DUA YA IMAM ZAYNUL ABIDIN
BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM DUA YA IMAM ZAYNUL ABIDIN (a.s.) KATIKA KUOMBA TAWBA
Ewe Mola wangu, ambaye sifa za kukusifu za wenye kukusifu haziwezi kutajika. Ewe mwenye mategemeo ambaye mategemeo hayawezi kwenda zaidi yako.Ewe ambaye kwako wewe malipo ya waja wako hayatapotea. Ewe unayeogopwa na waja wako. Ewe uliye khofu ya mja wako na hii ndiyo nafasi imemkuba ghafla kwa madhambi.
Ambaye amevutwa na zama za makosa na ambayo yameghalibiwa na sheitani. Kwa hivyo ameshindwa kabisa kutimiza yale uliyokuwa umemwamrisha kuyafanya na yeye hakuyafanya. Yeye amegang'ania tu katika yale uliyokuwa umeyaharamisha na kuyakataza kama kwamba haelewi uwezo ulionao juu yake. Au kama yule anayekanusha ukarimu wako mtukufu kwake yeye hadi macho ya hidaya kufunguliwa kwa ajili yake na mawingu (kiza) cha upofu (wa hidaya) ulipoondolewa kutoka kwake, na alipotambua kwa ukamilifu vile alivyojidhulumu nafsi yake na kuyazingatia kuwa amemwasi Muumba wake.
Kwa hivyo ameyaona maovu yake kwa mapana vile yalivyokuwa, akaona ukubwa na uasi na upinzani wake ulivyo kupita kiasi, kwa hivyo amekurejea wewe kwa kutaraji msaada wako kwa kuona aibu mbele yako, akielekea kwako wewe kwa hali halisi kutokana na woga wake, shauku yake ya kutaka kuondolewa kila kitu na hofu zake, ila ni wewe tu ndiye mwenye uwezo wa kuyadonoa hivyo. Hivyo amesimama mbele yako, akiomba.
Macho yake yakiwa yanatazama chini ardhini kwa utiifu, na kichwa chake chini kwa unyenyekevu wa Ukuu wako. Katika hali ya kudhalilika ya nafsi anaungama kwako kwa siri zake zote ambazo wewe wazijua zaidi kuliko mimi mwenyewe na katika aibu amezihisabu madhambi yake ambayo wewe umeishakwisha kumhesabia.
(Yeye anakuomba wewe kumwokoa kwa kumtoa kutoka madhambi makubwa ambayo ameingia humo wakati wewe unajua na ambavyo imemwaibisha kabisa katika heshima yako ya maamrisho yasiyotimizwa naye, starehe ambazo madhambi yamemgeukia na kumhukumia adhabu ambayo itakayokuwa daima juu yake. Yeye kamwe hakanushi uadilifu wako, Ewe Mola wangu! Iwapo wewe utamwadhibu.
Yeye anasadiki kuwa usamehevu kwako wewe ni jambo dogo. Iwap utamsamehe na kumhurumia yeye kwani wewe ni Bwana wa Hisani, ambaye hadhanii kuwa ni vigumu kwako wewe kumsamehe madhambi hata yakiwa makubwa kiasi gani. Ewe Mola wangu! Kwa hivyo shuhudia! Mimi nipo hapa.
Nimekuijia wewe katika Ibada (kuomba), katika hali ya utiifu wa amri zako, nikitaraji utimizo wa Ahadi yako, ambamo wewe umeahidi kujibu. Kwani wewe umesema "Niombeni, nitakuitikieni" (40:26). Ewe Mola wangu! Mbarikie Mtume Muhammad s.a.w.w. na Ahli Bayt yake toharifu. Naomba unijaalie msamaha wako kama vile nilivyokuijia kwa kuungama na kukiri. Naomba uniondoe kutoka vikwazo vya madhambi kwani nimeiwasilisha nafsi yangu mbele yako. Naomba unisitiri kwa usitiri wako kama vile ulivyoweza kuuchelewesha matimizo ya kisasi chako juu yangu. Ewe Mola wangu! Naomba unithibitishie maazimio yangu ya kukutii wewe! Unijaalie nguvu za fahamu zangu katika kukuabudu wewe.
Nijaalie rehema ya matendo ambayo yataweza kuosha na kutoa maambukizo ya makosa niliyo nayo mimi. Naombanife katika Dini yako na katika Ummah wa Mtume Muhammad s.a.w.w. Ewe Mola wangu! Mimi nafanya Tawba mbele yako katika hali hii ya madhambi yangu yaliyo makubwa mno. Na yaliyo madogo.
Ya makosa yangu yaliyo dhahiri na yaliyofichika na yaliyotangulia kutendwa na ambazo zimetendwa hivi karibuni kwa Tawba ambayo yeye hata hawezi kuisimulia nafsi yake, kwa kutotii, na wala hawezi kudhamiria kurudia maasi. Ewe Mola wangu! Kwa hakika wewe umesema katka kitabu chako (i.e. Quran) KItukufu kuwa unazikubali Tawba za waja wako, na unasamehe madhambi na unawapenda wale wafanyao Tawba (Qurani, 1:222), naomba ukubalie Tawba yangu kama vile wewe ulivyoahidi. Nisamehe madhambi yangu kama vile ulivyodhamini. Nijaalie mapenzi yako kama vile ulivyokubali. Ewe Mola wangu! Nakutolea ahadi yangu kuwa kamwe sitarudia katika kila kile ukichukiacho; na ni dhamana yangu kuwa kamwe sitarejea katika yale usiyoyataka; na ni maahadiano yangu kuwa nitayaacha matendo yote yale yenye kukuasi wewe.
Ewe Mola wangu! Kwa hakika wewe watambua na kujua vyema kabisa kila nilichokitenda. Kwa hivyo, naomba unisamehe yale unayoyajua. Kwa uwezo wako unirejeshe kwa kile ukipendacho mno. Ewe Mola wangu! Mimi nipo chini ya ushurutisho nisioukumbuka na baadhi ambayo nimeshakwisha sahau, lakini vyote hivyo vipo wazi mbele ya macho yako ambayo kamwe hayawezi kulala na mbele ya Ilm yako ambayo kamwe haisahau. Kwa hivyo naomba ufidie yanayostahiki kutoka kwangu. Ondoa mzigo wa yale (faradhi) juu yangu. Yafanye wepesi uzito wao kwa ajili yangu. Nihifadhi kwa kutorejelea tena karibu na hayo.
Ewe Mola wangu! Kwa hakika mimi siwezi kuwa mwanifu katika Tawba yangu isipokuwa msaada wako wa kunihifadhi. Wala siwezi kujizuia na madhambi isipokuwa kwa uwezo wako. Kwa hivyo, naomba uniimarishe mimi kwa nguvu ya kutosha na naomba unilinde kwa uhifadhi wako unaotakiwa. Ewe Mola wangu! Kiumbe chochote kile kinapofanya Tawba yako na ambaye, katika ukimu yako iliyofichika, ni lazima atakiuka viapo vyake vya Tawba na atarejea katika madhambi na maovu yake, kwa hivyo nahitaji hifadhi yako dhidi ya kutokea kwa hayo. Hivyo, ifanye Tawba yangu iwe ni majuto ambavyo stakuwa na haja ya kutubu tena - Tawba ambayo tafuta yale niliyokuwa nimeyatenda na usalama kwa yale yaliyosalia.
Ewe Mola wangu! Najitetea (kutaka radhi yako) mbele yako kwa ujahili wangu. Naomba msamaha wako kwa matendo yangu maovu. Kwa hivyo, naomba uniingize katika hifadhi zako. Nifunike kwa funiko zako za usalama na hisani zako. Natubia kwako kwa kila kitu ambacho kinapingana na Amri yako au ambacho kimepoteza mapenzi yako kwa kutokana na mafikirio ya moyo wangu, maono ya macho yangu na matamshi ya ulimi wangu kwa Tawba ambavyo kila kiungo cha mwili wangu kisalimike kutokana na adhabu zako na kuponea kwa khofu ya maumivu ya ghadhabu zako kwa mwenye kuasi. Kwa hivyo, nihurumie, Ewe Mola wangu, kwa unyenyekevu wangu mbele yako.
Juu ya roho yangu ambayo inadunda midundo ya kishindo kwa sababu ya khofu yako na Juu ya maungo ya mwili wangu ambayo yanatetemeka kwa hofu yako, kwa hakika, Ewe Mwenye kutunuku riziqi, madhambi yangu yameniweka mbele yako katika hali ya kudhalilika, ili kwamba nitakapobakia kimya, basi hakuna mwingine atakaye sema badala yangu. Iwapo nitajiombea uteteo, kwani mimi ni mtu nisiyestahiki hivyo.
Ewe Mola wangu! Bariki Mtume Muhammad s.a.w.w.na ahali Bayt yake a.s., rehema zako zinitetee maovu yangu. Yageuze maovu yangu kwa msamaha wako. Usinilipe adhabu yako kwa yale maovu yangu. Unitandazie juu yangu kwa uarimu wako. Nifunike kwa pazia yako. Unitendee yale ambayo bwana mwema amfanyiavyo mambo ya huruma kwa mtumwa wake asiye na uthamini, ambaye anaomba huruma yake au mtu tajiri anapomsaidia mbele yake kiumbe chenye mahitajio. Ewe Mola wangu! Hapana mwingine wa kunsitiri isipokuwa wewe tu, kwa hivyo Utukufu wako lazima unihifadhi. Hapana mwingine yeyote wa kunitetea kwako wewe. Kwa hivyo, huruma yako lazima inisuhulishie mimi. Kwa hakika makosa yangu yameniogopesha kupita kiasi, hivyo msamaha wako lazima yameniogopesha kupita kiasi, hivyo msamaha wako lazima unihakikishie hivyo.
Kwa chochote kile nilchokwisha kukisema si kutokana na ujahili wa matendo yangu maovu, wala si kwa usahilifu wa kile kilichotangulia, cha tabia zangu zinazolaumiwa bali yasikilizwe na mbingu zako, na yale yaliyomo na ardhi yako na yale yaliyo juu yake, yanisikilize yale nilyokuambia wewe katika hali ya majuto na masikitiko na kwa Tawba ambayo naombea usitiri, nikitegemea labda baadhi yako, kwa kupitia rehema zako, zinihurumie, kwa kutokana na hali yangu isiyo nzuri au udhaifu ule kwa ajili yangu labda naweza kupata dua yake inayostahili kukubaliwa kuliko maombi yangu au mateteo yaliyo na nguvu kuliko nijiteteavyo mimi na ambavyo inawekekana ikawa ni sababu ya kuokoka kwangu kutokana na ghadhabu zako na mafanikio ya ushindi wa idhini yako.
Ewe Mola wangu! Iwapo majuto na masikitiko yanatosheleza kwa Tawba mbele yako, basi mimi ni mjutaji sana baina ya wale wanaojuta na kusikitika. Iwap kuacha kutokutii wewe ni uongofu basi ni mwachaji mkubwa miongoni mwao. Iwapo kukuomba msamaha kunaondoa madhambi, basi mimi ni miongoni mwa wale wanaokuomba msamaha wako! Ewe Mola wangu! Kama vile Tawba, umedhamiria kuzikubalia, umetutia moyo wa kusali na umetuahidi kujibu; hivyo wabariki Mtume Muhammad s.a.w.w. na kizazi chake a.s.
Nikubalie Tawba yangu. Usinirejeshe nyuma kwa kutopatiwa niliyoyaazimia kutoka rehema zako. Kwa hakika wewe ni Mkuu wa mkubaliaji wa Tawba za wenye madhambi na mhurumiaji kwa wenye kupotoka ambao wanarejea kwako. Ewe Mola! Wabariki Mtume Muhammad s.a.w.w. na kizazi chake toharifu a.s. kama vile ulivyotuamrisha sisi. Wabariki Muhammad s.a.w.w. na kizazi chake a.s. kwa baraka ambazo zitatutetea kwako siku "ya kufufuliwa na siku ya Mahitajio." Kwa hakika wewe tu ndiye ulie na uwezo juu ya kila kitu na kila kitu ni saheli kwako wewe."
MWISHO