MTIZAMO WA MTUME (S.A.W.W) JUU YA SUALA LA UONGOZI
MTIZAMO WA MTUME (S.A.W.W) JUU YA SUALA LA UONGOZI
Suala hili linatakiwa kuangaliwa kwa makini kiakili, kwani iwapo tutaliangalia suala hili kimadhehebu tunaweza kupotea njia kayika kusimamisha dalili juu ya suala hili, basi iwapo mtu wa madhehebu ya Kishia ua ya Kisunni atajivua umadhehebu wake na kuliangalia suala hili akiwa nje ya dhehebu lake, na badala yake awe ni mwenye kutumia hoja zilizoegemea kwenye akili safi, hapo ndipo atapoweza kua ni hakimu mzuri katika suala hili.
Tukiliangalia kwa ufupi juu ya mtizamo wa Mtume (s.aw.w) katika suala la uongozi, tutaona kua suala hili alilipa uzito mkubwa kabisa na hakua ni mwenye kulipuzia suala hili na kuwaachia watu wafanye watakavyo wao katika kuteua anayefaa kua kiongozi wao, sfikirii kua inayumkini kuwepo mmoja miongoni mwetu anayeweza kusafiri na kuicha nyumba na familia yake bila ya kufikiria kua ni nani anyeweza kumteua ili azishike zile nyadhifa muhimu za familia yake. Na iwapo atakuwepo mtu wa aina hiyo, basi mtu huyo hatothaminiwa na jamii yake, basi vipi Mjumbe wa Alla leo tunasema kua ameuacha umma huu bila la kumteuwa kiongozi atakayeshika nafasi yake baada kuondoka kwake?
Leo kila mwenye Dhehebu lake anaamua kulitetea Dhehebu lake bila ya kufahamu kua dini si kuyashangiria yale yaliomo ndani ya Dehebu fulani bali dini kuyafuata yale alio yakweli.
Wengine wanadai kua Mtume amemchagua Abuu Bakar kua ndio kiongozi baada ya Mtume (s.a.w.w), na wengine wanadai kua Mtume (s.a.w.w) hakumchagua mtu kua kiongozi baada yake, bali aliwaacha watu wajichagulie wenyewe kiongozi wao! Basi ukweli ni upi kwenye msokotano huu? Basi anza kuutafuta ukweli na kuupima kwa akili yako huku ukizisikiliza hoja za pande zote mbili ili uweze kutoa hukumu isio na dosari, kwani hii ndiyo njia pekee ilio na usalama katika dini yako pamoja na dunia yako.
MWISHO