WEMA NA UOVU
BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
MWANADAMU BAINA YA MEMA NA MAOVU
Uislamu kama zilivyo jumbe nyingine za mbinguni, unategemea katika utengefu wake mkuu/enevu/jumla, juu ya kuilea nafsi ya mwanaadamu kabla ya kitu chochote. Ni kwa ajili hii basi, Uislamu unahusisha juhudi kubwa kwa lengo la kuingia ndani ya nafsi kupanda mafundisho yake ndani ya johari (kiini/kokwa) yake mpaka nafsi iweze kumeza dozi yake.
Na hazikudumu jumbe za Mitume na kuunda pembezoni mwake makundi ya waumini, ila ni kwa kuwa nafsi ya mwanaadamu ndio iliyo kuwa maudhui ya amali yake (hizo jumbe) na muhimili wa harakati zake. Kwani mafundisho yao (hao mitume) hayakuwa ni maganda yaliyo gandana yakaangukia kwenye nyundo ya maisha itukutikayo. Wala hayakuwa rangi zivutiazo macho ambazo hufifia kwa mpito wa siku. Hapana, hayakuwa hivyo. Hakika walichanganya misingi yao na makunjo/mageuko ya nafsi, kwa hiyo basi misingi hiyo ikawa ni kani (nguvu) inayo tawala wasiwasi wa maumbile ya kibinaadamu na kudhibiti mielekeo yake.
Na pengine mara nyingine, jumbe hizo za mbinguni zikazungumza kuhusiana na jamii na nyanja zake, utawala na aina zake na zikatoa dawa kwa maradhi yanayo zisibu pande hizi.
Pamoja na yote hayo, dini hazikuyaacha maumbile yake katika kuizingatia nafsi suluhivu/tengenevu ndio mpango bora wa utengenevu wote. Na tabia imara ndio dhamana ya kudumu ya kila ustaarabu. Na hapana katika hili, kupuuzia wala kufumbia macho kazi ya wadau wa ujenzi wa jamii na dola. Bali hilo ni dokezo la thamani ya utengenevu wa nafsi katika kuyahifadhi maisha na kuwanadisha saada walio hai.
Twendapo na nafsi tenge/pogo, hii huchochea fujo/uhovyo katika taratibu/mipango kamilifu. Na kwa upande mwingine nafsi tukufu/tengefu, huziba nyufa katika zile hali kombo na huchomoza utukufu wake kwa ndani yake. Basi huufanya mzuri utendaji na mwenendo.
Hakika kadhi/hakimu muadilifu, kwa sababu ya uadilifu wake hukamilisha/huziba mapungufu ya kanuni ambazo anazitumia katika kutoa hukumu. Ama kadhi dhaalimu, yeye huweza kuzipondosha nukuu nyoofu za kanuni. Na hivyo ndivyo ilivyo nafsi ya mwanaadamu pale inapo yaelekea mapito na fikira mbali mbali zilizomo Duniani na raghaba za maslahi.
Ni kutokea hapo, ndio utengenevu wa nafsi ukawa ni nguzo ya kwanza katika kuifanya kheri (wema) itawale katika maisha haya. Kwani nafsi zikito tengenea, ulimwengu huingia kiza na fitina zitatawala leo na mustakabali wa watu. Ni kwa ajili hiyo ndio Allah Ataadhamiaye anasema: “...HAKIKA ALLAH HABADILISHI YALIYOKO KWA WATU MPAKA WABADILI WAO YALIYOMO NAFSINI MWAO. NA ALLAH ANAPO WATAKIA WATU ADHABU HAKUNA CHA KUZUIA WALA HAWANA MLINZI YEYOTE BADALA YAKE”. [13:11]
Na anasema katika kuelezea sababu za kuhiliki kwa uma zilizo fisidika: “KAMA ADA YA WATU WA FIRAUNI NA WALIO KUWA KABLA YAO – WALIZIKATAA ISHARA (aya) ZA ALLAH. BASI ALLAH ALIWASHIKA (aliwaadhibu) KWA SABABU YA MADHAMBI YAO. NA HAKIKA ALLAH NI MWENYE NGUVU NA MKALI WA KUADHIBU. HAYO NI KWA SABABU ALLAH HABADILISHI KABISA NEEMA ALIZO WANEEMESHA WATU, MPAKA WAO WABADILISHE YALIYOMO NDANI YA NAFSI ZAO. NA HAKIKA ALLAH NI MWENYE KUSIKIA, MWENYE KUJUA”. [08:52-53]
Na Uislamu katika kuitibu kwake nafsi kwa kutaka kuitengeneza, unaitazama kwa pande mbili:
1.Kwamba ndani ya nafsi kuna umbile zuri/jema linalo kimbilia kwenye kheri na linafurahishwa kwa kuidiriki. Na linaijutia shari (uovu) na linahuzunika kutokana na kuitenda. Na huona ukunjufu wa uwepo wake na usihi wa maisha yake katika haki.
2.Na kwamba kando ya hilo, ndani ya nafsi kuna mipondoko isiyo na malengo inayo ikengeusha nafsi na njia ya sawa. Na inaipambia kutenda yale ambayo yanaitendea madhara.
Wala si muhimu kwetu hapa kuipekua mipondoko hii miovu kwa upande wa Tarekh (Historia). Ili tupate kujua, je mipondoko hii ni yenye kuzuka katika umbile la mwanaadamu au imo ndani ya umbile lake; yaani ameumbwa nayo? Lakini linalo tuhusu hapa, ni kwamba hili (umbile zuri/jema) na ile (mipondoko miovu) imo ndani ya mwanaadamu ikigombea uongozi ndani yake. Na mwisho wake umetundikwa kwenye upande ambao mtu amejisalimisha huko. Allah Atukukiaye amesema: “NA KWA NAFSI NA KWA ALIYE ITENGENEZA! KISHA AKAIFAHAMISHA UOVU WAKE NA WEMA WAKE. HAKIKA AMEFANIKIWA ALIYE ITAKASA, NA HAKIKA AMEKHASIRI ALIYE IVIZA”. [91:7-10]
Kazi/dhima ya Uislamu ni kutoa msaada timilifu na wa kutosha kwa huyu mwanaadamu ili kumuwezesha kuwa na nguvu kwa umbile lake na kwenda kwa kuufuata uongofu wake. Na kadhalika kumuwezesha kujinasua na wasi wasi wa madhambi unao mghuri na kujaribu kumpiga mweleka. Na kwa yakini Uislamu umejisifia wenyewe kwamba ni dini ya maumbile iliyo takata na kasoro/mapungufu yote haya. Allah Ataadhamiaye amesema ndani ya kitabu chake kitukufu: “BASI UELEKEZE USO WAKO SAWA SAWA KWENYE DINI – NDILO UMBILE LA ALLAH ALILO WAUMBIA WATU. HAPANA MABADILIKO KATIKA UUMBAJI WA ALLAH. HIYO NDIO DINI ILIYO NYOOKA SAWA. LAKINI WATU WENGI HAWAJUI”. [30:30]
Hakika dhima/kazi ya jicho ni kuona, muda wa kuwa halikuandamiwa na upofu. Na dhima ya sikio ni kusikia muda wa kuwa halikuandamiwa na uziwi. Na dhima ya umbile ni kwima (kusimama katika mstari nyoofu) pamoja na haki na lijipeleke kuielekea hiyo haki kwa kasi ya maji yaundeapo mteremko. Hivi ni iwapo umbile hilo halijazukiwa na kasoro zinazo zisimamisha hatamu zake na kuliondosha kwenye muelekeo wake wa mwanzo; kwenye ukamilifu, kheri na ubora.
Na vizuka fisidi umbile hivi, huenda pengine vimeundika kutokana na makapi/masalia ya karne zilizo pita au kutokana na mapokeo ya mazingira/jamii zilizo poromoka kimaadili/kiutu au kutokana na yote mawili pamoja. Masalia na mapokeo haya, yana hatari kubwa sana kwa sababu ya kasoro/maradhi yanayo liletea umbile la mwanaadamu. Na juhudi za kweli za wadau wa utengenefu zinapambana nayo (maradhi/kasoro hizo) na kuyavunja makali yake na kuliokoa umbile hilo kutoka kwenye majanga/masaibu yake. Mpaka liweze kurejea kwenye sifa asili zake na litekeleze dhima yake ya ukweli. Na Uislamu umekwisha ionyesha na kuiweka njia ya hilo.
Baada ya kuisoma katika kitabu cha Allah, aya iliyo tangulia kunukuliwa kwamba dini ndilo umbile, unaisoma sasa kauli yake Ataadhamiaye: “MUWE WENYE KUTUBIA KWAKE, NA MCHENI YEYE, NA SHIKENI SWALA, NA WALA MSIWE KATIKA WASHIRIKINA. KATIKA WALE AMBAO KWAMBA WAMEIGAWANYA DINI YAO, NA WAKAWA MAKUNDI MAKUNDI, KILA KIKUNDI KINAFURAHIA KILICHO NACHO”. [30:31-32]
Imani na si ukanaji wa kuwepo kwa Mungu, uchamngu na si uasi/uovu na umoja wa wenye kumuabudu Bwana Mlezi wao, hapana kuwafarakanisha katika huo. Nasaha hizi ndizo mlango wa kumrejesha mwanaadamu kwenye umbile lake nyoofu. Na Qur-ani Tukufu imekwisha ikariri maana hii kupitia kauli yake: “BILA YA SHAKA TUMEMUUMBA MTT KWA UMBO LILILO BORA KABISA. KISHA TUKAMRUDISHA CHINI KULIKO WALIO CHINI! LAKINI WALE WALIO AMINI NA WAKATENDA MEMA, HAO WATAPATA UJIRA USIO KWISHA”. [95:4-6]
Umbo bora kabisa hilo, ni kule kuijua haki na kushikamana nayo na kwenda kwa muktadha wake. Ni kuwa na shauku ya kufikia ubora na utukufu na kuvichunga viwili hivyo katika eneo la mtu na nafsi yake, na mtu pamoja na watu. Ni kuutangaza ukamilifu katika mfumo wake wa juu na kuufanya ghali kuliko kila kitu katika maisha haya. Hata hivyo, bado watu wengi wanazuiwa na matamanio nafsi yao kukifikia kiwango hiki kitukufu, kwa hivyo hubweteka katika ardhi. Kisha matamanio fuatwa yao huwafanya kuasi na hapo ndipo huporomoka kwa kasi kuelekea mahala pa mbali. Na huko ndiko chini kuliko walio chini ambako Allah atawarudisha huko. Huu mrudisho wa kimngu unakubaliana na taratibu/kanuni za uongofu na upotofu nazo ni kanuni makini adilifu, Qur-ani Tukufu imezitaja katika kauli yake: “NA HAIWI KWA ALLAH KUWAHISABU WATU KUWA WAMEPOTEA BAADA YA KWISHA WAONGOZA MPAKA AWABAINISHIE YA KUJIEPUSHA NAYO. HAKIKA ALLAH NI MWENYE KUJUA KILA KITU”. [09:115]
Na kauli yake: “NITAWATENGA NA ISHARA (aya) ZANGU WALE WANAO FANYA KIBURI KATIKA NCHI BILA YA HAKI. NA WAO WAKIONA KILA ISHARA HAWAIAMINI. WAKIIONA NJIA YA UWONGOFU HAWAISHIKI (hawaifuati) KUWA NDIO NJIA; LAKINI WAKIIONA NJIA YA UPOTOFU WANAISHIKA KUWA NDIO NJIA. HAYO NI KWA SABABU WAMEZIKANUSHA ISHARA ZETU, NA WAMEGHAFILIKA NAZO”. [07:146]
Na nani ambaye atakaye salikia kwenye umbile lake lililo bora kabisa na akaokoka kuporomokea kwenye Dunia duni? Jibu la swali hili liko katika aya: “...ILA WALE WALIO AMINI NA WAKATENDA MEMA...” [95:06]
Tayari umekwisha jua kwamba tabia njema, ni tunda lenye ujirani na imani ya wazi na amali njema.
MWISHO