Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

utafiti mbali mbali

KUWEKA MKONO WA KULIA JUU YA MOKONO WA KUSHOTO

KUWEKA MKONO WA KULIA JUU YA MOKONO WA KUSHOTO

KUWEKA MKONO WA KULIA JUU YA MKONO WA KUSHOTO NI BID'A ALIYOIANZISHA OMAR BIN KHATABI KWA KUWAIGA MAJUSI (WAABUDU MOTO) ۱ .  إنّ وضع إحدى اليدين على الأخرى حالة صلاة سنّة عند أكثر الجمهور إلّا مالك ؛ فقد قال في المغني لابن قدامة / ٥۱٤ : « ظاهر مذهبه الذي عليه أصحابه : إرسال اليدين وروي ذلك عن ابن الزبير والحسن  ». Hakika kuweka mmoja ya mikono juu ya mwingine wakati wa Swala imekuwa ni kama Sunnah kwa Ahlisuna isipokuwa Ma Maalik. Ibn Quddamah ameyasema hayo katika kitabu kiitwacho Al Mughniy UK 514, na madheheb ya wafuasi wake yanaitwa Adhwahiri, Dhwahiri wenyewe hunyoosha mikono kufuata mapaja wakati wa ku Swali na wamepokea hayo kutoka kwa Ibn Zubayr na Hassani.

Ufafanuzi

NI NANI AHLULBAYT (A.S) 3

NI NANI AHLULBAYT (A.S) 3 HLUBAITI RASUL AS, KILUGHA NI KUNDI KUBWA SANA LAKINI KISHERIA NI WATU MAALUM WASIOZIDI 14 AMBAO MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE SAWW WAMETIA MKAZO WA KUWATII NA KUFUATA, KWENDA KINYUME NA WAO NI KUMUASI MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE SAWW. WANAZUONI WAKUBWA WA AHLISUNA NA SHI'AH WANA MAKUBALIANO YA PAMOJA KATIKA KUWATAMBULISHA HAO AHLUBAITI RASUL AS KATIKA VITABU VYAO VYA HADITHI, TAFSIRI NA HISTORY Sunnah na Nyumba ya Mtume saww, Ahlul Bayt. Ni nani wanaunda Nyumba ya Mtume saww Ahlul Bayt? Swali jingine linahusu ile maana ya "Nyumba ya Mtume saww" katika hadithi nyingi zinazotuagiza kushikamana na Nyumba ya Mtume saww, wao wanarejelewa kwa jina la Ahlul Bayt au al Itrah. Maneno haya yanatumika juu ya nini na ni watu gani wamezungukwa na nafasi hiyo ya watu wa Nyumba ya Mtume saww? Je, inajumuisha yeyote na ndugu wote wa Mtukufu Mtume Saww?

Ufafanuzi

NI NANI AHLULBAYT (A.S) 2

NI NANI AHLULBAYT (A.S) 2 HLUBAITI RASUL AS, KILUGHA NI KUNDI KUBWA SANA LAKINI KISHERIA NI WATU MAALUM WASIOZIDI 14 AMBAO MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE SAWW WAMETIA MKAZO WA KUWATII NA KUFUATA, KWENDA KINYUME NA WAO NI KUMUASI MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE SAWW. WANAZUONI WAKUBWA WA AHLISUNA NA SHI'AH WANA MAKUBALIANO YA PAMOJA KATIKA KUWATAMBULISHA HAO AHLUBAITI RASUL AS KATIKA VITABU VYAO VYA HADITHI, TAFSIRI NA HISTORY Sunnah na Nyumba ya Mtume saww, Ahlul Bayt. Ni nani wanaunda Nyumba ya Mtume saww Ahlul Bayt? Swali jingine linahusu ile maana ya "Nyumba ya Mtume saww" katika hadithi nyingi zinazotuagiza kushikamana na Nyumba ya Mtume saww, wao wanarejelewa kwa jina la Ahlul Bayt au al Itrah. Maneno haya yanatumika juu ya nini na ni watu gani wamezungukwa na nafasi hiyo ya watu wa Nyumba ya Mtume saww? Je, inajumuisha yeyote na ndugu wote wa Mtukufu Mtume Saww?

Ufafanuzi

NI NANI AHLULBAYT (A.S) 1

NI NANI AHLULBAYT (A.S) 1 HLUBAITI RASUL AS, KILUGHA NI KUNDI KUBWA SANA LAKINI KISHERIA NI WATU MAALUM WASIOZIDI 14 AMBAO MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE SAWW WAMETIA MKAZO WA KUWATII NA KUFUATA, KWENDA KINYUME NA WAO NI KUMUASI MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE SAWW. WANAZUONI WAKUBWA WA AHLISUNA NA SHI'AH WANA MAKUBALIANO YA PAMOJA KATIKA KUWATAMBULISHA HAO AHLUBAITI RASUL AS KATIKA VITABU VYAO VYA HADITHI, TAFSIRI NA HISTORY Sunnah na Nyumba ya Mtume saww, Ahlul Bayt. Ni nani wanaunda Nyumba ya Mtume saww Ahlul Bayt? Swali jingine linahusu ile maana ya "Nyumba ya Mtume saww" katika hadithi nyingi zinazotuagiza kushikamana na Nyumba ya Mtume saww, wao wanarejelewa kwa jina la Ahlul Bayt au al Itrah. Maneno haya yanatumika juu ya nini na ni watu gani wamezungukwa na nafasi hiyo ya watu wa Nyumba ya Mtume saww? Je, inajumuisha yeyote na ndugu wote wa Mtukufu Mtume Saww?

Ufafanuzi

KILICHOTOKEA GHADIIR KHUM

KILICHOTOKEA GHADIIR KHUM KILICHOTOKEA GHADIIR KHUM Assalam Alaikum Jee, kulitokea nini Siku ya Ghadir Khum? Ghadir Khum ni sehemu iliyoko maili kadhaa kutoka Makka katika njia inayoelekea Madina. Wakati Mtume (s.a.w) alipopita sehemu hiyo tarehe 18 Dhul'Hijja (10 March 632) wakati anarudi kutoka Hijja yake ya mwago, aya, "Ewe Mtume fikisha uliyoteremshiwa…." Iliteremshwa, kwa hiyo alisimama ili kutangaza kwa mahujaji ambao alifuatana nao kutoka Makka na ambao walikuwa watawanyike njia panda hapo kila mtu kuelekea sehemu yake. Kwa amri ya Mtume (s.a.w) mimbari maalum ilitengenezwa kwa kutumia matandiko ya ngamia kwa ajili yake. Baada ya Salat ya mchana Mtume .(s.a.w) alipanda mimbari na akatoa Khutuba yake ya mwisho mbele ya mkusanyiko mkubwa kabla ya kifo chake miezi mitatu baadae. Sehemu ya kuvutia ya Khutuba yake, ni pake alipomchukuwa 'Ali (a.s) kwa mkono wake, Mtume s.a.w. aliwauliza wafuasi wake iwapo yeye ana mamlaka zaidi (awla) kwa waumini kuliko wao wenyewe. Kundi kubwa lile la watu likaitikia kwa sauti kubwa "Hivyo ndivyo ilivyo , Ewe Mtume wa Allah". Kisha akatangaza: "Yule ambaye kwamba mimi ni (mawla) mwenye kumtawalia mambo yake, huyu Ali vile vile ni (mawla) mwenye mkumtawalia mambo yake. Ewe Allah, kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki, na uwe adui kwa yule ambaye ni adui kwake."

Ufafanuzi

IMAMU WA KUMI NA MBILI

IMAMU WA KUMI NA MBILI IMAMU WA KUMI NA MBILI Kwa hakika, Imam Muhammad Bin Hassan Al-Askari ni mtoto wa Imam Hassan Al-Askari, Imamu wa 11 wa Shia, na alizaliwa mwaka 255 Hijri, kuzaliwa kwake kumeshuhudiwa na Maulamaa na wanahistoria wa Madhehebu zote za Kiislamu. Kichekesho kikubwa ni huko kwa ndugu zetu wa Kisuni wanaosema wamesoma dini kuamini kuwepo kwa Maimamu 11 hawa wanaokubaliwa na Shia kuwa walikuwepo na walikuwa niwatu wema, lakini wakati huo huo kuamini kuwa Imam Hassan Al-Askari ambaye ni imamunwa 11 hakuwa na mtoto ili wapate kusema kuwa Imamu wa 12 ni Imamu wa Kubuniwa kama mlivyosikia maneno haya hivi karibuni. Kichekesho kingine ni huko kwa watu kama wao kuamini kuwa Imamu huyo aitwaye "Al-mahdi" bado hajazaliwalakini atazaliwa na atakuwa ni katika kizazi cha Mtume Muhammad (s) sawa na itikadi ya Shia inayosema kuwa Imamu huyo wa 12 atakuwa ni katika kizazi cha Mtume Muhammad (s). Hivyo, iwapo amezaliwa au hajazaliwa Imamu huyo ni LAZIMA ATAKUWA NI KATIKA KIZAZI CHA MTUME MUHAMMAD (s), jambo hili pia kama wangeweza kulikataa wangelikataa na kutwambia kuwa Imamu huyo atakuwa katika kizazi cha Abu Sufiyan lakini wameshindwa kusema hayo!

Ufafanuzi

HARAKATI ZA WAKRISTO KUWASILIMISHA WAISLAM

HARAKATI ZA WAKRISTO KUWASILIMISHA WAISLAM HARAKATI ZA WAKRISTO KUWASILIMISHA WAISLAM Ni mara chache sana kumekuwa na mafanikio ya kuwabadilisha Waislamu kuingia katika Ukristo, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Waislamu wamekuwa wagumu sana kuingia katika dini nyingine ama iwe katika zama za Ukoloni au hata sasa. Harakati za kuwafikia Waislamu kwa lengo la kuwabadili itikadi zao haswa zilianza wakati wa ukoloni. Wamisionari wa makanisa mbalimbali walifanyakazi bega kwa bega na Serikali za Kikoloni, miongoni mwa majina maarufu sana ya Wamisionari kwa Waislamu ni kama yafuatayo: Henry Martyn, Pfander na William Cary India, Lafigerie huko Algeria na Samuel Zwemer na William Gairdner katika ulimwengu wa Kiarabu walitumia muda wote wa maisha yao bila hata kupata Muislamu mmoja aliyesilimu. Baada ya kuona kwamba harakati zao hazikuzaa matunda wamisionari waliitisha mkutano wa Misri uliofanyika CAIRO mwaka 1906 ili kuweka mikakati zaidi ya kuwasilimisha Waislamu. Ikielezewa kama ni ukurasa mpya wa harakati za kuwasilimisha Waislamu Mkutano huo wa Misri ulihudhuriwa na wawakilishi 60 kutoka katika makanisa takribani 30. Mkutano huo wa CAIRO ulifuatiwa na ule wa Edinburgh MWAKA (1910), Lucknow (1911) na Mkutano uliofanyika Jerusalem (1924). Mikutano hiyo kwa kiasi kikubwa ilipelekea kuchuliwa hatua mpya mfano maeneo ya Waislamu yaligawanywa kwa makanisa hayo na wamisionari wakaanza harakati zao za Ukoloni wa kiroho ambao hata hivyo ulishindwa kuonyesha mafanikio katika ulimwengu wa Kiislamu isipokuwa Indoniesia. Lakini wamisionari walionyesha uhai (nguvu) katika maeneo mengine ya Asia na Afrika. Mnamo mwaka 1985 takribani robo million ya wamisionari wa Magharibi walikuwa katika Afrika na Asia pekee wakiwakilisha jumuia 3500 za wamisionari huko Magharibi mwa Afrika.

Ufafanuzi

DUNIA SI CHOCHOTE SILOLOTE

DUNIA SI CHOCHOTE SILOLOTE DUNIA SI CHOCHOTE SILOLOTE Wakati unayoyoma na hakuna awezaye kuuzuia usiende. Hakuna tofauti nyengine baina yetu na wale waliotangulia mbele ya haki ila ni wakati tu. Hakika wakati ndio unaomfanya mtu kuwa mtoto, kijana au kizee. Haukuwepo wakati na hii ni Neema Zake Muumba. Ni wakati huu ndio unaoufanya mchana ukaondoka kwa kuupisha usiku. Hakika, kwetu sisi Waislamu hii Dunia si chochote ila ni wakati tu unaoiweka kuwepo hadi sasa. Matokeo yake ni baina ya mawili; ama tutaiacha sisi ama utatufikia wakati ambao Dunia itabidi iondoke na kila vilivyo Ulimwenguni tukiwemo sisi viumbe. Ni kitu gani, chatufanya kuhangaika na kuruka juu na chini bila ya kuchagua kilicho haramu au halali? Kibri chetu kitatufikisha wapi enyi ndugu wa Kiislamu? Tumefikia kupotozwa na kushughulishwa kwenye sinema na mambo ya michezo. Nani amekusanya mali zaidi ya Qaaruun? Mali yake yote aliyoikusanya haikumsaidia kuondoka hapa Duniani! Haujatufikia wakati wa sisi kuacha mzaha na Mola Wetu? Tambua kwamba Ibliys (Laana za Allaah Ziwe juu yake), ametoa ahadi ya kutupotosha kwa kuifanya Dunia kuwa tamu. Alisema Ibliys: {{Kisha nitawafikia kwa mbele yao na nyuma yao na kuumeni (kuliani) kwao na kushotoni kwao; wengi katika wao Hutawakuta (Hutawaona) ni wenye kukushukuru}} [Suratu al-A'raaf: 17] Basi yule mwenye kumfuata Ibliys kwa kupotezwa muda wake wote kwenye pumbazo, michezo, ufuska na maovu mengine hatokuwa miongoni mwa wenye kupata Rahma Zake Muumba.

Ufafanuzi

IBADA YA MASANAMU

IBADA YA MASANAMU IBADA YA MASANAMU Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, mwenye kurehemu Ibada ya masanamu Miongoni mwa maajabu ya dunia, eti mtu atengeneza sanamu kutokana na jiwe, au chuma, au shaba, au kitu kingine chochote na kisha alielekea sanamu hilo kuliabudu, kuomba dua na kuwa muwakilishi (wa mambo yake) - akilitolea dhabihu na kujikurubisha kwalo kwa kila namna ambayo kiumbe hujikurubisha kwa Muumba wake. Na ajabu ni kwamba, kwenye jamii (hiyo) wapo washairi, wasomi na wengineo. Kwa hakika akili haiwezi kuamini mfumo huu wa mawazo, pamoja na upungufu huu ambao binadamu huupupia. Na pengine mastaajbu kutokana na hayo yataondoka iwapo tu utajua kwamba, zama hizi wapo mamilioni ya Wahindi wanaabudu ngo'mbe - kwa kujipaka mkojo wake na kutabaruku (kutaka baraka) kwa kinyesi chake - wakati huu wa elimu na maendeleo (ustaarabu) na zama za watu kwenda mwezini (space ages). Na mvuto huu unaotokana na upungufu wa binadamu wa tangu kale kwenye ibada ya masanamu, na huu wa leo - kama tunavyoshuhudia kwenye ibada ya ngo'mbe - sio kingine isipokuwa ni nguvu ya kishetani! Je, humsikii Mtukufu (Mwenyezi Mungu) Aliyetakasika Utukufu wake: "Akasema: (Ibilisi) naapa kwa haki ya utukufu wako, bila shaka nitawapoteza wote. Isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliosafishwa." (38:83)

Ufafanuzi

ULIMWENGU ULIVYO ANZA

ULIMWENGU ULIVYO ANZA ULIMWENGU ULIVYO ANZA Profesa Alfred Kroner ni mmoja kati ya maulamaa wakubwa na maarufu sana ulimwenguni katika elimu ya jiolojia ambaye pia ni mwenyekiti wa idara ya jiolojia katika chuo kikuu cha Johannes - Gutenburg huko Ujerumani. Anasema Sheikh Abdul Majeed Al Zindani; "Tulikuwa katika mojawapo ya mikutano ya kujadili miujiza ya sayansi katika Qurani tukufu uliofanyika katika chuo kikuu cha mfalme Abdul Aziz huko Saudi Arabia, na mmoja kati ya waliohudhuria alinijia akiwa amefuatana na profesa Alfred Kroner, na baada ya kunijulisha naye akanambia kuwa huyu ni mtu asiyeamini Mungu, na kwamba nisije nikahatarisha imani yangu kwa kujadiliana naye juu ya mambo ya dini, kwani yeye ni mwerevu sana katika majadiliano ya namna hii." Nikamwambia; "Vizuri." Kisha nikamtaka profesa huyo akae na tuanze kujadiliana. Suali la mwanzo nililomuuliza lilikuwa; "Elimu ya sayansi inasema nini juu ya mwanzo wa dunia, yaani vipi ulimwengu huu ulianza hata zikatokea ardhi na sayari zote hizi" ? Akanijibu ; "Ulimwengu wetu huu ulianza kiasi cha miaka milioni 20,000 iliyopita, na tuna uhakika uliokwisha thibiti kielimu kuwa ardhi hii tunayoishi juu yake pamoja na sayari zote tunazoziona na tusizoziona huko juu vilikuwa kitu kimoja kilichokamatana na kwamba mada zote ambazo hivi sasa ni asili ya sayari zote hizi (elements) asili yake ni moja. Kwa muda wa miaka milioni nyingi vitu hivi viliendelea kuwa kitu kimoja kilichokamatana mpaka pale ulipotokea mripuko (mlipuko) mkubwa sana uliokuja kujulikana kwa jina la 'The Big Bang', ndipo mkamatano huo ulipogeuka kuwa moshi mwingi na mkubwa sana ulioanza kuzunguka kwa kasi kubwa sana na kwa muda wa miaka mingi sana huku ukijitenga tenga na kujikusanya na kujitengeneza kuwa ardhi yetu hii pamoja na sayari na nyota zinazoelea huko juu zinazokwenda kwa nidhamu ya hali ya juu kabisa".

Ufafanuzi

KUMTEGEMEA ALLA

KUMTEGEMEA ALLA KUMTEGEMEA ALLA Wengi katika waliomtegemea M/MUNGU katika ulinzi wake ni wenye kufaulu kwani M/MUNGU hashindwi na viumbe vyake kwa kuwa ndiye aliyeumba uhai na mauti basi hapana aliye na nguvu kumshinda. M/MUNGU ni mpururiaji na yanapowafika Binaadamu warudi na watafakari lakini wasipotoke kwa kudhani M/MUNGU kawasahau. Bali aliloandika limfike Mwanaadamu hapana wakudhuwiya ,ni vyema sote tuwe nafikira moja kuu nayo nikurudii kwake baada ya muda alotuandikia kuishi,mwenyewe MWENYEZI MUNGU anasema katika kitabu chake kitukufu ayya ya 51 Suraaat AT-TAWBA “Sema halitatusibu ila katuandikia M/MUNGU yeye ni mola wetu basi Waislam wamtegemee M/MUNGU tuu” Wengi walipewa nguvu na wakazitumia nguvu hizo vibaya ,wengi wakaneemeshwa mali na mali hizo zikawatia kiburi na jeuri .Bila shaka hivi ndivyo dunia ilivyotawaliwa na fikra potofu ya Mwanaadamu kumdharau Mwanaadamu mwenziwe .Mwenye nguvu humkandamiza mwengine ,na mwenye husda na fisadi kwa jamii nyengine hutafuta sababu na vipenyo kutimiza ndoto ya Ufisadi wake kwa lengo na madhumuni maovu zidi ya mwenziwe.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini