UGHAIBU (KUTOWEKA) KWA IMAMU (A.S)
UGHAIBU (KUTOWEKA) KWA IMAMU (A.S)
Muda wa kazi yake ya Uimamu umegawanyika katika sehemu mbili za Ughaibu. Moja inaitwa "Ghaibat-Sughra" (Ughaibu mfupi) na nyengine inaitwa "Ghaibati-i-Kubra" (Ughaibu mrefu). Yote hayo yamebashiriwa na dhuria wa Mtume (s.a.w.), kwa mfano:
(i) Mtume (s.a.w.) amesema, "Yeye ataendelea katika ughaibu mrefu wakati watu wengi wataingia katika kiza".
(ii) "Katika muda wa ughaibu wake, wale watakuobakia katika kuamini watakuwa wachache kama kibiriti".
(iii) Ali (a.s.) alisema, "Wa mwisho wetu sisi atakuwa ghaibu kwa muda mrefu. Ninaona jinsi wakati ule marafiki zetu watakavyohangaika kama ng'ombe wafanyavyo wanapotafuta chakula.
(iv) Mahala pengine Imamu Ali (a.s.) anasema, "Atadhihirika baada ya muda mrefu sana usiotambulika, wakati ambapo wenye imani ya kweli ndio watakaoweza kubakia na imani.

(v) lmamu Hasan (a.s.) amesema, "Allah atampa umri mrefu wakati wa kutokuwepo kwake".
(vi) Vile vile lmamu Husain (a.s.) na Imamu Baqir (a.s.) wamesema kwamba, "Muda wa ughaibu wake utakuwa mrefu wakati ambapo wengi watapotea".
(vii) Imamu Jaffar Sadiq (a.s.) amesema, "Mahdi atakuwa wa tano katika kizazi cha mtoto wangu, na ataendelea kufichika kutoka machoni mwenu."
(viii;) Mahala pengine lmamu Jaafar (a.s.) anasema, "katika zama za kutoonekana (Imam Mahdi) (a.s) ni lazima waumini wote wanaoamini wabaki katika njia yao ya unyofu na dini."
(ix) Imamu Musa Kadhim (a.s.) amesema, "Uso wake utaondoshwa mbele ya macho ya watu lakini jina litaendelea kukumbukwa na kubakia katika nyoyo za wanaoamini. Yeye atakuwa wa kumi na mbili wetu.''
(x) Imamu Ridha (a.s.) amesema, "Atakuwa anangojewa wakati wa kutokuwepo kwake".
(xi) Imamu Muhammad Taqi (a.s.) amesema, “Mahdi atangojewa wakati wa kutokuwepo kwake, na atakapodhihirika ni lazima atiiwe".
(xii) Imamu Ali Naqi (a.s.) amesema, "Wengi watasema kuhusu "Sahibul-Amr" kwamba hajazaliwa bado".
(xiii) Imamu Hasan Askari (a.s.) amesema, "Kutoweka kwa mtoto wangu kutakuwa kiasi ambacho wote watakuwa na shaka isipokuwa wale tu waliorehemewa na Mwenyezi Mungu."
(xiv) Vile vile Imamu Muhammad (a.s.) amesema, "Wa mwisho katika sisi atakuwa na vipindi viwili vya ughaibu; mmoja utakuwa mrefu na mwingine utakuwa mfupi".
(xv) Pia Imamu Jaafar Sadiq (a.s.) amesema, "kipindi kimoja (cha ughaibu) kitakuwa kirefu zaidi kuliko kingine".
Kuwa na elimu ya hadithi hizi zote na ubashiri kuliwaokoa wale walioamini katika kutokuwa na shaka yo yote kuhusu Imamu huyu baada ya Imamu Hasan Askari (a.s.), na hawakumkubali mdai hayo
MWISHO