Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UDUG WA UISLAMU

0 Voti 00.0 / 5


BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

UDUG WA UISLAMU

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesema katika ufunguzi wa kikao cha 23 cha kimataifa cha Wiki ya Umoja wa Kiislamu mjini Tehran, kwamba lengo kuu la kufanyika kikao hicho ni kuleta na kuimarisha udugu katika umma wa Kiislamu.

Akizungumza katika kikao cha ufunguzi cha mkutano huo wa kimataifa, Ayatullah Ali Taskhiri ametoa salamu za pongeza kwa washiriki wa kikao na Waislamu wote ulimwenguni kwa mnasaba huu adhuimu wa kuadhimisha kuzaliwa Mtukufu Mtume (SAW) na Imam Swadiq (AS) na kusema kwamba kufanyika vikao vya kieneo na kimataifa na hasa hiki cha Umoja wa Kiislamu ni miongoni mwa majukumu na malengo muhimu zaidi ya Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu.

Amesema vikao hivyo vinafanyika kwa lengo la kueneza utamaduni wa udugu wa Kiislamu miongoni mwa jamii za Kiislamu. Ayatullah Taskhiri amesisitiza kwamba, tokea wakati wa kuasisiwa taasisi hiyo hadi leo, asasi hiyo muhimu ya Kiislamu imeshughulikia masuala mengi ya kuimarisha utafiti na utamaduni na vilevile matatizo na changamoto mbalimbali zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu. Amesema, juhudi za kutatua matatizo hayo ambayo kimsingi yanatokana na tofauti pamoja na hitilafu za kimadhehebu zinafanyika kwa ushirikiano wa wasomi na wanafikra wa Kiislamu na kwamba tayari njia za kuyatatua kwa msingi wa vitabu za wafuasi wa madhehebu za Kisunni zimepatikana.

Ayatullah Taskhiri amebainisha shughuli mbalimbali za kukurubisha pamoja Waislamu zinazofanywa na Taasisi ya Kukurubisha pamoja Madhebeu ya Kiislamu na kuongeza kuwa, kuandaliwa mamia ya vikao vya kuleta umoja na udugu miongoni mwa Waislamu, kutuma jumbe mbalimbali za wasomi na wanafikra wa Kiislamu nje ya nchi, kuzinduliwa taasisi ya utafiti katika mji mtakatifu wa Qum, kufanya tafiti mbalimbali, kuchapisha mamia ya vitabu kwa lugha tofauti hai za dunia, kuandaa vipindi mbalimbali vya televisheni, kuanzisha Chuo Kikuu cha Madhehebu ya Kiislamu, kuzinduliwa shirika la habari la Taasisi ya Kukurubisha pamoja Mahdhebu ya Kiislamu, kuanzishwa kwa mtandao wa Taasisi ambao hivi sasa unatekeleza shughuli zake kwa lugha 12 za dunia kwa lengo la kukidhi mahitaji ya kiutamaduni ya Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia ni miongoni mwa majukumu muhimu ambayo yanatekelezwa na taasisi hiyo ya kimataifa.

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimaaifa ya Kukurubisha Pamoja Madhebeu ya Kiislamu ameongeza kuwa shughuli za taasisi hiyo zimekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha umoja na kuzibainishia nchi za dunia umuhimu wake. Amesema kuwa moja ya malengo muhimu ya vikao vya Umoja wa Kiislamu ni kuondoa tofauti na hitilafu nyingine ambazo zimejitokeza katika ulimwengu wa Kiislamu katika kipindi chote cha historia kutokana na hitilafu za kimadhehebu na kimakundi.

 

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini