Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

utafiti mbali mbali

NDOA YA MUDA

NDOA YA MUDA

NDOA YA MUDA Ni nini tofauti kati ya ndoa ya muda na kitendo cha zina? - Hussein Muigai Waweru wa Malindi Kenya. Katika kujibu swali hili, ni vyema tukumbushe hapa kwamba, kama unavyojua, dini tukufu ya Kiislamu ndiyo dini ya pekee iliyokamilika katika kila upande wa mahitaji ya maisha ya mwanadamu humu duniani na huko Akhera. Kwa ibara nyingine ni kwamba, dini hii ina majibu kwa kila mahitaji na matatizo yanayomkabili mwanadamu katika maisha yake humu duniani, bila ya kusahau kwamba, inazingatia pia mahitaji yake katika maisha yake ya baada ya kuondoka humu duniani. Mahitaji hayo ni pamoja na ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni na yanayomhusu mtu binafsi. Ndoa ni mojawapo ya mahitaji muhimu sana ya mwanadamu ambayo ni rehema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake humu duniani, na kwa lengo la kuleta utulivu na usalama katika jamii ya mwanadamu. Kama tulivyoliashiria suala hili katika vipindi vyetu vilivyopita, kuna ndoa aina mbili katika dini ya Kiislamu, ya kudumu na ya muda. Ndoa ya kudumu kama jina lake linavyoashiria, ni mkataba na makubaliano yanayofikiwa kati ya pande mbili za mume na mke kwa lengo la kuendelea kuishi pamoja daima katika maisha ya ndoa na familia. Mkataba au makubaliano hayo hubatilika pindi pande hizo zinapoamua kutengana kindoa au kupeana talaka au pale mmoja watu hao waliooana kindoa anapoaga dunia. Kutokana na kuwa tutajishughulisha zaidi na kujibu suala linalohusiana na ndoa ya muda, tunajiepusha kuzungumzia kwa urefu suala la ndoa ya daima kutokana na kuwa hatuna nafasi ya kutosha ya kujadili ndoa zote mbili kwa pamoja.

Ufafanuzi

HAKI ZA MAJIRANI

HAKI ZA MAJIRANI HAKI ZA MAJIRANI Tuanze na kujiuliza, jirani ni nani? Jirani tunayemkusudia hapa ni yule mtu aliye karibu yako kimakazi, yaani nyumba zenu zinakurubiana. Mtu mwenye wasifu huu ana haki kubwa juu yako, ewe muislamu. Itakaposadifu kwamba jirani yako ni ndugu yako wa nasabu na akawa ni muislamu mwenzako. Basi jirani huyu atakuwa ana haki tatu kwako; haki ya ujirani, haki ya udugu na haki ya Uislamu. Na akiwa jirani yako ni muislamu lakini si nduguyo wa nasabu, huyu atakuwa nazo kwako haki mbili; haki ya ujirani na haki ya Uislamu. Na iwapo jirani yako huyu si muislamu na hapana udugu baina yenu, jirani huyu atamiliki kwako haki moja tu nayo ni haki ya ujirani. Hivi ndivyo anavyotufundisha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: "Majirani ni watatu; jirani mwenye haki moja naye ndiye mwenye haki ndogo kuliko wote. Na jirani mwenye haki mbili na jirani mwenye haki tatu. Ama yule ambaye mwenye haki moja ni jirani mushriki (kafiri), na ama ambaye mwenye haki mbili ni jirani muislamu (ana) haki ya Uislamu na haki ya ujirani. Na ama yule mwenye haki tatu ni jirani muislamu aliye ndugu, (ana) haki ya Uislamu, haki ya ujirani na haki udugu". Al-Bazzaar & Abuu Nuaim.

Ufafanuzi

KUJIFANANISHA NA MAKAFIRI

KUJIFANANISHA NA MAKAFIRI KUJIFANANISHA NA MAKAFIRI Assalamu alaikum ndugu wasomaji Shukrani zote ni zake Mwenyezi Mungu , tunashuhudia ya kwamba hapana mola anaepaswa kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad (SAW) ni Mtume wake , ameufikisha ujumbe na kuifikisha amana aliyopewa , kwa hivyo tunakuomba Mola wetu umsalie na kumsalimu Mtume wako huyu mtukufu pamoja na Aali yake na Masahaba wake watukufu - Aamin. Amma baad, Katika mambo yanayosikitisha sana wakati huu ni kule vijana wetu kuzama na kupotea kabisa kwa kuwaigiza makafiri katika kila nyanja za maisha yao. Vijana wa Kiislamu, wengi wao wameipoteza tabia yao , wamekipoteza kitambulisho chao , kama kwamba wanaona haya kusema " Mimi ni Mwislamu". Anasema Sheikh Ahmed Deedat, " Nilipoingia Hong Kong , nilitamani nimuone Mwislamu angalau mmoja amevaa mavazi ya Kiislamu , nione dalili ya Uislamu angalau katika uso wa mmoja wao , nilitamani nimuone angalau mmoja tu anasema , "Mimi hapa Muislamu" natizama huku na kule , sikumuona hata mmoja , wote wamejificha ndani ya mavazi ya Kizungu." Anaendelea kusema Sheikh Deedat , " Nikawaona Masingasinga wamevaa mavazi yao, huku wakitafakhari kwa usingasinga wao, kama kwamba wanasema " Mimi hapa Mr. Singh" . (Mwisho wa maneno ya Sh.Deedat) Nilipoulizwa na mmoja katika wana Zanzinet, " Kwa nini huandiki juu ya maudhui haya ya vijana wa kiislamu kuwaiga makafiri?" Nikakikumbuka kisa hicho cha Sheikh Deedat na kwa bahati, siku ya pili nilipofungua tu, gazeti la kiarabu liitwalo Al Ittihad, katika makala yake ya dini nikayaona Maudhui haya yameandikwa kwa ufupi na kwa ukamilifu .

Ufafanuzi

VIZUIZI VYA UMOJA

VIZUIZI VYA UMOJA VIZUIZI VYA UMOJA Ulimwengu wa Kiislamu umekuwa ukikabiliwa na matatizo mbalimbali katika juhudi zake za kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu. Matatizo hayo yamekuwa yakitoka nje na ndani ya ulimwengu wa Kiislamu wenyewe. Waislamu wenyewe ndio wamekuwa wakijisababishia matatizo ya ndani, matatizo ambayo yanatokana na fikra finyu na za upande mmoja. Fikra hizo finyu kwa hakika zimekuwa zikisababisha harakati na matokeo hatari kwa ulimwengu wa Kiislamu. Vizuizi vya nje vimekuwa vikitokana na ujanja, hila na njama za dhahiri na siri za madola makubwa ya kikoloni ambayo yanautazama umoja wa Waislamu kama hatari kubwa kwao na hivyo kutoustahimili kabisa. Kwa kuzusha mifarakano, ugomvi na fitina miongoni mwa Waislamu, madola hayo yamekuwa yakijaribu kila njia iwezekanayo kuzuia kupatikana umoja wa kutegemewa miongoni mwa Waislamu, umoja ambao unaweza kuwapelekea kuunda harakati moja yenye nguvu duniani. Ni wazi kuwa mambo na vizuizi vinavyozuia kupatika umoja na nguvu katika ulimwengu wa Kiislamu ni hatari kubwa kwa Waislamu kwa sababu jambo hilo linazuia kabisa kupatikana njia za kielimu za kukabiliana na suala hilo. Pia ni wazi kuwa kughafilika na juhudi za kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu ni jambo linalopasa kuepukwa kwa kila njia. Pamoja na hayo tunapolinganisha madhara ya vizuizi vya ndani na nje katika kuzuia umoja wa Kiislamu tunaona kwamba vizuizi vya ndani ndivyo vilivyo na madhara makubwa zaidi kwa umoja huo.

Ufafanuzi

ITIKADI YA HAKI (JUSTICISM)

ITIKADI YA HAKI (JUSTICISM) UTANGULIZI WA KWANZA Siku moja, nikiwa Mkuu wa Idara ya Itikadi na mafunzo katika chama cha siasa(naomba nisikitaje),nilirushiwa swali na mtu mmoja akitaka nimweleze ni nini itikadi ya chama chetu na inatofautianaje na ya vyama vingine. Sehemu ya kwanza ya swali lake ilikuwa nyepesi kujibu,maswali zaidi yaliibuka katika kujitofautisha na wengine. Swali lake liligeuka kuwa mjadala mrefu ambao uliambatana na nukuu kama vile, wewe wasema unamwamini Mungu,mashetani nao wanaamini na kutetemeka,ni nini basi tofauti ya uumini wako na ibilisi. Yamkini tofauti ya kiitikadi baina ya vyama vya siasa nchini Tanzania, si dhahiri sana.Matharani, kwa vyama vya mageuzi ambavyo vimejitambulisha kama wafuasi wa itikadi ya Demokrasia ya Jamii haviko mbali na utambulisho wa chama tawala kiitikadi (hapa nidokeze kuwa TANU iliwahi kutaja kwamba inaamini katika Social Democracy) Taifa letu lina vyama vya siasa vipatavyo kumi na vinane(18), kwa maana hiyo kama kila chama kina itikadi yake, basi vyama hivi vinaamini katika masuala 18 yaliyo tofauti. Binafsi siamini kwamba hivyo ndivyo ilivyo. Yamkini pia baadhi ya vyama imani zao zinafanana, tofauti iko katika nani ana msimamo mkali,msimamo wa wastani au vinginevyo katika itikadi husika.

Ufafanuzi

JE TUNAJIFUNZA KUTOKA KWA WAKATOLIKI

JE TUNAJIFUNZA KUTOKA KWA WAKATOLIKI JE TUNAJIFUNZA KUTOKA KWA WAKATOLIKI Imebidi kuandika makala hii kutokana na makala iliyoandikwa na Kaanaeli Kaale yenye kichwa cha habari 'Kusigana kwa matokeo baina ya shule za Kikatoliki na Kiislamu' (Mwananchi 17 Oktoba 2006). Makala ilikuwa inaeleza yaliyojadiliwa katika mkutano ulioandaliwa na Shirika la Elimu ya Sheria Tanzania (TANLET) katika moja ya harakati za kumuenzi hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Katika mkutano huo, ilielezwa kuwa shule za Kikatoliki ndiyo shule bora zinazoshika nafasi 'kumi bora' kwa kutoa matokeo mazuri ya mitihani na shule za Kiislam ndiyo 'zinazoshika mkia' katika kutoa matokeo mabaya. Ama taarifa hizo za shule za Wakatoliki kufanya vyema katika mitihani si habari mpya ni jambo linalotangazwa na vyombo vya habari kila mwaka kwa hiyo linafahamika. Ila kitu cha kushangaza ni kuwa kimezidi nini hii leo hadi ikawa ni muhimu kujadili ufanisi wa shule za Waislam hadharani kisha tukapewa ushauri kuwa Waislamu tujifunze kutoka kwa Wakatoliki ili nasi shule zetu zifanye vyema kama zao ili huu upogo wa elimu kati ya Waislam na Wakristo utoweke? Ushauri huu umenitia simanzi kubwa na ndiyo hasa sababu ya kuandika makala hii. Bubu alizungumza kwa uchungu wa mwanaWe ni msemo mashuri. Leo hii sisi Waislam tumekuwa watu wa kusaidiwa na Wakatoliki tuelimike! Waswahili tuna msemo 'Akutukanae hakuchagulii tusi.'

Ufafanuzi

UMRI WA MWANAADAMU

UMRI WA MWANAADAMU UMRI WA MWANAADAMU Umri Haurudi kwa maana miaka unayoishi huisha tena tunavyoishi na muda wetu ni siri hakuna ajuaye ila aliyetuumba. Viungo hunyongonyea umri ukiwa mkubwa, nuru hupungua ya macho au kutoweka kabisa, Sauti hubadilika, na sisi hupinda mgongo kama tulikuwa ni warefu wa kimo hurudi kidogo. Nguvu zile za ujana na wingi wa starehe ama huzitamani tungekuwa nazo wakati wote au kwa uzee tunaofikia tukijipima na tukazihesabu amali zetu tulizozitenda ujanani zisizokuwa na kheri, baadhi yetu hulia hata katika sala au yakihadithiwa yale yetu na vikundi katika jamii, basi si hasha tukabadili hata njia maana pengine watu wakati huo wanafinyana masikio, “ndo huyo kiumbe” zama zimepita, alitamba zama zake. Basi baadhi yetu hatupendi kuyasikia yakikumbushwa yetu “yanatia haya” yanatufanya tujute, lakini pia yanawanyanyasisha wana wetu wanaposikia baba yao hatajwi kwa wema.

Ufafanuzi

SIRI ZA MAFANIKIO I

SIRI ZA MAFANIKIO I SIRI ZA MAFANIKIO I Kipindi cha matarajio na hamu ya kupata mafanikio Kipindi cha ujana ni kipindi cha hamu ya kupata na matarajio. Ni kipindi cha kuwa na furaha. Ni wakati ambao mustakbali wa kila kijana huja mbele ya macho yake katika sura ya ndoto tamu. Huanza kufikiria. Hufanya mipango na kuzipima raghba kuu katika moyo wake. Hata hivyo, wakati fulani hutokea mtu akashindwa katika kipindi cha ujana. Mtu huyo, hata baada ya kuwa mtu mzima. akawa hawezi kufikia hata moja katika matarajio yake. Wakati fulani pia hutokea, bila mategemeo, kwamba mtu akapata zaidi ya matarajio yake na ndoto zake tamu zikawa kweli. Kwa kweli, mtu mmoja kufanikiwa na mwingine kushindwa sio majaaliwa au bila sababu iliyo nyuma yake. Sababu za yote mawili lazima zitatokana na maisha ya wahusika. Tunaweza kuwa na hakika kuwa yule anayefanikiwa alianza maisha katika namna ambayo humpa uhakika wa mafanikio, na yule anayeshindwa, kwa kiasi kikubwa, hufanya hivyo kutokana na makosa yake mwenyewe. Ni kwa sababu amepita katika njia ambayo haikumpeleka kwenye makusudio yake.

Ufafanuzi

SIRI ZA MAFANIKIO II

 SIRI ZA MAFANIKIO  II SIRI ZA MAFANIKIO II Pendeleo na shauku Moja katika sababu za mafanikio ni kufanya kazi unayoipenda na ambayo inalingana na akili au uwezo wako wa kiakili. Mwenyezi Mungu hajatuumba sisi katika namna moja. Sisi wote hatukupewa uwezo wa kufanya kila kitu. Bali, ili kuendesha jamii kwa yakini, amempa kila mtu ladha na mwelekeo wa aina yake. Imekuwa hivyo, ili mtu aweze kuchukua utaalamu anaoupenda au unaolingana na kipaji cha akili yake, na unaomvutia; na hivyo kuzalisha faida kutokana na ustadi wa kiasili. Kwa ujumla, moja kati ya sababu za vijana kushindwa na hata kuanguka ni kutofuata kanuni hii imara. Na kutokana na propaganda mbaya na mafunzo ya kimakosa huziendea kazi ambazo haziendani na vipaji vyao.Huchukua shughuli zisizofaa. Husahau kanuni inayokubalika isemayo: “kila akili ina mwelekeo maalumu. Bahati nzuri ni kwa yule anayeupata”.

Ufafanuzi

KUTOA MSAADA

KUTOA MSAADA KUTOA MSAADA Kutowa kwa ajili ya M/Mungu nakutowa kwa ajili ya wengine wanaohitaji ni thawabu kubwa kwani watoao kwanjia hizo ndio watakao radhi za Mola wao na waliojuwa maana ya kuneemeshwa. Kuneemeshwa nako kuna sura nyingi kuna neema ya akili, kuna neema ya kiwiliwili, kuna neema ya mali, kuna neema ya watoto, kuna neema ya elimu na kadhalika. Sisi tulopewa utukufu tafauti na wanyama na viumbe wengine ndoo tupaswao kuzitumia neema hizo katika njia za kheri tupu. Tupo tulio na kasoro na ukosefu wa shukrani kwa kufanya ubaghili kwa neema hizo, au kudhalilisha kwa neema hizo. Ndio sisi tutesao wanyama kama punda au ng’ombe, kuwatwisha kazi nzito kutwa nzima bila  kuwapa malisho mazuri. Punda leo hii hutwishwa chasesi nzima ya lori anapumua hadi anaanguka! Punda leo hii anapakiwa mifuko ya saruji kama ana mwili wa chuma, punda leo hii anapakiwa nondo au boriti mchungaji na rafiki zake nao wakakaa juu ya gari hiyohiyo iliyo mabegani mwa mnyama, na kigongo anachopigiwa si cha kawaida tena hapachaguliwi pakupigwa, sikuhizi hupigwa hadi masikioni utashangaa ndoo anafanywa asikie amri au vipi! Lakini tunarudi wapi, kwani sisi wanaadamu tuna mtindo wakulaumiana sisi wenyewe tunapotendeana maovu pahala pakushukuriwa husema hee shukrani za punda mateke, lakini leo mabadiliko shukrani za Mwanaadamu vigongo na mzigo mzito, Punda wangekuwa na kauli nao wangesema, hiyo ni dhambi jamani.

Ufafanuzi

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 6

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 6 TOFAUTI KUU ZA SHERIA (6) USIMAMIZI NA MUUNDO WA SHERIA. Tofauti nyengine inahusiana na usimamizi na namna zinavyoundwa hizo sheria. Kawaida, jamii fulani inaunda sheria zake kwa ajili ya kutawala jamii husika na kuilinda. Mfano Hitler alipoingia madarakani alipitisha sheria ya kuuawa kwa Mayahudi wote ilimradi tu kulinda maslahi ya wajerumani walio wengi ndani ya Ujerumani. Alipoondoka madarakani sheria hii ikafa. Ama kwa Sheria ya Kiislamu, sio ya jamii fulani pekee. Inagusa ulimwengu mzima hata kwa wasio Waislamu. Kwa mfano kuna sheria baina ya taifa la Kiislamu linavyoishi na wasio Waislamu (Dhimmi). Muislamu hatakiwi kuimwaga damu ya binaadamu hata awe Dhimmi bila ya sababu. Ni dhambi kubwa kuimwaga damu ya Muislamu bila ya sababu yoyote. Maingiliano baina ya Waislamu na wasio Waislamu, uchumi wa Kiislamu na siasa za Kiislamu ni vipengele vilivyokuwa huru kutumiwa na walimwengu wote kwani kuna faida kubwa. Ikiwa ni Muislamu au sio Muislamu. Sheria ya Kiislamu ni ya ulimwengu mzima na watu wake wote. Tofauti na sheria za binaadamu ambazo haziwezi kwenda pamoja na maendeleo anayofanya mwanaadamu duniani. Ni lazima zitabadilika tu. Dhumuni kuu ya Sheria ya Kiislamu haikufungwa kuzunguka jamii pekee. Bali kumpa haki kila mmoja, kuunda jamii yenye tabia nzuri, taifa imara na mwisho kuifanya dunia sehemu inayofaa kuishi kwa mazingira yake mwenyewe binaadamu.

Ufafanuzi

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 5

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 5 TOFAUTI KUU ZA SHERIA (5) UTANGULIZI. Hamna shaka yoyote kuwa kuna tofauti kubwa baina ya Sheria za Kiislamu na zile atungazo mwanaadamu. Sababu hii ndiyo inayowafanya maadui wa Uislamu kuzitaka Sheria za Kiislamu ziwe ni kama za kwao. Masikio na macho yetu hayajaacha kushuhudia ni namna gani Sheria za Kiislamu zinavyopingwa mbele ya wale Makafiri na hata Waislamu poa. Kwa Muislamu wa kweli anaelewa fika kuwa ni sheria za Allah (Subhanahu Wataala) ndizo zitampa mafanikio hapa duniani na Akhera. Nimejitahidi kutoa maneno yalokuwa magumu na kutumia zaidi maneno ya Kiswahili ili makala hii iweze kusomeka na Waislamu wote. Yapo baadhi ya maneno ambayo nimeyawekea kwenye mabano kwa ueleo mzuri. Hali kadhalika nimeonelea kuonesha mifano michache kwa kutumia sheria za nchi ili kuweka wazi hoja.

Ufafanuzi

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 4

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 4 TOFAUTI KUU ZA SHERIA 4 Dalili zinaonesha kuwa sheria za Kiislamu ni za milele na hazihitaji marekebisho na wala marekebisho hayahitajiki kwa sheria za kiislamu. Sheria za Kiislamu zimewekwa kurekebisha tabia na matatizo ya jamii ya binaadamu kwa muda wote ambao atajaaliwa kuishi ndani ya dunia hii. Ingawa Sheria za Kiislamu msingi wake ni Qur-aan na isiyohitaji mabadiliko, lakini sheria hizi za Kiislamu zinaweza kuendelezwa na kupatiwa ufumbuzi wa mambo ambayo yana khitilafu ndogo ndogo. Hii ni kwa kutumia vipengele vya Fiqhi kama Qiyaas (ufumbuzi), kauli za Maswahabah, Sadd al-dharai (kuharamisha halali inayopelekea kwenye haramu) na nyenginezo. Kwa mfano asili ya kuharamishwa ulevi ni kuwa na athari mbaya kwa jamii, lakini Qur-aan imezungumzia kinywaji cha ulevi na sio kuhusu madawa ya kulevya kama kokeni na bangi. Hapa tunatumia Qiyaas ili kupata hukmu yake na kuona kuwa nayo pia yana athari mbaya kwa jamii, hivyo kila chenye madhara ni haramu. Na kupata hukmu ya madawa ya kulevya kuwa ni haramu pia.

Ufafanuzi

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 3

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 3 TOFAUTI KUU ZA SHERIA 3 SHERIA ZA KIISLAMU ZINAENDA NA WAKATI Dalili zinaonesha kuwa sheria za Kiislamu ni za milele na hazihitaji marekebisho na wala marekebisho hayahitajiki kwa sheria za kiislamu. Sheria za Kiislamu zimewekwa kurekebisha tabia na matatizo ya jamii ya binaadamu kwa muda wote ambao atajaaliwa kuishi ndani ya dunia hii. Ingawa Sheria za Kiislamu msingi wake ni Qur-aan na isiyohitaji mabadiliko, lakini sheria hizi za Kiislamu zinaweza kuendelezwa na kupatiwa ufumbuzi wa mambo ambayo yana khitilafu ndogo ndogo. Hii ni kwa kutumia vipengele vya Fiqhi kama Qiyaas (ufumbuzi), kauli za Maswahabah, Sadd al-dharai (kuharamisha halali inayopelekea kwenye haramu) na nyenginezo. Kwa mfano asili ya kuharamishwa ulevi ni kuwa na athari mbaya kwa jamii, lakini Qur-aan imezungumzia kinywaji cha ulevi na sio kuhusu madawa ya kulevya kama kokeni na bangi. Hapa tunatumia Qiyaas ili kupata hukmu yake na kuona kuwa nayo pia yana athari mbaya kwa jamii, hivyo kila chenye madhara ni haramu. Na kupata hukmu ya madawa ya kulevya kuwa ni haramu pia.

Ufafanuzi

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 2

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 2 TOFAUTI KUU ZA SHERIA (2 Hapana shaka kuwa binaadamu mmoja anatofautiana na mwengine, ni sababu hii imesababisha kuwepo mipaka ya nchi, tofauti ya lugha, kutofautiana kwa makabila na rangi. Ndivyo sheria za mwanaadamu zinavyotafautiana baina ya sheria moja na nyengine. Pia sheria hizi za leo ni tofauti na zile za miaka hamsini tu iliyopita. Sheria za Kiislamu zinajulikana na zitaendelea kuwa hazina mpaka (boundary) wowote wa tofauti ya wakati, taifa au sehemu anayoishi. Tuelewe kuwa mwananchi yeyote aliyekuwa chini ya Taifa la Kiislamu awe mweupe au mweusi, wa nchi yoyote, basi sheria ya mwizi (pindi ushahidi wa kweli ukithibitishwa) ni kukatwa kiganja cha mkono wa kulia, mlevi bakora 80 na mengineyo. Tofauti na sheria za binaadamu ambapo akibadili taifa na sheria zake zitabadilika. Kwa mfano, twaelewa sote namna ya gonjwa hatari la ukimwi linavyoangamiza dunia nzima. Lakini Tanzania ipo kimya kuhusu muathirika anayetambuwa kuwa ameathirika kujamiiana na asokuwa muathirika kwa lengo la kumuambukiza gonjwa la ukimwi kwa makusudi. Hali sio hiyo kwa Afrika ya Kusini kwani sheria zao zinaruhusu muathirika wa namna hiyo kufikishwa Mahakamani. Kwa upande wa silaha za nyuklia, Marekani na Israel zimejipa ruhusa ya kutengeneza na kuhifadhi silaha hizo ilhali nchi nyengine zote yawa ni haramu kwao sio tu kutengeneza, hata kuhifadhi mali asili zinazotumika kutengenezea nyuklia kama zebaki “mercury”. Pia vitendo vya liwaati vimezuiwa Zanzibar (kifungu namba 150 cha Sheria ya Jinai namba 6 ya mwaka 2004). Wakati sheria za Magharibi sio tu zinaruhusu maingiliano haya machafu, hata ndoa zafungwa baina ya watu wa jinsia moja.

Ufafanuzi

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 1

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 1 TOFAUTI KUU ZA SHERIA 1 UTANGULIZI. Hamna shaka yoyote kuwa kuna tofauti kubwa baina ya Sheria za Kiislamu na zile atungazo mwanaadamu. Sababu hii ndiyo inayowafanya maadui wa Uislamu kuzitaka Sheria za Kiislamu ziwe ni kama za kwao. Masikio na macho yetu hayajaacha kushuhudia ni namna gani Sheria za Kiislamu zinavyopingwa mbele ya wale Makafiri na hata Waislamu poa. Kwa Muislamu wa kweli anaelewa fika kuwa ni sheria za Allah (Subhanahu Wataala) ndizo zitampa mafanikio hapa duniani na Akhera. Nimejitahidi kutoa maneno yalokuwa magumu na kutumia zaidi maneno ya Kiswahili ili makala hii iweze kusomeka na Waislamu wote. Yapo baadhi ya maneno ambayo nimeyawekea kwenye mabano kwa ueleo mzuri. Hali kadhalika nimeonelea kuonesha mifano michache kwa kutumia sheria za nchi ili kuweka wazi hoja.

Ufafanuzi

KUPENDA DUNIA

KUPENDA DUNIA KUPENDA DUNIA Kila binadamu afahamu kuwa sababu kubwa ya udanganyifu wa mambo yote na kusahau Akhera ambayo ni nchi ya kudumu ni kupenda maisha ya dunia. Kwani mtu anapopenda maisha ya dunia na kusahau Akhera humtamanisha mtu huyo arefushe umri wake ili apate kuishi daima milele, na kumghafilisha mauti, na kumsahaulisha amsahau Mola wake na kumpunguzia mambo ya dini. Kama alivyomkataza Mwenyezi Mungu S.W.T. Mtume Wake S.A.W. ajiepushe na watu hao katika Suratin Najm aya ya 29, “Basi jiepushe na wale waupao kisogo ukumbusho Wetu huu, (Qurani) na wala hawataki ila maisha (ya starehe) ya dunia.” Pia alimkataza katika Surat Taha aya ya 131, Maana yake, “Wala usivikodolee macho yako tulivyowastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao (hao wabaya). Hivyo ni mapambo ya maisha ya dunia tu, ili tuwafanyie mtihani kwavyo.”

Ufafanuzi

WEMA NA UOVU

WEMA NA UOVU MWANADAMU BAINA YA MEMA NA MAOVU Uislamu kama zilivyo jumbe nyingine za mbinguni, unategemea katika utengefu wake mkuu/enevu/jumla, juu ya kuilea nafsi ya mwanaadamu kabla ya kitu chochote. Ni kwa ajili hii basi, Uislamu unahusisha juhudi kubwa kwa lengo la kuingia ndani ya nafsi kupanda mafundisho yake ndani ya johari (kiini/kokwa) yake mpaka nafsi iweze kumeza dozi yake. Na hazikudumu jumbe za Mitume na kuunda pembezoni mwake makundi ya waumini, ila ni kwa kuwa nafsi ya mwanaadamu ndio iliyo kuwa maudhui ya amali yake (hizo jumbe) na muhimili wa harakati zake. Kwani mafundisho yao (hao mitume) hayakuwa ni maganda yaliyo gandana yakaangukia kwenye nyundo ya maisha itukutikayo. Wala hayakuwa rangi zivutiazo macho ambazo hufifia kwa mpito wa siku. Hapana, hayakuwa hivyo. Hakika walichanganya misingi yao na makunjo/mageuko ya nafsi, kwa hiyo basi misingi hiyo ikawa ni kani (nguvu) inayo tawala wasiwasi wa maumbile ya kibinaadamu na kudhibiti mielekeo yake.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini