Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Mwanamke

Biblia Imetaja Hijaab

Biblia Imetaja Hijaab

BIBLIA IMETAJA HIJABU SWALI: Mimi ni mkristo, niliwahi kuambiwa kuwa kwenye biblia kuna aya zinazoonyesha kuwa ukristo unafundisha kuwa wanawake wavae hijabu. Na kuwa wanaume wavae kanzu na vilemba (hayo ndiyo mavazi matakatifu). Na kuwa Yesu alitawadha km waislam wanavyofanya. NAOMBA MNIPE MNISAIDIE MAANDIKO HAYO. JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Tunashukuru ndugu yetu katika utu na ubinadamu kwa swali lako hilo. Tunatumai kuwa katika majibu yetu utapata ukweli wa mambo na Dini ili kwa akili uliyopewa na Mungu uweze kujua ya haki na tunamuomba Mwenyezi Mungu Akupe moyo wa kuweza kuufuata ukweli. Hakika ni kuwa Mwenyezi Mungu Alituma Mitume na Manabii ili wawaelimishe na kuwafahamisha wanadamu kuwa njia ya kumjua na kumtambua Mwenyezi Mungu ni kufuata muongozo waliokuja nao. Mwenyezi Mungu Aliteremsha kitabu cha mwisho, Qur-aan ili kiwe ni uongofu kwa wanadamu wote. Mwenyezi Mungu Anasema: "Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi" (2: 185). "Hiki ni kitabu ambacho hakina shaka ndani yake ni uongofu kwa wamchao Mwenyezi Mungu" (2: 2). Wanadamu kwa kupita zama waliweza kubadilisha andiko ili wafuate matamanio ya nafsi zao. Jambo hili limebaki kuwa wazi hata katika mkusanyiko wa vitabu vilivyoteremshiwa Manabii wengine. Kubadilishwa huku kwa andiko kumewekwa wazi na Yeremia pale aliposema: "Mnawezaje kusema: 'Sisi tuna hekima, sisi tunayo sheria ya Mwenyezi Mungu,' hali waandishi wa sheria, wameipotosha sheria yangu" (Yeremia 8: . Katika nakala nyengine za Biblia zinasema: "Mwawezaje kusema kuwa sisi tuna akili kwa kuwa tuna Taurati ya Bwana ilhali kalamu za waandishi zimeifanya kuwa uongo". Hakika ni kuwa katika ile mistari iliyobakia utapata mambo mengi ambayo yanafanywa na Waislamu ilhali Wakristo wenyewe wameyawacha kabisa. Kati ya hayo ni kuwaita watu kwa ajili ya kuja kwa Ibada. Tazama Hesabu 10: 1-3, ambapo Mose anaagiziwa kufanya tarumbeta za fedha ili kuwaita watu wakati wa kuvunja kambi. Njia hii ya kuita watu haitumiki tena kwa tarumbeta bali sauti ya mtu ambaye anawaita watu kwa ajili ya Swalah (ibada), ambaye anaitwa muadhini.

Ufafanuzi

NAFASI YA UANAADAMU WA MWANAMKE

NAFASI YA UANAADAMU WA MWANAMKE UTANGULIZI Kwa jina la Muumba Mkamilifu ninaishika kalamu kwa dhamira ya kuielezea nafasi ya uwanaadamu wa mwanamke. Katika kurasa za makal hii, nitajaribu kuzifafanua baadhi ya fikra zinazoungalia Uislamu kuwa ni dini inayowakandamiza wanawake. Tuhuma mabali mbali ambazo kwa mara nyingi huwa ni zenye kuelekezwa katika dini mbali mbali, zinaweza kuwa ni zenye kusema kweli, na mara nyengine zikawa ni zenye kulenga malengo ya kuleta uadui fulani. Lakini watu wenye akili huwa hawayachukulii madai hayo kuwa ni madai ya uwongo, bali huyachukulia kuwa ni kama changamoto ya kuwatumbukiza wao katika uwanja wa utafiti kuhusiana na masuala hayo. Nami nimeamua kuwaiga wenye akili katika kulipekuwa suala la Uwanaadamu wa mwanamke, ili kuweza kuthisha au kukanusha tuhuma za unyanyasaji wa wanawake unaodaiwa kuwepo ndani ya dini ya Kiislamu. Kuwepo kwa unyanyasaji wa wanawake katika jamii mbali mbali, huwa kunategemea hali ya utamaduni wa jamii hizo ulivyo muweka mwanamke, hivyo basi unyanyasaji wa wanawake hauwezi tu kuegemezwa katika jamii za Kiisalmu, bali unaweza kuegemezwa juu ya migogo ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu, kwa kutokana na tamaduni na fikra zao zilivyo. Kutovutia upande mmoja katika suala la utafiti huu, kunaweza kumvutia kila mtu apendaye ukweli na mwenye busara. Ninamtaraji Mola aniongoze katika utafiti huu, ili nisije kuwatetea Waislamu kwa Uslamu wao, au Wakristo kwa Ukristo wao. Kwani kufanya hivyo kutaitoa thamani makala hii, na hakutompa msomaji shauku ya kuendelea na usomaji wake. Ninatarajia malengo yangu yatafanikiwa kwa uwezo wa Muumba Mkamilifu.

Ufafanuzi

DHULMA KWA UISLAMU NA WAISLAMU

DHULMA KWA UISLAMU NA WAISLAMU UTANGULIZI Nina mshukuru Muumba Mkamilifu kwa kunipa nguvu za kuweza kuleta picha maalumu iwezayo kutoa ufafanuzi juu ya dhulma mbali mbali zinazofanyika katika ulimwengu huu, na nina mshukuru tena kwa mara ya pili kwa kutuletea Mjumbe wake (s.a.w.w) aliyeweza kuingarisha dunia hii kwa nuru ya elimu itokayo kwa Muumba wake. Katika makala hii nitajaribu kuizungumzia hali halisi ya matokeo yanayotokea katika dunia hii, huku wengi wakidhania kuwa ni matokeo ya kawaida tu. Na wengi wetu huwa tunayaangalia matokeo mbali mbali ya ulimwengu huu kuwa ni yenye kutiririka kwa kupitia sindikizo lake wenyewe, na si wengi wanao zitafuta sababu matokeo haya. Nia hasa ya kuandika makala hii, ilikuwa ni kumzungumzia mwanamke mashuhuri wa Kiislamu aliye uliwa huko Ujerumani kwa sababu ya kuvaa hijabu. Lakini niliona kuwa kuna umuhimu kwanza kutoa ufafanuzi maalumu, juu ya mambo mbali mbali yanayotokea katika ulimwengu wetu huu. Ulimwengu leo umeyafikia mapevuko ya ufisadi wa aina mbali mbali, huku kila mmoja akidhania kuwa yeye ni mwenye kuujenga ulimwengu kwa matendo yake. Hakuna mtu katika ulumwengu huu anaye kubali kuwa yeye ni muovo, na kila mmoja hujitetea kwa kutumia njia tofauti ili aonekana kuwa yeye ni mjenga nchi.

Ufafanuzi

YVONE NA HIJABU

YVONE NA HIJABU Nilivyokuja Kuipenda Hijaab Nilikuwa nikiwaona wanawake wanaojisitiri ni kama, viumbe waliodhulumiwa - mpaka nilivyokamatwa na Taliban. Katika mwezi wa tisa mwaka wa 2001, masiku 15 baada ya mashambulizi ya kigaidi katika nchi ya Marekani, Nilikamatwa ndani ya Afghanistan, nikafunikwa kutoka kichwa hadi vidole vya miguu kwa burqa ya rangi ya samawati, nikiwa nimedhamiria kuandika gazeti kuhusu maisha chini ya uonevu wa mfumo wa utawala. Badala yake, niligunduliwa, na kukamatwa na kufungwa siku kumi. Niliwatemea mate na kuwatukana walionikamata; waliniita mwanamke "mbaya" lakini waliniachilia baada ya kutoa ahadi kuwa kuisoma Quran na kujifunza Uislamu. [kwa kweli, sina uhakika nani aliyekuwa mwenye furaha zaidi wakati nilipoachiliwa huru; wao ama mimi.] Niliporejea nyumbani London, niliweka nadhiri yangu ya kujifunza Uislam na nilistaajabu kwa yale niliyoyavumbua. Nilikuwa natarajia kuona kutoka katika surah za Quran kuwa vipi kumpiga mke wako na kuwadhulumu watoto wako; badala yake, nilikuta dondoo za uimarishaji wa ukombozi wa wanawake.

Ufafanuzi

QUR-AN INASISITIZA KUVAA HIJABU

QUR-AN INASISITIZA KUVAA HIJABU QUR-AN INASISITIZA KUVAA HIJABU. Katika Qur'an kumetaja kwamba, Qur'an inahimiza sana sana kuvaa Hijabu, na katika Aya nyingi za Qur-an umetajwa mkazo wa jambo hili, nasi tutataja baadaye baadhi ya Aya nyingi zinazohusu suala hili na kuzifasiri kwa kifupi. 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema; "Ewe Nabii, waambie wake zako na binti zako na wake wa waaminio, wateremshe shungi zao. Kufanya hivyo kutapelekea wao kutambulikana ( kwamba ni wanawake waungwana) hawatakerwa ( na watu waovu), na Allah ni Mwingi wa kusamehe (tena) Mwenye huruma".5 Katika Aya hii tukufu, Mwenyezi Mungu anamuamuru Nabii wake Muhammad (s.a.w), awaamrishe wanawake wa ki-Islamu waki-wemo wakeze, binti zake na wake wa waaminio, wajisitiri kwa kuvaa Hijabu iliyokamilika. Katika zama za mwanzo wa kuja Uislamu wanawake walikuwa wakitoka majumbani mwao bila kujisitiri miili yao kikamilifu, kama vile walivyokuwa wakitoka wanawake wa zama za Jahiliya ( kabla kuja Uislamu). Hali ya kutokujisitiri kikamilifu kwa wanawake, haikuridhiwa na sheria ya ki-Islamu, ndipo Mwenyezi Mungu alipomuamuru Mtume wake Muhammad (s.a.w.w) awaambie wanawake waumini wajisitiri na wavae Hijabu, na awakataze kutoka majumbani mwao bila sitara iliyokamilika kisheria. Akasema Allah s.w.t kumwambia Mtume (s.a.w.w), "Ewe Nabii waambie wake zako na binti zako na wake wa waaminio wateremshe shungi zao." Tamko (Jalabib) ambalo limetumika kwenye Aya ya hamsini na tisa, maana yake kilugha ni ushungi ambao hufunika kichwa cha mwanamke na uso wake na kumkinga asionekane kwa watu kwani kwa mujibu wa Q. 33:59 sheria haifai kuonesha mbele yao baadhi ya sehemu za mwili wake. Bali ilivyo ndivyo, ni mwanamke asitiri sawa maungo yake kama sheria inavyomtaka kuyasitiri.

Ufafanuzi

MKE ZAIDI YA MMOJA

MKE ZAIDI YA MMOJA MKE ZAIDI YA MMOJA Kwa hakika tunakubaliana kiakili kwamba kila aliyekitengeneza kitu basi atakuwa na uwezo na maarifa ya kukiendesha na kutoa miongozo yake katika kitu hicho. Sasa kama sisi ni binaadamu tena waislamu lazima tukubali na tuyakinishe kwamba huu ulimwengu umeumbwa, kwa hivyo aliye bora wa kutoa miongozo juu yetu ni Allah (S.W). Allah (S.W) amemuumba mwana-adamu na anamjua fika udhaifu wake, uwezo wake na matamanio yake. Kwa ajili hiyo hakumuacha ovyo kama mnyama akamuwekea utaratibu wa kufuata na kutatua matatizo yake na jinsi ya kumaliza matamanio yake.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini