UHURU WA MAWAZO
BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
UHURU WA MAWAZO
M/Mungu kamkirimu Binadamu, na kamzawadia akili iliyomtofautisha na viumbe wengine, ili awe na nguvu na uwezo wa kuvitawala viumbe wengine na kujenga nchi.Qur-an Al- Israa 70, inasema "Kwa hakika tumemkirimu mwanadamu, na tumempa uwezo wa kuvumbua vitu vya kumbeba baharini na nchi kavu (na anga) na tukamboresha sana juu ya viumbe wengi tuliowaumba." Uislamu unazingatia kutafakari na kutumia akili kwa ajili ya uvumbuzi na ugunduzi ni jambo la faradhi au la wajibu.Qur-an surat Qat 6-8 inasema "Je hawaangalii mbingu ilioko juu yao, na kutafakari namana tulivyoiumba na kuipamba. wala haina nyufa? na ardhi tumeitandika na kuitia humo milima, na tukatesha aina mbalimbali za mimea? hilo ni kwa ajii ya kuona na kukumbuka kwa kila mja mwenye kutubia na kurejea kwa Mola wake."
Uislamu haukubali wafuasi wake kukaa ovyo na kuiga rai na utamaduni wa watu wengine bila utambuzi.Qur-an sruat Al-baqara 166, inasema "Kumbuka siku (kiyama) amabayo viongozi watakapo wasuta wafuasi wao, wataiona adhabu na mahusiano yao yatakatika .Wafuasi watasema tunatamani lau kama tutarudi duniani nasi tukawasuta kama walivyotusuta. Hivyo ndivyo M/Mungu anavyo waonesha matendo yao kuwa ni majuto juu yao, na hawatatoka motoni" Hivyo basi kumuiga na kumfuata mtu kama kipofu katika kila kitu ni majuto siku ya kiyama. Kumuiga mtu katika kila jambo kama kipofu ni ishara ya udhaifu na unyonge, na Mwenyezi Mungu anampenda muumini mwenye nguvu.
Mtume(s.a.w) anasema "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendwa na Allah kuliko muumini dhaifu" Neno nguvu ni common noun, lina maanisha, nguvu katika imani, elimu, uchumi, afya, akili, fikra, hoja, n.k hivyo basi , umma wowote unaoishi kwa kuiga nyumati zingine hufeli na hadhi yake hupotea. Mtume(s.a.w) anasema "Asiwe mmoja wenu ni mwenye kuiga na kufuata watu wengine kama kipofu akisema mimi niko pamoja na watu, wakitenda wema nitakwenda nao na wakitenda ubaya nitakuwa nao, lakini ziwekeni katika umakini nafsi zenu, watu wakitenda wema nanyi tendeni na wakitenda ubaya ninyi epukeni ubaya wao" na maneno ya viongozi wema wa kiislamu waliotangulia kuhusu mtu kujitegemea kimawazo ni mengi sana hapa nitataja baaadhi :
1. Aliy bin A bitwalib R.A. anasema "Kila uchao kuwa ima mwalimu, au mwanafunzi wala usiwe mfuataji kama kipofu." 2. Abdilahi Ibn Masudi R.A. anasema "Mtu na asimuige mtu mwingine, akiamini nae aamini na kama atakufuru nae akufuru, kwani haifai kuiga watu katika ubaya."
3. Imamu Shafii R.A. anasema "Mtu anayepokea elimu bila hoja, ni kama yule mtu anae beba kuni, na kukiwa ndani yake kuna nyoka au nge anamuuma bila ya yeye kutambua" Bali haifai kumuiga mtu bila utambuzi, katika kila kitu, hata kama ni baba au babu n.k Quran suratil baqara 170 inasema "Na wanapoambiwa fuateni yale yaliyoteremshwa na Allah, wao husema, bali tutafuata yale tuliowakutanayo wazee wetu, je watafuata wazee wao hata kama hawakuwa na elimu wala uongofu?" hivyo basi ni katika uchache wa uelewa humuiga mtu mwingine bila ya ufafanunuzi na kuwa kama kivuli chake.
YAALLAH TWAKUOMBA UTUPE MAARIFA , NA UTUGHUFIRIE DHAMBI ZETU
MWISHO