuu :
Baada ya kumaliza kusoma Sura hii ya pili, anayeswali atasema Takbir (Tazama juu) kisha atainama hadi mikono yake aiweke kwenye magoti yake. Atasoma utajo huu dhikr mara moja akiwa amerukuu, atasema: Subhaana rabbiy al-`adhiimi wa bihamdih Utakatifu wote ni wa Mola wangu mkuu, na shukrani zote ni zake. Endelea ukiwa umesimama useme:
Sami`allaahu liman hamidah Mwenyezi Mungu humsikia anayemhimidi Sema Takbir, kisha utasujudu (sujud) Sujud yaani ni mtu kuweka paji lake la uso chini kwa njia maalum kwa nia ya kumnyenyekea Mwenyezi Mungu. Wakati ukifanya sujud, ni wajib viganja vyote vya mikono, magoti na vidole gumba vya miguu vyote viwe viko chini (ardhini). Na dhikr ifuatayo itasomwa mara moja wakati ukiwa umesujudu:
Subhaana rabbiy al-a`laa wa bihamdih Utakatifu ni wa Mola wangu aliye mtukufu na shukrani ni zake.
Na baada ya sijda ya kwanza, utainua paji lako la uso ukae katika hali ya kifundo cha mguu wa kulia kiwe juu ya nyayo ya mguu wa kushoto, huku mikono yako ikiwa juu ya mapaja na useme Takbir, kisha useme (ukipenda):
Astaghfirullaaha rabbii wa atuubu ilayh Namuomba msamaha Mola wangu na natubu kwake.
kisha usome Takbir tena. Utarudia kusujudu tena, kisha utakaa na useme Takbir. Kaa kwa muda, kisha uinuke huku ukisema (ukipenda):
Bihawlillaahi wa quwwatihi aquumu wa aq`ud Nasimama na nakaa kwa uwezo na kwa nguvu za Allah.
Rakaa ya pili Ukishainuka na kunyooka sawasawa, soma Surat al-Fatiha na Sura nyingine ya Qur'an tukufu kama ilivyokuwa katika rakaa ya kwanza. Kisha useme Takbir, na kisha utasoma Qunut.
Qunut :
Inua mikono yako mbele ya uso wako, viganja vyako vielekee juu, huku ukiwa umeishikamanisha mikono yote miwili na vidole pamoja. Na usome dua ifuatayo:
Rabbanaa aatinaa fi'd-dun-yaa hasanatan wa fi'l-aakhirati hasanatan wa qinaa `adhaab an-naar Ee Mola wetu! Tupe mema duniani, na utupe mema Akhera, na utukinge na adhabu ya moto [Qur'an, Sura 2, Aya 201]
[Taz.: Qunut si lazima, ila ukipenda utasoma] Kisha sema Takbir, kisha urukuu, kisha usujudu sijda mbili, kama ilivyoelezwa katika rakaa ya kwanza.
MWISHO