Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MTUME KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

0 Voti 00.0 / 5

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI.

MTUME KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

Washington Irving
(1783-1859 )Anayejulikana kama "The first American man of letters": " "Alikuwa na tabia tulivu na mwenye nidhamu katika chakula, na akifuata sana utratibu wa kufunga. Hakuvama katika kupenda mavazi ya mapambo, namna wanavyojionyesha wenye mawazo finyu; pia kunyenyekea kwake katika mavazi kuliathiri pia kulionyesha matokeo ya kutopenda kwake kujitofautisha... alikuwa muadilifu katika muamala wake wa kibinafsi. Aliamiliana na watu wote kwa usawa: marafiki na wageni, matajiri na maskini, na wenye nguvu na wanyonge; na alipendwa na watu walala hoi kwa kuwa jinsi alivyokuwa akiwapokea kwa vizuri, na kusikiliza matatizo yao... Ushindi wake wa kijeshi vitani haukumfanya awe na ujuba au kibri, kama ambavyo wengine wangefanya hivyo kwa kuathiriwa na ubinafsi. Alipokuwa katika enzi za utawala wake wenye nguvu, aliendelea kujiweka kinyenyekevu kama alivyokuwa katika siku za shida. Alijiweka mbali na heshima kuu ya uongozi na hakuwa akifurahishwa iwapo ataingia mahali na apewe heshima kuu mno."
[Life of Mahomet, London, 1889, Uk. 192-3, 199]

Annie Besant

(1847-1933) Mwingereza na kiongozi India.Pia Rais wa chama cha Indian National Congress mnamo mwaka 1917: " "Haiwezekani kwa atakayesoma maisha na tabia za Mtume mkuu wa Arabia, akajua vipi alifundisha na vipi aliishi, kuhisi chochote ila atahisi utukufu aliokuwa nao mtume huyo mkuu, mmoja kati ya wajumbe wakuu wa Mungu. Japo nitakayokueleza yatakuwa ni mengi yaliyozoeleka kwa watu wengi, lakini mimi binafsi ninapoyarudia kuyasoma nahisi kuyapenda upya na napata kuhisi heshima kubwa juu ya mwalimu huyo mkuu wa Arabia." [The Life And Teachings Of Muhammad, Madras, 1932, Uk. 4]

Edward Gibbon
(1737-1794) Anayechukuliwa kuwa ndiye mwanahistoria mkuu wa enzi zake. " "Alikuwa (Muhammad) na kumbukumbu pana na nzuri, mzaha wake ulikuwa wa kawaida na wa kushirikiana na watu, mwenye mawazo yenye kutia moyo, maamuzi yake yalikuwa ya wazi, ya haraka na ya kukata. Alikuwa na ujasiri wa kufikiri na kutenda." [History of the Decline and Fall of the Roman Empire, London, 1838, Juz. 5, Uk. 335]
Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Mitume (Qur'an 33:40)
Wasio Waislamu wanasema nini juu ya…
Muhammad

MTUME WA UISLAMU

(Rehma na amani zimshukie juu yake na juu ya kizazichake)
Ufuatao ni mkusanyiko wa nukuu fupi fupi kutoka kwenye marejeo mbalimbali ya watu mashuhuri wasiokuwa Waislamu mongoni mwa wasomi, waandishi, wanafalsafa, washairi, wanasiasa na wanaharakati wa kimashariki na kimagharibi. Tuwajuavyo, hakuna hata mmoja kati yao aliyewahi kuwa Muislamu. Kwa hivyo, maneno haya yanaonyesha maoni yao binafsi juu ya mitazamo mbalimbali ya maisha ya Mtume (s.a.w.w.).

Michael H. Hart
(1932- ) Profesa wa Unajimu ( Astronomy), Fizikia na elimu ya Historia anasema:
" "Chaguo langu la kumchagua Muhammad kuongoza katika orodha ya kuwa ni kiongozi wa kwanza mwenye uwezo wa uongozi duniani huenda likawashangaza baadhi ya wasomaji na kudadisiwa na wengine, lakini yeye alikuwa ndiye mtu pekee katika historia aliyefanikiwa sana upande wa kidini na kidunia."
[The 100: A Ranking Of The Most Influential Persons In History, New York, 1978, Uk. 33]

William Montgomery Watt
(1909- ) Profesa (Emeritus)wa lugha ya kiarabu na masomo ya kiislamu, Chuo kikuu cha Edinburgh:
" "Kuwa tayari kwake kuteseka kwa ajili ya imani yake, maadili ya hali ya juu ya watu waliomuamini na kumuona kuwa ni kiongozi, na ukuu wa mafanikio yake katika kufikia malengo yake - yote yanaonyesha uaminifu wake wa kimsingi. Kufikiria kuwa Muhammad ni mzushi, hakutatui matatizo bali huyazidisha. Hata hivyo, hakuna shakhsiya kuu katika Historia iliyopuuzwa nchi za Magharibi kama Muhammad."
[Mohammad At Mecca, Oxford, 1953, Uk. 52]

Alphonse de Lamartine
(1790-1869) Mshairi na kiongozi wa kifaransa:
" "Mwanafalsafa, msemaji, mtume, mwanasheria, shujaa, mshindi wa nadharia, aliyeweka imani ya kimantiki, ya dini isiyo ya kufikirika; mwanzilishi wa himaya ishirini za ulimwengu na moja ya kidini; huyo ni Muhammad. Ana daraja ambazo mwanaadamu yeyote mkuu anatakiwa apimwe kwazo, hata tungeliweza kuuliza, je kuna mwanaadamu aliye mkuu kuliko yeye?" [Imefasiriwa kutoka: Histoire De La Turquie, Paris, 1854, Juz. II, Uk. 276-277]

Reverend Bosworth Smith
(1794-1884) Koleji ya Trinity, Oxford. " "… yeye alikuwa ni Caesar na ni Papa (Pope); lakini alikuwa ni Pope bila ya kuwa na mambo ya Pope, na alikuwa ni Caesar bila ya kuwa na majeshi ya Caesar. Bila ya majeshi yaliyo tayari kwa vita, bila ya mlinzi, bila ya kasri, bila ya kuwa na pato maalum, ikiwa mtu ana haki ya kusema kuwa alitawala kwa haki ya Mungu, basi huyo alikuwa ni Mohammed; kwani yeye alikuwa na nguvu zote bila ya kutumia vifaa vyake na kuungwa mkono."
[Mohammed and Mohammedanism, London, 1874, Uk. 235]

Mohandas Karamchand Gandhi
(1869-1948) Mwanafikra wa India , kiongozi wa nchi:
" "....Nimeridhishwa kwa kukubali kabisa kwamba si upanga ulioupatia ushindi Uislamu katika siku hizo katika utaratibu wa maisha. Ulikuwa ni unyenyekevu mnyoofu, uzuri wa tabia wa Mtume, alivyokuwa akiuchukulia wito wake, kujitolea kwake kwa marafiki na wafuasi wake, ushujaa wake, ujasiri wake, kuamini kwake Mungu na wajibu wake katika kazi yake. Mambo haya, na si upanga, ndiyo yaliyowapatia kila kitu na kushinda kila tatizo."
[Jarida la Young India (periodical), 1928, Toleo X]

Edward Gibbon
(1737-1794) Anachukuliwa kuwa ni mwanahistoria mkuu wa Uingereza wa zama zake:.
" "Mafanikio makuu ya maisha ya Mohammad yalipatikana kutokana na nguvu ya maadili kamili bila ya kutumia upanga." [History Of The Saracen Empire, London, 1870]

John William Draper
(1811-1882) Mwanasayansi wa kimarekani, mwanafalsafa na mwanahistoria:
" "Miaka minne baaada ya kifo cha Justinian, A.D. 569, huko Makka, Arabia, alizaliwa Mohammed ambaye yeye, miongoni mwa watu wote, aliweza kuwaathiri wanaadamu."
[A History of the Intellectual Development of Europe, London, 1875, Juz.1, Uk. 329-330]

David George Hogarth
(1862-1927) Mwingereza mtunzi, na mwangalizi wa Makumbusho ya Ashmolean, Oxford:
" "Iwe ni jambo kubwa au dogo, lakini maadili yake ya kila siku yameunda kanuni inayotekelezwa na mamilioni ya watu kwa dhamira hasa. Hakuna katika wanaadamu anayechukuliwa kuwa ni mtu anayefuatwa kwa karibu zaidi kama yeye. Mwenendo wa mwanzilishi wa ukristo haukuathri maisha ya kawaida ya wafuasi wake. Aidha, hakuna mwanzilishi wa dini aliyekuwa na heshima ya utukufu wa kipekee kama wa Mtume wa kiislamu." [Arabia, Oxford, 1922, Uk. 52]

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini