VIAPO NDANI YA QUR-ANI
BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
VIAPO NDANI YA QUR-ANI
Kiapo ni sisitizo, na hutumiwa ili kuonesha umuhimu wa maudhui yanayotaka kuliwa kiapo, Kiapo kinatumiwa katika mambo ambayo ni muhimu sana ambayo yanahitajiwa kusisitizwa, (kusudio la sisitizo ni sisitizo liongezwalo kusisitizwa zaidi ya mara moja). Kiasi ya kwamba kutokana na kuwa haitoshelezi kutumia njia zitakazoweza kuthibitisha usisitizo wa jambo hilo, ndio hutumia kiapo ili kulithibitisha.
Ndani ya Qur-ani pia kumetumiwa njia za kiapo kama vile walivyokuwa wakitumia WaarabuHapo mwanzo tulielezea kuwa kiapo hutumika kwa kile kitu ambacho ni muhimu sana, kiasi ya kwamba huwafanya wasikilizaji wa kiapo hicho kuwa makini na kuzingatia ni kitu gani muhimu kilichopelekea kuliwa kiapo, kwa hiyo kwa hakika kiapo ni kitu kilicho thabiti kinachowapelekea watu kukubali bila ya kuwa na shaka na lile jambo au tokeo lililotokea ambalo limesababishia kuliwa kiapo. (yaani kwa kuthibitishwa na kukubaliwa na watu wote kile kitu ambacho kimeliwa kiapo yaani kwa lugha ya kiarabu wanasema (مقسم به), vile vile huthibitishwa na kukubaliwa na watu wote kile kitu ambacho kimesababisha kuliwa kiapo, (مقسم عليه)
NYENZO ZINAZOTUMIKA KATIKA KIAPO
Nyenzo zinazotumika katika kiapo ni hizi zifuatazo
. (مقسم به) 1-ni kile kitu ambacho huliwa kiapo. Yaani ni yale majina ambayo hutumiwa na wanaadamu kwa ajili ya kiapo hicho. Majina hayo ) ) yaaniمقسم به) ni katika sifa za dhati za Mwenyeezi Mungu, na baadhi ya wakati wanaadamu ili kuonyesha umuhimu au ukweli wa jambo hula kiapo hata kwa nafsi na nyoyo zao, au kwa nafsi za watu wengine, ama kiapo ambacho kinaleta athari za kisheria ni kula kiapo kwa kutumia sifa za dhati za Mwenyeezi Mungu. (kuna athari za aina mbili, athari nzuri na (athari mbaya.
(مقسم عليه) 2- yaani kile kitu ambacho kimesababisha kuliwa kiapo
- Kila amri au jambo muhimu ambalo linahitajika kusisitizwa - , na kwa sababu ya jambo hilo mtu hula kiapo
. (حرف قسم), 3- ni herufi ambazo hutumika katika kula kiapo, herufi hizo katika lugha ya Kiarabu ni hizi zifuatazo
(باء, تاء, واو, لام), herufi (واو, تاء, na لام), zimetajwa ndani ya Qur-ani, ama herufi (باء), ambayo ndiyo herufi asili inayotumika katika kula kiapo haijatajwa ndani ya Qur-ani (حرف جواب قسم), 1- ni herufi ambazo hutumika au (huja) katika jawabu ya kiapo, na zinaweka wazi lile jambo ambalo limesababisha kuliwa kiapo yaani (مقسم عليه), herufi hizo ni hizi zifuatazo
(لام مفتوحه, ان مشدد مكسوره,لا نافيه,ما نافيه,ان مخففه نافيه)
AINA ZA VIAPO NDANI YA QUR-ANI
Viapo vilivyotajwa ndani ya Qur-ani vimegawika katika sehemu tatu, nazo ni hizi zifuatazo
(قسم صريح)
1- VIAPO VINAVYOONEKANA WAZI (KWA LUGHA YA KIARABU WANASEMA
Viapi hivyo vilivyo wazi, ni viapo ambavyo huapwa kwa kutumia nyenzo zinazotumika katika kula kiapo, nyenzo hizo huonekanwa kwa uwazi kabisa, yaani mwanzo huanzwa kwa herufi ya kiapo, yaani (حرف قسم) baadaye huja (مقسم به), yaani lile jambo ambalo huliwa kiapo, na mwisho huja (مقسم عليه), yaani lile jambo ambalo limesababisha kuliwa kiapo. Viapo vingi vilivyokuja ndani ya Qur-ani ni aina ya viapo hivyo vilivyokuja kwa uwazi
Aina hiyo ya viapo katika Qur-ani imekuja ndani ya sura 29, katika sehemu 81. (Viapo vya aina hiyo kwa utaratibu vimo katika sura hizi zifuatazo:
Suratun-Nisaa Aya ya 85, Al-an-am aya ya 23 na 30, Yunus Aya ya 53, Yussuf Aya ya 73, 85, 91 na 95, Hijri aya ya 72 na 92, Nahli Aya ya 56 na 63, Anbiyaa Aya ya 57, Shuaraa Aya ya 97, Yaasin Aya ya 1-3, Saafaat Aya ya 1-4, Sad Aya ya 1, Dukhan Aya ya 1-3, Qaf Aya ya 1, Azaariyaat Aya ya 1-6, 7, 8, na Aya ya 23, Turi Aya ya 1-7, Najmi Aya ya 1 na 2, Qalam Aya ya 1 na 2, Mudathir Aya ya 32-35, Mursalati Aya ya 1-7, Naaziati Aya ya 1-6, Buruji Aya ya 1-4, Tariq Aya ya 1-4, Fajri aya ya 1- 5, Shamsi Aya ya 1-9, Layl Aya ya 1-4, Dhuha Aya ya 1-3, tiyni Aya ya 1-5, Adiyaati Aya ya 1-6, Asri Aya ya 1 na 2,[1] Katika sehemu hii tutatosheleza kwa kutaja mifano ya aina tatu zifuatazo
Allah (s.w) katika Suratul-Qalam Aya ya 1-2 anasema
ن وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ
مَا اَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ
Maana ya Aya hizo ni kama ifuatavyo
Nuun. (Naapa kwa) kalamu na yale wayaandikayo (kwa kalamu hizo)
Kwa neema ya Mola wako wewe si mwendawazimu. (Makafiri wakimwambia Mtume – kwa ajili ya kumtukana tu – kuwa yeye ni mwendawazimu)
Katika Aya ya mwanzo ya sura hiyo (واو) liyoko katika neno (وَالْقَلَمِ), ni herufi qasam (herufi inayotumika kwa ajili ya kula kiapo)
Na katika Surat Yussuf Aya ya 73 anasema
قَالُواْ تَاللهِ لَقَدْ عَلِمْتُم مَّا جِئْنَا لِنُفْسِدَ فِى الاَرْضِ وَمَا كُنَّا سَارِقِينَ
Maana ya Aya hiyo ni kama hivi ifuatavyo
Wakasema:- “Basi malipo yake yatakuwa nini kama nyinyi mnasema uwongo
Katika Aya hiyo ya 73 ya Surat Yussuf (تاء), inayoonekana katika neno (تَاللهِ), ni harfi qasam (herufi inayotumika kwa jili ya kula kiapo)
Katika Suratul-Hijri Aya ya 72 anasema
لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِى سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ[2]
Maana ya Aya hiyo ni kama ifuatavyo
Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao (wa maovu) wanahangaika ovyo.
Katika Aya hiyo ya 72 ya Suratul-Hijri kiapo kimetumika kwa ajili ya nafsi za Mitume ya Mwenyeezi Mungu
VIAPO VILIVYOKUJA NA HERUFI ZA KUKATAA
Katika Qur-ani kuna baadhi ya Aya Mwenyeezi Mungu amekula kiapo kwa kutumia (حرف منفي), yaani herufi zinazotumika kwa ajili ya kukataa, kwa mfano katika Suratul-Qiyama Aya ya 1, Allah (s.w) anasema
لاَ اُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ
Maana ya Aya hiyo ni kama ifuatavyo
Naapa kwa siku ya KiamaWafasiri wengi wamesema kuwa (حرف نفي لا) -yaani herufi inayomaanisha kukataa katika aina ya viapo hivyo vilivyokuja na herufi ya kukataa (inajulikana ni herufi iliyozidi, hii ni kutokana na kanuni za elimu ya Nahwu) na ili kuitafsiri aya hiyo kwa maana sahihi ni lazima tujaalie kuwa herufi hiyo imefutwa (yaani haipo). Kwa mfano katika Suratul-Waqia Aya 75 Allah (s.w) anasema
فَلاَ اُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ
Maana ya Aya hiyo ni kama hivi ifuatavyo
Basi Ninaapa kwa maanguko ya nyota
Herufi (لا), inayoonekana katika neno (فَلاَ), ni (لا) iliyozidi, ama uhakika na ukweli unavyoonekana katika Aya hizo, haimaanishi kuwa herufi hiyo ya (لا), imezidi, kama tulivyosema hapo mwanzo (kuwa tunajaalia tu kuwa imezidi), - kwani hayo ni maneno ya Mwenyeezi Mungu na kila herufi, neno, Aya n.k yana hikima zake – (kwa hiyo katika mifano ya aina kama hiyo ambayo Mwenyeezi Mungu hula kiapo kwa kutumia herufi zinazomaanisha kukataa), kwa hakika Mwenyeezi Mungu anataka kutuonesha ukubwa na umuhimu wa kiapo hicho. Kwa mfano katika Sura hiyo hiyo (Al-Waqiah) Aya ya 75 na 76 Allah (s.w) anasema
فَلاَ اُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ
وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ
Maana ya Aya hizo ni kama hivi ifuatavyo
Basi Ninaapa kwa maanguko ya nyota
Na hakika hicho bila ya shaka ni kiapo kikubwa, laiti mngalijua!
Kama tutaifasiri maana ya (لا), inayoonekana katika Aya ya mwanzo, Aya hiyo italeta maana hii, “Na siapi kwa maanguko ya nyota”basi hiyo sio maana sahihi, na maana sahihi ni (Basi ninaapa kwa maanguko ya nyota)
Basi ufahamu unaopatikana katika Aya hiyo ni huu: kulipa ukubwa lile jambo ambalo linaliwa kiapo (مقسم به), (yaani nyota), kwa kutumia kiapo, ni kama kulipa udogo jambo hilo, (yaani nyota sio kitu kikubwa), katika hali ambayo nyota ni kitu kikubwa sana, na kutokana na ukubwa wake hata zikaliwa kiapo hazilingani na kiapo hicho, yaani (nyota zina utukufu mkubwa zaidi kuliko kiapo). Na kwa sababu hiyo basi herufi (لا), imekuja na maana ya kukataa ili kufahamika ukubwa na utukufu wa nyota hizo. (rejea Tafsiri Kashaaf, juzuu ya 4, ukurasa wa 657-659)
Adadi ya viapo vinavyokataa ndani ya Qur-ani vimekuja katika aina 15, ambavyo vimekusanyika katika sura sita, na vimetajwa na (kuzikirishwa ndani ya Kitabu cha Elimu ya Qur-ani, ukurasa wa 299)
3. VIAPO VILIVYOKUJA KATIKA HALI YA MAFICHO
Katika Qur-ani kuna viapo vilivyokuja katika sentensi moja, na kuna viapo vilivyokuja katika sentensi mbili, viapo vilivyokuja katika sentensi mbili kwa kawaida hufuatiliwa na herufi ya lamu, herufi hiyo huja baada ya kiapo hicho ili kutilia mkazo na kusisitiza umuhimu wa kiapo hicho. (yaani herufi hiyo inamaanisha jawabu ya kiapo hicho). Herufi hiyo ya (لام) katika Lugha ya kiarabu inajulikana kwa jina la lamu muataa (لام موطئه)
Kabla ya kuingia katika maudhui ya viapo hivyo vilivyojificha kuna ulazima wa kuifahamu herufi hiyo ya (لام موطئه), - Yaani ni lamu inayokuja katika jawabu ya kiapo ili kulitilia mkazo lile jambo ambalo linaapiwa.
Kutokana na maandishi ya Ibni Hisham baadhi ya wakati inapokuja herufi moja wapo katika herufi za sharti hufuatiwa na herufi hiyo ya (لام) ili kuyafafanua maneno yanayoendelea katika sentensi hiyo ya kuwa ni jawabu ya kiapo na sio vipengele vya vinavyomaanisha jawabu ya sharti, (rejea Mughni Labiyb, ukurasa wa 122). Kwa mfano (والله لئن اتيتني لاتينك) (لام), ambayo inaonekana kabla ya herufi (ان), ni katika herufi za sharti ni (لام موطئه), na (لام) hiyo imeitwa (لام موطئه), -ikiwa na maana ya (ممهدة), au (مؤذنة), au (مشعرة), - kwa sababu jawabu iliyokuja katika mfano huu yaani (لاتينك), ni kwa ajili ya kiapo cha (والله), ili isibabaishike na jawabu ya sharti. (kutokana na kanuni za elimu ya nahwu, wakati wowote itakapokuja lamu muwti-a kabla ya herufi sharti, basi jawabu ya herufi ya sharti hiyo ni lazima ifutwe:
Baadhi ya wakati kiapo hicho – ambacho hutokea kabla ya herufi sharti – huwa mafichoni, (hakionekani), basi viapo vya aina kama hiyo ndani ya Qur-ani ni vingi sana. Kwa mfano Allah (s.w) katika (Suratul-Hashr Aya ya 12) anasema
لَئِنْ اُخْرِجُوا لاَ يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ وَلَئِن قُوتِلُوا لاَ يَنصُرُونَهُمْ وَلَئِن نَّصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ الاَدْبَارَ ثُمَّ لاَ يُنصَرُونَ[3]
Maana ya Aya hiyo ni kama hivi ifuatavyo
Kama wakifukuzwa hawatatoka pamoja nao, na kama wakipigwa hawatawasaidia; na kama wakiwasaidia kwa yakini watageuza migongo (wende mbio); kisha hawatanusuriwa.
- (لَئِنْ اُخْرِجُوا لاَ يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ ْ), (وَلَئِن قُوتِلُوا لاَ يَنصُرُونَهُمْ), (وَلَئِن نَّصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ الاَدْبَارَ
ثُمَّ لاَ يُنصَرُونَ)
Katika sentensi zote tatu hizo yaani
zinazoonekana ndani ya Aya hiyo, (مقسم به), yaani – lile jambo au neno ambalo limeliwa kiapo -, neno (والله), ambalo lipo kabla ya neno (لَئِنْ) halionekani na limejificha, aina hiyo ya viapo huitwa viapo vilivyojificha na katika Qur-ani viapo vya aina hiyo vimeainishwa katika sehemu 61, ambavyo vinaonesha (لام موطئه), imekuja na kiapo kilicho mafichoni (kisichoonekana). – yaani neno (والله), ambalo ndio kiapo halionekani katika Aya hiyo. Natuangalie mfano huu ufuatao, Allah (s.w) katika Suratul- Tawba Aya ya 75 anasema
وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللّهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ
Maana ya Aya hiyo ni kama hivi ifuatavyoNa miongoni mwao (hao wanafiki) wako waliomuahidi Mwenyeezi Mungu kuwa: “Akitupa katika fadhila zake tutatoa sadaqa na tutakuwa miongoni mwa watendao mema”
Katika Aya hiyo neno (عَاهَدَ), katika ibara (لَئِنْ آتَانَا), neno (والله) halionekani na liko mafichoni.
Baadhi ya wakati viapo hivyo vilivyojificha huonekana bila ya kuja (لام موطئه). Kwa mfano: Allah (s.w) katika Suratul-An-am Aya ya 121 anasema
وَلاَ تَاْكُلُواْ مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَي اَوْلِيَآئِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ وَإِنْ اَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ
Maana ya Aya hiyo ni kama ifuatavyo
Wala msile katika wale wasiosomewa jina la Mwenyeezi Mungu (yaani vilivyokufa wenyewe), maana (kula) huko ni uasi. Na kwa yakini mashetani wanawafunulia marafiki zao kubishana nanyi (katika mambo namna haya yasiyokuwa na maana). Na kama mkiwatii, mtakuwa washirikina
وَإِنْ اَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ
neno (والله) katika Aya hiyo halionekani, na ilikuwa ni jawabu. (إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ)
[1] (rejea kitabu cha Elimu ya Qur-ani, intisharati Tamhiydiy wa simat, ukurasa wa 297 na 298)
[2] (Suratul-Hijri Aya ya 72)
[3] (Suratul-Hashr Aya ya 12)
MWISHO