Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAKALA MBALIMBALI

MAMBO MUHIMU KWA ATAFUTAYE ELIMU

MAMBO MUHIMU KWA ATAFUTAYE ELIMU

MAMBO MUHIMU KWA ATAFUTAYE ELIMU " Mtu anayepaswa kutafuta elimu ni lazima, hatua ya kwanza kabisa, apitie utakaso wa kiroho, aingize taqwa (uchaji Mungu) ndani ya roho yake, aondoshe nia mabaya na malengo ya kidunia, na kujipima mara kwa mara kuangalia iwapo elimu yake anaitafuta kwa ajili malengo ya kidunia. Mtu ni lazima akumbuke kwamba kumcha Mungu ni sifa maalum ya 'alim (mwanachuoni) na yeyote asiye kuwa na ucha Mungu huyo yuko nje ya daraja za wenye elimu, hata akiwa amehifadhi vitu vingi moyoni au awe anavutia anapozungumza. " Katika kila hatua ya kutafuta elimu, ni lazima ufikiri kwa undani sana kuhusu lengo lako la msingi la kutafuta elimu. Jiulize: kwa nini natafuta elimu? Je ni kwa ajili ya kupata kazi nzuri, au kushindana na mwenzio au na kikundi, au kupata tuzo, shahada au nafasi kubwa katika jamii? Ikiwa unatafuta elimu ya juu, je waitafuta kwa ajili tu ya kuandika vitabu, nakala, au kutoa hotuba ili usifiwe kuwa ni mwanamume au mwanamke msomi? Au kwa sababu ya kumridhisha Mungu na kuwatumikia waja wake? " Elimu uipatayo ni lazima ikuongoze uwe mwema zaidi, ufanye vitendo vya uaminifu na ikufanye umpende na kumcha Mungu zaidi wakati ukiendelea. Elimu isiyomuongoza mtu kufanya mambo mema, hiyo si elimu ya kweli. Elimu inayoishia kwenye maneno tu na haina vitendo vyenye kuwatumikia viumbe wa Mwenyezi Mungu hiyo ni elimu duni sana na itatoweka na wakati.

Ufafanuzi

USHAURI WA KUTIBU HASIRA

USHAURI WA KUTIBU HASIRA USHAURI WA KUTIBU HASIRA Mtu mwenye tabia ya kuasirika mara kwa mara ni lazima ajue kwamba hasira ni uwezo aliopewa na Mwenyezi Mungu mtukufu kwa ajili ya kulinda, na kuwapo kwa wanaadamu, na kwa ajili ya kuwa na nidhamu, utaratibu wa kifamilia, kulinda haki za binadamu na sharia za Mungu. Iwapo mwanaadamu atakwenda kinyume na lengo hili la Mwenyezi Mungu na kutumia nguvu ya hasira dhidi ya mpango wa Mwenyezi Mungu, itakuwa ni kukiuka uaminifu ambapo kutastahili adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ni ujinga na dhulma iliyoje kwa kutofanya uaminifu na kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu! Kwa hivyo mtu ni lazima afikirie sana juu ya matendo maovu na ya kikatili yanayosababishwa na hasira, na kujaribu kuondoa yanayosababishwa na uovu, kila moja katika hayo yanayoweza kumsababishia matatizo mtu milele, hapa duniani na adhabu kesho Akhera. " Moja katika dawa ya hasira ni kujiepusha na sababu zinazoileta. Miongoni mwazo ni ubinafsi, unaofanya kupenda utajiri, ukuu, heshima, tamaa ya mtu kulazimisha apate matakwa yake na kupenda kupanua nguvu ya utawala wake kwa viumbe wa Mwenyezi Mungu. Mambo haya kwa kawaida yanachochea moto wa hasira, ambapo wale watu wanaokuwa nayo hupenda kuyatukuza mno. Mtu anapoyapenda mambo haya, huwa ni rahisi kughadhibika ikiwa moja kati ya malengo yake hayajatekelezwa. Sababu nyingine inayoichochea, ni kuwa mara nyingine hasira huchukuliwa kuwa ni sifa na hivyo kuonekana kama ni ushujaa kutokana na kutofahamu kwa mtu. Kwa hivyo hasira ni natija ya udhaifu wa kiroho. Upungufu wa imani, na kutokuwa na tabia na moyo mwema.

Ufafanuzi

HEKIMA ZA NABII YUUSUF(A.S)

HEKIMA ZA  NABII YUUSUF(A.S) HEKIMA ZA  NABII YUUSUF (A.S) ACHENI KATIKA MASHUKE YAKE Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema, " Yussuf! Ewe mkweli ! Tueleze hakika ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba dhaifu. Na mashuke saba mabichi na mengine yamekauka, ili nirejee kwa watu wapate kujua. Akasema: " Mtalima miaka saba mfululizo kwa juhudi (yaani limeni miaka saba kwa juhudi, kwani itaingia njaa kubwa baada ya miaka saba). Na mtakavyovivuna, viacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mnavyokula (ili mnavyoviacha mule miaka ya njaa itakayokuja.) Kisha inakuja baadaye miaka saba ya shida itakayokula vile mlivyoipa (yaani watu watakula ile akiba mliyoiweka) isipokuwa kidogo mtakachohifadhi (kwa ajili ya kupandia). Kisha baada ya haya, utakuja mwaka huo watu watasaidiwa na (Mwenyezi Mungu); na katika huo watakamua (vya kukamua)."

Ufafanuzi

UHURU WA MAWAZO

UHURU WA MAWAZO UHURU WA MAWAZO M/Mungu kamkirimu Binadamu, na kamzawadia akili iliyomtofautisha na viumbe wengine, ili awe na nguvu na uwezo wa kuvitawala viumbe wengine na kujenga nchi.Qur-an Al- Israa 70, inasema "Kwa hakika tumemkirimu mwanadamu, na tumempa uwezo wa kuvumbua vitu vya kumbeba baharini na nchi kavu (na anga) na tukamboresha sana juu ya viumbe wengi tuliowaumba." Uislamu unazingatia kutafakari na kutumia akili kwa ajili ya uvumbuzi na ugunduzi ni jambo la faradhi au la wajibu.Qur-an surat Qat 6-8 inasema "Je hawaangalii mbingu ilioko juu yao, na kutafakari namana tulivyoiumba na kuipamba. wala haina nyufa? na ardhi tumeitandika na kuitia humo milima, na tukatesha aina mbalimbali za mimea? hilo ni kwa ajii ya kuona na kukumbuka kwa kila mja mwenye kutubia na kurejea kwa Mola wake." Uislamu haukubali wafuasi wake kukaa ovyo na kuiga rai na utamaduni wa watu wengine bila utambuzi.Qur-an sruat Al-baqara 166, inasema "Kumbuka siku (kiyama) amabayo viongozi watakapo wasuta wafuasi wao, wataiona adhabu na mahusiano yao yatakatika .Wafuasi watasema tunatamani lau kama tutarudi duniani nasi tukawasuta kama walivyotusuta. Hivyo ndivyo M/Mungu anavyo waonesha matendo yao kuwa ni majuto juu yao, na hawatatoka motoni" Hivyo basi kumuiga na kumfuata mtu kama kipofu katika kila kitu ni majuto siku ya kiyama. Kumuiga mtu katika kila jambo kama kipofu ni ishara ya udhaifu na unyonge, na Mwenyezi Mungu anampenda muumini mwenye nguvu.

Ufafanuzi

MASHARTI YA UONGOZI

MASHARTI YA UONGOZI MASHARTI YA UONGOZI Maarifa ya sheria na uadilifu katika mtazamo wa Waislamu ni sharti na nguzo muhimu. Masuala mengine hayaingilii wala hayana udharura katika suala la uimamu. Kwa mfano elimu kuhusu Malaika, na utambuzi wa sifa za Mola Muumba haviingiliani na suala la uimamu. Kama ambavyo anayejua elimu zote za sayansi asilia (bayolojia, kemia na fizikia) na kuvumbua nguvu zote za maumbile, au mtaalamu wa muziki hastahiki kuwa khalifa wala haweza kutangulizwa mbele ya mtambuzi wa sheria za Kiislamu na muadilifu kwa ajili ya kuongoza serikali. Suala linaluhusiana na ukhalifa (uongozi wa Waislamu baada ya Mtume saw) na ambalo lilijadiliwa na kuzungumziwa katika zama za Mtume Muhammad (saw) na Maimamu wetu (as) na halikutiliwa shaka baina ya Waislamu ni kuwa, awali mtawala na khalifa anapaswa kuwa mjuzi wa sheria za Kiislamu, yaani mtaalamu wa sheria. Pili anapaswa kuwa muadilifu na mkamilifu katika itikadi na masuala ya kimaadili. Akili ya mwanadamu pia inahukumu hivyo, kwani serikali ya Kiislamu ni serikali ya sheria na kanuni na si ya kidhalimu au utawala wa watu juu ya watu wengine. Iwapo mtawala hajui masuala ya sheria hastahiki kutawala; kwani kama atakalidi, basi serikali itapoteza uwezo na haiba yake, na iwapo hatakalidi hawezi kuwa mtawala na mtekelezaji wa sheria za Kiislamu. Vilevile imethibiti kwamba "wanazuoni wa fiqhi ni wakuu wa watawala"(2) (kwa maana kwamba watawala Waislamu wanapaswa kuwafuata wanazuoni wa fiqhi na kuwauliza sheria na kisha kuzitekeleza. Wakati huo watawala halisi watakuwa ni wanazuoni wa fiqhi na sheria za Kiislamu. Hivyo basi, mamlaka yanapaswa kushikwa rasmi na wasomi wa fiqhi na si watu ambao wanalazimika kuwafuata wasomi hao kwa sababu ya kutojua sheria.

Ufafanuzi

UHUSIANO ULIOPO BAINA YA HAKI NA DINI

UHUSIANO ULIOPO BAINA YA HAKI NA DINI UTANGULIZI Kwa jina la Muumba wa Mbigu na Ardhi na Viumbe wote. Ninamshukuru Muumba Mkamilifu kwa kunipa uwezo wa kuandika Makala hii, kwani mara nyingi ninapotaka kushika kalamu na kuandika kitu fulani, huwa ninapatwa na uvivu wa kufanya hivyo kwa kukhofia mambo mbali mbali, lakini leo Mola Mtukufu amenipa uwezo wa kuandika Makala hii ambayo iko mbele yenu. Makala hii iegawika katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza inazungumzia masuala ya Haki na Dini pamoja na tofauti za kimaana zilizomo katika vitu viwili hivi, na sehemu ya pili ya Makala hii itazungumzia zaidi upande wa Haki pamoja na kugusia aina mbali mbali za Haki, ili kuweza kupata tafsiri sahihi ya neno hilo. Ifuatayo basi ni sehemu ya kwaza ya Makala hii. Sehumu hii ya kwanza ya Makala hii, ina dhamira ya kutoa changamoto kwa wale wote wapendao Haki, kwani Haki ndiyo ufunguo pekee wa mafanikio ya Wanaadamu. Hakuna jamii katika Ulimwengu huu isiyo furahia Haki, au hata kutangaza vita dhidi ya wapinga Haki. Lakini bila ya mtu kujifahamu pamoja na kuielewa nafasi aliyonayo katika jamii anayoishi, huwa ni vigumu kuweza kuifahamu Haki yake. Wengi leo katika jamii mbali mbali huwa ni wenye kugombea nyadhifa tofauti kwa kudhania kuwa wao ndiyo wenye kustahiki nyadhifa hizo, laiti wanajamii wangaliweza kuwafahamu watu hao kiundani zaidi, basi wangaliweza kuelewa kuwa, ni nani mwenye Haki zaidi ya kupewa nyadhifa hizo. Ni mara chache mno kuweza kupatikana jamii isiyo na baadhi ya viongozi wadanganyifu, lakini tatizo huwa haliko kwa viongozi hao, bali tatizo huwa liko kwenye upanda waliyowachagua viongozi hao.

Ufafanuzi

UMOJA NI JAMBO LA DHARURA

UMOJA NI JAMBO LA DHARURA UMOJA NI JAMBO LA DHARURA Profesa Burhanu Deen Rabbani, Rais wa zamani wa Afghanistan amesema katika kikao cha 23 cha kimataifa cha Umoja wa Kiislamu mjini Tehran kwamba, umoja katika umma wa Kiislamu si tu kwamba ni wadhifa bali ni jambo la dharura na hitajio muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu. Akizungumza hapo siku ya Jumanne katika kikao cha ufunguzi wa mkutano huo muhimu wa kimataifa, Bwana Rabbani amemshukuru Ayatullah Ali Taskhiri, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kudumisha na kuimarisha umoja miongoni mwa Waislamu. Rais huyo wa zamani wa Afghanista amesema kuwa nguzo za Uislamu zimesimama juu ya msingi wa umoja katika umma wa Kiislamu na kwamba Uislamu unauchukulia umoja kuwa msingi muhimu sio kwa ajili ya Waislamu tu bali kwa ajili ya jamii nzima ya mwanadamu. Amesema jambo hilo ndilo limeleta saada na msisimuko maalumu kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu katika kipindi chote cha historia. Rabbani ameongeza kuwa, tunaporejea historia tunatambua wazi kwamba Mtume Mtukufu (SAW)N mwanzoni mwa kuasisi serikali ya Kiislamu katika mji mtakatifu wa Madina kwa uungaji mkono wa Waislamu na Mayahudi, aliwapa wote haki sawa za kiraia na hivyo kusisitiza juu ya msingi wa umoja.

Ufafanuzi

QUDSI

QUDSI QUDSI Viongozi wa makundi ya mapambano ya Palestina wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ali Khamenei katika uzinduzi wa kongamano la Mshikamano wa Kitaifa na Kiislamu kwa Ajili ya Mustakbali wa Palestina. Ayatullah Ali Khamenei amesema katika mkutano huo kwamba Palestina na Quds Tukufu utarejea katika mikono ya umma wa Kiislamu chini ya kivuli cha mapambano, kusimama kidete na jihadi, na hatima ya utawala ghasibu wa Israel itakuwa ni kushindwa na kutoweka. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza mapambano ya kishujaa ya taifa la Palestina na wananchi wa Ukanda wa Gaza na akasema: "Hapana shaka kwamba Palestina itakombolewa chini ya kivuli cha kudumishwa mapambano ya taifa la Palestina, umoja wa makundi ya mapambano ya jihadi, imani na kumtegemea Mwenyezi Mungu; na waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni hawatapata lolote ghairi ya fedheha na jina baya katika historia. Amesema kuwa kusimama kidete kwa wananchi wa Palestina hususan huko Gaza ni jambo la kustaajabisha na linalotia nguvu na kuimarisha misimamo ya Wapalestina. Amelishukuru mno taifa la Palestina na akasema: "Kustahamili masaibu na mashinikizo yasiyokuwa na kikomo huko Gaza na katika ardhi yote ya Palestina ni jambo lisolowezekana bila ya hidaya na msaada wa Mwenyezi Mungu, na taifa la Palestina linastahili kupewa lakabu ya 'taifa shujaa kuliko yote katika historia'.

Ufafanuzi

UMOJA WA KIISLAMU

UMOJA WA KIISLAMU UMOJA WA KIISLAMU Baada ya kutekwa ardhi za Palestina na Uingereza pamoja na Wazayuni katika miaka ya baada ya Vita vya Kwanza na Pili vya Dunia, na kufuatia kushindwa kijeshi nchi za Kiarabu na utawala ghasibu wa Israel, wasiwasi wa kutekwa na kudhibitiwa nchi hizo na utawala huo uliongezeka maradufu. Kwa msingi huo suala la kuimarishwa umoja kati ya madhehebu ya Kiislamu liliwasilishwa na wanazuoni wa Kiislamu kuwa moja ya njia za kukabiliana na hatari hiyo ya Wazayuni. Kutokana na kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar katika zama hizo ndicho kilichokuwa kituo mashuhuri cha elimu ya kidini na pia cha zamani zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu, kilikuwa cha kwanza kutoa wito wa kuwepo umoja miongoni mwa Waislamu ili kukabiliana na hatari ya Wazayuni dhidi ya uliwengu wa Kiislamu. Ukaribu wa kimazingira na kijografia wa chuo hicho na pia kuwepo kwa manazuoni mashuhuri wa Kiislamu kama vile Sayyid Jamal ad-Deen Asadabadi. Sheikh Muhammad Abdou na wanafunzi wao ambao wote walikuwa walinganiaji wa umoja wa Kiislamu na vilevile kushiriki kwao katika vita dhidi ya Israel, ni jambo jingine lililoimarisha wito wa kuwepo umoja wa Kiislamu katika chuo hicho kuliko vituo vingine vyote vya Kiislamu. Wito huo ulipokelewa na kuungwa mkono mara moja na wanazuoni wengine wa Kiislamu katika pembe mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu. Ayatullah Burujerdi wa nchini Iran alikuwa miongoni mwa wanazuoni hao mashuhuri waliopokea kwa moyo mkunjufu wito huo wa kuimarishwa umoja miongoni mwa Waislamu na kuwataka wafanye hima ili kuhakikisha kwamba lengo hilo la umoja linafuatiliwa kwa karibu na Waislamu wote bila kujali madhehebu zao.

Ufafanuzi

ITHIOPIA NA UISLAMU

ITHIOPIA NA UISLAMU ITHIOPIA NA UISLAMU Uhabeshi ambayo hii leo inajulikana vyema kwa jina la Ethiopia ni nchi ambayo ni mashuhuri sana kwa Waislamu. Katika makala hii tumejaribu kadiri ya uwezo wetu kubainisha angaa kwa ufupi hali ya kihistoria, kijografia, kieneo kisiasa na kijamii ya nchi hiyo muhimu katika bara la Afrika. Katika sehemu nyingine tumejaribu pia kugusia hali ya dini tatu muhimu za Kiislamu, Kikatoliki na Kiothodoksi nchini humo. Sehemu ya mwisho ya makala hii inahusiana na hali ya hivi sasa ya Waislamu wa Ethiopia na pia uhusiano wa kiuchumi wa Iran na nchi hiyo. Maneno muhimu: Uhabeshi, Ethiopia, Uislamu, Ukristo, hajiri, jiografia, hali ya kihistoria na kisiasa, Italia, Haile Selassie, utawala wa kifalme na uhusiano wa kiuchumi. Uhabeshi inafahamika vyema kwa Waislamu kutokana na kuwa ndilo lililokuwa kimbilio la kwanza la maswahaba mashuhuri wa Mtume Mtukufu (SAW) mwanzoni mwa kudhihiri Uislamu. Kabla ya Uislamu kuenea huko Bara Arabu kundi la kwanza kabisa la Waislamu lilihajiri na kuhamia Uhabeshi kutokana na mateso makubwa waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa makafiri wa eneo hilo. Uhabeshi ilisamehewa jihadi kutokana na kuwahifadhi Waislamu hao waliohamia huko. Najashi alikuwa mfalme wa kwanza Mkristo kusilimu na hadi leo Waislamu hulizuru kaburi lake kwa ajili ya kutoa heshima zao kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika kuutetea Uislamu.

Ufafanuzi

UDUG WA UISLAMU

UDUG WA UISLAMU UDUG WA UISLAMU Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesema katika ufunguzi wa kikao cha 23 cha kimataifa cha Wiki ya Umoja wa Kiislamu mjini Tehran, kwamba lengo kuu la kufanyika kikao hicho ni kuleta na kuimarisha udugu katika umma wa Kiislamu. Akizungumza katika kikao cha ufunguzi cha mkutano huo wa kimataifa, Ayatullah Ali Taskhiri ametoa salamu za pongeza kwa washiriki wa kikao na Waislamu wote ulimwenguni kwa mnasaba huu adhuimu wa kuadhimisha kuzaliwa Mtukufu Mtume (SAW) na Imam Swadiq (AS) na kusema kwamba kufanyika vikao vya kieneo na kimataifa na hasa hiki cha Umoja wa Kiislamu ni miongoni mwa majukumu na malengo muhimu zaidi ya Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu. Amesema vikao hivyo vinafanyika kwa lengo la kueneza utamaduni wa udugu wa Kiislamu miongoni mwa jamii za Kiislamu. Ayatullah Taskhiri amesisitiza kwamba, tokea wakati wa kuasisiwa taasisi hiyo hadi leo, asasi hiyo muhimu ya Kiislamu imeshughulikia masuala mengi ya kuimarisha utafiti na utamaduni na vilevile matatizo na changamoto mbalimbali zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu. Amesema, juhudi za kutatua matatizo hayo ambayo kimsingi yanatokana na tofauti pamoja na hitilafu za kimadhehebu zinafanyika kwa ushirikiano wa wasomi na wanafikra wa Kiislamu na kwamba tayari njia za kuyatatua kwa msingi wa vitabu za wafuasi wa madhehebu za Kisunni zimepatikana.

Ufafanuzi

UHUSIANO ULIOPO BAINA YA HAKI NA DINI

UHUSIANO ULIOPO BAINA YA HAKI NA DINI UTANGULIZI Katika sehemu ya kwanza ya Makala hii tulizungumzia uhusiano uliopo baina ya Dini na Haki, pamoja na kutoa ufafanuzi wa kiasi fulani kuhusiana na uhakika wa vitu viwili hivyo, leo tena katika sehemu ya pili ya Makala hii tumeamua kuingia ndani zaidi katika kuipekua Haki na kuifafanua kwa upana zaidi. Jambo ambalo linaweza kuzibadilisha nadharia zetu na kuziongoza katika malengo yaliyo bobea fikra sahihi kwa ajili usalama wa jamii zetu, na vizazi vyetu. HAKI Neno Haki kilugha huwa lina maana ya uhakika wa jambo fulani lilivyo, au kuthibika kwa kitu fulani katika picha halisi ya kitu hicho kilivyo. Wakati mwengine neno Haki huwa lina maana ya kuwajibika kihalali ipaswavyo, na mara nyingi watu hulitumia neno hilo katika maana hiyo, kwa mfano pale anapoambiwa mmoja wetu, ni Haki yako kutenda jambo fulani, yaani ni wajibu wako kutenda jambo hilo, na hilo linamaanisha kuwa kutenda kwako huko kwa jambo hilo ndiko kunakoonyesha nafasi halisi uliyoishika katika jamii yako. Mwanazuoni maarufu ajulikanaye kwa jina la "Tabarsiy" anasema: "Neno Haki huwa lina maana ya kila kitu kukaa katika sehemu yake ipaswayo kukaa, hivyo basi wakati wowote ule mtu atapokuwa na itikadi ya kitu fulani kwa kupitia dalili iimara katika kuisimamisha itikadi hiyo, hapo basi itikadi hiyo itasadikika kuwa ni itikadi ya Haki, kwani kuthibitika itikadi fulani kwa kupitia misingi imara na dalili madhubuti ni Haki, na kinyume chake huwa ni Batili".

Ufafanuzi

KULINDA UMOJA

KULINDA UMOJA KULINDA UMOJA Mbinu na mikakati ya Uislamu ya kulinda umoja wa Umma Umoja wa Umma wa Kiislamu si maudhui ambayo imeanza kujadiliwa katika milenia hii ya 21, bali ni jambo la msingi ambalo siku zote limekuwa likisisitizwa na kufuatilia kwa karibu na Uislamu. Huku ikisisitiza umuhimu wa kubainishwa na kuwekwa mipaka kati ya makafiri na maadui wa Uislamu na wafuasi wa dini hii tukufu, Qur'ani Tukufu inatilia mkazo suala la kuwepo mapenzi, usamehevu, umoja na mahaba kati ya Waislamu. Inawasihi Waislamu kushikamana na kuwa na umoja katika msingi wa kamba ya Mwenyezi Mungu na kuutaja udugu na umoja huo kuwa neema Yake kubwa kwa wanadamu. Sira na maisha ya Mtume Mtukufu (SAW) pia yanasisitiza juu ya jambo hilo. Kwa ibara nyingine, tunaweza kusema kuwa tabia na maisha yote ya Mtume Mtukufu yanaakisi moja kwa moja mafundisho hayo muhimu ya Qur'ani Tukufu.

Ufafanuzi

MAPENDEKEZO 12 KWA AJILI YA UMOJA

MAPENDEKEZO 12 KWA AJILI YA UMOJA MAPENDEKEZO 12 KWA AJILI YA UMOJA Pamoja na kuwepo uhasama wa maadui kuhusiana na msimamo huu na hasa sehemu inayohusiana na umoja wa Waislamu, ambao mteteaji wake mkuu alikuwa ni marehemu Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu), lakini pamoja na hayo fikra hii imeendelea kuwa imara, ya kimantiki, inayoweza kutekelezwa na muhimu katika kulinda umoja wa Kiislamu. Kuhusiana na suala hilo tunapasa kufanya kila liwezekanalo ili kuepuka mitazamo inayopindukia mipaka na kukabiliana vilivyo na wale wanaoeneza fikra kama hizo potofu, wawe wako miongoni mwetu au katika upande wa pili. Watu ambao huwa hawajali maisha ya Mashia wala Masuni na kutosita katika kulipua mabomu yanayoleta hasara na maafa makubwa au kujilipua katika kufikia malengo yao haramu wanapaswa kung'olewa kutoka katika jamii ya Waislamu ili kuiepusha na madhara yao. Kwa kutumia uzoefu wa kihistoria na uchunguzi wa kisiasa, tumejaaliwa kutaja hapa baadhi ya misingi ambayo iwapo itazingatiwa na kutekelezwa ipaswavyo inaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuleta umoja na mfungamano katika jamii ya Kiislamu. Hata kama huenda misingi hii si mipya lakini huenda njia iliyotumika katika uwasilishaji wake ikatofautiana sana na njia zilizotumika huko nyuma na hivyo kumfanya msomaji kuizingatia.

Ufafanuzi

LENGO LA SHARAFU DIIN

LENGO LA SHARAFU DIIN LENGO LA SHARAFU DIIN Umoja wa Umma wa Kiislamu, lengo kuu la uandishi wa Sharafu Deen. Hata kama, kama walivyokuwa wanazuoni wengine muhimu katika historia ya Kiislamu, Sayyid Sharafu Deen alipambana na ukoloni, lakini alikuwa akiamini kwamba changamoto na matatizo muhimu zaidi ya Ulimwengu wa Kiislamu, ni ya ndani na wala hayatokani na madui wa nje, na wakati huohuo kusisitiza kwamba utatuzi wa matatizo hayo unahitajia mbinu za kielimu na kimantiki. Kwa kawaida fikra, umashuhuri, kiwango cha elimu, ubunifu na kina cha fikra cha kila mwandishi hujulikana kupitia maandishi yake. Ni maandishi hayo ndiyo huwafanya wasomaji kutambua elimu kubwa na maarifa aliyonayo msomi fulani katika uwanja unaomuhusu wa kielimu na hivyo kumpa majina na lakabu kama vile 'ensaiklopidia', 'allama' au majina mengine yanayoonyesha mtu aliye na kipaji kikubwa cha elimu. Amma, kuna waandishi wachache mno ambao katika vitabu vyao hujishughulisha na masuala maalumu na kuchukua misimamo mahususi kuhusiana na utatuzi wa matatizo yanayoikabili jamii. Ni wazi kuwa waaandishi kama hao wana thamani na umuhimu mkubwa zaidi katika jamii kwa sababu huongoza na kuielekeza katika upande maalumu, ikiwa inafuatilia maalengo maalumu pia. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, waandishi kama hao huyachukulia maisha humu duniani kuwa na malengo maalumu. Huyatazama maisha ya kijamii ya Waislamu pia katika mtazamo huohuo. Suala hilo bila shaka hufungamana na jambo linalochukuliwa na waandishi hao kuwa muhimu na nyeti katika zama zao na kwamba jamii inahitajia swali, jibu na utatuzi wake wa haraka. Huenda likawa ni jambo la busara kuwaita waandishi kama hao kuwa ni wasomi warekebishaji wa jamii. Marekebisho bila shaka hufanyika katika masuala ya kijamii au mara nyingine ya kisiasa, ambayo huishughulisha jamii kifikra. Ni kutokana na hali kama hiyo ndipo wasomi kama hao wa Kiislamu huamua huchukua misimamo na kufuata njia maalumu katika kuwaongoza wafuasi wao kwenye njia nyoofu.

Ufafanuzi

SEREKALI YA MTUME (S.AW.W)

SEREKALI YA MTUME (S.AW.W) SEREKALI YA MTUME (S.AW.W) Ushahidi na nyaraka za historia za kabla ya kudhihiri Uislamu zinaonyesha kuwa hakukuwepo utawala na serikali katika ardhi ya Hijaz na kwamba maisha ya Waarabu wa jangwani hayakutawaliwa na mfumo makhsusi wa kisiasa. (1) Ni baada ya kudhihiri dini ya Uislamu huko Makka na kuhamia Mtume Muhammad katika mji wa Madina ndipo mtukufu huyo alipoanzisha serikali kuu na kubadili mfumo wa kikabila uliokuwa ukitawala kwa kuasisi mfumo mpya wa kisiasa na kijamii. Mbali na kutoa mafunzo na malezi kwa jamii ya watu wa Hijaz, Mtume Muhammad (saw) pia aliongoza yeye binafsi jamii changa ya Kiislamu na kushika hatamu za mfumo wa kijamii wa Waislamu katika nyanja mbalimbali za sheria, utamaduni, siasa, masuala ya kijeshi na kiuchumi.(2) Suala hilo linaonekana wazi zaidi katika mtazamo wa aya za Qur'ani na ushahidi wa kihistoria kiasi kwamba hata wataalamu wa masuala ya Mashariki (orientalist) wasiokuwa Waislamu wamelifafanua kwa uwazi zaidi. Msomi wa Kitaliano Fel Lino anasema: Mtume Muhammad (saw) aliasisi dini na dola kwa pamoja na masuala yote hayo mawili yalipanuka na kukuwa sambamba katika kipindi cha uhai wake. (3) Dr. Strotmann anaamini kwamba: Uislamu ni tukio la kidini na kisiasa, kwani muasisi wake mbali na kuwa Mtume alishika hatamu za serikali na alikuwa na utaalamu kamili wa kuongoza serikali". (4) Hata hivyo katika karne za hivi karibuni baadhi ya waandishi (5) wametilia shaka uhakika kwamba serikali ya Mtume Muhammad (saw) ilikuwa serikali yenye uhusiano na wahyi na mafundisho ya Mwenyezi Mungu kutokana na kuathirika kwao na mafundisho ya fikra za kisekulari yanayotilia mkazo kutenganishwa dini na siasa. Waandishi hao wanasisitiza kuwa suala la serikali na uongozi ni suala la kibinadamu lizilokuwa na uhusiano wowote wa dini. Wanadai kuwa Nabii Muhammad (saw) hakuwa kiongozi wa kisiasa wala hakuamrishwa na Mwenyezi Mungu kuunda serikali na kuongoza masuala ya jamii. Kwa msingi huo, kama mtukufu huyo aliunda serikali na kuongoza masuala ya jamii alifanya hivyo kutokana na haja ya jamii hiyo na si wajibu wa kidini kutoka kwa Mwenyezi Mungu!

Ufafanuzi

KUKOMBOLEWA QUDS

KUKOMBOLEWA QUDS KUKOMBOLEWA QUDS Abdallah Fahd, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kuwait amesisitiza kwamba kukombolewa kwa Quds Tukufu kutoka kwenye makucha ya utawala ghasibu wa Israel kunahitajia muamko, azma na irada thabiti ya Waislamu wote duniani. Akizungumza katika kikao cha kimataifa cha "Quds katika Dhamiri ya Waarabu" kinachofanyika mjini Kuwait na ambacho kimefunguliwa na Nasir Muhammad Ahmad Swabah, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Fahd amesema kuwa nchi za Kiislamu zinapasa kuwa na mikakati madhubuti na ya pamoja kwa ajili ya kuikomboa Quds kutoka mikononi mwa walowezi wa Kizayuni. Amesema kuwa jambo hilo litathibiti tu iwapo nchi za Kiislamu zitaamua kushirikiana na kuwa na umoja pamoja na urafiki miongoni mwao. Amesema nchi za Kiislamu na Kiarabu zina majukumu mazito kuhusiana na suala la Palestina. Amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kwamba utawala ghasibu wa Israel umewafukuza mamilioni ya Wapalestina kutoka kwenye ardhi zao za jadi na kuwafanya waishi kama wakimbizi katika ardhi zao wenyewe na kwingineko huku ukiharibu kabisa sura ya mji wa Quds Tukufu ambao zamani ulikuwa nembo ya umoja na kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti.

Ufafanuzi

VIZUIZI NA CHANGAMOTO ZA UMOJA

VIZUIZI NA CHANGAMOTO ZA UMOJA VIZUIZI NA CHANGAMOTO ZA UMOJA Umoja wa umma wa Kiislamu ni lengo muhimu na aali ambalo wanafikra na maulamaa wa Kiislamu wamekuwa wakifanya jitihada kubwa tangu zama za awali za Uilslamu kwa ajili ya kufikia lengo hilo. Hivi sasa tumo katika Wiki ya Umoja kati ya Waislamu ambayo ilitangazwa na hayati Imam Khomeini kutokana na hitilafu za mapokezi kuhusu siku aliyozaliwa Mtume Muhammad (saw). Wiki hiyo inaanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal. Makala hii inazungumzia Umoja wa Umma wa Kiislamu, Vizuizi na Changamoto. Umoja wa umma wa Kiislamu ni lengo muhimu na aali ambalo wanafikra na maulamaa wa Kiislamu wamekuwa wakifanya jitihada kubwa tangu zama za awali za Uilslamu kwa ajili ya kufikia lengo hilo. Hadi sasa kumetolewa fikra nyingi na kuitishwa vikao na mikutano chungu nzima kujadili kadhia ya udharura wa kuwepo umoja na mshikamano kati ya Waislamu wote. Udharura wa umoja na mshikamano wa Kiislamu umesisitizwa mno katika maandiko ya kidini na dalili za kimantiki na kiakili. Hata hivyo inasikitisha kwamba Waislamu wanapokaribia kuungana na kuimarisha umoja na mshikamano wao hujitokeza vizuizi chungu nzima ambavyo kunahitajika juhudi kubwa, tadbiri na mwamko wa Waislamu ili kuweza kuviondoa na kukabiliana navyo. Baadhi ya vizuizi na vikwazo vya umoja wa Waislamu vinatokana na hitilafu za ndani ya umma wa Kiislamu japokuwa hapana shaka kwamba wakoloni na madola ya kibeberu daima yamekuwa yakifanya njama za kuzusha hitilafu na mifarakano katika umma wa Kiislamu.

Ufafanuzi

UMOJA WA WAISLAMU

UMOJA WA WAISLAMU UMOJA WA WAISLAMU Ayatullah Ali Taskhiri, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu katika mazungumzo yake na Shirika la Habari la Fars amebainisha malengo na shughuli za taasisi hiyo katika kukabiliana na vitendo vya uchochezi na mgawanyiko dhidi ya Waislamu. Amesema Taasisi ya Kukurubisha pamoja Mahdhebu ya Kiislamu imekuwa na nafasi muhimu katika kunyanyua uelewa wa Waislamu na kwamba ili kufikia lengo hilo taasisi hiyo imetuma jumbe mbalimbali katika vikao vya kimataifa na pia katika nchi tofauti kwa madhumuni ya kuondoa sutafahumu na shubha za kidini. Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesema, kuongezeka kwa uelewa katika ulimwengu wa Kiislamu kumekuwa na nafasi muhimu katika kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu na kwamba hilo ni moja ya malengo muhimu ya taasisi hiyo. Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri amesema kuwa juhudi kubwa zimefanywa na zingali zinafanywa na mabeberu wa dunia kwa lengo la kuharibia jina la Uislamu na Ushia na hasa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Ufafanuzi

UMOJA KWA WAISLAMU

UMOJA KWA WAISLAMU UMOJA KWA WAISLAMU Umoja wa Kiislamu Ayatulllah Taskhiri amesema kwa masikitiko kuwa, ukufurishaji wa Waislamu ni kizuizi kikubwa zaidi kinachozuia kukurubiana madhehebu ya Kiislamu na hii ni katika hali ambayo Uislamu umeweka wazi mipaka ya kuamini na kukufuru. Umoja wa Kiislamu ni lengo muhimu na tukufu ambalo wanafikra, viongozi, wasomi na wanazuoni wa Kiislamu wamekuwa wakilifuatilia kwa juhudi kubwa na kwa miaka mingi tokea mwanzoni mwa Uislamu. Ulimwengu wa Kiislamu unazijumuisha nchi ambazo kwa kawaida zina mifungamano mikubwa ya kijografia na kiutamaduni. Kutokana na utajiri mkubwa wa mafundisho yake, dini ya Kiislamu ilianzisha utamaduni na ustaarabu mkubwa pamoja na kuandaa mazingira bora ya kuwepo ushirikiano wa kidini na kiutamaduni kati ya mataifa mbalimbali. Lakini umoja na mshikamano wa ulimwengu wa Kiislamu katika kipindi ha historia umekuwa ukikabiliwa na hujuma ya kigeni na mara nyingine vitisho vya ndani. Moja ya mbinu zinazotumiwa na maadui wa ulimwengu wa Kiislamu ni kuzifanya baadhi ya tofauti za kimadhehebu na kifikihi za Waislamu kuonekana kuwa kubwa zaidi kupita kiasi.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini