Bibi Faatima (a.s)
KHUTBA YA FATIMA ZAHRAA (A.S)
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- NDUGU ZETU WA KIISLAMU
KHUTBA YA FATIMA ZAHRAA (A.S) KHUTBA YA MBORA WA WANAWAKE ULIMWENGUNI FATIMA ZAHRAA (A.S). Abdallah bin Hassan amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa baba zake juu yao rehma na amani ya kuwa: Pindi Abubakar na Omar walipo kata shauri la kumzuilia na kumnyima mwana Fatima shamba lake la Fadak, na habari hizo kumfikia bibi huyo, alijifunika ushungi wake (alijifunga ushungi) kichwani na kuvaa buibui lake na kutoka akiwa katika kundi la wahudumu wake (walio kuwa kati ya watu watatu au zaidi) na akiwa na wanawake wa kabila lake, huku akitembea kwa utulivu na kwa mwendo wa hatua fupifupi mwendo ulio shabihiana na mwendo wa baba yake Mtume (s.a.w), hadi akafika na kuingia kwa Abubakar, nae akiwa katika kundi la Muhajirina na Answar na wengineo. Akaikunja nguo yake ya kiunoni na kuketi chini kisha akatoa sauti ya mlio, sauti ambayo iliwafanya watu kulia kutokana na sauti hiyo ya kilio aliyo itoa, na majlisi (kikao) ile ikajawa na kelele za vilio, kisha akatulia kiasi hadi sauti za vilio za watu wale zikatulia, na hamasa pia huzuni zao zilipo tulia akaanza mazungumzo yake kwa kumsifia Mwenyezi Mungu kwa sifa njema na kumhimidi na kumtakia rehma Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w), kisha watu wakaangua tena kilio chao, na walipo nyamaza akaendelea na mazungumzo yake na kunena: Sifa zote njema na himidi zote ni zake Mwenyezi Mungu juu ya yale aliyo waneemesha nayo viumbe, na shukrani ni zake Mwenyezi Mungu juu ya ilhamu aliyo wapatia waja wake watakasifu, ilhamu ya kufahamu tawhidi (upweke wa Allah) ya Mwenyezi Mungu, na sifa pia shukurani na himidi zote ni zake kwa yale aliyo wapatia waja kama vile kuwepo kwao wakiwa hai, na kutokana na neema zote alizo waneemesha nazo (kama akili, uwezo wa kuzungumza na mengineyo).
MBAA MWEZI YA MWEZI WA DHAHABU
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- SALIM SAID AL- RAAJIHIY
MBAA MWEZI YA MWEZI WA DHAHABU UTANGULIZI Asalamu alaikum wasomaji wetu wapenzi Ninamshukuru Muumba Mkamilifu kwa kuniwezesha kuandika Makala hii inayomhusu mmoja kati ya watu watukufu wa uma wetu huu. Nitajaribu kutoa ufafanuzi kuhusiana na mtukufu huyu kwa kadri ya uwezo wangu wa kielimu utakavyoniruhusu, kwani kuwazungumzia watukufu mbali mbali huwa kunahitajia kalamu iliyobobea wino wa kielimu, wino ambao utaweza kufafanua kwa upeo uliyo wa wazi kabisa, kuhusiana na sifa za watukufu hao, na kwa upande mwengine sisi tunapotaka kuzielezea sifa mbali mbali za watukufu wa uma huu huwa tunahitajia mimeremeto mbali mbali ya wino wenye kupendeza katika rangi nzuri za kielimu, na mimi mwenyewe sijihisi kuwa nina uwezo wa kuziakisi sifa za watukufu hao ipaswavyo, hii ni kwa kutokana na uchanga wa nuru ya kielimu niliyo nao. Ninatarajia kuwa jitihada zangu zitaweza kutoa angalau picha ya kivuli tu cha sifa za Mtukufu huyu ninaye mkusudia kumuelezea katika makala hii, na hata kama nitashindwa kutoa picha halisi ya Mtukufu huyu, pia sitaacha kumshuru Mola wangu kwa kunionyesha angalau kivuli tu cha picha halisi ya sifa zake. Ninamuomba Mola Mtukufu atuwafikishe katika mema na atuepushe na yale yote yasiyompendeza Mola wetu. Aamin.
NAFASI YA FATIMA (A.S)
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- BARAZA
NAFASI YA BIBI FATIMA AZ-ZAHRAA (A.S) Waandishi wengi wa masuala ya historia ya Kiislamu, wa Kishia na Kisuni, wanaamini kwamba uzawa wa Bibi Fatimatu az-Zahra (AS) ulitimia mjini Makka tarehe 20 Jumadi Thani mwaka wa Tano wa kubaathiwa Mtume Mtukufu (SAW). Wengine wanasema kuwa ulikuwa ni mwaka wa tatu ilhali wengine wanaamini kuwa ulikuwa ni mwaka wa pili wa kupewa utume Mtume Mtukufu (SAW). Mwanahistoria na mwanahadithi mwingine wa Kisuni anasema kuwa bibi Zahra (AS) alizaliwa katika mwaka wa kwanza wa kubaathiwa Mtume (SAW). Bibi Fatimatu az-Zahra (AS) ni binti wa Mtume Mtukufu (SAW) na Bibi Khadija Kubra. Alikuwa binti wa nne wa Mtume. Lakabu zake Bibi Zahra (AS) ni: Zahra, Swiddiqa, Twahira, Mubaraka, Zakiyya, Radhiya, Mardhiyya, Muhaddatha na Batul. Ni wazi kuwa hata kama siku au mwaka wa kuzaliwa mtu na shakhsia yoyote mkubwa una thamani katika masuala ya uhakiki na utafiti wa kihistoria, lakini bila shaka jambo hilo halina umuhimu mkubwa katika uchambuzi wa tabia na maisha yake. Bibi Fatimatu az-Zahra (AS) alizaliwa na kulelewa kando ya baba yake, Mtume Mtukufu wa Mwenyezi Mungu (SAW) na katika nyumba ya utume, nyumba ambayo ilikuwa ni sehemu ya kuteremkia wahyi na aya za Qur'ani Tukufu. Hapo ni mahala ambapo kundi la mwanzo la Waislamu lilikuwa limekiri na kumwamini Mwenyezi Mungu mmoja na wakati huohuo kusimama imara katika imani hiyo.
FATIMA (A.S) NDIYE KIGEZO
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- AL-UDII
FATIMA (A.S) NDIYE KIGEZO FATIMA (A.S) NDIYE KIGEZO Bibi Fatimah (a.s.) ni mwanamke anayezingatiwa kuwa ni mwanamke wa kutolea mfano katika dini ya ki-Islamu, na pia ni kiigizo chema kwa kila mwanamke anayetafuta mafanikio katika maisha yake. Bibi Fatimah binti Muhammad (s.a.w.w) ndiye mwanamke bora ulimwenguni aliyezaliwa na kupata malezi katika nyumba iliyokuwa ikishuka ndani yake Wahyi kutoka mbingu-ni. 9Hadithi hii imenukuliwa kutoka ndani ya kitabu kiitwacho Tuhaful- Uquul. Katazo hili linaju-muisha mambo mengi na khususan mambo yote ambayo Mwenyezi Mungu hayaridhii na yanatendwa na maadui wa Mwenyezi Mungu. Mwislamu inamuwajibikia kujiepusha nayo vinginevyo hapatakuwa na tofauti kati ya Muumini na adui wa Mwenyezi Mungu. Mtarjumi.
- «
- Anza
- Iliyopita
- 1
- Inayofuata
- Mwisho
- »