UADILIFU WA MUNGU
BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
UADILIFU WA MUNGU
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema: “Mwenyezi Mungu na Malaika, na wenye elimu wameshuhudia kuwa hakuna aabudiwaye ila Yeye tu, ni Mwenye kusimamia uadilifu. Hakuna aabudiwaye isipokuwa Yeye tu, Mwenye nguvu na Mwenye hekima.” (Qur’ani, 3:18)
“Hakika wale wanaozikataa Aya za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa Manabii pasipo haki, na kuwauwa watu wanaoamuru mambo ya uadilifu, basi wape khabari ya adhabu iumizayo.” (Qur’ani, 3:21)
“Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mtoe ushahidi kwa uadilifu. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutowafanyia uadilifu fanyeni uadilifu, huko ndiko kunakomkurubisha mtu na ucha Mungu, na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda.” (Qur’ani, 5:8)
“Kwake ndio marejeo yenu nyote, ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Hakika Yeye ndiye huanzisha kiumbe kisha hukirudisha ili awalipe walioamini na kufanya vitendo vizuri kwa uadilifu. Na waliokufuru, (wao) watapata kinywaji cha maji yanayochemka, na adhabu yenye kuumiza kwa sababu walikuwa wakikataa.” (Qur’ani, 10:4)
“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu, na uovu, na uasi, anakuwaidhini, ili mpate kukumbuka.” (Qur’ani 16:90)
Ni lazima kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atende uadilifu. Kwa upande wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Yeye si muhitaji. Yeye ni huru katika haja na ni mmiliki wa msingi kamili wa hekima. Kwa hiyo haiwezekani kwamba Angekuwa dhalimu kwa viumbe vyake. Yule aliyedhalimu, hufanya hivyo kwa sababu hakuna chaguo adilifu la kumwezesha kutimiza malengo yake, kwa hiyo huvuka mipaka ya uadilifu na kunyonga haki za wengine. Lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) yupo mbali sana juu ya hili. Hahitaji chochote kutoka kwa viumbe vyake na aliumba kutokana na huruma Zake zisizo na ukomo, kwa hiyo kwa hakika tunaweza kuvihitimisha kwamba matendo yote ya Mungu (s.w.t.) na amri zote za Mungu (s.w.t.) ni adilifu.
Kwa uadilifu tuna maanisha kwamba kila kitu kimewekwa mahali kinapostahili, kila kitu kinapewa kile kinachostahiki na kuwa na uwezo wa kustahamili. Si kila mara uadilifu kuwa na maana ya usawa na katika zama zetu jamii nyingi zimeangukia kwenye imani hii ambayo kwa kweli ni mtego wa wasio fahamu. Kwa mfano, uadilifu unataka kwamba mtoto mchanga anyonyeshwe maziwa ya mama yake ambapo mtu mzima anaweza kula mkate (bofulo) na nyama. Usawa ungeamuru kwamba wote wawili mtoto mchanga na mtu mzima walishwe chakula cha aina moja. Ama wote wawili wanakunywa maziwa au wale mkate (bofulo) na nyama. Lakini mtu mzima hawezi kuendelea kuishi kwa kunywa maziwa peke yake ambapo mtoto mhanga hawezi kumeng’enya mkate (bofulo) na nyama. Kwa kweli mkate (bofulo) na nyama zingedhuru vikali sana afya ya mtoto. Usawa katika mfano huu haulingani na uadilifu, kwani haingekuwa uadilifu kwa binadamu na tembo kuwa na moyo wa saizi sawa. Moyo wa binadamu ni mdogo sana kuweza kuhimili mahitaji ya mwili mkubwa wa tembo ambapo moyo wa tembo haungeenea kwenye kifua cha binadamu. Usawa katika mfano huu ungesababisha kifo cha viumbe vyote viwili binadamu au tembo.
Mwisho Uadilifu usio na ukomo katika mpangilio maalum wa taswira pana ya ulimwengu wote unaweza tu kujulikana kwa hekima ya Mungu iliyo kamili. Kwa hiyo sharia zilizotungwa na Mungu ni za kufuatwa bila hoja, kwani zenyewe ni tiba timilifu ya dhuluma yoyote.
Kutumwa kwa Mitume na maandiko Matakatifu na ushawishi usio na mwisho wa kutenda mema na ukumbusho kuhusu maisha ya akhera ni dalili kwamba mwanadamu anayo sehemu katika kutengeneza hatima yake. Mungu (s.w.t.) hafanyi lolote bila sababu, kwa hiyo kuwaambia wanadamu kuamini ukweli na si udanganyifu kwa tishio la moto wa jahanamu inawezekana tu kuwa ni uadilifu kama binadamu analo chaguo katika jambo hili. Mtu asiye na hiari katika matendo yake hawezi kuwajibishwa kwayo. Katika mifumo ya kamahakama na mahakama za sharia, tunaona kwamba watoto au wale wanaofikiriwa kuwa akili zao si timamu hawapewi adhabu iliyo kamili, kama ambavyo angepewa mtu mzima mwenye akili timamu. Yote haya yanathibitisha kwamba mwanadamu anao uhuru wa kuamini atakavyo na kutenda apendavyo.
Kutumwa kwa Mitume na maandiko Matakatifu na ushawishi usio na mwisho wa kutenda mema na ukumbusho kuhusu maisha ya akhera ni dalili kwamba mwanadamu anayo sehemu katika kutengeneza hatima yake. Mungu (s.w.t.) hafanyi lolote bila sababu, kwa hiyo kuwaambia wanadamu kuamini ukweli na si udanganyifu kwa tishio la moto wa jahanamu inawezekana tu kuwa ni uadilifu kama binadamu analo chaguo katika jambo hili. Mtu asiye na hiari katika matendo yake hawezi kuwajibishwa kwayo. Katika mifumo ya kamahakama na mahakama za sharia, tunaona kwamba watoto au wale wanaofikiriwa kuwa akili zao si timamu hawapewi adhabu iliyo kamili, kama ambavyo angepewa mtu mzima mwenye akili timamu. Yote haya yanathibitisha kwamba mwanadamu anao uhuru wa kuamini atakavyo na kutenda apendavyo.
Hata hivyo ipo mipaka kwa yale anayoweza kuyafanikisha kwa hiari yake. Hiari yake haimuhusu yeye kuridhia vitu vije katika kufanya vyovyote kufuatana na matamanio yake. Hawezi akatoka na kuchukuwa chochote atakacho kirahisi, anywe maji ya bahari hadi yakauke ili akate kiu chake au ale chakula chote kilichopo duniani ili aridhishe tumbo lake. Mwanadamu anayo hiari, lakini ni katika mipaka hiyo tu ambayo Mungu (s.w.t.) amemwekea anaweza tu kuchaguwa miongoni mwa yale ambayo Mungu (s.w.t.) amempa na si zaidi ya hayo, kwa sababu hakuna kingine kilichopo kwa ajili yake.
Kwa hiyo, hiari ya mwanadamu haikukamilika. Vipo vitu fulani ambavyo binadamu anaweza kujichagulia na vitu vingine ambavyo hulazimishwa kwake na ulimwengu na watu wengine ambao wanayo hiari yao wenyewe. Kwa hiyo, uwezo wa binadamu kuunda hatima yake ni njia ya katikati.
Hana hiari ya kuamua chochote anachotaka, wala si kila kitu kimeamuriwa kwa ajili yake. Mungu (s.w.t.) humwekea kila binadamu kiasi fulani cha ukalimu na kila binadamu anawajibika kwa yale anayofanya na zawadi hizo.
Wapo wale wanaosema kwamba binadamu hana hiari kabisa kwamba kila kitu afanyacho, ama kizuri au kibaya, kimeamuriwa kwake na Mungu (s.w.t.). Fikira hii si sahihi kwa sababu mbili zilizo wazi.
Kwanza, ingekuwa na maana kwamba udhalimu wote hapa duniani ambao umefanywa katika historia ni matendo ya Mungu (s.w.t.) na si matendo ya watu ambao kupitia kwao yalifanyika; kwamba Mungu (s.w.t.) ni wa kulaumiwa kwa mauaji yote, wizi wote, ubakaji wote, ukandamizaji wote na uovu uliopata kufanywa.
Pili, hukumu ya akhera haingekuwa na umuhimu kama mwanadamu hakuwa na hiari katika mambo yake; pangekuwa na maana gani kumhukumu mtu ambaye hakuhusika na yaliyo mtokea?
Ukweli wa Qur’ani Tukufu ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa mfululizo huwaamuru wanadamu kufanya uadilifu na wema, na huwakataza wasifanye udhalimu na uovu. Hii inaonesha kwamba njia mbili zipo wazi kwa binadamu lakini hiari kufuata yoyote kati ya njia hizi, na atawajibishwa kwa chaguo hilo. Jinsi gani Mungu angeamuru kufanya mema na kuwa waadilifu na halafu avunje amri Yake mwenyewe?
Umuhimu wa Swala.
Alipoulizwa kuhusu umuhimu wa Swala Mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) Imamu Jafar Sadiq (a.s.) alisema yafuatayo:
1. Siku ya Hukumu kitu cha kwanza ambacho mtu atawajibika ni swala yake. Kama itakubaliwa, matendo yake mengine mema yatakubaliwa pia. Na kama swala itakataliwa matendo yake mengine mema yatakataliwa pia.
2. Mtu alikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akamwomba amfundishe somo la uadilifu. Mtume (s.a.w.w.) wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alisema “Usiruke swala kwa makusudi kwa sababu yeyote anayeacha kuswali kwa hiari yake mwenyewe atakuwa nje ya mpaka wa Uislamu. Hakuna tofauti baina ya kuamini na ukafiri isipokuwa kuacha swala.”
Sahaba alimuuliza Imamu Sadiq (a.s.) “Tendo gani lenye kustahili sifa ambalo humkaribisha mtu karibu zaidi na Mola wake Mlezi?” Alisema Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliulizwa kuhusu tendo lililo bora sana na alijibu: Katika matendo yote lililo bora sana ni swala iliyo swaliwa kwa wakati wake.
MWISHO