MKE ZAIDI YA MMOJA
BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
MKE ZAIDI YA MMOJA
HIKMA NA MTIZAMO WA UISLAMU JUU YA KUOA MKE ZAIDI YA MKE MMOJA
Kwa hakika tunakubaliana kiakili kwamba kila aliyekitengeneza kitu basi atakuwa na uwezo na maarifa ya kukiendesha na kutoa miongozo yake katika kitu hicho. Sasa kama sisi ni binaadamu tena waislamu lazima tukubali na tuyakinishe kwamba huu ulimwengu umeumbwa, kwa hivyo aliye bora wa kutoa miongozo juu yetu ni Allah (S.W).
Allah (S.W) amemuumba mwana-adamu na anamjua fika udhaifu wake, uwezo wake na matamanio yake. Kwa ajili hiyo hakumuacha ovyo kama mnyama akamuwekea utaratibu wa kufuata na kutatua matatizo yake na jinsi ya kumaliza matamanio yake.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Na katika alama zake (Allah S.W.), ni kukuumbieni nyinyi kutokana na Nafsi zenu (binaadamu mwezenu), wake ili mpate kutulia kwao, na akajaalia baina yenu mapenzi na huruma, hakika katika jambo hili kuna dalili tosha kwa watu wenye kutafakari (kutumia akili zao) sura 30:21.
Tunaweza kuona hapa kwamba kutulia kwa binaadamu katika hali yake na kuweza kuwa na huruma kwa jamii yake ni lazima mtu huyu, apate sababu ya mke (ndoa). Kwa ajili hiyo binaadamu akiishi bila ndoa au kuwa na mpenzi wa nje binaadamu, huyo hana utulivu wala huruma.
Sababu za uislamu kuruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja, kama tulivyoona kwamba utulivu wa maisha ni watu kuishi pamoja katika ndoa, na huo ndio uumbaji wa Allah.
Mwenyezi Mungu anasema;
" Na katika kila kitu tumeumbiwa viwili na viwili (pea) ili mpate kukumbuka " sura 51:49.
Sasa kama tulivyoona katika kustawi kwa maisha na kupatikana manufaa katika jamii ni lazima kuweko ushirikiano baina vitu viwili mfano usiku na mchana, jua na mvua katika nguvu za umeme Positive + negative n.k. Tunaelewa fika kwamba katika sisi binaadamu kuwa wanawake na wanaume na jinsia ya kike ni wengi zaidi kuliko ya kiume. Mfano : katika jamii inayosihi watu 5,000 basi utakuta wanawake ni wengi zaidi kuliko wanaume wanaostahili kuolewa na kuoa.
Tuangalie jaduweli ndogo kama mfano wa hayo:-
Watu wote
Wanawake
Wanaume
Wastahili kuolewa
Wastahili kuoa
Salio
Wk
Wu
5000
3500
1500
3500
1500
2000
Kwa mfano huu mdogo vuta fikra zako hawa wanawake waliosalia watafanya nini na haki ya maumbile ni kuishi wawili wawili: matokeo yake ni kutaka tamaa na maisha ya ndoa na baadae kutumbukia katika matendo ya zinaa na uchafu mwengineo.
Wanawake waliofiliwa na waume zao na hawa kadhalika washaonja maisha y ndoa, na wanataka kusimamia maisha yao katika jamii. Jee wataishi vipi bila kupatikana nusra ya ndoa?
Wajane- walioachwa na waume zao kutokana na hitilafu Fulani Fulani katika maisha, nao itakuwaje kama kila mtu aishi na mke mmoja. Kwa kweli hizi ni fkra za kikafiri hazina sehemu katika jamii ya kiislamu .
Wanawake waliokuja katika Imani ya Kiislamu (waliosilimu). Wanawake mfano wa hawa wamo katika jamii zetu na waliotokezea katika wakati wa Mtume ( S.A.W).
Mwenyezi Mungu anasema;
"Enyi mlioamini watakapokujieni wanawake waliohama basi wajaribuni Allah (S.W) anafahamu zaidi Imani zao na wala hamna ubaya juu yenu kuwaoa mtakapo wapa mahari yao ………." Sura 60;10.
Ndugu wa kiisalmu na kundi hili nalo litaishi vipi katika jamii ya kiislamu wakati halina stara ambayo ni waume. Ikiwa tutasema kuwa kila mtu mke mmoja hizi ni fikra za kutaka kuvuruga maadili ya kiislam).
Na mifano kama hiyo iko mingi tu. Jambo la kusikitisha utaona makafiri wanawatumia wanawake wa kiislamu wasioelewa. Elimu na Hikma ya Dini yao kueleza kwamba kuowa wake wengi kunawananyima Haki za wanawake- na zaidi la kusikitisha ni kusema kuwa kuoa wake wengi ni njia ya kueneza maradhi ya Ukimwi. Inna lilahi waina ilahi rajiun- Hizi ni katika Propaganda za makafiri katia kupaka matope Uislamu.
Tuchukuwe fikra ya kiakili – mtu ambaye ana kitu kimoja na haruhusiki kuwa na kingine na mtu ambaye ana vitu zaidi ya kimoja na anaruhusika kupata kingine, nani aliyekuwa rahisi kuingia katika makosa. Ukizingatia pupa ya mwanadamu wa rahisi kuingia katika makosa, ukiingia katika starehe na mali?
Jambo jengine binaadamu ana sehemu ya kupenda hiki na hiki na maumbile ya binaadamu hayako sawa, wengine wananguvu zaidi katika hali ya matamanio yao na ushamfunga hana ruhusa zaidi ya moja atafanyaje huyu? Kwa ajili hiyo Allah (S.W) akatuambia;
"Basi oeni wale waliokupendezesheni katika wanawake, wawili, watatu na wanne na mkichelea kutokufanya uadilifu basi mmoja.
Annisaa 4:3.
Kwa maana hiyo huyu Muislamu atahifadhika kutumbukia katika laana hii na huyu mwengine ambaye ana mmoja tu ambaye udhaifu wake unaeleweka kila mwezi ana ila, wakati wa ubebaji mimba mpaka kujifungua.
Uislamu ni Dini ambayo iko safi na Hekima zake hazina kiwango, tofauti na desturi au Mila na watu waliojiwekea wenyewe mbele ya Allah bila dalili. Tumche Allah enyi watu tusitafute dawa ya moto kwa moto turejee kwenye maamrisho ya Allah (S.W) na Mtume wake (S.A.W) tutaona huko dawa ya Ukimwi na Tiba yake " KINGA BORA KULIKO TUkimwi hautokingika kwa Propaganda za Uongo (za kikafiri wala kugawa Kondomu kwa kumalizia.
Tuchukue takwimu ndogo ya visiwa vyetu vya Zanzibar toka ulipoanza kugunduliwa na kugawa "kondomu salama" Ukimwi jee? Umepungua au Umeongezeka
Dawa ya Ukimwi sio kueneza Kondomu kwa Jamii sisi ni waislam, Allah (S.W) anatwambia;
"Basi waulizeni wenye utambuzi ikiwa hamuelewi – Qurani.
Huu ndio msaada wa masheikh wa kiislamu kwa wale waliotaka msaada huo na ndio mtizamo wa Uislamu katika suala zima la kuoa mke zaidi ya mmoja .
MWISHO