Midahalo
MJADALA KUHUSU MWANZO WA UUMBAJI
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- Taqee Zacharia
MJADALA KUHUSU MWANZO WA UUMBAJI Kutokana na hisia aliyoumbwa nayo kila mwanadamu,ni wazi kwamba hisia hii humpeleka Mwanadamu huyu kutaka kujua sababu ya kutokea au kuwepo kwa kila kitu akionacho mbele yake.Kamwe huwa hafikiria kuwa huenda vitu hivyo vimetokea au kudhihiri hivi hivi tu (vyenyewe) pasina sababu yoyote au chanzo chochote kilichopelekea kutokea kwa vitu hivyo. Kwa ibara nyingine tunasema kwamba:Mwanadamu haoni kuwa vitu hivyo vimedhihirika kiajali au kighafla.Mfano:Dereva ambaye gari lake husimama ghafla hushuka kutoka kwenye gari na kuanza kukagua na kutazama sehemu anayodhani kuwa inaweza kuwa na hitilafu ambayo imepelekea kusimama ghafla kwa gari lake.Huwezi kuamini kuwa gari lake ambalo liko katika hali nzuri ya kuendelea na mwendo linaweza kusimama ghafla bila ya kuwepo sababu yoyote ile iliyopelekea lisimame ghafla.! Anapotaka kuliendesha gari gari hilo hutumia vifaa vilivyowekwa kwenye gari hilo na kamwe hawezi kutegemea bahati nasibu.
JICHO LA MATUMAINI
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- NDUGU ZETU WA KIISLAMU
JICHO LA MATUMAINI Kwanza kabisa kuna masuala mawili yanayopaswa kuzingatia kwa kina na kupewa haki yanayostahiki bila ya moja kufanywa muhanga wa jingine. La kwanza ni umuhimu wa kulindwa umoja na mfungamano wa Umma wa Kiislamu na jingine ni kulindwa kiini cha Uislamu wenyewe. Umoja na mfungamano wa Waislamu haupaswi kupewa umuhimu na kuzingatiwa zaidi kwa madhara ya ukweli unaotawala ndani ya Uislamu wenyewe na kuchukuliwa tu kuwa suala lenye umuhimu mdogo. Kwa msingi huo, kusema ukweli na hakika ndilo linalopaswa kuwa jambo la msingi. Pamoja na hayo, mambo ambayo yamekuwa yakichochea uadui na chuki miongoni mwa Waislamu yanaweza kujumulishwa kama ifuatavyo: 1- Kujitenga na kupuuza mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu, Qur'ani Tukufu na ushauri wa wataalamu wa vitu viwili hivi. 2- Kuwategemea watu ambao wameharibu na kuchafua sura ya mafundisho ya Qur'ani tukufu na sunna za viongozi watoharifu wa dini. 3- Imani zisizo za kimantiki wala msingi. 4- Ukabila na ubaguzi wa rangi. 5- Tamaa ya masuala ya kidunia na kuvutiwa na mambo kama vile uchu wa madaraka, umashuhuri na mali. 6- Sera na siasa za mifarakano za madola makubwa kwa lengo la kubana na kuwadhibiti Waislamu, kupora mali na akili zao.
NJIA YA UZIMANI
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- Yasin Valerian Massawe
NJIA YA UZIMANI Njia ya uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache. UKWELI ni kwamba, Wakristo wana shahada (ubatizo) ambao hauhusiki na Nabii yeyote wa Mwenyezi Mungu. Sasa itakuwaje? Haya ni mambo ambayo Yesu aliyaona katika Roho kwamba watu watadanganywa kwa nguvu za shetani wamuitikadi kinyume na jinsi yeye mwenyewe alivyofundisha, hata akasema asiyeshika maneno yake atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba juu ya mchanga. Kujenga nyumba juu ya mchanga hata kama utaipamba namna gani na kuigharamia namna gani lakini ulilofanya ni sifuri (ziro). Mfano huu katika dini ni kushindwa kuelewa ile amri kuu (upweke wa Mungu) na kuwatambua Manabii wake wote kama alivyowaleta kwa haki ili wafundishe tumjue. Lile alilolilaani Yesu ndilo Wakristo wamelishika na lile alilolitukuza ndilo Wakristo wamelitupa. Hii inatokana na utabiri uliotoka mbali, kwani hata Nabii Isaya aliona katika Roho jinsi hali itakavyokuwa kuhusu chuo cha Qur'an kwani anasema: "... Vipofu wataona katika upofu na wenye akili, akili zao zitafichwa..." (Isaya 29:18) Qur'an imeletwa ili kuondoa giza. Basi wasiotaka kuelewa walete mfano wake kama wataweza (Qur'an 17:88). Na kama kweli ingelikuwa Qur'an ni mashairi aliyoyatunga Muhammad (s.a.w.) nadhani hicho kitabu kingesambaratikia mbali hata kizazi hicho kisijue jina la kitabu hicho isipokuwa labda katika historia tu.
- «
- Anza
- Iliyopita
- 1
- Inayofuata
- Mwisho
- »